Sheria Ndogo za (Hifadhi ya Mazingira) za Halmashauri ya Wilaya ya Mlele, 2017
Sheria Ndogo hizi huanza kutumika baada ya kutangazwa katika Gazeti la Serikali na zinatumika katika eneo lote chini ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlele.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo za (Hifadhi ya Mazingira) za Halmashauri ya Wilaya ya Mlele, 2017
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
Sheria Ndogo hizi huanza kutumika baada ya kutangazwa katika Gazeti la Serikali na zinatumika katika eneo lote chini ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlele. Herders under these by-laws must follow council directions on herd numbers, grazing areas, stock routes, dipping, vaccination, markings, training, and related contributions, and must not cut trees to drive away tsetse flies. Wafugaji wanazuiwa kufanya vitendo kadhaa vya malisho, usafirishaji, uuzaji na uchinjaji wa mifugo bila maeneo au vibali vinavyohitajika; Halmashauri pia ina majukumu ya kutenga malisho na njia za mifugo, na maafisa fulani wanaweza kukagua mashamba na nyumba. Residents of an area with damaged natural vegetation or local environment must restore it to its normal state. Ni marufuku kwa mtu yeyote kuchimba mchanga katika maeneo ambayo Halmashauri haijaruhusu, isipokuwa kama kuna ruhusa maalum ya Halmashauri.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo za (Hifadhi ya Mazingira) za Halmashauri ya Wilaya ya Mlele, 2017
Showing 6 of 6
- 3 Verify source ↗
Section 3
AI-assisted research summary: Sheria Ndogo hizi huanza kutumika baada ya kutangazwa katika Gazeti la Serikali na zinatumika katika eneo lote chini ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlele.
3. SEHEMU YA KWANZA UTANGULIZI Sheria Ndogo hizi zitaitwa Sheria Ndogo za (Hifadhi ya Mazingira) za Halmashauri ya Wilaya ya Mlele, 2017 na zitaanza kutumika baada ya kutangazwa katika Gazeti la Serikali. Sheria Ndogo hizi zitatumika katika eneo lote lililopo chini ya mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlele. Katika Sheria Ndogo hizi isipokuwa pale itakapoelezwa vinginevyo; “Afisa mwidhiniwa” maana yake ni Afisa yeyote wa umma atakayeteuliwa kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hizi; Sura 206 “Eneo la Hifadhi” maana yake ni maeneo ya milima, maeneo ya Vyanzo vya Maji, Hifadhi ya Misitu, Miteremko na maeneo mengine ambayo yatatangazwa na Halmashauri kuwa ni maeneo ya hifadhi; 1 Sheria Ndogo za (Hifadhi ya Mazingira) za Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Tangazo la Serikali Na. 26 (linaendelea) “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Mlele; “Kiwanda” maana yake ni Jengo au majengo ambapo vitu vinatengenezwa; “Kuvuna misitu” maana yake ni pamoja na kufyeka, kukata, kung’oa miti au visiki; “Mabwawa” maana yake ni sehemu yoyote yenye mkusanyiko wa maji kwa ajili ya matumizi mbalimbali; “Machungio” maana yake ni maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kulishia mifugo. Maji” maana yake ni kama ilivyo tafsiriwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira kuwa ni pamoja na maji ya yanayotiririka, kunywa, yaliyohifadhiwa, yaliyo katika visima, mabwawa, mifereji, madimbwi, maziwa, maji yaliyoko chini ya ardhi, maji yaliyoko katika makondo; vijito, maji ya mito, Na. 20 ya Mwaka 2004 Na. 20 ya Mwaka 2004 "Mazao ya misitu” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira kuwa ni kitu cho chote kinachopatikana au kuzalishwa kutokana na miti, mazao yanayoota au kupatikana msituni, ambayo ni pamoja na mianzi, magamba, mkaa, kuni, miti, fito, mbao, mbegu za miti, nta, asali, utaa, matunda, upapi, majani ya kulalia wanyama, majani, mizizi, gundi, utomvu, maranda, matete, kamba, makuto, nyuzi za wanyama, mimea au kitu chochote chenye uhai au kisicho kuwa na uhai kitakachotangazwa katika gazeti la Serikali kuwa ni zao la msitu; “Mazingira” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira kuwa ni maumbile halisi yawazungukao binadamu ikiwa ni pamoja na hewa, ardhi, maji, tabia ya nchi, sauti, mwanga, harufu, ladha, vijiumbe, hali ya kibiolojia za wanyama na mimea, raslimali za kitamaduni na masuala ya uchumi jamii na inahusisha mazingira asilia na yaliyoundwa na binadamu na jinsi yanavyoingiliana; 2 Sheria Ndogo za (Hifadhi ya Mazingira) za Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Tangazo la Serikali Na. 26 (linaendelea) “Mti” maana yake ni mti uliopandwa na miti asili ikiwa ni pamoja na mianzi, vichaka, mapori, maotea ya msituni ya umri mbalimbali na aina tofauti; “Mfugaji” maana yake ni mtu yeyote anayejishughulisha na ufugaji wa mifugo katika eneo la Halmashauri; “Mkurugenzi maana yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri au Afisa yeyote wa umma atakayeteuliwa kutekeleza majukumju ya Mkurugenzi; "Misitu maana yake ni eneo la ardhi ambalo limefunikwa angalau kwa asilimia 10 ya miti, uoto wa asili au iliyopandwa, au asilimia 50 zaidi, ya vichaka na miti na miti inayoota upya ambayo itajumuisha aina yote ya misitu ya hifadhi amabayo itatangazwa chini ya Sheria ya Misitu na mazao yote ya misitu ikijumuisha majani na nyasi ndani ya eneo la Halmashauri; “Taka” maana yake ni kama ilivyo tafsiriwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira kuwa ni kitu chochote kimiminika, kigumu, kinachotoa harufu mbaya, au kilichohifadhiwa katika mazingira ya hali ya ujazo, uozo au hali nyingine yoyote inayosababisha uharibifu wa mazingira inajumuisha taka; ambayo “Taka ngumu” maana yake ni kama ilivyo tafsiriwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira kuwa ni taka ambazo haziko katika umajimaji kutoka majumbani. Katika majengo ya biashara, viwandani na kutoka katika shughuli za kilimo, pamoja na taka za vyakula, karatasi, plastiki au taka laini zinazotokana na ujenzi au ubomoaji majengo utengenezaji bustani na shughuli za uchimbaji madini,mizoga ya wanyama na mabaki ya magari mabovu; “Uchafuzi wa mazingira” maana yake ni uchafuaji wa mazingira kwa namna yoyote ile unaotokana na utupaji wa kitu chochote baada ya kukitumia au uwekaji wa kitu chochote katika eneo ambalo hakikustahili kuwepo au mwingiliano wa sauti za juu kutoka kwa watu au 3 Na.14 ya mwaka 2002 Na. 20 ya Mwaka 2004 Sheria Ndogo za (Hifadhi ya Mazingira) za Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Tangazo la Serikali Na. 26 (linaendelea) vyombo mbalimbali ambavyo husababisha usumbufu wa kimazingira, hewa chafu, maji na vitu vyovyote vile ambavo husababisha uchafuzi katika hali yoyote ile; "Udongo maana yake ni kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira kuwa ni pamoja na ardhi, mchanga, mwamba,tope, madini, uoto na viumbe waishio humo na vyote vitokanavyo kama vile vumbi; ”Vitu hatari” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira. Kuwa kemikali yo yote, taka gesi, madawa, vidonge, mimea wanyama au viumbe hai visivyoonekana ambavyo ni hatari kwa afya ya binadamu, maisha au mazingira. “Uharibifu” maana yake ni mabadiliko ya moja kwa moja ya rasilimali za kimaumbile, hali ya joto, kemikali, kibaolojia ambazo ni kikwazo cha sehemu ya mazingira na hivyo kuleta madhara kwa matumizi yenye manufaa, au kusababisha hali ambayo ni hatari kwa jamii kiafya, kiusalama au ustawi wa binadamu na mazingira; SEHEMU YA PILI MASHARTI YA UFUGAJI Wajibu wa mfugaji
Part
SEHEMU YA PILI
- 4 Verify source ↗
Section 4
AI-assisted research summary: Herders under these by-laws must follow council directions on herd numbers, grazing areas, stock routes, dipping, vaccination, markings, training, and related contributions, and must not cut trees to drive away tsetse flies.
4. Kila mfugaji chini ya Sheria Ndogo hizi; (a) yaliyopangwa ya malisho Atatakiwa kufuga idadi ya mifugo kama itakavyoamriwa na Halmashauri; Atatakiwa kufuga na kulisha mifugo yake katika maeneo na Halmashauri; Atatakiwa kupitisha mifugo yake katika njia (stock routes) zilizopangwa na kutengwa na Halmashauri; Atatakiwa itakayoonesha aliyonayo; Atatakiwa kupeleka mifugo katika majosho kama atakavyoagizwa na Halmashauri; Atatakiwa kupeleka Mifugo yake katika Vituo ya Mifugo idadi na aina ya mifugo na Kadi kuwa (b) (c) (d) (e) (f) 4 Sheria Ndogo za (Hifadhi ya Mazingira) za Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Tangazo la Serikali Na. 26 (linaendelea) kama na vya Chanjo Halmashauri, na atalipia chanjo hiyo kama atatakiwa kufanya hivyo; Atatakiwa kuchangia gharama za ukarabati wa itakavyoamuriwa Majosho kama sehemu ya mchango wake, pale itakapobidi kufanya hivyo, na kwa gharama itakayopendekezwa na Halmashauri; Atatakiwa kuchangia gharama za uboreshaji wa maeneo ya malisho yaliyotengwa na Halmashauri; Atatakiwa kuweka alama kwenye mifugo yake (Branding, ear tags) na katika viungo vya mifugo vinavyopendekezwa ili kutoharibu zao la Ngozi; (g) (h) (i) (j) Atatakiwa kuhudhuria mafunzo ya ufugaji kama atakavyo hitajiwa na Halmashauri; (k) Atatakiwa kutokata miti kwa lengo la kufukuza Mbung’o. Masharti ya mfugaji - 5 Verify source ↗
Section 5
AI-assisted research summary: Wafugaji wanazuiwa kufanya vitendo kadhaa vya malisho, usafirishaji, uuzaji na uchinjaji wa mifugo bila maeneo au vibali vinavyohitajika; Halmashauri pia ina majukumu ya kutenga malisho na njia za mifugo, na maafisa fulani wanaweza kukagua mashamba na nyumba.
5. Ni marufuku kwa mfugaji yeyote:- (a) Kuchunga, kulisha, au kunywesha maji Mifugo katika maeneno ambayo hayakutengwa kwa ajili hiyo; (b) Kusafirisha Mifugo kwa kuiswaga Barabarani; (c) Kusafirisha au kuhamisha Mifugo kutoka eneo moja hadi lingine bila Kibali cha Afisa Kilimo na Mifugo; (d) Kuuza au kununua Mifugo katika maeneo ambayo siyo ya mnada, masoko au magulio ya mifugo yaliyoidhinishwa na Halmashauri; (e) Kufuga Mifugo mingi katika eneo dogo la (f) Halmashauri; Kupitisha mifugo yake katika maeneo ambayo hayakuidhinishwa na Halmashauri kupitisha Mifugo. Kuthibiti mifugo inayozurura ovyo 6(1) Halmashauri itakamata Mifugo au Mfugo wowote la kuchungia utakaoonekana unazurura hovyo katika eneo Halmashauri Mifugo. hapajaruhusiwa ambapo (2) Mfugo wowote utakaokamatwa utalipiwa faini kama itakavyopangwa na Halmashauri na baada ya kulipia gharama hizo Mfugaji atarudishiwa Mifugo yake. 5 Sheria Ndogo za (Hifadhi ya Mazingira) za Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Tangazo la Serikali Na. 26 (linaendelea) (3) (4) (5) (6) Ukaguzi wa mifugo 7(1) Endapo mwenye Mifugo au Mfugo hatakokea ndani ya siku saba tangu kukamatwa kwa Mifugo hiyo, Mkurugenzi wa Halmashauri atakuwa na haki ya kuuza kwa mnada Mfugo au mifugo hiyo baada ya kupata idhini ya Mahakama. Baada ya mauzo kufanyika, Mkurugenzi atakata fedha ya faini, gharama za mnada na gharama za ulinzi na fedha zitakazobaki atapewa mwenye Mifugo na kama hataonekana ndani ya siku kumi na nne (14) fedha hizo zitaingizwa katika vyanzo vya ndani vya mapato ya Halmashauri. Endapo mwenye Mifugo au Mfugo atakuwa na sababu za msingi za kutofika ndani ya siku kumi na nne (14) tangu kufanyika kwa mnada Halmashauri itarudisha fedha zake. Endapo kutatokea uharibifu kwa Mifugo au Mfugo Halmashauri haitawajibika na ulipaji wa gharama zozote isipokuwa kama uharibifu huo umesababishwa na uzembe wa Halmashauri, Halmashauri itawajibika kwa uzembe huo. Itakuwa halali kwa Afisa Kilimo na Mifugo, Maafisa Watendaji wa Kata na Vijiji, na Afisa yeyote wa Halmashauri atakayeteuliwa kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hizi kuingia katika Nyumba au jengo lo lote wakati wowote kwa madhumuni ya kukagua na kuhesabu idadi ya Mifugo iliyomo katika nyumba hiyo. (2) Mtu yeyote atakaye wazuia Maafisa Waidhiniwa katika Kifungu cha 7(1) kutekeleza wajibu wao chini ya Sheria Ndogo hizi atakuwa ametenda kosa. Wajibu wa Halmashauri (2) 8(1) Ni wajibu wa Halmashauri kutenga Maeneo maalumu kwa ajili ya shughuli za Malisho kwa kuzingatia idadi ya Mifugo ndani ya eneo la Halmashauri. Halmashauri itatenga njia maalumu ya kupitisha Mifugo kwenda na kurudi malishoni au minadani. Halmashauri itafanya sensa ya mifugo na kutoa kadi za Mifugo ikiwa ni pamoja na kusajiri mifugo yote na kutoa elimu ya ufugaji bora kwa jamii. (3) Taratibu za ufugaji 9(1) Wafugaji wote watatakiwa kuzingatia masharti ya kufuga kama yalivyo katika Sheria Ndogo hizi au Sheria 6 Sheria Ndogo za (Hifadhi ya Mazingira) za Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Tangazo la Serikali Na. 26 (linaendelea) Taratibu za kilimo Masharti kwa mkulima (2) (3) ye yote iliyotungwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kila mfugaji atatakiwa kupeleka mifugo au mfugo yake machinjioni au mahali huduma hiyo inapopatikana na itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kuchinjia mnyama mahali pengine popote. Ni marufuku kwa mtu yeyote kununua, kuuza au kufanya biashara ya kubadilishana aina yoyote ya mifugo katika eneo lolote la Halmashauri isipokuwa kwenye minada au magulio yaliyotengwa kwa shughuli hiyo. SEHEMU YA TATU KILIMO NA UHIFADHI WA ARDHI 10(1) Mtu atakayetaka kuendesha shughuli za Kilimo katika Halmashauri atatakiwa kuzingatia taratibu za kilimo kama zitakavyotolewa na Halmashauri. Itakuwa halali kwa Afisa kilimo kuingia katika shamba lolote kwa madhumuni ya kufanya ukaguzi na kuhakikisha utekelezaji wa Sheria Ndogo hizi. (2) (2) 11(1) Ni marufuku kwa mtu yeyote kulima katika miteremko, karibu na vyanzo vya maji, kandokando ya mito, mabwawa na maziwa au kufanya jambo lolote litakalo haribu hifadhi ya mazingira bila kuzingatia Ushauri wa Afisa Kilimo. Ni marufuku kwa mtu ye yote kutumia kinyume ardhi iliyotengwa kama kilimo kwa matumizi ilivyopangwa na kuidhinishwa na Halmashauri. Ni marufuku kwa mtu ye yote kusafisha Shamba kwa ajili ya kilimo kwa njia ya kuchoma moto isipokuwa kwa kibali maalum kutoka kwa Halmashauri. Kibali kitakachotolewa chini ya Sheria Ndogo hizi kitakuwa cha mandishi na kitaonyesha jina la mwenye kibali, tarehe na eneo analotaka kuchoma. ya (4) (3) (6) (5) Muda unaotakiwa kuchoma moto chini ya Sheria Ndogo hizi ni kuanzia saa 12:00 asubuhi hadi saa 4:00 asubuhi. Ni wajibu wa Halmashauri kusimamia shughuli za kilimo na kuhakikisha kuwa wanazuia kilimo cha kuhamahama na kuhimizi kilimo cha mzunguko (crops 7 Sheria Ndogo za (Hifadhi ya Mazingira) za Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Tangazo la Serikali Na. 26 (linaendelea) rotation). Uhifadhi wa uoto wa asili Uchimbaji mchanga na kokoto
Part
SEHEMU YA TATU
- 12 Verify source ↗
Ni wajibu wa wakazi wa eneo ambalo uoto wa asili au
AI-assisted research summary: Residents of an area with damaged natural vegetation or local environment must restore it to its normal state.
12. Ni wajibu wa wakazi wa eneo ambalo uoto wa asili au mazingira ya eneo husika yameharibiwa, kuhakikisha kuwa wanalirudisha katika hali yake ya kawaida kwa kupanda miti au kutoendelea kuharibu mazingira na kuwezesha uoto urudi katika hali yake ya awali. - 13 Verify source ↗
Ni marufuku kwa watu ye yote kuchimba mchanga
AI-assisted research summary: Ni marufuku kwa mtu yeyote kuchimba mchanga katika maeneo ambayo Halmashauri haijaruhusu, isipokuwa kama kuna ruhusa maalum ya Halmashauri.
13. Ni marufuku kwa watu ye yote kuchimba mchanga katika maeneo yasiyoruhusiwa na Halmashauri kama vile katika maeneo ya makazi ya watu, maeneo yaliyohifadhiwa kandokando ya mito au ndani ya mto, bwawa au ziwa isipokuwa kwa ruhusa maalum ya Halmashauri. Marufuku - 14 Verify source ↗
Ni marufuku kwa mtu ye yote kujenga Nyumba au
AI-assisted research summary: The by-laws prohibit harmful activities in protected areas, require the council and residents to protect trees and water sources, and impose fines or up to 12 months' imprisonment for breaches.
14. Ni marufuku kwa mtu ye yote kujenga Nyumba au Jengo lolote katika eneo la hifadhi. Wajibu wa kulinda vyanzo vya maji Kulinda eneo la hifadhi SEHEMU YA NNE HIFADHI YA VYANZO VYA MAJI 15 Halmashauri itawajibika kuanzisha, kusimamia na kulinda vyanzo vya maji. 16(1) Ni marufuku kwa mtu yeyote kulima, kukata miti, kuchanga mifugo katika katika umbali wa mita 60 toka vyanzo vya maji au kufanya jambo lolote linaloharibu kwa namna yoyote chanzo cha maji na hifadhi ya mazingira. (2) (3) Itakuwa ni wajibu wa Halmashauri kupanda miti isiyonyonya maji katika Vyanzo vya Maji kwa kuzingatia maelekezo ya Afisa Msitu. Ni marufuku kwa mtu yeyote kumiliki eneo la chanzo cha Maji isipokuwa Halmashauri. Uchafuzi wa vyanzo vya maji 17(1) Ni marufuru kwa mtu yeyote, Kiwanda, Taasisi, Shirika kuelekeza mabomba ya maji machafu kwenye mito mabwawa, ziwa, visima, mifereji, chemichemi au sehemu yo yote ambayo ni chanzo cha maji kwa ajili ya 8 Sheria Ndogo za (Hifadhi ya Mazingira) za Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Tangazo la Serikali Na. 26 (linaendelea) matumizi ya binadamu na wanyama au viumbe vingine vilivyo hai. (2) Ni marufuku mtu yeyote kuweka kitu chochote chenye sumu ndani ya maji ambayo yanatumiwa na binadamu au kiumbe cho chote hai. SEHEMU YA TANO HIFADHI YA MISITU Kuchoma au kusababisha moto 18(1) Ni marufuku kwa mtu yeyote kuchoma moto misitu kwa la ile katika misitu iliyoko eneo namna yoyote Halmashauri. (2) (3) Iwapo moto utatokea katika eneo la Halmashauri, Kiongozi wa eneo husika atawajibika kutoa ishara ya hatari kwa kutumia njia iliyozoeleka kuamuru wakazi wa eneo hilo kwenda kuzima moto huo unapoonekana kuwa na madhara kwa maisha, mali za watu na uharibifu wa mazingira katika eneo hilo. Kila mkazi wa eneo hilo atawajibika kushiriki katika zoezi la kuuzima moto huo endapo atatakiwa kufanya hivyo, na kama atashindwa kushiriki katika kuzima moto bila sababu ya msingi atakuwa ametenda kosa. Kibali cha kuchoma moto 19 Mtu ye yote aliyepata kibali cha kuchoma moto atalazimika kutoa taarifa ya siku saba (7) kabla ya kuchoma moto kwa majirani walioko katika eneo analotaka kuchoma moto na ataweka njia za kuzuia moto Ukataji miti 20(1) Ni marufuku kwa mtu yeyote kukata miti katika maeneo ya misitu iliyohifadhiwa kwa ajili ya matumizi ya aina yoyote bila kupata kibali kutoka Halmashauri. (2) Halmashauri itatakiwa kuhakiki kama miti inayovunwa imekomaa na inafaa kwa ajili ya matumizi husika. (3) Ni marufuku kwa mtu yeyote kuvuna miti katika msitu 9 Sheria Ndogo za (Hifadhi ya Mazingira) za Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Tangazo la Serikali Na. 26 (linaendelea) ambao umehifadhiwa kwa ajili ya viumbe maalumu amabao ni rasilimali kwa Taifa. (4) Watu wanao vuna miti ya kuchoma mkaa watatakiwa kuwa na eneo maalumu lililoidhinishwa na Halmashauri kwa ajili ya kuchoma mkaa. Wajibu wa kupanda miti 21 Kila mkazi wa Halmashauri atawajibika:- (a)Kupanda na kutunza miti katika eneo lake; (b)Kupanda na kutunza miti katika makazi yake; (c)Kupanda na kutunza miti katika shamba au mashamba anayomiliki Wajibu wa vijiji 22 Kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizi kila Kijiji; (a) Kitawajibika kutenga eneo la Hifadhi ya Msitu wa asili kwa ajili ya matumizi ya baadaye; (b) Kitalazimika kutunza miti yote inayopandwa katika eneo la kijiji; (c) Kitahakikisha kuwa kila kaya inapanda miti isiyopungua kumi kwenye eneo la nyumba yake; (d) Mtu yeyote atakayetaka kukata miti au mti kwa matumizi ya kuchonga vifaa, kujenga nyumba, kutengeneza zizi na shughuli zinginezo, itambidi apate kibali kutoka kwa cha maandishi Mwenyekiti wa Kijiji, Mtendaji wa Kijiji na Kibali cha Afisa Maliasili wa Wilaya au wasaidizi wake kwa miti iliyopandwa na kuhifadhiwa na Halmashauri; (e) kila shule au taasisi nyingine itapaswa kupanda miti kukinga upepo kuzunguka majengo yake na kuwa na shamba lilisopungua miti hekta mbili; (f) Kijiji kitapaswa kutunza na kuhifadhi miti na nyasi kwenye milima, makorongo na Vyanzo vingine vya maji ili kuzuia mmomonyoko wa udongo; (g) Kila Mwenyekiti wa Kitongoji, Mtendaji wa kijiji,au Mkuu wa Taasisi yoyote atahakikisha kuwa Kijiji au Taasisi ina msitu wa hifadhi ya miti iliyotengwa kwa ya kupandwa au ya asili 10 Sheria Ndogo za (Hifadhi ya Mazingira) za Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Tangazo la Serikali Na. 26 (linaendelea) madhumuni ya kuhifadhi Ardhi, Mazingira na matumizi ya baadaye. SEHEMU YA SITA TAKA NGUMU NA LAINI Utupaji wa taka ngumu na laini 23(1) Ni wajibu wa Halmashauri kutenga eneo kwa ajili ya kutupa taka ngumu na laini na kusimamia kwa karibu usafi katika eneo lake. (2) Mtu yeyote atakayetupa ovyo taka ngumu au laini, au kujisaidia katika kingo za maziwa, mabwawa au kwenye vyanzo vya maji vilivyoko katika Halmashauri atakuwa ametenda kosa. Uendeshaji wa viwanda 24 Ni marufuku kuendesha shughuli za karakana, mashine ya kusaga, kuranda mbao, kukamua maji ya matunda kuchomelea vyuma au kuendesha shughuli yo yote inayozalisha uchafu ambao unaleta athari kwa binadamu na viumbe wengi katika maeneo ya makazi ya watu bila kuzingatia taratibu za ujenzi. SEHEMU YA SABA MAKOSA NA ADHABU Makosa yanayohusu mifugo 25 Mtu ye yote atakuwa ametenda kosa ikiwa:- (a) ataingiza Mifugo katika eneo la Halmashauri bila kibali; (b) atasafirisha Mifugo bila kuwa na Kibali; (c) atalisha Mifugo katika maeneo yasiyoruhusiwa; (d) atafuga Mifugo zaidi ya idadi iliyoruhusiwa; (e) atavua Samaki kwa kutumia sumu au nyavu zenye matundu madogo. Makosa yanayohusu kilimo 26 Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya Kilimo, kuchimba Mchanga, katika maeneo Kokoto, Madini yasiyoruhusiwa na Halmashauri atakuwa ametenda kosa. 11 Sheria Ndogo za (Hifadhi ya Mazingira) za Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Tangazo la Serikali Na. 26 (linaendelea) Makosa yanayohusu Ardhi Makosa yanayohusu Maji 27 Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya kuhifadhi Ardhi atakuwa ametenda kosa. 28(1) Mtu yeyote atakayeharibu vyanzo vya maji au kushindwa kushiriki katika shughuli za kuhifadhi vyanzo vya maji atakuwa ametenda kosa. (2) Mtu ye yote atakayebainika kuwa ameweka sumu ya aina yo yote kwa namna yoyote ambayo itaathiri maisha ya binadamu na viumbe wengine ambao ni rasilimali ya Taifa atakuwa ametenda kosa. Makosa ya kuharibu misitu 29 atavuna Mazao ya misitu katika misitu Mtu ye yote atakuwa ametenda kosa ikiwa:- (a) atachoma au kusababisha moto katika misitu bila kibali au; (b) atashindwa kushiriki katika kuzima moto au; (c) iliyohifadhiwa na isiyohifadhiwa bila kibali au; (d) atachoma mkaa na kukata kuni bila kibali au; (e) atafyeka nyasi, kung’oa vichaka na visiki kwenye misitu bila kibali; (f) atachoma au kusababisha moto katika msitu bila kibali; (g) atachunga mifugo kwenye eneo lo lote lililopandwa miti au iliyohifadhiwa kama bustani ya miti; (h) atakata miti au kuchungia mifugo kwenye miti iliyopandwa kwa ajili ya kuzuia mmomonyoko wa udongo au kinga upepo; (i) atalima au kukata miti katika vyanzo vya maji, mlima, kando ya njia, makorongo na sehemu nyingine zozote zilizohifadhiwa ili kupunguza mmomonyoko wa udongo. Makosa yanayohusu taka ngumu na laini Makosa yanayohusu taka za majimaji 30 Mtu yeyote atakayetupa ovyo taka ngumu au laini katika maeneo yoyote yasiyoruhusiwa na Sheria Ndogo hizi au Sheria nyingine yo yote iliyotungwa na Bunge la Jamhuri ya Mungano wa Tanzania atakuwa ametenda kosa. 31 Mtu yoyote atakayetiririsha maji machafu yanayoleta madhara kwa binadamu na viumbe vingine hai atakuwa ametenda kosa. 12 Sheria Ndogo za (Hifadhi ya Mazingira) za Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Tangazo la Serikali Na. 26 (linaendelea) Makosa yanayohusu viwanda Adhabu 32 Mtu yeyote atakayeendesha shughuli za kiwanda au viwanda vidogo, karakana, mashine za kusaga na kukoboa nafaka, mashine za kuranda mbao katika makazi ya watu bila kuzingatia taratibu za mipango miji atakuwa ametenda kosa. 33 Mtu yeyote atakayekwenda kinyume na masharti ya Sheria Ndogo hizi atakuwa ametenda kosa na akipatikana na hatia atatozwa faini isiyozidi shilingi laki tatu (300,000/=) au kifungo kisichozidi miezi kumi na mbili au vyote kwa pamoja yaani faini na kifungo. Nembo ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlele imebandikwa katika Sheria hizi Ndogo kutokana na Azimio la kikao cha Halmashauri ya Wilaya ya Mlele kilichoketi tarehe 17 mwezi 07 mwaka 2015 na lakiri imebandikwa mbele ya:- GODWIN L. BENNE, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mlele. DUES J. BUNDALA, Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya Mlele. NAKUBALI, Dodoma, 09 Januari, 2017 GEORGE B. SIMBACHAWENE (MB) Waziri wanchi-or-Tamisemi. 13
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo za (Hifadhi ya Mazingira) za Halmashauri ya Wilaya ya Mlele, 2017
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in