Sheria Ndogo za (Uanzishaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii) za Halmashauri ya Wilaya ya Mlele 2017
This section names the by-laws and says they begin to apply after publication in the Government Gazette.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo za (Uanzishaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii) za Halmashauri ya Wilaya ya Mlele 2017
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This section names the by-laws and says they begin to apply after publication in the Government Gazette. This provision says the by-laws apply throughout the area under the authority of Mlele District Council. This section defines the main terms used in the by-laws. A voluntary Community Health Fund is established to provide health services, with households paying for the services and the government adding a financial contribution. The Fund’s purpose is to raise money from the community to provide better health services for its members, improve health services through sustainable plans, and strengthen community participation in health decisions.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo za (Uanzishaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii) za Halmashauri ya Wilaya ya Mlele 2017
Showing 27 of 27
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hizi zitaitwa Sheria Ndogo za (Uanzishaji wa
AI-assisted research summary: This section names the by-laws and says they begin to apply after publication in the Government Gazette.
1.Sheria Ndogo hizi zitaitwa Sheria Ndogo za (Uanzishaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii) za Halmashauri ya Wilaya ya Mlele 2017 na zitaanza kutumika baada ya kutangazwa kwenye Gazeti la Serikali. - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hizi zitatumika katika eneo lote lililo chini ya
AI-assisted research summary: This provision says the by-laws apply throughout the area under the authority of Mlele District Council.
2.Sheria Ndogo hizi zitatumika katika eneo lote lililo chini ya mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlele. - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hizi isipokuwa itakapoelezwa vinginevyo
AI-assisted research summary: This section defines the main terms used in the by-laws.
3.Katika Sheria Ndogo hizi isipokuwa itakapoelezwa vinginevyo:- “Ada ya Mtumiaji” maana yake ni ada inayotozwa na Hospitali, kituo cha afya au zahanati, kwa ajili ya huduma ya afya inayotolewa kwa mtumiaji; “Asasi” maana yake ni pamoja na shule, vyuo, vikundi mbalimbali vilivyosajiliwa kwa mujibu wa Sheria au asasi yoyote itakayokuwa imekubaliwa na kuidhinishwa na Bodi; Sura ya 287 “Bodi’’ maana yake ni Bodi ya Huduma za Afya ya Halmashauri iliyoundwa chini ya Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Sura ya 287; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Mlele; “Huduma za afya” maana yake ni huduma zote za afya zinazotolewa na hospitali za Serikali na watu binafsi, na zinajumuisha huduma nyingine za afya zilizoanzishwa kwa madhumuni ya kutoa huduma za afya ikiwa ni pamoja na vituo vya 1 Sheria Ndogo za (Uanzishaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii) za Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Tangazo la Serikali Na.27 (linaendelea) afya na Zahanati; “Kadi” maana yake ni kadi mwanachama wa Mfuko wa Afya ya Jamii. itakayotolewa na Bodi kwa “Kaya” maana yake ni : (a) mama, baba, watoto wenye umri chini ya miaka kumi na nane; (b) mwanachama yeyote aliyefikisha umri wa miaka kumi na nane au zaidi na awe na mtoto au bila mtoto mwenye umri wa miaka kumi na nane; (c) Taasisi au asasi yoyote. “Kituo cha huduma kilichoteuliwa” maana yake ni kituo kinachotoa huduma za afya na ni pamoja na kituo chochote kilichoanzishwa au kinachoendeshwa kwa malengo ya kutoa huduma za afya kiwe kinamilikiwa na Halmashauri, Serikali, asasi ya kidini, mtu au watu binafsi ambacho kinahusika na mfuko wa Afya ya Jamii. “Malipo ya huduma” maana yake ni malipo yanayotozwa na kituo cha tiba, kilichoteuliwa kwa watu ambao sio wanachama, wanapopatiwa huduma za afya katika kituo hicho; “Mchango au ada ya mwanachama” maana yake ni mchango wa hiari utakaotolewa na wanachama wa Mfuko wa Afya ya Jamii; “Mfuko au Mfuko wa Afya ya Jamii” (CHF) maana yake ni mfuko wa afya ya jamii ulioanzishwa chini ya Sheria Ndogo hizi. “Mganga Mkuu wa Wilaya” maana yake ni daktari ambaye ni msimamizi mkuu wa shughuli za huduma za afya katika Halmashauri. “Mwanachama” maana yake ni kaya inayochangia kwenye Mfuko wa Afya ya Jamii; “Tele kwa Tele” maana yake ni mkataba unaoeleza wajibu wa Halmashauri wajibu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii katika 2 Sheria Ndogo za (Uanzishaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii) za Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Tangazo la Serikali Na.27 (linaendelea) utekelezaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii. - 4 Verify source ↗
Section 4
AI-assisted research summary: A voluntary Community Health Fund is established to provide health services, with households paying for the services and the government adding a financial contribution.
4. (1) Mfuko wa Afya ya Jamii Kutakuwa na Mfuko wa Afya wa Jamii ambao ni mfuko wa hiari wenye lengo la kutoa huduma za afya, ambapo kaya zitakuwa zikilipia huduma hizo na Serikali itatoa mchango wake wa fedha kama jazilio kwa mchango kutoka kwenye kaya; (Tele kwa Tele) Madhumu ni ya Mfuko (2) Matumizi ya fedha yatafanywa na kusimamiwa na Bodi kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizi. - 5 Verify source ↗
Section 5
AI-assisted research summary: The Fund’s purpose is to raise money from the community to provide better health services for its members, improve health services through sustainable plans, and strengthen community participation in health decisions.
5. Madhumuni ya Mfuko yatakuwa ni: (a) Kutafuta vyanzo vya fedha kutoka katika jamii kwa ajili ya kutoa huduma bora za afya kwa wanachama; (b) Kutoa huduma bora za afya zinazopatikana kwa kutumia mipango endelevu; na (c) Kuboresha huduma za afya katika jamii kwa kugawanya madaraka na kuzipa nguvu jamii katika kufanya maamuzi na kuchangia katika masuala yanayohusu afya zao. - 6 Verify source ↗
Section 6
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima iwe na Mratibu wa Mfuko wa Afya ya Jamii, na mteule huyo husimamia shughuli za mfuko na kuandaa ripoti za robo mwaka na mwaka.
6. (1) Mratibu wa Mfuko wa Afya ya Jamii Kutakuwa na Mratibu wa Mfuko wa Afya ya Jamii wa Halmashauri atakayeteuliwa na Mkurugenzi baada ya kupokea mapendekezo kutoka Timu ya Wataalam wa Afya wa Halmashauri (CHMT). (2) Majukumu ya Mratibu wa Mfuko wa Afya ya Jamii yatakuwa kama ifuatavyo;- (a) Kufuatilia, kusimamia na kuratibu uendeshaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii kwenye vituo vya kutolea Huduma za Afya ya Jamii kwa kiwango kati ya Halmashauri, Jamii na wadau mbalimbali kwa ushirikiano na mhasibu wa Mfuko; na 3 Sheria Ndogo za (Uanzishaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii) za Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Tangazo la Serikali Na.27 (linaendelea) (b) Kuandaa taarifa za Mfuko wa Afya ya Jamii za robo mwaka na mwaka kwa kushirikiana na mhasibu wa Mfuko, pamoja na majukumu mengine atakayopangiwa na Halmashauri. Muundo wa Bodi - 7 Verify source ↗
Section 7
AI-assisted research summary: This section sets out who must be on the Board and which members may vote in Board decisions.
7. (1) Bodi itakuwa na wajumbe wafuatao;- (a) Wawakilishi wanne wa watumiaji huduma za lazima wawe ni afya kati yao wawili ni wanawake. (b) Mwakilishi mmoja kutoka watoa huduma za Afya binafsi bila faida na (c) Mwakilishi mmoja kutoka watoa huduma za Afya kwa faida waliochaguliwa na Halmashauri kutoka vituo vya kutolea huduma za afya binafsi kwa faida waliochaguliwa miongoni mwao. (d) Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu, Afya na Maji. (e) Afisa Mipango wa Halmashauri (f) Mganga Mkuu wa Halmashauri ambaye atakuwa Katibu wa Bodi. (g) Mwakilishi mmoja na Mwakilishi mmoja kutoka Timu ya Uendeshaji wa Huduma za Afya ya Mkoa. kutoka Hospitali (2) Mwenyekiti wa Bodi atachaguliwa kutoka miongoni mwa wajumbe waliotajwa katika aya (a)-(c) hapo juu. (3) Wajumbe waliotajwa katika aya (a)-(d) mbali na wajumbe waliotajwa katika aya (e)- (g) za kifungu kidogo cha (1) watakuwa na haki ya kupiga kura katika maamuzi ya Bodi. Kazi za Bodi - 8 Verify source ↗
Section 8
AI-assisted research summary: Bodi ya Mfuko wa Afya ya Jamii ina majukumu ya kusimamia mfuko, mapato yake, mipango ya afya, na kutekeleza maagizo ya Halmashauri; pia mjumbe wa bodi lazima akidhi masharti fulani ya uraia, umri, elimu, uzoefu na uanachama.
8. Ili kufanikisha malengo yake makuu, Bodi itakuwa na kazi zifuatazo:- (a) itasimamia masuala na shughuli zote zinazohusu Mfuko wa Afya ya Jamii; 4 Sheria Ndogo za (Uanzishaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii) za Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Tangazo la Serikali Na.27 (linaendelea) (b) itafanya kazi kwa kushauriana na Timu ya Uendeshaji ya Huduma za Afya ya Halmashauri na kuhakikisha kuwa huduma ya afya inayotolewa ni bora na ya kitaalamu; (c) kukusanya na kusimamia mapato ya Mfuko wa Afya ya Jamii. (d) kupendekeza kwa Halmashauri watu wanaostahili kusamehewa kutoa mchango kwenye Mfuko (e) kuweka malengo ya Mfuko. (f) kupitia ripoti na taarifa kutoka Kamati ya Afya ya Kata au chanzo kingine chochote. (g) kuratibu makusanyo, matumizi na kudhibiti mapato na; (h) kupanga mipango ya afya ya mwaka kwa ajili ya kuthibitishwa na Halmashauri. (i) kupanua na kuongeza utoaji wa huduma za afya kwa wanachama kulingana na mapato ya mfuko; (j) Bodi katika kutekeleza majukumu yake, itapokea na kutekeleza maagizo ya Halmashauri kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na taratibu Mjumbe wa Bodi atakuwa na sifa zifuatazo;- (a) Awe Raia wa Tanzania isipokuwa kwa wawakilishi kutoka katika Taasisi zisizo za Kiserikali. (b) awe na umri si chini ya miaka ishirini na tano na si zaidi ya miaka sabini; (c) awe amehitimu elimu ya Sekondari na kuendelea; (d) awe na uzoefu na amewahi kuonyesha uwezo wake wa kuongoza katika shughuli za huduma jamii; (e) awe na sifa za uongozi; na (f) Asiwe na wadhifa wowote wa kisiasa kupitia chama chochote cha siasa. (g) Awe mwanachama hai wa Mfuko wa Afya ya Jamii au Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya. - 9 Verify source ↗
Section 9
AI-assisted research summary: Kifungu hiki kina kichwa kuhusu sifa za wajumbe wa bodi na kinaanza kutaja muda wa kukaa madarakani, lakini maandishi yaliyotolewa hayajakamilika.
9. Sifa za wajumbe wa bodi Muda wa kukaa madaraka ni - 10 Verify source ↗
Section 10
AI-assisted research summary: Mjumbe wa Bodi hutumikia kwa miaka mitatu kuanzia tarehe ya kuchaguliwa, na anaweza kuchaguliwa tena kwa miaka mitatu tu. Nafasi iliyo wazi ya mjumbe wa Bodi inapaswa kujazwa kwa kumchagua mjumbe mwingine, isipokuwa hali fulani na pale kipindi kilichobaki ni chini ya miezi sita.
10. (1) Mjumbe wa Bodi atakuwa madarakani kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia tarehe aliyochaguliwa na anaweza kuchaguliwa tena kwa kipindi cha miaka mitatu tu. 5 Sheria Ndogo za (Uanzishaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii) za Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Tangazo la Serikali Na.27 (linaendelea) (2) Endapo nafasi yeyote ya mjumbe wa Bodi itaachwa wazi kwa sababu ya kifo, kujiuzulu, kukiuka maadili ya kazi au ulemavu utakaomfanya ashindwe kushiriki kikamilifu kama mjumbe au kwa sababu nyingine yeyote ile, mjumbe mwingine atachaguliwa kujaza nafasi hiyo iliyoachwa wazi. (3) Bila ya kuathiri masharti ya kifungu kidogo cha (2), iwapo haitaruhusiwa kuchagua mjumbe mwingine kipindi kilichobaki ni chini ya miezi sita. Mikutano ya Bodi - 11 Verify source ↗
Section 11
AI-assisted research summary: Mwenyekiti lazima aitishe mikutano ya kawaida ya Bodi kila robo mwaka, na anaweza kuitisha kikao cha dharula ikiwa kuna umuhimu.
11. (1) Mikutano ya kawaida ya Bodi itaitishwa na Mwenyekiti kila robo mwaka. (2) Ikiwa kuna umuhimu, mwenyekiti anaweza akaitisha kikao cha dharula kulingana na mahitaji maalumu. Uwajibik aji wa Bodi. - 12 Verify source ↗
Section 12
AI-assisted research summary: The Council (Halmashauri) is responsible for the matter through the relevant board committee.
12. itawajibika kwa Halmashauri kupitia Kamati Bodi husika. Vyanzo vya Mapato - 13 Verify source ↗
Section 13
AI-assisted research summary: This section lists the sources of income for the Fund.
13. Vyanzo vya mapato ya Mfuko vitatokana na:- (a) Fedha zote zitakazopokelewa kutokana na michango ya wanachama; (b) Ruzuku kutoka kwenye Halmashauri, Serikali Kuu, na wahisani mbalimbali toka ndani na nje ya Halmashauri; (c) Michango ya watu binafsi wanaoishi ndani na nje ya Halmashauri (d) Malipo ya fedha ya wasiokuwa wanachama wa Mfuko kwa kupata huduma ya afya. (e) Ushuru utakaotozwa na Halmashauri kutoka vyanzo mbalimbali na kutengwa kwa ajili ya Mfuko; na (f) Fedha zozote halali ambazo Mfuko unaweza kupata toka mahali pengine popote. 6 Sheria Ndogo za (Uanzishaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii) za Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Tangazo la Serikali Na.27 (linaendelea) (g) Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (h) Fedha zozote halali ambazo mfuko unaweza kupata kutoka mahali pengine popote Akaunti ya mfuko wa Bodi na watiaji saini - 14 Verify source ↗
Section 14
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima itumie akaunti maalumu kwa Mfuko, malipo yajadhibitiwe na Mkurugenzi, na fedha zisitolewe bila saini inayotakiwa.
14. (1) Kutakuwepo na akaunti maalumu itakayotumika na Halmashauri ambayo fedha zote zitakazokusanywa kwa ajili ya Mfuko zitahifadhiwa na kutolewa (2) Malipo yataidhinishwa na Mkurugenzi kwa kufuata taratibu za kanuni za fedha za Halmashauri. (3) Watia saini wa akaunti ya Mfuko watachaguliwa na Bodi na watakuwa ni mmoja kutoka kundi “A” na “B” na kwa namna yoyote hakuna pesa zitakazotolewa kwenye akaunti ya mfuko bila saini ya mmojawapo kutoka kundi “A” na “B” (4) Watia saini kwenye hundi za Mfuko watakuwa kama ifuatavyo:- (a) Mwenyekiti wa Bodi na mjumbe mmoja wa Bodi ambao watakuwa Kundi “A” (b) Katibu wa Bodi (Mganga Mkuu) na Mweka Hazina wa Halmashauri watakuwa Kundi “B” (5) Kila baada ya miezi mitatu, Bodi itakuwa inatoa taarifa ya akaunti ya Mfuko kwa Halmashauri; (6) Akaunti ya Mfuko na wakaguzi waliochaguliwa kwa mujibu wa Kanuni za fedha za Serikali za Mitaa. itakaguliwa - 15 Verify source ↗
Section 15
AI-assisted research summary: Bodi lazima iandae na kuwasilisha taarifa ya mapato na matumizi ya fedha ya mwaka kwa Halmashauri ndani ya mwezi mmoja baada ya mwaka wa fedha wa Halmashauri.
15. Taarifa ya fedha ya mwaka Mwezi mmoja baada ya mwaka wa fedha wa Halmashauri, Bodi itatakiwa kuandaa taarifa ya mapato na matumizi ya fedha ya mwaka na kuwasilisha kwa Halmashauri. 7 Sheria Ndogo za (Uanzishaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii) za Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Tangazo la Serikali Na.27 (linaendelea) - 16 Verify source ↗
Section 16
AI-assisted research summary: Bodi must prepare the annual budget two months before the council fiscal year starts, may prepare a supplementary budget if needed and conditions allow, and submit the fund budget plan to the Halmashauri for discussion and decision.
16. Mipango na Matumizi (1) Miezi miwili kabla ya kuanza kwa mwaka wa fedha wa Halmashauri, Bodi itaandaa mipango na bajeti ya mwaka kwa kuonyesha kiwango kinachotarajiwa kupatikana na mgawanyo wa fedha kwa ajili ya utoaji huduma za afya na maendeleo katika maeneo ya Halmashauri. (2) Bodi inaweza kuandaa bajeti ya nyongeza kama kutakuwa na haja ya kufanya hivyo na kama mazingira yataruhusu (3) Mipango ya bajeti ya Mfuko itaandaliwa kulingana na utaratibu kama ilivyoainishwa katika vifungu vidogo vya (1) na (2) hapo juu, ambayo ni lazima iwasilishwe kwa Halmashauri kwa ajili ya kujadiliwa na kutolewa maamuzi. (4) Matumizi yatazingatia mipango shirikishi ya maeneo husika ambayo itakuwa sehemu ya Mpango kabambe wa afya wa Halmashauri. Pia mipango hii itazingatia maelezo yaliyomo ndani ya Mkataba wa Tele kwa Tele. Usimamizi na uendeshaji wa Mfuko utakuwa chini ya :- (a) Halmashauri kupitia Bodi ya huduma za Afya ya Halmashauri katika ngazi ya Halmashauri. (b) Kamati ya Maendeleo ya Kata kupitia Kamati ya afya ya Kata, katika ngazi ya Kata; na (c) Serikali ya Kijiji kupitia Kamati ya Huduma za Jamii katika ngazi ya Kijiji. - 17 Verify source ↗
Section 17
AI-assisted research summary: Kipengele hiki kinaonyesha mada ya usimamizi wa Mfuko na Kamati ya Afya ya Kata, pamoja na wajumbe wake.
17. Usimam- izi wa Mfuko Kamati ya Afya ya kata Wajumbe wa Kamati ya Afya ya Kata - 19 Verify source ↗
Section 19
AI-assisted research summary: The Ward Health Committee must include the listed members, and the council may warn or dissolve it if it fails to perform its duties.
19. (1) Kamati ya Afya ya Kata itakuwa na wajumbe wafuatao:- (a) Diwani anayewakilisha Kata husika. (b) Afisa Mtendaji wa Kata; (c) Mwalimu Mkuu mmoja kutoka shule ya 8 Sheria Ndogo za (Uanzishaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii) za Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Tangazo la Serikali Na.27 (linaendelea) msingi na mmoja kutoka shule ya Sekondari ambayo ipo kwenye Kata husika; (d) Wajumbe wawili wanawakilisha jamii husika ambapo mmoja wao ni lazima awe mwanamke. (e) Mganga au Mganga Msaidizi wa Kituo cha Afya, ambaye atakuwa Katibu wa Kamati. (f) Mjumbe mmoja atakayeteuliwa na Kamati ya Maendeleo ya Kata kutokana na watu waliopendekezwa na Serikali za Mitaa zilizomo ndani ya eneo la Kata; na (g) Mjumbe mmoja atakayeteuliwa na Kamati ya Maendeleo ya Kata kutoka kwenye vyama vya kijamii kutoka kwenye Kata. Kazi na Majuku- mu ya Kamati ya Afya ya Kata (2) Mwenyekiti wa Kamati ya Afya ya Kata atachaguliwa kutoka miongoni mwa wajumbe. (3) Endapo Kamati ya Afya ya Kata itashindwa kutekeleza kazi zake, Halmashauri itatoa onyo au kuivunja na kufanya utaratibu wa uchaguzi wa wajumbe wengine katika muda usiozidi miezi mitatu. - 20 Verify source ↗
Section 20
AI-assisted research summary: Kamati ya Afya ya Kata must carry out listed health fund duties, meet every three months, and the secretary must give a written report one week before each meeting and send a meeting summary after the meeting.
20. (1) Kamati ya Afya ya Kata itakuwa na majukumu yafuatayo:- (a) Kuwahamasisha na kuandaa jamii kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii. (b) Kuandaa orodha na kuratibu idadi ya wajumbe wa Mfuko wa Jamii. (c) Kusimamia ukusanyaji wa michango ya Mfuko. uchangiaji kwenye (d) Kuratibu viwango vya huduma za afya; (e) Kupitia utendaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii na kutoa mapendekeo ya ufumbuzi; (f) Kuanzisha na kuratibu mipango ya Afya ya Jamii na; (g) Kuendesha mikutano ya wajumbe wa Mfuko wa Afya ya Jamii 9 Sheria Ndogo za (Uanzishaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii) za Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Tangazo la Serikali Na.27 (linaendelea) (2) Kamati ya Afya ya Kata, itakaa kila baada ya miezi mitatu, na Katibu atatoa taarifa ya maandishi wiki moja kabla ya siku ya Kikao. (3) Baada ya kikao Katibu atawasilisha muhtasari wa kikao hicho kwa Katibu wa Mfuko wa Halmashauri. - 21 Verify source ↗
Section 21
AI-assisted research summary: Fedha za Mfuko zinapaswa kutumika kwa madhumuni ya afya yaliyoidhinishwa na Wizara au Bodi.
21. Matumizi ya fedha za Mfuko Fedha zitakazokusanywa na Mfuko zitatumika kwa madhumuni yafuatayo:- (a) Masuala yanayohusiana na afya yaliyotajwa katika mpango wa afya na kuidhinishiwa na Wizara; na (b) Suala au shughuli yoyote muhimu ya afya kama itakavyoonekana inafaa na kama itaidhinishwa na Bodi - 22 Verify source ↗
Section 22
AI-assisted research summary: Wanachama wa Mfuko na wategemezi wao hupata kadi baada ya kulipa mchango wa mwaka; mwanachama aliyepewa msamaha hupata kadi ya uanachama, na Halmashauri lazima iandae utaratibu wa kulipia kadi hiyo.
22. Utoaji wa Kadi kwa wanacha ma (1) Kila mwanachama wa Mfuko na wategemezi wake, atapewa Kadi baada ya kulipa mchango wake wa mwaka kama ilivyoainishwa katika kifungu cha 24(1) cha Sheria Ndogo hizi Haki za mwanach ama na Utoaji wa Huduma za afya (2) Kwa kuzingatia kanuni za Mfuko wa afya ya jamii kila mwanachama atakayepewa msamaha ni lazima atapewa kadi ya uanachama na Halmashauri itaweka utaratibu wa kulipia kadi hiyo. - 23 Verify source ↗
Section 23
AI-assisted research summary: Wanachama na wategemezi wao wana haki za kupata huduma za afya, kutoa mapendekezo, na kushirikishwa katika mipango ya huduma za afya.
23. Kila mwanachama na wategemezi wake watakuwa na haki zifuatazo: (a) Kupata huduma ya afya aliyolipia anapougua ndani ya eneo la Halmashauri husika au katika kituo cha Afya kwenye Halmashauri nyingine itaingia makubaliano maalum na ambayo Halmashauri husika. (b) Kupata huduma ya afya kwa baba, mama na watoto wao wenye umri chini ya miaka kumi na nane; 10 Sheria Ndogo za (Uanzishaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii) za Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Tangazo la Serikali Na.27 (linaendelea) (c) Kutoa mapendekezo kuhusu huduma za afya kupitia kituo chake cha tiba ambayo yatafanyiwa kazi na Bodi; na (d) Kushirikishwa kikamilifu katika uandaaji na utekelezaji wa mpango wa upatikanaji wa huduma za afya, katika eneo la Halmashauri Kiwango cha mchango au ada ya mwanach ama - 24 Verify source ↗
Section 24
AI-assisted research summary: Anyone who wants to join the community health fund must pay TZS 10,000 each year. The council must also prepare a procedure for grouping certain households in local institutions or schools so they can access the fund’s services.
24. (1) (a) Mtu yeyote atakayetaka kuwa mwanachama wa mfuko wa afya ya jamii atapaswa kutoa kiasi cha shilingi elfu kumi (10,000) kila mwaka. (b) Mchango huo utalipwa na kila mtu anayetaka kuwa mwanachama wa mfuko mwanzoni mwa mwaka au kila mwaka wa fedha unapoanza au kama Bodi itakavyoelekeza. (c) Mtu yeyote ana hiari ya kulipa mchango wake wa uanachama kwa zaidi ya mwaka mmoja; (2) Bila kuathiri kifungu cha 24 (c) hapo juu mtu yeyote anayelipa mchango wa uanachama kwa zaidi ya mwaka mmoja, pale inapotokea mabadiliko ya kiwango cha mchango atawajibika kulipa tofauti ya kiwango kilichozidi kile cha awali. (3) Halmashauri itaandaa utaratibu wa kupanga kaya maalum zilizoko katika Taasisi/Shule mbalimbali zilizo ndani ya Halmashauri ili kuziwezesha kupata huduma ya mfuko wa Afya ya jamii. - 25 Verify source ↗
Section 25
AI-assisted research summary: Uanachama wa Mfuko wa Afya ya Jamii unaendelea mtu anapolipa ada yake ya mwaka; vinginevyo, uanachama unaisha kila mwaka hadi masharti ya kifungu cha 25(a) yatimizwe.
25. Muda wa uanach- ama (a) Mtu yeyote atabaki kuwa mwanachama wa Mfuko wa Afya ya Jamii wa kila atakapolipa ada yake ya mwaka. (b) Kila mwaka unapoisha uanachama wa mtu utafikia mwisho hadi pale atakapotimiza masharti ya kifungu cha 25 (a) hapo juu. Malipo ya papo kwa papo - 26 Verify source ↗
Section 26
AI-assisted research summary: Mtu asiye mwanachama wa mfuko huu lazima alipie mchango au malipo ya papo kwa papo anapokwenda kupata matibabu katika kituo cha afya.
26. (1) Mtu yeyote ambaye hatakuwa mwanachama wa mfuko huu, atalipa mchango au malipo ya papo kwa papo kila 11 Sheria Ndogo za (Uanzishaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii) za Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Tangazo la Serikali Na.27 (linaendelea) atakapoenda kupata matibabu katika kituo cha kutolea huduma za Afya. (2) Malipo ya papo kwa papo yatalipwa kama ifuatavyo; (a) Shilingi elfu moja (1,000/=) katika huduma za afya zinazotolewa na Zahanati katika eneo lolote la Halmashauri. (b) Shilingi elfu moja mia tano (1,500) kwa huduma za Afya zinazotolewa na kituo cha Afya kilichopo ndani ya Halmashauri. (c) Huduma za Hospitali za aina zote kulingana na Sera ya uchangiaji. - 27 Verify source ↗
Section 27
AI-assisted research summary: People unable to pay medical costs may receive an exemption paid by the Council after the listed local review steps are followed.
27. Misamaha kwa wasiojiwez a Misamaha kwa wasioweza kulipa gharama za matibabu itatolewa na kulipwa na Halmashauri baada ya kuzingatia utaratibu ufuatao;- (a) uongozi wa Kitongoji utawatambua, kuwaorodhesha na kuwasilisha majina ya wasio na uwezo wa kulipa gharama za matibabu katika Serikali ya Kijiji; (b) Serikali ya Kijiji katika vikao vyake itapokea, itajadili na kuwasilisha orodha sahihi kwenye Kamati ya Maendeleo ya Kata; (c) Kamati ya Maendeleo ya Kata itapokea,itajadili na kuwasilisha orodha sahihi ya wasioweza kulipa gharama za matibabu kwa Bodi ya Afya ya Halmashauri; na (d) Bodi ya Afya itapokea, na kujadili mapendekezo husika na kuyawasilisha pamoja na gharama zake kwa Halmashauri kwa ajili ya kujadiliwa na kutolewa maamuzi. Makosa - 28 Verify source ↗
Section 28
AI-assisted research summary: Mtu yeyote anayekiuka masharti ya Sheria Ndogo hizi, kuzuia kazi za Bodi, kutumia vibaya mali au madaraka ya Mfuko, au kushindwa kwa uzembe kutekeleza wajibu wake anaweza kukutwa na kosa.
28. Itakuwa ni makosa kwa mtu yeyote ambaye; (a) Atakwenda kinyume na masharti ya Sheria Ndogo hizi; au (b) Atafanya kitendo chochote ambacho kitazuia Bodi kufanya kazi zake kwa ufanisi; au (c) Atatumia vibaya mali na rasilimali za Mfuko na 12 Sheria Ndogo za (Uanzishaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii) za Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Tangazo la Serikali Na.27 (linaendelea) Adhabu 29 kusababisha kutofikia malengo ya Bodi; au (d) Atatumia vibaya madaraka aliyonayo kumzuia afisa wa Bodi kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria hii; (e) Atashindwa kwa uzembe kutekeleza wajibu wake kwa mujibu wa Sheria ndogo hizi. Mtu yeyote atakayekwenda kinyume na masharti ya Sheria Ndogo hizi atakuwa ametenda kosa na akipatikana na hatia atatozwa faini isiyozidi shilingi laki tatu (300,000/=) au kifungo kisichozidi miezi kumi na mbili au adhabu zote mbili kwa pamoja yaani faini na kifungo Nembo ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlele imebandikwa katika Sheria hizi Ndogo kutokana na Azimio la kikao cha Halmashauri ya Wilaya ya Mlele kilichoketi tarehe 17 mwezi 07 mwaka 2015 na lakiri imebandikwa mbele ya:- GODWIN L. BENNE, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mlele. DUES J. BUNDALA, Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya Mlele. NAKUBALI, Dodoma, 09 Januari, 2017 GEORGE B. SIMBACHAWENE (MB) Waziri wanchi-or-Tamisemi. 13 Sheria Ndogo za (Uanzishaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii) za Halmashauri ya Wilaya ya Mlele Tangazo la Serikali Na.27 (linaendelea) 14
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo za (Uanzishaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii) za Halmashauri ya Wilaya ya Mlele 2017
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in