Sheria Ndogo za (Ufugaji wa nyuki) za Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma za Mwaka 2017
These by-laws are called the Kigoma District Council Beekeeping By-laws, 2017, start after publication in the Government Gazette, and apply throughout the council area.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo za (Ufugaji wa nyuki) za Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma za Mwaka 2017
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
These by-laws are called the Kigoma District Council Beekeeping By-laws, 2017, start after publication in the Government Gazette, and apply throughout the council area. Halmashauri must carry out several duties to promote and develop modern beekeeping. Serikali ya Kijiji yenye wakazi wanaofuga nyuki lazima itenge maeneo ya ufugaji, iweke daftari la wafugaji, ianzishe miradi ya nyuki, ihamasishe uhifadhi wa mazingira na ufugaji bora, itunge sheria ndogo, na idhibiti uharibifu au wizi wa mizinga na mazao ya nyuki. Afisa Nyuki ana wajibu wa kusimamia masuala ya nyuki katika wilaya, kata au kijiji na kutekeleza majukumu mbalimbali ya uongozi, mafunzo, ufuatiliaji, na utekelezaji wa sheria. Kila mfugaji wa nyuki lazima atimize wajibu uliotajwa, ikiwemo kufuata masharti ya Sheria Ndogo hizi.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo za (Ufugaji wa nyuki) za Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma za Mwaka 2017
Showing 9 of 9
- 3 Verify source ↗
Section 3
AI-assisted research summary: These by-laws are called the Kigoma District Council Beekeeping By-laws, 2017, start after publication in the Government Gazette, and apply throughout the council area.
3. Sheria Ndogo hizi zitaitwa Sheria Ndogo za (Ufugaji wa nyuki) za Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma za Mwaka 2017 na zitaanza kutumika baada ya kutangazwa kwenye Gazeti la Serikali. Sheria Ndogo hizi zitatumika katika eneo lote la mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma. isipokuwa kama Katika Sheria Ndogo hii vinginevyo- “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni Afisa yeyote wa Halmashauri atakayeteuliwa kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hizi; itahitajika “Afisa Nyuki” maana yake ni mtaalamu wa Nyuki atakayekuwa na jukumu la usimamizi wa masuala ya ufugaji nyuki na biashara ya mazao ya nyuki katika eneo la Halmashauri; “Chama cha Ushirika” maana yake ni sawa na tafsiri iliyoko kwenye Sheria ya Vyama vya Ushirika; “Eneo la Ufugaji wa Nyuki” maana yake ni eneo lililokubaliwa au kutangazwa kutumika kwa ajili ya ufugaji wa Nyuki; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma; “Kibali” maana yake ni idhini ya maandishi inayotolewa na Halmashauri kwa ajili ya utekelezaji wa Sheria Ndogo 1 Sheria Ndogo za (Ufugaji wa nyuki) za Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Tangazo la Serikali Na. 99 (linaendelea) hizi; “Kilimo” maana yake ni shughuli yoyote ya uzalishaji mali inayofanywa na binadamu na itajumuisha kilimo cha mazao, ufugaji wa wanyama, samaki, nyuki na uvuvi. “Kituo cha Kukusanyia Mazao ya Nyuki” maana yake ni eneo lililokubaliwa na kuidhinishwa kutumika kwa ajili ya kukusanyia, kuchakatia, kufungasha, kuhifadhi, kuuza au kununua mazao ya nyuki. “Kundi la Nyuki” maana yake ni jamii ya nyuki wa asali wenye mchanganyiko wa Malkia mmoja, nyuki vibarua na madume. “Mazao ya Nyuki” maana yake ni Mazao yote yanatokana na ufugaji wa nyuki ambayo ni Asali, Nta, Ngundi ya Nyuki, Sumu ya nyuki, Maziwa ya Nyuki, Masega, na Chavua. “Mifugo” maana yake ni Ng’ombe, Mbuzi, Kondoo, Mbwa au wanyama wote wafugwao na binadamu. “Mfuko wa Misitu” maana yake ni kama ilivyo tafsiriwa katika Sheria ya Misitu ya 2002. “Mfugaji wa Nyuki” maana yake ni mtu yeyote anayejishughulisha na ufugaji wa Nyuki katika eneo la Halmashauri “Mkazi” maana yake ni Mtu ambaye kwa kawaida anaishi kwenye eneo la Mamlaka ya Halmashauri na ambaye ana kaya au anaishi katika kaya au taasisi iliyopo katika eneo la Halmashauri. “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa au na Afisa yeyote wa umma Halmashauri atakayeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi; “Orodha ya Wafugaji wa Nyuki” maana yake daftari litakalotumika kutunza kumbukumbu za majina ya wafugaji wa nyuki, mahali wanapofugia nyuki, idadi na aina ya mizinga ya kufugia nyuki na takwimu za mavuno ya mazao ya nyuki. “Vyanzo vya Maji” maana yake ni mito, vijito, visima, mabwawa, mifereji, maziwa, chemi chemi, ardhi oevu au ardhi chepechepe “Wadau wa ufugaji wa Nyuki” maana yake ni watu, vikundi, taasisi, kampuni au mtu yeyote anayejishughulisha na masuala ya ufugaji nyuki na biashara ya mazao ya 2 Sheria Ndogo za (Ufugaji wa nyuki) za Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Tangazo la Serikali Na. 99 (linaendelea) nyuki. Wajibu wa Halmashauri - 4 Verify source ↗
Section 4
AI-assisted research summary: Halmashauri must carry out several duties to promote and develop modern beekeeping.
4. “Wagani kazi” maana yake ni wananchi ambao wamepata mafunzo ya ugani nje ya vyuo ili kufanya kazi za maafisa ugani pale ambapo hawapo. “Zana za ufugaji wa nyuki” maana yake ni vifaa vilivyokubalika kutumika katika shughuli za ufugaji, uvunaji, uchakataji, ufungashaji na utunzaji wa asali na mazao mengine ya nyuki; “Zana haramu” maana yake ni zana zisizokubalika kitaalam kama mizinga ya magome ya miti, Mienge, au vyombo vilivyotumika kuwekea bidhaa nyingine. Ili kukuza na kuendeleza ufugaji bora na wa kisasa wa nyuki Halmashauri itakua na wajibu ufuatao- (a) (b) (c) (d) (e) (f) (g) (h) (i) (j) (k) (l) kuhakikisha kunakuwepo Mtaalamu wa nyuki katika kila kata au kijiji; kutunza daftari litakalokuwa na orodha ya wafugaji wa nyuki katika eneo la Halmashauri; kutoa elimu ya ufugaji wa nyuki na uhifadhi wa mazingira; kuhamasisha na kuanzisha Vikundi, Vyama vya Ushirika, na Vyama vya Akiba na Mikopo vya wafugaji wa nyuki katika kata na vijiji; kurahisisha upatikanaji wa miche bora ya miti ya asili au ya kigeni itakayotoa maua mengi ambayo nyuki watatumia kutengeneza asali; kusambaza bure au kwa bei rahisi miche ya miti kwa wakulima; kuandaa mashamba darasa ya ufugaji wa nyuki yanayotumia teknolojia bora kwa ajili ya ufugaji wa nyuki na kufundishia; kuwezesha upatikanaji rahisi wa zana na vifaa vya kisasa vya kuvunia asali; kuweka mazingira wezeshi ya upatikanaji wa soko la uhakika la asali na mazao mengine ya nyuki; kuwasaidia wakulima walioko katika vikundi kuanzisha vituo vya kukusanyia na kuuza asali; kuzihamasisha shule za Sekondari na za Msingi kuanzisha miradi ya ufugaji wa nyuki; kufanya tathmini ya kila mwaka ya ukuaji wa sekta ya ufugaji wa nyuki; 3 Sheria Ndogo za (Ufugaji wa nyuki) za Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Tangazo la Serikali Na. 99 (linaendelea) (m) (n) (o) (p) (q) (r) (s) (t) kuwawezesha maofisa ugani kwa kuwapatia vitendea kazi ili kuwapa unafuu wa kuhudumia wafugaji wa nyuki; kuandaa na kuwezesha wafugaji wa nyuki kuhudhuria maonesho mbalimbali; kushirikiana na vijiji katika kutenga maeneo maalum ya ardhi kwa ajili ya wafugaji wa nyuki; kuandaa, kusimamia na kutekeleza Sheria Ndogo za ufugaji wa nyuki ndani ya mamlaka ya Halmashauri; kusimamia ubora na viwango sahihi vya mazao ya nyuki; kutatua migogoro mbalimbali ya ufugaji wa nyuki itakayojitokeza; kutoa vibali mbalimbali vinavyohusu ufugaji na biashara ya mazao ya nyuki; na kutoza ada na ushuru wa vibali na biashara za mazao ya nyuki. Wajibu wa Serikali ya Kijiji - 5 Verify source ↗
Section 5
AI-assisted research summary: Serikali ya Kijiji yenye wakazi wanaofuga nyuki lazima itenge maeneo ya ufugaji, iweke daftari la wafugaji, ianzishe miradi ya nyuki, ihamasishe uhifadhi wa mazingira na ufugaji bora, itunge sheria ndogo, na idhibiti uharibifu au wizi wa mizinga na mazao ya nyuki.
5. Kila Serikali ya Kijiji ambayo wananchi wake wanafuga nyuki itakuwa na wajibu wa- (a) kutenga maeneo maalumu ya ufugaji wa nyuki; (b) kuanzisha daftari litakalokuwa na orodha ya wafugaji wa nyuki kijijini; (c) kuanzisha miradi ya ufugaji wa nyuki ya kijiji; (d) kuhamasisha uhifadhi wa mazingira na ufugaji bora wa nyuki kwa kuanzisha vikundi na vyama vya kuhifadhi mazingira vitakavyokua na jukumu la:- (i) (ii) kuzima moto au kupambana na wachoma moto; (iii) kupambana na kuzuia uvunaji au urinaji wa asali kuhimiza upandaji miti; wa kutumia moto. (e) kutunga Sheria Ndogo za Kijiji; (f) kudhibiti uharibifu na wizi wa mizinga na mazao ya Nyuki; na (g) kusimamia na kutekeleza Sheria Ndogo hizi za ufugaji wa nyuki 4 Sheria Ndogo za (Ufugaji wa nyuki) za Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Tangazo la Serikali Na. 99 (linaendelea) Wajibu wa Afisa Nyuki - 6 Verify source ↗
Section 6
AI-assisted research summary: Afisa Nyuki ana wajibu wa kusimamia masuala ya nyuki katika wilaya, kata au kijiji na kutekeleza majukumu mbalimbali ya uongozi, mafunzo, ufuatiliaji, na utekelezaji wa sheria.
6. Kila Afisa Nyuki atakuwa na wajibu wa kufanya yafuatayo- (a) atakuwa ndiye Afisa Mwidhiniwa wa masuala ya nyuki katika wilaya, kata au kijiji; (b) atatunza orodha ya wafugaji wote wa nyuki na Vikundi vya wafugaji nyuki katika wilaya, kata au kijiji; (c) atatoa mafunzo elekezi ya ufugaji bora wa nyuki katika kata au kijiji; (d) atasimamia mashamba darasa ya ufugaji wa nyuki katika kata au kila kijiji; (e) atatoa maelekezo kuhusu upatikanaji wa zana zote zinazohusiana na ufugaji wa nyuki; (f) ataandaa ratiba ya kuwatembelea wafugaji wa nyuki waliomo katika Kata au vijiji; (g) atahamasisha upandaji wa miti ili kufanikisha upatikanaji wa maua yanayotumiwa na nyuki kutengeneza asali; na (h) kwa kushirikiana na Afisa Mtendaji wa Kata au Kijiji atachukua hatua za kisheria dhidi ya wafugaji wa nyuki au mtu yeyote atakaye kwenda kinyume na masharti ya Sheria Ndogo hizi au sheria yoyote andishi ya ufugaji wa nyuki au hifadhi ya mazingira. Wajibu wa Mfugaji wa Nyuki - 7 Verify source ↗
Section 7
AI-assisted research summary: Kila mfugaji wa nyuki lazima atimize wajibu uliotajwa, ikiwemo kufuata masharti ya Sheria Ndogo hizi.
7. Kila mfugaji wa nyuki atakuwa na wajibu ufuatao- (a) kutunza kitambulisho na kumbukumbu mbalimbali za ufugaji wa nyuki; (b) kutekeleza maelekezo na maagizo ya Afisa Nyuki; (c) atatumia mizinga ya kisasa na ya asili iliyokubaliwa kutumika kufugia nyuki; (d) atarina asali kwa kuzingatia masharti ya kanuni bora za ufugaji wa nyuki; (e) atahifadhi mazingira kwa kutokata miti, kutochoma moto misitu na maeneo yanayotumika kufugia nyuki bila kibali; (f) atashiriki katika shughuli za uhifadhi wa mazingira; (g) atajiunga na vikundi vya ufugaji nyuki, vyama vya ushirika, akiba na mikopo vya wafugaji wa nyuki; (h) atatumia vyombo au vifaa vilivyo safi na salama kwa ajili ya kurinia na kuhifadhia asali; (i) atahudhuria mafunzo yatakayotolewa kuhusu ufugaji wa nyuki; 5 Sheria Ndogo za (Ufugaji wa nyuki) za Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Tangazo la Serikali Na. 99 (linaendelea) (j) kulipa ushuru kwa Halmashauri au Wakala wa Halmashauri (k) kufugia nyuki katika eneo lililokubalika; (l) kuzingatia masharti yaliyowekwa na Sheria Ndogo hizi; (m) kuuzia mazao ya nyuki katika vituo vya kukusanyia mazao ya nyuki vilivyosajiliwa na kuidhinishwa katika ngazi ya wilaya; (n) kutafuta utaalamu na kutoa taarifa mbalimbali kwa ajili ya kuboresha shughuli za ufugaji wa nyuki;na (o) kutoa elimu kwa jamii juu ya faida na mbinu bora za ufugaji wa nyuki. Orodha ya wafugaji nyuki. - 8 Verify source ↗
Section 8
AI-assisted research summary: Kila mfugaji wa nyuki lazima ajiorodheshe kwenye daftari la eneo lake na kupewa kitambulisho; daftari la wafugaji wa nyuki linatunzwa na Afisa Muidhiniwa katika Ofisi za Serikali.
8. (1) Itakuwa ni wajibu wa kila mfugaji wa nyuki kujiorodhesha katika daftari la wafugaji wa nyuki katika eneo lake na kupewa kitambulisho. (2) Daftari la orodha ya wafugaji wa nyuki litahusisha taarifa zifuatazo- (a) jina la mfugaji na anwani yake; (b) eneo analofugia; (c) aina ya nyuki anaofuga; (d) idadi na aina ya mizinga anayofugia nyuki; (e) maelezo ya vifaa anavyotumia kufugia, kurinia asalia, kuchakatia, kufungashia kuhifadhia na kusafirishia; (f) takwimu za uzalishaji wa asali na mazao mengine ya nyuki kwa kila msimu wa mavuno. (3) daftari la orodha ya wafuga nyuki litatunzwa na Afisa Muidhiniwa katika Ofisi za Serikali. Ufungashaji wa asali na mazao mengine ya nyuki - 9 Verify source ↗
Section 9
AI-assisted research summary: Wafugaji wa nyuki na wafanyabiashara wa asali au mazao mengine ya nyuki lazima wafuate masharti ya kufungasha bidhaa, ikiwemo kutumia vifungashio sahihi, kufungasha katika vituo vilivyokubalika, na kuweka taarifa za lebo zinazotakiwa.
9. Mfugaji wa nyuki au Mfanya biashara wa Asali au mazao mengine ya nyuki atalazimika kuzingatia masharti yafuatayo katika kufungasha bidhaa- (a) kwa kutumia vifungashio ambavyo havijawahi kutumika kwa kufungashia bidhaa nyingine yoyote, visivyoshika kutu, na vyenye mifuniko; (b) ufungashaji wa asali au mazao mengine ya nyuki utafanyika katika vituo vya kukusanyia asali na mazao ya nyuki vilivyokubalika; (c) bidhaa za asali au mazao mengine ya nyuki zitakuwa 6 Sheria Ndogo za (Ufugaji wa nyuki) za Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Tangazo la Serikali Na. 99 (linaendelea) Usafirishaji wa Asali na mazao mengine ya nyuki na alama zinazoonyesha Jina la mzalishaji na anwani yake, tarehe ya kufungasha bidhaa, Uzito, muda wa matumizi, na alama za ubora na maelekezo ya utunzaji na matumizi. - 10 Verify source ↗
Section 10
AI-assisted research summary: Asali na mazao ya nyuki lazima yasafirishwe kwa njia zinazolinda ubora na usafi; hayapaswi kupelekwa nje ya Halmashauri bila ushuru kulipwa na kibali maalum; na maafisa wa nyuki wanapaswa kukagua na kutekeleza sheria hizi.
10. -(1) Asali na mazao mengine ya nyuki yatasafirishwa katika mazingira yafuatayo- (a) (b) (c) ambayo yatalinda ubora na usafi; kwa kutumia vyombo nyingine kwa kutumika visivyoshika kutu na vyenye mifuniko; na kusafirishwa katika mazingira yanayoepusha joto na jua kali. havijawahi yeyote, shughuli ambavyo Ada na ushuru wa Asali na Mazao mengine ya Nyuki Ukaguzi 11 12 (2) Asali au mazao mengine ya nyuki hayatasafirishwa nje ya Halmashauri bila kulipiwa ushuru na kuwa na kibali maalum. Halmashauri itaweka utaratibu wa kutoza ada na ushuru kwa bidhaa, leseni au vibali vitakavyotolewa kuhusiana na uzalishaji na biashara ya asali na mazao mengine ya nyuki. (1)Itakuwa ni wajibu wa Afisa Nyuki au Afisa Mwidhiniwa kusimamia shughuli za ufugaji wa nyuki kwa kufanya ukaguzi katika mashamba ya ufugaji wa nyuki, vituo vya kukusanyia mazao ya nyuki, au sehemu yeyote inayojihusisha na shughuli za ufugaji au biashara ya mazao ya nyuki ili- (a) kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hizi; (b) kuhakikisha kuwa viwango vya ubora wa ufugaji, uvunaji, uchakataji, ufungashaji na usafirishaji wa asali na mazao ya nyuki vinazingatiwa; (c) kumchukulia hatua za kisheria mtu yeyote atakayevunja Sheria Ndogo hizi; (2) Bila kuathiri kifungu cha 12.(1) cha Sheria Ndogo hizi Maafisa hao watakuwa na uwezo wa kufanya ukaguzi baada ya saa za kazi, au siku za mapumziko au jumamosi na jumapili au siku za sikukuu ili mradi wawe na kibali cha Mkurugenzi; 7 Sheria Ndogo za (Ufugaji wa nyuki) za Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Tangazo la Serikali Na. 99 (linaendelea) Utatuzi wa Migogoro 13 (1) Endapo kutatokea mgogoro wowote kati ya wafugaji wa nyuki, na wakulima au wafugaji wa mifugo au kundi lolote lile mgogoro huo utatatuliwa na Halmashauri ya Kijiji au Halmashauri ya Wilaya. (2) Endapo mgogoro ulijitokeza unahusu wizi, uharibifu wa miundo mbinu ya ufugaji wa nyuki kwa makusudi, au jambo jinai mgogoro huo utasuluhishwa na Mahakama. lolote la Marufuku - 14 Verify source ↗
Ni marufuku
AI-assisted research summary: Kuna marufuku nyingi kuhusu ufugaji na biashara ya mazao ya nyuki, na mtu anayekiuka masharti anaweza kupigwa faini, kufungwa jela, na kulipia uharibifu aliosababisha.
14. Ni marufuku- (a) kufanya biashara ya mazao ya nyuki nje ya maeneo yaliyoidhinishwa; (b) Ni marufuku kuchanganya ufugaji wa nyuki na kilimo cha madawa katika sehemu moja; (c) Kuhifadhia na kufungashia mazao ya nyuki kwenye vyombo ambavyo vimetumika kuwekea vitu vingine (d) Kuchoma moto katika maeneo ya kufugia nyuki bila kibali; (e) Kukata miti, kuchuna kamba, kuokota kuni Uyoga, Dawa na kufanya shughuli za kibinadamu ndani ya hifadhi ya nyuki bila kibali; (f) Kufuga Nyuki wanaouma katika Makazi ya Watu. Nyuki wanaouma watafugwa katika eneo lenye umbali wa mita mia moja kutoka katika makazi ya watu; (g) Kuingia kwenye hifadhi ya nyuki bila kibali; (h) Kufuga, kuingiza, kupitisha na kuchungia mifugo kwenye eneo la kufugia Nyuki; (i) Kuvuna mazao ya nyuki kwa kutumia moto; (j) Kusafirisha mazao ya nyuki nje ya Halmashauri bila Kibali; (k) Kufanya biashara ya mazao ya nyuki bila kulipa ushuru nakufua tataratibu zilizowekwa; (l) Watu wenye uwezo kutokushiriki kuzima moto endapo watahitajika kufanya hivyo; na (m) Kuiba mazao au kuvuna asali kwenye mzinga usio wako. 8 Sheria Ndogo za (Ufugaji wa nyuki) za Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Tangazo la Serikali Na. 99 (linaendelea) Makosa 15 Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa endapo- (a) akirina asali kwa kutumia moto au madawa; (b) atauza asali iliyorinwa kwa moto au madawa; (c) atachanganya au amechanganya asali na vitu vingine ambavyo siyo asali; (d) atachoma moto misitu au eneo ambalo limetengwa kwa ajili ya wafugaji wa nyuki; (e) atakata miti bila kuwa na kibali; (f) atang’oa miti iliyopandwa kwa ajili ya kuhifadhi mazingira; (g) atatenda lolote linahatarisha maendeleo na ufugaji wa nyuki; ambalo jambo linadhuru au Adhabu 16 (h) atatenda kitendo chochote kinachohatarisha upatikanaji wa asali yenye ubora na salama; (i) atahujumu miundo mbinu ya ufugaji wa nyuki ya shule, kikundi, kijiji, kata, taasisi na mtu binafsi; na (j) atatenda jambo lolote ambalo ni kinyume na Sheria Ndogo hizi. (1)Mtu yeyote atakayekwenda kinyume na Masharti ya Sheria Ndogo hizi atakuwa ametenda Kosa na akipatikana na hatia atatozwa faini isiyozidi shilingi elfu hamsini (50,000/=) au kifungo kisichozidi miezi kumi na miwili jela au adhabu zote kwa pamoja yaani kifungo na faini (2) Pamoja na adhabu iliyotolewa chini ya kifungu cha 16(1) hapo juu mtu yeyote atakayeharibu miundombinu ya ufugaji wa nyuki atatakiwa kufidia gharama za uharibifu aliosababisha. Kufifilisha kosa 17 Mkurugenzi anaweza kumtoza mtu yeyote faini isiyozidi shilingi elfu hamsini (50,000/=) iwapo mkosaji atakiri kosa kwa maandishi na kukubali kulipa hasara aliyosababisha chini ya Jedwali la Sheria Ndogo hizi 9 Sheria Ndogo za (Ufugaji wa nyuki) za Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Tangazo la Serikali Na. 99 (linaendelea) ______ JEDWALI _______ HATI YA KUKIRI NA KUFIFILISHA KOSA (Chini ya kifungu cha 17) Mimi nakiri .................................................................................................................................. mbele ya ............................................................................ ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma, kwamba mnamo tarehe .........ya mwezi ..............Mwaka ............nilitenda kosa la kukiuka masharti ya kifungu cha ............... cha Sheria Ndogo za (Ufugaji wa Nyuki ) za Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Mwaka 2017 Kwa Mamlaka aliyopewa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, Niko tayari kulipa kiasi cha Ada/ Ushuru ninaodaiwa pamoja na faini. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU Leo tarehe ...............ya Mwezi............. Mwaka.................. Jina:....................................... Saini............................. Mbele ya : Jina : ...................................... Cheo : ..................................... Saini :...................................... Nembo ya Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma imebandikwa katika Sheria Ndogo hizi kwa azimio la kikao cha Mkutano wa Halmashauri kilichoitishwa na kufanyika tarehe 29/03/2016 na imebandikwa mbele ya: MICHAEL N. MWANDAZI, Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma 10 Sheria Ndogo za (Ufugaji wa nyuki) za Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma Tangazo la Serikali Na. 99 (linaendelea) ENOCK CHOBALIKO, Mwenyekiti wa Halmashauri, Wilaya ya Kigoma NAKUBALI, Dodoma, 9 Januari, 2017 GEORGE B. SIMBACHAWENE (MB.), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Tamisemi 11
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo za (Ufugaji wa nyuki) za Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma za Mwaka 2017
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in