Sheria Ndogo za (Uanzishaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii) za Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo za Mwaka 2017
These by-laws are titled as the Nsimbo District Council (Establishment of the Community Health Fund) By-laws, 2017, and they start to apply after publication in the Government Gazette.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo za (Uanzishaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii) za Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo za Mwaka 2017
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
These by-laws are titled as the Nsimbo District Council (Establishment of the Community Health Fund) By-laws, 2017, and they start to apply after publication in the Government Gazette. This section defines key terms used in the bylaw. A voluntary Community Health Fund is created to help pay treatment costs, with households contributing, government providing a matching contribution, and the Board managing spending under the by-laws. Mfuko huu una madhumuni ya kuboresha huduma za afya za jamii, kuwezesha jamii kushiriki maamuzi ya afya, kutoa huduma bora za afya kwa mipango endelevu, na kutafuta vyanzo vya mapato kutoka jamii kwa ajili ya huduma za afya kwa wanachama. Section 6 assigns oversight and day-to-day administration of the Fund to district, ward, village, and board-level bodies, and lists the duties of the Community Health Fund Coordinator.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo za (Uanzishaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii) za Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo za Mwaka 2017
Showing 24 of 24
- 2 Verify source ↗
Section 2
AI-assisted research summary: These by-laws are titled as the Nsimbo District Council (Establishment of the Community Health Fund) By-laws, 2017, and they start to apply after publication in the Government Gazette.
2. Sheria Ndogo hizi zitajulikana kama Sheria Ndogo za (Uanzishaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii) za Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo za Mwaka 2017, na zitaanza kutumika baada ya kutangazwa kwenye Gazeti la Serikali. Sheria Ndogo hizi zitatumika katika eneo lote la mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hizi
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the bylaw.
3. Katika Sheria Ndogo hizi isipokuwa kama itaelezwa Sura ya 287 vinginevyo- “Ada ya mtumiaji” maana yake ni ada anayolipa mtumiaji wa huduma kwa Hospitali, Kituo cha afya au Zahanati, kwa ajili ya Huduma ya Afya iliyotolewa kwa mtumiaji; ”Bodi” maana yake ni chombo kinachosimamia Huduma za Afya ya Halmashauri iliyoundwa kwa mujibu wa kifungu Na. 88 cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) Sura Na. 287; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo ; “Huduma za Afya” maana yake ni huduma zote za Afya zinazotolewa na Hospitali, Vituo cha Afya, Zahanati na Kliniki maalum zinazomilikiwa na Serikali, Mashirika ya Dini, Mashirika yasiyo ya Serikali au Watu binafsi; “Kadi” maana yake ni kadi itakayotolewa kwa Mwanachama wa Mfuko wa Afya ya Jamii; “Kaya” maana yake ni:- (a) Baba, Mama na Watoto wenye umri chini ya 1 Sheria Ndogo za (Uanzishaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii) za Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Tangazo la Serikali Na. 100 (linaendelea) miaka kumi na nane; na (b) Mwanachama yeyote aliyefikia umri wa miaka kumi na nane au zaidi na awe na Mtoto au bila Mtoto mwenye umri chini ya miaka kumi na nane; au (c) Taasisi yoyote; “Kituo cha Huduma kilichoteuliwa” maana yake ni kituo kinachotoa Huduma za Afya na ni pamoja na kituo chochote kilichoanzishwa au kinachoendeshwa kwa malengo ya kutoa Huduma za Afya kinachomilikiwa na Halmashauri, Serikali, Asasi za Kidini, Mtu au Watu binafsi ambacho kinahusika na Mfuko wa Afya ya Jamii; “Malipo ya huduma” maana yake ni malipo ya papo kwa papo yanayolipwa katika Kituo cha kutolea Huduma za Afya na Mtu au Watu ambao si Wanachama wa Mfuko wa Afya ya Jamii; “Mchango” maana yake ni mchango wa fedha wa hiari, utakaotolewa na Wanachama wa Mfuko wa Afya ya Jamii; “Mganga Mkuu wa Wilaya” maana yake ni Daktari ambaye ni Msimamizi Mkuu wa shughuli zote za Huduma za Afya katika Wilaya; “Mwanachama” ni Mtu yeyote ambaye anachangia mfuko wa Afya ya Jamii; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo au Afisa yeyote atakayeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi; “Taasisi” maana yake ni pamoja na Shule au Chuo kilichosajiliwa kwa mujibu wa Sheria au Taasisi yoyote itakayokuwa imekubaliwa na kuidhinishwa na bodi kuwa Mwanachama. “Wizara” maana yake ni Wizara yenye dhamana ya masuala ya Afya. Mfuko wa Afya ya Jamii - 4 Verify source ↗
Section 4
AI-assisted research summary: A voluntary Community Health Fund is created to help pay treatment costs, with households contributing, government providing a matching contribution, and the Board managing spending under the by-laws.
4. (1) Kutakuwa na mfuko wa Afya ya Jamii ambao ni mpango wa hiari wenye lengo la kutoa msaada kifedha katika kugharamia matibabu, ambapo kaya zitakuwa zikilipia 2 Sheria Ndogo za (Uanzishaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii) za Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Tangazo la Serikali Na. 100 (linaendelea) Madhumuni ya Mfuko Huduma za Afya, na Serikali itatoa mchango wake wa fedha kama Kaya jazilio kwa mchango kutoka kwenye Mwanachama; (2) Matumizi ya fedha yatafanywa na kusimamiwa na Bodi kwa Mujibu wa Sheria Ndogo hizi. - 5 Verify source ↗
Madhumuni ya Mfuko yatakuwa ni
AI-assisted research summary: Mfuko huu una madhumuni ya kuboresha huduma za afya za jamii, kuwezesha jamii kushiriki maamuzi ya afya, kutoa huduma bora za afya kwa mipango endelevu, na kutafuta vyanzo vya mapato kutoka jamii kwa ajili ya huduma za afya kwa wanachama.
5. Madhumuni ya Mfuko yatakuwa ni- (a) Kuboresha huduma za afya katika Jamii kwa kugawanya madaraka na kuzipa nguvu Jamii katika kufanya maamuzi na kuchangia katika masuala yanayohusu afya zao; (b) Kutoa huduma bora za afya zinazopatikana na kwa kutumia mipango endelevu; na (c) Kutafuta vyanzo vya mapato kutoka katika Jamii kwa ajili ya kutoa huduma bora za afya kwa Wanachama; Usimamizi wa Mfuko wa Afya ya Jamii. - 6 Verify source ↗
Section 6
AI-assisted research summary: Section 6 assigns oversight and day-to-day administration of the Fund to district, ward, village, and board-level bodies, and lists the duties of the Community Health Fund Coordinator.
6. (1) Usimamizi na uendeshaji wa Mfuko utakuwa chini ya:- (a) Halmashauri ya Wilaya kupitia Bodi ya Huduma za Afya ya Halmashauri ya Wilaya; na (b) Kamati ya Maendeleo ya Kata kupitia Kamati ya Afya ya Kata, katika ngazi ya Kata; (2) Mfuko kwa ujumla utakuwa chini ya usimamizi wa Bodi ambayo itakuwa na majukumu ya:- (a) kuratibu shughuli zinazohusu mfuko; (b) kusimamia, kudhibiti na kuelekeza usimamizi katika vyanzo vya mfuko; (c) kuhakikisha kuwa mfuko unatumika na kusimamiwa kikamilifu na kwa ufanisi; na (d) Serikali ya kijiji kupitia Kamati za Huduma za Jamii katika ngazi ya kijiji. (2) Majukumu ya Mratibu wa Mfuko wa Afya ya Jamii yatakuwa kama ifuatavyo:- (a) Kufuatilia, kusimamia na kuratibu uendeshaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii kwenye vituo vya kutolea Huduma za Afya. (b) Kuwa kiungo kati ya Halmashauri, Jamii na Wadau mbalimbali kwa ushirikiano na Mhasibu wa Mfuko, na 3 Sheria Ndogo za (Uanzishaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii) za Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Tangazo la Serikali Na. 100 (linaendelea) Bodi Muundo wa Bodi (c) Kuandaa taarifa za Mfuko wa Afya ya Jamii za robo na za Mwaka pamoja na majukumu mengine atakayopangiwa na Mkurugenzi. (d) Kuhudhuria vikao vyote vya Bodi na kutoa taarifa za utekelezaji wa shughuli za Mfuko wa Afya ya Jamii. - 7 Verify source ↗
Kutakuwa na Bodi ya Mfuko wa Afya ya Jamii itakayoundwa
AI-assisted research summary: This section establishes the Community Health Fund Board under the bylaws and says it will supervise health services in the council.
7. Kutakuwa na Bodi ya Mfuko wa Afya ya Jamii itakayoundwa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizi ambayo itakuwa ni chombo kinachosimamia huduma za afya katika Halmashauri. (1) Bodi itakuwa na wajumbe wafuatao:- - 8 Verify source ↗
Section 8
AI-assisted research summary: Section 8 lists the Board’s members, including women representation, and says certain technical members may not vote.
8. (a) Wawakilishi wanne wa Watumiaji wa Huduma za Afya, kati yao wawili lazima wawe ni Wanawake; (b) Mwakilishi mmoja kutoka kwa Watoa huduma za afya binafsi bila faida; (c) Mwakilishi mmoja kutoka kwa Watoa Huduma za Afya binafsi waliochaguliwa na Halmashauri kutoka katika Vituo ambavyo vina mkataba na Bodi wa kutoa Huduma za Afya ; (d) Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Afya, Elimu na Maji; (e) Wajumbe Wataalamu ambao ni- (i) Afisa Mipango wa Halmashauri. (ii) Mganga Mkuu wa Halmashauri ambaye atakuwa Katibu wa Bodi. (iii) Mwakilishi mmoja kutoka Hospitali ya Halmashauri. (iv) Mwakilishi mmoja kutoka Timu ya uendeshaji wa Huduma za Afya ya Mkoa. (2) Wajumbe wa Bodi waliotajwa katika kifungu cha 8(1) (e) (i) – (v) hawataruhusiwa kupiga kura. Sifa za Wajumbe wa Bodi (3) Mwenyekiti wa Bodi atachaguliwa kutoka miongoni mwa Wajumbe waliotajwa katika kifungu (1) (a) – (c) hapo juu. - 9 Verify source ↗
Mjumbe wa Bodi atakuwa na sifa zifuatazo
AI-assisted research summary: A board member must meet specified qualifications, including citizenship, age, education, experience, sound mind, clean criminal record, no political party office, active fund membership, and residence for elected members, with an exception for NGO representatives on citizenship.
9. Mjumbe wa Bodi atakuwa na sifa zifuatazo:- (a) Awe raia wa Tanzania, isipokuwa kwa Wajumbe kutoka Mashirika yasiyo ya Kiserikali; (b) Awe na umri usiopungua miaka ishirini na tano (25); 4 Sheria Ndogo za (Uanzishaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii) za Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Tangazo la Serikali Na. 100 (linaendelea) (c) Awe amehitimu Elimu ya Sekondari na kuendelea; (d) Awe na uzoefu na amewahi kuonyesha uwezo wake wa kuongoza katika shughuli za huduma ya jamii; (e) Awe na akili timamu; (f) Asiwe amewahi kutiwa hatiani kwa kosa lolote la jinai; (g) Asiwe na wadhifa wowote katika chama chochote cha siasa. (h) Awe Mwanachama hai wa Mfuko wa Afya ya Jamii , na (i) Mjumbe wa kuchaguliwa awe ni mkazi wa Halmashauri. Kazi za Bodi - 10 Verify source ↗
Section 10
AI-assisted research summary: Bodi ina kazi kadhaa za kusimamia Mfuko wa Afya ya Jamii na huduma za afya katika Halmashauri.
10. (1) Bodi itakuwa na kazi zifuatazo:- (a) Itasimamia masuala na shughuli zote zinazohusu Mfuko wa Afya ya Jamii ; (b) Kusimamia Huduma za Afya katika Halmashauri; (c) Kushauriana na Timu ya uendeshaji ya Huduma za Afya ya Halmashauri na kuhakikisha kuwa Huduma za Afya zinazotolewa ni bora na za Kitaalamu; (d) Kukusanya na kusimamia mapato ya Mfuko wa Afya ya Jamii ; (e) kupendekeza kwa Halmashauri Watu wanaostahili kusamehewa kutoa mchango kwenye Mfuko; (f) kubuni malengo ya Mfuko; (g) kupitia taarifa kutoka Kamati ya Afya ya Kata au chanzo kingine chochote; (h) kuratibu ukusanyaji wa michango na kudhibiti matumizi; na (i) Kupanga mipango ya afya ya Mwaka kwa ajili ya kuthibitishwa na Halmashauri; Muda wa kukaa Madarakani - 11 Verify source ↗
Section 11
AI-assisted research summary: The Board must receive and carry out Council instructions according to the law, regulations, and procedures. A Board member serves for three years from the Board’s inauguration date and may be re-elected once for another three-year term.
11. (2) Bodi katika kutekeleza majukumu yake, itapokea na kutekeleza maagizo ya Halmashauri kwa mujibu wa Sheria, Kanuni, na Taratibu. (1) Mjumbe wa Bodi atakuwa madarakani kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia tarehe ya uzinduzi wa Bodi na anaweza kuchaguliwa tena kwa kipindi kingine cha miaka mitatu (3) tu; 5 Sheria Ndogo za (Uanzishaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii) za Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Tangazo la Serikali Na. 100 (linaendelea) Akaunti ya Mfuko - 12 Verify source ↗
Section 12
AI-assisted research summary: Bodi lazima ichague wawekaji saini wa Akaunti ya Mfuko kutoka Kundi A na Kundi B; Halmashauri itumie Akaunti Maalum kwa fedha za Mfuko. Ikiwa nafasi ya Mjumbe wa Bodi itaachwa wazi, mjumbe mwingine achaguliwe kwa muda uliosalia, lakini si kama muda uliobaki ni chini ya miezi sita.
12. (2) Endapo nafasi yoyote ya Mjumbe wa Bodi itaachwa wazi kwa sababu ya kifo, kujiuzulu au kwa sababu nyingine yoyote ile, Mjumbe mwingine atachaguliwa kujaza nafasi hiyo iliyoachwa wazi kwa kipindi kilichobaki. (3) Bila kuathiri masharti ya kifungu kidogo cha (2) hapo juu, haitaruhusiwa kuchagua mjumbe mwingine iwapo kipindi kilichobaki ni chini ya miezi sita. (1) Kutakuwapo na Akaunti Maalum itakayotumika na Halmashauri ambayo fedha zote zitakazokusanywa kwa ajili ya Mfuko zitahifadhiwa na kutolewa. (2) Wawekaji saini wa Akaunti ya Mfuko watachaguliwa na Bodi na watakuwa ni wa kutoka Kundi “A” na Kundi “B”, kama ifuatavyo:- Kundi A Kundi B - 2 Verify source ↗
Mweka Hazina wa
AI-assisted research summary: The fund account must not be disbursed without a signature from one person from each group, and the fund account is to be audited under government financial regulations.
2. Mweka Hazina wa Bodi Halmashauri (3) Fedha hazitatolewa kwenye akaunti ya mfuko bila saini ya mmojawapo kutoka kila Kundi. (4) Akaunti ya Mfuko itakaguliwa kwa mujibu wa Kanuni za Fedha za Serikali. (5) Taarifa ya Fedha - 13 Verify source ↗
Bodi itaandaa na kuwasilisha kwa Halmashauri, taarifa ya
AI-assisted research summary: Bodi lazima iandae na kuwasilisha kwa Halmashauri taarifa ya mapato na matumizi ya fedha kila baada ya miezi mitatu.
13. Bodi itaandaa na kuwasilisha kwa Halmashauri, taarifa ya mapato na matumizi ya fedha ya kila baada ya miezi mitatu (3). Matumizi ya Fedha za Mfuko - 14 Verify source ↗
Fedha
AI-assisted research summary: Fedha za mfuko lazima zitumike kwa madhumuni ya afya yaliyotajwa, na baadhi ya masuala mengine yanaweza kutumika tu ikiwa Bodi imeyaidhinisha.
14. Fedha zitakazokusanywa na mfuko zitatumika kwa madhumuni yafuatayo- (a) Masuala yanayohusiana na afya yaliyotajwa katika mpango kabambe wa afya wa Halmashauri na kuidhinishwa na Halmashauri; na Suala itakayoonekana inafaa na kama itaidhinishwa na Bodi. shughuli yoyote muhimu afya au ya (b) Vyanzo vya mapato - 15 Verify source ↗
Vyanzo vya mapato ya mfuko vitatokana na
AI-assisted research summary: The fund’s revenue sources come from member contributions, grants, certain local and central government support, private contributions, earmarked local taxes, the National Health Insurance Fund, and any other lawful income.
15. Vyanzo vya mapato ya mfuko vitatokana na- (a) Fedha zote zitakazopokelewa kutokana na michango ya 6 Sheria Ndogo za (Uanzishaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii) za Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Tangazo la Serikali Na. 100 (linaendelea) Wanachama; (b) Ruzuku kutoka Halmashauri, na Serikali Kuu, Wahisani mbalimbali toka ndani na nje ya Halmashauri; (c) Michango ya watu binafsi wanaoishi ndani na nje ya Halmashauri; (d) Ushuru utakaotozwa na Halmashauri kutoka vyanzo mbalimbali na kutengwa kwa ajili ya mfuko; (e) Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya; na (f) Fedha zozote halali ambazo Mfuko unaweza kupata toka mahali pengine popote. Mipango - 16 Verify source ↗
Section 16
AI-assisted research summary: Bodi must prepare annual budget plans, handle the health plan, give comments on supplementary budgets when needed, and submit fund budget plans to Halmashauri for approval.
16. (1) Bodi itaandaa mipango ya Bajeti ya Mwaka kwa kuzingatia ratiba za vikao vya Bajeti vya Halmashauri; (2) Bodi itapokea, itajadili, itachambua na kuidhinisha mpango wa afya na kuwasilisha kwa Halmshauri kwa ajili ya kuidhinishwa kwa kupitia Kamati za Halmashauri; (3) Bodi itatoa maoni ya bajeti ya nyongeza kama kutakuwa na haja ya kufanya hivyo na kama mazingira yataruhusu; (4) Mipango ya bajeti ya Mfuko itaandaliwa kulingana na utaratibu kama ulivyoainishwa katika kifungu kidogo cha (1) hapo juu, ambayo ni lazima iwasilishwe Halmashauri kwa ajili ya kuidhinishwa. - 17 Verify source ↗
Kutakuwa na kamati ya Afya ya Kata kama ilivyotajwa
AI-assisted research summary: A ward health committee is to exist as referred to in the Community Health Fund law.
17. Kutakuwa na kamati ya Afya ya Kata kama ilivyotajwa kwenye Sheria ya Mfuko wa Afya ya Jamii. - 18 Verify source ↗
Section 18
AI-assisted research summary: The Ward Health Committee must consist of the listed members, choose its chairperson from among its members with some officeholders excluded, and the Council Board must arrange a new election within three months if the committee fails to perform its functions.
18. (1) Kamati ya Afya ya Kata itakuwa na Wajumbe wafuatao:- (a) Diwani anayewakilisha Kata husika; (b) Afisa Mtendaji wa Kata; (c) Mwalimu Mkuu mmoja kutoka kwenye Shule ya msingi ambayo ipo kwenye Kata husika; (d) Wajumbe wawili watakaowakilisha jamii husika ambapo mmoja wao ni lazima awe Mwanamke; (e) Tabibu Mfawidhi au Tabibu Mfawidhi Msaidizi; wa kituo cha Afya au Zahanati, ambaye atakuwa katibu wa Kamati; 7 Kamati ya Afya na Kata (SURA 409) Wajumbe wa kamati ya Afya ya Kata (SURA 409) Sheria Ndogo za (Uanzishaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii) za Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Tangazo la Serikali Na. 100 (linaendelea) (f) Mjumbe mmoja atakayeteuliwa na kamati ya maendeleo na watu kata waliopendekezwa na Kamati za Kata zilichomo ndani ya eneo la Kata; na kutokana ya Kazi na majukumu ya Kamati ya Afya ya Kata. (g) Mjumbe mmoja atakayeteuliwa na Kamati ya maendeleo ya Kata kutoka kwenye vyama vya kijamii kutoka kwenye Kata. (2) Mwenyekiti wa Kamati ya Afya ya Kata atachaguliwa kutoka miongoni mwa wajumbe lakini asiwe Diwani, Mtendaji wa Kata au Mtendaji wa Mtaa; (3) Endapo Kamati ya Afya ya Kata itashindwa kutekeleza itatoa onyo au kuivunja na kazi zake, Bodi Halmashauri itafanya utaratibu wa uchaguzi wa wajumbe wengine katika muda usiozidi miezi mitatu (3) tangu tarehe ya kuvunjwa kwa Kamati hiyo. - 19 Verify source ↗
Section 19
AI-assisted research summary: Kamati ya Afya ya Kata ina majukumu ya kuhamasisha na kuratibu shughuli za Mfuko wa Afya ya Jamii, na Katibu anatakiwa kutoa taarifa ya maandishi siku 7 kabla ya kikao.
19. (1) Kamati ya Afya ya Kata itakuwa na majukumu yafuatayo:- (a) Kuhamasisha na kuandaa Jamii kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii ; (b) Kuandaa na kuthibitisha orodha na kuratibu idadi ya Wanachama wa Mfuko wa Afya wa Jamii ; (c) Kusimamia ukusanyaji wa michango ya Mfuko; (d) Kuratibu viwango vya uchangiaji kwenye Huduma za Afya; (e) Kupitia utendaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii na kutoa mapendekezo na ufumbuzi kwa Halmashauri kupitia Bodi ya Afya; (f) Kuanzisha na kuratibu Mipango ya Afya na Jamii na, (g) Kuendesha mikutano ya Wanachama wa Mfuko wa Afya ya Jamii ndani ya Kata. (2) Kamati ya Afya ya Kata, itakaa kila baada ya miezi mitatu (3) na Katibu atatoa taarifa ya maandishi siku saba (7) kabla ya siku ya kikao. Utoaji wa Huduma za Afya. - 20 Verify source ↗
Kila Mwanachama
AI-assisted research summary: Kila Mwanachama ana haki ya kisheria kupata huduma ya afya aliyolipia kabla ya kuugua ndani ya eneo la Halmashauri.
20. Kila Mwanachama- (a) Atakuwa na haki ya kisheria kupata Huduma ya Afya aliyolipia kabla ya kuugua ndani ya eneo la Halmashauri 8 Sheria Ndogo za (Uanzishaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii) za Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Tangazo la Serikali Na. 100 (linaendelea) Mchango wa Mwanachama - 23 Verify source ↗
Section 23
AI-assisted research summary: Wanachama wa Mfuko wa Afya ya Jamii hulipa mchango wa kila mwaka wa Sh 15,000; wasio wanachama hulipa malipo ya papo kwa papo wanapotafuta matibabu, na Halmashauri inaweza kurekebisha viwango hivyo.
23. au eneo lingine lolote kadri itakavyo kubaliwa, (b) Atakuwa na haki ya kutoa mapendekezo kuhusu Huduma za Afya kupitia kamati husika ambayo yatafanyiwa kazi na Bodi; na (c) Atashirikishwa kikamilifu katika uandaaji na utekelezaji wa mpango wa upatikanaji wa Huduma za Afya katika eneo la Halmashauri. (a) Mtu yeyote atakayetaka kuwa Mwanachama wa Mfuko wa Afya ya Jamii atapaswa kulipa kila mwaka mchango kiasi cha Shilingi elfu kumi na tano tu (15,000/=) (b) Viwango hivi vinaweza kufanyiwa marekebisho na Halmashauri wakati wowote iwapo itaonekana kuna umuhimu wa kufanya marekebisho hayo. (a) Mtu yeyote atabaki kuwa Mwanachama wa Mfuko wa Afya ya Jamii kila atakapo lipa mchango wake wa Uanachama, na (b) Kila Mwaka utakapoisha Uanachama wa mtu utafikia mwisho hadi pale atakapotimiza masharti ya kifungu (a) hapo juu. (1) Mtu yeyote ambaye hatakuwa Mwanachama wa mfuko huu atalipa malipo ya papo kwa papo kila atakapoenda kupata matibabu katika kituo cha kutolea Huduma za Afya. (2) Malipo ya papo kwa papo yatalipwa kwa ajili ya kusajiliwa, kumwona Daktari, na kupewa dawa kwa mujibu wa viwango vitafuatavyo;- (a) Hospitali shilingi elfu nane (8,000/=); (b) Vituo ya Afya shilingi elfu tano ( 5,000/=); (c) Zahanati elfu tatu (3,000/=). Utaratibu wa Misamaha - 24 Verify source ↗
Misamaha kwa wasioweza kulipia gharama za matibabu
AI-assisted research summary: The council will grant and pay medical-cost exemptions for people who cannot afford treatment costs, after a set local review process is followed.
24. Misamaha kwa wasioweza kulipia gharama za matibabu utatolewa na kulipiwa na Halmashauri baada ya kuzingatia utaratibu ufuatao:- (a) Serikali ya Mtaa katika vikao vyake itawatambua, kuwajadili na kuwasilisha mapendekezo ya Orodha ya majina ya watu wanaostahili kupewa Msamaha kwenye 9 Sheria Ndogo za (Uanzishaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii) za Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Tangazo la Serikali Na. 100 (linaendelea) Kamati ya Maendeleo ya Kata, (b) Kamati ya Maendeleo ya Kata itawajadili wale wasioweza kulipia gharama na kuthibitisha orodha yao na kuiwasilisha kwenye Bodi, na (c) Bodi ya Afya itapokea na kujadili mapendekezo husika na kuyawasilisha pamoja na gharama zake kwa Halmashauri kwa ajili ya kulipiwa. Utoaji wa Kadi kwa Mwanachama - 25 Verify source ↗
Section 25
AI-assisted research summary: Wanachama wa Mfuko hupata kadi baada ya kulipa mchango wa mwaka; mtu aliyepewa msamaha wa mchango pia hupata kadi ya uanachama.
25. (1) Kila Kaya Mwanachama wa Mfuko atapewa kadi baada ya kulipa mchango wake wa Mwaka wa Shilingi elfu kumi kiwango kitakachopendekezwa na Bodi na kuidhinishwa na Halmashauri. (15,000/=) tano au na Makosa na Adhabu (2) Kila mtu atakayesamehewa kulipa mchango atapewa kadi ya Uanachama na Halmashauri italipa gharama ya kadi hiyo. (3) Viwango vya kulipia uanachama vitapendekezwa na Kamati ya Maendeleo ya Kata na kujadiliwa na Bodi kisha kuidhinishwa na Halmashauri. - 26 Verify source ↗
Mtu yeyote ambaye
AI-assisted research summary: Anyone who breaks the by-laws or interferes with the Board, the Fund’s assets, fraudulently benefits from the health services, or obstructs enforcement commits an offence and may be fined, jailed, or both.
26. Mtu yeyote ambaye:- (a) (b) (c) (d) (e) atakwenda kinyume na masharti yoyote ya Sheria Ndogo hizi; atafanya kitendo chochote ambacho kitazuia Bodi kufanya kazi zake kwa ufanisi; atatumia vibaya mali na rasilimali za Mfuko; atafanya udanganyifu ili aweze kunufaika na Huduma za Afya zitolewazo kwa utaratibu wa Mfuko wa Afya ya Jamii; au atazuia utekelezaji wa Sheria Ndogo hizi; Atakuwa ametenda kosa na akipatikana na hatia atatozwa faini isiyozidi shilingi laki tatu (300,000/=), au kifungo kisichozidi miezi kumi na miwili (12) au adhabu zote mbili kwa pamoja yaani faini na kifungo. 10 Sheria Ndogo za (Uanzishaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii) za Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Tangazo la Serikali Na. 100 (linaendelea) Nembo ya Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo imebandikwa kwenye Sheria Ndogo hizi kufuatia Azimio lililopitishwa kwenye Mkutano wa Halmashauri uliofanyika tarehe .................. na kubandikwa mbele ya:- MWAILWA SMITH PANGANI, Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo RAPHAEL A. KALINGA, Mwenyekiti, Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo NAKUBALI, Dodoma, 9 Januari, 2017 GEORGE B. SIMBACHAWENE, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - Tamisemi 11
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo za (Uanzishaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii) za Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo za Mwaka 2017
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in