AI-assisted research summary: Mwenye kibali lazima ajenge kituo cha mafuta kwa kufuata masharti yote ya usalama, viwango, umbali, na alama zilizoorodheshwa.
3. Mwombaji anapewa kibali cha ujenzi kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Mafuta katika Kiwanja Na. 28, Eneo la Mnazi Mmoja, Wilaya ya Lindi, Mkoa wa Lindi kwa masharti yafuatayo: (a) kituo cha mafuta kitajengwa kwa mujibu wa viwango vya Shirika la Viwango Tanzania Na. TZS 1115:2009 na TZS 1079:2008; 1 Notisi ya Kibali Cha Ujenzi wa Kituo Cha Mafuta kwa Fountain Petroleum Ltd Tangazo La Serikali Na. 328 (Linaendelea) (b) uangalifu wa kutosha utazingatiwa wakati wa uchimbaji na uwekaji wa matenki ya mafuta chini ya ardhi; (c) mpangilio wa kituo cha mafuta utapaswa kukidhi umbali wa kiusalama kwa mujibu wa viwango vya Shirika la Viwango Tanzania Na. TZS 1079:2008; (d) ufukiaji wa matenki ya kuhifadhia mafuta pamoja na mabomba chini ya ardhi ufanywe kwa namna ambayo italinda usalama wa vifaa hivyo ikiwemo kupata kutu; (e) matenki ya kuhifadhia mafuta, pampu na mabomba husika pamoja na vifaa vyote vinavyounganishwa pamoja navyo vitapaswa kufungwa vizuri ili kuzuia uvujaji wowote wa mafuta; (f) matenki ya kuhifadhia mafuta na pampu ya mafuta itapaswa kufanyiwa uhakiki wa usahihi wa vipimo na Wakala wa Vipimo Tanzania aliyeanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Vipimo Tanzania; (g) eneo la mbele la kituo cha mafuta na kuzunguka eneo la pampu litasakafiwa kwa zege madhubuti isiyoweza kupenyeza mafuta na kuhakikisha kuwepo kwa mitaro ambayo itakusanya maji na mafuta wakati wa mvua na kuyaelekeza kwenye chemba ya kutenganisha maji na mafuta; Sura ya 340 (h) kuweka ya swichi eneo linaloonekana na kufikika kirahisi ili wakati wa dharura iwe ni rahisi kuzima umeme wa kituo kizima; dharura katika (i) kuhakikisha uwepo wa vyoo vya kutosha vya wanawake na wanaume vilivyo safi wakati wote; (j) kuhakikisha kuwa alama za usalama zinawekwa sehemu ya kuingia na ya kutoka kwenye kituo cha mafuta na eneo la pampu zikijumuisha “zima injini”, “zima simu” na “usivute sigara”; (k) kuhakikisha kila tenki la kuhifadhia mafuta 2 Notisi ya Kibali Cha Ujenzi wa Kituo Cha Mafuta kwa Fountain Petroleum Ltd Tangazo La Serikali Na. 328 (Linaendelea) linaunganishwa na bomba la kupumulia lenye urefu usiopungua mita 3.6 kutoka ardhini na bomba hilo linatakiwa kuwa angalau mita 1.5 kutoka kwenye mpaka wa kiwanja na angalau mita 4 kutoka kwenye dirisha au kifaa chochote cha kuvuta hewa ikiwemo kiyoyozi; (l) pampu za kuuza mafuta na sehemu ya kushushia mafuta zinatakiwa kuwa angalau mita 4.5 kutoka kwenye mpaka wa kiwanja, anagalu mita 8 kutoka katika kifaa chochote ambacho kinaweza kuwa chanzo cha moto ikiwemo jokofu na angalau mita 10 kutoka kwenye nyaya za kusafirishia umeme; (m) kuhakikisha kila pampu ya mafuta inalindwa na kizuizi na kizuizi kinapaswa kuwa na urefu wa mita moja kutoka juu ya ardhi; (n) mifumo ya upakuaji wa mafuta kwenye kituo cha mafuta itapaswa kujengwa kwa kufuata Kanuni na taratibu zinazokubalika kwenye sekta ya mafuta; (o) kuhakikisha kuwa kituo cha mafuta kinakuwa na paa linalofunika eneo lote lenye pampu za mafuta na linajengwa kwa mujibu wa viwango na taratibu zinazokubalika kwenye sekta ya mafuta; na (p) kuhakikisha kuwa kituo cha mafuta kinakuwa na bango la bei ambalo litawekwa mahala ambapo panaonekana kirahisi ili wateja waweze kuona bei za mafuta kabla ya kuingia kituoni. Ukomo wa kibali cha ujenzi