Kanuni za Usimamizi Jumuishi wa Ukanda wa Pwani za mwaka 2024
This provision gives the regulations’ name and then begins a section on “Matumizi” (use), but the provided text cuts off.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Kanuni za Usimamizi Jumuishi wa Ukanda wa Pwani za mwaka 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This provision gives the regulations’ name and then begins a section on “Matumizi” (use), but the provided text cuts off. Kanuni hizi zinatumika katika ukanda wa pwani wa Tanzania Bara. This section defines key terms used in the regulations, including coastal zone, protected area, sensitive environment area, coastal resources, coastal management, integrated coastal zone management, and the Minister. Kanuni hizi zinaweka malengo ya kusimamia ukanda wa pwani kwa pamoja, kulinda mazingira ya pwani, kukuza matumizi na ugawanaji wa faida za rasilimali za pwani, na kuimarisha elimu, utafiti, uelewa wa umma, na ubia kati ya sekta za umma na binafsi. Waziri ana mamlaka ya kutoa miongozo ya sera, kutangaza maeneo ya ukanda wa pwani kuwa nyeti au lindwa, na kuteua au kuelekeza taasisi kutekeleza majukumu yanayoweza kuathiri mazingira ya ukanda wa pwani.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Kanuni za Usimamizi Jumuishi wa Ukanda wa Pwani za mwaka 2024
Showing 25 of 25
- 1
AI-assisted research summary: This provision gives the regulations’ name and then begins a section on “Matumizi” (use), but the provided text cuts off.
1. Kanuni hizi zitajulikana kama Kanuni za Usimamizi Jumuishi wa Ukanda wa Pwani za mwaka 2024. Matumizi - 2
AI-assisted research summary: Kanuni hizi zinatumika katika ukanda wa pwani wa Tanzania Bara.
2. Kanuni hizi zitatumika katika ukanda wa pwani wa Tanzania Bara. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Jina
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the regulations, including coastal zone, protected area, sensitive environment area, coastal resources, coastal management, integrated coastal zone management, and the Minister.
3. Katika Kanuni hizi isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “Baraza” maana yake ni kama ilivyoainishwa katika Sheria; “eneo la mazingira lindwa” maana yake ni eneo lolote la ukanda wa pwani lililotangazwa na Waziri chini ya kifungu cha 47 cha Sheria; “eneo la mazingira nyeti” maana yake ni eneo lolote la ukanda wa pwani lililotangazwa na Waziri kuwa eneo la mazingira nyeti chini ya kifungu cha 51 cha Sheria; “Mkurugenzi wa Mazingira” maana yake ni kama iliyoainishwa chini ya Sheria; “Mkurugenzi Mkuu” maana yake ni kama iliyoainishwa chini ya Sheria; “rasilimali za pwani” maana yake ni rasilimali zote hai na 3 Kanuni za Usimamizi Jumuishi wa Ukanda wa Pwani Tangazo la Serikali Na. 384 (Linendelea) Sura ya 191 zisizo hai ambazo zina thamani ya kimazingira, kiuchumi ma kijamii zinazounda mifumo jumuishi ya kiekolojia ya nchi kavu na baharini na mazao yake; “Sheria” maana yake ni Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; “ukanda wa pwani” maana yake ni eneo la bahari katika mpaka wa nchi, upande wa nchi kavu hadi mita sitini kutoka ufukwe wa pwani ya Tanzania Bara; “usimamizi wa pwani” hujumuisha- (a) udhibiti, usimamizi, ulinzi, uhifadhi na urejeshaji wa mazingira ya pwani; (b) udhibiti na usimamizi wa matumizi na uendelezaji wa ukanda wa pwani na rasilimali zake; na (c) ufuatiliaji na uzingatiaji wa sheria na sera zinazodhibiti shughuli za binadamu katika ukanda wa pwani; “usimamizi jumuishi wa ukanda wa pwani” maana yake ni usimamizi endelevu wa mazingira ya ukanda wa jumuishi na pwani unaojumuisha michakato shirikishi la lengo inayohusisha wadau kwa kupanga, kusimamia, kuhifadhi na kulinda mifumo ya kiekolojia na rasilimali za bahari na nchi kavu; kwa kuzingatia umuhimu, unyeti, mwingiliano, matumizi pamoja na matokeo yake kwa lengo la kuhakikisha maendeleo endelevu; “Waziri” maana yake ni Waziri mwenye dhamana ya mazingira. SEHEMU YA PILI MADHUMUNI Madhumuni
Part
SEHEMU YA PILI
- 4 Verify source ↗
Madhumuni
AI-assisted research summary: Kanuni hizi zinaweka malengo ya kusimamia ukanda wa pwani kwa pamoja, kulinda mazingira ya pwani, kukuza matumizi na ugawanaji wa faida za rasilimali za pwani, na kuimarisha elimu, utafiti, uelewa wa umma, na ubia kati ya sekta za umma na binafsi.
4. Malengo ya Kanuni hizi ni- (a) kuweka mifumo jumuishi ya usimamizi wa ukanda wa pwani; (b) kulinda na kuhifadhi mazingira ya kanda za 4 Kanuni za Usimamizi Jumuishi wa Ukanda wa Pwani Tangazo la Serikali Na. 384 (Linendelea) pwani; (c) kuhamasisha matumizi sawa ya fursa na ugawanaji faida za rasilimali za pwani; (d) kuhamasisha usimamizi na matumizi endelevu ya rasilimali za pwani; (e) Kuwajengea uwezo maofisa wa serikali na jamii; (f) kuhamasisha utoaji elimu na kufanya utafiti kuhusu usimamizi jumuishi wa ukanda wa pwani; (g) kukuza uelewa wa umma kuhusu usimamizi jumuishi wa ukanda wa pwani; na (h) kuimarisha ubia baina ya sekta za umma na binafsi katika masuala yanayohusu usimamizi jumuishi wa ukanda wa pwani. SEHEMU YA TATU UTAWALA NA MUUNDO WA KITAASISI Majukumu ya Waziri
Part
SEHEMU YA TATU
- 5 Verify source ↗
Majukumu ya Waziri
AI-assisted research summary: Waziri ana mamlaka ya kutoa miongozo ya sera, kutangaza maeneo ya ukanda wa pwani kuwa nyeti au lindwa, na kuteua au kuelekeza taasisi kutekeleza majukumu yanayoweza kuathiri mazingira ya ukanda wa pwani.
5.-(1) Kwa madhumuni ya kutekeleza masharti ya Kanuni hizi, Waziri- (a) atakuwa na mamlaka ya jumla kwa masuala yanayohusiana na usimamizi jumuishi wa mazingira ya ukanda wa pwani na kwa msingi huo atatoa miongozo muhimu ya kisera kwa ajili ya na usimamizi endelevu wa mazingira ya ukanda wa pwani; kuhamasisha, kuhifadhi kulinda, (b) atakuwa na mamlaka ya kutangaza eneo lolote linalopendekezwa la ukanda wa pwani kuwa eneo la mazingira nyeti au lindwa; na (c) atateua, na pale inapobidi atazielekeza taasisi ndani ya muda utakaowekwa, kutekeleza jukumu au shughuli yoyote ambayo matokeo yake yanaweza kuathiri mazingira ya ukanda wa pwani. 5 Kanuni za Usimamizi Jumuishi wa Ukanda wa Pwani Tangazo la Serikali Na. 384 (Linendelea) Majukumu ya Mkurugenzi wa Mazingira - 6 Verify source ↗
Majukumu ya Mkurugenzi wa Mazingira
AI-assisted research summary: The Environment Director must prepare a national integrated coastal zone environmental management strategy, submit an integrated coastal zone management plan to the Minister, and advise the Minister on all related matters.
6. Mkurugenzi wa Mazingira- (a) ataandaa Mkakati wa Kitaifa wa Usimamizi Jumuishi wa Mazingira ya Ukanda wa Pwani; (b) atawasilisha kwa Waziri Mpango Jumuishi wa Usimamizi wa Ukanda wa Pwani; na (c) atamshauri Waziri masuala yote yanayohusiana na usimamizi jumuishi wa ukanda wa pwani. Majukumu ya Baraza - 7 Verify source ↗
Majukumu ya Baraza
AI-assisted research summary: Baraza must oversee compliance with these Regulations and carry out coordination, research, reporting, advisory, and warning functions for coastal zone environmental management.
7. Baraza- (a) litasimamia uzingatiaji na utekelezaji wa Kanuni hizi; (b) litashirikiana na wizara zingine za kisekta katika kufuatilia na kudhibiti usimamizi na uhifadhi bora wa mazingira ya ukanda wa pwani; (c) litaratibu, kufanya au kukusanya tafiti katika nyanja za mazingira ya ukanda wa pwani na kutoa taarifa ya matokeo ya tafiti hizo; (d) litatoa ushauri na msaada wa kitaalamu pale inapowezekana, kwa Kamati ya Kitaifa ya Utendaji ya Usimamizi Jumuishi wa Ukanda wa Pwani ili kuiwezesha kutekeleza majukumu yake; (e) litapokea na kufanya majumuisho ya taarifa za utekelezaji wa Mipango ya Usimamizi Jumuishi wa Ukanda wa Pwani zilizowasilishwa na Wataalamu wa Mazingira wa mikoa husika na kuwasilisha taarifa hiyo kwa Mkurugenzi wa Mazingira; (f) litawezesha kufanya mapitio ya tafiti za mazingira, ripoti ya hali na mwenendo wa mifumo ya kiikolojia ya pwani na baharini, na kutoa hadhari kwa mamlaka za serikali za mitaa husika kuhusu changamoto za mazingira zinazojitokeza; (g) litamshauri Waziri kuhusu uteuzi wa Wakaguzi wa Mazingira wa Ukanda wa Pwani. 6 Kanuni za Usimamizi Jumuishi wa Ukanda wa Pwani Tangazo la Serikali Na. 384 (Linendelea) Majukumu ya Wizara za Kisekta Majukumu wa Sekretarieti ya Mkoa - 8 Verify source ↗
Majukumu ya Wizara za Kisekta
AI-assisted research summary: Wizara za Kisekta lazima ziandae miongozo ya kisera, ziingize Mkakati wa Kitaifa katika mipango ya ndani, zifuatilie ufuatiliaji wa mkakati huo, na ziweze kutoa mwongozo wa shughuli nyingine za pwani inapohitajika.
8. Wizara za Kisekta- (a) zitatoa miongozo ya kisera ya dira ya jumla ya usimamizi jumuishi wa ukanda wa pwani katika sekta zao; (b) zitahakikisha Mkakati wa Kitaifa wa Usimamizi Jumuishi wa Mazingira ya Pwani umejumuishwa katika mpango ya ndani jumuishi wa usimamizi wa ukanda wa pwani; (c) zitasimamia uzingatiaji wa jumla wa Mkakati wa Kitaifa wa Usimamizi wa Mazingira ya Pwani; na (d) zitatoa mwongozo wa shughuli zingine za pwani kama itakavyohitajika. - 9 Verify source ↗
Majukumu ya Sekretarieti za Mikoa
AI-assisted research summary: Sekretarieti ya Mkoa lazima itekeleze majukumu ya kuratibu, kuunganisha, kusaidia kitaalamu, kuwezesha mapitio na utekelezaji, kushauri mamlaka za mitaa, na kuwasilisha taarifa kuhusu usimamizi jumuishi wa ukanda wa pwani.
9. Sekretarieti ya Mkoa- (a) itaratibu masuala yote ya usimamizi jumuishi wa ukanda wa pwani katika mikoa yao; (b) itakuwa kiunganishi baina ya Mkurugenzi wa Mazingira na Mkurugenzi Mkuu kuhusu uzingatiaji na utekelezaji wa Kanuni hizi; (c) itatoa msaada wa kitaalamu wakati wa kutayarisha mpango wa jumla wa usimamizi wa eneo lindwa la bahari na mpango wa usimamizi wa eneo maalumu na programu endelevu za usimamizi jumuishi wa mazingira ya ukanda wa pwani; (d) itawezesha kufanya mapitio ya tafiti za mazingira, ripoti ya hali na mwenendo wa mifumoikolojia ya pwani na baharini, na kutoa hadhari kwa mamlaka za serikali za mitaa husika kuhusu changamoto za mazingira zinazojitokeza; (e) itawezesha utekelezaji wa matumizi sawa ya fursa na ugawanaji faida za rasilimali katika ngazi zote; (f) itashauri na kutoa msaada wa kitaalamu kwa 7 Kanuni za Usimamizi Jumuishi wa Ukanda wa Pwani Tangazo la Serikali Na. 384 (Linendelea) mamlaka za serikali za mitaa wa masuala yanayohusu usimamizi jumuishi wa ukanda wa pwani; na (g) itawasilisha katika Baraza taarifa ya utekelezaji wa mipango jumuishi ya usimamizi wa ukanda wa pwani. Majukumu ya mamlaka za serikali za mitaa - 10 Verify source ↗
Majukumu ya Mamlaka za Serikali za Mitaa
AI-assisted research summary: Local authorities must carry out integrated coastal zone management tasks, including preparing a plan, building community capacity, supervising implementation, and submitting the plan to the Regional Secretariat.
10. Kuhusiana na usimamizi jumuishi wa mazingira wa ukanda wa pwani mamlaka ya serikali za mitaa- (a) itaandaa mpango jumuishi wa usimamizi wa ukanda wa pwani katika maeneo yao; (b) itaijengea jamii katika masuala uwezo yanayohusu usimamizi jumuishi wa ukanda wa pwani; (c) itakuza uelewa na kuhamasisha ili kuimarisha usimamizi jumuishi wa ukanda wa pwani; jamii (d) itasimamia utekelezaji wa mpango jumuishi wa usimamizi wa ukanda wa pwani; (e) itafanya mapitio ya tafiti za mazingira, na kutoa taarifa ya hali na mwenendo wa mifumo wa kiekolojia wa pwani na baharini, na kutoa hadhari kwa mamlaka za serikali za mitaa husika kuhusu changamoto za mazingira zinazojitokeza; (f) itaendeleza na kutekeleza utaratibu wa matumizi sawa ya fursa na ugawanaji faida za rasilimali katika ngazi zote; (g) itaunda Kamati ya Wataalamu ya Wilaya katika wilaya husika; (h) itashughulikia changamoto za usimamizi wa mazingira ya ukanda wa pwani; na (i) itawasilisha katika Sekretarieti ya Mkoa mpango jumuishi wa usimamizi wa ukanda wa pwani ulioandaliwa chini ya Kanuni hizi. 8 Kanuni za Usimamizi Jumuishi wa Ukanda wa Pwani Tangazo la Serikali Na. 384 (Linendelea) Wakaguzi wa Mazingira - 11 Verify source ↗
Wakaguzi wa Mazingira
AI-assisted research summary: Wakaguzi wa Mazingira walioteuliwa na Waziri wana wajibu wa kusimamia mazingira ya ukanda wa pwani.
11. Wakaguzi wa Mazingira walioteuliwa na Waziri miongoni mwa watumishi wa serikali za mitaa, wizara au taasisi yoyote ya umma wana wajibu wa kusimamia mazingira ya ukanda wa pwani. SEHEMU YA NNE USIMAMIZI WA MAZINGIRA YA UKANDA WA PWANI (a) Mpango Jumuishi wa Usimamizi wa Ukanda wa Pwani Mpango Jumuishi wa Usimamizi wa Ukanda wa Pwani
Part
SEHEMU YA NNE
- 12 Verify source ↗
Mpango Jumuishi wa Usimamizi wa Ukanda wa Pwani
AI-assisted research summary: Mamlaka ya serikali za mitaa lazima itayarishe Mpango Jumuishi wa Usimamizi wa Ukanda wa Pwani katika eneo lake.
12.-(1) Kila mamlaka ya serikali za mitaa, katika eneo lake la kiutawala itatayarisha Mpango Jumuishi wa Usimamizi wa Ukanda wa Pwani kulingana na Dira ya Taifa ya Usimamizi wa Ukanda wa Pwani, Mkakati wa Kitaifa wa Usimamizi wa Mazingira ya Pwani, Mpango Maalumu wa Kitaifa wa Mazingira wa Afua za Kimkakati, Mpangokazi wa Kitaifa wa Mazingira na waraka mwingine unaohusiana na mazingira. (2) Kila Mpango Jumuishi wa Usimamizi wa Ukanda wa Pwani unaorejelewa chini ya kanuni ndogo ya (1)- (a) utaendana na Dira ya Kitaifa ya Usimamizi wa Ukanda wa Pwani, Mpango Maalumu wa Kitaifa wa Mazingira wa Afua za Kimkakati, Mpangokazi wa Kitaifa wa Mazingira na waraka mwingine unaohusiana na mazingira; (b) utazingatia viwango vya kitaifa vya mazingira; (c) utatayarishwa kwa ushirikiano na wadau muhimu; na (d) utatoa mbinu jumuishi za usimamizi wa ukanda wa pwani. Maudhui ya Mpango Jumuishi wa Usimamizi wa Ukanda - 13 Verify source ↗
Maudhui ya Mpango Jumuishi wa Usimamizi wa Ukanda wa
AI-assisted research summary: The integrated coastal zone management plan must include specified content such as objectives, strategies, indicators, environmental challenges, sustainable resource-use methods, and participatory governance arrangements.
13. Mpango Jumuishi wa Usimamizi wa Ukanda wa Pwani utajumuisha- (a) malengo ya mpango huo; (b) vipaumbele na mikakati ya kutimiza malengo 9 Kanuni za Usimamizi Jumuishi wa Ukanda wa Pwani Tangazo la Serikali Na. 384 (Linendelea) wa Pwani hayo; (c) viashiria muhimu vya utendaji ili kupima maendeleo na mafanikio ya malengo hayo; (d) changamoto za mazingira zilizopo katika ukanda wa pwani husika na mapendekezo ya hatua za kukabiliana nazo; (e) mbinu za matumizi endelevu ya rasilimali za pwani; (f) Tamaduni na taratibu bora za usimamizi wa mazingira ya ukanda wa pwani; (g) muundo wa utawala shirikishi ili kutekeleza hatua zilizoainishwa kwenye mpango huo ambao- (i) unabainisha majukumu ya wadau na jamii zinazotegemea rasilimali za pwani kwa maisha yao; na (ii) unawezesha uratibu wa usimamizi jumuishi wa ukanda wa pwani. (b) Udhibiti wa Rasilimali za Ukanda wa Pwani Udhibiti wa rasilimali za pwani - 14
AI-assisted research summary: Kila mamlaka ya serikali za mitaa lazima idhibiti na kuhakikisha matumizi endelevu na uhifadhi wa rasilimali za pwani katika eneo lake.
14. Kila mamlaka ya serikali za mitaa itadhibiti na kuhakikisha matumizi endelevu na uhifadhi wa rasilimali za pwani katika eneo lake. Usimamizi na ulinzi wa eneo la mazingira nyeti au lindwa la ukanda wa pwani - 15 Verify source ↗
ukanda wa pwani
AI-assisted research summary: Wizara husika, mamlaka za serikali za mitaa, na wadau lazima wachukue hatua za usimamizi jumuishi wa ukanda wa pwani, ikiwemo uhamasishaji wa jamii, kutunga na kutekeleza sheria ndogo, na kuingiza shughuli hizo katika mipango ya mwaka.
15.-(1) Endapo eneo lolote la ukanda wa pwani limetangazwa kuwa eneo la mazingira nyeti au eneo lindwa chini ya masharti ya Sheria, wizara husika zitajenga uelewa na uwezo kwa jamii husika na umma kwa ujumla. (2) Bila kuathiri kanuni ndogo ya (1), mamlaka za serikali za mitaa, chini ya sheria husika na kwa kushirikiana na wizara za kisekta, zitaandaa na kutekeleza sheria ndogo za usimamizi jumuishi wa ukanda wa pwani. (3) Kwa madhumuni ya kutimiza malengo ya Kanuni hizi, wizara husika, mamlaka za serikali za mitaa, na wadau watajumuisha shughuli jumuishi za usimamizi wa 10 Kanuni za Usimamizi Jumuishi wa Ukanda wa Pwani Tangazo la Serikali Na. 384 (Linendelea) ukanda wa pwani katika mipango yao ya mwaka. Zuio la matumizi ya flora na fauna Haki ya njia katika eneo la mazingira nyeti au lindwa - 16 Verify source ↗
Zuio la matumizi ya flora na fauna
AI-assisted research summary: Matumizi ya flora na fauna katika maeneo ya mazingira nyeti au lindwa kwenye ukanda wa pwani hayaruhusiwi, isipokuwa kama wakati wa kutangaza eneo hilo itaelekezwa vinginevyo.
16. Matumizi ya flora na fauna katika maeneo ya mazingira nyeti au lindwa katika ukanda wa pwani hayataruhusiwa isipokuwa kama imeelekezwa vinginevyo wakati wa kutangaza eneo husika. - 17 Verify source ↗
Haki ya njia katika eneo la mazingira nyeti au lindwa
AI-assisted research summary: A person entering a sensitive or protected area to use a right of way must not carry out listed activities, and breaches can be a criminal offence with a fine, imprisonment, or both.
17.-(1) Kwa kuzingatia masharti ya kanuni ndogo ya (2), na kwa maslahi ya umma haki ya njia katika eneo ya mazingira nyeti au lindwa inaweza kutolewa. (2) Mtu anayeingia katika eneo la mazingira nyeti au lindwa kwa madhumuni ya kutumia haki ya njia iliyotolewa chini ya kanuni ndogo ya (1) hatafanya vitendo vifuatavyo- (a) kukata, kuangusha, kuchimbua, kuchoma, kung'oa, kuharibu au kuondoa mmea wowote; (b) kuingiza flora au fauna yoyote, sehemu ya flora au fauna, ya kigeni au asilia, iliyo kufa au iliyo hai; (c) kutupa aina yoyote ya taka; (d) kuweka kambi, kufanya mashindano ya magari, kufanya michezo au shughuli zozote zilizopigwa marufuku; (e) kumiliki au kuishi katika eneo hilo; (f) kujenga jengo lolote; (g) kujenga barabara, njia, madaraja, reli, mifereji au uwanja wa ndege; (h) kuchimba madini; (i) kuchukua au kuondoa miamba, mawe, mchanga, magamba au udongo; (j) kuruhusu kuingiza au kulisha mifugo; na (k) kuchukua fauna ya aina yoyote au kuvuna mazao yao. (3) Mtu anayekiuka masharti ya- (a) kanuni ndongo (2) ya kanuni hii; au (b) kanuni ya 16, 11 Kanuni za Usimamizi Jumuishi wa Ukanda wa Pwani Tangazo la Serikali Na. 384 (Linendelea) (c) anatenda kosa na akitiwa hatiani atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi elfu hamsini na isiyozidi shilingi bilioni moja au kutumikia kifungo na kisichozidi miaka saba au vyote. kisichopungua miezi mitatu Uwekezaji TS. Na 349 la 2005 - 18 Verify source ↗
Uwekezaji
AI-assisted research summary: Investment in the coastal zone must comply with the Environmental Management Regulations on environmental impact assessment and audit.
18. Uwekezaji katika ukanda wa pwani utafanyika kwa mujibu wa masharti ya Kanuni za Usimamizi wa Mazingira (Tathmini ya Athari kwa Mazingira na Ukaguzi). Maombi ya kibali - 19 Verify source ↗
Maombi ya kibali
AI-assisted research summary: A person intending to invest in the coastal zone must apply for an investment permit under the relevant law.
19. Mtu anayekusudia kuwekeza katika ukanda wa pwani ataomba kibali cha uwekezaji kwa mujibu wa sheria husika. Ukaguzi wa mazingira TS. Na. 349 la 2005 - 20 Verify source ↗
Ukaguzi wa mazingira
AI-assisted research summary: Shughuli za pwani zinazofanyika bila cheti cha tathmini ya athari kwa mazingira lazima zikaguliwe mazingira.
20. Shughuli zinazoendelea katika ukanda wa pwani zinazofanyika bila kupata cheti cha tathmini ya athari kwa mazingira, zitahitaji kufanyiwa ukaguzi wa mazingira kwa mujibu wa Kanuni za Tathmini ya Athari kwa Mazingira na Ukaguzi. Matumizi ya rasilimali za pwani - 21 Verify source ↗
Matumizi ya rasilimali za pwani
AI-assisted research summary: Use of coastal resources must comply with the relevant sector ministries’ laws, subject to regulation 16.
21. Kwa kuzingatia masharti ya kanuni ya 16, matumizi ya rasilimali za pwani yatazingatia masharti ya sheria za wizara za sekta husika. SEHEMU YA TANO MASHARTI YA JUMLA Makosa na adhabu
Part
SEHEMU YA TANO
- 22 Verify source ↗
Makosa na adhabu
AI-assisted research summary: A person who carries out coastal zone activities without a written permit, breaches permit conditions, gives false or misleading information to obtain a permit, or violates these regulations commits an offence and may be fined or imprisoned.
22. Mtu ambaye- (a) atafanya shughuli katika ukanda wa pwani bila kibali cha maandishi kilichotolewa na wizara au mamlaka ya sekta husika; (b) atakiuka vigezo na masharti yaliyoambatishwa katika kibali kilichotolewa chini ya sheria husika; (c) atatoa za uongo, upotoshaji taarifa au udanganyifu ili kupata kibali chochote; au 12 Kanuni za Usimamizi Jumuishi wa Ukanda wa Pwani Tangazo la Serikali Na. 384 (Linendelea) (d) atakiuka masharti ya Kanuni hizi, (e) anatenda kosa na akitiwa hatiani atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi elfu hamsini na isiyozidi shilingi bilioni moja au kutumikia na kifungo kisichozidi miaka saba au vyote. kisichopungua miezi mitatu Ufuatiliaji na tathmini - 23
AI-assisted research summary: Ufuatiliaji na tathmini ya Mpango Jumuishi wa Usimamizi wa Kanda ya Pwani lazima ifanyike mara kwa mara, na tathmini ifanyike kila baada ya miaka miwili ya utekelezaji.
23. Ufuatiliaji na tathmini ya mpango jumuishi wa usimamizi wa ukanda wa pwani itafanyika mara kwa mara. (2) Kwa mujibu wa kanuni ndogo ya (1), ufuatiliaji utazingatia- (a) viashiria vya ubora wa makazi au mazalia ya viumbe hai, ubora wa maji na fukwe; (b) ongezeko la mrundikano au mmomonyoko wa udongo, kilimo na uzalishaji wa mazao ya baharini; na (c) kiashiria chochote cha ubora wa uchumi-jamii kama itakayohitajika. (3) Bila kujali masharti ya kanuni ndogo ya (1), tathmini itafanyika kila baada ya miaka miwili ya utekelezaji wa Mpango Jumuishi wa Usimamizi wa Kanda ya Pwani. Kipindi cha mpito - 24
AI-assisted research summary: Person carrying out activities in the coastal zone must comply with these Regulations within 12 months from the commencement date.
24. Mtu anayefanya shughuli katika maeneo ya ukanda wa pwani atatakiwa kuzingatia Kanuni hizi ndani ya miezi kumi na miwili kuanzia tarehe ya kuanza kutumika. Rufaa - 25 Verify source ↗
Ufuatiliaji na tathmini
AI-assisted research summary: Mtu asiye ridhishwa na uamuzi chini ya Kanuni hizi anaweza kukata rufaa; ikiwa rufaa inaenda kwa Waziri, lazima iwasilishwe kwa barua na viambatisho vinavyohitajika, Waziri aamue ndani ya siku 14 na amjulishe mleta rufaa ndani ya siku 7 baada ya uamuzi.
25.-(1) Mtu ambaye hajaridhishwa na uamuzi uliotolewa chini ya Kanuni hizi, anaweza kukata rufaa kwa mujibu wa masharti ya Sheria. thelathini kuanzia (2) Endapo rufaa chini ya kanuni ndogo ya (1) inaenda kwa Waziri, Rufaa hiyo itawasilishwa ndani ya Siku siku ya kutolewa uamuzi unaokatiwa rufaa na itakuwa kwa njia ya barua ambayo imeambatishwa na nakara ya uamuzi na nyaraka nyingine ambayo Waziri anaweza kuhitaji. 13 Kanuni za Usimamizi Jumuishi wa Ukanda wa Pwani Tangazo la Serikali Na. 384 (Linendelea) (3) Waziri atatakiwa kutoa maamuzi yake ndani ya siku kumi na nne kuanzia siku ya kupokelewa kwa rufaa. (4) Waziri atatakiwa kumjulisha mleta rufaa uamuzi wake na sababu za uamuzi huo ndani ya siku saba kuanzia siku aliyotoa uamuzi Dodoma, SELEMANI SAIDI JAFO 3 Mei, 2024. Waziri wa Nchi- Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira 14
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Kanuni za Usimamizi Jumuishi wa Ukanda wa Pwani za mwaka 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in