Kanuni za Haki ya Fidia za Mwaka 2024
The regulations are named the Compensation Rights Regulations, 2024, and the text then begins an interpretation section.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Kanuni za Haki ya Fidia za Mwaka 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
The regulations are named the Compensation Rights Regulations, 2024, and the text then begins an interpretation section. This section defines several terms used in the regulation, including owner, operator, hazardous activity, public authority, environmental damage, compensation, and minister. Kanuni hizi zinaweka utaratibu wa uwajibikaji na fidia, na zinatoa haki ya fidia kwa watu au madhara yanayohusiana na ulinzi wa mazingira na uharibifu wa mazingira. Baraza must enforce these Regulations and carry out environmental-management, compensation, public participation, education, reconciliation, assessment, record-keeping, and other minister-directed duties. The Director must promote good environmental management, strengthen sector coordination and stakeholder engagement, enable relevant research, and carry out other tasks assigned by the Minister.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Kanuni za Haki ya Fidia za Mwaka 2024
Showing 26 of 26
- 1
AI-assisted research summary: The regulations are named the Compensation Rights Regulations, 2024, and the text then begins an interpretation section.
1. Kanuni hizi zitajulikana kama Kanuni za Haki ya Fidia za Mwaka 2024. Tafsiri - 2 Verify source ↗
Jina
AI-assisted research summary: This section defines several terms used in the regulation, including owner, operator, hazardous activity, public authority, environmental damage, compensation, and minister.
2. Katika Kanuni hizi, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “Baraza” maana yake ni kama ilivyoainishwa kwenye Sheria; “fidia” maana yake ni malipo ya fidia au kitendo kingine chochote ambacho mahakama au mamlaka nyingine inaamuru kifanywe na mmiliki au mwendeshaji ambaye kutenda au kutotenda kwake kumesababisha- (a) kifo au majeraha kwa mtu; (b) upotevu au uharibifu wa mali ambayo si mali iliyo chini ya udhibiti wa mwendeshaji kwenye eneo la shughuli hatarishi; (c) hasara au uharibifu wa mazingira ambao hautachukuliwa kuwa ni uharibifu kwa maana iliyo katika aya (a) au (b) na utajikita katika gharama zilizoingiwa au zitakazoingiwa katika kurejesha mazingira; (d) mtu yeyote kuingia gharama za hatua za kuzuia madhara au uharibifu; “mazingira” maana yake ni kama ilivyoainishwa chini ya Sheria; “mamlaka ya umma” maana yake ni wizara, idara, mamlaka au taasisi ya serikali ambayo ina taarifa zinazohusu mazingira; “Mkurugenzi wa Mazingira” maana yake ni kama ilivyoainishwa chini ya Sheria; “mmiliki” maana yake ni mtu anayemiliki eneo, majengo, mitambo au vifaa vinavyotumika katika shughuli hatarishi; “mwendeshaji” maana yake ni mtu anayesimia shughuli hatarishi; “mtu” maana yake ni kama ilivyoainishwa chini ya Sheria; “Sheria” maana yake ni Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; “shughuli hatarishi” maana yake ni shughuli inayoweza kusababisha athari mbaya za moja kwa moja, zisizo za moja kwa moja, za papo kwa hapo au zinazojitokeza baadaye kwa afya ya binadamu, mazingira au mali; “uharibifu wa mazingira” maana yake ni mabadiliko yasiyotakiwa au kero zinazojitokeza katika mazingira kutokana na umwagikaji, utokaji au 3 Sura ya 191 Tangazo La Serikali Na. 385 (Linaendelea) Kanuni za haki fidia uhamaji wa dutu na taka hatarishi kupita ukomo wa kiwango, ambayo yanaweza kuleta athari mbaya katika afya ya binadamu, mali na ubora wa mazingira; “Waziri” maana yake ni kama ilivyoainishwa kwenye Sheria. SEHEMU YA PILI MALENGO NA MISINGI YA JUMLA Madhumuni
Part
SEHEMU YA PILI
- 3 Verify source ↗
Madhumuni
AI-assisted research summary: Kanuni hizi zinaweka utaratibu wa uwajibikaji na fidia, na zinatoa haki ya fidia kwa watu au madhara yanayohusiana na ulinzi wa mazingira na uharibifu wa mazingira.
3. Malengo ya Kanuni hizi ni kuweka utaratibu wa uwajibikaji na fidia na kutoa haki ya fidia kwa- (a) mtu aliyepata madhara akiwa analinda mazingira au kutokana na uharibifu wa mazingira; (b) uharibifu wa mazingira unaotokana na ukiukaji wa viwango vya ulinzi wa mazingira; na (c) uharibifu wa mali unaotokana na uharibifu wa mazingira. SEHEMU YA TATU UTAWALA NA MUUNDO WA TAASISI
Part
SEHEMU YA TATU
- 4
AI-assisted research summary: Baraza must enforce these Regulations and carry out environmental-management, compensation, public participation, education, reconciliation, assessment, record-keeping, and other minister-directed duties.
4. Katika masuala yanayohusu utekelezaji wa masharti ya Kanuni hizi, Baraza - (a) (b) (c) (d) litahakikisha utekelezaji na uzingatiaji wa Kanuni hizi; litahamasisha utendaji bora ili kuhakikisha usimamizi thabiti wa mazingira; litachukua hatua kwa ajili ya upatikanaji wa fidia zinazotokana na uharibifu wa mazingira; litaratibu na kuhamasisha ushiriki wa umma katika shughuli zinazoashiria vihatarishi vya uharibifu wa mazingira; (e) litaandaa na kutoa elimu ya haki ya fidia; (f) litawezesha usuluhishi kati ya mlalamikaji na mlalamikiwa; (g) kwa kushirikiana na mamlaka husika za udhibiti, litafanya tathmini ya kina ili kujua kiwango cha uharibifu wa mazingira na kubaini sababu na hasara iliyopatikana; litatunza kumbukumbu za matukio ya uharibifu wa mazingira; litatekeleza majukumu mengine kama Waziri atakavyoelekeza chini ya Kanuni hizi. (h) (i) - 5
AI-assisted research summary: The Director must promote good environmental management, strengthen sector coordination and stakeholder engagement, enable relevant research, and carry out other tasks assigned by the Minister.
5. Kwa madhumuni ya utekelezaji wa masharti ya Kanuni hizi, Mkurugenzi- (a) (b) (c) (d) atahamasisha usimamizi bora wa mazingira; ataimarisha uratibu wa kisekta na uhamasishaji wa wadau kwa ajili ya udhibiti na usimamizi bora wa shughuli zinazoashiria vihatarishi vya uharibifu wa mazingira; atawezesha utafiti unaozingatia zinazoashiria vihatarishi vya uharibifu wa mazingira; na atatekeleza majukumu mengine atakayoelekezwa na Waziri. sera kuhusu shughuli - 6
AI-assisted research summary: Wizara za kisekta lazima zitoe ushauri wa kitaalamu, kiutawala na kisheria kuhusu haki ya fidia, zihamasishe uelewa wa umma, na zitimize majukumu mengine yatakayopangwa na Waziri baada ya kushauriana na waziri wa sekta.
6. Wizara za kisekta - (a) zitatoa ushauri wa kisekta wa kitaalamu, kiutawala na kisheria kuhusu haki ya fidia; (b) zitahamasisha uelewa kwa umma kuhusu haki ya fidia; na (c) zitatekeleza majukumu mengine kama Waziri atakavyoelekeza, baada ya kushauriana na waziri wa sekta. 4 Majukumu ya Baraza Majukumu ya Mkurugenzi Majukumu ya wizara za kisekta Tangazo La Serikali Na. 385 (Linaendelea) Kanuni za haki fidia Majukumu ya sekretarieti za mikoa Majukumu ya mamlaka za serikali za mitaa Uwajibikaji katika fidia - 7
AI-assisted research summary: Regional secretariats must coordinate and advise on compensation rights matters, run capacity-building programs, and carry out other duties as directed by the Minister after consultation with the minister responsible for local government.
7. Sekretarieti za mikoa, ndani ya maeneo ya mamlaka yao- (a) zitaratibu na kushauri tawala za mikoa na mamlaka za serikali za mitaa masuala yanayohusu haki ya fidia; (b) zitaratibu programu za kujenga uwezo katika tawala za mikoa na mamlaka za serikali za mitaa kuhusu masuala ya haki ya fidia; na (c) zitatekeleza majukumu mengine kama Waziri atakavyoelekeza, baada ya kushauriana na waziri mwenye dhamana ya serikali za mitaa. - 8 Verify source ↗
Majukumu ya Baraza
AI-assisted research summary: Mamlaka za serikali za mitaa lazima zitekeleze na kuhakikisha uzingatiaji wa Kanuni hizi ndani ya maeneo yao, zipokee malalamiko kuhusu haki za fidia, zisaidie jamii kwa elimu na ushauri, na zitekeleze majukumu mengine yatakayoelekezwa na Waziri.
8. Mamlaka za serikali za mitaa, ndani ya maeneo yao ya mamlaka- (a) zitahakikisha uzingatiaji na utekelezaji wa Kanuni hizi; (b) zitapokea malalamiko ya masuala yanayohusu haki za fidia; (c) zitahamasisha ujengaji wa uwezo kwa jamii na viongozi wa vijiji kuhusu masuala ya haki ya fidia; (d) zitatoa ushauri wa kitaalamu, kiutawala na kisheria kwa jamii kuhusu masuala ya haki ya fidia; na (e) zitatekeleza majukumu mengine kama Waziri atakavyoelekeza, baada ya kushauriana na waziri mwenye dhamana ya serikali za mitaa. SEHEMU YA NNE UWAJIBIKAJI KATIKA FIDIA
Part
SEHEMU YA NNE
- 9
AI-assisted research summary: Mmiliki au mwendeshaji anaweza kulazimika kulipa fidia na gharama za uharibifu ikiwa vitendo au kutotenda kwake vimesababisha madhara kwa mtu, mali, au mazingira.
9.-(1) Mmiliki au mwendeshaji ambaye kutenda au kutotenda kwake moja kwa moja, kwa namna isiyo ya moja kwa moja, papo kwa hapo au kwa baadaye wakati wa kulinda mazingira, kumesababisha madhara kwa mtu au mali atawajibika kulipa fidia na gharama za uharibifu husika uliojitokeza. (2) Bila kujali kanuni ndogo ya (1), ikiwa tukio linajumuisha tukio endelevu, wamiliki au waendeshaji wanaosimamia kwa kufuatana shughuli hatarishi inayosababisha uharibifu husika watawajibika kwa pamoja na mmoja mmoja. (3) Endapo ajali inajumuisha mfululizo wa matukio yenye chanzo kimoja inayotokana na shughuli hatarishi, wamiliki au waendeshaji wakati wa tukio watawajibika kwa pamoja au mmoja mmoja: Isipokuwa kwamba, endapo mmiliki au mwendeshaji atathibitisha kuwa kutokea kwa uharibifu huo kulichangiwa naye, atalazimika kufidia sehemu ya uharibifu aliochangia. (4) Bila kujali kanuni ndogo ya (2) na (3), Kanuni hizi hazitaathiri haki yoyote ya mmliki au mwendeshaji dhidi ya mtu mwingine. (5) Kwa madhumuni ya kuondoa shaka, aina za uwajibikaji wa uharibifu zinaweza kuamuliwa kwa misingi ya kuangalia chanzo, nia, namna na uzito wa madhara yaliyotokea kwa mtu au mali iliyoharibiwa au mazingira kama ifuatavyo: (a) uwajibikaji wa kiutawala; (b) uwajibikaji wa madai; na (c) uwajibikaji wa jinai. (6) Bila kuathiri masharti yaliyotangulia ya kanuni hii, kiwango cha uwajibikaji katika mahakama kuhusu masuala yanayohusu fidia kitakuwa uwajibikaji usiozingatia nia. Jukumu la
Part
sehemu ya uharibifu aliochangia.
- 10 Verify source ↗
11. Msamaha
AI-assisted research summary: Mmiliki au mwendeshaji ndiye anayebeba jukumu la kuthibitisha kuwa uharibifu unaodaiwa haukutokea.
10. Jukumu la kuthibitisha kutotokea kwa uharibifu unaodaiwa 5 Tangazo La Serikali Na. 385 (Linaendelea) Kanuni za haki fidia kuthibitisha kufanyika chini ya kanuni ya 9 litakuwa la mmiliki au mwendeshaji. Msamaha - 11 Verify source ↗
Msamaha
AI-assisted research summary: Mmiliki au mwendeshaji hana wajibu wa kulipa fidia kwa uharibifu unaotokana na hali fulani maalum zilizoainishwa katika kifungu hiki.
11. Mmiliki au mwendeshaji hatawajibika kulipa fidia ya uharibifu ambao- (a) ulisababishwa na matukio ya vita, uhasama, ugaidi, vita vya wenyewe kwa wenyewe, uasi au tukio la asili la kipekee, lisiloepukika na lisilozuilika; (b) umetokana na uzingatiaji wa amri mahususi au hatua ya lazima ya mamlaka ya umma; (c) ulisababishwa na uchafuzi wa mazingira katika viwango vinavyohimilika chini ya mazingira yanayohusika; au (d) ulisababishwa na shughuli hatarishi zilizofanyika kisheria kwa maslahi au ridhaa ya mtu aliyepata madhara hayo. Kosa la aliyepata madhara - 12 Verify source ↗
Kosa la aliyepata madhara
AI-assisted research summary: Fidia inaweza kutochaguliwa au kupunguzwa ikiwa mtu alipata madhara kutokana na kosa lake au kwa kuchangia madhara hayo.
12. Endapo mtu anapata madhara kutokana na kosa au uchangiaji wake mwenyewe kutokea kwa madhara hayo, fidia haitatolewa au itapunguzwa kwa kuzingatia mazingira husika. SEHEMU YA TANO UPATIKANAJI WA TAARIFA Upatikanaji wa taarifa kutoka mamlaka ya umma
Part
SEHEMU YA TANO
- 13 Verify source ↗
mwendeshaji
AI-assisted research summary: Mtu anaweza kuomba na kupata taarifa za mazingira kutoka kwa mamlaka ya umma, na mamlaka lazima ijibu kwa maandishi ndani ya siku 30.
13.-(1) Mtu anaweza, kwa njia ya maombi kupata taarifa zinazohusu mazingira kutoka katika mamlaka ya umma. (2) Haki ya kupata taarifa inaweza kuwekewa vizuizi chini ya sheria yoyote pale inapoathiri usiri wa- (a) mamlaka za umma; (b) uhusiano wa kimataifa; (c) usalama wa taifa; (d) usalama wa umma; (e) maslahi ya umma; (f) masuala yanayoendelea katika mahakama, au yaliyo chini ya uchunguzi, ikijumuisha uchunguzi wa kinidhamu, au ambayo yapo katika mwenendo wa uchunguzi wa awali; (g) haki za kibiashara au viwanda, ikijumuisha hakimiliki; (h) taarifa binafsi; au (i) taarifa zilizo chini ya au zilizotolewa na mtu mwingine ambaye hana wajibu wa kisheria wa kufanya hivyo. (3) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (2), taarifa kutoka mamlaka ya umma inaweza kutolewa kwa sehemu pale inapowezekana kutenganisha taarifa kuhusu masuala yaliyorejewa. (4) Maombi ya kupata taarifa yanaweza kukataliwa ikiwa- (a) yanahusisha usambazaji wa nyaraka ambazo hazijakamilika, taarifa au mawasiliano ya ndani; au (b) ni dhahiri kuwa hayana msingi. (5) Mamlaka ya umma itamjibu kwa maandishi mtu aliyeomba taarifa ndani ya siku thelathini kuanzia tarehe ya kupokea maombi. (6) Mtu anayetaka kupata taarifa za kimazingira kutoka katika mamlaka ya umma atalipa gharama kama zilivyoainishwa katika Kanuni za Ada na Tozo za Usimamizi wa Mazingira. T.S Na. 387 la 2021 Upatikanaji wa taarifa - 14
AI-assisted research summary: Mahakama inaweza kuamuru mmiliki au mwendeshaji kutoa taarifa; pia mmiliki au mwendeshaji lazima atoze taarifa fulani kuhusu vifaa na dutu zilizotumika katika shughuli iliyosababisha madhara kwa afya au mazingira.
14.-(1) Mahakama inaweza wakati wowote, kwa ajili ya utoaji wa haki, kuamuru mmiliki au mwendeshaji kutoa taarifa mahususi zinazohusu 6 Tangazo La Serikali Na. 385 (Linaendelea) Kanuni za haki fidia mahususi zilizopo kwa mmiliki au mwendeshaji madai ya fidia chini ya Kanuni hizi. (2) Mmiliki au mwendeshaji atalazimika kutoa taarifa kuhusu kifaa au mashine iliyotumika, aina na wingi wa dutu zilizotumika katika shughuli iliyosababisha athari mbaya kwa afya ya binadamu au mazingira. (3) Hatua za upataji taarifa chini ya Kanuni hizi hazitaathiri hatua yoyote ya uchunguzi ambayo inaweza kuamriwa kisheria chini ya sheria yoyote. Katazo la matumizi ya taarifa - 15 Verify source ↗
Upatikanaji wa taarifa mahususi
AI-assisted research summary: Aliyepewa taarifa chini ya Kanuni hizi haruhusiwi kuitumia nje ya madhumuni ya kutolewa kwake, kuivuruga, au kuisambaza bila kibali cha maandishi cha mtoa taarifa.
15. Mtu ambaye amepata taarifa chini ya masharti ya Kanuni hizi- (a) hatatumia taarifa kwa madhumuni mengine zaidi ya madhumuni ya kutolewa kwake; (b) hatatumia taarifa hiyo katika mazingira yanayokiuka masharti yaliyotajwa katika kanuni ya 13(2); (c) hatapotosha kwa namna yoyote taarifa iliyopatikana; au (d) bila kibali cha maandishi cha mtoa taarifa, hatahamisha, hatadurufu, hatahariri, hatasambaza au vinginevyo hatatumia taarifa zilizopatikana kwa njia nyingine yoyote. SEHEMU YA SITA MADAI YA FIDIA NA MADAI MENGINE Muda wa ukomo
Part
SEHEMU YA SITA
- 16 Verify source ↗
Muda wa ukomo
AI-assisted research summary: Mtu anayefungua madai ya fidia kwa uharibifu wa mazingira chini ya Kanuni hizi lazima afanye hivyo ndani ya miaka mitatu kuanzia siku ambayo alijua au alipaswa kujua madhara hayo.
16. Ukomo wa muda kwa mtu kufungua madai ya fidia kutokana na uharibifu wa mazingira chini ya Kanuni hizi utakuwa miaka mitatu kuanzia tarehe ambayo mdai alijua au alipaswa kujua madhara hayo. Vigezo vya kupata fidia Maombi ya fidia - 17 Verify source ↗
18. Maombi ya fidia
AI-assisted research summary: Mtu anaweza kulipwa fidia chini ya Kanuni hizi ikiwa alipata madhara akiwa analinda mazingira, alipata madhara kutokana na uharibifu wa mazingira, au mali yake iliharibika kutokana na uharibifu wa mazingira.
17. Mtu anaweza kulipwa fidia chini ya Kanuni hizi endapo- (a) alipata madhara wakati akilinda mazingira; (b) alipata madhara kutokana na uharibifu wa mazingira; au (c) mali yake iliharibika kutokana na uharibifu wa mazingira. - 18 Verify source ↗
Maombi ya fidia
AI-assisted research summary: Mtu aliyejeruhiwa au aliyeathirika, au wakili wake au mwakilishi wake, anaweza kuwasilisha maombi ya fidia kwa Baraza kwa maandishi.
18.-(1) Mtu aliyejeruhiwa au aliyeathirika, wakili wake au mwakilishi aliyemteua anaweza kuwasilisha maombi katika Baraza kwa maandishi kwa ajili ya madai ya fidia. (2) Maombi yatawasilishwa kwa njia ya barua inayoainisha taarifa zifuatazo: jina na anwani ya mtu aliyeathirika; (a) (b) jina na anwani ya mmiliki au mwendeshaji anayedaiwa fidia; (c) eneo ambalo uharibifu wa mazingira unadaiwa kutokea; (d) maelezo ya kiini cha madai; (e) aina ya nafuu au fidia inayoombwa; na (f) taarifa nyingine yoyote muhimu inayohusu madhara yaliyojitokeza. (3) Nyaraka zifuatazo zitaambatishwa kwenye maombi, pale zinapohitajika: (a) taarifa ya uchunguzi wa kitabibu kutoka kwa daktari au afisa wa afya; (b) maoni ya kitaalamu kutoka kwa mamlaka husika ya udhibiti na usimamizi; taarifa ya mtaalamu wa mazingira; (c) (d) taarifa ya uchambuzi kutoka maabara iliyopendekezwa; (e) (f) nyaraka nyingine yoyote ambayo Baraza linaweza kuona inafaa. taarifa ya tathmini ya tukio; na 7 Tangazo La Serikali Na. 385 (Linaendelea) Kanuni za haki fidia Usuluhishi - 19 Verify source ↗
Usuluhishi
AI-assisted research summary: Maombi yanayowasilishwa kwa Baraza yatashughulikiwa kwa usuluhishi, na Baraza lazima litume nakala kwa mhusika husika na notisi ya wito ndani ya siku 7.
19.-(1) Maombi yanayowasilishwa kwenye Baraza chini ya kanuni ya 18, yataamuliwa kwa njia ya usuluhishi. (2) Baraza, ndani ya siku saba kuanzia siku ya kupokea maombi, litatuma nakala ya maombi kwa mmiliki au mwendeshaji aliyetajwa kwenye maombi hayo, pamoja na notisi ya wito kwa ajili ya usuluhishi katika tarehe iliyopangwa. (3) Usuluhishi utafanyika ndani ya siku ishirini na nane kuanzia tarehe iliyoainishwa kwenye notisi ya wito. (4) Ukomo wa muda wa usuluhishi, kwa maombi ya pande zote mbili katika maombi hayo, unaweza kuongezwa kwa siku zisizozidi ishirini na nane. (5) Endapo usuluhishi umefanikiwa, Baraza litaweka katika maandishi masharti yaliyokubaliwa na pande zote zitatia saini hati ya makubaliano ya usuluhishi na makubaliano hayo yatakuwa uamuzi wa mwisho na utapaswa kuzingatiwa na pande zote. (6) Makubaliano ya usuluhishi yaliyofikiwa chini ya kanuni hii yatatekelezwa kama tuzo ya mahakama. (7) Mhusika anaweza kuwasilisha maombi ya utekelezaji wa makubaliano ya usuluhishi katika Mahakama Kuu. (8) Endapo litaandika kushindikana kwa usuluhishi huo na upande wowote unaweza kufungua kesi ya madai ya fidia katika mahakama yenye mamlaka. umeshindikana, Baraza usuluhishi (9) Suala lolote lililokubaliwa na upande wowote katika usuluhishi katika kesi halitatumika kama ushahidi wa kumuwajibisha mhusika iliyofunguliwa mahakamani. (10) Mashauri chini ya Kanuni hizi mbele ya Baraza au mahakama hayatatozwa malipo. - 20 Verify source ↗
Uhudhuriaji mbele ya Baraza
AI-assisted research summary: Wahusika lazima wahudhurie wenyewe au kupitia mawakili au wawakilishi wao.
20.-(1) Wahusika watahudhuria wenyewe au kupitia mawakili au wawakilishi wao. (2) Watu wanaowawakilisha wahusika katika usuluhishi watakuwa na hati ya uthibitisho wa uwakilishi inayowaidhinisha kuwawakilisha na kuamua kwa niaba ya wahusika. - 21 Verify source ↗
Utaratibu wa kufungua madai ya fidia mahakamani
AI-assisted research summary: Claims for compensation for environmental damage must be filed and handled in court under the procedure set out in the Civil Procedure Act.
21. Madai ya fidia ya uharibifu wa mazingira yatawasilishwa na kuendeshwa mahakamani kwa kuzingatia utaratibu ulioainishwa katika Sheria ya Mwenendo wa Mashauri ya Madai. Uhudhuriaji mbele ya Baraza Utaratibu wa kufungua madai ya fidia mahakamani Sura ya 33 SEHEMU YA SABA MASHARTI YA JUMLA Taarifa kuhusu maradhi au kifo
Part
SEHEMU YA SABA
- 22 Verify source ↗
23. Wajibu wa kutunza kumbukumbu
AI-assisted research summary: Registered doctors, health officers, and certain environmental/resource specialists must report certain suspected disease or death cases to the local council or local government authority immediately.
22.-(1) Daktari aliyesajiliwa ambaye, baada ya kufanya uchunguzi ana sababu za kuamini kuwa mtu amepata maradhi au amefariki kutokana na shughuli iliyosababisha athari kwa mazingira au afya ya binadamu, atatoa taarifa katika Baraza au mamlaka ya serikali ya mtaa husika mara moja. 8 Tangazo La Serikali Na. 385 (Linaendelea) Kanuni za haki fidia (2) Daktari, afisa wa afya au mtaalamu wa mazingira au rasilimali asilia ambaye anaamini kuwa maradhi fulani au kifo cha binadamu au wanyama kimetokana na uharibifu wa mazingira atatoa taarifa katika Baraza au mamlaka ya serikali ya mtaa husika mara moja. Wajibu wa kutunza kumbukumbu - 23 Verify source ↗
Wajibu wa kutunza kumbukumbu
AI-assisted research summary: A person carrying out activities that cause serious harm to human health or the environment must keep records of all process steps and submit those records to the Council at the end of each year.
23.-(1) Mtu anayefanya shughuli zinazosababisha madhara makubwa kwa afya ya binadamu au mazingira, atatunza kumbukumbu za michakato yote ya shughuli hiyo. (2) Kumbukumbu zitakazotunzwa kwa mujibu wa kanuni ndogo ya (1) zitajumuisha jina, maelezo na anwani ikiwamo barua pepe, msimbo wa posta kama upo, nukushi na namba za simu za watu waliohusika katika michakato hiyo na jambo lingine lolote ambalo linaweza kuelezwa au kujumuishwa katika masharti ya utekelezaji wa shughuli hiyo. (3) Kumbukumbu zilizotunzwa kwa mujibu wa kanuni ndogo ya (1) na (2) zitawasilishwa katika Baraza kila mwisho wa mwaka katika namna ambayo inaweza kuainishwa na Baraza. - 24 Verify source ↗
Matakwa ya tathmini ya maabara iliyoteuliwa
AI-assisted research summary: Maabara iliyoteuliwa inapaswa kufanya tathmini ya kiwango cha uharibifu kwa ajili ya ulipaji wa fidia chini ya Kanuni hizi.
24. Kwa madhumuni ya ulipaji wa fidia chini ya Kanuni hizi, tathmini ya kiwango cha uharibifu kutokana na shughuli hatarishi kwa afya ya binadamu au mazingira itafanywa na maabara iliyoteuliwa. Matakwa ya tathmini ya maabara iliyoteuliwa Rufaa - 25 Verify source ↗
26. Mamlaka ya kutoa miongozo au maelekezo ya kisera
AI-assisted research summary: A person dissatisfied with a decision under these Regulations may appeal. If the appeal goes to the Minister, it must be filed within 30 days and include a letter stating the reasons, the decision copy, and any other required documents. The Minister must decide within 14 days of receiving the appeal and notify the appellant with reasons within 7 days of making the decision.
25.-(1)Mtu ambaye hajaridhikaa na uamuzi uliotolewa chini ya Kanuni hizi anaweza kukata rufaa kwa mujibu wa masharti ya Sheria. (2) Endapo rufaa chini ya kanuni ndogo ya (1) inaenda kwa Waziri, rufaa hiyo itawasilishwa ndani ya siku thelathini kuanzia siku ya kutolewa uamuzi unaokatiwa rufaa na itakuwa kwa njia ya barua inayoeleza sababu za rufaa na itaambatishwa na nakala ya uamuzi uliotolewa kwa mujibu wa Kanuni hizi na nyaraka nyingine ambayo Waziri anaweza kuhitaji. (3) Waziri atatoa uamuzi ndani ya siku kumi na nne kuanzia siku ya kupokelewa kwa rufaa. (4) Waziri atatakiwa kumjulisha mleta rufaa uamuzi wake na sababu za uamuzi ndani ya siku saba kuanzia siku aliyotoa uamuzi. - 26 Verify source ↗
Mamlaka ya kutoa miongozo au maelekezo ya kisera
AI-assisted research summary: Waziri anaweza, baada ya kushauriana na wizara husika za kisekta, kutoa miongozo au maelekezo ya kisera ili kusaidia utekelezaji bora wa Kanuni hizi.
26. Waziri, baada ya kushauriana na wizara husika za kisekta, anaweza kutoa miongozo au maelekezo ya kisera kwa ajili ya kuwezesha utekelezaji bora wa Kanuni hizi. Mamlaka ya kutoa miongozo au maelekezo ya kisera Dodoma, ........………., 2024 SELEMANI SAIDI JAFO Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira 9
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Kanuni za Haki ya Fidia za Mwaka 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in