Kanuni za Upatikanaji na Mgawanyo wa Faida za Rasilimali za Kijenetiki za Mwaka 2024
Kanuni hizi zinaitwa Kanuni za Upatikanaji na Mgawanyo wa Faida za Rasilimali za Kijenetiki za Mwaka 2024.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Kanuni za Upatikanaji na Mgawanyo wa Faida za Rasilimali za Kijenetiki za Mwaka 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
Kanuni hizi zinaitwa Kanuni za Upatikanaji na Mgawanyo wa Faida za Rasilimali za Kijenetiki za Mwaka 2024. The Regulations apply to benefit-sharing from the use of genetic resources or traditional knowledge for research, commercial, or other non-commercial use in or outside Tanzania, but they do not apply in the listed exception cases. Section 3 gives key definitions for terms used in these Regulations, including benefit, access permit, National Coordinator, and prior written consent. Kanuni hizi zinaweka madhumuni ya kusimamia upatikanaji wa rasilimali za kijenetiki, mgawanyo wa faida, uhamasishaji wa matumizi endelevu ya bioanuai, elimu kwa jamii, na kulinda haki za msingi za jamii kuhusu rasilimali hizo na maarifa ya asili. The Government is given the power to identify, control, and coordinate access to Tanzania’s genetic resources or traditional knowledge, for the people’s benefit, under the Regulations and any applicable law.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Kanuni za Upatikanaji na Mgawanyo wa Faida za Rasilimali za Kijenetiki za Mwaka 2024
Showing 39 of 39
- 1
AI-assisted research summary: Kanuni hizi zinaitwa Kanuni za Upatikanaji na Mgawanyo wa Faida za Rasilimali za Kijenetiki za Mwaka 2024.
1. Kanuni hizi zitajulikana kama Kanuni za Upatikanaji na Mgawanyo wa Faida za Rasilimali za Kijenetiki za Mwaka 2024. - 2
AI-assisted research summary: The Regulations apply to benefit-sharing from the use of genetic resources or traditional knowledge for research, commercial, or other non-commercial use in or outside Tanzania, but they do not apply in the listed exception cases.
2.-(1) Kanuni hizi zitatumika kwenye mgawanyo wa faida zitokanazo na matumizi ya rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili, zinazotokea kiasili au kuasiliwa kulingana na mazingira katika eneo lake au nje ya eneo lake zinazokusudiwa kutumika kwa utafiti, biashara au matumizi mengine yasiyo ya kibiashara ndani na nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. (2) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo (1), Kanuni hizi hazitatumika kwenye upatikanaji wa rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili ambazo- (a) zinazalishwa na jamii kwa matumizi yao wenyewe; (b) zimethibitishwa kwa matumizi ya chakula au matumizi mengine kama ilivyoainishwa na sheria mahususi za sekta au ambazo hazitokani na madhumuni ya kibiashara au si kwa ajili ya 4 Kanuni za Upatikanaji na Mgawanyo wa Faida za Rasilimali za Kijenetiki Tangazo la Serikali Na. 387 (Linaendelea) kuingizwa nchini au kusafirishwa kwenda nchi nyingine isiyo ya asili; (c) zinatokana na wanyama na mimea kama zinazosimamia sheria ilivyofafanuliwa uzalishaji wa aina mbalimbali; na (d) zimekusudiwa kwa madhumuni ya utafiti wa kielimu ulioidhinishwa katika taasisi za taaluma na na kusimamiwa na mamlaka husika; au utafiti Tanzania zinazotambuliwa (e) zinatokana na binadamu. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Jina
AI-assisted research summary: Section 3 gives key definitions for terms used in these Regulations, including benefit, access permit, National Coordinator, and prior written consent.
3. Katika Kanuni hizi, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “Baraza” maana yake ni kama ilivyoainishwa chini ya Sheria; “faida” maana yake ni faida yoyote ya kifedha au isiyo ya kifedha au faida au riba au manufaa yanayotokana na au inayozalishwa kutokana na matumizi ya kibiashara, yasiyo ya kibiashara, matumizi ya viwandani au matumizi ya kiuchumi ya rasilimali za kibaiolojia au kijenetiki au maarifa yake ya kiasili yanayotumika kupata, kuendeleza au kuboresha bidhaa au mchakato; “faida za kifedha” maana yake ni malipo ya kifedha yanayofanywa au faida inayotokana na matumizi ya rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili; “haki miliki” maana yake ni wazo, uvumbuzi au ubunifu ambao msingi wake una dhamira ya umma ya kutoa hadhi ya umiliki wa mali; “jukwaa la taarifa” maana yake ni jukwaa la kimtandao la kubadilishana taarifa ili kuwezesha utekelezaji wa Itifaki ya Nagoya; “kibali cha upatikanaji” maana yake ni hati inayotolewa na mamlaka ya usimamizi ambayo inamruhusu mtu kupata rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya 5 Kanuni za Upatikanaji na Mgawanyo wa Faida za Rasilimali za Kijenetiki Tangazo la Serikali Na. 387 (Linaendelea) kiasili; “kibali cha kusafirisha nje ya nchi” maana yake ni hati inayotolewa na Mratibu wa Kitaifa kwa mtu anayekusudia kusafirisha rasilimali za kijenetiki kwenda nje ya nchi iwe kwa biashara au si kwa biashara; “kibali cha utafiti” maana yake ni hati inayotolewa na Mamlaka ya Usimamizi wa utafiti kwa mtu anayekusudia kufanya utafiti wa rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili; “matumizi ya kibiashara” maana yake ni matumizi ya rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili kwa faida ya kifedha au madhumuni mengine yenye uelekeo wa faida; “maarifa yake ya kiasili” maana yake ni maarifa yaliyopatikana ambayo ni muhimu kwa uhifadhi na matumizi endelevu ya rasilimali za kijenetiki au ambayo yana thamani ya kijamii na kiuchumi, na ambayo yameendelezwa kwa miaka mingi katika jamii; “makubaliano ya mgawanyo wa faida” maana yake ni makubaliano baina ya mwombaji na Mamlaka ya Usimamizi kwa madhumuni ya kuainisha jinsi ya kugawana faida itokanayo na matumizi ya rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili; “makubaliano ya kubadilishana takwimu” maana yake ni mkataba rasmi ambao unaainisha aina ya takwimu zitakazoweza kutumika kwa pamoja na matumizi yake stahiki; “makubaliano ya uhamishaji vinasaba” maana yake ni makubaliano kati ya Mamlaka ya Usimamizi au mwakilishi wake na mkusanyaji, yanayoweka masharti kuhusu namna rasilimali za kijenetiki zinaweza kuhamishwa kutoka upande mmoja kwenda mwingine; “Mamlaka ya Usimamizi” maana yake ni ofisi ya Serikali, 6 Kanuni za Upatikanaji na Mgawanyo wa Faida za Rasilimali za Kijenetiki Tangazo la Serikali Na. 387 (Linaendelea) wizara, idara, mamlaka ya udhibiti, taasisi za utafiti, mamlaka ya serikali za mitaa, au wakala inayohusika na usimamizi wa suala lolote la rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili; “masharti yanayokubaliwa kwa pamoja” maana yake ni masharti yaliyowekwa katika makubaliano kati ya mtoa huduma na mkusanyaji kwa ajili ya upatikanaji na utumiaji wa rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili pamoja na mgawanyo wa faida unaotokana na matumizi yake; “matumizi ya rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili” maana yake ni matumizi ya rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili kwa madhumuni ya kibiashara au yasiyo ya kibiashara; “matumizi yasiyo ya kibiashara” maana yake ni matumizi ya rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili kwa madhumuni ya kitaaluma, utafiti au madhumuni mengine yasiyo na uelekeo wa kibiashara; “mgawanyo wa faida” maana yake ni mgawanyo wa haki na usawa wa faida ya kifedha na isiyo ya kifedha inayotokana na au kutoka katika matumizi ya rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili kati ya mkusanyaji na mmiliki halali; “mkusanyaji” maana yake ni mtu au wakala wake ambaye amepata kibali cha upatakanaji wa rasilimali za kijenetiki au bidhaa zake zitokanazo na au maarifa yake ya kiasili yanayotakana na au yenye asili ya Tanzania; “Mratibu wa Kitaifa” maana yake ni Wizara yenye dhamana ya mazingira; “mwombaji” maana yake ni mtu ambaye anatuma maombi rasmi ya kupata rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili; “Ridhaa ya Awali ya Maandishi” maana yake ni idhini ya maandishi ya awali inayotolewa na Mamlaka ya Usimamizi au jamii husika kwa mkusanyaji ili 7 Kanuni za Upatikanaji na Mgawanyo wa Faida za Rasilimali za Kijenetiki Tangazo la Serikali Na. 387 (Linaendelea) kupata rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya asili; “rasilimali ya kijenetiki” maana yake ni kama ilivyoainishwa katika Sheria; Sura ya 191 “Sheria” maana yake ni Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; “upatikanaji” maana yake ni kupata, kumiliki na kutumia rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili yanayohifadhiwa, iwe bidhaa zinazotokana na, na pale ambapo inatumika, sehemu ya rasilimali isiyoshikika, kwa madhumuni ya utafiti, utafutaji wa viumbe hai, uhifadhi, matumizi ya viwandani au matumizi ya kibiashara; “utaratibu wa haki na usawa” maana yake ni hatua zinazochukuliwa kuhakikisha faida zinazotokana na matumizi ya rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili, pamoja na matumizi na biashara zitakazotokana nazo zinagawanywa kwa njia ya haki na usawa miongoni mwa taasisi au jamii zote zilizotambuliwa katika kuchangia usimamizi wa rasilimali, utafiti na maendeleo au biashara; “utafutaji wa viumbe hai” maana yake ni utafutaji na ukusanyaji wa rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili kwa madhumuni ya biashara au yasiyo ya kibiashara; “vinasaba” maana yake ni kama ilivyoainishwa katika Sheria; “Waziri” maana yake ni Waziri mwenye dhamana ya mazingira. SEHEMU YA PILI MADHUMUNI Madhumuni
Part
SEHEMU YA PILI
- 4 Verify source ↗
Madhumuni
AI-assisted research summary: Kanuni hizi zinaweka madhumuni ya kusimamia upatikanaji wa rasilimali za kijenetiki, mgawanyo wa faida, uhamasishaji wa matumizi endelevu ya bioanuai, elimu kwa jamii, na kulinda haki za msingi za jamii kuhusu rasilimali hizo na maarifa ya asili.
4. Madhumuni ya Kanuni hizi ni- (a) kuainisha utaratibu na namna ya kupata rasilimali za kijenetiki; 8 Kanuni za Upatikanaji na Mgawanyo wa Faida za Rasilimali za Kijenetiki Tangazo la Serikali Na. 387 (Linaendelea) (b) kuhamasisha usimamizi na matumizi endelevu ya bioanuai; (c) kuweka utaratibu wa mgawanyo wa faida rasilimali za zitokanazo na matumizi ya kijenetiki au maarifa yake ya kiasili; (d) kutoa elimu na kukuza uelewa wa jamii kuhusu upatikanaji wa rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili; na (e) kutambua, kulinda, na kutunza haki za msingi za jamii kuhusu rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili yanayopatikana ndani ya eneo lao. SEHEMU YA TATU USIMAMIZI WA RASILIMALI ZA KIJENETIKI Umiliki wa rasilimali za kijenetiki
Part
SEHEMU YA TATU
- 5
AI-assisted research summary: The Government is given the power to identify, control, and coordinate access to Tanzania’s genetic resources or traditional knowledge, for the people’s benefit, under the Regulations and any applicable law.
5. Haki ya kutambua, kudhibiti na kuratibu upatikanaji wa rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili ya Tanzania imekasimiwa kwa Serikali kwa manufaa ya watu na itatekelezwa kwa mujibu wa Kanuni hizi na sheria yoyote husika. Jukumu la kulinda maslahi ya Taifa - 6 Verify source ↗
Umiliki wa rasilimali za kijenetiki
AI-assisted research summary: A person exercising authority under these Rules must consider the interests of Tanzania.
6. Mtu yoyote anayetekeleza mamlaka yake kwa mujibu wa Kanuni hizi katika kufanya uamuzi, kutoa amri, kutekeleza mamlaka yoyote, au utendaji wa kazi, au wajibu wowote atazingatia maslahi ya Taifa la Tanzania. SEHEMU YA NNE MUUNDO WA KIUTAWALA NA KITAASISI Mratibu wa Kitaifa
Part
SEHEMU YA NNE
- 7
AI-assisted research summary: Wizara yenye dhamana ya mazingira itakuwa Mratibu wa Kitaifa wa Itifaki ya Nagoya kuhusu upatikanaji, matumizi, na ugawanyo wa faida zitokanazo na rasilimali za kijenetiki.
7. Wizara yenye dhamana ya mazingira itakuwa ni Mratibu wa Kitaifa wa Itifaki ya Nagoya kuhusu Upatikanaji, Matumizi na Mgawanyo wa Haki na Usawa wa Faida zitokanazo na Rasilimali za Kijenetiki. Majukumu ya - 8
AI-assisted research summary: Mratibu wa Kitaifa lazima afanye kazi kadhaa za kusimamia upatikanaji na mgawanyo wa faida za rasilimali za kijenetiki, ikiwemo kutoa vibali vya usafirishaji nje ya nchi.
8. Mratibu wa Kitaifa atapaswa- 9 Kanuni za Upatikanaji na Mgawanyo wa Faida za Rasilimali za Kijenetiki Tangazo la Serikali Na. 387 (Linaendelea) Mratibu wa Kitaifa (a) kuhakikisha kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inanufaika kutokana na rasilimali za kijenetiki kiasili yaliyopatikana; au maarifa yake ya (b) kutoa kibali cha usafirishaji nje ya nchi wa rasilimali za kijenetiki; (c) kuanzisha mawasiliano na ushirikiano wa kitaifa, kikanda na mashirika na taasisi za kimataifa; (d) kutoa na kuratibu mwongozo wa kisera wa masuala yanayohusu upatikanaji na mgawanyo wa faida itokanayo na matumizi ya rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; (e) kushirikiana na ofisi au wizara yenye dhamana ya mazingira ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa masuala yanayohusu upatikanaji na mgawanyo wa faida chini ya Itifaki ya Nagoya; (f) kuhakikisha uendeshaji wa Jukwaa la Kitaifa la kubadilishana taarifa za masuala ya rasilimali za kijenetiki zinazopatikana, kusafirishwa nje ya nchi, kuingiza ndani ya nchi au kupitishwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; (g) kushirikiana na wadau katika kuwezesha ujengaji wa uwezo kwa masuala yanayohusu utekelezaji wa Kanuni hizi; (h) kuratibu, kufuatilia na kutathmini utekelezaji na usimamizi wa matakwa ya Kanuni hizi; (i) kufuatilia na kutathmini ufanisi na utekelezaji wa shughuli zinazotekelezwa na Mamlaka ya Usimamizi hizi zinazingatiwa; kuhakikisha Kanuni ili (j) kuhamasisha ushiriki wa jamii na kujenga uelewa kuhusu upatikanaji na mgawanyo wa faida unaotokana na matumizi ya rasilimali za kijenetiki na maarifa yake ya kiasili; 10 Kanuni za Upatikanaji na Mgawanyo wa Faida za Rasilimali za Kijenetiki Tangazo la Serikali Na. 387 (Linaendelea) Mamlaka ya Usimamizi Sura ya 226 Majukumu ya Mamlaka ya Usimamizi (k) kupokea kutoka kwenye Mamlaka ya Usimamizi taarifa za ukaguzi wa vibali kutoka kwenye nchi ambayo rasilimali za kijenetiki zilizoingizwa ndani ya au kusafirishwa kutoka au kupitia Tanzania zimetokea; na (l) kutekeleza majukumu mengine yoyote yanayowezesha utekelezaji wa Kanuni hizi. - 9 Verify source ↗
10. Majukumu ya Mamlaka za Usimamizi
AI-assisted research summary: Certain government bodies and research-related institutions are recognized as Supervisory Authorities for compliance and enforcement, and the Tanzania Commission for Science and Technology is also a Supervisory Authority for research oversight matters.
9.-(1) Kwa madhumuni ya uzingatiaji na utekelezaji wa Kanuni hizi, ofisi za serikali, wizara, idara, wakala, mamlaka ya serikali za mitaa na taasisi zinazohusika na usimamizi wa rasilimali mahususi za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili zitatambulika kama Mamlaka ya Usimamizi. (2) Bila kuathiri kanuni ndogo ya (1), Tume ya Sayansi na Teknolojia ya Tanzania iliyoanzishwa na Sheria ya Tume ya Sayansi na Teknolojia ya Tanzania itakuwa Mamlaka ya Usimamizi katika masuala yanayohusu usimamizi, ufuatiliaji, uhamasishaji na uratibu wa tafiti za rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili. - 10 Verify source ↗
Majukumu ya Mamlaka za Usimamizi
AI-assisted research summary: Mamlaka ya Usimamizi ina majukumu ya kupokea na kushughulikia maombi, kushirikiana na mamlaka nyingine, kulinda haki za jamii, kuweka hifadhi ya nakala, na kuwasilisha taarifa za mwaka.
10. Kila Mamlaka ya Usimamizi itakuwa na majukumu yafuatayo: (a) kupokea na kushughulikia maombi ya kibali cha upatikanaji wa rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili; (b) kupitia maombi na kupendekeza kwa Mratibu wa Kitaifa kwa maandishi, kuhusu utoaji wa kibali cha usafirishaji nje ya nchi rasilimali za kijenetiki; (c) kushirikiana na wizara yenye dhamana ya serikali za mitaa katika mchakato wa maombi ya kupata rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili yanayosimamiwa na serikali za mitaa au jamii; 11 Kanuni za Upatikanaji na Mgawanyo wa Faida za Rasilimali za Kijenetiki Tangazo la Serikali Na. 387 (Linaendelea) (d) kushirikiana na Mratibu wa Kitaifa au mamlaka nyingine zinazohusika, kufuatilia matumizi ya rasilimali za kijenetiki; (e) Kuhakikisha haki za jamii ambapo rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili yanapatikana zinalindwa; (f) kuanzisha hifadhi ya nakala ya sampuli, taarifa, teknolojia au maarifa ya kiasili ya vinasaba vya kijenetiki, zilizopatikana, zilizoingizwa nchini au kusafirishwa nje ya nchi; (g) kuwasilisha kwa Mratibu wa Kitaifa taarifa za mwaka zinazohusiana na utekelezaji wa Kanuni hizi; (i) kuwezesha majadiliano (h) kuhakikisha kwamba uhaulishaji wa teknolojia taarifa kuhusiana na au ubadilishanaji wa rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili unatekelezwa na watu wanaopata rasilimali hizo; uingiaji wa makubaliano ya uhamishaji wa vinasaba, takwimu na makubaliano ya kubadilishana masharti pamoja yakijumuisha vigezo na masharti ambayo kwayo upatikanaji utaruhusiwa; yanayokubaliwa kwa na na yanayojitosheleza (j) kuhakikisha kwamba makubaliano yote ya uhamishaji wa vinasaba, makubaliano ya masharti takwimu kubadilishana yanayokubaliwa kwa pamoja yanajumuisha masharti ya mgawanyo wa faida zitokanazo na matumizi ya rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili ya Tanzania; (k) kuhakikisha na ushirikishwaji wa jamii husika katika mchakato wa upatikanaji wa rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili yanayopatikana katika eneo lao, ikijumuisha ridhaa yao ya awali; na ujumuishaji, uhusishwaji kwa ajili 12 Kanuni za Upatikanaji na Mgawanyo wa Faida za Rasilimali za Kijenetiki Tangazo la Serikali Na. 387 (Linaendelea) (l) kutekeleza majukumu mengine yoyote kwa ajili ya utekelezaji wa Kanuni hizi. Majukumu ya mamlaka za serikali za mitaa - 11 Verify source ↗
Majukumu ya mamlaka za serikali za mitaa
AI-assisted research summary: Mamlaka ya serikali za mitaa husika inayosimamia rasilimali za kijenetiki au maarifa ya kiasili lazima isaidae mwombaji, ilinde haki za jamii, ishiriki katika upatikanaji, itoe ushauri, ilinde kanuni na urithi wa kitamaduni, na ihifadhi kumbukumbu za makubaliano na ridhaa ya awali ya maandishi.
11. Kwa madhumuni ya kuondoa shaka, mamlaka ya serikali za mitaa husika inayosimamia rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili katika maeneo ya kiutawala itakuwa na wajibu wa- (a) kuwezesha mwombaji kupata rasilimali za Wajibu wa jamii kijenetiki au maarifa yake ya kiasili; (b) kuhakikisha haki za jamii kuhusu rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili zinalindwa; (c) kushiriki katika mchakato wa upatikanaji wa rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili; (d) kutoa ushauri kuhusu masuala yanayohusiana na rasilimali za upatikanaji au matumizi ya kijenetiki au maarifa yake ya kiasili; (e) kulinda kanuni za kitamaduni, haki, thamani au urithi kwenye rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili; na (f) kuweka kumbukumbu za makubaliano na ridhaa ya awali ya maandishi. - 12 Verify source ↗
Wajibu wa jamii
AI-assisted research summary: Jamii zina wajibu wa kutoa ridhaa ya awali ya maandishi kwa matumizi ya rasilimali za kijenetiki au maarifa ya kiasili ndani ya maeneo yao, na pia kuyalinda, kuyasimamia, na kuyatumia kwa njia endelevu.
12. Jamii zitakuwa na wajibu wa- (a) kutoa ridhaa ya awali ya maandishi kuhusu utumiaji wa rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili yanayopatikana ndani ya maeneo yao kama ilivyoainishwa kwenye Jedwali la Kwanza; (b) kuhifadhi na kusimamia rasilimali za kijenetiki; (c) kutunza na kulinda mila, desturi na maadili rasilimali za yanayotokana na uwepo wa kijenetiki au maarifa yake ya kiasili; (d) kutumia rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili yanazopatikana ndani ya maeneo yao ya kiutawala kwa njia endelevu; na (e) kutunza na kulinda maarifa mengine ya kiasili. 13 Kanuni za Upatikanaji na Mgawanyo wa Faida za Rasilimali za Kijenetiki Tangazo la Serikali Na. 387 (Linaendelea) SEHEMU YA TANO UDHIBITI NA USIMAMIZI WA UPATIKANAJI NA MGAWANYO WA FAIDA ZA RASILIMALI ZA KIJENETIKI Upatikanaji wa rasilimali za kijenetiki
Part
SEHEMU YA TANO
- 13 Verify source ↗
14. Maombi ya Kibali cha Upatikanaji
AI-assisted research summary: A person may not obtain, develop, or use Tanzania’s genetic resources or associated traditional knowledge without a permit from the supervising authority.
13. Mtu hataweza kupata, kuendeleza au kutumia rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kijamii ya Tanzania bila kibali kutoka kwa Mamlaka ya Usimamizi. Maombi ya kibali cha upatikanaji Taratibu za maombi ya kibali cha upatikanaji - 14 Verify source ↗
Maombi ya Kibali cha Upatikanaji
AI-assisted research summary: A person who intends to obtain genetic resources or their indigenous knowledge for commercial or non-commercial purposes must apply for an access permit from the supervisory authority.
14. Mtu anayekusudia kupata rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili kwa madhumuni ya kibiashara au yasiyo ya kibiashara, ataomba kibali cha upatikanaji kutoka kwa Mamlaka ya Usimamizi. - 15 Verify source ↗
Taratibu za maombi ya Kibali cha Upatikanaji
AI-assisted research summary: Mamlaka ya Usimamizi inapaswa kuzingatia masharti na mambo yaliyoorodheshwa wakati wa kushughulikia maombi ya kibali cha upatikanaji wa rasilimali za kijenetiki au maarifa ya kiasili.
15. -(1) Taratibu za maombi ya kibali cha upatikanaji zitakuwa ni kwa mujibu wa sheria mahususi zinazosimamia rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili. (2) Bila kuathiri kanuni ndogo ya (1) na sheria zingine zinazohusiana na rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili, kila Mamlaka ya Usimamizi itapaswa, wakati inaposhughulikia maombi ya kibali cha upatikanaji wa rasilimali hizo, kuzingatia yafuatayo: (a) ridhaa ya awali ya maandishi iliyopatikana kutoka kwa jamii au mamlaka husika ya serikali za mitaa; (b) makubaliano ya mgawanyo wa faida ulioanzishwa kwa mujibu wa Kanuni hizi; (c) kama hali ya uhifadhi wa rasilimali ya kijenetiki inajulikana; (d) kama tathmini ya athari kwa jamii imefanyika; (e) kama upatikanaji unaweza kusababisha upotevu wa kijenetiki au kuathiri mfumo wa ikolojia; (f) upatakanaji hauathiri usalama wa chakula; (g) matumizi ya rasilimali ya kijenetiki au maarifa yake ya kiasili si kwa madhumuni yaliyo 14 Kanuni za Upatikanaji na Mgawanyo wa Faida za Rasilimali za Kijenetiki Tangazo la Serikali Na. 387 (Linaendelea) kinyume na maslahi ya Taifa; (h) matumizi ya rasilimali ya kijenetiki au maarifa yake ya kiasili si kwa ajili ya kutengeneza silaha za kibaiolojia au kikemikali kwa madhumuni ya matumizi ya kijeshi au kigaidi; (i) mwombaji hajawahi kutenda kosa chini ya sheria yoyote inayotumika ndani au nje ya Tanzania; (j) mwombaji amefilisika; asiwe ametangazwa kuwa (k) maombi yanazingatia matakwa ya Kanuni hizi au sheria nyingine yoyote; na (l) matumizi ya rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili yasiwe kinyume na makubaliano ya kimataifa yanayohusika au hati ambazo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni mwanachama. - 16 Verify source ↗
Wajibu wa mmiliki wa Kibali cha Upatikanaji
AI-assisted research summary: Mmiliki wa kibali cha upatikanaji lazima azingatie makubaliano husika, aripoti ugunduzi kwa Mamlaka ya Usimamizi, atoee taarifa za nusu mwaka na mwaka, atoee taarifa ya mwisho kwa ukusanyaji wa miezi mitatu au chini, na ahakikishe faida zinagawanywa kwa mujibu wa Kanuni hizi.
16. Mmiliki wa kibali cha upatikanaji atakuwa na wajibu wa- (a) kuzingatia makubaliano ya uhamishaji wa vinasaba au kubadilishana takwimu kwa mujibu wa Kanuni hizi; (b) kuitaarifu Mamlaka ya Usimamizi kuhusu ugunduzi wote utakaofanyika katika kipindi chote cha kibali; (c) kutoa taarifa ya nusu mwaka na ya mwaka kuhusu maendeleo ya ukusanyaji unaoendelea wa rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili; (d) ikiwa ukusanyaji ni wa muda wa miezi mitatu au chini ya hapo, kutoa taarifa ya mwisho ya ukusanyaji wa rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili; na Wajibu wa mmiliki wa kibali cha upatikanaji (e) kuhakikisha faida zinazotokana na rasilimali za kiasili kijenetiki zinagawanywa kwa mujibu wa Kanuni hizi. au maarifa yake ya 15 Kanuni za Upatikanaji na Mgawanyo wa Faida za Rasilimali za Kijenetiki Tangazo la Serikali Na. 387 (Linaendelea) Zuio la kusafirisha nje ya nchi - 17 Verify source ↗
18. Maombi ya Kibali cha kusafirisha nje ya nchi
AI-assisted research summary: Mtu hapaswi kusafirisha rasilimali za kijenetiki kwenda nje ya nchi bila kibali cha kusafirisha kwenda nje ya nchi kilichoainishwa katika Jedwali la Pili.
17. Mtu hatasafirisha rasilimali za kijenetiki kwenda nje ya nchi bila kuwa na kibali cha kusafirisha kwenda nje ya nchi kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Pili. Maombi ya ibali cha usafirishaji nje ya nchi ambaye - 18 Verify source ↗
Maombi ya Kibali cha kusafirisha nje ya nchi
AI-assisted research summary: Mtu anayetaka kusafirisha rasilimali za kijenetiki nje ya nchi kwa shughuli za kibiashara au zisizo za kibiashara lazima aombe kibali kwa Mratibu wa Kitaifa.
18.-(1) Mtu anakusudia kusafirisha rasilimali za kijenetiki kwenda nje ya nchi kwa madhumuni ya kibiashara au yasiyo ya kibiashara, ataomba kibali cha usafirishaji nje ya nchi kwa Mratibu wa Kitaifa. (2) Maombi ya kibali cha usafirishaji nje ya nchi yatafanywa kupitia fomu iliyoainishwa katika Jedwali la Tatu. Nyaraka za kuambatisha - 19
AI-assisted research summary: Maombi ya kibali cha usafirishaji nje ya nchi lazima yaambatanishwe na nyaraka na taarifa zilizoainishwa.
19. Maombi ya kibali cha usafirishaji nje ya nchi yataambatishwa na- (a) ridhaa ya awali ya maandishi kutoka kwa jamii inayosimamia rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili; (b) kibali cha upatikanaji au kibali cha utafiti kinachotolewa na Mamlaka ya Usimamizi; (c) Makubaliano ya Mgawanyo wa Faida; (d) vigezo vilivyokubaliwa kwa pamoja; (e) Makubaliano ya Uhamishaji wa Vinasaba; (f) uthibitisho wa malipo ya ada ya maombi iliyoainishwa katika Jedwali la Nne; na (g) maelezo muhimu nyingine au zinazoweza kuhitajika na Mratibu wa Kitaifa wakati wa kuwasilisha maombi. nyaraka Uthibitisho wa kibali cha kuingiza au kupitisha nchini - 20
AI-assisted research summary: Mtu anayeingiza au kusafirisha rasilimali za kijenetiki kupitia Tanzania lazima aziweke wazi kwa Maafisa Forodha na atoе ushahidi wa kisheria wa upatikanaji kutoka nchi asili.
20. Kwa madhumuni ya kuzingatia Itifaki ya Nagoya, mtu anayeingiza ndani au anayesafirisha rasilimali za kijenetiki kupitia Tanzania ataweka wazi rasilimali za kijenetiki zilizopo kwenye miliki yake au zilizo chini ya udhibiti wake kwa Maafisa Forodha katika kituo cha kuingia au kutoka nchini, na atatoa ushahidi wa kisheria wa upatikanaji wa rasilimali hizo za kijenetiki 16 Kanuni za Upatikanaji na Mgawanyo wa Faida za Rasilimali za Kijenetiki Tangazo la Serikali Na. 387 (Linaendelea) kutoka nchi asili. Zuio la kuhamisha umiliki wa kibali Haki miliki kwa jamii - 21
AI-assisted research summary: Bila idhini ya mamlaka iliyotoa kibali, kibali cha usafirishaji nje ya nchi au kibali cha upatikanaji hakihamishwi.
21. Umiliki wa kibali cha usafirishaji nje ya nchi au kibali cha upatikanaji kilichotolewa chini ya Kanuni hizi hautahamishwa bila idhini ya mamlaka iliyokitoa. - 22
AI-assisted research summary: Mratibu wa Kitaifa lazima kuwezesha ulinzi wa haki miliki za jamii zinazotokana na desturi, mila na sheria za kimila. Uchapishaji wa taarifa kuhusu rasilimali za kijenetiki au maarifa ya kiasili hauzuii jamii kutumia haki zake.
22.-(1) Mratibu wa Kitaifa atawezesha ulinzi wa haki miliki za jamii kama zilivyohifadhiwa na kulindwa chini ya desturi, mila na sheria za kimila zinazopatikana ndani ya iwe sheria hizo zimeandikwa au hazijaandikwa. jamii (2) Utangazaji wa taarifa za kimaandishi au matamshi ya rasilimali za kijenetiki, maarifa yake ya kiasili, uwepo wa rasilimali za kijenetiki katika benki ya jeni, makusanyo mengine yoyote au matumizi yake ya kiasili hayatazuia jamii kutumia haki zake za haki miliki kuhusiana na rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili. Uhalali wa kibali cha usafirishaji nje ya nchi - 23
AI-assisted research summary: A permit for exporting goods outside the country is valid for the period stated in the permit and only covers the genetic resources or traditional knowledge identified in it.
23. Kibali cha usafirishaji nje ya nchi kilichotolewa chini ya Kanuni hizi- (a) kitakuwahalali kwa kipindi kilichoainishwa kwenye kibali hicho; na (b) kitatumika kwa rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili yaliyoainishwa katika Kibali hicho. Kusitishwa kwa kibali cha usafirishaji nje ya nchi - 24 Verify source ↗
ya Nchi
AI-assisted research summary: Mmiliki wa kibali cha usafirishaji nje ya nchi lazima ajibu notisi ndani ya siku 30, na Mratibu wa Kitaifa lazima atoe notisi, aamue ndani ya siku 14 za kazi, na atangaze uamuzi wa kusitisha, kufuta au kubatilisha kibali kwenye magazeti matatu makubwa ikiwa kibali kimeondolewa.
24.-(1) Endapo mmiliki anatakiuka vigezo au masharti yaliyowekwa, Mratibu wa Kitaifa kupitia notisi ya maandishi atamjulisha mmiliki wa kibali kuhusu nia ya kusitisha, kufuta au kubatilisha kibali hicho. (2) Mmiliki wa kibali cha usafirishaji nje ya nchi atatakiwa, ndani ya siku thelathini tangu kupokea notisi, kuwasilisha utetezi wa kwanini kibali hicho kisisitishwe, kisifutwe au kubatilishwa. (3) Mratibu wa Kitaifa baada ya kupokea 17 Kanuni za Upatikanaji na Mgawanyo wa Faida za Rasilimali za Kijenetiki Tangazo la Serikali Na. 387 (Linaendelea) uwasilishwaji, ndani ya siku kumi na nne za kazi, atamjulisha mmiliki wa kibali cha usafirishaji nje ya nchi uamuzi wake. (4) Endapo Mratibu wa Kitaifa amesitisha, amefuta au amebatilisha kibali cha usafirishaji nje ya nchi atatangaza uamuzi huo angalau katika magazeti matatu yenye mzunguko mkubwa nchini. Ufuatiliaji wa uzingatiaji wa kibali cha upatikanaji au usafirishaji nje ya nchi - 25 Verify source ↗
Nje ya Nchi
AI-assisted research summary: The Supervisory Authority monitors compliance with conditions in an access permit, and the National Coordinator monitors compliance with conditions in an export permit.
25.-(1) Mamlaka ya Usimamizi itafuatilia uzingatiaji wa vigezo na masharti yaliyowekwa kwenye kibali cha upatikanaji kwa mujibu wa Kanuni hizi au sheria inayosimamia rasilimali husika za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili. (2) Mratibu wa Kitaifa atafuatilia uzingatiaji wa vigezo na masharti yaliyowekwa katika kibali cha usafirishaji nje ya nchi. SEHEMU YA SITA UTARATIBU WA MGAWANYO WA FAIDA Mgawanyo wa faida iliyopatikana
Part
SEHEMU YA SITA
- 26 Verify source ↗
Mgawanyo wa faida
AI-assisted research summary: Faida kutoka kwa makusanyo, maboresho, na matumizi ya rasilimali za kijenetiki au maarifa ya kiasili lazima zigawanywe kwa haki na usawa, kwa masharti yanayokubaliwa kwa pamoja.
26.-(1) Faida kwenye makusanyo, maboresho na matumizi ya rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili zitagawanywa kwa mujibu wa misingi ya haki na usawa na masharti yanayokubaliwa kwa pamoja. kutoka (2) Mmiliki wa kibali cha usafirishaji nje ya nchi atawezesha mgawanyo wa faida ya kifedha na isiyo ya kifedha itokanayo na matumizi ya rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili. (3) Kwa madhumuni ya kanuni hii- (a) faida ya kifedha inaweza kujumuisha- (i) ada ya upatikanaji na ada ya sampuli iliyokusanywa au iliyopatikana; (ii) malipo ya uchanganuzi wa sampuli iliyokusanywa au iliyopatikana; (iii) malipo ya awali; 18 Kanuni za Upatikanaji na Mgawanyo wa Faida za Rasilimali za Kijenetiki Tangazo la Serikali Na. 387 (Linaendelea) (iv) malipo ya hatua kwa hatua; (v) malipo ya mirabaha; (vi) fedha za utafiti; (vii) umiliki wa pamoja wa haki miliki husika; (viii) ubia; (ix) ada ya leseni ikiwa rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili zitatumika kwa madhumuni ya kibiashara; ada itakayolipwa inayosaidia endelevu ya bioanuai; ada ya kusafirisha nje ya nchi kwa kila sampuli iliyokusanywa au kupatikana; na (xii) mishahara na ada za kitaalamu pale kwenye mifuko na matumizi uhifadhi (xi) (x) ambapo kuna makubaliano ya pamoja; (b) faida isiyo ya kifedha inaweza kujumuisha- (i) (ii) (iii) (iv) ushirikiano na uchangiaji katika utafiti wa kisayansi na programu za maendeleo; kubadilishana matokeo ya utafiti na maendeleo; ushiriki katika uendelezaji wa bidhaa; idhini ya kutumia miundombinu ya ikijumuisha za kijenetiki rasilimali maabara pande za kanzidata na zinazoshirikiana; uhawilishaji wa maarifa na teknolojia zinazohusiana na rasilimali za kijenetiki; kujenga uwezo; ruhusa ya kutumia taarifa za kisayansi zinazohusiana na uhifadhi na matumizi endelevu ya rasilimali za kibaiolojia; idhini ya kukusanya sampuli; (ix) msaada wa vifaa na miundombinu; au (x) msaada kwa maendeleo ya jamii. (v) (vi) (vii) (viii) (4) Endapo rasilimali za kijenetiki au maarifa yake lindwa, ya kiasili yamekusanywa kwenye maeneo 19 Kanuni za Upatikanaji na Mgawanyo wa Faida za Rasilimali za Kijenetiki Tangazo la Serikali Na. 387 (Linaendelea) mkusanyaji atalipa ada ya kuingia na ada nyingine husika kwa Mamalaka ya Usimamizi. (5) Gawio la faida lililotokana na matumizi ya rasilimali ya kijenetiki au maarifa yake ya kiasili litagawanywa kwa mujibu wa Kanuni hizi na masharti yanayokubaliwa kwa pamoja. Makundi ya mgawanyo wa faida - 27 Verify source ↗
Makundi ya mgawanyo wa faida
AI-assisted research summary: Makubaliano ya Mgawanyo wa Faida yanahusishwa na lengo mahususi la kupata rasilimali za kijenetiki au maarifa ya asili, na yanaweza kuhusiana na matumizi ya kibiashara au yasiyo ya kibiashara. Pia kuna marejeo ya ridhaa ya awali ya maandishi.
27. Makubaliano ya Mgawanyo wa Faida yatategemea dhumuni mahususi la upatikanaji wa rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili ambalo linaweza kuwa la kibiashara au lisilo la kibiashara. Ridhaa ya awali ya maandishi Makubaliano ya Mgawanyo wa Faida - 28 Verify source ↗
Ridhaa ya Awali ya Maandishi
AI-assisted research summary: Mtu haruhusiwi kukusanya rasilimali za kijenetiki au maarifa ya kiasili ya Tanzania bila ridhaa ya awali ya maandishi kutoka kwa Mamlaka husika ya Usimamizi.
28.-(1) Mtu hatakusanya rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili ya Tanzania bila kuwa na ridhaa ya awali ya maandishi kutoka kwa Mamlaka husika ya Usimamizi. (2) Bila kuathiri kanuni ndogo ya (1), ridhaa ya awali ya maandishi itatolewa kwa mujibu wa taratibu inayosimamia zilizoainishwa katika rasilimali mahususi za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili. sheria husika - 29 Verify source ↗
Makubaliano ya Mgawanyo wa Faida
AI-assisted research summary: Kabla ya kupata au kutumia rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili, mwombaji na Mamlaka husika ya Usimamizi lazima wajadiliane na kuingia katika Makubaliano ya Mgawanyo wa Faida.
29.-(1) Kkabla ya upatikanaji au utumiaji wa rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili, mwombaji na Mamlaka husika ya Usimamizi watajadili na kuingia katika Makubaliano ya Mgawanyo wa Faida. (2) Makubaliano ya Mgawanyo wa Faida yatajumuisha yafuatayo: (a) taarifa kamili za wahusika wa makubaliano ambazo zinajumuisha- (i) (ii) (iii) (iv) (v) jina; utambulisho; anuani; namba ya usajili na anuani ya biashara kwa mfanyabiashara; na nyingine taarifa inayohusika yoyote 20 Kanuni za Upatikanaji na Mgawanyo wa Faida za Rasilimali za Kijenetiki Tangazo la Serikali Na. 387 (Linaendelea) ambayo inaweza kuhitajika na Mamlaka ya Usimamizi; (b) taarifa na maelezo ya rasilimali za kijenetiki zinazokusudiwa kupatikana ambazo zinaweza kujumuisha - (i) (ii) (iii) (iv) (v) rasilimali jina la rasilimali ya kijenetiki au maarifa yake ya kiasili yatakayopatikana; aina ya rasilimali za kijenetiki; kiasi za cha itakayokusanywa; eneo la kijiografia au kiikolojia ambalo rasilimali ya kijenetiki zitakusanywa; na taarifa nyingine yoyote inayohusiana ambayo inaweza kuhitajika na Mamlaka ya Usimamizi; kijenetiki (c) maelezo ya muda unaokusudiwa kutumika katika upatikanaji na hatua nyingine za matumizi ya rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili; (d) maelezo ya madhumuni ya upatikanaji wa rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili; rasilimali za (e) matumizi yaliyokusudiwa ya kijenetiki au maarifa yake ya kiasili; (f) utaratibu na aina ya mgawanyo wa faida; (g) haki na wajibu wa pande zinazotoa au kupata rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili na Makubaliano ya Mgawanyo wa Faida; (h) umiliki na usimamizi wa takwimu na matokeo ya utafiti; (i) sababu ya kusitisha au kuvunja makubaliano; (j) utaratibu wa kufuta Kibali cha Upatikanaji; (k) madhara ya kukiuka vigezo na Masharti yanayokubaliwa kwa pamoja; (l) masharti kuhusiana na haki miliki zinazohusiana na rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili; (m) vizuizi kama vipo kuhusiana na matumizi ya 21 Kanuni za Upatikanaji na Mgawanyo wa Faida za Rasilimali za Kijenetiki Tangazo la Serikali Na. 387 (Linaendelea) rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili; (n) mkakati kuhusiana na hifadhi ya bioanuai; (o) haki na wajibu wa wahusika; (p) utatuzi wa migogoro; (q) marekebisho; (r) maelezo ya majanga yasiyoepukika; na (s) taarifa nyingine husika kama zinavyoweza ajili ya uwezeshaji wa kuhitajika kwa Makubaliano ya Mgawanyo wa Faida. Nakala za makubaliano - 30 Verify source ↗
31. Mapitio ya Makubaliano ya Mgawanyo wa Faida
AI-assisted research summary: Makubaliano yaliyofikiwa chini ya Kanuni hizi yanapaswa kuwepo kwenye nakala halisi na kusambazwa kwa wahusika waliotajwa.
30. Makubaliano yoyote yatakayofikiwa chini ya sita Kanuni hizi yatakuwa kwenye nakala halisi zitakazosambazwa kwa- (a) mwombaji au mkusanyaji; (b) Mamlaka ya Usimamizi; (c) Mratibu wa Kitaifa; (d) msimamizi au mwakilishi aliyeidhinishwa wa rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili; (e) mamlaka ya serikali za mitaa ambapo rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili yanapatikana; na (f) jamii ikiwa rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili yanasimamiwa na mtu. Mapitio ya Makubaliano ya Mgawanyo wa Faida - 31 Verify source ↗
Mapitio ya Makubaliano ya Mgawanyo wa Faida
AI-assisted research summary: The terms and conditions in the benefit-sharing agreement must be reviewed within the agreed time and included in the agreement between the parties. Changes to any part of the agreement may be made after consultation and approval by the parties.
31.-(1) Vigezo na masharti kwenye Makubaliano ya Mgawanyo wa Faida yatapitiwa ndani ya muda uliokubaliwa na kuwekwa katika makubaliano kati ya wahusika. (2) Kipengele chochote cha Makubalino ya kinaweza Mgawanyo wa kurekebishwa baada ya mashauriano na idhini ya wahusika wa makubaliano. yaliyosainiwa Faida 22 Kanuni za Upatikanaji na Mgawanyo wa Faida za Rasilimali za Kijenetiki Tangazo la Serikali Na. 387 (Linaendelea) HAKI KUHUSU UPATIKANAJI NA MGAWANYO WA FAIDA ZA RASILIMALI ZA KIJENETIKI SEHEMU YA SABA Haki ya jamii
Part
SEHEMU YA SABA
- 32
AI-assisted research summary: Jamii zina haki za kutumia rasilimali za kijenetiki au maarifa ya kiasili yaliyopo katika maeneo yao na kushiriki katika ridhaa ya awali ya maandishi, utafiti, na kugawana faida.
32. Jamii itakuwa na haki zifuatazo pale ambapo rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili yanapatikana ndani ya maeneo yao: (a) kutumia rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili; (b) kushirikishwa kwa ajili ya kutoa ridhaa ya awali ya maandishi katika upatikanaji wa rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili; (c) kushiriki katika utafiti wa kisayansi na shughuli nyingine zinazohusisha rasilimali za kijenetiki au maarifa yao ya kiasili zilizokusanywa kutoka kwenye maeneo yao ya kiutawala; na (d) kugawana faida ya kifedha au isiyo ya kifedha rasilimali za kiasili zitokanazo na matumizi ya kijenetiki yanayopatikana ndani ya eneo lao la kiutawala. au maarifa yake ya Haki ya mmiliki wa kibali cha upatikanaji au usafirishaji nje ya nchi - 33 Verify source ↗
Nchi
AI-assisted research summary: Mmiliki wa kibali cha upatikanaji au cha usafirishaji nje ya nchi ana haki fulani chini ya Kanuni hizi.
33. Mmiliki wa kibali cha upatikanaji au kibali cha usafirishaji nje ya nchi atakuwa na haki ya- (a) kupata rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili kwa mujibu wa kibali cha upatikanaji kilichotolewa; (b) kuwa na matumizi endelevu kwa mujibu wa vigezo na masharti yaliyotolewa kwenye kibali cha upatikanaji au kibali cha usafirishaji nje ya nchi; (c) mgawanyo wa haki na usawa wa faida zitokanazo na matumizi ya rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili kwa mujibu wa Kanuni hizi; na (d) kuhuisha au kuongeza muda wa kibali cha upatikanaji kwa mujibu wa sheria mahususi 23 Kanuni za Upatikanaji na Mgawanyo wa Faida za Rasilimali za Kijenetiki Tangazo la Serikali Na. 387 (Linaendelea) zinazosimamia Mamlaka ya Usimamizi iliyotoa kibali husika. SEHEMU YA NANE MASHARTI YA JUMLA Makosa na adhabu
Part
SEHEMU YA NANE
- 34 Verify source ↗
Makosa na adhabu
AI-assisted research summary: Mtu anayepata rasilimali za kijenetiki au maarifa ya asili bila idhini ya maandishi, anayevunja masharti ya kibali, anayeshindwa kutoa taarifa zinazohitajika, au anayetoa taarifa za uongo ili kupata kibali anatenda kosa na anaweza kupewa faini, kifungo, au vyote.
34.-(1) Mtu ambaye- (a) anapata rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili bila idhini ya maandishi iliyotolewa na Mamlaka ya Usimamizi inayotambulika; (b) anavunja vigezo na masharti yoyote yaliyoambatishwa katika kibali kilichotolewa chini ya Kanuni hizi au sheria nyingine yoyote inayohusika; (c) anashindwa kutoa taarifa kuhusu upatikanaji wa rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili zinazotakiwa chini ya Kanuni hizi au sheria zinazohusika; (d) anatoa taarifa za uongo, udanganyifu au ulaghai ili kupata kibali; au (e) amekiuka masharti yoyote ya Kanuni hizi, (f) anatenda kosa na akitiwa hatiani atawajibika kulipa faini isiyopungu shilingi laki tano na isiyozidi shilingi bilioni moja au kifungo kisichopungua miezi mitatu na kisichozidi miaka saba au vyote. (2) Mtu akitiwa hatiani chini ya kanuni ndogo ya (1) atazuiliwa kupata rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili ya Tanzania. Kipindi cha mpito cha upatikanaji - 35 Verify source ↗
Kipindi cha mpito
AI-assisted research summary: Wamiliki wa vibali waliokuwa wakijihusisha na upatikanaji wa rasilimali za kijenetiki au maarifa ya kiasili kabla ya Kanuni hizi kuanza kutumika wanapaswa kuzingatia Kanuni hizi ndani ya miezi 12. Malipo yanayohusiana na upatikanaji huo yanalipwa wakati wa kipindi cha mpito.
35.-(1) Mmiliki wa kibali anayejihusisha katika upatikanaji wa rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili kabla ya kuanza kutumika kwa Kanuni hizi, atatakiwa kuzingatia matakwa ya Kanuni hizi ndani ya miezi kumi na mbili tangu tarehe ya kuanza kutumika kwa Kanuni hizi. 24 Kanuni za Upatikanaji na Mgawanyo wa Faida za Rasilimali za Kijenetiki Tangazo la Serikali Na. 387 (Linaendelea) (2) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (1), malipo yoyote yanayolipwa kwa ajili ya upatikanaji wa rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili kwa mujibu wa Kanuni hizi au sheria nyingine yoyote yatalipwa katika kipindi cha mpito. Wajibu wa kutoa mrejesho - 36 Verify source ↗
Wajibu wa kutoa mrejesho
AI-assisted research summary: Mmiliki wa kibali cha upatikanaji au kibali cha usafirishaji nje ya nchi lazima atohe mrejesho kuhusu matokeo, maendeleo, au aina zozote zisizo za asili zinazohusiana na rasilimali za kijenetiki au maarifa ya kiasili yaliyopatikana.
36. Mmiliki wa kibali cha upatikanaji au kibali cha usafirishaji nje ya nchi kilichotolewa chini ya Kanuni hizi au sheria nyingine, atatakiwa kutoa mrejesho wa matokeo, maendeleo au aina zisizo za asili zozote zenye uhusiano na rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili yaliyopatikana. Utunzaji wa kumbukumbu - 37 Verify source ↗
Utunzaji wa kumbukumbu
AI-assisted research summary: Mmiliki wa kibali cha upatikanaji au kibali cha usafirishaji nje ya nchi lazima atunze taarifa, nyaraka na kumbukumbu za miamala zinazohusu rasilimali za kijenetiki au maarifa ya kiasili yaliyopatikana.
37. Mmiliki wa kibali cha upatikanaji au kibali cha usafirishaji nje ya nchi, atatakiwa kutunza taarifa, nyaraka na kumbukumbu za miamala kuhusu rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili yaliyopatikana. Rufaa Mamlaka ya kutoa miongozo au maelekezo ya - 38 Verify source ↗
Rufaa
AI-assisted research summary: Mtu asiyeidhika na uamuzi chini ya Kanuni hizi anaweza kukata rufaa kwa mujibu wa sheria. Ikiwa rufaa inakwenda kwa Waziri, lazima iwasilishwe ndani ya siku 30, Waziri aamue ndani ya siku 14, na amjulishe mleta rufaa uamuzi na sababu ndani ya siku 7.
38.-(1) Mtu ambaye hajaridhishwa na uamuzi uliofanywa chini ya Kanuni hizi, anaweza kukata rufaa kwa mujibu wa masharti ya Sheria. (2) Endapo rufaa chini ya kanuni ndogo ya (1) inaenda kwa Waziri, rufaa hiyo itawasilishwa ndani ya thelathini kuanzia siku ya kutolewa uamuzi siku unaokatiwa itakuwa kwa njia ya barua itakayoambatishwa na nakala ya uamuzi na nyaraka nyingine ambayo Waziri anaweza kuhitaji. rufaa na (3) Waziri atatakiwa kutoa uamuzi ndani ya siku kumi na nne kuanzia siku ya kupokelewa kwa rufaa. (4) Waziri atatakiwa kumjulisha mleta rufaa uamuzi wake na sababu za uamuzi ndani ya siku saba kuanzia siku aliyotoa uamuzi. - 39 Verify source ↗
Mamlaka ya kutoa miongozo ya kisera au ya jumla
AI-assisted research summary: Waziri anaweza kutoa miongozo au maelekezo ya kisera kwa ajili ya kuwezesha utekelezaji bora wa Kanuni hizi.
39. Waziri anaweza kutoa miongozo au maelekezo ya kisera ili kuwezesha utekelezaji bora wa Kanuni hizi. 25 Kanuni za Upatikanaji na Mgawanyo wa Faida za Rasilimali za Kijenetiki Tangazo la Serikali Na. 387 (Linaendelea) kisera ______________ JEDWALI LA KWANZA ________________ (Limetengenzwa chini ya kanuni ya 12(a)) _____________ FOMU YA RIDHAA YA AWALI KWA AJILI YA UPATIKANAJI WA RASILIMALI ZA KIJENETIKI AU MAARIFA YAKE YA KIASILI _ Mimi/sisi ........................................................................................................................ ................................ nikiwa/tukiwa msimamizi/wasimamizi/muangalizi/waangalizi wa rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili ambazo ni: ........................................................................................................................ ................................ ........................................................................................................................ ................................ (Taja aina za rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili) Toa taarifa za eneo- Kijiji/mtaa: ………………………………………………………………. Kata: ………………………………………………………………………… Wilaya/Mji/Manispaa/Jiji: …………………………………………….. Mkoa: ……………………………………………………………………… Naridhia/tunaridhia ..................................................................................................... (Jina na anuani ya mwombaji kwa ajili ya ridhaa ya awali) anaweza kuomba kwa Mamlaka ya Usimamizi kwa ajili ya kufikiriwa kupata rasilimali za kijenetiki au maarifa yake ya kiasili yaliyotajwa hapo juu yanayopatikana katika usimamizi/uangalizi wangu/wetu. kwamba 26 Kanuni za Upatikanaji na Mgawanyo wa Faida za Rasilimali za Kijenetiki Tangazo la Serikali Na. 387 (Linaendelea) Ridhaa hii imetolewa kwa masharti yafuatayo- (1) ..................................................................................... (2) ..................................................................................... (3) ..................................................................................... (4) ..................................................................................... Ridhaa hii leo .................................... 20….... imetolewa tarehe ............................. mwezi wa ……………………………………….. Saini /Lakiri ya Mamlaka ya Usimamizi _______________ JEDWALI LA PILI ____________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 17) JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KANUNI ZA UPATIKANAJI NA MGAWANYO WA FAIDA ZA RASILIMALI ZA KIJENETIKI ZA MWAKA __________ KIBALI CHA USAFIRISHAJI NJE YA NCHI Kibali Na. ...................……. Hii ni kuthibitisha kwamba kusafirisha idhini ………………..................................…… wa S.L.P. ………....……………… imetolewa kutoka nchi ...................................................................……. (jina la nchi ya asili ya rasilimali za .............................................................................................. (taja nchi kijenetiki) kwenda zitakazopitia inayokwenda) zipo) (kama ……………………………………………………………………………………… rasilimali kijenetiki nchi nje na ya za Taja kwa majina, aina na ukubwa wa rasilimali za kijenetiki zilizokusanywa na zinazokusudiwa nchi ………………………………………………………………………………………………… kusafirishwa nje ya 27 Kanuni za Upatikanaji na Mgawanyo wa Faida za Rasilimali za Kijenetiki Tangazo la Serikali Na. 387 (Linaendelea) ………………………………………………………………………………………………… ………………………………………………………………………………………………… …………… Kibali hiki ni kwa ajili ya kutambua kwamba mkusanyaji aliyetajwa hapo juu, alipata Kibali cha Upatikanaji kama takwa kwa ajili ya ridhaa ya usafirishaji wa rasilimali za kijenetiki nje ya nchi zinazotajwa hapo juu zenye asili ya Tanzania. Kibali ni kwa ajili ya kuidhinisha kwamba mmiliki wa kibali aruhusiwe kupitisha na akubaliwe katika nchi anayokwenda na rasilimali hizo za kijenetiki. Kibali hiki hakitakuwa halali kwa usafirishaji mwingine wa nje ya nchi. Vigezo na masharti ya Kibali hiki yameambatanishwa. Jina…………………………….…………………...…. Saini ……………….……………………………... Tarehe……………………….………………… Waziri mwenye dhamana ya Mazingira _____________ JEDWALI LA TATU ____________ (Limetengenezwa chini ya kanuni 18(2)) ____________ MAOMBI YA KIBALI CHA USAFIRISHAJI NJE YA NCHI Kwa*: ...........................................................(anuani ya Mratibu wa Kitaifa) ................................................................... ............................................................ ….. ……………………………………………. Mimi/sisi*............................................................wa.....................................................................naom ba/tunaomba........................................................................................................................................... .............. Kibali cha Usafirishaji Nje ya Nchi kinaombwa kwa ajili ya rasilimali za kijenetiki zifuatazo (ambatisha Kibali cha Upatikanaji kilichotolewa na Mamlaka husika ya Usimamizi) ........................................................................................................................................................ ..................................................................................................................................................... Mimi/sisi* naendelea/tunaendelea kutamka kwamba kwa uelewa wangu/wetu kwamba taarifa 28 Kanuni za Upatikanaji na Mgawanyo wa Faida za Rasilimali za Kijenetiki Tangazo la Serikali Na. 387 (Linaendelea) iliyotolewa katika maombi haya ni sahihi na kweli. __________________________ ______________________________ Tarehe mwombaji KWA MATUMIZI YA OFISI TU Saini ya Maombi yamepokelewa na kufanyiwa kazi na ................................................................................ (jina la afisa) tarehe Leo ……………………………………….. 20……… *Futa lolote lisilohusika ……………………………………….. mwezi wa _____________ JEDWALI LA NNE ____________ (Limetengenezwa chini ya kanuni 19(f)) ADA KWA AJILI YA KIBALI CHA USAFIRISHAJI NJE YA NCHI DHUMUNI SIYO LA KIBIASHARA ASIYE RAIA Maombi ya Kibali cha Usafirishaji wa rasilimali za kijenetiki Nje ya Nchi ADA ZILIZOAINISHWA Mtu binafsi: USD 150 Kampuni: USD 300 LA KIBIASHARA Maombi ya Kibali cha Usafirishaji wa rasilimali za kijenetiki Nje ya Nchi Madawa: USD 1,000 Bidhaa nyingine: USD 1,500 SIYO LA KIBIASHARA RAIA Maombi ya Kibali cha Usafirishaji wa rasilimali za kijenetiki Nje ya Nchi Mtu binafsi: TZS 50,000/= Kampuni: TZS 150,000/= LA KIBIASHARA Maombi ya Kibali cha Madawa: TZS 200,000/= 29 Kanuni za Upatikanaji na Mgawanyo wa Faida za Rasilimali za Kijenetiki Tangazo la Serikali Na. 387 (Linaendelea) Usafirishaji wa rasilimali za kijenetiki Nje ya Nchi Bidhaa nyingine: TZS 1,000,000/= Dodoma, 3 Mei, 2024. Waziri wa Nchi- Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira SELEMANI SAIDI JAFO 30
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Kanuni za Upatikanaji na Mgawanyo wa Faida za Rasilimali za Kijenetiki za Mwaka 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in