Sheria Ndogo ya Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Same ya Mwaka 2024
This section gives the short title of the by-law: the Same District Council Construction Mining Tax By-law, 2024.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Same ya Mwaka 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This section gives the short title of the by-law: the Same District Council Construction Mining Tax By-law, 2024. These By-laws apply throughout the entire area of the Same District Council. This section defines key terms used in the by-laws. A person, company, or institution planning to open a building-material mine in the council area must apply to the Director for a mining permit using the council’s form. Wanaopewa kibali cha uchimbaji wa madini ya ujenzi lazima waombe kibali, walipe ada ya kila mwaka wakati uchimbaji unaendelea, wazingatie masharti, na walipe ushuru na tozo za Halmashauri.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Same ya Mwaka 2024
Showing 19 of 19
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria
AI-assisted research summary: This section gives the short title of the by-law: the Same District Council Construction Mining Tax By-law, 2024.
1.- Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Same ya Mwaka 2024. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hizi zitatumika katika eneo lote
AI-assisted research summary: These By-laws apply throughout the entire area of the Same District Council.
2.- Sheria Ndogo hizi zitatumika katika eneo lote la mamlaka ya Halmashauri ya wilaya ya Same. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii isipokuwa kama
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the by-laws.
3.- Katika Sheria Ndogo hii isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo: “afisa mwidhiniwa” maana yake ni afisa yeyote aliyeteuliwa na Mkurugenzi kwa lengo la kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hizi; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauriya Wilaya ya Same; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi wa 1 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Same Tangazo la Serikali Na. 412 (Linaendelea) Halmashauri ya wilaya ya Same au afisa yeyote aliyeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi; “madini ya ujenzi” maana yake ni tarazo, moramu, udongo, kifusi, kokoto, mawe, mchanga, chokaa na madini mengine yanayotumika katika ujenzi; “mchimba madini” maana yake ni mtu mwenye kibali kutoka mamlaka husika, kinachomhalalisha kumiliki eneo lililotengwa kwa ajili ya kuchimba madini ya ujenzi; “kibali” maana yake ni idhini au ruhusa ya maandishi inayotolewa na Halmashauri; Sura ya 290 “Sheria” maana yake ni sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa; “ushuru” maana yake ni tozo inayotozwa na Halmashauri kwa shughuli au huduma mbalimbali zinazotolewa katika eneo la halmashauri; na “wakala” maana yake mtu binafsi, kikundi, taasisi, kampuni au asasi iliyoteuliwa na Halmashauri kukusanya ushuru au ada kwa niaba ya Halmashauri kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. Maombi ya kibali - 4 Verify source ↗
(1) Taasisi, kampuni
AI-assisted research summary: A person, company, or institution planning to open a building-material mine in the council area must apply to the Director for a mining permit using the council’s form.
4.-(1) Taasisi, kampuni au mtu yeyote 2 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Same Tangazo la Serikali Na. 412 (Linaendelea) anayekusudia kuanzisha machimbo ya madini ya ujenzi katika eneo la Halmashauri atatakiwa kuwasilisha kwa Mkurugenzi maombi ya kibali cha uchimbaji wa madini ya ujenzi kwa kujaza fomu maalum itakayotolewa na Halmashauri. (2) Maombi ya kibali chini ya kanuni ndogo ya (1) yataambatishwa na taarifa zifuatazo: (a) leseni ya uchimbaji wa madini iliyotolewa na mamlaka husika; (b) aina ya madini yanayokusudiwa kuchimbwa; (c) umiliki pamoja na ukubwa wa eneo linalokusudiwa kuchimbwa madini ya ujenzi; (d) mpango wa utunzaji wa mazingira katika eneo la machimbo; na (e) muhtasari wa kijiji ambacho uchimbaji wa madini ya ujenzi utafanyika ukionesha kukubaliana na uchimbaji huo. (3) Mkurugenzi, ndani ya muda wa siku saba tangu kupokea maombi, atatakiwa kukagua eneo ambalo uchimbaji wa madini ya ujenzi unakusudiwa kufanyika ili kujiridhisha iwapo eneo hilo linafaa kwa shughuli za uchimbaji. (4) Bila kuathiri masharti yaliyowekwa katika kanuni ndogo ya (3) Mkurugenzi baada ya kukamilika 3 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Same Tangazo la Serikali Na. 412 (Linaendelea) kwa ukaguzi wa eneo linaloombewa kibali atatakiwa kukubali au kukataa maombi na iwapo atakataa atatoa sababu za kukataa maombi hayo. Wajibu mwenye lesenikibali wa - 5 Verify source ↗
Taasisi, kampuni au mtu yeyote aliyepewa
AI-assisted research summary: Wanaopewa kibali cha uchimbaji wa madini ya ujenzi lazima waombe kibali, walipe ada ya kila mwaka wakati uchimbaji unaendelea, wazingatie masharti, na walipe ushuru na tozo za Halmashauri.
5.- Taasisi, kampuni au mtu yeyote aliyepewa kibali cha uchimbaji wa madini ya ujenzi atatakiwa: (a) kuomba kibali kama kilivyoainishwa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizi; (b) kulipa ada ya kibali cha uchimbaji wa madini ya ujenzi kila mwaka ambao shughuli ya uchimbaji utakuwa ukifanyika kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Kwanza la Sheria Ndogo hii (c) kuzingatia masharti ya Sheria Ndogo hiii na masharti ya kibali cha uchimbaji wa madini ya ujenzi; na (d) kulipa ushuru na tozo mbalimbali zinazotozwa na Halmashauri kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii au sheria ndogo nyingine zilizotungwa na Halmashauri Muda uchimbaji masharti usafirishaji wa na ya - 6 Verify source ↗
(1) Shughuli za uchimbaji, uuzaji na ununuzi
AI-assisted research summary: Shughuli za uchimbaji, uuzaji na ununuzi wa madini ya ujenzi katika eneo la Halmashauri zifanyike kati ya saa 12 asubuhi na saa 12 jioni kila siku, isipokuwa Mkurugenzi akitoa kibali maalum. Mwenye gari linalosafirisha madini ya ujenzi lazima ahakikishe gari limefunikwa wakati wote wa usafirishaji.
6.-(1) Shughuli za uchimbaji, uuzaji na ununuzi wa madini ya ujenzi katika eneo la Halmashauri zitafanyika kuanzia saa kumi na mbili kamili asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni kila siku. 4 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Same Tangazo la Serikali Na. 412 (Linaendelea) (2) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (1), Mkurugenzi anaweza kutoa kibali maalum kuruhusu shughuli za uchimbaji, uuzaji na ununuzi wa madini ya ujenzi kufanyika nje ya muda ulioainishwa. (3) Kila mmiliki wa gari linalosafirisha madini ya ujenzi atatakiwa kuhakikisha kuwa gari hilo limefunikwa wakati wote wa usafirishaji wa madini ya ujenzi. Ushuru wa madini ya ujenzi - 7 Verify source ↗
(1) Kutakuwa na ushuru wa madini ya ujenzi
AI-assisted research summary: Wafanyabiashara, wachimbaji na wauzaji wa madini ya ujenzi katika eneo la Halmashauri wanatakiwa kulipa ushuru wa madini ya ujenzi, na Halmashauri inaweza kuwazuia kuuza au kusafirisha ikiwa kuna ukiukwaji.
7.-(1) Kutakuwa na ushuru wa madini ya ujenzi ambao utalipwa na msafirishaji, mchimbaji na muuzaji wa madini ya ujenzi katika eneo la Halmashauri. (2) Ushuru wa madini ya ujenzi utatozwa kwa viwango vilivyoainishwa katika Jedwali la Pili la Sheria Ndogo hii. (3) Halmashauri itakuwa na uwezo wa kumzuia msafirishaji, mchimbaji, muuzaji na kuzuia chombo cha usafirishaji kuuza au kusafirisha madini ya ujenzi kama ikibainika kuna ukiukwaji wa Sheria Ndogo hii. Vituo ukaguzi vya - 8 Verify source ↗
(1) Kutakuwa na vituo vya ukaguzi wa malipo
AI-assisted research summary: Madereva wa magari yanayobeba madini ya ujenzi lazima wasimame katika kituo cha ukaguzi na kuonyesha stakabadhi ya kielektroniki ya malipo. Gari lililokamatwa machimboni halitolewi mpaka faini na ushuru unaodaiwa ulipwe, ikiwa dereva au mmiliki amekimbia.
8.-(1) Kutakuwa na vituo vya ukaguzi wa malipo ya ushuru wa madini ya ujenzi katika njia zinazoingia au kutoka katika maeneo ya machimbo. (2) Kila dereva wa chombo cha usafiri 5 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Same Tangazo la Serikali Na. 412 (Linaendelea) kilichobeba madini ya ujenzi atatakiwa kusimama katika kituo cha ukaguzi na kuonesha stakabadhi ya kielektroniki ili kuthibitisha kulipwa kwa ushuru wa madini ya ujenzi yaliyo katika chombo cha usafiri. (3) Chombo cha usafiri kitakachokamatwa kwenye eneo la machimbo na dereva au mmiliki wake akakimbia au kutoroka, chombo hicho hakitaruhusiwa kutoka mpaka kitakapolipiwa faini na ushuru unaodaiwa. Utoaji stakabadhi malipo wa za - 9 Verify source ↗
(1) Ada au ushuru utakaotozwa kwa mujibu
AI-assisted research summary: Mlipaji wa ada au ushuru lazima alipe kwa halmashauri au wakala na anapaswa kudai na kuhakiki stakabadhi ya malipo ya kielektroniki.
9.-(1) Ada au ushuru utakaotozwa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii, utalipwa kwa halmashauri au wakala ambaye atatoa stakabadhi ya kielektroniki kama kielelezo cha malipo yaliyofanyika. (2) Utakuwa ni wajibu wa kila mlipa ada au ushuru kudai na kuhakiki stakabadhi ya malipo kulingana na kiasi cha fedha alicholipa. (3) Utakuwa sio utetezi kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizi, mtu kudai kuwa amelipa ada au ushuru lakini hakupewa stakabadhi ya kielektroniki. Mamlaka ya afisa mwidhiniwa - 10 Verify source ↗
Bila kuathiri masharti ya Sheria Ndogo hii,
AI-assisted research summary: Afisa mwidhiniwa anaweza kuingia katika maeneo yanayochimbwa madini ya ujenzi wakati wa saa maalum ili kufanya ukaguzi na kutoa ushauri.
10.- Bila kuathiri masharti ya Sheria Ndogo hii, afisa mwidhiniwa anaweza kuingia katika eneo lolote yanapochimbwa madini ya ujenzi kuanzia saa kumi na 6 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Same Tangazo la Serikali Na. 412 (Linaendelea) mbili asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni kwa nia ya kufanya ukaguzi na kutoa ushauri wa uendeshaji wa shughuli za uchimbaji. Kufutwa au kusimamishwa kwa kibali - 11 Verify source ↗
(1) Halmashauri
AI-assisted research summary: The council may revoke or suspend a building-minerals extraction permit if it finds a breach, must give 7 days’ notice first, and the permit holder must stop extraction if the permit is revoked or suspended.
11.-(1) Halmashauri inaweza kufuta au kusimamisha kibali cha uchimbaji wa madini ya ujenzi endapo itajiridhisha kuwa kuna ukiukwaji wa masharti ya Sheria Ndogo hii au masharti ya kibali cha uchimbaji wa madini ya ujenzi. (2) Kwa kuzingatia masharti ya kanuni ya ndogo ya (1), halmashauri kabla ya kufuta au kusimamisha kibali itatakiwa kutoa notisi ya siku saba ya kusudio la kufuta au kusimamisha kibali kwa mtu yeyote aliyepewa kibali cha uchimbaji. (3) Notisi itakayotolewa kwa mujibu wa kanuni ndogo ya (2) itaainisha sababu za kufuta au kusimamisha kibali husika. (4) Endapo kibali kitafutwa au kusimamishwa, mtu yeyote aliyopewa kibali cha uchimbaji wa madini ya ujenzi atasimama kuchimba madini hayo. Uteuzi wa wakala - 12 Verify source ↗
(1) Halmashauri itakuwa na mamlaka ya
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kuteua wakala wa kukusanya ada au ushuru kwa niaba yake.
12.-(1) Halmashauri itakuwa na mamlaka ya kuteua wakala kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizi, kukusanya ada au ushuru kwa niaba yake. 7 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Same Tangazo la Serikali Na. 412 (Linaendelea) (2) Wakala aliyeteuliwa kwa mujibu wa kanuni ndogo ya (1) atakuwa na wajibu wa- (a) kukusanya na kupokea ada au ushuru kwa niaba ya halmashauri katika eneo alilopangiwa na kwa viwango vilivyoainishwa katika Sheria Ndogo hizi; na (b) kukusanya ada au ushuru kwa kutumia mfumo wa kielektroni na kuwasilisha makusanyo yote kwa kuzingatia masharti ya mkataba wa uwakala alioingia na halmashuri; Makosa - 13 Verify source ↗
Taasisi, kampuni au mtu yeyote atakuwa
AI-assisted research summary: This section says a person, company, or institution commits an offence if they carry out listed acts involving construction minerals without permission, without paying tax, outside allowed times, in an uncovered vehicle, or by evading inspection and compliance.
13.- Taasisi, kampuni au mtu yeyote atakuwa ametenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii endapo- (a) ataanzisha machimbo ya madini ya ujenzi bila kuwa na kibali kilichotolewa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii; (b) atasafirisha madiniya ujenzi bila kulipa ushuru; (c) atachimba madini ya ujenzi kabla au baada ya muda ulioruhusiwa kuchimba; (d) atasafirisha madini ya ujenzi katika gari ambalo halijafunikwa; (e) atamshawishi mtu au kundi la watu kutolipa ushuru; (f) atakataa kutii agizo lolote atakalopewa na afisa mwidhiniwa wakati wa utekelezaji wa Sheria Ndogo hizi; (g) atakataa kulipa ushuru au kumzuia afisa 8 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Same Tangazo la Serikali Na. 412 (Linaendelea) mwidhiniwa au wakala kutekeleza wajibu wake; (h) atakwepa kulipa ushuru kwa kupita njia tofauti na kituo cha ukaguzi; (i) atachimba madini yasiyoidhinishwa; au (j) atachimba shimo kubwa kwa ajili ya madini na kuliacha bila kupanda miti au mimea mara baada ya madini hayo kumalizika. katika maeneo Adhabu Kufifilisha makosa Sura ya 290 - 14 Verify source ↗
Mtu yeyote anayekiuka masharti ya Sheria
AI-assisted research summary: Anyone who violates the bylaw commits an offence and, if convicted, may be fined, imprisoned, or both.
14.- Mtu yeyote anayekiuka masharti ya Sheria Ndogo hii anatenda kosa na akitiwa hatiani atawajibika kulipa faini isiyopungua Shilingi laki mbili na isiyozidi shilingi milioni moja au kifungo kisichopungua miezi kumi na mbili na kisichozidi miezi ishirini na nne au vyote. - 15 Verify source ↗
Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa
AI-assisted research summary: Mkurugenzi ana uwezo wa kufifilisha kosa kwa kutoza mtu aliyekiri kosa kwa hiari na yuko tayari kujaza fomu maalum na kulipa ada au ushuru unaodaiwa.
15.- Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha makosa kwa kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii kwa mujibu wa Sheria, iwapo mkosaji atakiri kosa kwa hiari na kuwa tayari kujaza fomu maalum iliyoainishwa katika Jedwali la Tatu la Sheria Ndogo hii na kulipa ada au ushuru anaodaiwa. Kufutwa T. S Na. 382 ya 2020 - 16 Verify source ↗
Sheria Ndogo ya Ushuru wa Madini ya
AI-assisted research summary: This section repeals the Same District Council construction minerals levy by-law of 2020.
16.- Sheria Ndogo ya Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Same ya Mwaka 2020 inafutwa. 9 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Same Tangazo la Serikali Na. 412 (Linaendelea) _________________ JEDWALI LA KWANZA ___________________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 5(b)) ADA YA UCHIMBAJI MADINI YA UJENZI NAMBA AINA YA MADINI KIASI CHA ADA YA KIBALI (SHILINGI)
Part
JEDWALI LA KWANZA
- 1 Verify source ↗
Section 1
AI-assisted research summary: The table lists a fee of 50,000/= for all construction minerals per permit.
1. Madini yote ya ujenzi 50,000/= kwa kila kibali __________________ JEDWALI LA PILI __________________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 7 (2)) USHURU WA MADINI YA UJENZI NAMBA AINAYAMADINI
Part
JEDWALI LA PILI
- 8 Verify source ↗
Section 8
AI-assisted research summary: The section lists materials: sand, gravel, soil/clay, rubble, stones, bricks, magnesite, feldspar, bauxite, and gypsum.
8. Mchanga Kokoto Morum Udongo/Kifusi Mawe Matofali Magnesite Feldsper Bauxite Gypsum - 11 Verify source ↗
Section 11
AI-assisted research summary: Hii ni fomu ya kukiri kosa mbele ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Same na kukubali kulipa ushuru unaodaiwa pamoja na faini.
11. Shaba KIWANGO M3 M3 M3 M3 M3 M3 M3 M3 M3 M3 M3 KIWANGO CHA USHURU (SHILINGI) 1500/= 1500/= 1500/= 1000/= 1500/= 1000/- 1500/= 1500/= 2500/= 1000/= 5,000/= 10 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Same Tangazo la Serikali Na. 412 (Linaendelea) __________________ JEDWALI LA TATU ________________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 15) FOMU YA KUKIRI NA KUFIFILISHA KOSA Mimi;…………………………………………. nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya;………………………………………..…….ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Same, kwamba mnamo tarehe;…….... mwezi;…................................…. Mwaka; ……..….… nilitenda kosa la kukiuka masharti ya Aya ya …..….. ya Sheria Ndogo ya (Ushuru wa Madini ya Ujenzi) ya Halmashauri ya Wilaya ya Same. Kwa Mamlaka aliyopewa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Same, niko tayari kulipa kiasi cha Ushuru ninaodaiwa pamoja na faini. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA MIMI MWENYEWE KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU: Leo tarehe;…....... ya Mwezi;………… Mwaka;………….. Jina;…………………………………..……………………. Saini;…………………………..…………………………… MBELE YANGU : Jin;…………………………….………..…………………… Wadhifa;…………………………………………………..… Saini;………………………………………………………… Tarehe;……………………………………………………. 11 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Same Tangazo la Serikali Na. 412 (Linaendelea) Nembo ya Halmashauri ya Wilaya ya Same imebandikwa kwenye Sheria Ndogo hizi kufuatia azimio lililopitishwa kwenye Mkutano wa Halmashauri uliofanyika mnamo tarehe 05 mwezi Mei mwaka 2023, Mbele ya; ANASTAZIA TUTUBA Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Same YUSTO M. MAPANDE(DIWANI) Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya Same NAKUBALI, L.S Dodoma 25 Machi, 2024. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais MOHAMED OMARY MCHWENGERWA (MB) Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa 12
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Ushuru wa Madini ya Ujenzi ya Halmashauri ya Wilaya ya Same ya Mwaka 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in