Sheria Ndogo ya Ushuru wa Stendi ya Halmashauri ya Wilaya ya Same za Mwaka 2024
This provision gives the short title of the by-law: the Same District Council Stage Tax By-law, 2024.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Ushuru wa Stendi ya Halmashauri ya Wilaya ya Same za Mwaka 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This provision gives the short title of the by-law: the Same District Council Stage Tax By-law, 2024. This by-law applies throughout the entire area under the jurisdiction of Same District Council. This section defines key terms used in the by-law, including who counts as an authorised officer, what a bus station is, and the categories of buses. Halmashauri inatoza ushuru wa stendi kwa vyombo vyote vya usafiri, kwa viwango vilivyo kwenye Jedwali la Kwanza; baadhi ya vyombo vimeondolewa, na ushuru wa kuingiza abiria stendi hulipwa na wamiliki, madereva, makondakta au watu walioteuliwa. Halmashauri lazima ianzishe stendi ya kupakia na kushusha abiria na mizigo, na inaweza pia kuanzisha stendi ndogo katika vijiji inapofaa.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Ushuru wa Stendi ya Halmashauri ya Wilaya ya Same za Mwaka 2024
Showing 14 of 14
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria
AI-assisted research summary: This provision gives the short title of the by-law: the Same District Council Stage Tax By-law, 2024.
1.- Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Ushuru wa Stendi ya Halmashauri ya Wilaya ya Same za Mwaka 2024. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la
AI-assisted research summary: This by-law applies throughout the entire area under the jurisdiction of Same District Council.
2.- Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la mamlaka ya Halmashauri ya wilaya ya Same. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii isipokuwa kama
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the by-law, including who counts as an authorised officer, what a bus station is, and the categories of buses.
3.- Katika Sheria Ndogo hii isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo: “afisa mwidhiniwa” maana yake ni afisa yeyote aliyeteuliwa na Mkurugenzi kwa lengo la kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya wilaya ya Same; “mabasi” maana yake magari yote yanayosafirisha au 1 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Stendi ya Halmashauri ya Wilaya ya Same Tangazo la Serikali Na. 414 (Linaendelea) kubeba abiria ila hayahusishi taksi; “mabasi makubwa” maana yake ni mabasi yote yenye uwezo wa kubeba abiria 36 au zaidi; “mabasi ya kati” maana yake ni mabasi yanayobeba abiria 21 hadi 35; “mabasi madogo” maana yake ni mabasi yote yenye uwezo wa kubeba abiria wasiozidi 20; “mmiliki” maana yake ni mtu mwenye gari, dereva, kondakta au mtu mwingine yeyote aliyeidhinishwa na mwenye gari kuwa na mamlaka ya juu ya gari wakati inaingia stendi; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Same au afisa yeyote aliyeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi chini ya Sheria Ndogo hiii; Sura ya 290 “Sheria” maana yake ni sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa; “stendi” maana yake ni eneo maalum lililotengwa au kujengwa na Halmashauri kwa ajili ya kupakia na kushusha abiria au mizigo; “Wakala” maana yake ni mtu binafsi au kikundi cha watu, shirika, taasisi au kampuni ambayo limeteuliwa na Halmashauri kufanya kazi yoyote chini ya Sheria Ndogo hii kwa niaba ya Halmashauri; 2 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Stendi ya Halmashauri ya Wilaya ya Same Tangazo la Serikali Na. 414 (Linaendelea) Ushuru wa stendi - 4 Verify source ↗
(1) Halmashauri itatoza ushuru wa stendi kwa
AI-assisted research summary: Halmashauri inatoza ushuru wa stendi kwa vyombo vyote vya usafiri, kwa viwango vilivyo kwenye Jedwali la Kwanza; baadhi ya vyombo vimeondolewa, na ushuru wa kuingiza abiria stendi hulipwa na wamiliki, madereva, makondakta au watu walioteuliwa.
4.- (1) Halmashauri itatoza ushuru wa stendi kwa vyombo vyote vya usafiri kwa mujibu wa viwango vilivyoainishwa katika Jedwali la Kwanza la Sheria Ndogo hii. (2) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (1), ushuru wa kuingiza abiria stendi utalipwa na mmiliki wa gari, dereva, kondakta au mtu mwingine yeyote atakayepewa madaraka na mwenye gari kufanya hivyo kwa ushuru huo kukabidhiwa kwa wakala. (3) Vyombo vya usafiri vinavyomilikiliwa na Serikali, Wanadiplomasia, majeshi na magari ya kubeba wagonjwa havitatozwa ushuru wa stendi. Uanzishaji wa stendi - 5 Verify source ↗
Section 5
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima ianzishe stendi ya kupakia na kushusha abiria na mizigo, na inaweza pia kuanzisha stendi ndogo katika vijiji inapofaa.
5.- (1) Halmashauri itaanzisha stendi itakayotumika kupakia au kushusha abiria na mizigo. (2) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (1), Halmashauri inaweza kuanzisha stendi ndogo katika maeneo ya vijiji kadri Halmashauri itakavyoona inafaa. Wajibu wa kufanya usafi eneo la stendi - 6 Verify source ↗
(1) Kila dereva, dbiria au mtu yeyote
AI-assisted research summary: Watu wanaotumia stendi lazima waendelee kutunza usafi wa maeneo ya stendi, na mtu yeyote haruhusiwi kutupa takataka katika maeneo yasiyoruhusiwa.
6.- (1) Kila dereva, dbiria au mtu yeyote anayetumia stendi atakuwa na wajibu wa kutunza usafi wa maeneo ya stendi. (2) Mtu yeyote hataruhusiwa kutupa takataka za 3 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Stendi ya Halmashauri ya Wilaya ya Same Tangazo la Serikali Na. 414 (Linaendelea) aina yoyote katika maeneo ya stendi yasiyoruhusiwa. Kushusha na kupakia abiria - 7 Verify source ↗
(1) Mabasi yote yatokayo au kuelekea Dar es
AI-assisted research summary: Buses on the listed routes must enter the main bus stand, nobody may stop a bus to load or unload passengers at an unauthorized place, and vehicle owners must pay storage costs if their vehicle is impounded and kept in a garage for violating this bylaw.
7.- (1) Mabasi yote yatokayo au kuelekea Dar es Salaam, Moshi, Mwanga Korogwe, Hedaru, Makanya, Kisiwani, Ndungu, Myamba, Mwembe, Chome, Vudee Mamlaka ya afisa mwidhiniwa na Ruvu yatalazimika kuingia Stendi Kuu. (2) Mtu yeyote hataruhusiwa kusimamisha basi kwa madhumuni ya kushusha au kupakia abiria sehemu isiyoidhinishwa kuwa ni stendi. (3) Kila mmiliki ambaye gari lake litakuwa limekamatwa na kuhifadhiwa karakana kutokana na kukiuka Sheria Ndogo hii atalipa gharama ya kuhifadhi gari lake. - 8 Verify source ↗
(1) Afisa mwidhiniwa atakuwa na mamlaka ya
AI-assisted research summary: An authorized officer may seize and remove a vehicle that loads or unloads passengers outside the stand area.
8.-(1) Afisa mwidhiniwa atakuwa na mamlaka ya kukamata na kuondoa chombo cha usafiri ambacho kitapakia au kushusha abiria nje ya eneo la stendi. (2) Chombo cha usafiri kilichokamatwa kwa mujibu wa masharti ya aya ndogo ya (1), kitaondolewa na kuhifadhiwa kwenye yadi ya Halmashauri au sehemu yoyote kama itakavyoamriwa na Mkurugenzi. (3) Halmashauri itakuwa na mamlaka ya kuuza chombo kilichokamatwa baada ya kupata idhini ya Mahakama iwapo mmiliki wa chombo hicho atashindwa 4 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Stendi ya Halmashauri ya Wilaya ya Same Tangazo la Serikali Na. 414 (Linaendelea) kulipa gharama za uangalizi pamoja na gharama za kukamata chombo hicho ndani ya siku 14 tangu tarehe ya kukamatwa. (4) Bila kuathiri masharti yaliyowekwa kwenye aya ndogo ya (3), Halmashauri kabla ya kuuza chombo kilichokamatwa, Mkurugenzi atatoa taarifa ya maandishi kwa umma juu ya kusudio la kuuza chombo hicho. (5) Halmashauri haitawajibika na hasara yoyote na kwa namna yoyote ile itakayotokea wakati wa kukamata au kushikilia mali iliyokamatwa isipokuwa pale itakapobainika kuwa Halmashauri ilitumia mamlaka yake kinyume na Sheria. Uteuzi wakala wa - 9 Verify source ↗
(1) Halmashauri itakuwa na mamlaka ya
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kuteua wakala kukusanya ada au ushuru kwa niaba yake, na wakala huyo lazima akusanye na kuwasilisha makusanyo kulingana na eneo, viwango, mfumo wa kielektroniki, na masharti ya mkataba wa uwakala.
9.- (1) Halmashauri itakuwa na mamlaka ya kuteua wakala kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizi, kukusanya ada au ushuru kwa niaba yake. (2) Wakala aliyeteuliwa kwa mujibu wa aya ndogo ya (1) atakuwa na wajibu wa- (a) kukusanya na kupokea ada au ushuru kwa niaba ya Halmashauri katika eneo alilopangiwa na kwa viwango vilivyoainishwa katika Sheria Ndogo hii; (b) kukusanya ada au ushuru kwa kutumia mfumo wa kielektroniki na kuwasilisha makusanyo yote 5 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Stendi ya Halmashauri ya Wilaya ya Same Tangazo la Serikali Na. 414 (Linaendelea) kwa kuzingatia masharti ya mkataba wa uwakala alioingia na Halmashauri. Uvaaji wa vitambulisho - 10 Verify source ↗
Wafanyakazi
AI-assisted research summary: Wafanyakazi wote wa mabasi wanaouza tiketi kwenye Stendi kuu lazima wavae sare na vitambulisho vinavyoonyesha kuwa ni mawakala.
10.- Wafanyakazi wote wa mabasi wanaojihusisha na uuzaji wa tiketi sehemu za Stendi kuu watalazimika kuvaa sare na vitambulisho vitakavyokuwa vinawatambulisha kuwa wao ni mawakala. Makosa - 11 Verify source ↗
Kila mmiliki wa gari katika eneo
AI-assisted research summary: Mmiliki wa gari katika eneo la Halmashauri anatakiwa asifanye vitendo vilivyotajwa, kama kuingiza gari stendi kwa kukataa, kuosha au kutengeneza gari stendi, kutoa matusi, kuwasumbua abiria, kufanya uharibifu, kupakia au kushusha abiria nje ya stendi, kukataa kupitisha gari Stendi kuu au stendi iliyoidhinishwa, au kukwepa/kushindwa kulipa ushuru.
11.- Kila mmiliki wa gari katika eneo la Halmashauri atakuwa ametenda kosa endapo- (a) atagoma kuingiza gari lake ndani ya stendi; (b) ataosha au kutengeneza gari ndani ya stendi; (c) atatoa lugha ya matusi; (d) atasababisha au kuleta usumbufu wowote kwa abiria; (e) atafanya uharibifu wowote ndani ya stendi; (f) atakayesimama na kupakia au kushusha abiria nje ya eneo la stendi; (g) atakayekataa kupitisha gari lake Stendi kuu pamoja na stendi yeyote itakayoidhinishwa na Halmashauri; (h) atakwepa au kushindwa kulipa ushuru uliopangwa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. 6 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Stendi ya Halmashauri ya Wilaya ya Same Tangazo la Serikali Na. 414 (Linaendelea) Adhabu - 12 Verify source ↗
Mtu yeyote anayekiuka masharti ya Sheria
AI-assisted research summary: Any person who violates these subsidiary rules commits an offence and may be fined, imprisoned, or both if convicted.
12.Mtu yeyote anayekiuka masharti ya Sheria Ndogo hii anatenda kosa na akipatikana na hatia atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi laki mbili na isiyozidi shilingi milioni moja au kifungo kisichopungua miezi kumi na mbili na kisichozidi miezi ishirini na nne au vyotea. Kufifilisha kosa - 13 Verify source ↗
Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa na kumtoza mtu aliyekosa, ikiwa mkosaji anakiri kosa kwa hiari, yuko tayari kujaza fomu maalum, na kulipa ushuru unaodaiwa.
13.- Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa Sura ya 290 kufifilisha kosa kwa kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizo kwa kuzingatia Sheria, iwapo mkosaji atakiri kosa kwa hiari na kuwa tayari kujaza fomu maalum iliyoainishwa katika Jedwali la Pili la Sheria Ndogo hizi na kulipa ushuru anaodaiwa. ___________________ JEDWALI LA KWANZA ____________________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 4 (1) VIWANGO VYA USHURU WA STENDI NAMBA AINA YA TOZO KIASI CHA TOZO (SHILINGI)
Part
JEDWALI LA KWANZA
- 3 Verify source ↗
Section 3
AI-assisted research summary: This section lists several vehicle-related fees and a form for admitting an offence and agreeing to pay the tax owed plus a fine.
3. 4 Mabasi madogo Mabasi ya kati Mabasi makubwa 1,000/= kwa safari 1,500/= kwa safari 2,000/= kwa safari Magari binafsi 1,000/=kwa siku 7 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Stendi ya Halmashauri ya Wilaya ya Same Tangazo la Serikali Na. 414 (Linaendelea) 5 6 7 8 9 Texi Bajaji Pikipiki Ada ya kutunza gari lililokamatwa au kuzuiliwa Ada ya maegesho 1,000/=kwa siku 300/=kwa siku 200/=kwa siku 10,000/= kwa siku 2,000/= Malori kwa siku 5,000/=Mitambo ya ujenzi kwa siku ____________________ JEDWALI LA PILI __________________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 13) FOMU YA KUKIRI NA KUFIFILISHA KOSA Mimi.............................................................nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya ................................................................ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Same, kwamba mnamo tarehe..........ya mwezi.......................Mwaka...........................nilitenda kosa la kukiuka masharti ya Aya ya ...............ya Sheria Ndogo ya (Ushuru wa Stendi) ya Halmashauri ya Wilaya ya Same ya Mwaka, 2024. Kwa mamlaka aliyopewa Mkurugenzi wa Halamashauri ya Wilaya ya Same, niko tayari kulipa kiasi cha ushuru ninaodaiwa pamoja na faini. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA MIMI MWENYEWE KWA HIARI YANGU NA KADRI YA UFAHAMU WANGU. Leo tarehe.....................ya Mwezi.........................Mwaka...................................... Jina.................................................... Saini............................................................. Mbele ya: Jina:............................................................ Wadhifa:..................................................... Saini............................................................ Tarehe......................................................... 8 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Stendi ya Halmashauri ya Wilaya ya Same Tangazo la Serikali Na. 414 (Linaendelea) Nembo ya Halmashauri ya Wilaya ya Same imebandikwa kwenye Sheria Ndogo hizi kufuatia azimio lililopitishwa kwenye Mkutano wa Halmashauri uliofanyika mnamo tarehe 05 Mwezi Mei Mwaka 2023, Mbele ya; ANASTAZIA TUTUBA Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Same YUSTO MAPANDE (DIWANI) Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya Same NAKUBALI, L.S Dodoma MOHAMED OMARY MCHENGERWA(MB) 25 Machi 2024. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Na Serikali 9
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Ushuru wa Stendi ya Halmashauri ya Wilaya ya Same za Mwaka 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in