Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko ya Halmashauri ya Wilaya ya Same ya Mwaka 2024
This section states the official short title of the bylaw.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko ya Halmashauri ya Wilaya ya Same ya Mwaka 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This section states the official short title of the bylaw. This provision says the bylaw applies throughout the area under the Same district council. This section defines key terms used in the by-law, including authorized officer, broker, council, permit, markets, Director, trader, market manager, the law, market stakeholders, and agent. Halmashauri lazima ikusanye ushuru na ada, isimamishe na iendeshe masoko, na isimamie usafi, usalama, huduma za kijamii, mgao wa nafasi, maeneo ya magulio, na usajili wa wafanyabiashara. A market officer is to be appointed by the council to manage market development and related market operations.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko ya Halmashauri ya Wilaya ya Same ya Mwaka 2024
Showing 27 of 27
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria
AI-assisted research summary: This section states the official short title of the bylaw.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko ya Halmashauri ya Wilaya ya Same ya Mwaka 2024. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la
AI-assisted research summary: This provision says the bylaw applies throughout the area under the Same district council.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la mamlaka ya halmashauri ya wilaya ya Same. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii isipokuwa kama
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the by-law, including authorized officer, broker, council, permit, markets, Director, trader, market manager, the law, market stakeholders, and agent.
3. Katika Sheria Ndogo hii isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo: “afisa mwidhiniwa” maana yake ni afisa yeyote wa halmashauri aliyeteuliwa kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “dalali” maana yake ni mtu yeyote anayeuza bidhaa za sokoni kwa njia ya mnada kwa niaba ya mwenye bidhaa kwa mujibu wa sheria na 1 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko ya Halmashauri ya Wilaya ya Same Tangazo la Serikali Na. 415 (Linaendelea) taratibu za soko; “halmashauri” maana yake ni halmashauri ya wilaya ya Same; “kibali” maana yake ni idhini ya maandishi inayotolewa na halmashauri kwa mujibu Sheria Ndogo hiii; “masoko” maana yake ni maeneo maalum ya biashara yalilotengwa na halmashauri kwa matumizi ya kuuzia au kununulia bidhaa; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Same au afisa yeyote atakayeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi; “mfanyabiashara” maana yake ni mtu yeyote anayeuza bidhaa sokoni au gulioni kwa jumla au rejareja; “mkuu wa soko” maana yake ni mtu yeyote aliyeteuliwa au aliyeajiriwa na halmashauri kusimamia shughuli zote katika soko; Sura ya 290 “Sheria” maana yake ni sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa; “wadau wa soko” maana yake ni mfanyabiashara binafsi, vikundi vilivyoandikishwa katika kamati za wadau wa soko au gulio na kuwasilishwa kwa mkuu wa soko, au vyama 2 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko ya Halmashauri ya Wilaya ya Same Tangazo la Serikali Na. 415 (Linaendelea) vya ushirika vinavyofanya shughuli za biashara katika soko; “wakala” maana yake ni mtu binafsi au kikundi cha watu, kampuni au shirika ambalo limeteuliwa na halmashauri kufanya kazi yoyote chini ya Sheria Ndogo hizi kwa niaba ya halmashauri; Wajibu wa Halmashauri - 4 Verify source ↗
Halmashauri itakuwa na wajibu wa
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima ikusanye ushuru na ada, isimamishe na iendeshe masoko, na isimamie usafi, usalama, huduma za kijamii, mgao wa nafasi, maeneo ya magulio, na usajili wa wafanyabiashara.
4. Halmashauri itakuwa na wajibu wa- (a) kukusanya ushuru na ada mbalimbali kutoka kwa wafanyabiashara wa masoko, minada au magulio; (b) kuanzisha, kusimamia na kuendesha masoko kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizi; (c) kuendeleza masoko; (d) kusimamia usafi na usalama wa masoko; (e) kusimamia ufikishaji wa huduma za kijamii katika masoko; (f) kugawa na kupangisha masoko kwa vyumba au meza au vizimba; (g) kutenga maeneo kwa ajili ya magulio; na (h) kusajili wafanyabiashara wote katika masoko yote ya Halmashauri. Mkuu wa soko - 5 Verify source ↗
(1) Kutakuwa
AI-assisted research summary: A market officer is to be appointed by the council to manage market development and related market operations.
5.-(1) Kutakuwa na mkuu wa soko 3 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko ya Halmashauri ya Wilaya ya Same Tangazo la Serikali Na. 415 (Linaendelea) atakayeteuliwa na halmashauri kwa ajili ya kusimamia shughuli za uendelezaji wa soko pamoja na- (a) kusimamia ukusanyaji wa ushuru na ada mbalimbali kama zilivyoainishwa katika Jedwali la Pili la Sheria Ndogo hii; (b) kusimamia usajili wa wadau wa soko kwa kushirikiana na kamati ya wadau wa soko; (c) kuimarisha huduma za ulinzi, maji na umeme katika masoko; (d) kusimamia usafi na uondoshaji wa taka katika soko; (e) kuhakikisha kuwa bidhaa haziuzwi kwenye eneo ambalo haliruhusiwi kwa shughuli hiyo; (f) kuzuia ujenzi holela katika soko; na (g) kutekeleza majukumu mengine yoyote yatakayoagizwa na halmashauri. (2) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (1), mkuu wa soko atakuwa na mamlaka ya kutoa kibali cha kutumia soko kwa mtu au mfanyabiashara yeyote atakayeomba kibali kwa mujibu wa Jedwali la Kwanza la Sheria Ndogo hizi. Uteuzi wa wakala
Part
Jedwali la Pili la Sheria Ndogo hii;
- 6 Verify source ↗
(1) Halmashauri itakuwa na mamlaka ya
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kuteua wakala, na wakala aliyechaguliwa atasimamia uendeshaji wa soko kwa mwaka mmoja kuanzia tarehe ya uteuzi.
6.-(1) Halmashauri itakuwa na mamlaka ya kuteua wakala kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizi, 4 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko ya Halmashauri ya Wilaya ya Same Tangazo la Serikali Na. 415 (Linaendelea) atawajibika katika uendeshaji wa soko kwa niaba ya halmashauri. (2) Wakala atakayeteuliwa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii atasimamia shughuli za uendeshaji wa soko kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia tarehe ya uteuzi wake. Kamati ya wadau wa soko - 7 Verify source ↗
(1) Kutakuwa na kamati ya wadau wa soko
AI-assisted research summary: A market stakeholders committee must be formed, meet monthly, serve for three years, and carry out specified market administration duties.
7.-(1) Kutakuwa na kamati ya wadau wa soko ambayo itaundwa na wadau wa soko kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. (2) Wajumbe wa kamati ya wadau wa soko watakuwa ni mwenyekiti na katibu kutoka kila kikundi cha ushirika ndani ya soko. (3) Kamati ya wadau wa soko itatakiwa kuweka utaratibu maalum wa kuwapata viongozi wake, kuwaondoa madarakani na uendeshaji wa shughuli zake na kuuwasilisha halmashauri. (4) Vikao vya kamati ya wadau wa soko vitafanyika mara moja kila mwezi. (5) Mkuu wa soko atakuwa katibu katika vikao vyote vya kamati ya wadau wa soko. (6) Muda wa kamati ya wadau wa soko kuwa madarakani ni miaka mitatu. 5 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko ya Halmashauri ya Wilaya ya Same Tangazo la Serikali Na. 415 (Linaendelea) Majukumu ya kamati 8-. Kamati ya wadau wa soko itakuwa na majukumu yafuatayo: (a) kuhakiki biashara zinazoendeshwa katika soko; (b) kuboresha ustawi wa wadau wa soko; (c) kuhakikisha uwepo wa nidhamu katika shughuli za soko; (d) kuhakikisha wadau wote wa soko analipa ushuru na ada kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii; (e) kukuza na kuendeleza mfumo wa biashara; (f) kuhakikisha kila eneo la mnada na soko linakuwa safi muda wote; (g) kutekeleza kazi nyingine watakazoelekezwa na mkuu wa soko kulingana na Sheria Ndogo hii; na (h) kuhakikisha ulinzi na usalama unakuwepo sokoni. Usajili wa wadau - 9 Verify source ↗
Mtu yeyote anayetaka kufanya biashara
AI-assisted research summary: Mtu anayefanya biashara katika eneo la soko lazima asajiliwe na mkuu wa soko kwa kushirikiana na kamati ya wadau wa soko.
9.- Mtu yeyote anayetaka kufanya biashara katika eneo la soko atatakiwa kusajiliwa na mkuu wa soko akishirikiana na kamati ya wadau wa soko kwa lengo la kumtambua na kumuorodhesha katika rejesta ya wadau wa soko. 6 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko ya Halmashauri ya Wilaya ya Same Tangazo la Serikali Na. 415 (Linaendelea) Vikao vya kamati ya soko - 10 Verify source ↗
(1) Kutakuwa na kikao cha kamati ya wadau
AI-assisted research summary: Kamati ya wadau wa soko lazima ikutane mara moja kila mwezi; mkuu wa soko ni katibu wa kikao, na mwenyekiti huchaguliwa miongoni mwa wajumbe.
10.-(1) Kutakuwa na kikao cha kamati ya wadau wa soko kitakachofanyika mara moja kila mwezi ambapo mkuu wa soko atakuwa katibu wa kikao na mwenyekiti atachaguliwa miongoni mwa wajumbe wa kamati ya wadau wa soko. (2) Kamati ya wadau inaweza kukutana kwa jinsi itakavyoona inafaa nje ya kikao cha kisheria kwa ajili ya kutekeleza maazimio yaliyoainishwa katika kikao cha kamati ya wadau wa soko. Majukumu ya wadau wa kamati ya soko - 11 Verify source ↗
Kamati ya wadau wa soko itakuwa na
AI-assisted research summary: Kamati ya wadau wa soko must perform the listed market duties, including checking businesses, promoting order, cleanliness, security, and ensuring taxes and fees are paid.
11.- Kamati ya wadau wa soko itakuwa na majukumu yafuatayo: (a) kuhakiki biashara zinazoendeshwa katika soko; (b) kuboresha ustawi wa wadau wa soko; (c) kuhakikisha uwepo wa nidhamu katika shughuli za soko; (d) kuhakikisha wadau wote wa soko wanalipa ushuru na ada kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii; (e) kukuza na kuendeleza mfumo wa biashara; (f) kuhakikisha kila eneo la mnada na soko linakuwa safi muda wote; (g) kuhakikisha ulinzi na usalama unakuwepo sokoni; na 7 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko ya Halmashauri ya Wilaya ya Same Tangazo la Serikali Na. 415 (Linaendelea) (h) kutekeleza kazi nyingine watakazoelekezwa na mkuu wa soko kulingana na Sheria Ndogo hii. Kamati ndogo - 12 Verify source ↗
Kamati ya wadau wa soko itaunda kamati
AI-assisted research summary: Kamati ya wadau wa soko lazima iunde kamati ndogo mbili zenye wajumbe watatu kila moja, kutoka miongoni mwa wajumbe wake.
12.- Kamati ya wadau wa soko itaunda kamati ndogo zenye wajumbe watatu kutoka miongoni mwa wajumbe wa kamati ya wadau wa soko ambazo ni- (a) kamati ndogo ya utawala na biashara; na (b) kamati ndogo ya ulinzi na usalama Kufuta kibali - 13 Verify source ↗
(1) Mkuu wa soko anaweza kufuta kibali
AI-assisted research summary: Mkuu wa soko anaweza kufuta kibali, but must give 30 days' notice. A trader may object within 14 days, and the Director must decide the objection within 7 days.
13.-(1) Mkuu wa soko anaweza kufuta kibali kilichotolewa chini ya Sheria Ndogo hizi, baada ya kutoa notisi ya siku thelathini iwapo mwenye kibali hicho- (a) atakuwa na malimbikizo ya ada au ushuru; (b) atakuwa amesimamisha shughuli zake kwa miezi mitatu bila taarifa; (c) atakuwa na mwenendo unaokiuka masharti ya Sheria Ndogo hizi; (d) atawashawishi wafanyabiashara wengine kutofuata Sheria Ndogo hii au kusababisha uvunjaji wa amani; au (e) atatumia chumba, kibanda, meza au kizimba alichopanga kinyume na madhumuni ya 8 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko ya Halmashauri ya Wilaya ya Same Tangazo la Serikali Na. 415 (Linaendelea) kufanyia biashara kama yalivyoainishwa kwenye mkataba wa upangishaji au maelekezo yatakayotolewa na halmashauri. (2) Mfanyabiashara ambaye hatoridhika na uamuzi wa kufutiwa kibali anaweza kuwasilisha pingamizi lake kwa Mkurugenzi katika kipindi cha siku kumi na nne tangu tarehe ya kufutiwa kibali. (3) Baada ya kupokea pingamizi, Mkurugenzi atatakiwa kutoa uamuzi wa pingamizi ndani ya siku saba tangu tarehe ya kupokea pingamizi husika. Muda wa biashara - 14 Verify source ↗
(1) Soko litakuwa wazi siku zote kuanzia
AI-assisted research summary: Soko lazima liwe wazi kila siku kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 12 jioni; mkuu wa soko anaweza kulifunga kwa matengenezo au dharura, lakini kwa matengenezo lazima atoe notisi ya siku 7 kwa wadau wa soko.
14.-(1) Soko litakuwa wazi siku zote kuanzia saa kumi na mbili kamili asubuhi hadi saa kumi na mbili kamili jioni . (2) Mkuu wa soko, kwa kushauriana na Mkurugenzi anaweza kufunga soko kwa ajili ya matengenezo au sababu nyingine yoyote ya dharura pale itakapoonekana inafaa. (3) Isipokuwa kwa sababu nyingine za dharura, mkuu wa soko hatakuwa na mamlaka ya kufunga soko kwa sababu za matengenezo isipokuwa tu baada ya kutoa notisi ya siku saba kwa wadau wa soko kuhusu kusudio la kufunga soko kwa ajili ya matengenezo. 9 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko ya Halmashauri ya Wilaya ya Same Tangazo la Serikali Na. 415 (Linaendelea) Kibali cha watumiaji wengine - 15 Verify source ↗
(1) Mtu au mfanyabiashara ambaye anataka
AI-assisted research summary: Mtu au mfanyabiashara anayefanya biashara mpya au biashara isiyo na eneo sokoni lazima aombe kibali kwa mkuu wa soko. Kibali hutolewa baada ya kulipa ada na ni cha mwaka mmoja, kisha huomba tena baada ya kuisha.
15.-(1) Mtu au mfanyabiashara ambaye anataka kufanya biashara ambayo awali haikuwepo au haikuwa na eneo ndani ya soko ataomba kibali kwa mkuu wa soko na masharti ya aya ya 9 ya Sheria Ndogo hizi yatatumika (2) Kibali hicho kitatolewa kwa mwombaji baada ya kulipa ada na kitadumu kwa muda wa mwaka mmoja toka siku ya kupewa. (3) Mfanyabiashara atakayetaka kuendelea kufanya biashara katika soko mara baada ya kibali chake kwisha muda wa kutumika, atatakiwa kuomba tena kibali kingine kwa mkuu wa soko. Usafi wa soko - 16 Verify source ↗
(1) Kila mfanyabiashara
AI-assisted research summary: Wafanyabiashara wa soko lazima waweke maeneo yao safi, wafuate kanuni za afya, na washiriki katika usafi wa jumla wa soko; mkuu wa soko na kamati husika hupanga siku na muda wa kufunga soko mara moja kwa wiki kwa ajili ya usafi.
16.-(1) Kila mfanyabiashara anayefanya biashara katika eneo la soko atawajibika kuweka eneo lake katika hali ya usafi wakati wote. (2) Mkuu wa soko kwa kushirikiana na kamati ya wadau wa soko watapanga siku na muda wa kufunga soko mara moja kwa juma kwa ajili ya kufanya usafi wa jumla katika eneo lote la soko. (3) Kila mfanyabiashara atatakiwa kuzingatia kanuni za afya. (4) Kila mfanyabiashara katika soko atatakiwa kushiriki katika usafi wa jumla wa soko bila kukosa. 10 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko ya Halmashauri ya Wilaya ya Same Tangazo la Serikali Na. 415 (Linaendelea) Uingizaji wa bidhaa sokoni - 17 Verify source ↗
(1) Bidhaa zote zitakazoingizwa katika soko
AI-assisted research summary: Goods brought into the market must be kept in special transport crates; spoiled goods may not be brought into the market, and bringing leaf-wrapped goods into the market is an offence.
17.-(1) Bidhaa zote zitakazoingizwa katika soko zitatakiwa kuhifadhiwa kwenye makasha maalum ya kusafirishia bidhaa. (2) Ni marufuku kwa mkulima au mfanyabiashara au dalali au mtu mwingine yeyote kuingiza sokoni bidhaa zilizoharibika. (3) Mtu atakayeingiza sokoni bidhaa zilizofungwa kwa majani atakuwa ametenda kosa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. Kodi ya upangishwaji - 18 Verify source ↗
(1) Kila mfanyabishara katika soko atalipa
AI-assisted research summary: Market traders must pay a rental/space fee set by the council.
18.-(1) Kila mfanyabishara katika soko atalipa kodi ya upangishwaji kwa viwango ambavyo vitapangwa na halmashauri. (2) Kodi ya upangishwaji italipwa kwa halmashauri au wakala wake (3) Halmashauri itatoza kodi ya kupanga eneo la biashara ambayo italipwa na mfanyabiashara yeyote aliyesajiliwa kufanya biashara katika eneo la soko. Marufuku - 19 Verify source ↗
Itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote
AI-assisted research summary: Anyone is prohibited from doing a range of activities inside the market, including posting notices without the market chief’s approval, political activity, littering, damaging market infrastructure, and other listed conduct.
19.- Itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote- (a) kubandika tangazo au kubandua tangazo lolote bila ya idhini ya mkuu wa soko; (b) kuweka bendera ya chama chochote cha siasa ndani ya eneo la soko; 11 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko ya Halmashauri ya Wilaya ya Same Tangazo la Serikali Na. 415 (Linaendelea) (c) kufanya shughuli za siasa ndani ya soko; (d) kutumia lugha ya matusi ndani ya soko; (e) kuharibu miundombinu ya soko; (f) kufanya shughuli yoyote kwenye eneo ambalo haliruhusiwi au halijajengwa kwa shughuli hiyo; (g) kupangisha kizimba au eneo la biashara kwa mfanyabiashara mwingine; (h) kufanya biashara nje ya eneo la soko; (i) kutupa takataka ovyo na kutiririsha maji machafu; (j) kufunga chumba cha biashara kwa madai ya kukitumia kama stoo au matumizi mengine yasiyoainishwa katika mkataba au leseni; au (k) kuwasha moto maeneo yasiyohusika ndani ya soko. Huduma ya usafi, ulinzi, maji na umeme - 20 Verify source ↗
Kila mfanyabiashara
AI-assisted research summary: Kila mfanyabiashara katika soko lazima alipe gharama za ulinzi, usafi, maji na umeme kila mwezi kulingana na mahitaji yake na utaratibu wa kamati ya wadau wa soko.
20.- Kila mfanyabiashara katika soko atawajibika kugharamia huduma ya ulinzi, usafi, maji na umeme kulingana na mahitaji yake kila mwezi kufuatana na utaratibu utakaowekwa na kamati ya wadau wa soko. Wajibu wa - 21 Verify source ↗
Kila mfanyabiashara katika eneo la soko
AI-assisted research summary: Wafanyabiashara wote katika eneo la soko wanapaswa kuzingatia masharti ya soko, ikiwemo usajili, usafi, ulipaji wa ushuru na ada kwa wakati, na kufuata maeneo na maelekezo yanayoruhusiwa.
21.- Kila mfanyabiashara katika eneo la soko 12 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko ya Halmashauri ya Wilaya ya Same Tangazo la Serikali Na. 415 (Linaendelea) mfanyabishara atakuwa na wajibu wa: (a) kusajiliwa na mkuu wa soko katika rejesta ya wadau wa soko; (b) kulinda na kuhifadhi miundombinu ya soko; (c) kufanya biashara katika maeneo yanayoruhusiwa; (d) kufanya usafi katika eneo lake la biashara; (e) kulipa ushuru na ada kwa wakati; (f) kutobandika au kutobandua tangazo bila idhini ya mkuu wa masoko; (g) kutotumia lugha ya matusi au kuudhi au kashfa katika eneo la soko; (h) kushiriki usafi wa jumla wa soko; (i) kutoweka bendera ya chama chochote cha siasa ndani ya eneo la soko; (j) kutofanya shughuli za kisiasa katika eneo la soko; (k) kutotupa taka ovyo au kutiririsha maji machafu; (l) kutowasha moto maeneo yasiyohusika ndani ya soko; na (m) kuheshimu masharti ya upangaji aliyopewa na halmashauri na maelekezo atakayopewa mkuu wa masoko na kamati ya wadau wa soko. 13 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko ya Halmashauri ya Wilaya ya Same Tangazo la Serikali Na. 415 (Linaendelea) Ujenzi ukarabati na - 22 Verify source ↗
Mtu hataruhusiwa kufanya ujenzi,
AI-assisted research summary: A person may not build, repair, or alter a room, kiosk, table, or cage without written approval from the council.
22.- Mtu hataruhusiwa kufanya ujenzi, ukarabati au marekebisho ya chumba, kibanda, meza au kizimba pasipo idhini ya maandishi ya halmashauri. Makosa na adhabu - 23 Verify source ↗
Mtu atakuwa ametenda kosa na akipatikana
AI-assisted research summary: A person who commits the offence, if convicted, is subject to a fine of not less than 200,000 and not more than 1,000,000 shillings, or imprisonment of 12 to 24 months, or both.
23.- Mtu atakuwa ametenda kosa na akipatikana na hatia atatozwa faini isiyopungua Shilingi laki mbili na isiyozidi Shilingi Milioni moja au kifungo kisichopungua miezi kumi na mbili na kisichozidi miezi ishirini na nne au adhabu zote kwa pamoja. Kufifilisha makosa - 24 Verify source ↗
Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa
AI-assisted research summary: Mkurugenzi ana uwezo wa kufifilisha kosa na kumtoza mtu aliyetenda kosa la Sura ya 290 chini ya Sheria Ndogo hizi, ikiwa mkosaji anakiri kwa hiari, anajaza fomu maalum, na analipa ada au ushuru unaodaiwa.
24.- Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha kosa kwa kumtoza mtu yeyote aliyetenda Sura ya 290 kosa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii kwa mujibu wa Sheia, iwapo mkosaji atakiri kosa kwa hiari na kuwa tayari kujaza fomu maalum iliyoainishwa katika Jedwali la Pili la Sheria Ndogo hizi na kulipa ada au ushuru anaodaiwa. _____________________ JEDWALI LA KWANZA ______________________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 5(2) KIBALI CHA KUTUMIA SOKO
Part
JEDWALI LA KWANZA
- 1 Verify source ↗
Section 1
AI-assisted research summary: This section is a heading for the applicant’s name in the Same District Council market tax by-law notice.
1. Jina la mwombaji……………………………………………………………………………… 14 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko ya Halmashauri ya Wilaya ya Same Tangazo la Serikali Na. 415 (Linaendelea) - 6 Verify source ↗
Section 6
AI-assisted research summary: This section is a permit application form asking for the applicant’s details, the permit requested, the area where it will apply, the permit period, and any conditions for use.
6. Anuani ya mwombaji…………………………………………………………………………. Kibali cha……………………………………………………………………………………… Eneo ambalo kibali hicho kitatumika……………………………………………………….. Muda wa kibali ni kuanzia tarehe………………………hadi tarehe………………………. Msharti ya kutumia kibali hicho a)……………………………………………………………………………………………… b)……………………………………………………………………………………………… c)……………………………………………………………………………………………… d)……………………………………………………………………………………………… - 7 Verify source ↗
Section 7
AI-assisted research summary: Section 7 is a heading that mentions an approved meeting date and a summary.
7. Tarehe ya kikao iliyoidhinishwa kibali………………………………………………………. Muhtasari Na…………………………………………………………………………………. - 8 Verify source ↗
Section 8
AI-assisted research summary: This section contains a form for voluntarily admitting an offence before the district council director and stating willingness to pay the fee or tax owed plus a fine.
8. Imesainiwa na: Jina:…………………………………………….. Saini…………………………………………….. …………………………….. Mkuu wa soko Saini ya mwombaji tarehe…………………………………… Tarehe……………………. Mhuri……………………………………………………………………………………………. ________________ JEDWALI LA PILI ________________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 24) FOMU YA KUKIRI NA KUFIFILISHA MAKOSA Mimi;……………………………………………. nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya;……………………………..…….ambaye ni Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Same, kwamba mnamo tarehe;…… ya mwezi;….…......... Mwaka;…….....… nilitenda kosa la kukiuka masharti ya aya ya …..….. ya Sheria Ndogo ya (Ushuru wa Masoko) ya Halmashauri ya Wilaya ya Same ya Mwaka. 15 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko ya Halmashauri ya Wilaya ya Same Tangazo la Serikali Na. 415 (Linaendelea) Kwa Mamlaka aliyopewa Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Same, niko tayari kulipa kiasi cha ada au ushuru ninaodaiwa pamoja na faini. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA MIMI MWENYEWE KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU: Leo tarehe;….............. ya Mwezi;....………… Mwaka;………….. Jina;…………………………………..……………………. Saini;…………………………..…………………………… MBELE YANGU : Jina;…………………………….………..…………………… Wadhifa;…………………………………………………..……. Saini;………………………………………………………… Tarehe;………………………………………………………. 16 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko ya Halmashauri ya Wilaya ya Same Tangazo la Serikali Na. 415 (Linaendelea) Nembo ya Halmashauri ya Wilaya ya Same imebandikwa kwenye Sheria Ndogo hizi kufuatia azimio lililopitishwa kwenye Mkutano wa Halmashauri uliofanyika mnamo tarehe 05 Mwezi Mei mwaka 2023. Mbele ya; ANASTAZIA TUTUBA Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya ya Same YUSTO M. MAPANDE(DIWANI) Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya Same NAKUBALI, L.S Dodoma. MOHAMED OMARY MCHENGERWA (MB) 25 Machi, 2024. Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa 17
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Ushuru wa Masoko ya Halmashauri ya Wilaya ya Same ya Mwaka 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in