Kanuni za Usimamizi wa Kodi (Ukusanyaji wa Kodi Kwenye Mapato ya Upangishaji kwa Watu Binafsi), za Mwaka 2024
This section is titled “Interpretation” and introduces Part Two on registration of property owners and tenants.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Kanuni za Usimamizi wa Kodi (Ukusanyaji wa Kodi Kwenye Mapato ya Upangishaji kwa Watu Binafsi), za Mwaka 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This section is titled “Interpretation” and introduces Part Two on registration of property owners and tenants. This section is about registering property owners and tenants, and it sits within a part on collecting tax from rental income. This section appears to cover rental tax payment, interest, and penalties. This section concerns cooperation between local government authorities and the Tanzania Revenue Authority on service charges. These rules are named the Tax Administration Regulations (Collection of Tax on Rental Income for Individuals) of 2024.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Kanuni za Usimamizi wa Kodi (Ukusanyaji wa Kodi Kwenye Mapato ya Upangishaji kwa Watu Binafsi), za Mwaka 2024
Showing 14 of 14
- 2 Verify source ↗
Section 2
AI-assisted research summary: This section is titled “Interpretation” and introduces Part Two on registration of property owners and tenants.
2. Jina. Tafsiri. SEHEMU YA PILI USAJILI WA WAMILIKI MALI NA WAPANGAJI
Part
SEHEMU YA PILI
- 4 Verify source ↗
Section 4
AI-assisted research summary: This section is about registering property owners and tenants, and it sits within a part on collecting tax from rental income.
4. Usajili wa wamiliki wa mali na wapangaji. Vigezo vya usajili. SEHEMU YA TATU UKUSANYAJI WA KODI KWA MAPATO YATOKANAYO NA UPANGISHAJI MALI - 3 Verify source ↗
(1) Kamishna Mkuu anaweza kumuomba
AI-assisted research summary: The Commissioner General may ask the Council Director to help identify and register property owners and tenants, and local executive officers must keep, update, and report the required register and tenancy information.
3.-(1) Kamishna Mkuu anaweza kumuomba Mkurugenzi wa Halmashauri amsaidie katika jukumu la kuwatambua na kuwasajili wamiliki mali na wapangaji kwenye eneo la mamlaka ya Mkurugenzi huyo wa Halmashauri. (2) Kwa madhumuni ya kanuni ndogo ya (1), Mkurugenzi wa Halmashauri ambaye ameombwa msaada na Kamishna Mkuu chini ya Kanuni hii, atateua Maafisa Watendaji wa Mitaa au Maafisa Watendaji wa Vijiji ili kumsaidia Kamishna Mkuu katika jukumu la kuwatambua na kuwasajili wamiliki wa mali na wapangaji katika kila eneo lake. (3) Katika kumsaidia Kamishna Mkuu kwa mujibu wa kanuni ndogo ya (2), Afisa Mtendaji wa Mtaa au Afisa 4 Kanuni za Usimamizi wa Kodi (Ukusanyaji wa Kodi Kwenye Mapato ya Upangishaji Kwa Watu Binafsi) Tangazo La Serikali Na. 427 (Linaendelea)) Mtendaji wa Kijiji, kwa kadri itakavyokuwa, atawajibika:- (a) kuhifadhi rejista ya wamiliki wa mali na wapangaji wa mali za kukodi zilizopo katika Mtaa wake; (b) kuhakikisha wapangaji wote wanaingia katika mikataba rasmi ya upangaji na wamiliki wa mali katika eneo lake iliyotayarishwa kwa kuzingatia vigezo vilivyotajwa katika Jedwali hili; (c) kutunza rejista ya mikataba yote ya upangishaji mali iliyoingiwa katika eneo lake; (d) kufuatilia utekelezaji wa mikataba ya wapangaji na kuhakikisha mabadiliko ya viwango vya kodi na usitishaji wa mikataba inarekodiwa au kuhuishwa kwenye rejista yake ipasavyo; (e) kutoa taarifa, kwenye Ofisi ya Kamishna Mkuu iliyo karibu, zinazohusiana na hali ya rejista na maelezo au taarifa nyingine kwa namna ambayo Kamishna Mkuu anaweza kuelekeza kwa kutoa notisi katika, vyombo vya habari au waraka wa kiutawala; na (f) kutekeleza jukumu lingine lolote linalohusiana na Kanuni hizi kama litakavyo elekezwa na Kamishna Mkuu. (4) Rejista iliyotajwa chini ya kanuni ndogo ya (2) itakuwa na taarifa zifuatazo: (a) jina na anwani ya mmiliki wa mali na mpangaji wake; (b) anuani halisi ya eneo la mali inayopangishwa; (c) idadi ya mali inayopangishika, iliyopo ikijumuisha nyumba, vyumba, au mali nyingine yoyote ya kupangisha; (d) mali iliyokodishwa kwa mpangaji ikiwa ni pamoja na idadi ya vyumba, nyumba inayojitegemea au mali nyingine yoyote iliyopangishwa; (e) TIN ya mmiliki wa mali na mpangaji; (f) nambari ya simu ya mmiliki wa mali na 5 Kanuni za Usimamizi wa Kodi (Ukusanyaji wa Kodi Kwenye Mapato ya Upangishaji Kwa Watu Binafsi) Tangazo La Serikali Na. 427 (Linaendelea)) mpangaji wake; (g) muda wa mkataba wa upangishaji; (h) kiwango cha kodi ya kila mwezi na utaratibu wa muda wa malipo yake; na (i) taarifa nyingine yoyote ambayo Kamishna Mkuu anaweza kuona inafaa. (5) Mikataba yote ya kupangisha itakayosajiliwa chini ya kanuni hizi itafanyika au kuandaliwa kwa kuzingatia Fomu iliyoainishwa kwenye Jedwali la Kanuni hizi. (6) Kila Afisa Mtendaji wa Mtaa au Kijiji anatakiwa kuitaarifu ofisi ya Kamishna Mkuu iliyo karibu nae katika maelezo yaliyoorodheshwa katika kanuni ndogo ya (4) kwa kutumia utaratibu uliowekwa na Kamishna Mkuu. kuhusu mabadiliko yoyote (7) Rejista itawekwa katika kila ofisi ya Afisa Mtendaji wa Mtaa au Ofisi ya Afisa Mtendaji wa Kijiji kwa utaratibu utakaoainishwa na Kamishna Mkuu na taarifa zilizomo zitawasilishwa kwa Kamishna Mkuu kwa njia na utaratibu utakaowekwa na Kamishna Mkuu. (8) Afisa Mtendaji wa Mtaa au Kijiji anaweza, isipokuwa kwa dosari yoyote ya msingi, kurekebisha dosari yoyote ya kiuandishi kwenye rejista au hati nyingine iliyo na dondoo kutoka kwenye Rejista. Vigezo vya usajili Sura ya 332 - 4 Verify source ↗
(1) Mtu binafsi ambaye anamiliki mali kwa
AI-assisted research summary: Some private property owners do not need to register, but certain rented properties must be reported to the local village or street executive officer within 30 days, and all owners and tenants must prepare new tenancy agreements using the prescribed form.
4.-(1) Mtu binafsi ambaye anamiliki mali kwa matumizi yake binafsi au matumizi yake ya biashara hatastahili kusajiliwa chini ya Kanuni hizi, isipokuwa kwa mtu binafsi ambaye mali yake- (a) imepangishwa yote, iwe kwa makazi, biashara, uhifadhi, au matumizi mengine yoyote; (b) imepangishwa kwa sehemu na wakati huo huo inatumika kwa matumizi na mwenye mali, iwe sehemu iliyopangishwa ni ndogo, kibanda au sehemu ya mali hiyo; (c) inapangishwa mara kwa mara kwa madhumuni ya kuendesha hafla, sherehe, makongamano au shughuli nyingine yoyote; au (d) imepangishwa kwa ajili ya kilimo. 6 Kanuni za Usimamizi wa Kodi (Ukusanyaji wa Kodi Kwenye Mapato ya Upangishaji Kwa Watu Binafsi) Tangazo La Serikali Na. 427 (Linaendelea)) (2) Mtu binafsi ambaye anamiliki mali iliyotajwa chini ya aya za (a), (b) na (c) za kanuni ndogo ya (1) atalazimika, si zaidi ya muda wa siku thelathini tangu tarehe ya kupangishwa kwa mali husika, kutoa taarifa kwa Afisa Mtendaji wa Mtaa au Kijiji kuhusu uwepo wa mali hiyo kwa ajili ya madhumuni ya kusajiliwa; Isipokuwa kwamba, kwa mali zote ambazo zilipangishwa kabla ya kuchapishwa kwa kanuni hizi, taarifa ya mali husika zitatolewa na mwenye mali kwa Afisa Mtendaji wa Mtaa au Kijiji ndani ya muda wa siku thelathini tangu tarehe ambayo Kamishna Mkuu atatoa Notisi kwa Umma kupitia vyombo vya habari inayotaka wamiliki wa mali kujisajili. (3) Kuanzia tarehe ya kuchapishwa kwa Kanuni hizi, wamiliki wa mali na wapangaji wote watatayarisha mikataba yao mipya ya upangaji kwa kuzingatia Fomu iliyoainishwa kwenye Jedwali la Kanuni hizi. SEHEMU YA TATU UKUSANYAJI WA KODI KWA MAPATO YATOKANAYO NA UPANGISHAJI MALI, RIBA NA ADHABU Malipo ya kodi ya upangishaji Sura ya 332
Part
SEHEMU YA TATU
- 7 Verify source ↗
Section 7
AI-assisted research summary: This section appears to cover rental tax payment, interest, and penalties.
7. Malipo ya kodi ya upangishaji. Riba. Adhabu. SEHEMU YA NNE 1 Kanuni za Usimamizi wa Kodi (Ukusanyaji wa Kodi Kwenye Mapato ya Upangishaji Kwa Watu Binafsi) Tangazo La Serikali Na. 427 (Linaendelea)) MASHARTI YA JUMLA - 5 Verify source ↗
(1) Jukumu la kulipa kodi ya mapato ya
AI-assisted research summary: Mmiliki wa mali iliyopangishwa lazima alipe kodi ya mapato ya upangishaji mali, awasilishe uthibitisho wa malipo, na aripoti nakala ya stakabadhi kwa Afisa Mtendaji wa Mtaa au Kijiji.
5.-(1) Jukumu la kulipa kodi ya mapato ya upangishaji mali ipo kwa mmiliki wa mali iliyopangishwa. (2) Mmiliki aliyesajiliwa chini ya kanuni hizi atalazimika kwa kila malipo ya kodi atakayopokea toka kwa mpangaji kulipa kodi ya mapato kwenye Akaunti ya Benki ya Kamishna Mkuu kwa utaratibu ulioainishwa katika Kanuni hizi. (3) Kiwango cha kodi, kitakacholipwa na mmiliki wa mali ni kile kilichotajwa chini ya Sheria ya Kodi ya Mapato kuhusiana na malipo ya kodi itokanayo na mapato ya upangishaji mali. (4) Malipo kwa wamiliki wa mali yatafanywa ama kwa kila mwezi au kwa mkupuo, na endapo - (a) mpangaji anayemlipa mwenye mali kwa kila mwezi, tarehe ya malipo ya kodi ya mapato ni tarehe ya siku husika ya malipo ya upangishaji iliyotajwa katika mkataba wa au tarehe 7 Kanuni za Usimamizi wa Kodi (Ukusanyaji wa Kodi Kwenye Mapato ya Upangishaji Kwa Watu Binafsi) Tangazo La Serikali Na. 427 (Linaendelea)) upangishaji, yoyote kati ya iliyotangulia; tarehe hizo (b) mpangaji anayemlipa mwenye mali mapema kwa mkupuo kwa mujibu wa masharti ya mkataba wa upangaji, tarehe ya malipo ya kodi ya mapato itakuwa tarehe ya malipo ya mkupuo au tarehe ya malipo ya upangishaji iliyopo kwenye mkataba, yoyote kati ya hizo iliyotangulia; au (c) mpangaji anayemlipa mwenye mali baada ya kutumia mali hiyo, iwe kwa mkupuo au kwa awamu kwa mujibu wa mkataba wa upangaji, tarehe ya malipo ya kodi itakuwa kama ilivyoonyeshwa kwenye mkataba wa upangaji. (5) Kila mmiliki wa mali atapaswa, ndani ya muda wa siku saba kuanzia tarehe ya malipo ya upangishaji, iliyorejewa katika kanuni ndogo ya (3), kulipa kiwango cha kodi kwenye akaunti ya benki ya Kamishna Mkuu kupitia mfumo wa malipo wa kielektroniki ulioidhinishwa na kuwasilisha uthibitisho wa malipo hayo kwa Kamishna Mkuu. (6) Stakabadhi za malipo ya kodi iliyopokelewa kupitia mfumo wa malipo ya kielektroniki, zitatolewa moja kwa moja kwa njia ya kielektroniki kwa mpangaji. (7) Kila mmiliki wa mali baada ya kupokea stahabadhi ya malipo ya kielektroniki, atamjulisha Afisa Mtendaji wake wa Mtaa au Kijiji kwa kupeleka nakala ya stakabadhi hiyo kwa Afisa Mtendaji wake wa Mtaa au Kijiji kwa madhumuni ya kumbukumbu na ufuatiliaji. - 6 Verify source ↗
(1) Mmiliki wa mali, ambaye malipo yake ya
AI-assisted research summary: If income tax filing or payment is late, the property owner must pay interest and a penalty; if the tenant caused the delay, the tenant pays instead.
6.-(1) Mmiliki wa mali, ambaye malipo yake ya kodi ya mapato yamechelewa kuwasilishwa au kulipwa kwenye akaunti ya benki ya Kamishna Mkuu kwa mujibu wa kanuni hizi kama inavyotakiwa chini ya kanuni ya 5, atawajibika kulipa riba kwa kiwango kilichoidhinishwa kisheria na adhabu kama inavyotakiwa chini ya Sheria ya Usimamizi wa Kodi. (2) Mmiliki wa mali hatolazimika kulipa riba na adhabu tajwa pale ambapo kuna uthibitisho kwamba mpangaji alisababisha uchelewaji huo, ambapo mpangaji 8 Riba Kanuni za Usimamizi wa Kodi (Ukusanyaji wa Kodi Kwenye Mapato ya Upangishaji Kwa Watu Binafsi) Tangazo La Serikali Na. 427 (Linaendelea)) atawajibika moja kwa moja kulipa riba na adhabu husika. Adhabu - 7 Verify source ↗
(1) Mpangaji au mmiliki wa mali ambaye
AI-assisted research summary: Mpangaji au mmiliki wa mali lazima azingatie masharti ya kanuni hizi na ajisajili katika Rejista iliyoanzishwa na Kanuni hizi.
7.-(1) Mpangaji au mmiliki wa mali ambaye atashindwa kuzingatia masharti ya kanuni hizi atakua ametenda kosa na atawajibika, baada ya kutiwa hatiani, kulipa faini isiyopungua pointi za fedha 10 na isiyozidi pointi za fedha 200. (2) Bila kuathiri kifungu kidogo cha (1), mpangaji au mwenye mali ambaye atashindwa kujisajili katika Rejista iliyowekwa na Kanuni hizi, atakuwa ametenda kosa na atawajibika baada ya kutiwa hatiani kulipa faini ya pointi za fedha zisizopungua 100. SEHEMU YA NNE MASHARTI YA JUMLA Ushirikiano kati ya mamlaka ya serikali za mitaa na Mamlaka ya Mapato Tanzania
Part
SEHEMU YA NNE
- 10 Verify source ↗
Section 10
AI-assisted research summary: This section concerns cooperation between local government authorities and the Tanzania Revenue Authority on service charges.
10. Ushirikiano kati ya mamlaka ya serikali za mitaa na Mamlaka ya Mapato Tanzania. Ada za utoaji wa huduma. Ushirikiano wa jumla kutoka kwa mamlaka za serikali za mitaa. _________ JEDWALI _________ 2 Kanuni za Usimamizi wa Kodi (Ukusanyaji wa Kodi Kwenye Mapato ya Upangishaji Kwa Watu Binafsi) Tangazo La Serikali Na. 427 (Linaendelea)) Jina Tafsiri Sura ya 288 Sura ya 287 Sura 287 Sura ya 332 Sura ya 332 SEHEMU YA KWANZA MASHARTI YA AWALI - 8 Verify source ↗
(1) Kwa madhumuni ya kutekeleza majukumu
AI-assisted research summary: Wahusika waliotajwa wanaweza kushauriana au kushirikiana katika masuala ya kiufundi na kiutendaji kwa ajili ya kutekeleza majukumu, mradi timu ziwe ndogo ya angalau maafisa wawili kila upande na zifuate masharti ya kumbukumbu, uidhinishaji, na uteuzi wa uongozi wa timu.
8.-(1) Kwa madhumuni ya kutekeleza majukumu chini ya Kanuni hizi, Kamishna Mkuu, Afisa muidhinishwa na Mkurugenzi wa Halmashauri au Afisa wake au kushirikiana katika masuala ya kiufundi na kiutendaji, ili mradi– aliyeidhinishwa, wanaweza kushauriana (a) mashauriano au ushirikiano huo ni kati ya timu za kiufundi au za uendeshaji zilizochaguliwa ambazo idadi ya wanachama wake hawawezi kuwa chini ya maafisa wawili kutoka kila upande; (b) uteuzi wa timu utajumuisha maafisa ambao wana ujuzi wa jukumu husika; (c) kumbukumbu za kila mashauriano au ushirikiano zitatayarishwa na kuwekwa ama kwa njia ya kielektroniki au nakala ngumu kwa madhumuni ya utekelezaji na marejeo; (d) maamuzi ya timu za kiufundi au za uendeshaji yatafikiwa juu ya makubaliano ya pande zote mbili kwa kuridhiwa na Mkurugenzi wa Halmashauri husika na Meneja wa Kodi wa Mkoa, Afisa Msimamizi wa Wilaya au Msimamizi wa Kituo cha Kodi kwa niaba ya 9 Kanuni za Usimamizi wa Kodi (Ukusanyaji wa Kodi Kwenye Mapato ya Upangishaji Kwa Watu Binafsi) Tangazo La Serikali Na. 427 (Linaendelea)) Kamishna Mkuu, kadri itakavyokuwa; (e) baada ya kuidhinishwa na wakuu husika, mawasiliano hayo yatafanywa kati ya timu kwa madhumuni ya kusajili uidhinishaji wa utekelezaji; na ya maamuzi uthibitisho rasmi na Posho na vifaa vya utendaji kazi (f) timu itateua mwenyekiti na katibu. - 9 Verify source ↗
(1) Kamishna Mkuu ataweka vigezo na utaratibu
AI-assisted research summary: Kamishna Mkuu ataweka vigezo na utaratibu wa kulipa posho kwa maafisa watendaji wa mitaa au vijiji, kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Halmashauri husika. Anaweza pia kutoa vifaa muhimu na mafunzo kwa ajili ya kuboresha utendaji wao.
9.-(1) Kamishna Mkuu ataweka vigezo na utaratibu kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Halmashauri husika wa namna ya kulipa posho kwa maafisa watendaji wa mitaa au vijiji ili kufanikisha utekelezaji endelevu wa majukumu yaliyo chini ya Kanuni hizi. (2) Bila kuathiri kanuni ndogo (1), Kamishna Mkuu anaweza kutoa vifaa muhimu na mafunzo kwa maafisa watendaji wa mitaa au vijiji kwa ajili ya kuwezesha utendaji bora wa shughuli za maafisa hao chini ya kanuni hizi. Ushirikiano wa jumla kutoka kwa mamlaka ya serikali za mitaa - 10 Verify source ↗
Kamishna Mkuu, katika kuboresha taarifa
AI-assisted research summary: The Commissioner General may consult the District Council Director for tax-administration purposes. In the rental agreement form, the tenant must remit withheld tax electronically, the parties must report terminations or amendments, and the property owner bears taxes, fees, and contract-signing costs.
10. Kamishna Mkuu, katika kuboresha taarifa zilizopo kwenye Rejista au kwa madhumuni mengine yoyote ya usimamizi wa kodi, anaweza kushauriana na Mkurugenzi wa Halmashauri kwa madhumuni ya - (a) kurasimisha usimamizi wa kodi katika eneo lolote la serikali ya mitaa; (b) kusajili watu binafsi kwa madhumuni ya kodi; (c) kuwezesha ukusanyaji bora wa mapato ya Serikali; na (d) kufanya jambo lingine lolote muhimu kwa madhumuni ya usimamizi wa kodi kwa ujumla. _______ JEDWALI 10 Kanuni za Usimamizi wa Kodi (Ukusanyaji wa Kodi Kwenye Mapato ya Upangishaji Kwa Watu Binafsi) Tangazo La Serikali Na. 427 (Linaendelea)) _______ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 3(5)) Fomu ya Mkataba wa Upangisha kati ya Mmiliki wa Mali na Mpangaji MKATABA WA UPANGISHAJI KATI YA ……………………… (Mmiliki wa Mali) NA…………………………(Mpangaji) Umeandikwa na: ……………………………… ……………………………… TAREHE ………………….. MKATABA WA UPANGISHAJI MKATABA HUU unafanyika leo ………….., siku ya ……….., 20…..., KATI YA…………………………, ambaye ni (mwenye mali/mwakilishi aliyeidhinishwa na mwenye mali) aliyetajwa kama ………….., mwenye TIN …………………… ya mwenye mali, na anwani ya makazi iliyoko mtaa/kijiji …….., Kiwanja Na. …….., Wilaya ya …………….. ndani ya Halmashauri ya …………. Sanduku la Posta ………..... Nambari ya Simu ya Mkononi ………………… (hapa anajulikana kama “Mmiliki wa Mali”) wa Upande wa kwanza; NA …………………………, ambaye ni (mpangaji/mwakilishi aliyeidhinishwa na mpangaji) aliyetajwa kama ………….., mwenye TIN ……………………ya mpangaji, na anwani ya makazi iliyoko mtaa/kijiji …….., Kiwanja Na. …….., Wilaya ya …….. ndani ya Halmashauri ya …………. Sanduku la Posta …... Nambari ya Simu ya Mkononi ………………… (hapa anajulikana kama “Mpangaji”) wa Upande wa pili. AMBAPO: Mmiliki wa Mali anamiliki mali aina ya ………………………… ambayo ipo katika mtaa/Kijiji wa/cha ………….. kwenye Kiwanja Na. ………. Kitalu ………. Kilichopo Kata ya …………………. katika Wilaya ya ………….. ndani ya Halmashauri ya …………….. Mkoa wa …………. pamoja na maboresho yote yaliyoko. (hapa inajulikana kama "Mali"); na Mmiliki wa Mali ameamua kupangisha mali hiyo kwa Mpangaji, kwa muda wa …………. Kwa kiasi cha TZS ……………. kwa mwezi na Mpangaji amekubali kupangisha mali hiyo chini ya kanuni na masharti yaliyotajwa katika mkataba huu wa upangaji. HIVYO SASA: 11 Kanuni za Usimamizi wa Kodi (Ukusanyaji wa Kodi Kwenye Mapato ya Upangishaji Kwa Watu Binafsi) Tangazo La Serikali Na. 427 (Linaendelea)) KANUNI NA MASHARTI MUDA WA UPANGISHAJI NA MALIPO YA KUPANGISHA. ambayo Mmiliki wa mali atapangisha mali hiyo kwa Mpangaji kwa muda wa ………….. kwa malipo ya TZS ………………. Kwa Mwezi, ifuatavyo; ………………………………………………………………………………………………… ………………………………………………………………………………………………… ….. Mpangaji amekubali kupangishwa kwa muda wa ……………… na kulipa malipo ya TZS ………………… kwa mwezi, malipo yatalipwa kwa mwenye mali baada ya Mpangaji kukata kodi ya zuio ya TZS …………….. na kumlipa mwenye mali kiasi kilichobaki cha TZS …………… Mpangaji atapeleka kiasi alichokizuia kwenye Akaunti ya Benki ya Kamishna Mkuu kwa njia ya kielektroniki baada ya kupewa namba ya malipo na Afisa Mtendaji wa Mtaa/Kijiji. yatalipwa kama WAJIBU WA MMILIKI WA MALI: Mmiliki wa mali anaahidi kufanya yafuatayo mara tu baada ya Mpangaji kufanya malipo ya kodi ya upangaji. ………………. ………………. WAJIBU WA MPANGAJI: Mpangaji anakubali kutekeleza majukumu yafuatayo: ……………….; ……………….; UTATUZI WA MIGOGORO: ……………..; ……………...; ………………. USITISHAJI WA MKATABA: ………………; …………….…; Pande zote zinakubali kwamba endapo mkataba utasitishwa na kufanyiwa marekebisho yoyote, taarifa hizo ni lazima ziwasilishwe kwa Mtendaji wa Mtaa/Kijiji. MASHARTI YA JUMLA: ……………..….. ………………... 12 Kanuni za Usimamizi wa Kodi (Ukusanyaji wa Kodi Kwenye Mapato ya Upangishaji Kwa Watu Binafsi) Tangazo La Serikali Na. 427 (Linaendelea)) ………………... Mmiliki wa mali, atawajibika kulipa aina zote za kodi, ada pamoja na gharama zinazohusiana na utiaji saini wa mkataba huu. KWA USHUHUDA ULIOPO, pande zote za mkataba huu, wametia saini mkataba huu kama inavyonekana hapa chini, katika siku na mwaka kama ifuatavyo; MMILIKI WA MALI: IMESAINIWA na KUTHIBITISHWA na …………. } …………….…………………………………………. } ________ MMILIKI DOLE GUMBA Ambaye ametambulishwa kwangu na ………………} Na mwisho, kumfahamu binafsi kama} Leo ………….. Mwezi wa ………. Mwaka, 20…} MBELE YA: JINA …………………… SAINI ……………………. ANUANI CHEO/WADHIFA: …………… .............................. MPANGAJI WA MALI: IMESAINIWA na KUTHIBITISHWA na …………. } …………….…………………………………………. } ____________ MPANGAJI DOLE GUMBA Ambaye ametambulishwa kwangu na ………………….} Na mwisho, kumfahamu binafsi kama} Leo ………….. Mwezi wa ………. Mwaka, 20.….. } MBELE YA: JINA …………………………….. SAINI …………………………….. ANUANI …………………….. CHEO/WADHIFA: ………………….. MKATABA HUU UMESIMAMIWA, KUTHIBITISHWA NA KUHIFADHIWA NA; JINA ……………………………. 13 Kanuni za Usimamizi wa Kodi (Ukusanyaji wa Kodi Kwenye Mapato ya Upangishaji Kwa Watu Binafsi) Tangazo La Serikali Na. 427 (Linaendelea)) SAINI ……………………………. ANUANI …………………….. CHEO/WADHIFA: AFISA MTENDAJI WA MTAA/KIJIJI UMEANDIKWA NA:- ………………… ………………… …………………. Dodoma, 20 Mei, 2024 MWIGULU LAMECK NCHEMBA MADELU Waziri wa Fedha 14
Part
SEHEMU YA KWANZA
- 1 Verify source ↗
Kanuni hizi zitajulikana kama Kanuni za
AI-assisted research summary: These rules are named the Tax Administration Regulations (Collection of Tax on Rental Income for Individuals) of 2024.
1. Kanuni hizi zitajulikana kama Kanuni za Usimamizi wa Kodi (Ukusanyaji wa Kodi Kwenye Mapato ya Upangishaji kwa Watu Binafsi), za Mwaka 2024. - 2 Verify source ↗
Katika Kanuni hizi, isipokuwa kama muktadha
AI-assisted research summary: Sehemu hii inaweka maana ya maneno na misamiati inayotumika katika Kanuni hizi.
2. Katika Kanuni hizi, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “Afisa Mtendaji wa Kijiji” maana yake ni afisa wa serikali za mitaa anayefanya kazi kama msimamizi wa shughuli za serikali za mitaa katika ngazi ya kijiji na inajumuisha mtumishi mwingine yeyote wa umma ambaye ameteuliwa na Mkurugenzi wa Halmashauri kutekeleza majukumu ya Afisa Mtendaji wa Kijiji; “Afisa Mtendaji wa Mtaa” maana yake ni afisa wa serikali za mitaa anayefanya kazi kama msimamizi wa shughuli za serikali za mitaa katika ngazi ya Mtaa na inajumuisha mtumishi mwingine yeyote wa umma ambaye ameteuliwa na Mkurugenzi wa Halmashauri kutekeleza majukumu ya Afisa Mtendaji wa Mtaa; “Kata” maana yake ni eneo la mamlaka ya serikali za mitaa kama lilivyogawanywa chini ya Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) au Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya); “kijiji” maana yake ni eneo la utawala wa serikali za mitaa chini ya usimamizi wa Afisa Mtendaji wa Kijiji ndani ya Kata; “kodi ya mapato” maana yake ni kodi ya mapato itokanayo na mapato ya pango au ukodishaji mali ambayo hukusanywa wakati wa kulipia pango au ukodishaji wa mali kupitia utaratibu uliopo chini ya Sheria ya Kodi ya Mapato; “mali” maana yake ni nyumba, jengo au kipande cha ardhi ambacho mtu binafsi anapokea malipo ya pango au ukodishaji; Sura ya 287 “Mamlaka ya Serikali za Mitaa” maana yake ni mamlaka 3 Kanuni za Usimamizi wa Kodi (Ukusanyaji wa Kodi Kwenye Mapato ya Upangishaji Kwa Watu Binafsi) Tangazo La Serikali Na. 427 (Linaendelea)) Sura ya 288 Sura ya 287 Sura ya 288 Sura 287 ya wilaya kama ilivyoainishwa katika Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) au Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji); “Mkurugenzi wa Halmashauri” maana yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya, Mkurugenzi wa Jiji, Mkurugenzi wa Manispaa au Mkurugenzi wa Jiji kama ilivyoainishwa chini ya Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) au Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji); “Mtaa” maana yake ni eneo la utawala wa serikali za mitaa chini ya usimamizi wa Afisa Mtendaji wa Mtaa ndani ya Kata; “mtu binafsi” maana yake ni mtu yeyote ambaye si kampuni au shirika hodhi; Sura ya 438 “pointi za fedha” ina maana sawa na ilivyotafsiriwa chini Sura ya 438 Sura ya 438 ya Sheria ya Usimamizi wa Kodi; “Sheria” maana yake ni Sheria ya Usimamizi wa Kodi; na “TIN” maana yake ni Nambari ya Utambulisho wa Mlipakodi kama ilivyoainishwa kwenye Sheria ya Usimamiza wa Kodi. SEHEMU YA PILI USAJILI WA WAMILIKI MALI NA WAPANGAJI Usajili wa wamiliki wa mali na wapangaji
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Kanuni za Usimamizi wa Kodi (Ukusanyaji wa Kodi Kwenye Mapato ya Upangishaji kwa Watu Binafsi), za Mwaka 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in