Sheria Ndogo ya Uhifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Hai ya Mwaka 2024
This provision gives the by-law its short title: the Hai District Council Environmental Conservation By-Law, 2024.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Uhifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Hai ya Mwaka 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This provision gives the by-law its short title: the Hai District Council Environmental Conservation By-Law, 2024. This by-law applies throughout the entire area of the Hai District Council. This section defines key terms used in the by-law. Halmashauri must set aside grazing areas, provide a special livestock route, and conduct a livestock census with livestock cards and farmer education. Kila mfugaji lazima azalishe na kulisha mifugo katika malisho yaliyopangwa, atumie njia zilizotengwa na Halmashauri, awe na kadi ya mfugo, ahudhurie mafunzo yanapohitajika, asikate miti, na asajili mifugo kwenye rejista ya Kijiji.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Uhifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Hai ya Mwaka 2024
Showing 27 of 27
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itaijulikana kama Sheria Ndogo
AI-assisted research summary: This provision gives the by-law its short title: the Hai District Council Environmental Conservation By-Law, 2024.
1. Sheria Ndogo hii itaijulikana kama Sheria Ndogo ya Uhifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Hai ya Mwaka 2024. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la
AI-assisted research summary: This by-law applies throughout the entire area of the Hai District Council.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la Mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya ya Hai. Tafasiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii isipokuwa pale muktadha
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the by-law.
3. Katika Sheria Ndogo hii isipokuwa pale muktadha utahitaji vinginevyo: “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni afisa yeyote aliyeteuliwa na Mkurugenzi kwa lengo la kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “eneo la hifadhi” maana yake ni maeneo ya milima, Mbuga za Wanyama, maeneo ya vyanzo vya maji, hifadhi ya misitu, miteremko na maeneo mengine ambayo yatatangazwa na Halmashauri kuwa ni maeneo ya hifadhi; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Hai; “uhifadhi wa mazingira” maana yake ni utunzaji endelevu wa ardhi, mimea, hewa, viumbe hai na visivyo hai na vyanzo vya maji kwa mujibu wa Sheria ya Ndogo hii au Sheria nyingine yoyote; “kiwanda” maana yake ni jengo au eneo ambapo vitu vinatengenezwa au kuongezewa thamani; 1 Sheria Ndogo ya Uhifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Hai Tangazo La Serikali Na. 457 (Linaendelea) “kuvuna misitu” maana yake ni uvunaji wa mazao ya misitu, ikiwa ni pamoja na kufyeka, kukata au kung’oa miti au visiki; “maeneo ya malisho” maana yake ni maeneo yaliyotengwa na Halmashauri kwa ajili ya malisho ya mifugo; “maji” kama ilivyoelezwa katika Sheria ya Usimamizi Mazingira; Sura ya 191 Sura ya 191 “maji taka” kama ilivyoelezwa katika Sheria ya Usimamizi Mazingira; Sura ya 323 “mazao ya misitu” maana yake kama ilivyoelezwa katika Sura ya 191 “mazingira” kama ilivyoelezwa katika Sheria ya usimamizi Sheria ya misitu; wa Mazingira; “mfugaji” maana yake ni mtu yeyote anaejishughulisha na ufugaji mifugo katika eneo la Halmashauri; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai au Afisa yeyote aliyeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi chini ya Sheria Ndogo hii; Sura ya 191 “Mazingira” kama ilivyoelezwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; “Mifugo” maana yake ni wanyama wanaofugwa na Sura ya 323 “misitu” maana yake kama ilivyoelezwa katika Sheria ya binadamu; misitu; “Miti iliyohifadhiwa” maana yake ni pamoja na Mvule, Mkufi, Mninga, ikiwa ni miti yote (Kafuri) iliyotangwaza au itakayotangazwa katika gazeti la Serikali. “taka” kama ilivyo katika Sheria ya Usimamizi Mazingira; “taka ngumu” maana yake ni kama ilivyoelezwa katika Sheria ya Usimamizi Mazingira; Sura ya 191 Sura ya 191 Sura ya 191 “taka za viwandani” maana yake ni kama ilivyoelezwa Sura ya 191 “uchafu Hatari” maana yake ni kama ilivyoelezwa katika katika Sheria ya usimamizi wa Mazingira; Sheria ya usimamizi wa Mazingira; Sura ya 191 “uchafu wa mazingira” maana yake ni kama ilivyoelezwa Sura ya 191 “udongo” maana yake ni kama ilivyoelezwa katika Sheria katika Sheria ya usimamizi wa Mazingira; Sura ya 191 “vitu hatari” maana yake ni kama ilivyoelezwa katika Sheria ya usimamizi wa Mazingira; 2 Sheria Ndogo ya Uhifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Hai Tangazo La Serikali Na. 457 (Linaendelea) Wajibu wa Halmashauri Wajibu waMfugaji Marufuku kwa Mfugaji ya usimamizi wa Mazingira; - 4 Verify source ↗
(1) Halmashauri itakuwa na wajibu wa kutenga
AI-assisted research summary: Halmashauri must set aside grazing areas, provide a special livestock route, and conduct a livestock census with livestock cards and farmer education.
4.-(1) Halmashauri itakuwa na wajibu wa kutenga maeneo maalum kwa ajili ya shughuli za malisho ndani ya eneo la Halmashauri. (2) Halmashauri itatenga njia maalum ya kupitisha mifugo kwenda na kurudi malishoni au minadani. (3) Halmashauri itafanya sensa ya mifugo na kutoa kadi za mifugo na elimu ya ufugaji bora kwa jamii. - 5 Verify source ↗
Kila mfugaji chini ya Sheria Ndogo hii
AI-assisted research summary: Kila mfugaji lazima azalishe na kulisha mifugo katika malisho yaliyopangwa, atumie njia zilizotengwa na Halmashauri, awe na kadi ya mfugo, ahudhurie mafunzo yanapohitajika, asikate miti, na asajili mifugo kwenye rejista ya Kijiji.
5. Kila mfugaji chini ya Sheria Ndogo hii: (a) atatakiwa kufuga na kulisha mifugo katika na ya malisho yaliyopangwa maeneo Halmashauri; (b) atatakiwa kupitisha mfugo au mifugo yake katika njia zilizopangwa na kutengwa na Halmashauri; (c) atatakiwa kuwa na kadi ya mfugo au mifugo idadi na aina ya mifugo itakayoonyesha aliyonayo; (d) atatakiwa kuhudhuria mafunzo ya ufugaji kama atakavyohitajiwa na Halmashauri; (e) kutokata miti; na (f) kusajili mfugo au mifugo katika rejista ya Kijiji. - 6 Verify source ↗
Itakuwa marufuku kwa mfugaji yeyote
AI-assisted research summary: It is forbidden for any livestock keeper to graze, feed, or water livestock in areas not set aside for that purpose, move livestock on roads for more than 30 kilometres, bring livestock into an area of the Halmashauri without permission, or pass livestock through areas not approved by the Halmashauri.
6. Itakuwa marufuku kwa mfugaji yeyote: (a) kuchunga au kulisha, au kunywesha maji mfugo au mifugo katika maeneo yote ambayo hayakutengwa kwa ajili hiyo; (b) kusafirisha mfugo au mifugo kwa kuiswaga barabarani zaidi ya kilometa thelathini; (c) kuingiza mfugo au mifugo katika eneo Halmashauri bila kibali cha Halmashauri; la (d) kupitisha mfugo au mifugo katika maeneo ambayo hayakuidhinishwa na Halmashauri. Marufuku - 7 Verify source ↗
(1) Mtu yoyote Hatoruhusiwa kujenga, kufanya
AI-assisted research summary: This section prohibits building or doing activities in a protected area, using land contrary to an approved land-use plan, burning a farm to clear it for agriculture unless the council gives written permission, and dumping pesticide waste or washing sprayers into water sources or rivers.
7.-(1) Mtu yoyote Hatoruhusiwa kujenga, kufanya shughuri au jambo lolote katika eneo la hifadhi. (2) Mtu hatotumia ardhi kinyume na mpango wa matumizi uliopangwa na kuidhinishwa na Halmashauri. (3) Ni marufuku kwa mtu yeyote kusafisha shamba kwa ajili ya kilimo kwa njia ya kuchoma moto isipokuwa 3 Sheria Ndogo ya Uhifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Hai Tangazo La Serikali Na. 457 (Linaendelea) kwa kibali maalum cha maandishi kutoka Halmashauri. (4) Ni marufuku kwa mtu yeyote kutupa mabaki ya vifungashio vya viuatilifu au kusafisha vipulizi au kumwaga mabaki ya viuatilifu katika chanzo cha maji au mto. - 8 Verify source ↗
Muda unaotakiwa kusafisha shamba kwa kuchoma
AI-assisted research summary: This provision sets the time for clearing a field by burning under the subsidiary legislation.
8. Muda unaotakiwa kusafisha shamba kwa kuchoma moto chini ya Sheria Ndogo hii ni kuanzia Saa kumi na mbili kamili asubuhi hadi Saa nne kamili asubuhi. - 9 Verify source ↗
Mtu yeyote aliyepata kibali cha kuchoma moto
AI-assisted research summary: Anyone with a fire-burning permit must give two days’ notice to neighbors in the area before burning and put in place measures to stop the fire spreading.
9. Mtu yeyote aliyepata kibali cha kuchoma moto atalazimika kutoa taarifa ya siku mbili kabla ya kuchoma moto kwa majirani walioko katika eneo analotaka kuchoma na ataweka njia za kuzuia moto kusambaa maeneo mengine. - 10 Verify source ↗
Ni wajibu wa wakazi wa eneo ambalo uoto wa
AI-assisted research summary: Residents of areas where native vegetation or local environment has been damaged must restore it by planting trees.
10. Ni wajibu wa wakazi wa eneo ambalo uoto wa asili au mazingira ya eneo husika yameharibiwa, kuhakikisha kua wanalirudisha katika hali yake ya kawaida kwa kupanda miti ili kutoendelea kuharibu mazingira na kurejesha uoto katika hali yake ya asili. Muda wa kuchoma moto Kibali cha kuchoma Moto Uhifadhi wa Uoto wa Asili Uchimbaji Mchanga na Kokoto - 11 Verify source ↗
Mtu hatoruhusiwa kuchimba mchanga au kifusi,
AI-assisted research summary: Mtu haruhusiwi kuchimba mchanga, kifusi au kokoto au kuchoma tofali katika maeneo yaliyotajwa bila ruhusa ya Halmashauri.
11. Mtu hatoruhusiwa kuchimba mchanga au kifusi, kuchimba kokoto au kuchoma tofali katika makazi ya watu, maeneo yaliyohifadhiwa, kando kando ya mito au ndani ya mto, bwawa au ziwa isipokuwa kwa ruhusa ya Halmashauri. Wajibu wa kulinda vyanzo vya Maji - 12 Verify source ↗
(1) Halmashauri
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima isimamie na kulinda vyanzo vya maji, na Halmashauri pamoja na jamii husika lazima wapande miti isiyonyonya maji kwa kufuata maelekezo ya Afisa Misitu. Pia, mtu haruhusiwi kumiliki eneo la chanzo cha maji.
12.-(1) Halmashauri itawajibika kusimamia na kulinda vyanzo vya maji. (2) Itakuwa ni wajibu wa Halmashauri na jamii husika kupanda miti isiyonyonya maji katika vyanzo vya maji kwa kuzingatia maelekezo ya Afisa Misitu. (3) mtu hatoruhusiwa kumiliki eneo la chanzo cha maji. Ukataji Miti - 13 Verify source ↗
Ni marufuku kwa mtu yeyote kukata miti kwa
AI-assisted research summary: Watu hawaruhusiwi kukata au kuvuna miti bila kibali cha Halmashauri, na wavunaji wa miti kwa ajili ya mkaa lazima wawe na eneo maalum lililoidhinishwa.
13. Ni marufuku kwa mtu yeyote kukata miti kwa ajili ya matumizi ya aina yoyote bila kupata kibali kutoka Halmashauri. (2) Ni marufuku kwa mtu yeyote kuvuna miti katika msitu ambao umehifadhiwa kwa ajili ya viumbe hai maalum ambao ni rasilimali kwa Taifa. (3) Watu wanaovuna miti kwa ajili ya kuchoma mkaa wanatakiwa kuwa na eneo maalum lililoidhinishwa na 4 Sheria Ndogo ya Uhifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Hai Tangazo La Serikali Na. 457 (Linaendelea) Utaratibu wa kupata kibali cha kukata mti Wajibu wa kupanda miti Wajibu wa Halmashauri ya Kijiji Halmashauri kwa ajili ya kuchoma mkaa. - 14 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote anayetaka kukata mti au miti
AI-assisted research summary: Anyone who wants to cut a tree or trees must write to the Village Executive Officer. The application is reviewed by the Village Environmental Committee and may be approved or rejected.
14.-(1) Mtu yeyote anayetaka kukata mti au miti atatakiwa kuandika barua kwenda kwa Mtendaji wa Kijiji ikionesha nia ya kukata mti au miti. (2) maombi hayo yatajadiliwa na Kamati ya Mazingira ya Kijiji na yanaweza kukubaliwa au kukataliwa. (3) Endapo maombi yatakubaliwa na kuidhinishwa na Halmashauri ya Kijiji yatapelekwa kwa Mkurugenzi kwa ajili ya kuidhinisha kibali cha kukata miti. (4) Endapo maombi ya kukata mti au miti yatakataliwa, muombaji atajulishwa kwa maandishi sababu za kukataliwa. (5) Kibali kitakachotolewa kwa ajili ya kukata mti au miti kitadumu kwa siku saba. - 15 Verify source ↗
Kila mkazi wa Halmashauri atawajibika
AI-assisted research summary: Wakazi wa Halmashauri lazima wapande na kutunza miti kwenye maeneo yao, ikiwa ni pamoja na angalau miti kumi katika makazi yao. Taasisii ndani ya Halmashauri nazo lazima zipande miti ya kukinga upepo kuzunguka majengo yao.
15. Kila mkazi wa Halmashauri atawajibika: (a) kupanda na kutunza miti katika eneo lake; (b) kupanda na kutunza miti isiyopungua kumi katika makazi yake; na (c) kupanda na kutunza miti katika shamba au mashamba anayomiliki. (2) kila Taasisii ndani ya Halmashauri itapaswa kupanda miti ya kukinga upepo kuzunguka majengo yake na kuwa na shamba lisilopungua miti hekta mbili. (3) Upandaji wa miti utatakiwa kufuata ushauri wa Mtaalamu; - 16 Verify source ↗
Kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii kila Kijiji
AI-assisted research summary: Kila Kijiji lazima kitenge na kitetunze maeneo na miti ya uhifadhi; watu wanaokata miti lazima wapande miti badala yake na baadhi lazima wajisajili kwa ajili ya msumeno wa moto.
16. Kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii kila Kijiji: (a) kitawajibika kutenga eneo la hifadhi ya Msitu wa asili kwa ajili ya matumizi ya baadaye; (b) kitatunza miti yote inayopandwa katika eneo la Kijiji; (c) kinapanda na kumiliki shamba la miti lenye ukubwa wa ekari mbili kila mwaka na kulitunza; (d) kinatunza na kuhifadhi miti na nyasi kwenye milima, makorongo na vyanzo vya maji ili kuzuia mmomonyoko wa udongo; (e) Mtu yeyote atalazimika kupanda miti mitano (5) kwa kila mti mmoja anaoukata ili apate kibali cha kukata mti na kama eneo analokata mti au 5 Sheria Ndogo ya Uhifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Hai Tangazo La Serikali Na. 457 (Linaendelea) Utupaji wa Taka Ngumu na Laini Uendeshaji wa Viwanda, Vituo vya Mafuta, Huduma za Ujenzi n.k Makosa yanayohusu Mifugo miti ni kwa ajili ya matumizi ya ujenzi atahakikisha anapeleka miti mitano (5) kwa Uongozi wa Kijiji husika; na (f) Mtu yeyote anayemiliki au anataka kutumia msumeno wa moto katika uvunaji wa miti au mti atalazimika kusajiliwa na kuwa na hati ya usajili itakayotolewa na Halmashauri. - 17 Verify source ↗
(1) Ni wajibu wa Halmashauri kutenga eneo kwa
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima itenge eneo la kutupia taka ngumu au laini na isimamie usafi; mtu yeyote haruhusiwi kutupa taka ovyo kwenye kingo za mabwawa au vyanzo vya maji ndani ya Halmashauri.
17.-(1) Ni wajibu wa Halmashauri kutenga eneo kwa ajili ya kutupa taka ngumu au laini na kusimamia kwa karibu usafi katika eneo lake. (2) Mtu yeyote atakayetupa ovyo taka ngumu au laini katika kingo za mabwawa au kwenye vyanzo vya maji vilivyoko katika Halmashauri atakuwa ametenda kosa. - 18 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote anayeendesha shughuli za
AI-assisted research summary: Watu wanaoendesha shughuli fulani za uzalishaji au viwanda katika maeneo ya makazi wanatakiwa kufuata masharti ya kanuni hii na kuzingatia tahadhari za athari za mazingira.
18.-(1) Mtu yeyote anayeendesha shughuli za karakana, mashine ya kusaga, kuranda mbao, kukamua maji ya matunda, kuchomelea vyuma au kuendesha shughuli yoyote inayozalisha uchafu ambao unaleta athari kwa binadamu na viumbe wengine hai katika maeneo ya makazi ya watu atatakiwa kuzingatia masharti ya Sheria Ndogo hii. (2) Endapo mtu yeyote anataka kuendesha shughuli za kiwanda, kituo cha mafuta, kituo cha huduma mbalimbali za ujenzi atatakiwa kuzingatia tahadhari ya athari za mazingira. (3) Mtu yeyote akienda kinyume na kifungu kidogo cha (1) na (2) cha kanuni hii atakuwa ametenda kosa - 19 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa ikiwa
AI-assisted research summary: Mtu yeyote anatenda kosa akiingiza, akisafirisha, akilisha mifugo bila kibali au katika maeneo yasiyoruhusiwa, au akivua samaki kwa sumu au nyavu zenye matundu madogo.
19.-(1) Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa ikiwa: (a) ataingiza mfugo au mifugo katika eneo la Halmashauri bila kibali; (b) atasafirisha mfugo au mifugo bila kuwa na kibali; (c) atalisha mfugo au mifugo katika maeneo yasiyoruhusiwa; (d) atavua samaki kwa kutumia sumu au nyavu zenye matundu madogo (kokoro). Makosa yanayohusu Kilimo - 20 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya kilimo,
AI-assisted research summary: Mtu yeyote anayekiuka masharti ya kilimo anatenda kosa.
20. Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya kilimo, atakuwa ametenda kosa. 6 Sheria Ndogo ya Uhifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Hai Tangazo La Serikali Na. 457 (Linaendelea) Makosa yanayohusu Hifadhi ya Ardhi Makosa yanayohusu vyanzo vya Maji Makosa yanayohusu Kuvuna, Kuuza, Kusafirisha na Kuhifadhi Mazao ya Misitu - 21 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya kuhifadhi
AI-assisted research summary: Any person who violates the land conservation conditions commits an offence.
21. Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya kuhifadhi ardhi atakuwa ametenda kosa. - 22 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote atakayeharibu chanzo cha maji
AI-assisted research summary: Anyone who damages a water source, fails to take part in conserving water sources, or puts any poison that harms human or other living beings commits an offence.
22.-(1) Mtu yeyote atakayeharibu chanzo cha maji au kushindwa kushiriki katika shughuli za kuhifadhi vyanzo vya maji atakuwa ametenda kosa. (2) Mtu yeyote atakayebainika kuwa ameweka sumu ya aina yoyote kwa namna yoyote ambayo inaathiri maisha ya binadamu na viumbe hai wengine ambao ni rasilimali ya taifa atakuwa ametenda kosa. - 23 Verify source ↗
Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa ikiwa
AI-assisted research summary: Anyone commits an offence if they carry out the listed forest-related acts, including burning in forests, failing to help extinguish fires, harvesting forest produce, making charcoal, cutting firewood, grazing livestock in protected or planted forest areas, stripping bark, or farming/cutting trees in protected water-source and erosion-control areas, without a permit where required.
23. Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa ikiwa: (a) atachoma au kusababisha moto katika misitu bila kibali; (b) atashindwa kushiriki katika kuzima moto; (c) atavuna mazao ya misitu katika misitu iliyohifadhiwa na isiyohifadhiwa bila kibali; (d) atachoma mkaa na kukata kuni bila kibali; (e) atafyeka nyasi, kung’oa vichaka na kung’oa visiki kwenye misitu bila kibali; kwenye (f) atachunga mifugo lolote lililopandwa miti, iliyohifadhiwa kama bustani ya miti, msitu ya asili au iliyopandwa kwa ajili ya hifadhi; eneo (g) atakata miti au kuchungia mifugo kwenye miti iliyopandwa kwa ajili ya kuzuia mmomonyoko wa udongo au kinga upepo; (h) atabandua magome ya miti kwa ajili ya kutengeneza vilindo, mzinga na vitu vingine bila ya kuwa na kibali; na (i) atalima au kukata miti katika vyanzo vya maji, milima, kando ya njia, makorongo na sehemu nyingine zozote zinazohifadhiwa ili kupunguza mmomonyoko wa udongo. Makosa yanayohusu taka ngumu na laini - 24 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayetupa ovyo taka ngumu au
AI-assisted research summary: Ni kosa kutupa ovyo taka ngumu au laini katika maeneo yasiyoruhusiwa na Sheria Ndogo hii.
24. Mtu yeyote atakayetupa ovyo taka ngumu au laini katika maeneo yoyote yasiyoruhusiwa na Sheria Ndogo hii atakuwa ametenda kosa. makosa yanayohusu - 25 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayetiririsha maji machafu
AI-assisted research summary: Mtu yeyote haruhusiwi kutiririsha maji machafu yanayosababisha madhara kwa binadamu au viumbe hai wengine.
25. Mtu yeyote atakayetiririsha maji machafu 7 Sheria Ndogo ya Uhifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Hai Tangazo La Serikali Na. 457 (Linaendelea) maji taka Adhabu yanayoleta madhara kwa binadamu na viumbe hai wengine atakuwa ametenda kosa. - 26 Verify source ↗
Mtu yeyote atakaye tenda kosa na kupatikana na
AI-assisted research summary: Anyone who commits an offence and is found guilty faces a fine, imprisonment of up to 12 months, or both.
26. Mtu yeyote atakaye tenda kosa na kupatikana na hatia atatozwa faini isiyopungua Shilingi elfu hamsini na isiyozidi Shilingi laki tatu au kifungo kisichozidi miezi kumi na mbili jela au adhabu zote mbili kwa pamoja yaani faini na kifungo. Kufifilisha Kosa - 27 Verify source ↗
Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa na kutoza Shilingi 50,000 ikiwa mkosaji anakiri kosa na kukubali kujaza fomu maalum.
27. Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha kosa kwa kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii kiasi cha Shilingi elfu hamsini endapo mkosaji atakiri kosa na kuwa tayari kujaza fomu maalum iliyoainishwa katika Jedwali la Kwanza la Sheria Ndogo hii. ________________ JEDWALI LA KWANZA __________________ (Limetungwa chini ya Kifungu cha 33) FOMU YA KUKIRI NA KUFILILISHA KOSA nakiri KWA HIARI YANGU Mimi ……………………………………………………… MWENYEWE mbele ya …………………………………………. ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai, kwamba mnamo tarehe …… ya mwezi ……. Mwaka …… nilitenda kosa la kukiuka masharti ya Kifungu cha …… cha Sheria Ndogo ya Hifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Hai ya Mwaka, 2024. Kwa Mamlaka aliyopewa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai, niko tayari kulipa kiasi cha Ada au Ushuru ninaodaiwa. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA MIMI MWENYEWE KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU Leo tarehe…………. ya Mwezi…………..… Mwaka ……………. Jina……………………………….. Saini……………………… MBELE YANGU: Jina:……………………………………..…………………… Saini………………………….…………………………..……… Wadhifa: ………………………………………………………… Tarehe…………………………………………………………. 8 Sheria Ndogo ya Uhifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Hai Tangazo La Serikali Na. 457 (Linaendelea) Nembo ya Halmashauri ya Wilaya ya Hai imebandikwa kwenye Sheria Ndogo hizi kufuatia azimio lililopitishwa kwenye mkutano wa Baraza la Madiwani uliofanyika tarehe 12 mwezi Mei, Mwaka 2022. Lakari hii iligongwa DIONIS M. MYINGA Mkugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Hai EDMUND RUTARAKA Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya Hai NAKUBALI, L.S Dodoma, MOHAMED OMARY MCHENGERWA (MB) 5 Disemba, 20243 Waziri wa Nchi – Ofisi ya Rais (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa) 9
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Uhifadhi ya Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Hai ya Mwaka 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in