Sheria Ndogo ya Uhifadhi wa Misitu ya Halmashauri ya Wilaya ya Hai ya Mwaka 2023
This provision gives the short title of the by-law: the Hai District Council Forest Conservation By-law, 2023.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Uhifadhi wa Misitu ya Halmashauri ya Wilaya ya Hai ya Mwaka 2023
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This provision gives the short title of the by-law: the Hai District Council Forest Conservation By-law, 2023. This by-law applies throughout the whole area of Hai District Council. This section defines key terms used in the by-law, including protected areas, the authorized officer, the council, forest harvesting, farmer, director, forests, and protected trees. Ni marufuku kwa mtu yeyote kuchoma au kusababisha moto katika eneo la misitu ndani ya Halmashauri. Mtu aliyepewa kibali cha kuchoma moto lazima awajulishe majirani siku saba kabla na aweke njia za kuzuia moto.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Uhifadhi wa Misitu ya Halmashauri ya Wilaya ya Hai ya Mwaka 2023
Showing 17 of 17
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya
AI-assisted research summary: This provision gives the short title of the by-law: the Hai District Council Forest Conservation By-law, 2023.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Uhifadhi wa Misitu ya Halmashauri ya Wilaya ya Hai ya Mwaka 2023. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la
AI-assisted research summary: This by-law applies throughout the whole area of Hai District Council.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la Halmashauri ya Wilaya ya Hai. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa pale itakapoelezwa
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the by-law, including protected areas, the authorized officer, the council, forest harvesting, farmer, director, forests, and protected trees.
3. Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa pale itakapoelezwa vinginevyo “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni maana yake ni Afisa Maliasili, Afisa Misitu, Afisa Wanyamapori, Afisa nyuki, wasaidizi misitu pamoja na Afisa yeyote wa Halmashauri atakayeteuliwa kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; ‟Eneo la Hifadhi” ni maeneo ya Milima, Mbuga za Wanyama, Maeneo ya vyanzo vya Maji, Hifadhi ya Misitu, Miteremko na maeneo mengine ambayo yatatangazwa na Halmashauri kuwa ni maeneo ya hifadhi; “Halmashauri” maana yake ni Halmshauri ya Wilaya ya Hai; “hifadhi ya mazingira” maana yake ni utunzaji endelevu wa ardhi, mimea, hewa, viumbe hai na visivyo hai na vyanzo vya maji na maelekezo yatakayotolewa na Afisa Mwidhiniwa chini ya Sheria ya Ndogo hii au Sheria nyingine yoyote; vinavyozingatia masharti ‟Kiwanda” maana yake ni jengo au kundi la majengo au eneo ambapo vitu vinatengenezwa au kuongezewa thamani; ‟Kuvuna misitu” maana yake ni pamoja na kufyeka, kukata au 1 Sheria Ndogo ya Uhifadhi wa Misitu ya Halmashauri ya Wilaya ya Hai Tangazo La Serikali Na. 458(Linaendelea) kung’oa miti,visiki; Sura ya 191 “maji” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Sura ya 191 Usimamizi Mazingira ; “maji taka” kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Usimamizi Sura ya 323 “mazao ya misitu” maana yake kama ilivyotafsiriwa katika Sheria Mazingira; Sura ya 191 Sura ya 323 Sura ya 191 Sura ya 191 Sura ya 191 Sura ya 191 Sura ya 191 Sura ya 191 ya misitu; “mfugaji” maana yake ni mtu yeyote anaejishughulisha na ufugaji mifugo katika eneo la Halmashauri; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai; “mazingira” kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya usimamizi wa Mazingira; “Misitu” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa kwenye Sheria ya Misitu; “taka” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa kwenye Sheria ya Usimamizi Mazingira; “taka ngumu” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa kwenye Sheria ya Usimamizi Mazingira; “taka za viwandani” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa kwenye Sheria ya Usimamizi Mazingira; “uchafu Hatari” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa kwenye Sheria ya Usimamizi Mazingira; “uchafuzi wa mazingira” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa kwenye Sheria ya Usimamizi Mazingira; “udongo” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa kwenye Sheria ya Usimamizi Mazingira; “vitu hatari” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa kwenye Sheria ya Usimamizi Mazingira; “Miti iliyohifadhiwa” ni pamoja na Mvule, Mkufi, Mninga, camphor (Kafuri), ikiwa ni miti yote iliyotangazwa au itakayotangazwa katika gazeti la Serikali; ‟Waziri” maana yake ni Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa. Kuchoma au kusababisha moto - 4 Verify source ↗
(1) Ni marufuku kwa mtu yoyote kuchoma au
AI-assisted research summary: Ni marufuku kwa mtu yeyote kuchoma au kusababisha moto katika eneo la misitu ndani ya Halmashauri.
4.-(1) Ni marufuku kwa mtu yoyote kuchoma au kusababisha moto katika eneo la Misitu ndani ya Halmashauri. (2) Iwapo moto utatokea katika eneo la Halmashauri, Kiongozi wa eneo husika atawajibika kutoa ishara ya hatari kwa kutumia njia iliyozoeleka kuamuru wakazi wa eneo hilo kwenda kuzima moto huo unapoonekana kuwa na madhara kwa maisha, 2 Sheria Ndogo ya Uhifadhi wa Misitu ya Halmashauri ya Wilaya ya Hai Tangazo La Serikali Na. 458(Linaendelea) Kibali cha kuchoma moto Ukataji miti mali za watu na uharibifu wa mazingira katika eneo hilo. (3) Kila mkazi wa eneo hilo atawajibika kushiriki katika zoezi la kuzima moto huo endapo atatakiwa kufanya hivyo, kama atashindwa kushiriki katika kuzima moto bila sababu ya msingi atakuwa ametenda kosa. - 5 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote aliyepata kibali cha kuchoma moto
AI-assisted research summary: Mtu aliyepewa kibali cha kuchoma moto lazima awajulishe majirani siku saba kabla na aweke njia za kuzuia moto.
5.-(1) Mtu yeyote aliyepata kibali cha kuchoma moto atalazimika kutoa taarifa kwa majirani walioko katika eneo analotaka kuchoma moto siku saba kabla ya kuchoma, na atatakiwa kuweka njia za kuzuia moto. - 6 Verify source ↗
(1) Hairuhusiwi kwa mtu yoyote kukata miti katika
AI-assisted research summary: Kukata au kuvuna miti katika maeneo yaliyohifadhiwa au binafsi kunahitaji kibali cha Afisa Misitu; pia kuna ukaguzi wa ukomavu wa miti, masharti ya eneo la kuchoma mkaa, na ushuru wa asilimia 5 kwa uvunaji fulani.
6.-(1) Hairuhusiwi kwa mtu yoyote kukata miti katika maeneo ya misitu iliyohifadhiwa au maeneo binafsi kwa ajili ya matumizi ya aina yoyote bila kupata kibali kutoka kwa Afisa Misitu. (2) Wataalamu wa Misitu watatakiwa kuhakiki kama miti inayovunwa imekomaa na inafaa kwa ajili ya matumizi. (3) Ni marufuku kwa mtu yoyote kuvuna miti katika msitu ambao umehifadhiwa kwa ajili ya viumbe maalumu ambao ni rasilimali kwa Taifa. (4) Watu wanaovuna miti kwa ajili ya kuchoma mkaa lililoidhinishwa na watatakiwa kuwa na eneo maalum Halmashauri kwa ajili ya kuchoma mkaa. (5) Mtu yeyote atakayevuna miti ya asili na au iliyohifadhiwa kisheria atatakiwa kulipia ushuru wa asilimia 5 kulingana na miongozo iliyopo baada ya vipimo vya ujazo wa mti kuchukuliwa na wataalamu. Wajibu wa kupanda miti - 7 Verify source ↗
Kila Mkazi wa Halmashauri atawajibika kupanda na
AI-assisted research summary: Mkazi wa Halmashauri lazima apande na atunze miti katika eneo lake na ashiriki kampeni za upandaji miti kama anavyoelekezwa na Halmashauri.
7. Kila Mkazi wa Halmashauri atawajibika kupanda na kutunza miti katika eneo lake kama atakavyoelekezwa na Halmashauri na kushiriki katika kampeni za upandaji wa miti katika Wilaya, Kata au kijiji chake anakoishi. Utaratibu wa kupata kibali cha kukata mti - 8 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote anayetaka kukata mti au miti:,
AI-assisted research summary: Anyone who wants to cut a tree or trees must write to the Village Executive Officer, the application is reviewed by the village environment committee, and approved requests go to the District Executive Director’s office for permit approval.
8.-(1) Mtu yeyote anayetaka kukata mti au miti:, (a) atatakiwa kuandika barua kwenda kwa Mtendaji wa Kijiji ikionyesha nia ya kukata mti au miti; (b) maombi hayo yatajadiliwa na Kamati ya Mazingira ya Kijiji husika, na yakikubaliwa yatapelekwa kwenye Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Wilaya kwa ajili ya kuidhinisha kibali cha kukata miti. (c) kama maombi yake yatakataliwa atajulishwa kwa 3 Sheria Ndogo ya Uhifadhi wa Misitu ya Halmashauri ya Wilaya ya Hai Tangazo La Serikali Na. 458(Linaendelea) Udanganyifu maandishi sababu za kukataliwa. (2) Kibali kitakachotolewa kwa ajili ya kukata mti au miti kitadumu kwa siku saba. - 9 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote ambaye atadanganya kuwa ana kibali
AI-assisted research summary: Mtu yeyote asidanganye kuwa ana kibali cha kukata miti kama hana; afisa anayeshindwa kusimamia vibali au kutumia vibali visivyo taratibu anaweza kuchukuliwa hatua kali za kinidhamu.
9.-(1) Mtu yeyote ambaye atadanganya kuwa ana kibali cha kukata miti wakati hana kibali hicho ikithibitika atalipa faini isiyopungua shilingi milioni moja au kifungo cha miezi kumi na mbili au vyote kwa pamoja yaani faini na kifungo (2) Afisa ambaye atashindwa kusimamia vibali vya ukataji miti au atatumia vibali ambavyo havijafuata taratibu ikithibitika Afisa huyo atakuwa ametenda kosa na atachukuliwa hatua kali za kinidhamu. Eneo la hifadhi ya misitu - 10 Verify source ↗
(1) Kila kijiji kitatenga eneo la hifadhi ya Msitu kwa
AI-assisted research summary: Kijiji, shule, taasisi, na mwenye nyumba wana majukumu ya kupanda na kutunza miti; pia kuna marufuku ya kutumia chain saw isiyosajiliwa.
10.-(1) Kila kijiji kitatenga eneo la hifadhi ya Msitu kwa ajili ya matumizi ya baadaye. (2) Kila kijiji kitatunza miti yote inayopandwa katika eneo la kijiji. (3) Kila Kijiji kitahakikisha ya kuwa kila kaya inapanda miti isiyopungua kumi kwenye eneo la nyumba yake kutokana na ushauri wa wataalam. (4) Mtu yeyote anayetaka kukata miti au mti wa matumzi ya kuchonga vifaa, kujenga nyumba, kutengeneza zizi na shughulli nyinginezo, atatakiwa kupata kibali cha maandishi kutoka kwa Afisa Maliasili au Misitu wa Wilaya baada ya kuwasilisha maombi kupitia kwa Mtendaji wa kijiji husika kwa maandishi na kukaguliwa kama yamekidhi vigezo. (5) Ni marufuku kutumia msumeno wa moto (Chain saw) usiokuwa na usajili kwa kuchana mbao katika maeneo yote ya Halmashauri. (6) Kila Kijiji kinatakiwa kupanda miti isiyopungua 15,000 na kuitunza. (7) Kila Shule au Taasisi yoyote katika Halmashauri itapaswa kupanda miti ya kukinga upepo kuzunguka majengo yake na kuwa na shamba lisilopungua miti 1000 kwa matumizi ya Shule au Taasisi husika. (8) Kijiji kitapaswa kutunza na kuhifadhi miti na nyasi kwenye milima, makorongo na vyanzo vya maji ili kuzuia mmomonyoko wa udongo. (9) Kijiji kitahakikisha kuwa kila anayeandaa shamba kwa ajili ya kilimo hatumii moto na anapanda miti kwenye mipaka ya shamba lake kama kinga upepo. 4 Sheria Ndogo ya Uhifadhi wa Misitu ya Halmashauri ya Wilaya ya Hai Tangazo La Serikali Na. 458(Linaendelea) Hifadhi ya vyanzo vya maji Taratibu za kilimo Sura ya 113 Sura ya 114 Masharti kwa Mkulima (10) Kila Mwenye Nyumba atawajibika kupanda miti kwenye eneo lake na kando ya barabara inayopita mbele ya nyumba yake na kuitunza. - 11 Verify source ↗
(1) Ni marufuku kwa mtu yeyote kulima, kukata miti,
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima zipande miti rafiki kwa mazingira kwenye vyanzo vya maji; watu wote wamepigwa marufuku kulima, kukata miti, kuchunga mifugo, kumiliki eneo la chanzo cha maji (isipokuwa Halmashauri husika), au kuchimba mchanga/kuondoa mawe katika maeneo ya mto, chanzo cha maji, au hifadhi bila kibali.
11.-(1) Ni marufuku kwa mtu yeyote kulima, kukata miti, kuchunga mifugo au kufanya jambo lolote linaloharibu kwa namna yoyote chanzo cha maji na hifadhi ya mazingira. (2) Itakuwa ni wajibu wa kila Halmashauri kupanda miti iliyo rafiki na Mazingira katika vyanzo vya maji kwa kuzingatia maelekezo ya Afisa Misitu na Afisa Mazingira. (3) Ni marufuku kwa mtu yeyote kumiliki eneo la chanzo cha Maji isipokuwa Halmashauri husika pekee. (4) Ni marufuku mtu yeyote kuchimba mchanga au kuondoa mawe eneo lolote la mto, chanzo cha maji au eneo lolote la hifadhi bila kuwa na kibali kutoka mamlaka zinazotambuliwa na Serikali. - 12 Verify source ↗
(1) Mtu atakayetaka kuendesha shughuli za kilimo
AI-assisted research summary: Whoever wants to carry out farming activities within the Council must follow the agricultural procedures issued by the Council.
12.-(1) Mtu atakayetaka kuendesha shughuli za kilimo katika Halmashauri atatakiwa kuzingatia taratibu za kilimo kama zitakavyotolewa na Halmashauri kwa kuzingatia Sheria ya Ardhi na Sheria ya Ardhi ya Vijiji na Sheria nyingine zitakazotungwa na Bunge. (2) Itakuwa halali kwa Afisa Mwidhiniwa kuingia katika lolote kwa madhumuni ya kufanya ukaguzi na shamba kuhakikisha utekelezaji wa Sheria Ndogo hii. - 13 Verify source ↗
(1) Ni marufuku kwa mtu yeyote kulima katika
AI-assisted research summary: Mtu yeyote haruhusiwi kulima au kufanya shughuli zinazoharibu misitu na mazingira katika maeneo hatarishi bila kuzingatia ushauri wa maafisa husika, na kuchoma moto shamba karibu na misitu au hifadhi ya mazingira kunahitaji kibali maalumu cha Halmashauri.
13.-(1) Ni marufuku kwa mtu yeyote kulima katika miteremko, karibu na vyanzo vya maji, kandokando ya mito, bwawa na ziwa au kufanya jambo lolote litakalo haribu hifadhi ya Misitu au Mazaingira bila kuzingatia ushauri wa Afisa wa Kilimo na wa wataalam wengine wa Halmashauri. (2) Ni marufuku kwa mtu yeyote kusafisha shamba lililo karibu na misitu au hifadhi ya mazingira kwa ajili ya kilimo kwa njia ya kuchoma moto isipokuwa kwa kibali maalumu kutoka Halmashauri. (3) Kibali kitakachotolewa chini ya Sheria Ndogo hii kitakuwa cha maandishi na kitaonyesha jina la mwenye kibali, tarehe na eneo analotaka kuchoma moto. (4) Muda unaotakiwa kuchoma moto chini ya Sheria Ndogo hii ni kuanzia saa 12:00 Asubuhi hadi saa 4.00 asubuhi. (5) Ni wajibu wa Halmashauri kusimamia shughuli za 5 Sheria Ndogo ya Uhifadhi wa Misitu ya Halmashauri ya Wilaya ya Hai Tangazo La Serikali Na. 458(Linaendelea) Kilimo na kuhakikisha kuwa wanazuia Kilimo cha kuhamahama na kuhimiza Kilimo cha mzunguko (crops rotation). Uhifadhi wa uoto wa asili Uchimbaji wa mchanga na kokoto - 14 Verify source ↗
Kila mkazi wa eneo ambalo uoto wa asili au mazingira
AI-assisted research summary: Kila mkazi wa eneo lililoharibiwa lazima alirejeshe eneo hilo katika hali yake ya kawaida kwa kupanda miti au kuacha kuharibu mazingira na kuruhusu uoto urudi.
14. Kila mkazi wa eneo ambalo uoto wa asili au mazingira ya eneo husika umeharibiwa, ana wajibu wa kuhakikisha kuwa analirudisha katika hali yake ya kawaida kwa kupanda miti au kutoendelea kuharibu mazingira na kuwezesha uoto urudi katika hali yake. - 15 Verify source ↗
(1) Ni marufuku kwa mtu yeyote kuchimba mchanga
AI-assisted research summary: People are prohibited from digging sand or removing stones in places not allowed by the Council, and from building houses or other structures in protected areas.
15.-(1) Ni marufuku kwa mtu yeyote kuchimba mchanga au kuondoa mawe katika maeneo yasiyoruhusiwa na Halmashauri kama vile katika maeneo ya makazi ya watu, maeneo yaliyohifadhiwa, kando kando ya mito au ndani ya mto, bwawa au ziwa isipokuwa kwa ruhusa maalumu ya Halmashauri. (2) Ni marufuku kwa mtu yeyote kujenga nyumba au jengo lolote katika eneo la hifadhi. Makosa na adhabu - 16 Verify source ↗
Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa endapo
AI-assisted research summary: Mtu yeyote anaweza kutenda kosa akivuna, kuuza, kununua, kusafirisha, kuzuia, kushawishi kuvunja sheria, au kukwepa masharti ya Sheria Ndogo hii kuhusu mazao ya misitu.
16. Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa endapo;- (a) atavuna au atauza mazao ya misitu kinyume na Sheria Ndogo hii; (b) atanunua mazao ya misitu kinyume na Sheria Ndogo hii; (c) atasafirisha mazao ya misitu bila ya kuwa na nyaraka; (d) atamshawishi mtu au kundi la watu kukiuka matakwa ya Sheria Ndogo hii; (e) atakataa au kushindwa kutii maagizo ya Afisa Mwidhiniwa; (f) atamzuia Afisa Mwidhiniwa au Mtumishi yeyote wa Halmashauri kutekeleza majukumu yake chini ya Sheria Ndogo hii; (g) atatishia uhai wa Mtumishi wa Halmashauri au Afisa Mwidhiniwa wakati akitekeleza majukumu yake; (h) atalazimisha kupita katikaa vituo vya ukaguzi wa mazao ya misitu kwa nguvu bila kukaguliwa; (i) atatumia msumeno wa moto usiokuwa na usajili katika shughuli zote za uvunaji wa miti; (j) ataendesha biashara ya mazao ya misitu bila kuwa na leseni ya biashara kutoka Halmashauri; (k) atanunua mazao ya misitu bila kulipa ushuru wa mazao ya misitu wa asilimia 5 kwa Halmashauri; (l) atanunua, kuuza au kutorosha mazao ya misitu kwa 6 Sheria Ndogo ya Uhifadhi wa Misitu ya Halmashauri ya Wilaya ya Hai Tangazo La Serikali Na. 458(Linaendelea) madhumuni ya kukwepa masharti ya Sheria Ndogo hii; (m) atasafirisha mazao ya misitu bila kulipa ushuru. - 17 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya Sheria Ndogo hii
AI-assisted research summary: Mtu yeyote anayekiuka masharti ya Sheria Ndogo hii anatenda kosa na anaweza kupewa faini, kifungo, au vyote kwa pamoja.
17. Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya Sheria Ndogo hii atakuwa ametenda kosa na akipatikana na hatia atatozwa faini isiyopungua elfu hamsini kwa kila kosa na isiyozidi Milioni moja kwa kila kosa au kifungo cha miezi isiyozidi kumi na mbili au adhabu zote kwa pamoja, yaani faini na kifungo. 7 Sheria Ndogo ya Uhifadhi wa Misitu ya Halmashauri ya Wilaya ya Hai Tangazo La Serikali Na. 458(Linaendelea) Nembo ya Halmashauri ya Wilaya ya Hai imebandikwa kwenye Sheria Ndogo hizi kufuatia azimio lililopitishwa kwenye mkutano wa Baraza la Madiwani uliofanyika tarehe 12 mwezi Mei, mwaka . DIONIS M. MYINGA Mkugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Hai EDMUND RUTARAKA Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya Hai NAKUBALI, L.S Dodoma, MOHAMED OMARY MCHENGERWA (MB) 5 Disemba, 20243 Waziri wa Nchi – Ofisi ya Rais (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa) 8
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Uhifadhi wa Misitu ya Halmashauri ya Wilaya ya Hai ya Mwaka 2023
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in