Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya za Uvinza za mwaka 2024
This provision gives the local by-law its official name: the Uvinza District Council Service Levy By-Law, 2024.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya za Uvinza za mwaka 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This provision gives the local by-law its official name: the Uvinza District Council Service Levy By-Law, 2024. This bylaw applies throughout the area of the Uvinza District Council authority. Section 3 defines key terms used in the by-law, including the council, director, service levy payer, business entity, and the service levy threshold. The council must charge and collect a service levy from licensed business taxpayers, including a 0.3% rate for those who file sales accounts with Tanzania Revenue Authority, and a different schedule rate for those who do not. Service taxpayers must pay, file monthly sales information and final accounts, keep records, and present documents for inspection. The Director may require tax payers and other informed persons to provide sales, business, accounts, and records information, and may authorize inspection and collection-related actions.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya za Uvinza za mwaka 2024
Showing 12 of 12
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo
AI-assisted research summary: This provision gives the local by-law its official name: the Uvinza District Council Service Levy By-Law, 2024.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya za Uvinza za mwaka 2024. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la
AI-assisted research summary: This bylaw applies throughout the area of the Uvinza District Council authority.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la Mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii isipokuwa pale ambapo
AI-assisted research summary: Section 3 defines key terms used in the by-law, including the council, director, service levy payer, business entity, and the service levy threshold.
3. Katika Sheria Ndogo hii isipokuwa pale ambapo muktadha utaelekeza vinginevyo: “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni afisa yeyote aliyeteuliwa na Mkurugenzi kwa lengo la kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza; “Hesabu” maana yake ni jumla ya mauzo au matumizi ikiwa ni pamoja na ushuru na ada katika mwaka; “Hesabu za mwisho” maana yake ni hesabu za mwisho zinazowasilishwa na taasisi yoyote ya kibiashara baada ya kipindi cha hesabu pamoja na nyaraka au maelezo yatakayotakiwa kutolewa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii; “jumuisho” maana yake ni taarifa, nyaraka au hesabu au maelezo yoyote yahusuyo kiasi na thamani ya kifedha ya bidhaa au huduma zilizozalishwa, zilizosambazwa, au kuuzwa kibiashara na ikiwa ni pamoja na jumuisho la awali zilizotolewa na, 1 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza Tangazo La Serikali Na. 461 (Linaendelea) au la mwisho; Sura ya 212 “kampuni” maana yake ni kampuni iliyosajiliwa kwa mujibu wa Sheria ya Makampuni; “kipindi maalum cha hesabu” maana yake ni muda ambao mfanyabiashara anatakiwa kuwasilisha hesabu za biashara kwa Halmashauri; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza au afisa yeyote aliyeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi chini ya Sheria Ndogo hii; “mlipa ushuru wa huduma” maana yake ni kampuni, tawi la leseni la au mfanyabiashara mwenye zake shughuli katika eneo kampuni anayefanya Halmashauri; “mwaka wa mapato” maana yake ni kipindi cha miezi kumi na mbili ya kalenda ya mwaka; Sura ya 290 “Sheria” maana yake ni Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa. “taasisi ya kibiashara” maana yake ni taasisi iliyosajiliwa kwa mujibu wa Sheria ya Makampuni au Sheria ya Majina ya kibiashara inayojihusisha na shughuli za kiuchumi za uzalishaji wa bidhaa au mazao ya kilimo, usambazaji wa bidhaa au utoaji wa huduma na, au biashara ikiwemo uagizaji wa bidhaa kutoka nje ya Nchi; “tawi la kampuni” maana yake ni tawi la kampuni iliyosajiliwa kwa mujibu wa Sheria ya Makampuni; “ushuru wa huduma” maana yake ni ushuru unaotozwa na kukusanywa na Halmashauri kutoka kwa kampuni, tawi la kampuni au mfanyabiashara yeyote mwenye leseni ya biashara ambaye mauzo yake kwa mwaka ni zaidi ya shilingi milioni nne kutokana na huduma anazopata na kutumia miundombinu ya umma inayomuwezesha kufanya biashara katika eneo la Halmashauri; “Wakala” maana yake ni mtu binafsi au kikundi cha watu, limeteuliwa na kampuni au Halmashauri kufanya kazi yoyote chini ya Sheria Ndogo hii kwa niaba ya Halmashauri husika. shirika ambalo Ushuru wa huduma - 4 Verify source ↗
(1) Halmashauri itatoza na kukusanya ushuru wa
AI-assisted research summary: The council must charge and collect a service levy from licensed business taxpayers, including a 0.3% rate for those who file sales accounts with Tanzania Revenue Authority, and a different schedule rate for those who do not. Service taxpayers must pay, file monthly sales information and final accounts, keep records, and present documents for inspection.
4.-(1) Halmashauri itatoza na kukusanya ushuru wa 2 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza Tangazo La Serikali Na. 461 (Linaendelea) huduma kwa kiwango cha asilimia sifuri nukta tatu ya mauzo baada ya kutoa kodi ya ongezeko la thamani na ushuru wa bidhaa kutoka kwa mtu yeyote mwenye leseni ya biashara anayewasilisha hesabu za mauzo katika Mamlaka ya Mapato Tanzania. (2) Bila kuathiri masharti ya Kanuni ndogo ya (1), Halmashauri itatoza na kukusanya ushuru wa huduma kwa kiwango kilichoainishwa katika Jedwali la Kwanza kutoka kwa wafanyabiashara wenye leseni za biashara ambao hawawasilishi hesabu za mauzo katika Mamlaka ya Mapato Tanzania. 5 -(1) Kila mlipa ushuru wa huduma atakuwa na wajibu wa- (a) kulipa ushuru wa huduma kwa kiwango kilichoainishwa katika Sheria Ndogo hii; (b) kuwasilisha taarifa sahihi za mauzo ya kila mwezi endapo anawasilisha taarifa za hesabu za mauzo katika Mamlaka ya Mapato Tanzania; Wajibu wa Mlipa Ushuru wa Huduma (c) kuwasilisha hesabu sahihi na za kweli; (d) kuwasilisha nyaraka au inayotakiwa kuwasilishwa kwa Halmashauri katika muda uliowekwa; taarifa (e) kutunza kumbukumbu za kitabu cha hesabu; (f) kuonesha kumbukumbu yoyote au nyaraka kwa ajili ya uchunguzi; (2) Kila mlipa ushuru wa huduma atatakiwa kulipa ushuru wa huduma si zaidi ya siku kumi na nne tangu tarehe ya kuwasilisha taarifa za mauzo ya kila mwezi. (3) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (2), Halmashauri inaweza kukubaliana na mlipa ushuru wa huduma utaratibu wa kulipa ushuru huo. (4) Kila mlipa ushuru atatakiwa kuwasilisha Halmashauri hesabu za mwisho katika kipindi cha miezi mitatu tangu kumalizika kwa kipindi cha hesabu. (5) Endapo mlipa ushuru hajawasilisha hesabu za mwisho kwa mwaka wa fedha husika na ametakiwa kufanya hivyo kwa notisi ya siku thelathini, Mkurugenzi au Afisa Mwidhiniwa anaweza kwa kadri atakavyoona inafaa, kuamua kiwango cha hesabu za mlipa ushuru huyo kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. 3 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza Tangazo La Serikali Na. 461 (Linaendelea) (6) Ushuru uliothaminiwa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii, utalipwa katika kipindi cha siku thelathini tangu tarehe ya kufanya tathmini. (7) Endapo mlipa ushuru hajawasilisha majumuisho ya hesabu zake kwa mwaka wowote wa mapato, na endapo Mkurugenzi au Afisa Mwidhiniwa anafikiri kwamba mlipa ushuru huyo ana wajibu wa kulipa ushuru kwa mwaka huo wa fedha, anaweza kwa kadri atakavyoona, kuamua kiwango cha hesabu za mlipa ushuru huyo, isipokuwa tathmini hiyo haitaathiri wajibu wowote wa mlipa ushuru anayostahili kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii, kwa kushindwa kwake kuwasilisha hesabu hizo. Mamlaka ya Mkurugenzi - 6 Verify source ↗
Section 6
AI-assisted research summary: The Director may require tax payers and other informed persons to provide sales, business, accounts, and records information, and may authorize inspection and collection-related actions.
6. -(1) Endapo mlipa ushuru wa huduma anayetakiwa kuwasilisha taarifa ya mauzo chini ya Sheria Ndogo hii atashindwa kuwasilisha taarifa sahihi za mauzo kwa wakati, Mkurugenzi anaweza kutoa notisi ya kumtaka mlipa ushuru wa huduma kuwasilisha taarifa hiyo ndani ya siku thelathini kuanzia tarehe ya kutolewa kwa notisi. (2) Mkurugenzi anaweza kumtaka kwa maandishi mtu yeyote mwenye taarifa kuhusu mfanyabiashara anayepaswa kulipa ushuru wa huduma kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii kuwasilisha kwake taarifa ambazo zitatumika kama taarifa sahihi. (3) Mkurugenzi kwa maandishi Afisa Mwidhiniwa kuingia kwenye jengo au eneo la mlipa ushuru wa huduma kwa nia ya kufanya uchunguzi na tathmini ya kumbukumbu za biashara, vitabu vya hesabu na taarifa kwa ajili ya kupata na kujua kiwango sahihi cha ushuru anachotakiwa kulipa. kumwagiza anaweza (4) Mkurugenzi anaweza kumteua Kamishna wa kodi ya forodha au kodi ya mapato kwa ajili ya kutathmini na kukusanya ushuru wa huduma na kuwasilisha kwa Halmashauri kwa lengo la kupata ushuru wa huduma pamoja na madeni yake. (5) Mkurugenzi kwa taarifa ya maandishi anaweza kumtaka mlipa ushuru yeyote kuwasilisha hesabu zenye taarifa kamili za shughuli za kibiashara zikionesha thamani ya kiasi na thamani ya kifedha ya bidhaa au huduma zilizozalishwa, kuuzwa kibiashara na taarifa ya fedha katika kipindi maalum kusambazwa kutolewa au 4 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza Tangazo La Serikali Na. 461 (Linaendelea) kisichozidi siku thelathini tangu tarehe ya taarifa hiyo. siku (6) Mkurugenzi anaweza, kwa taarifa ya maandishi ya saba kumtaka mlipa ushuru kuwasilisha kumbukumbu za kibiashara na vitabu vya hesabu kwa nia ya kupata taarifa kwa ajili ya kufanyiwa tathmini au kukusanya ushuru wa huduma kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Pili. Uteuzi wa Wakala
Part
Jedwali la Pili.
- 7 Verify source ↗
(1) Bila ya kuathiri masharti yaliyowekwa na
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kumteua Wakala wa kukusanya ushuru kwa niaba ya Halmashauri, na Wakala aliyechaguliwa lazima akusanye, apokee, na awasilishe makusanyo ya ushuru kwa kufuata eneo lililo pangwa, viwango vilivyoidhinishwa, mfumo wa kielektroniki, na masharti ya mkataba wa uwakala.
7.-(1) Bila ya kuathiri masharti yaliyowekwa na Sheria Ndogo hii, Mkurugenzi anaweza kuteua Wakala wa kukusanya ushuru kwa niaba ya Halmashauri. (2) Wakala aliyeteuliwa kwa mujibu wa kanuni ndogo ya (1) atakuwa na wajibu wa- Uwezo wa Afisa Mwidhiniwa (a) kukusanya na kupokea ushuru kwa niaba ya Halmashauri katika eneo alilopangiwa na kwa viwango vilivyoidhinishwa katika Sheria Ndogo hii; na (b) kukusanya ushuru kwa kutumia mfumo wa kielektroniki na kuwasilisha makusanyo yote kwa kuzingatia masharti ya mkataba wa uwakala alioingia na Halmashauri. - 8 Verify source ↗
Afisa Mwidhiniwa anaweza
AI-assisted research summary: Afisa Mwidhiniwa anaweza kukubali na kutathmini hesabu za mlipa ushuru, kukataa hesabu za mwisho zenye mashaka ya usahihi, na kuingia eneo la mlipa ushuru wakati wa mchana kwa ajili ya kuchunguza taarifa na kumbukumbu.
8. Afisa Mwidhiniwa anaweza: (a) kupokea na kukubali hesabu za mlipa ushuru na kuzifanyia tathmini, kuhusu kiwango cha hesabu cha mlipa ushuru endapo hesabu hizo zitakuwa si sahihi; (b) kukataa hesabu za mwisho iwapo atakuwa na sababu za msingi za kuamini kuwa hesabu hizo siyo sahihi; na (c) kuingia kwenye eneo lolote la mlipa ushuru kuanzia saa moja na nusu asubuhi hadi saa kumi na mbili kamili jioni kwa ajili ya kutafuta taarifa au kuchunguza hesabu, vitabu au taarifa zozote kama ataona inafaa. Ukokotoaji wa ushuru wa huduma - 9 Verify source ↗
Halmashauri itakokotoa ushuru wa huduma wa
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima ikokotoe ushuru wa huduma wa taarifa za mauzo kwa kuzingatia taarifa zinazowasilishwa na mlipa ushuru wa huduma katika kipindi maalum cha hesabu.
9. Halmashauri itakokotoa ushuru wa huduma wa taarifa za mauzo katika mlipa ushuru anaewasilisha Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa kuzingatia taarifa zinazowasilishwa na mlipa ushuru wa huduma katika kipindi maalum cha hesabu. 5 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza Tangazo La Serikali Na. 461 (Linaendelea) Makosa - 10 Verify source ↗
Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa endapo
AI-assisted research summary: This section makes it an offence for any person to give false sales or tax information, fail to pay service tax on time, obstruct officers, or destroy or falsify tax-related records and equipment.
10. Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa endapo- (a) atashindwa kuwasilisha Halmashauri taarifa sahihi za mauzo katika muda ulioainishwa katika Sheria Ndogo hii; (b) atawasilisha Halmashauri taarifa zisizo sahihi; (c) atashindwa kulipa ushuru wa huduma katika muda ulioainishwa katika Sheria Ndogo hii; (d) atamshawishi mlipa ushuru wa huduma kukataa au kukwepa kulipa ushuru; (e) atamzuia Afisa Mwidhiniwa au Wakala wa Halmashauri kutekeleza masharti ya Sheria Ndogo hii; (f) atatoa taarifa isiyokuwa sahihi kuhusu jambo lolote linaloweza kuathiri jukumu lake au la mtu mwingine la kulipa ushuru; (g) ataharibu kwa makusudi taarifa au mfumo wa taarifa; (h) ataharibu kwa makusudi vitendea kazi vya kukusanyia ushuru; (i) atafanya hesabu za uongo kwa kupunguza au kutoa hesabu zisizo sahihi; au (j) ataandaa au kutengeneza au kusababisha kuandaliwa au kutengenezwa kwa vitabu vya uongo vya hesabu au kumbukumbu. Adhabu Kufifilisha Kosa - 11 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya kanuni
AI-assisted research summary: Anyone who violates any regulation in this subsidiary legislation commits an offence and, if convicted, may be fined, imprisoned, or both.
11. Mtu yeyote atakayekiuka masharti ya kanuni yoyote katika Sheria Ndogo hii atakuwa anatenda kosa na akitiwa hatiani atatozwa faini isiyopungua shilingi laki mbili na isiyozidi shilingi milioni moja au kifungo kisichopungua miezi kumi na mbili na kisichozidi miezi ishirini na nne au vyote kwa pamoja. - 12 Verify source ↗
Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa kwa kumtoza mkosaji, ikiwa mkosaji anakiri kosa kwa hiari, yuko tayari kujaza fomu ya Jedwali la Tatu, na analipa ushuru unaodaiwa.
12. Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha kosa kwa kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii, kwa mujibu wa Sheria, iwapo mkosaji atakiri kosa kwa hiari na kuwa tayari kujaza fomu maalum iliyoainishwa katika Jedwali la Tatu na kulipa ushuru anaodaiwa. 6 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza Tangazo La Serikali Na. 461 (Linaendelea) ____________ JEDWALI LA KWANZA ____________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 4(2)) ___________ USHURU WA HUDUMA Namba Aina ya malipo Leseni ya biashara Kiasi cha malipo ya Ushuru wa Huduma kwa Mwaka (Shilingi)
Part
JEDWALI LA KWANZA
- 8 Verify source ↗
Section 8
AI-assisted research summary: Mlipaji wa ushuru wa huduma anatakiwa kulipa deni lililo kwenye hati ya madai ndani ya siku 14 baada ya kupokea hati hiyo.
8. 0 hadi 15,000/= 20,000/= hadi 35,000/= 40,000/= hadi 45,000/= 50,000/= hadi 60,000/= 65,000/= hadi 100,000/= 105,000/= hadi 150,000/= 155,000/= hadi 200,000/= 5000/= 10,000/= 15,000/= 30,000/= 40,000/= 50,000/= 100,000/= Malipo ya leseni za vilabu vya pombe za asili 12,000/= kwa miezi sita(6) _________ JEDWALI PILI ___________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 6(6)) HATI YA MADAI YA USHURU WA HUDUMA Kwa; Bw/Bi:..……………………… Pata taarifa kuwa wewe kama Mlipaji wa Ushuru wa Huduma chini ya Sheria Ndogo ya (Ushuru wa Huduma) ya Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza ya Mwaka 2024 unadaiwa jumla ya Sh .......................................……………………………....................................... ikiwa ni malimbikizo ya ushuru wa huduma ambao unapaswa kulipa ndani ya siku kumi na nne toka tarehe ya kupokea hati hii. NAKIRI KUPOKEA HATI Jina ............................................................... Wadhifa………………….. Saini ........................................Tarehe ....................................................... Lipa ushuru huo kwa wakati ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza. ________________________ Mkurugenzi Mtendaji, HALMASHAURI YA WILAYA YA UVINZA 7 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza Tangazo La Serikali Na. 461 (Linaendelea) __________ JEDWALI LA TATU _____________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 12) _____________ FOMU YA KUKIRI NA KUFIFILISHA KOSA Mimi ……………………………………………………… nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya …………………………………………. ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza, kwamba mnamo tarehe …… ya mwezi ……. Mwaka …… nilitenda kosa la kukiuka masharti ya Kanuni ya……........ cha Sheria Ndogo ya (Ushuru wa Huduma) ya Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza ya Mwaka, 2024. Kwa Mamlaka aliyopewa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza, niko tayari kulipa kiasi cha Ada au Ushuru ninaodaiwa pamoja na faini badala ya kushtakiwa Mahakamani. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA MIMI MWENYEWE KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU Leo tarehe…………. ya Mwezi…………..… Mwaka ……………. Jina……………………………….. Saini……………………… MBELE YANGU: Jina: ……………………………………..…………… Saini………………………….………………………….. Wadhifa: ………………………………………………… Tarehe…………………………………………………………. 8 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza Tangazo La Serikali Na. 461 (Linaendelea) Nembo ya Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza imegongwa kwenye Sheria Ndogo hii kufuatia azimio lililopitishwa katika mkutano wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya Uvinza uliofanyika tarehe 18 mwezi Disemba Mwaka 2023 na kushuhudiwa Lakari hiyo ikigongwa mbele ya :- ACLAND DOMINIC KAMBILI Mkugenzi Mtendaji Mkurugenzi wa Halmashauri Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza JACKSON FREDRICK MATESO Meya/Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya Uvinza NAKUBALI, L.S Dodoma, MOHAMED OMARY MCHENGERWA (MB) 25 Machi, 2024 Waziri wa Nchi – Ofisi ya Rais (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa) 9
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya za Uvinza za mwaka 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in