Sheria Ndogo za (Kuzuia na Kudhibiti Sumukuvu) Halmashauri ya Wilaya ya Newala za Mwaka 2024
This section says the by-laws are called the Newala District Council (Prevention and Control of Aflatoxin) By-Laws, 2024.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo za (Kuzuia na Kudhibiti Sumukuvu) Halmashauri ya Wilaya ya Newala za Mwaka 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This section says the by-laws are called the Newala District Council (Prevention and Control of Aflatoxin) By-Laws, 2024. These by-laws apply throughout the area of the Newala District Council Authority. This section defines key terms used in the bylaws. Halmashauri inaweza kuratibu na kusimamia shughuli za kilimo ndani ya eneo lake, na kufanya ukaguzi katika mashamba, vyombo vya usafirishaji wa mazao, maghala, kiwanda au eneo la usindikaji ili kuzuia na kudhibiti sumukuvu na kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hizi. A person intending to carry out agricultural activities must follow proper farm-preparation practices, prepare the field on time, and not burn the field.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo za (Kuzuia na Kudhibiti Sumukuvu) Halmashauri ya Wilaya ya Newala za Mwaka 2024
Showing 19 of 19
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hizi zitajulikana kama Sheria
AI-assisted research summary: This section says the by-laws are called the Newala District Council (Prevention and Control of Aflatoxin) By-Laws, 2024.
1. Sheria Ndogo hizi zitajulikana kama Sheria (Kuzuia na Kudhibiti Sumukuvu) Ndogo za Halmashauri ya Wilaya ya Newala za Mwaka 2024. - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hizi zitatumika katika eneo
AI-assisted research summary: These by-laws apply throughout the area of the Newala District Council Authority.
2. Sheria Ndogo hizi zitatumika katika eneo lote la Mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya ya Newala. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hizi, isipokuwa kama
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the bylaws.
3. Katika Sheria Ndogo hizi, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni Afisa yeyote la aliyeteuliwa na Mkurugenzi kwa kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hizi; lengo “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Newala. “kanuni bora za kilimo” maana yake ni uandaaji wa shamba kwa usahihi, upandaji mbegu bora kwa wakati na kwa nafasi sahihi, upaliliaji, utumiaji mbolea kwa usahihi, udhibiti wa wadudu na wanyama waharibifu, uvunaji na hifadhi sahihi ya mazao; “kilimo” maana yake ni shughuli ya uzalishaji wa mazao; “mkulima” maana yake ni mtu, taasisi, kampuni au kikundi cha watu wanaojihusisha na shughuli za kilimo; 1 Sheria Ndogo za (Kuzuia Na Kudhibiti Sumukuvu) Halmashauri ya Wilaya ya Newala Tangazo La Serikali Na. 464 (Linaendelea) “mfanyabiashara’’ maana yake ni taasisi, kampuni, kikundi cha watu au mtu binafsi anayejihusisha na shughuli za kuuza au kununua mazao ya kilimo; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala au afisa yeyote aliyeteuliwa kutekeleza kazi za Mkurugenzi chini ya Sheria Ndogo hizi; “mazao’’ maana yake ni punje zinazotokana na mmea wa mhindi, mpunga, uwele, mtama, karanga, ngano, ufuta, alizeti, shayiri, ulezi na mazao ya mizizi yatokanayo na mihogo au viazi; “Kuvu’’ maana yake ni ukungu unaoota kwenye mazao; Sura ya 287 “Sheria” maana yake ni Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya); “sumukuvu” maana yake ni sumu zinazozalishwa na kuvu wanao ota kwenye mazao; “uhifadhi” maana yake ni utaratibu wa kutunza mazao katika sehemu ambayo haisababishi mazingira ya uotaji wa kuvu; “ukaushaji” maana yake ni taratibu sahihi za kupunguza unyevu kwenye mazao kwa ajili ya matumizi au uhifadhi; “usindikaji” maana yake ni hatua ya uchakataji wa zao kwa lengo la kuongeza thamani; “uvunaji” maana yake ni uondoaji wa mazao kutoka kwenye mmea baada ya kukomaa au kukauka; “viashiria vya sumukuvu” maana yake ni dalili zinazoonyesha uwepo wa sumukuvu kwenye mazao ya mahindi, mpunga, uwele, mtama, karanga, ngano, ufuta, alizeti, shayiri, ulezi zilizovunjika, na mazao ambayo hayajauka vizuri; “viuatilifu” maana yake ni sumu ya kuua au kuzuia wadudu waharibifu wa mazao; Uratibu na usimamizi wa shughuli za kilimo na udhibiti wa Sumukuvu - 4 Verify source ↗
(1) Halmashauri itakuwa na mamlaka ya
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kuratibu na kusimamia shughuli za kilimo ndani ya eneo lake, na kufanya ukaguzi katika mashamba, vyombo vya usafirishaji wa mazao, maghala, kiwanda au eneo la usindikaji ili kuzuia na kudhibiti sumukuvu na kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hizi.
4.-(1) Halmashauri itakuwa na mamlaka ya kuratibu na kusimamia shughuli za kilimo ndani ya eneo la Halmashauri kwa lengo la kuzuia na kudhibiti sumukuvu. (2) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya 2 Sheria Ndogo za (Kuzuia Na Kudhibiti Sumukuvu) Halmashauri ya Wilaya ya Newala Tangazo La Serikali Na. 464 (Linaendelea) (1), Halmashauri itakuwa na mamlaka ya kufanya ukaguzi katika mashamba au vyombo vya usafirishaji wa mazao au maghala au kiwanda au eneo la usindikaji kwa lengo la kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hizi. Uandaaji wa shamba - 5 Verify source ↗
Mtu yeyote anayekusudia kufanya shughuli
AI-assisted research summary: A person intending to carry out agricultural activities must follow proper farm-preparation practices, prepare the field on time, and not burn the field.
5. Mtu yeyote anayekusudia kufanya shughuli za kilimo, atapaswa kuzingatia misingi ifuatayo: (a) kufuata njia sahihi za uandaaji wa shamba; (b) kutayarisha shamba kwa wakati; na (c) kutochoma moto shamba. Upandaji wa mazao - 6 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayepanda mazao atapaswa
AI-assisted research summary: Anyone who plants crops must follow proper planting methods.
6. Mtu yeyote atakayepanda mazao atapaswa kuzingatia njia sahihi za upandaji ikiwa ni pamoja na: Utunzaji wa mazao shambani Uvunaji wa mazao Ukaushaji wa mazao (a) kutumia mbegu bora; (b) kupanda mara mvua zinapoanza kunyesha; na (c) kupanda kwa nafasi sahihi. za kupandia - 7 Verify source ↗
Mtu aliyepanda mazao atapaswa kuyatunza
AI-assisted research summary: Mtu aliyepanda mazao anapaswa kuyatunza kwa njia sahihi, ikiwemo kutumia mbolea, kupalilia kwa wakati, na kudhibiti magonjwa, wadudu, au wanyama waharibifu.
7. Mtu aliyepanda mazao atapaswa kuyatunza kwa kuzingatia njia sahihi za utunzaji wa mazao ikiwa ni pamoja na: (a) kutumia mbolea; (b) kupalilia kwa wakati; na (c) kudhibiti magonjwa, wadudu na/au wanyama waharibifu. - 8 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayevuna mazao atapaswa
AI-assisted research summary: Anyone who harvests crops must do so using good harvesting practices.
8. Mtu yeyote atakayevuna mazao atapaswa kuvuna kwa kuzingatia kanuni bora za uvunaji ikiwa ni pamoja na- (a) kuvuna mara baada ya mazao kukomaa au kukauka; (b) kusafirisha na kuhifadhi vizuri; na (c) kusafisha shamba baada ya kuvuna. - 9 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayevuna mazao, atapaswa
AI-assisted research summary: Anyone who harvests crops must dry them properly immediately after harvest.
9. Mtu yeyote atakayevuna mazao, atapaswa kuyakausha kwa kutumia njia sahihi mara tu baada ya kuvuna ikiwa ni pamoja na- (a) njia za asili zisizoruhusu kuvu kuota; (b) kutumia maturubai, mikeka na vichanja 3 Sheria Ndogo za (Kuzuia Na Kudhibiti Sumukuvu) Halmashauri ya Wilaya ya Newala Tangazo La Serikali Na. 464 (Linaendelea) vinavyozuia uchafuzi wa mazao; na (c) kukausha kwa itakayoelekezwa na mtaalam. njia yoyote sahihi Uhifadhi wa mazao - 10 Verify source ↗
(1) Mtu atawajibika kuhifadhi mazao kwa
AI-assisted research summary: A person must store crops using proper traditional or modern methods that prevent mold growth.
10.-(1) Mtu atawajibika kuhifadhi mazao kwa kutumia njia sahihi za kiasili au za kisasa ambazo zitazuia kuota kwa kuvu. (2) Njia sahihi zitakazotumika kuhifadhi mazao ni pamoja na matumizi ya- (a) mifuko isiyopitisha hewa; (b) magunia ya kawaida kwa ajili ya mazao yaliyowekwa viuatilifu; (c) kihenge na kichanja bora cha asili; (d) silo au pipa maalum; (e) ghala bora lililo safi; (f) kutumia viuatilifu kwenye mazao kwa kuzingatia ushauri wa kitaalam; au (g) njia nyingine kadiri itakavyoshauriwa na wataalamu. Wajibu wa Halmashauri - 11 Verify source ↗
(1) Halmashauri, katika utekelezaji wa
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima ichukue hatua kadhaa za kusaidia uzalishaji, uhifadhi, mafunzo, na masoko ya mazao, na inaweza kumteua Afisa Mwidhiniwa kusimamia utekelezaji.
11.-(1) Halmashauri, katika utekelezaji wa Sheria Ndogo hizi itakuwa na wajibu wa- (a) kuhamasisha na kutoa elimu ya uzalishaji na usimamizi wa mazao; (b) kuhamasisha uhifadhi wa mazao katika ili kuepuka eneo au mahala salama uchafuzi wa sumukuvu; (c) kuweka mazingira wezeshi ya upatikanaji wa pembejeo za kilimo; (d) kutunza kumbukumbu za mashamba yote ya mazao ya kilimo katika Kata na Vijiji ili kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hizi; (e) kuanzisha, kuendeleza mashamba darasa na vituo maalum kwa ajili ya kutolea mafunzo ya udhibiti wa sumukuvu; (f) kuanzisha na kuhamasisha wakulima na sehemu za wadau wengine kujenga kuhifadhia mazao; na (g) kuandaa uwepo wa vituo maalum vya 4 Sheria Ndogo za (Kuzuia Na Kudhibiti Sumukuvu) Halmashauri ya Wilaya ya Newala Tangazo La Serikali Na. 464 (Linaendelea) kuuza na kununua mazao. (1), Halmashauri (2) Bila ya kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya inaweza kumteua Afisa Mwidhiniwa kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hizi. Wajibu wa mkulima
Part
sehemu za
- 12 Verify source ↗
Kila mkulima atakuwa na wajibu wa
AI-assisted research summary: Kila mkulima lazima afanye kilimo kwa kanuni bora, awajulishe Halmashauri dalili za kuvu kwenye mazao, na ahudhurie mafunzo ya kudhibiti sumukuvu na kutumia alichojifunza.
12. Kila mkulima atakuwa na wajibu wa- (a) kufanya shughuli za kilimo kwa kuzingatia kanuni bora za kilimo na usimamizi wa mazao, kabla na baada ya kuvuna; (b) kutoa taarifa kwa Halmashauri kuhusu uwepo wa dalili za kuvu katika mazao; na (c) kushiriki mafunzo yaliyoandaliwa na Halmashauri ya kudhibiti sumukuvu na kutekeleza ujuzi uliopatikana kwenye mafunzo hayo. Wajibu wa msafirishaji Wajibu wa mfanyabiashara - 13 Verify source ↗
Mtu anayesafirisha mazao atapaswa
AI-assisted research summary: Mtu anayesafirisha mazao lazima ahakikishe vifungashio na vifaa vya kusafirisha mazao ni vikavu au vinazuia maji, unyevu, na vumbi kuingia.
13. Mtu anayesafirisha mazao atapaswa kuhakikisha vifungashio na vifaa anavyotumia kusafirisha mazao ni vikavu au visivyoruhusu maji au unyevu na vumbi kuingia ndani ili kuepusha kuvu kuota kwenye mazao. - 14 Verify source ↗
Kila mfanyabiashara wa mazao atakuwa na
AI-assisted research summary: Mfanyabiashara wa mazao lazima ahakikishe mazao anayohifadhi, kuyasafirisha, au kuyauza hayana viashiria vya sumukuvu kulingana na Jedwali la Kwanza.
14. Kila mfanyabiashara wa mazao atakuwa na wajibu wa kuhakikisha anahifadhi, anasafirisha au kuuza mazao ambayo hayana viashiria vya uwepo wa sumukuvu kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Kwanza. ananunua, Wajibu wa msindikaji
Part
Jedwali la Kwanza.
- 15 Verify source ↗
Kila msindikaji atakuwa na wajibu wa
AI-assisted research summary: Kila msindikaji lazima asindike mazao yasiyoonyesha viashiria vya uwepo wa sumukuvu kulingana na Jedwali la Kwanza.
15. Kila msindikaji atakuwa na wajibu wa kusindika mazao ambayo hayana viashiria vya uwepo wa sumukuvu kama inanyoonekana katika Jedwali la Kwanza. Makosa na adhabu - 16 Verify source ↗
Mtu ambaye
AI-assisted research summary: Mtu anayefanya vitendo vilivyoorodheshwa kuhusu mazao—kama kuchelewa kuvuna, kukausha vibaya, kuuza au kutumia mazao yenye viashiria vya sumukuvu—anatenda kosa.
16. Mtu ambaye- (a) atashindwa kuandaa, kupanda, kutunza shamba na mazao kwa usahihi; (b) atashindwa kuvuna kwa wakati mara baada ya mazao kukomaa; (c) atachelewa kuondoa mazao shambani 5 Sheria Ndogo za (Kuzuia Na Kudhibiti Sumukuvu) Halmashauri ya Wilaya ya Newala Tangazo La Serikali Na. 464 (Linaendelea) baada ya kuvuna; (d) ataanika kwenye udongo, vumbi au mchanga; (e) atakausha mazao katika mazingira yanayoweza kusababisha sumukuvu; viuatilifu (f) atatumia vilivyozuiliwa kutumika kwenye mazao; (g) atauza mazao yenye viashiria vya sumukuvu. (h) atasafirisha njia mazao zitakazosababisha mazingira ya kuvu kuota; kwa (i) atatumia mazao yenye viashiria vya sumukuvu wakati wa usindikaji; au (j) atatenda jambo lolote lililokatazwa na Sheria Ndogo hizi, anatenda kosa na akitiwa hatiani atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi elfu hamsini na isiyozidi Shilingi laki tatu au kifungo kwa kipindi kisichozidi miezi kumi na miwili, au vyote kwa pamoja. - 17 Verify source ↗
Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa ikiwa mkosaji anakiri kosa kwa hiari kwa maandishi na kujaza fomu maalum ya Jedwali la Pili, kwa mujibu wa kifungu cha 158.
17. Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha kosa kwa mujibu wa masharti ya kifungu cha 158 cha Sheria, iwapo mkosaji atakiri kosa kwa hiari yake mwenyewe kwa maandishi kwa kujaza fomu maalum iliyoambatishwa kwenye Jedwali la Pili. Ufifilishaji wa makosa 6 Sheria Ndogo za (Kuzuia Na Kudhibiti Sumukuvu) Halmashauri ya Wilaya ya Newala Tangazo La Serikali Na. 464 (Linaendelea) ______________ JEDWALI LA KWANZA ______________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 14 na 15) Na.
Part
JEDWALI LA KWANZA
- 1 Verify source ↗
Section 1
AI-assisted research summary: The text appears to describe maize and signs of mould or moisture in the kernels.
1. Aina ya Mazao Mahindi VIASHIRIA VYA SUMUKUVU Hali ya Unyevu au Kuvu Punje kuwa na unyevu - 2 Verify source ↗
Section 2
AI-assisted research summary: Hii ni fomu ya kukiri kosa kwa hiari mbele ya Mkurugenzi, na inaonyesha kwamba mtu anaweza kukubali kulipa ushuru na faini badala ya kupelekwa mahakamani.
2. Karanga Punje kuwa na unyevu Mwonekano wa Punje Punje kuwa na ukungu au kuvu - rangi kahawia au nyeusi au kijani au njano kuwa na harufu ya uvundo Punje kuwa na ukungu au kuvu – rangi kahawia au nyeusi au kijani au njano kuwa na harufu ya uvundo ____________ JEDWALI LA PILI _____________ (Limetengenezwa chini ya Kanuni ya 17) FOMU YA KUKIRI NA KUFIFILISHA KOSA Mimi…………………………………………. nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya …………………………………………………ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Newala, kwamba mnamo tarehe ………mwezi………. mwaka………. nilitenda kosa la kukiuka masharti ya Aya ya ……………. ya Sheria Ndogo ya (KUZUIA NA KUDHIBITI SUMUKUVU) ya Halmashauri ya Wilaya ya Newala ya mwaka 2024. Kwa mamlaka aliyopewa Mkurugenzi wa Halamashauri ya Wilaya ya Newala, Niko tayari kulipa ushuru na kiasi cha faini nitakayokuwa nadaiwa badala ya kupelekwa Mahakamani. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI KWELI NA NINAYATOA KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU Leo tarehe………………ya Mwezi…………………. Mwaka………………… Jina………………………………………..……………Saini………………………………… Mbele ya: Jina…………………….……………………………...Cheo……………………………………. Saini…………………………………………………Tarehe…………………………………… 7 Sheria Ndogo za (Kuzuia Na Kudhibiti Sumukuvu) Halmashauri ya Wilaya ya Newala Tangazo La Serikali Na. 464 (Linaendelea) Nembo ya Halmashauri ya Wilaya ya Mafia imegongwa kwenye Sheria Ndogo hii kufuatia azimio lililopitishwa katika mkutano wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya Mafia uliofanyika tarehe 31 mwezi 05 Mwaka 2022 na kushuhudiwa Lakari hiyo ikigongwa mbele ya:- KASSIM SEIF NDUMBO Mkugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya mafia JUMA SALUM ALLY Mwenyekiti wa Halmashauri Halmashauri ya Wilaya Mafia NAKUBALI, / L.S Dodoma, MOHAMED OMARY MCHENGERWA (MB) 25 Machi, 2024 Waziri wa Nchi – Ofisi ya Rais (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa) 8
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo za (Kuzuia na Kudhibiti Sumukuvu) Halmashauri ya Wilaya ya Newala za Mwaka 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in