Sheria Ndogo za (Afya na Usafi wa Mazingira) Halmashauri ya Wilaya ya Mafia za Mwaka 2024
This section states the name of the by-laws.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo za (Afya na Usafi wa Mazingira) Halmashauri ya Wilaya ya Mafia za Mwaka 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This section states the name of the by-laws. These by-laws apply throughout the area under the Mafia District Council’s authority. This section defines key terms used in the by-laws, including fees, authorized officers, health, food, water sources, toilets, nuisance, the council, households, noise, permits, waste, wastewater facilities, residents, wastewater, and solid waste. Mkazi anayemiliki nyumba, kiwanja, au biashara lazima aweke eneo lake safi, aondoe taka kwa njia ya Halmashauri, ajenge shimo la taka na choo kinachofaa, na ahakikishe hakuna mazalia ya wadudu hatarishi. Owners of houses, factories, or business wastewater areas must have a wastewater holding pit, empty it when full, and not discharge wastewater onto roads, alleys, rivers, water sources, open areas, storm drains, or other places not set aside for wastewater storage.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo za (Afya na Usafi wa Mazingira) Halmashauri ya Wilaya ya Mafia za Mwaka 2024
Showing 43 of 43
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hizi zitajulikana kama Sheria
AI-assisted research summary: This section states the name of the by-laws.
1. Sheria Ndogo hizi zitajulikana kama Sheria Ndogo za (Afya na Usafi wa Mazingira) Halmashauri ya Wilaya ya Mafia za Mwaka 2024. - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hizi zitatumika katika eneo lote
AI-assisted research summary: These by-laws apply throughout the area under the Mafia District Council’s authority.
2. Sheria Ndogo hizi zitatumika katika eneo lote lililo chini ya Mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya ya Mafia. - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hizi isipokuwa kama
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the by-laws, including fees, authorized officers, health, food, water sources, toilets, nuisance, the council, households, noise, permits, waste, wastewater facilities, residents, wastewater, and solid waste.
3. Katika Sheria Ndogo hizi isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “ada” maana ni yake ni malipo yanayolipwa kwa Halmashauri kwa ajili ya huduma ya kuzoa taka; “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni Afisa yeyote aliyeteuliwa kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hizi; “afya” maana yake hali timilifu ya kimwili, kiakili na kijamii na wala sio tu kutokuwa na ugonjwa au ulemavu; chakula” maana yake ni kitu kinacholiwa au kunywewa na binadamu isipokuwa madawa; “chanzo cha maji” maana yake ni eneo lolote ambalo limetengwa kwa ajili ya kuwa chanzo cha maji kwa matumizi ya jamii ikiwemo visima, mito, yote chemchemi, maeneo vijito, na 1 Sheria Ndogo za (Afya Na Usafi wa Mazingira) Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Tangazo La Serikali Na. 465 (Linaendelea) yanayopatikana maji; “choo bora” maana yake ni choo chochote cha maji chenye sakafu inayosafishika, banda imara la kudumu, limeezekwa, lina mlango imara, bomba la kutolea hewa chafu na lenye mfuniko kwenye tundu la choo na shimo salama na safi kwa ajili ya kutupa kinyesi na mkojo wa binadamu, lililojengwa kwa vifaa vya kudumu; “chukizo au kero” maana yake ni kitu ambacho kipo katika hali yoyote iwe kinatumika, kimewekwa, kimejengwa, au ni kichafu kiasi cha kusababisha: (a) hatari kwa viumbe na maisha ya binadamu; (b) harufu mbaya au harufu ya kuudhi au kuleta kinyaa; (c) kuzaliana kwa wadudu hatari kama vile inzi, mende, sisimizi, panya, nyoka, nyuki, kunguni au viumbe wengine hatari; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Mafia; “kaya” maana yake mtu mzima anayejitegemea mwanamke au mwanaume, na mtoto au watoto inayoishi aidha kwenye nyumba nzima au ndani ya chumba kimoja kwenye eneo la Halmashauri; “kelele” maana yake ni kero isababishwayo na sauti ambayo kwa asili inakataliwa au ile ambayo inaweza kusababisha athari mbaya kwa afya ya binadamu au mazingira; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia au Afisa yeyote ya atakayeteuliwa Mkurugenzi; kutekeleza majukumu “kizimba cha “kibali” maana yake ni idhini ya maandishi inayotolewa na Halmashauri kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii; taka” maana yake ni eneo maalum lililotengwa na Halmashauri kwa ajili ya kuhifadhi taka ngumu; “kituo cha maji machafu” maana yake ni sehemu maalumu iliyotengenezwa kwa ajili ya ukaguzi wa mfereji ambao una mfuniko usioruhusu hewa kutoka; “kuchakata taka” maana yake ni kuzichambua, 2 Sheria Ndogo za (Afya Na Usafi wa Mazingira) Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Tangazo La Serikali Na. 465 (Linaendelea) kuzitenganisha na kuzibadili kuwa kitu kingine chenye manufaa kwa jamii; “mabwawa ya maji taka” maana yake ni mabwawa yaliyojengwa kwa madhumuni ya kuhifadhi na kutakasa maji taka yanayotokana na kuosha vyombo, kutoka vyooni, kutoka bafuni, kufua nguo, kuosha nywele au shughuli zozote za nyumbani na viwanda; “mkazi” maana yake ni mtu yeyote ambaye kwa kawaida anaishi kwenye eneo lililoko chini ya mamlaka ya Halmashauri na ambaye ama ana kaya au anaishi katika kaya au taasisi iliyopo katika eneo la Halmashauri; “maji taka” maana yake ni ile iliyoanishwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; “taka” maana yake ni ile iliyoanishwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; “taka ngumu” Maana yake ni ile iliyoainishwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira. - 4 Verify source ↗
Itakuwa ni wajibu wa kila mkazi anayemiliki
AI-assisted research summary: Mkazi anayemiliki nyumba, kiwanja, au biashara lazima aweke eneo lake safi, aondoe taka kwa njia ya Halmashauri, ajenge shimo la taka na choo kinachofaa, na ahakikishe hakuna mazalia ya wadudu hatarishi.
4. Itakuwa ni wajibu wa kila mkazi anayemiliki la nyumba, kiwanja au biashara kuhakikisha eneo kwamba- (a) mazingira yanayozunguka eneo lake yanakuwa safi wakati wote; (b) taka zote zinakusanywa na kufukiwa au kuondolewa kwa njia itakayoelekezwa na Halmashauri; Sura 191 Sura 191 Sura 191 Wajibu wa kufanya usafi wa mazingira (d) anajenga (c) anachimba shimo la kutupia taka litakalokuwa na urefu usiopungua kimo cha futi 3 na upana usiopungua futi 2; choo kudumu imara kilichojengwa kwa matofali na kuezekwa kwa bati, tembe, majani, vigae chenye mlango unaofunga na kufunguka na kuhakikisha kwamba choo kinatumika wakati wote na kuwe na chombo cha maji tiririka na sabuni ya kunawa mikono; cha (e) eneo lake halina mazalia ya mbu, panya na wadudu wengine hatarishi. Uhifadhi wa - 5 Verify source ↗
Kila mmiliki wa nyumba, kiwanda au eneo la
AI-assisted research summary: Owners of houses, factories, or business wastewater areas must have a wastewater holding pit, empty it when full, and not discharge wastewater onto roads, alleys, rivers, water sources, open areas, storm drains, or other places not set aside for wastewater storage.
5. Kila mmiliki wa nyumba, kiwanda au eneo la 3 Sheria Ndogo za (Afya Na Usafi wa Mazingira) Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Tangazo La Serikali Na. 465 (Linaendelea) maji taka biashara atatakiwa- (a) kuhakikisha kuwa analo karo la kuhifadhi maji taka; (b) kunyonya maji taka pale karo linapojaa; na (c) kutotiririsha au kutoelekeza maji kutoka vyooni, bafuni, karoni au viwandani kwenda barabarani, uchochoroni, mtoni, kwenye vyanzo vya maji, maeneo ya wazi, kwenye mfereji wa maji ya mvua au sehemu yoyote isiyotengwa kuhifadhia maji taka. Utengenezaji na uuzaji wa vyakula - 6 Verify source ↗
Mtu anayetengeneza, kuchoma, kupika,
AI-assisted research summary: A person who makes, burns, cooks, boils, or sells food in the council area must comply with the health conditions and regulations made under the law and these by-laws.
6. Mtu anayetengeneza, kuchoma, kupika, kuchemsha au kuuza chakula cha aina yoyote katika eneo la Halmashauri atatakiwa kutimiza masharti na kanuni za afya zilizowekwa kwa mujibu wa Sheria na Sheria Ndogo hizi. Ada ya ukaguzi wa kiafya Upimaji wa afya Ada ya kuzoai taka - 7 Verify source ↗
Kutakuwa na ada ya ukaguzi wa kiafya na
AI-assisted research summary: A health inspection fee is payable by the owner or operator of the listed business and service premises.
7. Kutakuwa na ada ya ukaguzi wa kiafya na italipwa na mmiliki au mhudumu katika majengo ya biashara, vituo vya afya na zahanati za watu binafsi, famasi au maduka ya madawa, hoteli, migahawa, mama au baba lishe, watoa tiba asili, majengo ya biashara na kama na maeneo mengine vioski ilivyoainishwa katika katika Jedwali la Kwanza. (groceries) - 8 Verify source ↗
Itakuwa ni wajibu wa kila mhudumu wa hoteli,
AI-assisted research summary: Wahudumu wa hoteli, migahawa, baa, nyumba za kulala wageni, bucha, waoka mikate, na wauzaji wa vyakula vilivyopikwa lazima wapime afya zao kila baada ya miezi sita.
8. Itakuwa ni wajibu wa kila mhudumu wa hoteli, migahawa, baa, nyumba za kulala wageni, bucha, waoka mikate, au watu wanaoshughulika na kuuza vyakula vilivyopikwa kuhakikisha kwamba wanapima afya zao kila baada ya miezi sita. - 9 Verify source ↗
(1) Kutakuwa na ada ya uzoaji taka ambayo
AI-assisted research summary: Halmashauri must charge a waste collection fee, and the fee must be paid monthly on the 28th to the authorised officer, who must issue an electronic receipt and record it in the waste producers register.
9.-(1) Kutakuwa na ada ya uzoaji taka ambayo itatozwa na Halmashauri kwa lengo la kufanikisha utekelezaji wa shughuli za usimamizi wa mazingira kama ilivyoainishwa kwenye Jedwali la Pili. (2) Ada ya uzoaji taka italipwa tarehe ishirini na nane ya kila mwezi na italipwa kwa Afisa Mwidhiniwa ambaye atatoa stakabadhi ya malipo kwa njia ya kieletroniki na atajaza katika rejista ya wazalishaji taka. (3) Iwapo mzalishaji wa taka atashindwa kulipia gharama ya huduma ya uzoaji taka kwa kipindi cha miezi 4 Sheria Ndogo za (Afya Na Usafi wa Mazingira) Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Tangazo La Serikali Na. 465 (Linaendelea) miwili mfululizo, Halmashauri itamchukulia hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani. Mamlaka ya Afisa Mwidhiniwa Vifaa vya kuhifadhi taka ngumu Ukusanyaji taka ngumu eneo - 10 Verify source ↗
Afisa Mwidhiniwa atakuwa na mamlaka ya
AI-assisted research summary: Afisa Mwidhiniwa ana mamlaka ya kuingia maeneo ya Halmashauri wakati wa saa zilizotajwa na kutoa ushauri au maelekezo kuhusu kutokukaa katika jengo hatarishi.
10. Afisa Mwidhiniwa atakuwa na mamlaka ya- (a) kuingia katika lolote ndani ya Halmashauri kuanzia saa moja kamili asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni kwa lengo la kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hizi; na (b) kushauri au kuelekeza watu au mtu kutokuishi katika jengo ambalo linahatarisha afya au maisha ya watu na viumbe hai. - 11 Verify source ↗
(1) Kila mmliki wa jengo la makazi au
AI-assisted research summary: Wamiliki, wapangaji, na wafanyabiashara ndani ya Halmashauri lazima wawe na chombo cha taka chenye mfuniko na wakusanye taka katika maeneo yaliyotengwa; kwa nyumba zilizo katika ukanda wa kijani kwenye maeneo ambayo hayajapimwa, lazima kuwe na shimo kubwa la taka ngumu.
11.-(1) Kila mmliki wa jengo la makazi au mpangaji wa jengo la makazi au mtu yeyote anayefanyia biashara katika eneo lolote ndani ya Halmashauri atatakiwa kuwa na chombo cha kuhifadhia taka chenye mfuniko na atawajibika kukusanya taka hizo kwenye vizimba vya kuzolea taka katika maeneo yaliyoainishwa. (2) Kila mmiliki wa jengo au mpangaji wa nyumba iliyoko katika ukanda wa kijani, katika maeneo ambayo hayajapimwa atalazimika kuwa na shimo kubwa la kukusanyia taka ngumu katika eneo lake. - 12 Verify source ↗
(1) Halmashauri itawajibika kukusanya taka
AI-assisted research summary: The council must collect solid waste from designated bins in each ward, and people may not put liquid waste or explosive/harmful items into bins or burn/bury solid waste without council permission.
12.-(1) Halmashauri itawajibika kukusanya taka ngumu kutoka katika vizimba vya taka vilivyoainishwa katika kila kata. (2) Taka ngumu zote zitakazokusanywa kwenye mapipa ya taka zitabaki kuwa mali ya mkazi au mmliki wa eneo lile mpaka zitakapokuwa zimefikishwa kwenye kizimba cha taka au zitakapokuwa zimetolewa na Wakala kutoka katika eneo lake. (3) Haitaruhusiwa kwa mtu yeyote- (a) kuweka uchafu wenye asili ya maji maji taka au kitu chochote kusababisha la kulipuka na kwenye pipa kinachoweza madhara; na (b) kuchoma au kufukia taka ngumu bila kibali cha Halmashauri. Eneo la kutupa - 13 Verify source ↗
Halmashauri itakuwa na wajibu wa
AI-assisted research summary: Halmashauri must set aside a designated waste disposal area, provide special waste containers, and offer waste collection services for a fee.
13. Halmashauri itakuwa na wajibu wa- 5 Sheria Ndogo za (Afya Na Usafi wa Mazingira) Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Tangazo La Serikali Na. 465 (Linaendelea) taka (a) kutenga eneo maalum kwa ajili ya kutupia Udhibiti utupaji wa taka taka; (b) kuweka vyombo maalum vya kutunzia taka; na (c) kutoa huduma ya uzoaji taka kwa malipo kutoka kwa wazalishaji wa taka hadi kwenye dampo. - 14 Verify source ↗
(1) Watumiaji wa vyombo vya usafiri binafsi
AI-assisted research summary: Users of private or public transport must not throw rubbish outside the vehicle and must place all waste in the container inside the vehicle. People must not dump waste anywhere informal, and residents or other persons must use designated waste bins in designated areas.
14.-(1) Watumiaji wa vyombo vya usafiri binafsi au vya umma hawataruhusiwa kutupa taka nje ya vyombo hivyo, na taka zote zitatakiwa kuwekwa kwenye chombo cha kuhifadhia taka kilichomo kwenye chombo husika. (2) Mtu hataruhusiwa kutupa taka ovyo katika maeneo ya makazi, biashara, mifereji ya maji ya mvua, hifadhi ya barabara au mahali popote ambapo si rasmi kwa ajili ya kutupa taka. (3) Mtu au mkazi atakuwa na wajibu wa kuhakikisha kwamba anatupa uchafu au taka katika vyombo maalum vilivyowekwa kwa ajili ya kutunzia taka katika maeneo maalum yaliyotengwa. Udhibiti wa kelele kupita kiasi - 15 Verify source ↗
Mtu hataruhusiwi kusababisha au kufungulia
AI-assisted research summary: A person must not create or release excessive noise, including music, factory noise, a generator, or any other sound pollution, unless they have permission from the authorised officer.
15. Mtu hataruhusiwi kusababisha au kufungulia kwa kelele kupita kiasi iwe muziki, kelele za kiwanda, jenereta au kitu kingine chochote (sound pollution) bila kupata kibali cha Afisa Mwidhiniwa. Kutiririsha maji taka - 16 Verify source ↗
(1) Mtu hataruhusiwa kutiririsha au kumwaga
AI-assisted research summary: Mtu hapaswi kumwaga au kuachia maji taka barabarani, kwenye mifereji, mtoni, kwenye vyanzo vya maji, au sehemu isiyoruhusiwa; viwanda vinavyotoa maji taka na wamiliki wa nyumba wana wajibu wa kuchukua hatua za kuhifadhi na kushughulikia maji taka.
16.-(1) Mtu hataruhusiwa kutiririsha au kumwaga au kuruhusu au kusababisha kutiririsha au kumwaga maji taka barabarani, uchochoroni kwenye mifereji, mtoni, kwenye vyanzo vya maji au sehemu yoyote ambayo si rasmi kwa ajili ya kuhifadhi maji taka. (2) Kila kiwanda kinachozalisha maji taka kitakuwa na wajibu wa kuhakikisha kuwa kinaunganisha maji taka au kujenga mifereji na mabwawa kwa ajili ya kuhifadhi maji taka. (3) Kila mmiliki wa nyumba atatakiwa- (a) kuhakikisha kuwa ana karo la kuhifadhi maji taka na atawajibika kunyonya maji taka pale karo hilo linapojaa; na (b) itakuwa ni marufuku kwa mtu kuacha karo kujaa na kutiririsha maji taka barabarani au 6 Sheria Ndogo za (Afya Na Usafi wa Mazingira) Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Tangazo La Serikali Na. 465 (Linaendelea) Utengenezaji na uuzaji vyakula Uzuiaji wa shughuli wakati wa magonjwa ya mlipuko Ukamataji wakati wa zuio sehemu yoyote isiyoruhusiwa.
Part
sehemu yoyote isiyoruhusiwa.
- 17 Verify source ↗
(1) Mtu hataruhusiwa kutengeneza, kuchoma,
AI-assisted research summary: Mtu haruhusiwi kutengeneza, kupika, kuchemsha, kuchoma au kuuza chakula mahali popote au ndani ya nyumba kabla hajatimiza masharti ya afya yaliyowekwa na sheria. Mwendesha biashara ya vyakula vya kupikwa au kukaangwa lazima ahifadhi vyakula hivyo kwenye sanduku la mbao safi na lenye kioo ili kuzuia nzi, vumbi na wadudu.
17.-(1) Mtu hataruhusiwa kutengeneza, kuchoma, kupika, kuchemsha na kuuza chakula cha aina yoyote mahali popote au kwenye nyumba yoyote mpaka awe ametimiza masharti na kanuni za afya yaliyowekwa kwa mujibu wa sheria. (2) Kila mtu anayeendesha biashara ya vyakula vya kupikwa au kukaangwa atakuwa na wajibu wa kuhakikisha vyakula hivyo vinahifadhiwa kwenye sanduku lililotengenezwa kwa mbao safi na kuwekwa kioo kuzuia nzi, vumbi na wadudu waletao madhara kwa afya ya binadamu. - 18 Verify source ↗
Mkurugenzi anaweza kutoa amri ya kuzuia
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kuzuia shughuli fulani au shughuli yoyote ikiwa ana sababu ya kuamini zinaweza kueneza magonjwa ya mlipuko na kuathiri maisha ya binadamu.
18. Mkurugenzi anaweza kutoa amri ya kuzuia shughuli yoyote isifanyike kama vile utengenezaji wa vyakula, pombe, mijumuiko, sherehe na mikusanyiko yoyote kwa kutangaza kwa njia ya kipaza sauti, maandishi au kupitia vyombo vya habari endapo atakuwa na sababu ya kuamini kwamba shughuli hiyo inaweza kusababisha kuenea kwa magonjwa ya mlipuko na kuleta athari kwa maisha ya binadamu. - 19 Verify source ↗
(1) Halmashauri itakuwa na mamlaka ya
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kumkamata mtu anayekiuka amri ya zuio la uuzaji wa vyakula wakati wa mlipuko, na inaweza kuharibu au kuhifadhi vyakula vilivyokamatwa kulingana na aina yake.
19.-(1) Halmashauri itakuwa na mamlaka ya kumkamata mtu yeyote ambaye atakaidi amri ya zuio la kufanyika kwa shughuli ya uuzaji wa vyakula wakati wa magonjwa ya mlipuko. (2) Endapo mtu aliyekamatwa alikuwa anauza vyakula ambavyo vinaharibika kwa haraka, Halmashauri itaharibu vyakula hivyo. (3) Bila kuathiri kanuni ndogo ya (1) na (2), iwapo vyakula vilivyokamatwa vitakuwa haviharibiki kwa haraka, Halmashauri la kuvihifadhi hadi mwisho wa amri ya zuio. itakuwa na jukumu (4) Halmashauri haitahusika na gharama zozote zitakazotokea isipokuwa kama uharibifu huo utakuwa umesababishwa kwa uzembe wa Afisa wa Halmashauri. Wajibu wa mfanyabiashara wa bucha na maduka ya - 20 Verify source ↗
Kila mfanyabiashara wa bucha au duka la
AI-assisted research summary: Wafanyabiashara wa bucha au duka la nyama lazima wahakikishe wana leseni, vifaa na mazingira yanayohitajika, na wauze nyama tu katika bucha au maduka maalum.
20. Kila mfanyabiashara wa bucha au duka la nyama atatakiwa kuhakikisha kuwa- (a) ana leseni na vibali vya kufanya biashara hiyo; 7 Sheria Ndogo za (Afya Na Usafi wa Mazingira) Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Tangazo La Serikali Na. 465 (Linaendelea) nyama (b) kuna kabati la vioo la kuzuia nzi na wadudu wengine wataambao; (c) kuna pipa la kuhifadhia taka ngumu na laini; (d) kuna jokofu la kuhifadhia nyama; (e) jengo lake la biashara lina mwanga wa kutosha, umeme, maji safi na salama, visu, meza, mzani wa kawaida au mzani wa kielektroniki, na misumeno maalumu ya kukatia nyama; (f) nyama imekaguliwa mkaguzi aliyeidhinishwa na kugongwa muhuri na inauzwa ndani ya jengo; na Siku ya usafi (g) muuzaji anavaa sare nyeupe muda wote ambazo ni mabuti, koti na kofia; na (h) biashara ya nyama inafanyika katika bucha na maduka maalum na si vinginevyo. - 21 Verify source ↗
(1) Kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi
AI-assisted research summary: Kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi ni siku maalum ya usafi wa mazingira, na wakazi pamoja na watu wote wanatakiwa kushiriki au kuhakikisha maeneo yao yanakuwa safi.
21.-(1) Kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi itakuwa ni siku maalam ya kufanya usafi wa mazingira katika maeneo ya makazi na umma. (2) Itakuwa ni wajibu na lazima kwa kila mkazi katika kijiji na kitongoji kushiriki usafi wa mazingira kwa siku iliyopangwa na Halmashauri katika maeneo yao na maeneo ya umma. (3) Kila mtu atahakikisha eneo la makazi yake na vichochoro vilivyomzunguka, eneo analofanyia biashara, eneo la wazi lililokaribu naye kwa umbali wa mita kumi na eneo la mazingira ya ofisi ni safi kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizi. Wajibu wa kuwa na choo na kukitumia - 22 Verify source ↗
(1) Kila mmiliki wa nyumba au mpangaji
AI-assisted research summary: Mmiliki wa nyumba au mpangaji lazima ahakikishe nyumba ni salama kwa matumizi ya wakazi, ina choo safi, na ina sehemu ya kunawia mikono yenye maji safi na sabuni ya kimiminika.
22.-(1) Kila mmiliki wa nyumba au mpangaji atakuwa na wajibu wa kuhakikisha kwamba- ina choo safi, (a) nyumba yake imara kwa matumizi ya wakazi wa nyumba hiyo; (b) anaweka sehemu maalum ya kunawia mikono ikiwa na maji safi na sabuni maalum ya kimiminika. (2) Choo kinatakiwa kijengwe umbali wa mita sitini (60) kutoka chanzo chochote cha maji. Vyoo vya - 23 Verify source ↗
(1) Halmashauri inaweza kujenga choo cha
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kujenga choo cha umma au kuruhusu watu wengine wajenge vyoo vya umma mahali panapofaa, na vyoo hivyo vinapaswa kuwa vya kudumu na kuwa na vifaa vilivyotajwa.
23.-(1) Halmashauri inaweza kujenga choo cha 8 Sheria Ndogo za (Afya Na Usafi wa Mazingira) Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Tangazo La Serikali Na. 465 (Linaendelea) umma umma au kumruhusu mtu binafsi, vikundi vya watu au taasisi kujenga vyoo vya Umma katika maeneo ambayo Halmashauri itaona inafaa. (2) Vyoo vitakavyojengwa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii vitatakiwa viwe vya kudumu na- (a) vyenye matundu yasiyopungua mawili (2) kwa wanawake na mawili (2) kwa wanaume; (b) vyenye mfumo madhubuti wa maji na uwepo wa maji ya kutosha yaliyo safi na salama; (c) kuwepo na chombo cha kuhifadhia maji ya akiba; (d) kuwepo kwa bafu ya wanaume na wanawake; (e) kuwepo na chumba maalum cha kuvutia sigara; (f) kuwepo na sehemu ya haja ndogo kwa wanaume; na (g) kuwepo na chombo maalumu chenye mfuniko cha kuhifadhia taka zisizoweza kusukumwa na maji; Vyoo vya muda katika mikusanyiko - 24 Verify source ↗
Ni wajibu wa mtu yeyote, kikundi au taasisi
AI-assisted research summary: Watu, vikundi au taasisi zinazoandaa mkutano, sherehe au mkusanyiko lazima ziweke vyoo vya muda ikiwa eneo halina vya kudumu, na pia ziombe idhini kutoka Halmashauri.
24. Ni wajibu wa mtu yeyote, kikundi au taasisi yoyote yenye lengo la kukusanya watu kwa madhumuni ya mkutano au sherehe au mkusanyiko wowote, kuweka au kujenga vyoo vya muda endapo eneo hilo hakuna vyoo vya kudumu na atatakiwa kuomba idhini kutoka Halmashauri. Ilani ya kujenga au kurekebisha choo Ilani ya kuondoa kero - 25 Verify source ↗
Afisa Mwidhiniwa atafanya ukaguzi wa afya
AI-assisted research summary: Afisa Mwidhiniwa hufanya ukaguzi wa afya na, akigundua nyumba haina choo au choo hakifai, hutoa ilani kwa mmiliki au mpangaji.
25. Afisa Mwidhiniwa atafanya ukaguzi wa afya na iwapo katika ukaguzi huo itagundulika kuwa nyumba yoyote haina choo au choo kilichopo kimejaa au hakifai kwa matumizi ya binadamu, Afisa Mwidhiniwa atatoa ilani kwa mmiliki wa nyumba au mpangaji akiainisha masharti ya kurekebisha hali hiyo kama ilivyoainishwa kwenye Jedwali la Tatu. - 26 Verify source ↗
(1) Katika ukaguzi afya, Afisa Mwidhiniwa
AI-assisted research summary: Ikiwa Afisa Mwidhiniwa atakuta kero wakati wa ukaguzi wa afya, lazima atoe ilani ndani ya siku 7 kwa mmiliki, mpangaji, mtumiaji au mtu mwingine anayehusika, akitakiwa kuiondoa kulingana na Jedwali la Nne.
26.-(1) Katika ukaguzi afya, Afisa Mwidhiniwa akigundua kuwa eneo alilokagua lina kero yoyote atatoa ilani ndani ya siku saba (7) kwa mmiliki wa nyumba, mpangaji, mtumiaji au mtu yeyote anayehusika, akimtaka kuondoa kero hiyo kama ilivyoainishwa kwenye Jedwali la Nne. 9 Sheria Ndogo za (Afya Na Usafi wa Mazingira) Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Tangazo La Serikali Na. 465 (Linaendelea) Vikundi vya usafi Wajibu wa mfugaji (2) Mtu atakayeshindwa kutekeleza masharti ya ilani aliyopewa ndani ya muda ulioainishwa kwenye ilani atakuwa anatenda kosa. - 27 Verify source ↗
Halmashauri itahamasisha uundaji wa ikundi
AI-assisted research summary: Halmashauri must encourage the formation and recognition of community groups so they can handle solid waste control and environmental cleanliness in streets, after contracting with the Halmashauri.
27. Halmashauri itahamasisha uundaji wa ikundi Jamii na kuvitambua ili kuviwezesha kufanya shughuli za udhibiti wa taka ngumu pamoja na usafi wa mazingira katika mitaa, baada ya kuingia mkataba na Halmashauri. - 28 Verify source ↗
Kila mfugaji chini ya Sheria Ndogo hizi
AI-assisted research summary: Kila mfugaji lazima atimize masharti ya kusimamia mifugo yake kama yalivyoorodheshwa katika kifungu hiki.
28. Kila mfugaji chini ya Sheria Ndogo hizi atatakiwa- (a) kupitisha mfugo au mifugo yake katika njia zilizopangwa na kutengwa na Halmashauri; (b) kufuga na kulisha mifugo katika maeneo ya malisho yaliyopangwa na Halmashauri; (c) kuwa na kadi ya mfugo au mifugo idadi na aina ya mifugo itakayoonyesha aliyonayo; (d) kuchangia gharama za ukarabati wa josho kama sehemu ya mchango wake, pale itakapobidi kufanya hivyo, na kwa gharama itakayopendekezwa na Halmashauri; (e) kupeleka mfugo au mifugo yake katika vituo vya na Halmashauri, na atalipia chanjo hiyo kama atatakiwa kufanya hivyo; itakavyoamriwa chanjo kama (f) kuchangia gharama za uboreshaji wa maeneo ya malisho yaliyotengwa na Halmashauri; (g) kuweka alama kwenye mfugo au mifugo yake na katika viungo vya mfugo au mifugo vinavyopendekezwa na mamlaka husika ili kutoharibu zao la ngozi; (h) kupeleka mfugo au mifugo katika josho kama atakavyoagizwa na Halmashauri. Kudhibiti mifugo inayozurura ovyo - 29 Verify source ↗
(1) Halmashauri itakamata mfugo au mifugo
AI-assisted research summary: Halmashauri must capture livestock found roaming in the area, may auction unclaimed livestock after 7 days with court approval, and must notify the owner and the public before sale.
29.-(1) Halmashauri itakamata mfugo au mifugo yoyote itakayoonekana inazurura ovyo katika eneo la Halmashauri. (2) Mfugo wowote utakaokamatwa mahali pasipostahili utatozwa faini kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Tano. 10 Sheria Ndogo za (Afya Na Usafi wa Mazingira) Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Tangazo La Serikali Na. 465 (Linaendelea) (3) Endapo mfugo uliokamatwa hautachukuliwa na mmiliki ndani ya kipindi cha siku saba (7) tangu kukamatwa, Halmashauri itakuwa na haki ya kuuza kwa mnada mfugo huo baada ya kupata idhini ya Mahakama, na fedha zitakazopatikana zitarejeshwa kwa mmliki wa mfugo huo baada ya kutoa faini inayodaiwa, gharama za kuhifadhi mfugo, gharama ya Mahakama na gharama ya mnada. (4) Bila kuathiri kanuni ndogo ya (3), Halmashauri kabla ya kuuza mfugo huo kwa mnada, itamjulisha mmliki na umma juu ya kusudio hilo. na (5) Endapo kutatokea kufa kwa mfugo au mifugo kutokana ile, Halmashauri yoyote haitawajibika na ulipaji wa gharama zozote isipokuwa kama vifo hivyo vimesababishwa na uzembe wa watumishi wa Halmashauri. sababu Marufuku
Part
Jedwali la Tano.
- 30 Verify source ↗
Ni marufuku
AI-assisted research summary: Section 30 inakataza vitendo kadhaa vya uchafuzi, uendeshaji wa biashara fulani bila leseni, na shughuli nyingine za hatari au zisizoidhinishwa.
30. Ni marufuku- (a) kwa mtu yeyote kuendesha biashara ya upulizaji dawa au biashara ya kuua wadudu au wanyama waharibifu katika nyumba yoyote au mahali popote bila cheti cha taaluma kinachotambuliwa na Serikali na leseni kutoka Halmashauri; (b) kwa mfanyabiashara yeyote kupanga bidhaa nje ya jengo lake la biashara au barabarani au vichochoroni au katika eneo lolote ambalo halikuidhinishwa kwa ajili ya shughuli hiyo; (c) kwa mtu yeyote kutupa taka za aina yoyote barabarani au eneo lolote la wazi au kwenye vichochoro au kwenye chanzo chochote cha maji ambalo halikutengwa kwa ajili ya shughuli hiyo; (d) kwa mtu yeyote aliye ndani ya gari kudondosha taka ngumu nje ya gari likiwa ndani au nje ya kituo cha magari na sehemu yoyote ile ambapo gari hilo linapita; katika lolote eneo au (e) kwa mtu yeyote kuweka kitu chochote kwenye maji taka ambacho kinaweza kuathiri mtu yeyote au kuharibu mfumo wa tiba ya maji taka au kinachoweza kusababisha kuzuia 11 Sheria Ndogo za (Afya Na Usafi wa Mazingira) Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Tangazo La Serikali Na. 465 (Linaendelea) mtiririko wa maji taka; (f) kwa mtu yeyote kulima kilimo cha matuta yanayosababisha maji kutuama ndani ya eneo la katikati ya mji; (g) kuchimba mchanga au kokoto au mawe katika vyanzo vya maji au mito barabarani; (h) kuchafua au kuoga au kufulia au kuvuruga maji yanayotumika kwa ajili ya matumizi ya binadamu au wanyama; (i) kuuza mchanga au kokoto na mawe kandokando mwa barabara; (j) kufanya biashara ya pombe ya aina yoyote katika nyumba au kwenye maeneo ya akiba za barabara au mitaani; (k) kuuza matunda au bidhaa nyingine za vyakula barabarani au kuanzisha masoko au magenge ya kuuzia matunda au vyakula au biashara nyingine ndogo bila ruhusa ya Halmashauri; (l) kuunganisha bomba la taka vimiminika katika mifereji ya maji ya mvua; (m) kufungulia au kutiririsha maji ya choo au taka vimiminika katika mkondo asili wa maji ya mvua au barabara au mfereji wa barabara wa maji ya mvua; (n) kujisaidia haja ndogo au haja kubwa barabarani au mitaani au sehemu yoyote isiyokusudiwa kwa madhumuni hayo; ya (o) kufanya mikusanyiko au kiutamaduni au kijamii wakati wa milipuko ya magonjwa ya kuambukiza, isipokuwa kwa ruhusa maalum ya Halmashauri na usimamizi wa Afisa Afya; na kidini (p) kuweka uchafu wenye asili ya maji maji taka au kitu chochote kusababisha la kulipuka na kwenye pipa kinachoweza madhara. Makosa - 31 Verify source ↗
Itakuwa ni kosa chini ya Sheria Ndogo hizi
AI-assisted research summary: Section 31 makes it an offence for any person to carry out listed sanitation, waste, food-vending, toilet, and vehicle-washing activities contrary to the by-laws or without Council permission.
31. Itakuwa ni kosa chini ya Sheria Ndogo hizi kwa mtu yeyote- (a) kujenga choo chini ya umbali wa mita 60 kutoka kisimani, bwawani, mtoni, au chanzo 12 Sheria Ndogo za (Afya Na Usafi wa Mazingira) Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Tangazo La Serikali Na. 465 (Linaendelea) kingine cha maji yanayotumika, kwa matumizi ya binadamu; (b) kutoa kinyesi au kusababisha kinyesi, mkojo, maji machafu, yenye kinyesi kutoka kwenye choo chake au bafu lake au karo la kuoshea vyombo au nguo au kutoka kwenye bomba lolote na kuyatitirisha kwenye barabara, mitaa, au kwenye mifereji ya maji ya mvua, au mfereji wowote uliowazi; linalochukua maji machafu (c) kutupa taka au kusababisha mtu mwingine atupe taka mahali popote pasiporuhusiwa na Halmashauri; (d) kutolipa ada ya taka kwa miezi miwili mfululizo; (e) kutembeza vyakula mitaani bila kibali cha Halmashauri; (f) kutokuwa na pipa la taka lenye mfuniko katika eneo la biashara; (g) kutokuwa na choo au kukutwa na choo kibovu au kilichojaa; (h) kukutwa na shimo la maji taka lililojaa au ambalo halina mfuniko; (i) kutokuwa na chombo maalum cha kukusanyia taka ndani ya gari la abiria; na (j) atafanya biashara ya kuosha gari, pikipiki au mtambo wowote katika eneo la makazi, eneo la wazi au eneo ambalo si rasmi kwa kufanya shughuli hiyo au kuruhusu eneo lake kutumika kwa shughuli za kuosha vyombo vya moto katika maeneo ambayo hayakutengwa kwa shughuli hizo bila kupata kibali rasmi kutoka Halmashauri; Adhabu - 32 Verify source ↗
Mtu atakayekiuka masharti ya Sheria Ndogo
AI-assisted research summary: A person who breaches these by-laws commits an offence and, if convicted, may be fined, imprisoned, or both.
32. Mtu atakayekiuka masharti ya Sheria Ndogo hizi atakuwa anatenda kosa na akitiwa hatiani atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi elfu hamsini na isiyozidi shilingi laki tatu au kifungo kisichozidi miezi kumi na mbili, au vyote kwa pamoja. Ufifilishaji wa - 33 Verify source ↗
Mkurugenzi
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa fulani ikiwa mkosaji anakiri kosa kwa hiari kwa maandishi, anajaza fomu maalum, na analipa ada au ushuru unaodaiwa.
33. Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa 13 Sheria Ndogo za (Afya Na Usafi wa Mazingira) Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Tangazo La Serikali Na. 465 (Linaendelea) makosa lililoainishwa kwenye Sheria Ndogo hizi kwa mujibu wa masharti ya kifungu cha 158 cha Sheria, iwapo mkosaji atakiri kosa kwa hiari yake mwenyewe kwa maandishi kwa kujaza fomu maalum iliyoambatishwa kwenye Jedwali la Sita na kulipa ada au ushuru anaodaiwa. 14 Sheria Ndogo za (Afya Na Usafi wa Mazingira) Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Tangazo La Serikali Na. 465 (Linaendelea) _______________ JEDWALI LA KWANZA _______________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 7) NA. AINA YA BIASHARA ADA KWA MWAKA ADA YA UKAGUZI WA AFYA 1 2 3 4 5 6 7 8 Baa na maduka ya vinywaji (groceries), bucha Migahawa na mama lishe Nyumba za wageni (Guest House) na hoteli Kumbi za starehe au mikutano Ukaguzi wa mitambo, maeneo ya madini ikiwemo ya ujenzi Majengo mengine ya biashara Viwanda vikubwa Viwanda vidogo Hoteli za kitalii (TZS) 5,000/= 2,000/= 10,000/= 10,000/= 30,000/= 7,000/= 100,000/= 20,000/= 100,000/= 15 Sheria Ndogo za (Afya Na Usafi wa Mazingira) Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Tangazo La Serikali Na. 465 (Linaendelea) ___________ JEDWALI LA PILI ___________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 9(1)) ADA YA UZOAJI TAKA KATIKA MAJENGO NA MAENEO MENGINE NA. ENEO ADA KWA MWEZI Kaya moja Maduka la rejareja Mashine ya kukamua mauta ya nazi Maduka la jumla Migahawa (Restaurant) Mashine za kukoboa/kusaga Vilabu vya pombe za kienyeji, baa, grocery Mama lishe/Baba lishe, nyama choma/chipsi inayojitegemea (TZS) 1,000/= 3,000/= 5,000/= 5,000/= 3,000/= 5,000/= 5,000/= 3,000/= Viwanda vidogo vya useremala na mashine za mbao, 10,000/=
Part
JEDWALI LA PILI
- 15 Verify source ↗
Kituo cha kuuza mafuta (Filling station)
AI-assisted research summary: Section title: Filling station.
15. Kituo cha kuuza mafuta (Filling station) - 22 Verify source ↗
Majengo/maeneo ya kuoshea magari/pikipiki
AI-assisted research summary: The section lists monetary charges for "Majengo/maeneo ya kuoshea magari/pikipiki" and includes several amounts, including an annual amount.
22. Majengo/maeneo ya kuoshea magari/pikipiki 16 5,000/= 5,000/= 3,000/= 10,000/= 7,000/= 10,000/= 10,000/= 10,000/= 5,000/= 2,000/= 100,000/= (kwa mwaka) 10,000/= 5,000/= Sheria Ndogo za (Afya Na Usafi wa Mazingira) Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Tangazo La Serikali Na. 465 (Linaendelea) - 23 Verify source ↗
Section 23
AI-assisted research summary: This provision is titled “Zahanati/kituo cha afya au hospitali” (clinic/health center or hospital).
23. Zahanati/kituo cha afya au hospitali - 24 Verify source ↗
Majengo mengine yasiyotajwa
AI-assisted research summary: Section 24 lists “other unspecified buildings” and shows amounts of 20,000/= and 20,000/=.
24. Majengo mengine yasiyotajwa 20,000/= 20,000/= - 26 Verify source ↗
Maeneo yanayochimbwa madini mfano mchanga na
AI-assisted research summary: The provision mentions mining areas such as sand and rubble and includes an amount of 5,000/=, but the exact rule is unclear from the fragment.
26. Maeneo yanayochimbwa madini mfano mchanga na 5,000/= vifusi - 27 Verify source ↗
Viwanda vikubwa
AI-assisted research summary: Hii ni ilani ya ukaguzi inayomwambia mpokeaji kwamba choo hakipo, kimejaa, au kimeharibika, na kwamba anatakiwa kutekeleza hatua zitakazofuata.
27. Viwanda vikubwa 10,000/= 17 Sheria Ndogo za (Afya Na Usafi wa Mazingira) Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Tangazo La Serikali Na. 465 (Linaendelea) _____________ JEDWALI LA TATU ____________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 25) ILANI YA KUJENGA CHOO AYA YA I Ndugu ………………………..……simu………………..wa Kitongoji ……………………………….Kijiji………………..Kata……………………….. ……………………Unaarifiwa kwamba katika ukaguzi uliofanyika cha Tarafa tarehe …………………mwezi……………..mwaka……………katika nyumba yako ya biashara/kuishi/kutolea huduma/Namba iliyopo eneo la …………………….katika Kitongoji/Mtaa*………….……….Kijiji cha …………….………Kata ya …………………. Imekuwa haina choo/choo kimejaa/kimeharibiwa*, hivyo unaamriwa kutekeleza mambo yafuatayo: -
Part
JEDWALI LA TATU
- 4 Verify source ↗
……………………………………………………………………………
AI-assisted research summary: Mtu anayepokea ilani lazima atimize maelekezo yote ya aya ya I ndani ya siku 30 tangu kupokea ilani.
4. …………………………………………………………………………… AYA YA II Unapewa muda wa siku thelathini (30) tu tangu siku ya kupokea ilani hii kutekeleza maelekezo yote yaliyoelezwa katika aya ya I ya ilani hii. Ukaguzi wa kuthibitisha utekelezaji wa maelekezo uliyopewa utafanyika tarehe ……………. Endapo utashindwa kutekeleza maelekezo ndani ya muda uliopewa Halmashauri itachukua hatua kali za kisheria AYA YA III bila kukupa taarifa nyingine. Saini …………………………………………… Majina…………………………………………. Simu…………………………………………… Aya hii mtu aliyekosa kama amepatikana wakati wa kutoa ilani. SHAHIDI ALIYETHIBITISHA NI: IMETOLEWA NA: Saini ……………………………………….. Saini ……………………………….. 18 Sheria Ndogo za (Afya Na Usafi wa Mazingira) Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Tangazo La Serikali Na. 465 (Linaendelea) Majina ……………………………………. …………………………….. Simu ……………………………………… …………………………… Tarehe ……………………………………. …………………………….. *Futa lisilohusika Majina Wadhifa Tarehe 19 Sheria Ndogo za (Afya Na Usafi wa Mazingira) Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Tangazo La Serikali Na. 465 (Linaendelea) ____________ JEDWALI LA NNE ___________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 26(1)) ILANI YA KUONDOA KERO AYA YA I Ndugu ………………………simu…………………..wa Kitongoji …………………….Kijiji……………………..Kata…………….. ………………………Unaarifiwa kwamba katika ukaguzi uliofanyika cha Tarafa tarehe …………………mwezi……………..mwaka……………katika nyumba yako ya biashara/kuishi/kutolea huduma/Namba iliyopo eneo la …………………….katika Kitongoji/Mtaa*………….……….Kijiji cha …………….………Kata ya …………………. Tumekuta machukizo/kero/uchafu*, hivyo unaamriwa kutekeleza mambo yafuatayo:-
Part
JEDWALI LA NNE
- 4 Verify source ↗
……………………………………………………………………………
AI-assisted research summary: Ilani hii inaelekeza kurekebisha, kuondoa, au kusafisha kwa Aya ya II.
4. …………………………………………………………………………… Kwa ilani hii unaamriwa kurekebisha/kuondoa/kusafisha* kwa: AYA YA II - 4 Verify source ↗
……………………………………………………………………………
AI-assisted research summary: A person who receives the notice must comply with everything set out in Part II within 7 days; if they do not, the Council may take legal action without giving any further notice.
4. …………………………………………………………………………… AYA YA III 20 Sheria Ndogo za (Afya Na Usafi wa Mazingira) Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Tangazo La Serikali Na. 465 (Linaendelea) Unapewa muda wa siku saba (7) tangu siku ya kupokea ilani hii, unatakiwa kutekeleza yote yaliyoelezwa katika sehemu ya II ya Ilani hii, kushindwa kwako kutekeleza ndani ya muda uliopewa Halmashauri italazimika kukuchukulia hatua kali za kisheria bila kukupa taarifa nyingine. Saini ……………………………………….Majina………………………………….simu……… Aya hii mtu aliyekosa kama amepatikana wakati wa kutoa ilani. SHAHIDI ALIYETHIBITISHA NI: Saini ………………………………………..Saini Majina ……………………………………. Majina Simu………………………………………...Simu IMETOLEWA NA: Wadhifa……………………………………..Wadhifa Tarehe ………………………………………Tarehe *Futa lisilohusika 21 Sheria Ndogo za (Afya Na Usafi wa Mazingira) Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Tangazo La Serikali Na. 465 (Linaendelea) ______________ JEDWALI LA TANO _____________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 29(2)) VIWANGO VYA FAINI KWA MFUGO AU MIFUGO INAYOZURURA NA. AINA YA MFUGO Ng’ombe Punda Mbuzi Kondoo 1
Part
JEDWALI LA TANO
- 2 Verify source ↗
Section 2
AI-assisted research summary: Hii ni jedwali la viwango vya faini na fomu ya kukiri kosa chini ya Sheria Ndogo za Afya na Usafi wa Mazingira za Halmashauri ya Wilaya ya Mafia.
2. 2 3 4 KIWANGO CHA FAINI (TZS) 50,000/= kila ng’ombe 40,000/= kila punda 30,000/= kila mbuzi 30,000/= kila kondoo Wanyama wengine 15,000/= kila nguruwe 22 Sheria Ndogo za (Afya Na Usafi wa Mazingira) Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Tangazo La Serikali Na. 465 (Linaendelea) _____________ JEDWALI LA SITA _____________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 33) HATI YA KUFIFILISHA KOSA Mimi;………………………………………………………. nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya;…………………………………….ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia, kwamba mnamo tarehe;…… ya Mwezi;….…. Mwaka;…….… nilitenda kosa la kukiuka masharti ya aya ya …… ya Sheria Ndogo ya (Afya na Usafi wa Mazingira) ya Halmashauri ya Wilaya ya Mafia ya Mwaka 2024. Kwa Mamlaka aliyopewa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mafia, niko tayari kulipa kiasi cha Ada au Ushuru ninaodaiwa pamoja na faini. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA MIMI MWENYEWE KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU: Leo tarehe;…....... ya Mwezi;………… Mwaka;………….. Jina;…………………………………..……………………. Saini;…………………………..…………………………… MBELE YANGU : Jina;…………………………….………..…………………… Wadhifa;…………………………………………………..……. Saini;………………………………………………………… Tarehe;………………………………………………………. 23 Sheria Ndogo za (Afya Na Usafi wa Mazingira) Halmashauri ya Wilaya ya Mafia Tangazo La Serikali Na. 465 (Linaendelea) Nembo ya Halmashauri ya Wilaya ya Mafia imegongwa kwenye Sheria Ndogo hii kufuatia azimio lililopitishwa katika mkutano wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya Mafia uliofanyika tarehe 31 mwezi 05 Mwaka 2022 na kushuhudiwa Lakari hiyo ikigongwa mbele ya:- KASSIM SEIF NDUMBO Mkugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mafia JUMA SALUM ALLY /Mwenyekiti wa Halmashauri Halmashauri ya Wilaya Mafia NAKUBALI, L.S Dodoma, MOHAMED OMARY MCHENGERWA (MB) Waziri wa Nchi – Ofisi ya Rais (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa) 24
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo za (Afya na Usafi wa Mazingira) Halmashauri ya Wilaya ya Mafia za Mwaka 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in