Sheria Ndogo ya Afya na Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza za Mwaka 2024
This section gives the short title of the by-law.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Afya na Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza za Mwaka 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This section gives the short title of the by-law. This section says the by-law applies throughout the Uvinza District Council area. This section defines terms used in the by-law, including official, food, water source, council, director, hand sanitizer, waste pit, wastewater, resident, service provider, law, waste, solid waste, waste collection fee, agent, and animals. Wakazi au wamiliki wa nyumba, viwanja au biashara lazima waweke maeneo yao safi na kutimiza masharti ya usafi na afya yaliyoorodheshwa hapa. Halmashauri must notify landlords or tenants to fix toilet problems, may close unsafe or dirty toilets, may stop use of a house or building until instructions are followed, and must notify people to remove nuisances found in inspected areas.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Afya na Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza za Mwaka 2024
Showing 31 of 31
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria
AI-assisted research summary: This section gives the short title of the by-law.
1.Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Afya na Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza za Mwaka 2024. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la
AI-assisted research summary: This section says the by-law applies throughout the Uvinza District Council area.
2.Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza. Tafsiri Sura ya 331 - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii isipokuwa pale
AI-assisted research summary: This section defines terms used in the by-law, including official, food, water source, council, director, hand sanitizer, waste pit, wastewater, resident, service provider, law, waste, solid waste, waste collection fee, agent, and animals.
3. Katika Sheria Ndogo hii isipokuwa pale ambapo muktadha utaelekeza vinginevyo: “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni Afisa yeyote atakayeteuliwa kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “chakula” maana yake ni kitu chochote kinacholiwa au kunywewa na binadamu isipokuwa madawa; “chanzo cha maji” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa chini ya Sheria ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza au Afisa yeyote atakayeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi; 1 Sheria Ndogo ya Afya Na Usafi wa Mazingira za Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza Tangazo La Serikali Na. 466(Linaendelea) Sura ya 191 Sura ya 287 Sura ya 191 Sura ya 191 “kitakasa mikono” maana yake ni sabuni au kemikali ambayo inatumika kuangamiza vidudu na virusi wa aina mbalimbali katika mikono. “kizimba cha taka” maana yake ni kizimba cha taka au chombo maalum kilichowekwa na Halmashauri kwa ajili ya jamii kuhifadhia taka ngumu kabla jalala kuu ya kuzisafirishwa hadi kwenye lililoidhinishwa na Halmashauri; “maji taka” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; “mkazi” maana yake ni mtu yeyote ambaye kwa kawaida anaishi kwenye eneo lililoko ndani ya Halmashauri na ambaye ana kaya au anaishi katika kaya au taasisi iliyopo katika eneo la Halmashauri; “mtoa huduma” ni mfanyakazi kwenye sehemu za biashara zinazotoa huduma ya chakula, malazi au vinywaji mbalimbali; “Sheria” maana yake ni Sheria ya Serikali za Mita ana Mamlaka za Wilaya. “taka” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; “taka ngumu” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; “Ushuru wa uzoaji taka” maana yake ni malipo yanayotozwa na Halmashauri kwa ajili ya huduma ya uzoaji taka; “wakala “maana yake ni, kampuni, taasisi, kikundi au mtu binafsi aliyeteuliwa na halmashauri kwa ajili ya kutoa huduma ya kuzoa taka; “Wanyama” maana yake ni ng’ombe, mbuzi, kondoo, nguruwe, punda, mbwa pamoja na wanyama wengine wafugwao. Wajibu wa kufanya usafi wa Mazingira - 4 Verify source ↗
Itakuwa ni wajibu wa kila mkazi anayeishi,
AI-assisted research summary: Wakazi au wamiliki wa nyumba, viwanja au biashara lazima waweke maeneo yao safi na kutimiza masharti ya usafi na afya yaliyoorodheshwa hapa.
4.Itakuwa ni wajibu wa kila mkazi anayeishi, anayemiliki eneo la nyumba, kiwanja au biashara kuhakikisha kwamba- 2 Sheria Ndogo ya Afya Na Usafi wa Mazingira za Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza Tangazo La Serikali Na. 466(Linaendelea) (a) mazingira yanayozunguka eneo lake yanakuwa safi wakati wote; (b) taka zote zinakusanywa na kuondolewa kwa (c) anachimba njia itakayoelekezwa na Halmashauri; kutupia taka litakalokuwa na urefu usiopungua kimo cha futi tatu na upana usiopungua futi mbili; shimo la (d) anajenga choo chenye mlango imara cha kudumu kwa matofali na kuezeka kwa bati, tembe, majani, na vigae kufunguka na kuhakikisha kwamba choo kinatumika wakati wote na kuwe na chombo cha maji tiririka na sabuni ya kunawa mikono; unaofunga (e) eneo lake halina mazalia ya mbu, panya na wadudu wengine hatarishi; (f) maji yote yanayotumika kwa kunywa ni safi na salama bila kujali yametoka kwenye chanzo gani cha maji; (g) kuwa na chombo chenye maji tiririka pamoja na kitakasa mikono mbele ya sehemu ya biashara na kuhakikisha kuwa kila muhitaji huduma ananawa au kujitakasa mikono kabla ya kupata huduma. Ilani ya kufunga au katazo au marekebisho - 5 Verify source ↗
(1) Halmashauri itatoa ilani kwa mwenye
AI-assisted research summary: Halmashauri must notify landlords or tenants to fix toilet problems, may close unsafe or dirty toilets, may stop use of a house or building until instructions are followed, and must notify people to remove nuisances found in inspected areas.
5.-(1) Halmashauri itatoa ilani kwa mwenye nyumba au mpangaji kumtaka arekebishe hali ya choo baada ya kugundulika kuwa nyumba yake au anayoishi haina choo au choo kilichopo kimejaa au hakifai kwa matumizi ya binadamu kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Kwanza. (2) Halmashauri itakuwa na uwezo wa kufunga choo chochote ambacho kitaonekana kichafu au cha kuhatarisha maisha ya binadamu na hakitaruhusiwa itakaporidhika na kutumika mpaka Halmashauri matengenezo yaliyofanyika. (3) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (1) 3 Sheria Ndogo ya Afya Na Usafi wa Mazingira za Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza Tangazo La Serikali Na. 466(Linaendelea) Halmashauri inaweza kuamuru nyumba au jengo hilo lisitumike kwa shughuli za makazi au biashara au taasisi ametimiza mpaka mmiliki wake maelekezo aliyopewa. atakapokuwa (4) Halmashauri itatoa ilani kwa mtu yeyote kama atagundua kuwa eneo alilokagua lina kero yoyote ili aondoe kero hiyo. Uhifadhi wa maji taka
Part
Jedwali la Kwanza.
- 6 Verify source ↗
Kila mmiliki wa nyumba au kiwanda au eneo
AI-assisted research summary: Wamiliki wa nyumba, viwanda au maeneo ya biashara lazima wawe na karo la kuhifadhia maji taka, wanyonye maji taka likijaa, wasimwage maji machafu sehemu zisizoruhusiwa, na waepuke kusababisha harufu mbaya yenye madhara.
6. Kila mmiliki wa nyumba au kiwanda au eneo la biashara anatakiwa- (a) kuhakikisha kuwa anakaro la kuhifadhia maji taka; (b) kunyonya maji takakila wakati karo linapojaa; (c) kutotiririsha au kutoelekeza maji kutoka vyooni, bafuni, karoni au viwandani kwenda barabarani, uchochoroni, mtoni, kwenye vyanzo vya maji, maeneo ya wazi, kwenye mfereji wa maji ya mvua au sehemu yoyote ambayo haijatengwa kwa ajili ya kuhifadhia maji taka; na (d) kuhakikisha hasababishi harufu yenye shughuli madhara na zinazofanyika katika eneo hilo. inayotokana Utengenezaji na uuzaji wa vyakula - 7 Verify source ↗
Mtu yeyote anayetengeneza, kuchoma,
AI-assisted research summary: Anyone making, cooking, boiling, or selling food in the council area must follow health rules, hold a permit from the Council Health Officer, store food in a clean covered container, and keep uncooked food raised above the ground.
7. Mtu yeyote anayetengeneza, kuchoma, kupika, kuchemsha au kuuza chakula cha aina yoyote katika eneo la Halmashauri atatakiwa- (a) kutimiza masharti na kanuni za afya; (b) kuwa na kibali kutoka kwa Afisa Afya wa Halmashauri; (c) kuhifadhi vyakula katika chombo safi chenye mfuniko kinachozuia inzi, vumbi na wadudu waletao madhara kwa afya ya binadamu; na (d) kuuza vyakula visivyopikwa vikiwa juu, ya meza au chombo vimewekwa 4 Sheria Ndogo ya Afya Na Usafi wa Mazingira za Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza Tangazo La Serikali Na. 466(Linaendelea) Ukaguzi na upimaji wa afya Mamlaka ya Afisa Mwidhiniwa kisichoruhusu vyakula hivyo kuwa chini. - 8 Verify source ↗
(1) Kila mfanyabiashara au mmiliki au
AI-assisted research summary: Wafanyabiashara na wahudumu wa hoteli, migahawa, baa, nyumba za kulala wageni na wauzaji wa vyakula vilivyopikwa lazima wapimwe afya kila baada ya miezi sita na walipe ada ya upimaji. Halmashauri pia lazima ihifadhi orodha ya waliopimwa na kutoza ada ya ukaguzi wa afya kabla ya kutoa leseni ya biashara.
8.-(1) Kila mfanyabiashara au mmiliki au mhudumu wa hoteli, migahawa, baa, nyumba za kulala wageni, au watu wanaoshughulika na kuuza vyakula vilivyopikwa atahakikisha kwamba anapima afya kila baada ya miezi sita na kulipa ada ya upimaji kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Pili. bucha, waoka mikate, (2) Halmashauri itahifadhi orodha ya majina ya watoa huduma wote ambao wamepimwa afya zao ili kurahisisha uhakiki wa afya za watumiaji hata kama mtoa huduma (mhudumu) au mfanyakazi amehama kwenda sehemu nyingine ndani ya Halmashauri aweze kutambulika kwa urahisi. (3) Halmashauri itatoza ada ya ukaguzi wa afya ambayo italipwa kwa mwaka kabla ya mwombaji kupewa leseni ya biashara kama ilivyoainishwa katika Sheria Ndogo hii. - 9 Verify source ↗
(1) Afisa Mwidhiniwa atakuwa na mamlaka
AI-assisted research summary: Afisa Mwidhiniwa ana mamlaka ya kuingia maeneo ya Halmashauri kwa saa maalum, kutoa ushauri au maelekezo kuhusu jengo hatarishi, kuzuia shughuli wakati wa mlipuko wa magonjwa, na kufunga au kuagiza kufungwa kwa biashara au jengo lisilokaguliwa au linalokiuka masharti ya afya.
9.-(1) Afisa Mwidhiniwa atakuwa na mamlaka ya kuingia katika eneo lolote ndani ya Halmashauri kuanzia saa moja na nusu asubuhi hadi saa tisa na nusu alasiri kwa lengo la kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii. (2) Afisa Mwidhiniwa atakuwa na mamlaka ya kushauri au kuelekeza watu au mtu kutokuishi katika jengo ambalo linahatarisha afya au maisha ya watu na viumbe hai. (3) Afisa Mwidhiniwa atakuwa na mamlaka ya kuzuia shughuli mbalimbali wakati wa mlipuko wa magonjwa ikiwa pamoja na kukamata vyombo au vifaa vingine vinavyotumika na ambavyo vinaweza kuleta madhara kwa wakazi wa Halmashari. (4) Afisa Mwidhiniwa atakuwa na mamlaka ya kufunga au kuagiza kufungwa kwa biashara yoyote au jengo ambalo halijakaguliwa au lililokaguliwa na kukutwa limekiuka kanuni na masharti ya afya. 5 Sheria Ndogo ya Afya Na Usafi wa Mazingira za Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza Tangazo La Serikali Na. 466(Linaendelea) Ukaguzi wa jengo la biashara - 10 Verify source ↗
Kila mfanyabiashara atakuwa na wajibu wa
AI-assisted research summary: Every trader must make sure the business building is inspected by an authorized officer before starting the business.
10. Kila mfanyabiashara atakuwa na wajibu wa kuhakikisha jengo la biashara linakaguliwa na Afisa Mwidhiniwa kabla ya kuanzisha biashara. Vifaa vya kuhifadhia taka ngumu Taratibu za kubomoa jengo Ada ya uzoaji taka jengo - 11 Verify source ↗
(1) Kila mmliki wa jengo la makazi au
AI-assisted research summary: Wamiliki, wapangaji na wafanyabiashara ndani ya Halmashauri lazima wawe na vyombo vya kuhifadhia taka vilivyo na mfuniko na wakusanye taka kwenye vizimba vilivyoainishwa; katika maeneo ya kijani yasiyopimwa lazima pia wawe na shimo kubwa la taka ngumu; na wamiliki au madereva wa magari ya abiria lazima wahifadhi na kutupa taka za ndani ya gari sehemu maalum ya Halmashauri.
11.-(1) Kila mmliki wa jengo la makazi au mpangaji wa la makazi au mtu yeyote anayefanyia biashara katika eneo lolote ndani ya Halmashauri atatakiwa kuwa na chombo cha kuhifadhia takataka chenye mfuniko na atawajibika kukusanya takataka hizo kwenye vizimba vya kuzolea takataka katika maeneo yaliyoainishwa. (2) Kila mmiliki wa jengo au mpangaji wa nyumba iliyoko katika ukanda wa kijani, katika maeneo ambayo hayajapimwa atalazimika kuwa na shimo kubwa la kukusanyia taka ngumu katika eneo lake. (3) Mtu yeyote anaemiliki au dereva wa chombo cha kusafirisha abiria atahakikisha kwamba anaweka chombo cha kuhifadhia taka zitakazozalishwa ndani ya chombo cha usafiri na kuzitupa katika sehemu maalum iliyotengwa na Halmashauri kwa ajili hiyo. - 12 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote anaetaka kubomoa au
AI-assisted research summary: Anyone who wants to demolish a building or part of a building must have a permit from the Council.
12.-(1) Mtu yeyote anaetaka kubomoa au kusababisha kubomoka jengo au sehemu ya jengo anatakiwa kuwa na kibali cha Halmashauri. (2) Mtu yeyote atakayeomba na kupata kibali cha kubomoa jengo au sehemu ya jengo atahakikisha- (a) anazuia uchafuzi wa hali ya hewa; na (b) anaondoa na kutupa mabaki ya jengo alilobomoa, mahali alipoelekezwa kwa mujibu wa kibali. - 13 Verify source ↗
Halmashauri itawajibika kukusanya taka
AI-assisted research summary: Halmashauri must collect the specified solid waste in each ward, and waste producers must pay the collection fee or levy for waste bins.
13. Halmashauri itawajibika kukusanya taka takataka ngumu vilivyoainishwa katika kila kata, na wazalishaji takataka watalipia ada au ushuru wa ukusanyaji wa takataka vizimba kutoka katika vya 6 Sheria Ndogo ya Afya Na Usafi wa Mazingira za Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza Tangazo La Serikali Na. 466(Linaendelea) Ukusanyaji taka ngumu kama ilivyooneshwa katika Jedwali la Tatu. - 14 Verify source ↗
(1) Hairuhusiwi kuweka uchafu wenye asili
AI-assisted research summary: A person must have a council permit before burning or burying solid waste.
14.-(1) Hairuhusiwi kuweka uchafu wenye asili ya maji maji kwenye pipa au chombo chochote cha taka ngumu au kitu chochote kinachoweza kulipuka na kusababisha madhara. (2) Taka ngumu zote zitakazokusanywa kwenye pipa au chombo cha taka zitabaki kuwa mali ya mkazi lile mpaka zitakapokuwa au mmliki wa eneo zimefikishwa au cha kizimba kwenye zitakapokuwa zimetolewa na wakala kutoka katika eneo lake. taka (3) Mtu atatakiwa kuwa na kibali cha Halmashauri ili kuchoma au kufukia taka ngumu. Eneo la kutupa taka - 15 Verify source ↗
(1) Halmashauri itakuwa na wajibu wa
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima itenge eneo la kutupia taka, iweke vyombo maalum vya kuhifadhia taka, na itoe huduma ya uzoaji taka kwa malipo; Serikali ya Kijiji lazima itenge eneo la dampo kwa ajili ya taka ngumu.
15.-(1) Halmashauri itakuwa na wajibu wa- (a) kutenga eneo maalum kwa ajili ya kutupia Usafi kaya katika taka; (b) kuweka vyombo maalum vya kutunzia taka katika maeneo ya Halmashauri; na (c) kutoa huduma ya uzoaji taka kwa malipo kutoka kwa wazalishaji wa taka hadi kwenye dampo. (2) Serikali ya Kijiji itawajibika kutenga eneo la dampo kwa ajili ya utupaji wa taka ngumu. - 16 Verify source ↗
(1) kila mkazi, mwenye nyumba, mpangaji,
AI-assisted research summary: Wakazi, wenye nyumba, wapangaji, na wamiliki wanapaswa kuwa na choo, kusafisha na kutunza usafi wa eneo la nyumba, kuweka madirisha ya ukubwa unaotakiwa, na kuwa na mfumo wa taka; wamiliki wa biashara pia wanapaswa kuweka vifaa vya kunawia mikono kwa wateja.
16.-(1) kila mkazi, mwenye nyumba, mpangaji, au mmiliki atalazimika kuwa na choo na kupalilia majani na kufagia kila mara na kutunza mazingira safi kwa umbali wa futi kumi kutoka ukuta wa jengo kama ilivyo katika vipimo vilivyowekwa na kukubalika na Halmashauri. (2) kila mkazi mwenye nyumba au mmiliki atapaswa kuweka lake madirisha makubwa yasiyopungua 1/8 ya eneo la sakafu ya chumba au vipimo vilivyowekwa na kukubaliwa na Halmashauri jengo (3) Kila mkazi mwenye nyumba au mmiliki atalazimika kuwa na shimo la taka au pipa la taka 7 Sheria Ndogo ya Afya Na Usafi wa Mazingira za Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza Tangazo La Serikali Na. 466(Linaendelea) pembeni mwa nyumba yake na kuhakikisha taka hizo zinaondolewa au kuteketezwa mara pipa linapojaa. (4) kila mmiliki wa biashara ni lazima kuwa na ndoo ya kunawia maji tiririka ikiwa pamoja na sabuni au kuwa na kitakasa mikono kwa ajili ya wateja wake. Udhibiti wa taka maji Machinjio Wajibu wa mmiliki wa duka la kuuza nyama hoteli mgahawa - 17 Verify source ↗
Mtu yeyote, kaya, taasisi, kampuni, kiwanda,
AI-assisted research summary: Watu, nyumba, taasisi, kampuni, viwanda na ofisi zinazokusanya watu lazima zitunze maeneo yao na zihifadhi choo cha kiwango kinachokubalika, kijengwe angalau mita 60 kutoka chanzo cha maji ya nyumbani, kichonyezwe kikijaa kwa gharama zao, na kuwa na kichanja cha kuanikia vyombo vilivyoshwa.
17. Mtu yeyote, kaya, taasisi, kampuni, kiwanda, ofisi, yoyote wanapokusanyika watu, kama vile soko, minada, magulio, makanisa, misikiti, itatunza maeneo yake ikiwa ni pamoja na kufanya yafuatayo: na majengo (a) kuwa na choo chenye hadhi inayokubalika kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii na kitahesabika kujaa kukisalia futi tatu kufikia usawa wa sakafu ya karo; (b) choo kinatakiwa kujengwa umbali wa mita sitini kutoka katika kisima au chanzo chochote cha maji kinachotumika kwa matumizi ya nyumbani; (c) kunyonya choo kikijaa kwa gharama zake mwenyewe; (d) kuwa na kichanja kwa ajili ya kuanika vyombo baada ya kuoshwa. - 18 Verify source ↗
Kila mtu atatakiwa kupeleka mfugo au
AI-assisted research summary: Watu wote lazima wapeleke mifugo yao machinjioni au mahali huduma hiyo ilipo, na hairuhusiwi kuchinja mahali pengine isipokuwa kwa kutoa taarifa kwa Afisa Mwidhiniwa.
18. Kila mtu atatakiwa kupeleka mfugo au mifugo yake machinjioni au mahali huduma hiyo inapopatikana na itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kuchinja mfugo au mifugo mahali pengine popote ambapo sio machinjio, isipokuwa kwa kutoa taarifa kwa Afisa Mwidhiniwa na atalazimika kulipia gharama za machinjio. - 19 Verify source ↗
Itakuwa ni wajibu wa kila mmiliki wa duka
AI-assisted research summary: Each meat shop owner must keep the shop and attendant hygiene conditions specified in this section.
19. Itakuwa ni wajibu wa kila mmiliki wa duka la kuuzia nyama kuhakikisha kwamba- jengo (a) ana la kudumu lililosakafiwa na kuwekwa marumaru nyeupe kwenye sakafu na kuta kwa urefu wa futi sita kutoka usawa 8 Sheria Ndogo ya Afya Na Usafi wa Mazingira za Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza Tangazo La Serikali Na. 466(Linaendelea) wa sakafu; (b) jengo lina maji safi, gogo na misumeno ya kukatia nyama; (c) kuna pipa la kuhifadhia taka; (d) muhudumu ana koti jeupe pamoja na viatu vyeupe aina ya buti; (e) muhudumu anapima afya kila baada ya miezi sita. Wajibu wa kushiriki shughuli za usafi wa mazingira - 20 Verify source ↗
(1) Kila jumamosi ya kila mwisho wa mwezi
AI-assisted research summary: Kila jumamosi ya mwisho wa mwezi ni siku maalumu ya usafi wa mazingira, na wananchi pamoja na wamiliki wa maeneo fulani wanatakiwa kushiriki na kuhakikisha maeneo yao ni safi.
20.-(1) Kila jumamosi ya kila mwisho wa mwezi itakuwa ni siku maalamu ya kufanya usafi wa mazingira katika maeneo yote ya Halmashauri. (2) Itakuwa ni wajibu na lazima kwa kila mwananchi kushiriki usafi wa mazingira kwa siku iliyopangwa na Halmashauri katika maeneo yao na maeneo ya umma. (3) Kila mtu atahakikisha- (a) eneo lake la makazi na linalomzunguka; (b) eneo analofanyia biashara; (c) eneo la wazi lililokaribu naye kwa umbali wa mita kumi; na (d) eneo la mazingira ya ofisi, ni safi kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. (4) Itakuwa ni wajibu wa kila mmiliki wa jengo au kiwanja au eneo lolote ambalo halijaendelezwa kufanya usafi katika eneo hilo mara kwa mara. Vikundi vya usafi - 21 Verify source ↗
Halmashauri
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima ihamasishe na itambue vikundi jamii ili viweze kufanya kazi za udhibiti wa taka ngumu na usafi wa mazingira, baada ya kuingia mkataba na Halmashauri.
21. Halmashauri itahamasisha uundaji wa vikundi jamii na kuvitambua ili kuviwezesha kufanya shughuli za udhibiti wa taka ngumu pamoja na usafi wa mazingira katika vijiji na vitongoji baada ya kuingia mkataba na Halmashauri. Marufuku - 22 Verify source ↗
Ni marufuku
AI-assisted research summary: Kifungu hiki kinapiga marufuku vitendo kadhaa vya usafi, mazingira, biashara na matumizi ya maeneo ya umma.
22. Ni marufuku- (a) mtu yeyote kuendesha biashara ya upulizaji 9 Sheria Ndogo ya Afya Na Usafi wa Mazingira za Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza Tangazo La Serikali Na. 466(Linaendelea) dawa au biashara ya kuua wadudu au wanyama waharibifu katika nyumba yoyote au mahali popote bila cheti cha taaluma kinachotambuliwa na Serikali na leseni kutoka Halmashauri; lake jengo (b) mfanyabiashara yeyote kupanga bidhaa nje la biashara, barabarani, ya vichochoroni au katika eneo lolote ambalo halikuidhinishwa kwa ajili ya shughuli hiyo; (c) mfugaji kuruhusu mfugo au mifugo kuzurura ovyo mitaani au barabarani; au katika (d) mtu yeyote kutupa taka za aina yoyote barabarani au eneo lolote la wazi, kwenye vichochoro au kwenye chanzo chochote cha maji ambalo halijatengwa kwa ajili ya shughuli hiyo; (e) mtu yeyote aliye ndani ya gari kudondosha taka ngumu nje ya gari likiwa ndani au nje ya kituo cha magari na sehemu yoyote ile ambapo gari hilo linapita; lolote eneo Sura ya 191 (f) mtu yeyote kuanzisha shughuli za kiwanda au mradi wowote unaoweza kuathiri mazingira bila kufanya utafiti wa mazingira kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; (g) mtu yeyote kuzuia maji kupitia njia yake ya asili kwa kujenga au kulima au kuweka kitu ya maji chochote kitakachoingilia mtiririko wa asili wa maji katika chanzo cha maji; kwenye njia (h) mtu yeyote kuweka kitu chochote kwenye maji taka ambacho kinaweza kuathiri mtu yeyote au kuharibu mfumo wa tiba ya maji taka au kusababisha kuzuia mtiririko wa maji taka; (i) mtu yeyote kulima kilimo cha matuta yanayosababisha maji kutuama ndani ya eneo la katikati ya mji; 10 Sheria Ndogo ya Afya Na Usafi wa Mazingira za Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza Tangazo La Serikali Na. 466(Linaendelea) (j) mtu yeyote kufanya matengenezo ya magari, pikipiki na mitambo kwenye maeneo ya Halmashauri bila kibali; (k) mtu yeyote kuegesha gari bovu kwenye njia ya miguu, mtaa, uchochoro, mtaro, maeneo ya wazi, barabarani na kusababisha adha kwa wakazi au watumiaji wa njia hiyo; (l) mtu yeyote kuchinja au kuuza nyama ya aina yoyote katika maeneo yasiyokuwa machinjio au maduka ya kuuza nyama au katika maeneo yasiyoruhusiwa na Halmashauri. Makosa - 23 Verify source ↗
Itakuwa ni kosa chini ya Sheria Ndogo hii
AI-assisted research summary: This section makes it an offence for anyone to do any of the listed sanitation, waste, food-selling, burial, vehicle, and public-cleanliness acts.
23. Itakuwa ni kosa chini ya Sheria Ndogo hii kwa mtu yeyote- (a) kujenga choo umbali usiozidi mita sitini kutoka kisimani, bwawani, mtoni, au chanzo cha maji yanayotumika, kwa matumizi ya binadamu; (b) kutoa kinyesi au kusababisha kinyesi, mkojo, au taka maji yenye kinyesi kutoka kwenye choo chake au bafu lake au karo la kuoshea vyombo au nguo au kutoka kwenye bomba lolote linalochukua taka maji na kuyatitirisha kwenye barabara, mitaa, au kwenye mifereji ya maji ya mvua, au mfereji wowote ulio wazi; (c) kutupa taka au kusababisha mtu mwingine atupe taka mahali popote pasiporuhusiwa na Halmashauri; (d) kutiririsha maji taka barabarani, ziwani, mashambani, mitaani au katika eneo la nyumba ya jirani, mitaro ya barabara au eneo la wazi; (e) kuendesha mashine ya kusaga na kukoboa katika jengo ambalo halijatekeleza masharti ya afya; (f) kuuza nyama iliyotundikwa chini ya mti, 11 Sheria Ndogo ya Afya Na Usafi wa Mazingira za Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza Tangazo La Serikali Na. 466(Linaendelea) kuuza nyama ya mnyama aliyechinjwa bila kibali cha Afisa Mwidhiniwa au kwenye bucha ambalo sio safi na halijatekeleza masharti kama yalivyo katika Sheria Ndogo hii; (g) kuuza ambalo katika halijatengwa au kusajiliwa kwa ajili ya shughuli hiyo; (h) kuzika maiti ambalo katika halikuainishwa kwa shughuli hiyo bila taarifa maalum kwa Afisa Mwidhiniwa; chakula eneo eneo (i) kutolipa ushuru wa kuzoa taka; (j) kufanya biashara ya kuuza vyakula vya aina yoyote barabarani, mitaani na nje ya majengo bila kuweka ndani ya chombo safi chenye mfuniko; (k) kuchezesha michezo au kuonesha michezo au burudani katika maeneo yasiyoruhusiwa na Halmashauri; (l) kuegesha gari bovu na kuliacha kando ya barabara au kichochoroni au eneo la wazi ambalo halijaidhinishwa kwa shughuli za gereji na kuliacha zaidi ya siku moja; (m) kulima kandokando au ndani ya mita sitini kutoka kwenye chanzo cha maji; (n) kutokuwa na pipa au chombo cha taka chenye mfuniko katika eneo la biashara; (o) kutokuwa na choo au kukutwa na choo kibovu au kilichojaa; (p) kukutwa na shimo la taka maji lililojaa au ambalo halina mfuniko; (q) kusafirisha nyama bila kutumia gari ya kusafirishia nyama ambayo imekaguliwa na kupewa kibali cha kusafirisha nyama kwa ajili ya matumizi ya binadamu; (r) kutoshiriki katika zoezi la usafi kiwilaya kila siku ya alhamisi ya kila mwisho wa mwezi 12 Sheria Ndogo ya Afya Na Usafi wa Mazingira za Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza Tangazo La Serikali Na. 466(Linaendelea) kulingana na mwongozo wa kitaifa wa zoezi hilo; (s) kuziba kichochoro; na (t) kutokuwa na chombo maalum cha kukusanyia takataka ndani ya gari la abiria. Adhabu Kufifilisha kosa - 24 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayetenda kosa katika Sheria
AI-assisted research summary: Anyone who commits an offence under this by-law, if convicted, faces a fine, imprisonment, or both.
24. Mtu yeyote atakayetenda kosa katika Sheria Ndogo hii, akitiwa hatiani, atatozwa faini isiyopungua shilingi elfu hamsini na isiyozidi shilingi laki tatu au kifungo kisichozidi miezi kumi na mbili jela au vyote kwa pamoja. - 25 Verify source ↗
Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa na kumtoza mkosaji ikiwa anakiri kosa na yuko tayari kujaza fomu maalum ya Jedwali la Nne.
25. Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha kosa kwa kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii kwa mujibu wa Sheria, iwapo mkosaji atakiri kosa na kuwa tayari kujaza fomu maalum iliyoainishwa katika Jedwali la Nne. JEDWALI LA KWANZA (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 5(1)) ILANI YA KUZUIA AU KUKATAZA AU KUFANYA MAREKEBISHO SEHEMU YA KWANZA Ndugu…………wa Mtaa/Kijiji..…….Kaya ya…………Unaarifiwa kwamba katika ukaguzi uliofanyika Tarehe………Mwezi………………Mwaka……………katika jengo au eneo lako la biashara/makazi/kutolea huduma/taasisi Namba … . iliyopo eneo la ……………...………………..katika kitongoji/Mtaa………………Kijiji cha…………. Kata ya…………… Imekuwa haina choo/choo kimejaa/kimeharibiwa hivyo unaamriwa kutekeleza mambo yafuatayo: 13 Sheria Ndogo ya Afya Na Usafi wa Mazingira za Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza Tangazo La Serikali Na. 466(Linaendelea)
Part
SEHEMU YA KWANZA
- 4 Verify source ↗
……………………………………………………………………
AI-assisted research summary: Mtu anayepokea ilani hii lazima atekeleze maelekezo yote ya sehemu ya I ndani ya muda uliotolewa kuanzia tarehe ya kupokea ilani.
4. ……………………………………………………………………... SEHEMU YA PILI Unapewa muda wa siku ……………….. kuanzia tarehe ya kupokea ilani hii i l i kutekeleza maelekezo yote yaliyoelezwa katika sehemu ya I ya ilani hii. SEHEMU YA TATU Ukaguzi wa kuthibitisha utekelezaji wa maelekezo uliyopewa utafanyika tarehe…………………… endapo utashindwa kutekeleza maelekezo ndani ya muda uliopewa Halmashauri itachukua hatua za kisheria bila kukupa taarifa nyingine. IMETOLEWA NA IMEPOKELEWA NA: Jina…………………………… Jina………………..… Saini…………………….. Saini………………………… Wadhifa……………………………Wadhifa……………………….. Tarehe……………………………...Tarehe………………………… *Futa lisilohusika SEHEMU YA KWANZA ILANI YA KUONDOA KERO Ndugu……………………………………..wa Mtaa/Kijiji………………………….Kata ya…………………………Unaarifiwa uliofanyika kwamba katika la lako tarehe………mwezi…………mwaka…………katika la eneo Huduma/taasisi/kiwanja biashara/makazi/kutolea …………………... jengo iliyopo ukaguzi Pamekutwa machukizo/kero/uchafu ifuatavyo: na kama
Part
SEHEMU YA
- 2 Verify source ↗
………………………………………………………………………
AI-assisted research summary: 2. ..……………………………………………………………………… 14 Sheria Ndogo ya Afya Na Usafi wa Mazingira za Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza Tangazo La Serikali Na. 466(Linaendelea)
2. ..……………………………………………………………………… 14 Sheria Ndogo ya Afya Na Usafi wa Mazingira za Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza Tangazo La Serikali Na. 466(Linaendelea) - 3 Verify source ↗
………………………………………………………………………
AI-assisted research summary: Hii sehemu inaonyesha amri ya kurekebisha, kuondoa, au kusafisha vitu vilivyoainishwa kwenye ilani.
3. ..……………………………………………………………………… SEHEMU YA PILI Kwa ilani hii unaamriwa kurekebisha/kuondoa/kusafisha kwa:
Part
SEHEMU YA PILI
- 3 Verify source ↗
……………………………………………………………………
AI-assisted research summary: Ukipewa muda katika ilani hii, unatakiwa kutekeleza yaliyoelezwa katika Sehemu ya II.
3. ...……………………………………………………………………... SEHEMU YA TATU ilani hii, Unapewa muda wa siku ……………. unatakiwa kutekeleza yote yaliyoelezwa katika sehemu ya II ya Ilani hii, kushindwa kwako kutekeleza ndani ya muda uliopewa Halmashauri italazimika kukuchukulia hatua kali za kisheria bila kukupa taarifa nyingine. tangu siku ya kupokea IMETOLEWA NA : IMEPOKELEWA NA : Jina…………………………………Jina…………………… Saini………………………………..Saini…………………… Wadhifa……………………………Wadhifa………………… Tarehe……………………………...Tarehe………………..... JEDWALI LA PILI ADA YA UPIMAJI WA AFYA (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 8(1)) Namba
Part
JEDWALI LA PILI
- 9 Verify source ↗
Section 9
AI-assisted research summary: Kifungu hiki kinaweka viwango vya kila mwezi vya ushuru wa uzoaji taka ngumu kwa kaya na aina mbalimbali za biashara/huduma.
9. Aina ya Biashara Nyumba ya starehe (baa, vilabu vya pombe za kienyeji na nyumba ya kulala wageni Duka la bidhaa Nyumba ya kutengeneza na kuuzia vyakula na au nyama choma. Duka la nyama Viwanda vya kati Viwanda vidogo vya vyakula Mhudumu wa chakula Kiwango cha Ada kwa Shilingi 5,000/= kwa kila mfanyakazi/Mhudumu 3,000/= kwa kila mfanyakazi/Mhudumu 5,000/= kila mfanyakazi/Mhudumu 5,000/= kwa kila mfanyakazi/Mhudumu 3,000/=Kwa kila mfanyakazi/Mhudumu 5,000/= kwa kila mfanyakazi/Mhudumu 5,000/= kila mfanyakazi/Mhudumu JEDWALI LA TATU 15 Sheria Ndogo ya Afya Na Usafi wa Mazingira za Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza Tangazo La Serikali Na. 466(Linaendelea) (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 13) Ushuru wa Uzoaji Taka ngumu SEHEMU A Namba. Eneo Kiwango cha Ushuru (Shilingi) kwa mwezi 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17 Kaya moja Maduka la rejareja Mashine ya kukamua mafuta ya alizeti Maduka la jumla Migahawa(Restaurant) Mashine za kukoboa au kusaga 2,000/= 5,000/= 5,000/= 10,000/= 5,000/= 5,000/= Vilabu vya pombe za kienyeji, baa, grocery, 5,000/= Mama lishe au Baba lishe, Nyama choma au 2,000/= chipsi Inayojitegemea Viwanda vya uselemala na mashine za mbao 5,000/= Bucha(Maduka ya Nyama, samaki) Nyumba za kulala wageni Saluni (Ususi/Vinyozi) Gereji ndogo Gereji kubwa Godown (Ghala) Kituo cha kuuza mafuta (Filling station) Ofisi za Taasisi mbalimbali 5,000/= 10,000/= 5,000/= 5,000/= 10,000/= 10,000/= 10,000/= 5,000/= 16 Sheria Ndogo ya Afya Na Usafi wa Mazingira za Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza Tangazo La Serikali Na. 466(Linaendelea) 18 19 20 21 22 21 22 23 24 25 26 Hospitali Vituo vya Afya Zahanati Shughuli za ushonaji Vioski au ibanda vya biashara Viwanda vikubwa Viwanda vidogo Wauzji wa mbao Kumbi za starehe Mafundi Vyuma Stoo za Mkaa 15,000/= 10,000/= 5,000/= 2,000/= 2,000/= 10,000/= 5,000/= 10,000/= 10,000/= 5,000/= 5,000/= 17 Sheria Ndogo ya Afya Na Usafi wa Mazingira za Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza Tangazo La Serikali Na. 466(Linaendelea) SEHEMU B Namba Maeneo ya Uzalishaji Kiwango cha Ushuru kwa Shilingi Taka vya za Vijiji Senta Busekela, Bukima, Kome, Murangi, Rusoli, Masinono, Saragana, Suguti, Kusenyi, Kwikuba, Bwai Mugango, KuUvinza, Busekela, Rukuba na Etaro Duka la rejareja Duka la jumla Biashara ya huduma 500/= 1,000/= 2,000/=
Part
SEHEMU B
- 3 Verify source ↗
Section 3
AI-assisted research summary: This section is a form for admitting an offence and stating willingness to pay any owed fee, charge, or fine.
3. JEDWALI LA TATU _____________ (Limetengenezwa Chini ya kanuni ya 25) _____________ KUFIFILISHA KOSA Mimi;………………………………………………………. nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya;………………………………………..…….ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashuri ya Wilaya ya Uvinza, kwamba mnamo tarehe;…… ya Mwezi;….…. Mwaka;…….… nilitenda kosa la kukiuka masharti ya Kanuni ya;….….. ya Sheria Ndogo ya (Afya na Usafi wa Mazingira) ya Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza ya Mwaka 2024. Kwa Mamlaka aliyopewa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza, niko tayari kulipa kiasi cha Ada au Ushuru ninaodaiwa pamoja na faini. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA MIMI MWENYEWE KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU: Leo tarehe;…....... ya mwezi;………… mwaka;………….. Jina:…………………………………..……………………. Saini:…………………………..…………………………… MBELE YANGU : Jin:…………………………….………..…………………… Wadhifa:…………………………………………………..… Saini:………………………………………………………… Tarehe:………………………………………………………. 18 Sheria Ndogo ya Afya Na Usafi wa Mazingira za Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza Tangazo La Serikali Na. 466(Linaendelea) Nembo ya Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza imegongwa kwenye Sheria Ndogo hii kufuatia azimio lililopitishwa katika mkutano wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya Uvinza uliofanyika tarehe 18 mwezi Disemba Mwaka 2023 na kushuhudiwa Lakari hiyo ikigongwa mbele ya:- ACLAND DOMINIC KAMBILI Mkugenzi Mtendaji /Mkurugenzi wa Halmashauri Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza JACKSON FREDRICK MATESO Meya/Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya Uvinza NAKUBALI, / L.S Dodoma, MOHAMED OMARY MCHENGERWA (MB) 25 Machi, 2024 Waziri wa Nchi – Ofisi ya Rais (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa) 19
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Afya na Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza za Mwaka 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in