Sheria Ndogo ya Ushuru wa Mazao ya Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa ya Mwaka 2024
This section gives the bylaws their title: Kondoa District Council Produce Tax Bylaws, 2024.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Ushuru wa Mazao ya Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa ya Mwaka 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This section gives the bylaws their title: Kondoa District Council Produce Tax Bylaws, 2024. This section says the by-law applies throughout the area of the Kondoa District Council. This section defines key terms used in the bylaw, including officer, market place, council, produce, trader, buyer, seller, levy, and agent. Halmashauri lazima itoze na kukusanya ushuru wa mazao kwa viwango vya Jedwali la Kwanza; mnunuzi analipa ushuru na, akihitajika, aoneshe stakabadhi ya malipo kwa Afisa Mwidhiniwa. Mazao lazima yapimwe kwa mizani au kipimo kilichothibitishwa; mtu haruhusiwi kufunga, kuuza au kusafirisha mazao ya lumbesa, na mnunuzi haruhusiwi kupokea au kusafirisha mazao ambayo hayajalipiwa ushuru unaotakiwa.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Ushuru wa Mazao ya Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa ya Mwaka 2024
Showing 22 of 22
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya
AI-assisted research summary: This section gives the bylaws their title: Kondoa District Council Produce Tax Bylaws, 2024.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Ushuru wa Mazao ya Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa ya Mwaka 2024. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la
AI-assisted research summary: This section says the by-law applies throughout the area of the Kondoa District Council.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la Mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama muktadha
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the bylaw, including officer, market place, council, produce, trader, buyer, seller, levy, and agent.
3. Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni Afisa yeyote aliyeteuliwa na Mkurugenzi kwa lengo la kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “gulio” maana yake ni eneo maalumu au sehemu yoyote ya wazi au iliyotengwa na Halmashauri kwa ajili ya shughuli za kuuza na kununua mazao ya nafaka, misitu au bidhaa za viwandani kwa siku maalum; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa; “lumbesa” maana yake ni ufungashaji wa bidhaa za mazao kwa ujazo usiozingatia vipimo sahihi katika magunia au vifungashio; “mazao” maana yake ni mavuno yanayotokana na kilimo, misitu au uvuvi yanayozalishwa katika eneo la Halmashauri; “mfanyabiashara” maana yake ni mtu binafsi, taasisi, kampuni au kikundi cha watu wanaojishughulisha na shughuli za kuuza na kununua bidhaa au mazao kwa lengo la kupata faida; 1 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Mazao ya Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Tangazo la Serikali Na.490 (Linaendelea,) “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa au Afisa yeyote aliyeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi; “mnunuzi” maana yake ni mtu, kikundi cha watu, kampuni au shirika lolote linalonunua bidhaa au mazao katika eneo la Halmashauri; “muuzaji” maana yake ni mtu, kikundi cha watu, kampuni au shirika linalouza mazao katika eneo lililoidhinishwa na Halmashauri; “ushuru” maana yake ni tozo inayotozwa na Halmashauri kwa shughuli au huduma mbalimbali zinazofanywa katika eneo la Halmashauri; “Wakala” maana yake ni mtu binafsi, kampuni, kikundi cha watu au shirika lililoteuliwa kukusanya ushuru kwa niaba ya Halmashauri chini ya Sheria Ndogo hii. - 4 Verify source ↗
(1) Halmashauri itatoza na kukusanya ushuru wa
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima itoze na kukusanya ushuru wa mazao kwa viwango vya Jedwali la Kwanza; mnunuzi analipa ushuru na, akihitajika, aoneshe stakabadhi ya malipo kwa Afisa Mwidhiniwa.
4. -(1) Halmashauri itatoza na kukusanya ushuru wa mazao yatakayozalishwa katika eneo la Halmashauri kwa viwango vilivyoainishwa katika Jedwali la Kwanza. (2) Ushuru wa mazao utalipwa na mnunuzi kwa kuzingatia masharti ya Sheria Ndogo hii. (3) Baada ya kulipa ushuru mnunuzi atapewa stakabadhi ya malipo na atawajibika kuionesha kwa Afisa Mwidhiniwa atakapotakiwa kufanya hivyo. (4) Stakabadhi zitakazotolewa kwa malipo ya ushuru wa mazao zitakuwa za kielektroniki. (5) Malipo yote yatafanywa kwa Afisa Mwidhiniwa, benki au kwa Wakala atakayekuwa ameteuliwa na Halmashauri kwa ajili ya kazi hiyo. Ushuru wa mazao Matumizi ya vipimo sahihi mazao vya - 5 Verify source ↗
(1) Upimaji wa mazao utafanyika kwa mizani au
AI-assisted research summary: Mazao lazima yapimwe kwa mizani au kipimo kilichothibitishwa; mtu haruhusiwi kufunga, kuuza au kusafirisha mazao ya lumbesa, na mnunuzi haruhusiwi kupokea au kusafirisha mazao ambayo hayajalipiwa ushuru unaotakiwa.
5. -(1) Upimaji wa mazao utafanyika kwa mizani au kipimo chochote kingine kilichothibitishwa na Halmashauri au mamlaka nyingine iliyowekwa kisheria. (2) Mtu hataruhusiwa kufunga, kuuza au kusafirisha mazao yaliyofungwa kwa lumbesa. (3) Mnunuzi hataruhusiwa kupokea au kusafirisha mazao ambayo hayajalipiwa ushuru kwa kiwango kilichoainishwa chini ya Sheria Ndogo hii. Uteuzi wa Wakala - 6 Verify source ↗
Halmashauri inaweza kumteaua mtu binafsi, kikundi,
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kumteua mtu, kikundi, kampuni au taasisi kuwa wakala wa kukusanya ushuru, na wakala huyo lazima atekeleze masharti yote ya kutoza ushuru yaliyowekwa na Sheria Ndogo hii.
6. Halmashauri inaweza kumteaua mtu binafsi, kikundi, 2 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Mazao ya Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Tangazo la Serikali Na.490 (Linaendelea,) kampuni au taasisi kuwa Wakala wa kukusanya ushuru chini ya Sheria Ndogo hii na Wakala huyo atawajibika kutekeleza masharti yote ya kutoza ushuru yaliyoainishwa na Sheria Ndogo hii. Wajibu wa Wakala - 7 Verify source ↗
Wakala aliyeteuliwa chini ya kifungu cha 6 atakuwa
AI-assisted research summary: A designated agent under section 6 must submit collected levy amounts to the Council, collect the levy at the approved rate, report refusals or evasion, and advise the Council on levy collection.
7. Wakala aliyeteuliwa chini ya kifungu cha 6 atakuwa na wajibu wa- (a) kuwasilisha kwa Halmashauri kiasi cha ushuru alioukusanya; (b) kukusanya ushuru kwa kiwango kilichoidhinishwa katika Sheria Ndogo hii; (c) kutoa taarifa kwa Halmashauri kuhusiana na mtu yeyote ambaye amekataa au anakwepa kulipa ushuru; na (d) kuishauri Halmashauri ukusanyaji wa ushuru. namna ya kuboresha Rejesta ya wanunuzi wa mazao - 8 Verify source ↗
(1) Halmashauri itakuwa na Rejesta maalumu ya
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima iwe na rejesta maalumu ya wanunuzi wa mazao, na kila mnunuzi lazima ajisajili humo.
8. (1) Halmashauri itakuwa na Rejesta maalumu ya orodha ya wanunuzi wa mazao ndani ya eneo la Halmashauri na itakuwa ni wajibu wa kila mnunuzi kuhakikisha amejiandikisha kwenye rejesta hiyo. (2) Kila kijiji kitawajibika kutunza Rejesta yake kwa ajili ya kumbukumbu ya wanunuzi wa mazao kwenye eneo lake. Leseni ya biashara - 9 Verify source ↗
Mfanyabiashara atatakiwa kuwa na leseni ya biashara
AI-assisted research summary: A trader must have a business licence and a permit from the Council to do business in the Council area.
9. Mfanyabiashara atatakiwa kuwa na leseni ya biashara pamoja na kibali toka Halmashauri kitakachomruhusu kufanya biashara katika eneo la Halmashauri. Ushuru wa mazao misitu ya - 10 Verify source ↗
(1) Halmashauri itatoza ushuru kwa mazao ya misitu
AI-assisted research summary: Halmashauri itatoza ushuru kwa mazao ya misitu yanayosafirishwa ndani na nje ya Halmashauri, na mnunuzi lazima alipe ushuru kabla ya kusafirisha mazao; pia hairuhusiwi kusafirisha mazao ya misitu bila kibali maalumu.
10. -(1) Halmashauri itatoza ushuru kwa mazao ya misitu yatakayosafirishwa ndani na nje ya Halmashauri kwa viwango vilivyoorodheshwa katika Jedwali la Pili. (2) Ushuru wa mazao utalipwa kwa Afisa Mwidhiniwa au Wakala aliyeteuliwa kukusanya ushuru kwa niaba ya Halmashauri na utalipwa kabla ya mnunuzi kusafirisha mazao yake. (3) Mnunuzi hataruhusiwa kusafirisha mazao ya misitu bila kuwa na kibali maalumu kwa shughuli hiyo. (4) Kibali kitaonesha jina la mnunuzi, aina ya mazao aliyonunua, sehemu yaliponunuliwa na maoni ya Halmashauri. 3 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Mazao ya Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Tangazo la Serikali Na.490 (Linaendelea,) Ushuru wa uvuvi wa samaki - 11 Verify source ↗
(1) Halmashauri itatoza ushuru wa uvuvi wa samaki
AI-assisted research summary: Halmashauri must charge fishing tax on fish caught in ponds within its area at the rates set out in the Third Schedule.
11.-(1) Halmashauri itatoza ushuru wa uvuvi wa samaki watakaovuliwa katika mabwawa yaliyopo ndani ya eneo lake kwa viwango vilivyoainishwa katika Jedwali la Tatu. (2) Samaki wabichi na waliokaushwa watapimwa katika mizani ili kupata uzito kabla ya kulipiwa ushuru. Uanzishaji wa masoko - 12 Verify source ↗
Kila kijiji ndani ya Halmashauri kitatenga eneo
AI-assisted research summary: Kila kijiji ndani ya Halmashauri lazima kitenge eneo maalumu la biashara ya bidhaa au mazao, na kila mfanyabiashara lazima auze bidhaa au mazao yake katika eneo hilo.
12. Kila kijiji ndani ya Halmashauri kitatenga eneo maalumu kwa ajili ya biashara ya bidhaa au mazao na kila mfanyabiashara atauzia bidhaa au mazao yake katika eneo hilo. Ushuru wa trekta - 13 Verify source ↗
(1) Kila trekta litakaloingizwa au kutumika kwa
AI-assisted research summary: Tractors used or brought in for farming in the council area must get a permit and pay tax, and the permit is issued by specified local officers.
13.-(1) Kila trekta litakaloingizwa au kutumika kwa shughuli za kilimo katika eneo la Halmashauri litapaswa kuombewa kibali na kulipiwa ushuru. (2) Kibali kitatolewa na Afisa Mwidhiniwa, mtendaji wa Kata au mtendaji wa Kijiji. (3) Malipo ya ushuru wa trekta yatafanyika kwa kila msimu wa kilimo na yatakuwa katika kiwango kilichoainishwa katika Jedwali la Nne. Muda wa Kusafirisha mazao - 14 Verify source ↗
(1) Mnunuzi atatakiwa kusafirisha mazao kuanzia
AI-assisted research summary: Mnunuzi lazima asafirishe mazao ndani ya saa zilizoainishwa, na akikiuka muda huo lazima aombe kibali na awe amelipa ushuru kwanza.
14. -(1) Mnunuzi atatakiwa kusafirisha mazao kuanzia saa 1:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni. (2) Mnunuzi atakayesafirisha mazao kinyume na muda ulioainishwa chini ya kanuni ndogo ya (1) atapaswa kuomba kibali kwa mtendaji wa kijiji au kata na kabla ya kuomba kibali hicho awe amelipia ushuru kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. Makosa - 15 Verify source ↗
(1) Mnunuzi anatenda kosa ikiwa
AI-assisted research summary: This section says a buyer, seller, or agent commits an offence if they do certain acts related to produce, tax payment, licences, receipts, or reporting.
15.-(1) Mnunuzi anatenda kosa ikiwa (a) anasafirisha mazao yaliyonunuliwa kabla ya kulipa ushuru; (b) anasafirisha mazao wakati wa usiku; (c) anasafirisha mazao bila kulipia ushuru; (d) ananunua mazao bila kuwa na leseni na kibali; au (e) anakataa kuonesha stakabadhi ya malipo aliyolipia ushuru kwa Afisa Mwidhiniwa; (f) anampa mtu, kampuni, taasisi, kikundi au Wakala mwingine kibali chake; au (g) anafungasha au kusafirisha mazao katika mtindo wa lumbesa. (2) Muuzaji anatenda kosa ikiwa- (a) anauza mazao katika maeneo yasiyoruhusiwa au 4 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Mazao ya Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Tangazo la Serikali Na.490 (Linaendelea,) kutengwa kwa shughuli hiyo; au (b) anafanya jambo lolote litakalosababisha Mnunuzi kukwepa kulipa Ushuru. (3) Wakala anatenda kosa ikiwa- (a) anachelewa kuwasilisha ushuru kwa Halmashauri; (b) anatoa taarifa za uongo kuhusu idadi ya watu, kampuni au taasisi wanaolipa Ushuru na thamani yake; (c) anawasilisha kwa Halmashauri kiwango kidogo cha fedha kinyume na makubaliano; au (d) anamshawishi mtu, kikundi, kampuni au taasisi kutolipa ushuru. Adhabu. Kufifilisha kosa - 16 Verify source ↗
Mtu atakayetiwa hatiani kwa kutenda kosa kinyume
AI-assisted research summary: A person convicted of an offence against this bylaw must pay a fine, go to prison, or both.
16. Mtu atakayetiwa hatiani kwa kutenda kosa kinyume cha Sheria Ndogo hii atawajibika kulipa faini ya kiasi kisichopungua shilingi laki mbili na isiyozidi shilingi milioni moja au kifungo kisichopungua miezi kumi na mbili na kisichozidi miezi ishirini na nne au vyote. - 17 Verify source ↗
Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha kosa
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa kwa kumtoza mtenda kosa shilingi laki mbili, ikiwa anakiri kosa, yuko tayari kujaza fomu maalumu ya Jedwali la Tano, na kulipa ada au ushuru unaodaiwa.
17. Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha kosa kwa kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa kinyume cha Sheria Ndogo hii kiasi cha shilingi laki mbili endapo mkosaji atakiri kosa na kuwa tayari kujaza fomu maalumu iliyoainishwa katika Jedwali la Tano la Sheria Ndogo hii na kulipa ada au ushuru anaodaiwa. Kufutwa T. S Na.177 la 2013
Part
Jedwali la Tano la Sheria Ndogo hii na kulipa ada au ushuru
- 18 Verify source ↗
Sheria Ndogo za (Ushuru wa Mazao) za Halmashauri
AI-assisted research summary: The 2013 Kondoa District Council by-laws on crop tax are repealed.
18. Sheria Ndogo za (Ushuru wa Mazao) za Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa za Mwaka, 2013 zinafutwa. 5 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Mazao ya Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Tangazo la Serikali Na.490 (Linaendelea,) AINA YA MAZAO Mahindi Alizeti Ufuta Maharage NA. - 17 Verify source ↗
Mashudu
AI-assisted research summary: This section lists tax rates for different agricultural products and package sizes.
17. Mashudu ________ JEDWALI LA KWANZA ______ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 4(1)) USHURU WA MAZAO KIWANGO CHA USHURU Tshs. 1,000/= Kwa gunia la Kg 100 Tshs. 1,000/= Kwa gunia la Kg 65 Tshs. 1,500/= Kwa gunia la Kg 100 Tshs. 2,000/= Kwa gunia la Kg 100 Tshs. 1,000/= Kwa gunia la Kg 100 Tshs. 2,000/= kwa gunia la Kilo 100 Tshs. 2,000/= kwa gunia la Kilo 100 Tshs. 1,000/= kwa gunia la Kilo 100 Tshs. 1,000/= Kwa gunia la Kg 100 Tshs. 6,000/= Kwa kila tani Tshs. 500/= Kwa Mkungu Tshs. 1,000/= kwa kiroba Tshs. 1,500/= kwa gunia Tshs. 1,000/= kwa tenga Tshs. 200/= Kwa gunia la Kg 100 Tshs. 1,000/=kwa Ndoo ya Lita 20 Tshs. 500/= kwa gunia _________ JEDWALI LA PILI _________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 10(1)) USHURU WA MAZAO YA MISITU NA. AINA YA BIDHAA
Part
JEDWALI LA PILI
- 5 Verify source ↗
Section 5
AI-assisted research summary: This table sets ushuru amounts for specific goods, including hardwood timber, softwood timber, charcoal, honey, and wax.
5. Mbao za miti migumu Mbao za miti laini Mkaa Asali Nta UJAZO Kila ubao mmoja Kila ubao mmoja Gunia moja Kwa kila -Lita 20 Kwa Ndoo ya Lita 20 USHURU Tshs. 2,000/= Tshs. 1,000/= Tshs. 2,000/= Tshs. 5,000/= Tshs. 500/= 6 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Mazao ya Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Tangazo la Serikali Na.490 (Linaendelea,) _______ JEDWALI LA TATU ________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 11(1)) NA.
Part
JEDWALI LA TATU
- 2 Verify source ↗
Section 2
AI-assisted research summary: This provision lists tax rates for fish products: fresh fish at Tshs. 500 per kilo and dry fish at Tshs. 300 per kilo.
2. AINA YA USHURU Ushuru wa Samaki Wabichi Ushuru wa Samaki wakavu USHURU WA MAZAO YA UVUVI NA SAMAKI KIASI CHA USHURU Tshs. 500/= kwa kilo Tshs. 300/= kwa kilo _______ JEDWALI LA NNE ________ (Limetengenezwa chini kanuni ya 13(3)) USHURU WA TREKTA NA
Part
JEDWALI LA NNE
- 1 Verify source ↗
Section 1
AI-assisted research summary: Ushuru wa kuingiza trekta kwa shughuli za kilimo ni Tshs 30,000 kwa msimu wa kilimo.
1. AINA YA USHURU Ushuru wa kuingiza Trekta kwa shughuli za kilimo KIASI CHA USHURU Tshs. 30,000/= kwa msimu wa Kilimo 7 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Mazao ya Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Tangazo la Serikali Na.490 (Linaendelea,) _________ JEDWALI LA TANO _______ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 17) HATI YA KUKIRI NA KUFIFILISHA KOSA Mimi ......................................................wa S.L.P .................................. Namba ya Simu: ................................... Nakiri kwa hiari yangu mwenyewe mbele ya ............................... ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa, kwamba mnamo tarehe ..................ya Mwezi ......................... Mwaka ..................... nilitenda kosa la kukiuka masharti ya kanuni ya .................. ya Sheria Ndogo ya Ushuru wa Mazao ya Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa ya Mwaka 2024. Kwa mamlaka aliyopewa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri, niko tayari kulipa kiasi cha ada/ushuru ninaodaiwa pamoja na faini. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU. Leo tarehe ........................................ya Mwezi..................................Mwaka......................... Jina::.......................................................... Saini:......................................................................... MBELE YA: Jina:............................................................... Cheo:............................................................ Saini:............................................................. 8 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Mazao ya Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa Tangazo la Serikali Na.490 (Linaendelea,) Lakiri ya Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa imegongwa kwenye Sheria Ndogo hii kufuatia Azimio lililopitishwa katika Mkutano wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa uliofanyika tarehe 28/4/2022 na kushuhudiwa Lakiri hiyo ikigongwa mbele ya:- SHABANI KAPALA MILLAO, Mkurugenzi Mtendaji (w), Halmashauri ya Wilaya Kondoa ABDALLAH SALUM MAGUO, Mwenyekiti, Halmashauri ya Wilaya Kondoa L.S NAKUBALI, Dodoma, 25 Machi, 2024 MOHAMED OMARY MCHENGERWA, Waziri wa Nchi-OR-Tamisemi 9
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Ushuru wa Mazao ya Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa ya Mwaka 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in