Sheria Ndogo ya Ushuru wa Nyumba za Kulala Wageni ya Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto ya mwaka 202
This section gives the short title of the by-law.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Ushuru wa Nyumba za Kulala Wageni ya Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto ya mwaka 202
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This section gives the short title of the by-law. This by-law applies throughout the entire area of Lushoto District Council. This section defines key terms used in the by-law, including the appointed officer, the council, the Director, guesthouse tax payer, owner, guest, guesthouse accounts, accounting period, returns, and agent. Halmashauri lazima itozeshe na kukusanya ushuru wa nyumba ya kulala wageni kwa kiwango cha asilimia 10 ya mapato ya kila mwezi kutoka kwa kila mmiliki. Mmiliki wa nyumba ya kulala wageni lazima alipe ushuru kwa Halmashauri kwa wakati, aweke nyumba ikiwa safi, atumie daftari la wageni, atoe stakabadhi ya kielektroniki, alipe leseni kwa wakati, aweke nyaraka wazi wakati wa ukaguzi, asajili kila mgeni, na asiruhusu kitanda kutumiwa na wageni wawili au zaidi wa jinsia moja.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Ushuru wa Nyumba za Kulala Wageni ya Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto ya mwaka 202
Showing 14 of 14
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo
AI-assisted research summary: This section gives the short title of the by-law.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Ushuru wa Nyumba za Kulala Wageni ya Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto ya mwaka 2024. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la
AI-assisted research summary: This by-law applies throughout the entire area of Lushoto District Council.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la Mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the by-law, including the appointed officer, the council, the Director, guesthouse tax payer, owner, guest, guesthouse accounts, accounting period, returns, and agent.
3. Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni afisa yeyote aliyeteuliwa na Mkurugenzi kwa madhumuni ya kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto; “hesabu za mwisho” maana yake ni hesabu za mwisho wa mwezi zinazowasilishwa na mmiliki wa nyumba ya kulala wageni baada ya kipindi cha hesabu pamoja na nyaraka au maelezo yatakayotakiwa kutolewa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii; “kipindi cha hesabu” maana yake ni muda ambao mmiliki anatakiwa wa nyumba ya kulala wageni kuwasilisha hesabu za biashara yake; “marejesho” maana yake ni taarifa inayotaja jina la nyumba ya kulala wageni, aina ya vyumba, 1 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Nyumba Za Kulala Wageni ya Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto Tangazo la Serikali Na.502 (Linaendelea.) gharama ya kila aina ya chumba, jumla ya vyumba vilivyopangishwa ikiwa ni pamoja na ushuru unaopaswa kulipwa kwa mwezi husika. “mgeni” maana yake ni mtu yeyote ambaye analipa pango la kukaa kwenye chumba cha kulala wageni ama kwa siku nzima au sehemu ya siku; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto au afisa yeyote aliyeteuliwa kutekeleza kazi za Mkurugenzi chini ya Sheria Ndogo hii; “mlipa ushuru wa nyumba ya kulala wageni” maana yake ni mtu binafsi au kampuni inayomiliki nyumba ya kulala wageni inayopaswa kuwa na leseni ya kufanya biashara ya kutoa huduma ya malazi katika eneo la Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto; “mmiliki” inajumuisha mtu yeyote aliyepewa jukumu la kusimamia nyumba ya kulala wageni au hoteli au mwajiriwa au mtu yeyote anayehusika kukusanya gharama za pango kutoka kwa mgeni kutokana na kulala kwenye nyumba ya kulala wageni; jengo la kupata kipato au faida, “nyumba ya kulala wageni” maana yake ni jengo lililojengwa kwa ajili ya kupokea wageni kwa lengo isipokuwa la kupumzikia viongozi wa mabweni, Serikali na jengo lililosajiliwa chini ya Sheria ya Utalii kwa ajili ya kutoa huduma kwa watalii; “Wakala” maana yake ni mtu binafsi au kikundi cha watu, limeteuliwa na kampuni au shirika ambalo Halmashauri kufanya kazi yoyote chini ya Sheria Ndogo hii kwa niaba yake. Wajibu wa Halmashauri Wajibu wa mmiliki wa - 4 Verify source ↗
Halmashauri itatoza na kukusanya ushuru wa
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima itozeshe na kukusanya ushuru wa nyumba ya kulala wageni kwa kiwango cha asilimia 10 ya mapato ya kila mwezi kutoka kwa kila mmiliki.
4. Halmashauri itatoza na kukusanya ushuru wa nyumba ya kulala wageni kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii kutoka kwa kila mmiliki wa nyumba ya kulala wageni kwa kiwango cha asilimia kumi ya mapato ya nyumba ya kulala wageni kwa mwezi husika. - 5 Verify source ↗
Kila mmiliki wa nyumba ya kulala wageni
AI-assisted research summary: Mmiliki wa nyumba ya kulala wageni lazima alipe ushuru kwa Halmashauri kwa wakati, aweke nyumba ikiwa safi, atumie daftari la wageni, atoe stakabadhi ya kielektroniki, alipe leseni kwa wakati, aweke nyaraka wazi wakati wa ukaguzi, asajili kila mgeni, na asiruhusu kitanda kutumiwa na wageni wawili au zaidi wa jinsia moja.
5. Kila mmiliki wa nyumba ya kulala wageni atahakikisha kuwa- 2 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Nyumba Za Kulala Wageni ya Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto Tangazo la Serikali Na.502 (Linaendelea.) nyumba ya kulala wageni (a) analipa ushuru wa nyumba ya kulala wageni kwa Halmashauri kila ifikapo tarehe moja na si zaidi ya tarehe tano ya mwezi ikiwa ni ushuru wa mwezi ulioisha; (b) nyumba ya kulala wageni inakuwa safi muda usafi na masharti mengine ya wote yanazingatia; (c) ana kitabu alichopata kutoka Halmashauri kwa ajili ya kuandika orodha ya wageni na wote kukitumia wanaoingia na kulala kila siku; kuorodhesha wageni Mlipa ushuru kuwasilisha taarifa ya hesabu za mwisho wa mwezi (d) anatoa stakabadhi ya kieletroniki baada ya kupokea malipo; (e) analipa ada ya leseni ya biashara ya nyumba ya kulala wageni ndani ya muda uliowekwa kwa mujibu wa sheria; (f) anaweka wazi vitabu vya kumbukumbu vya wageni na nyaraka nyingine wakati wa ukaguzi; (g) kila mgeni anasajiliwa kwenye daftari la kulala wageni kwa kuingiza taarifa zote muhimu bila kujali muda aliokitumia chumba; na (h) kitanda hakiruhusiwi kutumika na wageni wawili au zaidi wa jinsia moja. - 6 Verify source ↗
(1) Kila mlipa ushuru wa nyumba ya kulala
AI-assisted research summary: Mlipa ushuru wa nyumba ya kulala wageni lazima awe na daftari la kuandikisha wageni na awasilishe taarifa sahihi za wageni na ushuru kwa Halmashauri kila mwisho wa mwezi kwa kutumia fomu zilizotajwa.
6.-(1) Kila mlipa ushuru wa nyumba ya kulala wageni anatakiwa kuwa na daftari maalumu kwa ajili ya kuorodhesha wageni wanaoingia kupata huduma ya malazi. (2) Kila mlipa ushuru atatakiwa kuwasilisha kwa Halmashauri taarifa sahihi ya idadi ya wageni kwa kila chumba kilichopangishwa pamoja na ushuru wa nyumba ya kulala wageni kwa kila mwisho wa mwezi kwa kutumia fomu Na. H.L 1, H.L 2 na H.L 3 kama zilivyoainishwa katika Jedwali la Kwanza la Sheria Ndogo hii. (3) Endapo itabainika kuwa kuna mgeni au wageni ambao hawajaorodheshwa katika daftari maalumu la wageni, Halmashauri itakuwa na mamlaka ya kumtoza mmiliki wa nyumba ya kulala wageni ushuru kwa kiwango cha idadi ya vyumba vyote vya nyumba husika. 3 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Nyumba Za Kulala Wageni ya Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto Tangazo la Serikali Na.502 (Linaendelea.) Leseni ya kuendesha biashara ya nyumba ya kulala wageni - 7 Verify source ↗
Leseni ya kuendesha biashara ya nyumba ya
AI-assisted research summary: Leseni ya kuendesha biashara ya nyumba ya kulala wageni itatolewa tu baada ya Halmashauri kujiridhisha kuwa jengo linakidhi masharti ya usafi, usalama, vifaa, vyoo, mabafu na huduma za wafanyakazi.
7. Leseni ya kuendesha biashara ya nyumba ya kulala wageni itatolewa baada ya Halmashauri kujiridhisha kuwa jengo hilo- (a) lina mwanga na hewa ya kutosha; (b) lina nafasi, vifaa na samani za kutosha; (c) linafanyiwa usafi wa jumla wa jengo na vifaa vyake; (d) lina mfumo wa uondoshaji wa maji taka na taka ngumu wa kuaminika; (e) lina vyoo na mabafu kwa jinsia zote; (f) lina vifaa vya kuzima moto; (g) lina tanki la kuhifadhia maji safi; (h) lina vyoo na bafu vilivyosakafiwa vema kwa vigae au marumaru na kuta zake zimewekwa vigae kiasi cha futi sita kutoka usawa wa sakafu; (i) kwa katika kila kitanda, kuna jozi zaidi ya mbili za mashuka, foronya za mito na magodoro na ziwe na rangi isiyoficha uchafu; (j) lina sehemu maalumu ya kufulia na kuanikia nguo; na (k) lina stoo na chumba cha kubadilishia nguo kwa ajili ya wafanyakazi. Mamlaka ya kuitisha taarifa - 8 Verify source ↗
Mkurugenzi anaweza kutaka taarifa kimaandishi
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kuomba taarifa kwa maandishi kutoka kwa mtu au taasisi yoyote inayopaswa kulipa ushuru wa nyumba ya kulala wageni.
8. Mkurugenzi anaweza kutaka taarifa kimaandishi kwa mtu yeyote au taasisi yoyote inayopaswa kulipa ushuru wa nyumba ya kulala wageni kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. Uteuzi wa Wakala - 9 Verify source ↗
Halmashauri
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kuteua Wakala wa kukusanya ushuru wa nyumba ya kulala wageni kwa niaba yake.
9. Halmashauri inaweza kuteua Wakala wa kukusanya ushuru wa nyumba ya kulala wageni kwa niaba yake. Majukumu ya Wakala - 10 Verify source ↗
Wakala aliyeteuliwa na Halmashauri atakuwa
AI-assisted research summary: The appointed agent must ensure the guesthouse owner uses a special guest register and must remit collected tax on time under the contract.
10. Wakala aliyeteuliwa na Halmashauri atakuwa na majukumu yafuatayo: (a) kuhakikisha kuwa mmiliki wa nyumba ya kulala wageni anatumia daftari maalumu la kuandikisha wageni; na 4 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Nyumba Za Kulala Wageni ya Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto Tangazo la Serikali Na.502 (Linaendelea.) (b) kuwasilisha ushuru aliokusanya kwa wakati katika kipindi maalumu kwa mujibu wa mkataba wake. Mamlaka ya kuingia kwenye jengo - 11 Verify source ↗
(1) Afisa Mwidhiniwa anaweza kuingia
AI-assisted research summary: An authorized officer may enter a guest house at specified hours to inspect guest registers and related information, and may also enter after working hours if needed to investigate guest numbers and the tax payable.
11.-(1) Afisa Mwidhiniwa anaweza kuingia kwenye nyumba ya kulala wageni kuanzia saa kumi kamili jioni hadi saa sita kamili usiku kwa lengo la kufanya ukaguzi na tathmini ya usahihi wa uandikishaji wageni katika vitabu vya wageni na taarifa nyingine zozote. (2) Bila kujali kanuni ndogo ya (1), Afisa Mwidhiniwa anaweza kuingia kwenye nyumba ya kulala wageni baada ya muda wa kazi kwa lengo la kufanya ukaguzi na tathmini ya usahihi wa uandikishaji wageni katika vitabu vya wageni na taarifa nyingine zozote kama atakavyoona inafaa kufanyiwa uchunguzi kwa ajili ya kupata na kujua idadi sahihi ya wageni na ushuru anaotakiwa kulipa. Kiwango cha ulipaji wa ushuru wa nyumba ya kulala wageni na riba - 12 Verify source ↗
(1) Kila mlipa ushuru wa nyumba ya kulala
AI-assisted research summary: Mlipa ushuru wa nyumba ya kulala wageni anatakiwa kulipa ushuru wa asilimia 10 ya mapato yake kila tarehe 1 ya mwezi unaofuata.
12.-(1) Kila mlipa ushuru wa nyumba ya kulala wageni anapaswa kulipa ushuru katika kiwango cha asilimia kumi ya mapato ya nyumba ya kulala wageni kila tarehe moja ya mwezi unaofuata. (2) Ushuru ambao hautalipwa kwa wakati utatozwa riba ya asilimia ishirini na tano ya ushuru uliopaswa kulipwa kwa mwezi husika. Makosa na adhabu - 13 Verify source ↗
(1) Mtu ambaye
AI-assisted research summary: A person who blocks an officer from carrying out duties under these by-laws commits an offence and may be fined or imprisoned.
13.-(1) Mtu ambaye- (a) anashindwa kuwasilisha ushuru wa nyumba ya kulala wageni na hesabu sahihi kulingana na idadi ya wageni waliopata huduma katika nyumba ya kulala wageni; (b) anashindwa kuwasilisha nyaraka, maelezo au taarifa inayotakiwa kuwasilishwa Halmashauri katika muda uliowekwa; (c) anashindwa kuonesha kumbukumbu yoyote au nyaraka kwa ajili ya ukaguzi wa hesabu zake; (d) anashindwa kuandaa au kutengeneza hesabu au kumbukumbu zozote za nyumba za kulala au wageni kuandaliwa anaelekeza au 5 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Nyumba Za Kulala Wageni ya Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto Tangazo la Serikali Na.502 (Linaendelea.) kutengenezwa kitabu cha wageni, hesabu au kumbukumbu zozote za nyumba za kulala wageni zisizo sahihi; (e) anashindwa kuwasilisha taarifa sahihi kuhusu idadi ya wageni katika nyumba yake ya kulala wageni; (f) anashindwa kutumia daftari maalumu la kuandikishia wageni; au (g) anashindwa kuandaa na kutunza kumbukumbu sahihi kwenye kitabu au daftari alilopewa na Halmashauri kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii; au (h) anamzuia au kumzuia Afisa kujaribu Mwidhiniwa kutekeleza majukumu yake aliyopewa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii, Kufifilisha kosa anatenda kosa na akipatikana na hatia atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi laki mbili na isiyozidi shilingi milioni moja au kifungo kisichopungua miezi kumi na mbili na kisichozidi miezi ishirini na nne au vyote. - 14 Verify source ↗
Mkurugenzi anaweza kumtoza mtu yeyote kiasi
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kumtoza mtu yeyote shilingi 200,000 mtu huyo akikiri kosa kwa fomu ya Jedwali la Pili na kulipa ushuru anaodaiwa au kukubali kutekeleza wajibu wake.
14. Mkurugenzi anaweza kumtoza mtu yeyote kiasi cha shilingi laki mbili iwapo mtu huyo atakiri kosa kwa kujaza fomu iliyoainishwa katika Jedwali la Pili la Sheria Ndogo hii na kulipa kiasi cha ushuru anachodaiwa au kukubali kutekeleza wajibu wake chini ya Sheria Ndogo hii. 6 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Nyumba Za Kulala Wageni ya Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto Tangazo la Serikali Na.502 (Linaendelea.) _____________ JEDWALI LA KWANZA ______________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 6(2)) TAARIFA YA HESABU FOMU H.L.1 ………………………..……………… ………………………… Jina la nyumba ya kulala wageni Siku ambayo marejesho Jumla gharama ya Maoni kila Gharama kwa chumba (ukijumlisha za gharama Kifungua kinywa chakula na Aina vyumba ya Jumla vyumba ya Vyumba vilivyopang ishwa Chumba cha mmoja mtu Chumba cha watu wawili Chumba cha watu watatu Upande Vinginevyo (Eleza) Jumla 7 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Nyumba Za Kulala Wageni ya Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto Tangazo la Serikali Na.502 (Linaendelea.) FOMU H.L.2 MAREJESHO YA MWEZI Kwa Mkurugenzi Marejesho kwa ajili ya mwezi wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto. ……………..20…….. Kutoka: ……………………………………… (Jina la nyumba ya kulala wageni) Anuani: …………………………………….. ……………………………………. ……………………………………. Aina Vyumba ya ya Jumla vyumba Vilivyopangish wa kwa mwezi Jumla ya tozo ya ushuru wa nyumba ya kulala wageni kwa mwezi Maoni cha cha cha Chumba mtu mmoja Chumba watu wawili Chumba watu watatu Upande Vinginevyo (Eleza) Jumla Jumla ya tozo ya ushuru kwa mwezi Tsh…………………………….. Kiwango cha tozo kinachotumika……………………………………. Kiasi cha kodi kinachodaiwa Tsh. …………………………………….. Pamoja na marejesho hayo, tafadhali pokea kiasi cha pesa taslim/cheki Na………….. ya kiasi cha Tsh. ………..…………….. Nathibitisha kwamba maelezo haya ni ya kweli na kiasi cha ushuru wa nyumba ya kulala wageni unaodaiwa kimekokotolewa kwa mujibu wa Sheria Ndogo za Ushuru wa Nyumba za kulala Wageni za Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto. Tarehe: ……………… Sahihi: …………………. Mmiliki wa nyumba ya kulala wageni KWA MATUMIZI YA OFISI TU Tarehe iliyopokelewa : ……………… Marejesho yamekaguliwa na: 8 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Nyumba Za Kulala Wageni ya Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto Tangazo la Serikali Na.502 (Linaendelea.) Ndg… ……………………………… Maoni: ……………………………… Exchequer Receipt Voucher Tarehe:……………………………… No. ………………… Sahihi:……………………………….. FOMU H.L.3 TAARIFA ZA HOTELI Kwa Mkurugenzi, Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto. S.L.P 32, Lushoto. (Iwasilishwe nakala tatu) Jina la nyumba ya kulala wageni ……………………………………… Anuani: ………………… Simu Na: ……..…………………………… Aina ya Umiliki: Weka alama √ Binafsi Ubia Kampuni Aina nyingine (Eleza) Idadi ya Vyumba ……………… Idadi ya Vitanda ……………… Huduma zitolewazo na nyumba ya kulala wageni: Jaza neno - Ndiyo au Hapana Kifungua kinywa Chakula Huduma nyingine (Eleza) ……..………………………………………………… Nyaraka na Vitabu vya hesabu vinatunzwa katika nyumba ya kulala wageni: Weka alama √ Ndiyo Hapana Taarifa za Mmiliki wa nyumba ya kulala wageni: Jina: ……………………………………………. Wadhfa: ………………………………………… Anuani: ………………………………………… Idadi ya Waajiriwa: ……………………………. 9 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Nyumba Za Kulala Wageni ya Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto Tangazo la Serikali Na.502 (Linaendelea.) Saini; …………………………………………. Malipo ya kawaida kwa makazi kwa siku. Maelezo Idadi ya vyumba Maoni Chumba cha mtu mmoja. Tsh. ………… ……………….. …………………… Chumba cha watu wawili. Tsh. ……… ………………… ……….…………… Upande. Tsh. ………… Vyumba vingine: ………. ………………… ………………... ……………………. ……..…………… Tamko: Mimi/sisi …………………………………ninatamka/tunatamka kwamba taarifa nilizotoa/ tulizotoa ni sahihi na zimekamilika na kwamba nitakutaarifu/tutakutaarifu iwapo kutatokea mabadiliko yeyote. …………………... ……………………………………… Tarehe muhuri wa ofisi na saini KWA MATUMIZI YA OFISI TU Kiwango kinachotumika kwa nyumba ya kulala wageni: ……………………… Tarehe: …………………………………. …………………………… Saini 10 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Nyumba Za Kulala Wageni ya Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto Tangazo la Serikali Na.502 (Linaendelea.) ___________ JEDWALI LA PILI ____________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 14) FOMU YA KUFIFILISHA KOSA Mimi…………………………………………. nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya …………………………ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto kwamba mnamo Tarehe……………ya Mwezi…………….. Mwaka ……………………….nilitenda kosa la kukiuka masharti ya kanuni ya ………… Sheria Ndogo ya Ushuru wa Nyumba za Kulala Wageni ya Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto ya Mwaka 2024. Kwa Mamlaka aliyopewa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto, niko tayari kulipa kiasi cha ushuru ninachodaiwa pamoja na faini badala ya kushtakiwa mahakamani. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA MIMI MWENYEWE KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU Leo tarehe…………… ya Mwezi…………… Mwaka ………..…. Jina………………………….…………………..….. Saini…………………………..………………..…. MBELE YA: Jina……………………………………….. Cheo……………………………………… Saini……..……………………………….. Tarehe: …………………………………. 11 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Nyumba Za Kulala Wageni ya Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto Tangazo la Serikali Na.502 (Linaendelea.) Lakiri ya Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto imebandikwa katika hizi Sheria Ndogo za Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto kufuatia Azimio la kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto kilichofanyika tarehe 12/5/2023 na kushuhudiwa, Lakiri imebandikwa mbele ya:- IKUPA H. MWASYOGE, Mkurungenzi mtendaji, Halmashauri ya Wilaya, Lushoto MATHEW MBARUKU, Mwenyekiti, Halmashauri ya wilaya, Lushoto L.S NAKUBALI, Dodoma, MOHAMED OMARY MCHENGERWA (MB.), 25 Machi, 2024 Waziri wa Nchi -OR-Tamisemi, 12
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Ushuru wa Nyumba za Kulala Wageni ya Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto ya mwaka 202
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in