Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa ya Mwaka 2024
This section says the by-law is to be known as the Nyasa District Council Service Levy By-law, 2024.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa ya Mwaka 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This section says the by-law is to be known as the Nyasa District Council Service Levy By-law, 2024. Sheria Ndogo hii inatumika katika eneo lote la Mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa. This section defines key terms used in the by-law, including the service levy, service levy payer, Council, Director, officer, final accounts, and agent. Halmashauri must charge and collect a service levy from business-licence holders, at 0.3% of sales after VAT and excise for those who submit sales accounts to the Tanzania Revenue Authority, and at the First Schedule rate for those who do not. Mlipa ushuru wa huduma lazima alipe ushuru, awasilishe taarifa na hesabu sahihi, ahifadhi kumbukumbu, na aonyeshe nyaraka kwa uchunguzi.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa ya Mwaka 2024
Showing 14 of 14
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria
AI-assisted research summary: This section says the by-law is to be known as the Nyasa District Council Service Levy By-law, 2024.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa ya Mwaka 2024. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote
AI-assisted research summary: Sheria Ndogo hii inatumika katika eneo lote la Mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la Mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the by-law, including the service levy, service levy payer, Council, Director, officer, final accounts, and agent.
3. Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “afisa mwidhiniwa” maana yake ni afisa yeyote aliyeteuliwa na Mkurugenzi kwa lengo la kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa; “hesabu za mwisho” maana yake ni hesabu za mwisho zinazowasilishwa na Taasisi yoyote ya kibiashara baada ya kipindi cha hesabu pamoja au maelezo nyaraka yatakayotakiwa kutolewa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii; na “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa au afisa yeyote aliyeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi chini ya Sheria Ndogo hii; 1 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Tangazo la Serikali Na.504 (Linaendelea.) “mlipa ushuru wa huduma” maana yake ni mtu mwenye leseni anayefanya shughuli zake katika eneo la Halmashauri; “ushuru wa huduma” maana yake ni ushuru unaotozwa na kukusanywa na Halmashauri kutoka kwa mtu yeyote mwenye leseni ya biashara ambaye mauzo yake kwa mwaka ni zaidi ya shilingi milioni nne kutokana na huduma kutumia miundombinu ya umma inayomuwezesha kufanya la Halmashauri; anazopata biashara katika eneo na Ushuru wa huduma Wajibu wa mlipa ushuru wa huduma “Wakala” maana yake ni mtu ambaye ameteuliwa na Halmashauri kwa ajili ya kukusanya ushuru chini ya Sheria Ndogo hii kwa niaba ya Halmashauri. - 4 Verify source ↗
(1) Halmashauri
AI-assisted research summary: Halmashauri must charge and collect a service levy from business-licence holders, at 0.3% of sales after VAT and excise for those who submit sales accounts to the Tanzania Revenue Authority, and at the First Schedule rate for those who do not.
4.-(1) Halmashauri itatoza na kukusanya ushuru wa huduma kwa kiwango cha asilimia sifuri nukta tatu ya mauzo baada ya kutoa kodi ya ongezeko la thamani na ushuru wa bidhaa kutoka kwa mtu yeyote mwenye leseni ya biashara anayewasilisha hesabu za mauzo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania. (2) Bila kuathiri kanuni ndogo ya (1), itatoza na kukusanya ushuru wa Halmashauri huduma kwa kiwango kilichoainishwa katika Jedwali la Kwanza kutoka kwa mfanyabiashara mwenye leseni za biashara ambaye hawawasilishi hesabu za mauzo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania. - 5 Verify source ↗
(1) Kila mlipa ushuru wa huduma atakuwa
AI-assisted research summary: Mlipa ushuru wa huduma lazima alipe ushuru, awasilishe taarifa na hesabu sahihi, ahifadhi kumbukumbu, na aonyeshe nyaraka kwa uchunguzi.
5.-(1) Kila mlipa ushuru wa huduma atakuwa na wajibu wa- (a) kulipa ushuru wa huduma kwa kiwango kilichoainishwa katika Sheria Ndogo hii; (b) kuwasilisha taarifa sahihi za mauzo ya kila mwezi endapo anawasilisha taarifa za hesabu za mauzo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania; 2 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Tangazo la Serikali Na.504 (Linaendelea.) (c) kuwasilisha hesabu sahihi na za kweli; (d) kuwasilisha inayotakiwa Halmashauri katika muda uliowekwa; au kuwasilishwa nyaraka taarifa kwa (e) kutunza kumbukumbu za hesabu; na (f) kuonesha yoyote kumbukumbu au nyaraka kwa ajili ya uchunguzi. (2) Mlipa ushuru atalipa ushuru wa huduma si zaidi ya siku kumi na nne tangu tarehe ya kuwasilisha taarifa za mauzo ya kila mwezi. (3) Bila kuathiri kanuni ndogo ya (2), Halmashauri inaweza kukubaliana na mlipa ushuru utaratibu wa kulipa ushuru. (4) Mlipa kwa ushuru Halmashauri hesabu za mwisho katika kipindi cha miezi mitatu tangu kumalizika kwa kipindi cha hesabu. atawasilisha (5) Endapo mlipa ushuru hatawasilisha hesabu za mwisho kwa mwaka wa fedha husika na ametakiwa kufanya hivyo kwa notisi ya siku thelathini, Mkurugenzi kadiri atakavyoona inafaa, kufanya makadirio ya kiwango cha hesabu za mlipa ushuru huyo kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. anaweza kwa (6) Endapo mlipa ushuru hatawasilisha majumuisho ya hesabu zake kwa mwaka wowote wa mapato, na endapo Mkurugenzi au afisa mwidhiniwa anaona kwamba mlipa ushuru huyo ana wajibu wa kulipa ushuru kwa mwaka huo, anaweza kwa kadiri atakavyoona inafaa kufanya tathmini ya makadirio ya kiwango cha hesabu za mlipa ushuru huyo, isipokuwa tathmini hiyo haitaathiri wajibu wowote wa mlipa ushuru chini ya Sheria Ndogo hii, kwa kushindwa kwake kuwasilisha hesabu hizo. (7) Ushuru unaotokana na makadirio kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii utalipwa katika kipindi cha siku thelathini tangu tarehe ya kufanyika kwa makadirio hayo. 3 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Tangazo la Serikali Na.504 (Linaendelea.) Mamlaka ya Mkurugenzi - 6 Verify source ↗
(1) Endapo mlipa ushuru wa huduma
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kutoa notisi na maagizo yanayohusiana na taarifa za mauzo, taarifa za hesabu, ukaguzi wa kumbukumbu, na ukusanyaji wa ushuru wa huduma.
6.-(1) Endapo mlipa ushuru wa huduma anayetakiwa kuwasilisha taarifa ya mauzo chini ya Sheria Ndogo hii atashindwa kuwasilisha taarifa sahihi za mauzo kwa wakati, Mkurugenzi anaweza kutoa notisi ya kumtaka mlipa ushuru wa huduma kuwasilisha taarifa hiyo ndani ya siku thelathini kuanzia tarehe ya kutolewa kwa notisi. (2) Mkurugenzi anaweza kumtaka, kwa maandishi, mtu yeyote mwenye taarifa kuhusu mfanyabiashara anayepaswa kulipa ushuru wa huduma kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii kuwasilisha kwake taarifa ambazo zitatumika kama taarifa sahihi. (3) Mkurugenzi anaweza kumuagiza, kwa maandishi, afisa mwidhiniwa kuingia kwenye jengo au eneo la mlipa ushuru wa huduma kwa nia ya kufanya uchunguzi wa kumbukumbu za biashara, vitabu vya hesabu na taarifa kwa madhumuni ya kufanya tathmini ya kiwango sahihi cha ushuru anachotakiwa kulipa. (4) Mkurugenzi anaweza kumteua kamishna wa kodi ya forodha au kodi ya mapato kwa ajili ya kutathmini na kukusanya ushuru wa huduma na kuwasilisha Halmashauri kwa madhumuni ya kupata ushuru wa huduma pamoja na madeni yake. (5) Mkurugenzi, kwa notisi, anaweza kumtaka mlipa ushuru kuwasilisha taarifa za hesabu zikijumuisha taarifa kamili za shughuli za biashara zikionesha kiasi na thamani ya bidhaa au huduma zilizozalishwa, kutolewa, kusambazwa au kuuzwa pamoja na taarifa ya fedha ndani ya siku thelathini tangu tarehe ya notisi hiyo. (6) Mkurugenzi anaweza kutoa notisi ya siku saba kuwasilisha kumtaka mlipa kumbukumbu za biashara na vitabu vya hesabu kwa madhumuni ya kupata taarifa kwa ajili ya kufanya makadirio au kukusanya ushuru wa huduma. ushuru Uteuzi wa Wakala - 7 Verify source ↗
(1) Bila kuathiri masharti mengine katika
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kuteua wakala wa kukusanya ushuru kwa niaba ya Halmashauri, na wakala huyo lazima akusanye na kupokea ushuru katika eneo alilopangiwa na kwa viwango vilivyoidhinishwa.
7.-(1) Bila kuathiri masharti mengine katika Sheria Ndogo hii, Mkurugenzi anaweza kuteua 4 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Tangazo la Serikali Na.504 (Linaendelea.) Wakala wa kukusanya ushuru kwa niaba ya Halmashauri. (2) Wakala atakayeteuliwa kwa mujibu wa kanuni ndogo ya (1) atakuwa na wajibu wa- (a) kukusanya na kupokea ushuru kwa niaba ya Halmashauri katika eneo alilopangiwa na kwa viwango vilivyoidhinishwa katika Sheria Ndogo hii; na kielektroniki (b) kukusanya ushuru kwa kutumia mfumo wa kuwasilisha makusanyo yote kwa kuzingatia masharti ya mkataba wa uwakala alioingia na Halmashauri. na Mamlaka ya afisa mwidhiniwa - 8 Verify source ↗
Afisa mwidhiniwa anaweza
AI-assisted research summary: An authorized officer may accept and assess a taxpayer’s accounts, reject final accounts on reasonable grounds of inaccuracy, and enter a taxpayer’s premises during the stated daytime hours to search for information or inspect accounts, books, or other records.
8. Afisa mwidhiniwa anaweza- (a) kupokea na kukubali hesabu za mlipa ushuru na kuzifanyia tathmini kuhusu kiwango cha hesabu cha mlipa ushuru endapo hesabu hizo zitakuwa si sahihi; (b) kukataa hesabu za mwisho iwapo atakuwa na sababu za msingi za kuamini kuwa hesabu hizo si sahihi; na (c) kuingia kwenye eneo lolote la mlipa ushuru kuanzia saa moja na nusu asubuhi hadi saa kumi na mbili kamili jioni kwa ajili ya kutafuta taarifa au kuchunguza hesabu, vitabu au taarifa zozote kama ataona inafaa. Ukokotoaji wa ushuru wa huduma Makosa - 9 Verify source ↗
Ushuru wa huduma wa mlipa ushuru
AI-assisted research summary: Ushuru wa huduma wa mlipa ushuru anayewasilisha taarifa za mauzo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania utahesabiwa kwa kuzingatia taarifa zilizowasilishwa katika kipindi maalumu cha hesabu.
9. Ushuru wa huduma wa mlipa ushuru anayewasilisha taarifa za mauzo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania utakokotolewa kwa kuzingatia taarifa zinazowasilishwa na mlipa ushuru wa huduma katika kipindi maalumu cha hesabu. - 10 Verify source ↗
Mtu anatenda kosa endapo mtu huyo
AI-assisted research summary: Mtu anatenda kosa akishindwa kuwasilisha taarifa sahihi za mauzo au kulipa ushuru wa huduma kwa wakati, akitoa taarifa zisizo sahihi, akiwashawishi walipaji kukwepa, au akizuia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii.
10. Mtu anatenda kosa endapo mtu huyo- (a) anashindwa kuwasilisha kwa Halmashauri taarifa sahihi za mauzo ndani ya muda ulioainishwa katika Sheria Ndogo hii; (b) anawasilisha kwa Halmashauri taarifa 5 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Tangazo la Serikali Na.504 (Linaendelea.) zisizo sahihi; (c) anashindwa kulipa ushuru wa huduma ndani ya muda ulioainishwa katika Sheria Ndogo hii; (d) anamshawishi mlipa ushuru wa huduma kukataa au kukwepa kulipa ushuru; (e) anamzuia afisa mwidhiniwa au wakala kutekeleza masharti ya Sheria Ndogo hii; (f) anatoa taarifa isiyo sahihi kuhusu jambo lolote linaloweza kuathiri jukumu lake au la mtu mwingine la kulipa ushuru; (g) anaharibu kwa makusudi taarifa au mfumo wa taarifa; au (h) anaharibu kwa makusudi vitendea kazi vya kukusanyia ushuru. Adhabu Ufifilishaji wa makosa - 11 Verify source ↗
Mtu atakayetiwa hatiani kwa kutenda kosa
AI-assisted research summary: A person convicted of offending against this bylaw must pay a fine, go to prison, or both.
11. Mtu atakayetiwa hatiani kwa kutenda kosa kinyume cha Sheria Ndogo hii atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi laki mbili na isiyozidi shilingi milioni moja au kifungo kisichopungua miezi kumi na mbili na kisichozidi miezi ishirini na nne au vyote. - 12 Verify source ↗
Mkurugenzi anaweza kumtaka mtu
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kumtaka mtu aliyefanya kosa chini ya Sheria Ndogo hii kulipa shilingi laki mbili, ikiwa mkosaji anakiri kosa kwa maandishi katika fomu maalumu na yuko tayari kutimiza wajibu wake.
12. Mkurugenzi anaweza kumtaka mtu aliyetenda kosa kinyume cha Sheria Ndogo hii kulipa kiasi cha shilingi laki mbili endapo mkosaji atakiri kosa kwa maandishi katika fomu maalumu iliyoainishwa katika Jedwali la Pili la Sheria Ndogo hii na kuwa tayari kutimiza wajibu wake kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. Kufutwa kwa Sheria Ndogo TS Na. 897 la 2019 - 13 Verify source ↗
Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya
AI-assisted research summary: This section repeals the Nyasa District Council service levy bylaw of 2019.
13. Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya Nyasa ya Mwaka 2019 inafutwa. Commented [H1]: Jiridhishe na usahihi wa jina la sheria ndogo rejewa ya 2019 6 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Tangazo la Serikali Na.504 (Linaendelea.) ___________ JEDWALI LA KWANZA ____________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 4(2)) USHURU WA HUDUMA Namba Aina ya malipo Leseni ya biashara Kiasi cha malipo ya Ushuru wa Huduma kwa Mwaka (Shilingi)
Part
JEDWALI LA KWANZA
- 8 Verify source ↗
Section 8
AI-assisted research summary: Kuna jedwali la kiasi cha ushuru/leseni na fomu ya kukiri kosa kwa hiari mbele ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa.
8. 0 hadi 15,000/= 20,000/= hadi 35,000/= 40,000/= hadi 45,000/= 50,000/= hadi 60,000/= 65,000/= hadi 100,000/= 105,000/= hadi 150,000/= 155,000/= hadi 200,000/= Malipo ya leseni za vilabu vya pombe za asili 5000/= 10,000/= 15,000/= 30,000/= 40,000/= 50,000/= 100,000/= 12,000/= kwa miezi sita(6) 7 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Tangazo la Serikali Na.504 (Linaendelea.) _________ JEDWALI LA PILI ________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 12) FOMU YA KUFIFILISHA MAKOSA Mimi ……………………………………………………… nakiri kwa hiari yangu mwenyewe mbele ya ………………………………………….ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa, kwamba mnamo tarehe …… ya mwezi ……. mwaka …… nilitenda kosa la kukiuka masharti ya kanuni ya …… ya Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa ya Mwaka 2024. Na kwamba nipo tayari kulipa kiasi cha ushuru ninaodaiwa pamoja na faini badala ya kushtakiwa mahakamani. Nathibitisha kwamba maelezo niliyotoa hapo juu ni ya kweli na nimeyatoa mimi mwenyewe kwa hiari yangu kadri ya ufahamu wangu. Leo tarehe…………. ya mwezi…………..… mwaka ……………. Jina……………………………….. Saini……………………… MBELE YANGU : Jina:……………………………………..……………………..... Saini………………………….…………………………..……… Wadhifa: ………………………………………………………… Tarehe…………………………………………………………… 8 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Tangazo la Serikali Na.504 (Linaendelea.) Lakiri ya Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa imegongwa kwenye Sheria Ndogo hii kufuatia Azimio lililopitishwa katika Mkutano wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Nyasa uliofanyika tarehe 15/5/2023 na kushuhudiwa Lakiri imebandikwa mbele ya:- KHALID A. KHALIF, Mkurungenzi mtendaji, Halmashauri ya Wilaya, Nyasa MHE. STEWART J NOMBO, Mwenyekiti, Halmashauri ya wilaya, Lushoto L.S NAKUBALI, Dodoma, MOHAMED OMARY MCHENGERWA (MB.), 30 Januari, 2024 Waziri wa Nchi -OR-Tamisemi, 9
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa ya Mwaka 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in