SHERIA NDOGO YA ADA NA USHURU YA HALMASHAURI YA WILAYA YA LONGIDO YA MWAKA 2024
This by-law is titled the Longido District Council Fees and Charges By-law, 2024.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- SHERIA NDOGO YA ADA NA USHURU YA HALMASHAURI YA WILAYA YA LONGIDO YA MWAKA 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This by-law is titled the Longido District Council Fees and Charges By-law, 2024. This by-law applies throughout the entire area of the Longido District Council. This section defines key terms used in the by-law, including fees, permits, traffic vehicles, markets, fines/levies, and the authorized officer and agent. Halmashauri lazima itoe ada au ushuru kwa vibali, leseni, na huduma zake zilizoainishwa katika Jedwali la Kwanza. Mtu anayepaswa kulipa ada au ushuru chini ya Sheria Ndogo hii lazima alipe kwa viwango vilivyoainishwa humo.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of SHERIA NDOGO YA ADA NA USHURU YA HALMASHAURI YA WILAYA YA LONGIDO YA MWAKA 2024
Showing 47 of 47
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria
AI-assisted research summary: This by-law is titled the Longido District Council Fees and Charges By-law, 2024.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Ada na Ushuru ya Halmashauri ya Wilaya ya Longido ya Mwaka 2024. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la
AI-assisted research summary: This by-law applies throughout the entire area of the Longido District Council.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la Mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya ya Longido. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the by-law, including fees, permits, traffic vehicles, markets, fines/levies, and the authorized officer and agent.
3. Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo: “ada” maana yake ni malipo yanayolipwa kwa Halmashauri kwa ajili ya vibali au leseni mbalimbali zinazotolewa na Halmashauri; “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni afisa yeyote aliyeteuliwa na Mkurugenzi kwa lengo la kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “chombo cha usafiri” maana yake ni chombo chochote kinachotumika kusafirisha abiria na mizigo kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine isipokuwa baiskeli, mkokoteni au wanyama 1 Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru ya Halmashauri ya Wilaya ya Longido Tangazo la Serikali Na. 559 (Linaendelea) wanaotumika kusafirisha watu au mizigo; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Longido; “kibali” maana yake ni idhini au ruhusa ya maandishi inayotolewa na Halmashauri; “kituo cha mabasi” maana yake ni eneo maalum lililotengwa na Halmashauri kwa madhumuni ya kupakia na kuteremsha abiria na mizigo ya abiria; “machinjio” maana yake ni sehemu iliyotengwa na Halmashauri kwa ajili ya kuchinjia wanyama na kuanika ngozi ikiwa ni pamoja na maeneo ya taasisi ya umma au watu binafsi yaliyopo katika eneo la Halmashauri; “madini ya ujenzi” maana yake ni tarazo, moramu, udongo, kifusi, kokoto, mawe, mchanga, chokaa na madini mengine yanayotumika katika ujenzi; “maegesho” maana yake ni sehemu yoyote iliyotengwa na Halmashauri kwa ajili ya kuegesha chombo cha usafiri kwa muda; “matangazo” maana yake ni taarifa zinazotolewa kwa njia ya vipaza sauti, maandishi, picha au michoro itakayochorwa au kuandikwa au kubandikwa katika vibao, ukuta wa nyumba, vitambaa, kwenye gari au chombo chochote kwa madhumuni ya kunadi biashara, huduma au bidhaa; 2 Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru ya Halmashauri ya Wilaya ya Longido Tangazo la Serikali Na. 559 (Linaendelea) mhudumu” maana yake ni mtu yeyote anayehudumia wateja katika eneo la biashara; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido au afisa yeyote aliyeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi; "mnada” maana yake ni soko la wazi ambalo mali au vitu mbalimbali vinauzwa kwa ushindani wa bei kwa kauli na kwa kibali maalumu cha Halmashauri; “soko” maana yake ni ni eneo au soko liliotengwa na linalomikiwa na Halmashauri kama soko; “ushuru” maana yake ni tozo inayotozwa na Halmashauri kwa shughuli au huduma mbalimbali zinazofanywa katika eneo la Halmashauri; “shughuli za utamaduni” maana yake ni sanaa za maonyesho, sanaa za ufundi,muziki wa asili,ususi,michezo,muziki wa dansi,video,muziki wa taarabu,maonyesho ya sinema, mazingaombwe,tiba za jadi na matumizi ya viwanja vya michezo; na “Wakala” maana yake ni kampuni iliyoteuliwa kukusanya ushuru kwa niaba ya Halmashauri chini ya Sheria Ndogo hii. Utozaji wa ada au ushuru - 4 Verify source ↗
(1) Halmashauri itatoza ada au ushuru
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima itoe ada au ushuru kwa vibali, leseni, na huduma zake zilizoainishwa katika Jedwali la Kwanza.
4.-(1) Halmashauri itatoza ada au ushuru kwa ajili ya vibali au leseni na huduma 3 Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru ya Halmashauri ya Wilaya ya Longido Tangazo la Serikali Na. 559 (Linaendelea) mbalimbali zinazotolewa na Halmashauri kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Kwanza. (2) Ushuru unaotozwa chini ya Sheria Ndogo hii utalipwa kwa Halmashauri au Wakala kwa kadiri Halmashauri itakavyoelekeza. (3) Ada zinazotozwa chini ya Sheria Ndogo hii zitalipwa kwa Halmashauri. (4) Malipo ya ada au ushuru yatalipwa kabla au wakati wa kupokea huduma inayotozwa ada au ushuru chini ya Sheria Ndogo hii. Wajibu wa kulipa ada au ushuru - 5 Verify source ↗
Mtu yeyote anayestahili kulipa ada au ushuru
AI-assisted research summary: Mtu anayepaswa kulipa ada au ushuru chini ya Sheria Ndogo hii lazima alipe kwa viwango vilivyoainishwa humo.
5. Mtu yeyote anayestahili kulipa ada au ushuru kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii atatakiwa kulipa ada au ushuru huo kwa kuzingatia viwango vilivyoainishwa katika Sheria Ndogo hii. Muda wa kukusanya ada au ushuru - 6 Verify source ↗
(1) Muda wa kukusanya ada au ushuru
AI-assisted research summary: Ada au ushuru hukusanywa kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 12 jioni, isipokuwa kwa kibali maalum cha Mkurugenzi.
6.-(1) Muda wa kukusanya ada au ushuru utakuwa ni kuanzia saa kumi na mbili kamili asubuhi hadi saa kumi na mbili kamili jioni. (2) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (1), Halmashauri au Wakala, kwa kibali maalum kutoka kwa Mkurugenzi, anaweza kukusanya ada au ushuru baada ya muda uliotajwa katika kanuni ndogo ya (1). (3) Malipo ya ada au ushuru yatafanyika kila siku au kwa mwezi au kwa namna yeyote itakayokubalika kulingana na makubaliano yatakayowekwa kati ya 4 Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru ya Halmashauri ya Wilaya ya Longido Tangazo la Serikali Na. 559 (Linaendelea) Halmashauri na mlipa ada au ushuru. (4) Malipo ya ada au ushuru yanayotozwa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii yatalipwa kwa Halmashauri au Wakala wake na kutolewa stakabadhi ya kielektroniki ya Halmashauri kama kielelezo cha malipo yaliyofanyika. Mabadiliko ya viwango vya ada au ushuru - 7 Verify source ↗
(1) Endapo
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kubadilisha viwango vya ada na ushuru ikiwa inaona inafaa, na inapofanya marekebisho hayo lazima ifuate taratibu zote za utungaji zilizotajwa.
7.-(1) Endapo itaonekana kuwa inafaa, Halmashauri inaweza kubadilisha viwango vya ada na ushuru kwa kufuta, kurekebisha au kuweka viwango vipya. (2) Katika kufanya marekebisho ya viwango vya ada na ushuru au kipengele chochote katika Sheria Ndogo hii, Halmashauri itafuata taratibu zote za utungaji Sura ya 287 wa Sheria Ndogo zinazoelekezwa na Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya). Ukusanyaji wa madeni - 8 Verify source ↗
(1) Halmashauri inaweza kukusanya ushuru
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kukusanya deni la ushuru kupitia Mahakama, kukamata na kushikilia mali, na kuuza mali zilizokamatwa baada ya siku 30 au mapema ikiwa zinaweza kuharibika, kwa kupata idhini ya Mahakama.
8.-(1) Halmashauri inaweza kukusanya ushuru kwa njia ya Mahakama endapo mtu binafsi, kikundi, taasisi au kampuni itakuwa imeshindwa kulipa ada au ushuru kwa muda uliokubaliwa. (2) Bila kuathiri masharti yaliyowekwa katika kanuni ndogo ya (1), Halmashauri inaweza kukusanya madeni ya ushuru kwa njia ya kukamata au kushikilia mali zinazohamishika za mdaiwa zenye thamani sawa na deni la ushuru pamoja na gharama za kukamata. (3) Baada ya kipindi cha siku thelathini kupita 5 Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru ya Halmashauri ya Wilaya ya Longido Tangazo la Serikali Na. 559 (Linaendelea) tangu kukamatwa kwa mali za mdaiwa chini ya kanuni ndogo ya (2), Halmashauri itakuwa na mamlaka ya kuziuza kwa njia ya mnada baada ya kupata idhini ya Mahakama. (4) Endapo mali zilizokamatwa zinaweza kuharibika kwa haraka, Halmashauri itakuwa na uwezo wa kuziuza kabla hazijaharibika baada ya kupata idhini ya Mahakama. (5) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (3) na (4), Halmashauri kabla ya kuuza mali yoyote iliyokamatwa, Mkurugenzi atatoa taarifa ya siku saba kwa mdaiwa na umma juu ya kusudio la kuuza mali hizo. (6) Halmashauri haitawajibika kwa hasara yoyote ile itakayotokea ama wakati wa kukusanya madeni au kwa mali itakayokamatwa na kushikiliwa na Halmashauri, isipokuwa kama hasara hiyo itakuwa imesababishwa na uzembe wa watumishi wa Halmashauri au Wakala. Uteuzi wa Wakala - 9 Verify source ↗
(1) Halmashauri
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kuteua kampuni iliyosajiliwa kukusanya ushuru, na wakala aliyechaguliwa lazima akusanye na kupokea ushuru kwa niaba ya Halmashauri.
9.-(1) Halmashauri itakuwa na mamlaka ya kuteua kampuni iliyosajiliwa kwa mujibu wa sheria kukusanya ushuru kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. (2) Wakala aliyeteuliwa kwa mujibu wa kanuni ndogo ya (1) atakuwa na wajibu wa: (a) kukusanya na kupokea ushuru kwa niaba ya Halmashauri katika eneo alilopangiwa na kwa viwango vilivyoidhinishwa katika Sheria 6 Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru ya Halmashauri ya Wilaya ya Longido Tangazo la Serikali Na. 559 (Linaendelea) Ndogo hii; na (b) kukusanya ushuru kwa kutumia mfumo wa kielektroniki na kuwasilisha makusanyo yote kwa kuzingatia masharti ya mkataba wa uwakala alioingia na Halmashauri. Mamlaka ya Afisa Mwidhiniwa - 10 Verify source ↗
Bila kuathiri masharti yaliyowekwa na Sheria
AI-assisted research summary: Afisa Mwidhiniwa anaweza kuingia katika eneo, jengo au chombo cha usafiri katika saa zilizotajwa ili kukusanya ada au ushuru, kufanya tathmini, au kushughulikia mambo yanayohusu ada, ushuru, leseni au kibali.
10. Bila kuathiri masharti yaliyowekwa na Sheria Ndogo hii, Afisa Mwidhiniwa anaweza kuingia katika eneo, jengo au chombo cha usafiri kuanzia saa kumi na mbili kamili asubuhi hadi saa kumi na mbili kamili jioni kwa nia ya kukusanya ada au ushuru, kufanya tathmini au kufanya jambo lolote linalohusu ada, ushuru, leseni au kibali kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. Kamati Mapato ya - 11 Verify source ↗
(1) Kutakuwa na Kamati ya Mapato ya
AI-assisted research summary: Kamati ya Mapato ya Halmashauri itaundwa na Mkurugenzi na lazima ifanye majukumu yake ya kusimamia mapato na itoe taarifa ya utendaji kazi kila mwezi kwa Menejimenti.
11.-(1) Kutakuwa na Kamati ya Mapato ya Halmashauri itakayoundwa na Mkurugenzi ambayo itakuwa na majukumu yafuatayo: (a) kuratibu utendaji kazi wa kikosi kazi cha kukusanya mapato; (b) kuishauri Halmashauri kuhusu namna ya kuongeza mapato na kubuni vyanzo vipya vya mapato; na (c) kufanya tathmini ya makusanyo katika kila chanzo kwa mwaka ili kuweka maoteo ya 7 Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru ya Halmashauri ya Wilaya ya Longido Tangazo la Serikali Na. 559 (Linaendelea) mwaka unaofuata. (2) Kamati ya Mapato itawajibika kutoa taarifa ya utendaji kazi kwa Menejimenti kila mwezi kuonyesha namna ilivyofanya kazi katika kipindi husika. Kikosi kazi cha - 12 Verify source ↗
(1) Kutakuwa na kikosi kazi cha kufuatilia
AI-assisted research summary: A task force to monitor and control revenue and revenue leakage must be formed by the Director, with experts from different council sectors, and it is responsible to the Revenue Committee.
12.-(1) Kutakuwa na kikosi kazi cha kufuatilia kudhibiti Mapato na kudhibiti utoroshaji wa mapato ambacho kitaundwa na Mkurugenzi kikihusisha wataalamu kutoka sekta mbalimbali za Halmashauri. (2) Kikosi kazi kitakachoundwa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii kitawajibika kwa Kamati ya Mapato. Wajibu wa - 13 Verify source ↗
(1) Bila kuathiri wajibu wa kulipa ada au
AI-assisted research summary: Mlipa ada au ushuru lazima azingatie masharti mengine yanayohusiana na chanzo cha mapato anacholipia, pamoja na masharti ya matumizi ya maeneo maalumu na baadhi ya marufuku.
13.- (1) Bila kuathiri wajibu wa kulipa ada au kuzingatia masharti mengine ushuru, mlipa ada au ushuru atawajibika kuzingatia masharti mengine kulingana na chanzo cha mapato anachokilipia ada au ushuru ambayo ni- (a) kutumia maeneo maalumu yaliyotengwa kwa ajili ya uchinjaji wa mifugo (machinjio); (b) kutumia stendi kwa ajili ya kushusha na kupakia abiria na mizigo yao; (c) kuegesha gari katika maeneo maalumu yaliyotengwa kwa ajili ya maegesho ya 8 Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru ya Halmashauri ya Wilaya ya Longido Tangazo la Serikali Na. 559 (Linaendelea) vyombo vya usafiri; (d) kutochimba madini ya ujenzi katika kingo za mito, hifadhi ya barabara, katika vyanzo vya maji na kuchimba bila kibali cha Halmashauri; (e) kutunza mazingira, kutotupa taka ovyo, kutunza maeneo ya hifadhi na/au kutochoma moto ovyo; na (f) kuzingatia masharti mengine yaliyowekwa na Sheria Ndogo nyingine za Halmashauri. Makosa - 14 Verify source ↗
Mtu yeyote
AI-assisted research summary: Mtu yeyote anayefanya au kusaidia vitendo vilivyoorodheshwa kuhusu ada au ushuru anatenda kosa.
14. Mtu yeyote- (a) anayekusanya ada au ushuru bila kibali cha maandishi au mkataba kutoka kwa Halmashauri; (b) anayejaribu au kukusanya ada au ushuru kwa kiwango tofauti na kilichotajwa na Sheria Ndogo hii; (c) atakayeshindwa kuwasilisha au kuwasilisha pungufu ya kiwango cha ada au ushuru alichokubaliwa katika mkataba; (d) anayekusanya ada na ushuru kwa mbinu tofauti na alizoelekezwa na Halmashauri; (e) atakayeshindwa au atadharau au atakwepa au atakataa kulipa ada au ushuru au kutekeleza 9 Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru ya Halmashauri ya Wilaya ya Longido Tangazo la Serikali Na. 559 (Linaendelea) agizo lolote alilopewa na Halmashauri kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii; (f) atakayemshawishi mtu au kundi la watu kukwepa au kukataa kulipa ada au ushuru; (g) atakayemzuia Mkurugenzi au Afisa Mwidhiniwa au Wakala kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii; (h) atakayetumia nyaraka za kughushi kwa nia ya kujipatia manufaa yatokanayo na ukusanyaji wa ada au ushuru ndani ya Halmashauri; (i) atakayetoa taarifa za uongo kwa Halmashauri au Wakala kuhusu huduma zinazohitaji kulipiwa ushuru na zinazohitaji kibali au leseni ya Halmashauri; na (j) atakayetumia chombo chochote kile kusafirishia bidhaa ambayo haijalipiwa ushuru au ada, anatenda kosa. Adhabu - 15 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayekiuka au kwenda kinyume
AI-assisted research summary: Anyone who breaches any section of this bylaw commits an offence and may be fined, imprisoned, or both if convicted.
15. Mtu yeyote atakayekiuka au kwenda kinyume na Kifungu chochote cha Sheria Ndogo hii atakuwa ametenda kosa na akipatikana na hatia atatozwa faini ya kiasi kisichopungua shilingi laki mbili na isiyozidi shilingi milioni moja au kifungo kisichopungua miezi kumi na mbili na kisichozidi miezi ishirini na nne au adhabu zote mbili kwa pamoja yaani faini na kifungo. 10 Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru ya Halmashauri ya Wilaya ya Longido Tangazo la Serikali Na. 559 (Linaendelea) Kufililisha kosa - 16 Verify source ↗
Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha
AI-assisted research summary: The Director may compound an offence by charging up to shilingi laki mbili if the offender admits the offence, is ready to fill the prescribed form in the Second Schedule, and pays any fee or duty owed.
16. Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha kosa kwa kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii kiasi cha shilingi laki mbili endapo mkosaji atakiri kosa na kuwa tayari kujaza fomu maalum iliyoainishwa katika Jedwali la Pili na kulipa ada au ushuru anaodaiwa. Kufutwa TS Na. - 17 Verify source ↗
Sheria Ndogo ya Ada na Ushuru ya
AI-assisted research summary: This section repeals the Longido District Council Fees and Charges By-law of 2017.
17. Sheria Ndogo ya Ada na Ushuru ya Halmashauri ya Wilaya ya Longido ya Mwaka 2017 108 la 2017 inafutwa. ________ JEDWALI LA KWANZA ___________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 4(1)) A. ADA YA KUKODI MALI ZA HALMASHAURI NA KODI KWENYE MAENEO YANAYOTOA HUDUMA KWA UMMA Huduma Na. Kiwango (Shilingi)
Part
JEDWALI LA KWANZA
- 1 Verify source ↗
Section 1
AI-assisted research summary: Kifungu kinaweka ada za kukodi ukumbi wa Halmashauri na baadhi ya majengo au vyumba kwa matumizi tofauti kama vikao, warsha, sherehe, kantini na nyumba.
1. Kukodi ukumbi wa Halmashauri kwa ajili ya Mikutano/ Vikao na Sherehe 2 Majengo, Nyumba, Vyumba na sehemu za Halmashauri 11 200,000/= kwa Ukumbi Mkubwa kwa siku moja kwa shughuli za Vikao na Warsha. 300,000/= kwa Ukumbi mkubwa kwa shughuli za Sherehe 150,000/= kwa Ukumbi mdogo kwa shughuli za Sherehe. 100,000/= kwa Ukumbi mdogo kwa shughuli za Vikao au kulingana na Mkataba 100,000/= kwa Kantini kwa Mwezi au zaidi kulingana na Mkataba 100,000/= kwa Nyumba moja 200,000/= kwa Mwezi kwa Nyumba au kulingana na Mkataba. Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru ya Halmashauri ya Wilaya ya Longido Tangazo la Serikali Na. 559 (Linaendelea) 3 Kukodi vifaa vipaza sauti (PA System) - 7 Verify source ↗
Section 7
AI-assisted research summary: Hii sehemu inaweka ratiba ya ada za kukodisha na matumizi ya baadhi ya vitu/rasilimali, pamoja na viwango vinavyotegemea muda au umbali.
7. Kukodi samani Kukodi Gari: Magari madogo Magari makubwa Mitambo (Trekta, Total station, Vifaa vya GPS) Vibanda vya Biashara mzunguko wa Masoko, Minada, Magulio na Stendi katika Mamlaka za Vijiji na Kata ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Longido 300,000/= hadi 400,000/= kwa masaa sita kwa Vikao 400,000/= hadi 600,000/= kwa zaidi ya masaa sita kwa Sherehe, matangazo na promotion 500/= kila Kiti kimoja kwa siku 1,000/= kwa Meza moja kwa siku 100,000/= kwa kila Kilomita 100 60,000/= chini ya Kilometa 100 200,000/= kwa kila Kilomita 100 80,000/= chini ya Kilometa 100 200,000/= kwa kila masaa 8 Kwa mujibu wa Mkataba B. USHURU WA SOKO, MINADA NA MAGULIO Na. Zao - 9 Verify source ↗
Section 9
AI-assisted research summary: This section lists goods: maize, cassava, sweet potatoes, oranges, coconuts, tomatoes, fish, rice, wheat, unhusked rice, onions, bananas, and carrots.
9. Gunia la Mahindi Gunia la Mhogo, Viazi vitamu, Machungwa, Nazi. Tenga la Nyanya Tenga la Samaki Gunia la Mchele/Ngano Gunia la Mpunga Gunia la Vitunguu aina zote Mkungu wa Ndizi mbivu/mbichi Gunia la Karoti - 12 Verify source ↗
Section 12
AI-assisted research summary: The section lists a tax rate based on the market value of the relevant forest produce, with percentages shown in the text.
12. Mazao ya Misitu kwa gari 12 Kiwango cha ushuru kwa thamani ya bei soko ya zao husika 3% 3% 3% 5% 3% 3% 3% 3% 3% 3% 3% 5% Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru ya Halmashauri ya Wilaya ya Longido Tangazo la Serikali Na. 559 (Linaendelea) - 13 Verify source ↗
Section 13
AI-assisted research summary: This text appears to be a heading for a fee schedule about slaughterhouse services, meat inspection, and butchery, but it does not state a specific rule.
13. Mazao Mchanganyiko kwa Wafanyabiashara wa rejareja 2,000 kwa siku C. ADA YA HUDUMA ZA MACHINJIO, UKAGUZI WA NYAMA NA BUCHA Na. Maelezo Kiwango (Shilingi) - 4 Verify source ↗
Section 4
AI-assisted research summary: This section sets fees for slaughter and meat inspection, livestock slaughter/butchery charges, cultural and entertainment permits, gambling charges, and business advertising signs.
4. Ada ya Machinjio na Ukaguzi wa nyama kwa kila Ng’ombe 5,000/=Ng’ombe mmoja Ada ya Machinjio na Ukaguzi wa nyama kwa kila Kondoo, Mbuzi, Nguruwe na kuku 2,000/= kila Mfugo mmoja atakayechinjwa Kuwamba na kukausha ngozi eneo la machinjio Ng’ombe Mbuzi, Kondoo Ushuru wa Bucha la Ng’ombe, Mbuzi, Kondoo, Nguruwe, na Samaki 700/=kwa siku 300/=kwa siku 2,000/=kwa siku D. ADA YA KUENDESHA SHUGHULI ZA UTAMADUNI, BURUDANI NA MICHEZO Na. Maelezo Kiwango (Shilingi) Kibali cha ngoma za jadi Kibali cha kuchezesha disco, Maonyesho ya bendi, Sanaa za maonyesho 35,000/= kwa mwezi 100,000/= kwa onyesho Michezo ya Pooltable na michezo mingineyo maeneo ya starehe kuchezesha Michezo Ushuru wa Kubahatisha Kibali cha Mechi za Mipira katika Uwanja wa Halmashauri ya E. ADA YA MATANGAZO YA BIASHARA Na. 1 2 3 4 Aina ya Bango Bango lisilo la Mng’ao (Non-Illuminated Sign) Bango Mng’ao (Illuminated Sign) Mabango ya Biashara yaliandikwa na kuchora kwenye kuta za Majengo (Wall Sign) Mabango ya Kietroniki (Electronic Sign) 13 30,000 kwa Mwezi kwa kila eneo panapochezwa mchezo huo 60,000/= kwa mwezi 10% ya Mapato kwa kila Mechi Kiwango (Shilingi) 7,000/= Kwa Kila Futi Moja ya Mraba 10,000/= Kwa Kila Futi Moja ya Mraba 10,000/= Kwa Kila Futi Moja ya Mraba. 10,000/= Kwa Kila Futi Moja ya Mraba. - 5 Verify source ↗
Section 5
AI-assisted research summary: Hii sehemu inaorodhesha viwango vya ada/ushuru kwa aina mbalimbali za matangazo, ikiwemo mabango ya magari, mabango ya eneo la biashara, matangazo ya kukuza biashara, na matangazo ya muda mfupi.
5. Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru ya Halmashauri ya Wilaya ya Longido Tangazo la Serikali Na. 559 (Linaendelea) Bango kwenye Gari (Vehicular advertisement) 5 6 7 Bango kwenye gari kwa mmiliki wa gari anayetangaza biashara yake mwenyewe (Vehicular Advertisement branding own products) Bango kwenye eneo la Biashara (Point of sale display): (a) Bango lisilo la Mng’ao (Non illuminated) Bango Mng’ao (Illuminated) Mabango ya kukuza Biashara kwa mabango 100 ya awali kwa kila bango (Every poster promotion for first 100 posters). (b) 8 (i) 10,000/= Kwa Kila Futi Moja ya Mraba. 4,000/= Kwa Kila Futi Moja ya Mraba. 7,000/= Kwa Kila Futi Moja ya Mraba. 10,000/= Kwa Kila Futi Moja ya Mraba. 50,000/= (ii) Mabango ya kukuza Biashara kwa mabango 50,000/= 100 ya kundi lingine kwa kila bango (For every other bunch of 100 posters or part thereof). 9 (Matangazo ya muda mfupi kwa siku (Short term advertisement or promotion per day). 50,000/= F. USHURU WA STENDI YA MABASI, NA MAEGESHO KWA MAENEO YALIYOTENGWA Na. Ushuru wa maegesho Kiwango (Shilingi) - 6 Verify source ↗
Section 6
AI-assisted research summary: Kifungu hiki kinaonyesha ada/ushuru wa kila siku kwa aina mbalimbali za magari na pikipiki.
6. Pikipiki za magudurumu matatu/ Teksi Lori chini ya tani 7, Pick up/, Basi dogo Lori zaidi ya tani 7 na kuendelea Mabasi ya chini ya abiria 30 Mabasi ya abiria zaidi ya 30 Pikipiki za magurudumu mawili 1,000/= kwa siku 5,000/= kwa siku 10,000/= kwa siku 3,000/= kwa siku 10,000/= kwa siku 500/= kwa siku G. USHURU WA MADINI YA UJENZI Na. Ukubwa wa chombo/ Gari Ushuru (Shilingi) - 6 Verify source ↗
Section 6
AI-assisted research summary: The provision lists fees for vehicle trips by tonnage and fees for building permits and building alterations.
6. Chini ya tani 1 Gari tani 1-2 Gari tani 3 Gari tani 4-6 Gari tani 7-9 Gari tani 10 na kuendelea 5,000/=Kwa safari (tripu) 10,000/=Kwa safari 35,000/=Kwa safari 45,000/=Kwa safari 55,000/=Kwa safari 85,000/= Kwa safari H. ADA YA HUDUMA ZA UPIMAJI WA ARDHI NA UTOAJI WA VIBALI VYA UJENZI. Na. Ada kwa kila kibali (Shilingi) Kibali cha ujenzi 14 Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru ya Halmashauri ya Wilaya ya Longido Tangazo la Serikali Na. 559 (Linaendelea) A. Miundombinu, mnara ya simu, mawasiliano na vyombo vya habari Ghorofa Nyumba za Biashara Nyumba ya Makazi. Kituo cha mafuta. Majengo ya Taasisi Binafsi. Maghala na Bohari. Kiwanda Taasisi ya elimu binafsi Uwekezaji kwenye Burudani Uwekezaji mwingine wowote B. Ada ya mabadiliko (alteration) ya jengo lililopo 500,000/=kwa kila muundombinu 500,000/=kwa kila ghorofa moja(floor) 10,000/= kwa kila Jengo 10,000/=kwa mita moja ya mraba 500,000/= 300,000/= 500,000/= - 0 Verify source ↗
1% ya mtaji wa Uwekezaji
AI-assisted research summary: The text states a 0.1% amount based on investment capital and mentions 100,000/= for every 1,000,000/= building value.
0.1% ya mtaji wa Uwekezaji 100,000/= kwa kila Jengo 1,000,000/= - 0 Verify source ↗
1% ya mtaji wa uwekezaji
AI-assisted research summary: Hii ni jedwali la ada na ushuru; linaonyesha viwango mbalimbali vya malipo kwa vibali na huduma za ardhi, pamoja na ada ya kuogesha mifugo katika majosho ya umma na binafsi.
0.1% ya mtaji wa uwekezaji Kwa kila Kibali (Shilingi) Nyumba ya kuishi na biashara Nyumba ya Biashara. Nyumba ya kuishi Ghorofa. Kiwanda, Bohari, Ghala. 50,000/= 70,000/= 40,000/= 200,0000/=kwa kila gorofa 500,000/= Mabadiliko ya matumizi ya ardhi (Makazi) Mabadiliko ya matumizi ya ardhi (Biashara) VIWANDA/MAJENGO MAKUBWA 50,000/= 200,000/= C. Ada za huduma ya Ardhi Kiwango (Shilingi) Hati halisi ya Hati miliki ya kimila (Original R/O) Utafiti wa kitaalum (Official search) Kubadili umiliki (Transfer of R/O) Mchoro wa upimaji 5,000/= Kwa Nakala 5,000/= kwa kila huduma 5,000/= kwa kila moja 50,000/= kwa kila mchoro Mchoro wa Mpango Mji 50,000/= kwa kila Mchoro Kutambua eneo (Plot identification) Kurudishia mawe yanaonesha mipaka na mawe ya upimaji (Beacon replacement) 10,000/= kwa kila plot 5,000/= kwa kila jiwe Upimaji wa Shamba 25,000 kwa kila ekari I. USHURU WA MAJOSHO Na. Ada ya kuogesha mifugo katika Majosho ya umma na binafsi kwa kila siku ya kuogesha Kiwango cha Ada (Shilingi) 15 Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru ya Halmashauri ya Wilaya ya Longido Tangazo la Serikali Na. 559 (Linaendelea) - 3 Verify source ↗
Section 3
AI-assisted research summary: Hii sehemu inaweka ada/ushuru wa kiasi fulani kwa mbuzi/kondoo, ng’ombe, na mnyama mwingine yeyote.
3. Mbuzi/kondoo Ng’ombe 100/= kwa kila Mbuzi/Kondoo 200/= kwa kila Ng’ombe Mnyama mwingine yeyote 200/= kwa kila mnyama J. USHURU WA USAFI WA MAZINGIRA KWA MAZAO NA BIDHAA ZINGINE ZINAZOVUKA MPAKA Na. - 1 Verify source ↗
Section 1
AI-assisted research summary: The text lists service fees for agricultural produce transport by truck, with different shilling amounts based on truck size.
1. (a) Ada za huduma Kiwango (Shilingi) Ushuru wa mazao ya kilimo ambayo ni; Mahindi/Maharage/Mchele/Ng’wara/U wele/Mtama/Karanga/, jamii zingine za Kunde/Tumbaku/Pareto, Sukari na Mazao mengine yatokanayo na Miwa, Konge na Mazao yatokanayo na Mkonge, Vitunguu aina zote Lori la tani 10 hadi 40 70,000/- (b) Lori tani 7 hadi 9 40,000/- (c) Lori chini ya tani 7 30,000/- - 2 Verify source ↗
Section 2
AI-assisted research summary: Kiwango cha ada kimewekwa kwa lori za kusafirisha nyanya, matunda na mbogamboga kulingana na uzito wa lori.
2. Nyanya na Matunda aina zote na Mbogamboga (a) Lori la tani 10 hadi 40 70,000/- (b) Lori tani 7 hadi 9 40,000/- (c) Lori chini ya tani 7 30,000/- - 3 Verify source ↗
Section 3
AI-assisted research summary: Ada ya lori hutegemea uzito wa lori: tani 10 hadi 40 hulipa 60,000/-, tani 7 hadi 9 hulipa 30,000/-, na chini ya tani 7 hulipa 20,000/-.
3. Mashudu aina zote (a) Lori la tani 10 hadi 40 60,000/- 16 Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru ya Halmashauri ya Wilaya ya Longido Tangazo la Serikali Na. 559 (Linaendelea) (b) Lori tani 7 hadi 9 30,000/- (c) Lori chini ya tani 7 20,000/- - 4 Verify source ↗
Section 4
AI-assisted research summary: Hii sehemu inaweka ada za lori kulingana na uzito wa mzigo wa dagaa, samaki, mazao mengine ya baharini, maziwa na mito.
4. Dagaa, Samaki na Mazao mengine ya Baharini, Maziwa na Mito (a) Lori la tani 10 hadi 40 70,000/- (b) Lori tani 7 hadi 9 40,000/- (c) Lori chini ya tani 7 30,000/- - 5 Verify source ↗
Section 5
AI-assisted research summary: Fee amounts are set for trucks carrying certain minerals, based on truck weight.
5. Makaa ya mawe, Chokaa, Udongo , Chuma na Madini mengineyo (a) Lori la tani 10 hadi 40 100,000/- (b) Lori tani 7 hadi 9 70,000/- (c) Lori chini ya tani 7 50,000/- - 6 Verify source ↗
Section 6
AI-assisted research summary: This provision sets fees for forest products by cubic-meter ranges.
6. mazao ya misitu, magome ya miti, mbao, Magogo, Mabanzi, asali, mlonge na mazao mengine ya misitu (a) Mita za ujazo 1-20 20,000/- (b) Mita za ujazo 21-40 30,000/- (c) Mita za ujazo 41-60 50,000/- - 7 Verify source ↗
Section 7
AI-assisted research summary: Kuna ada kwa gari kwa baadhi ya mazao ya mifugo, nyama, na bidhaa za viwandani kulingana na aina ya mzigo na uzito wa lori.
7. mazao ya mifugo Ngozi ya Mbuzi/Kondoo/kwato, Ng’ombe/ngozi ya Maziwa, 30,000/- kwa gari 17 Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru ya Halmashauri ya Wilaya ya Longido Tangazo la Serikali Na. 559 (Linaendelea) Nyama 50,000/= kwa gari 8 9 Bidhaa za viwandani ikijumuisha; Chokaa, Nondo, Saruji, Rangi za kupaka Nyumba, Mbolea, Sigara, Vinywaji aina yote kwa matumizi ya binadamu, Nyaya za shaba, Bati aina zote na vifaa vingine vya ujenzi Vigae (a) Lori la tani 10 hadi 40 80,000/- (b) Lori tani 7 hadi 9 50,000/- (c) Lori chini ya tani 7 40,000/- - 10 Verify source ↗
Section 10
AI-assisted research summary: The text states a charge of 70,000/- per vehicle for fuel, gas, and similar goods.
10. Mafuta, Gesi na bidhaa nyinginezo zenye asili zinazofanana 70,000/- kwa gari - 11 Verify source ↗
Section 11
AI-assisted research summary: The text mentions shoes and clothing of all kinds with an amount of 50,000 per vehicle.
11. Viatu na mavazi aina zote 50,000/-kwa gari - 12 Verify source ↗
Section 12
AI-assisted research summary: Inaweka kiwango cha 30,000/- kwa kila tani moja ya ujazo kwa "Bidhaa nyingine Mchanganyiko".
12. Bidhaa nyingine Mchanganyiko 30,000/- kwa kila tani moja ya ujazo - 14 Verify source ↗
Section 14
AI-assisted research summary: The text lists service charges per vehicle for certain goods passing through Longido.
14. 15 madawa ya Mifugo na binadamu, chumvi inazotumika kwa ajili ya mifugo viwandani na binadamu, sabuni aina zote pamoja na kemikali zozote Karatasi , boksi tupu na bidhaa aina zote zinazotokana na karatasi ama mazao ya misitu mafuta ya kula na vyakula vya aina yote zinazo zalishwa kiwandani 50,000/- kwa kila gari 30,000/- kwa gari 30,000/- kwa gari K. USHURU WA USAFI WA MAZINGIRA KWA MIFUGO INAYOPITA AU INAYOINGIA LONGIDO Na. Ada za huduma Kiwango (Shilingi) 18 Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru ya Halmashauri ya Wilaya ya Longido Tangazo la Serikali Na. 559 (Linaendelea) - 1 Verify source ↗
Section 1
AI-assisted research summary: A charge of 40,000/= applies per vehicle for cattle, donkeys, and pigs, or 1,000/= per animal passed.
1. Ng’ombe, Punda na Nguruwe 40,000/= kwa kila gari Au 1000 kwa kila mfugo anayepitishwa - 2 Verify source ↗
Section 2
AI-assisted research summary: Kuna ada ya 30,000/= kwa kila gari au 500 kwa kila mfugo anayepitishwa, na pia kuna kichwa cha ada za huduma za utupaji taka.
2. Ushuru wa Mbuzi, Kondoo 30,000/= kwa kila gari Au 500 kwa kila Mfugo anayepitishwa L. USHURU WA UTEKETEZAJI TAKA Na. Ada za huduma Kiwango (Shilingi) - 2 Verify source ↗
Section 2
AI-assisted research summary: This section lists charges for solid waste disposal, sewage disposal, and parking of transport vehicles.
2. Uteketezaji wa taka ngumu 100,000/= Kila tani ya gari Uteketezaji maji taka kwa lita 8,000 20,000/= kwa lita 8,000 50,000/= kwa lita zaidi ya 8,000 M. USHURU WA KULAZA VYOMBO VYA USAFIRI KATIKA MAEGESHO Na. - 3 Verify source ↗
Section 3
AI-assisted research summary: The provision lists nightly charges for different types of vehicles: 3,000 for large vehicles of 10 tons and above, 2,000 for small vehicles under 10 tons, and 1,000 for bajaji and motorcycles.
3. Chombo cha Usafiri Magari makubwa yenye uzito wa tani 10 na kuendelea Magari madogo yenye uzito chini ya tani 10 Bajaji na pikipiki Kiwango (Shilingi) 3,000/= kwa usiku mmoja 2,000/= kwa usiku mmoja 1,000/=kwa usiku mmoja N. ADA NA USHURU WA HUDUMA NYINGINE Na. Aina ya Huduma Kiwango (Shilingi) - 4 Verify source ↗
Section 4
AI-assisted research summary: The provision lists local fees and charges, including health-check fees for certain hospitality workers, permit fees for events, environmental cleanliness charges for commercial cross-border vehicles, and tourist visitor charges.
4. Ada ya kupima afya kwa wahudumu wa Baa, Hoteli, Nyumba za wageni na Migahawa. 10,000/= kwa kila Mtoa huduma kila baada ya Miezi sita Kibali cha washereheshaji 100,000/= kwa kila Sherehe Ushuru wa Usafi wa Mazingira kwa Magari ya Biashara yanayovuka Mpaka 10,000//=kwa Lori 10,000/= Mabasi ya Abiria 10,000/=Magari ya Wageni wanaotembelea Vivutio nchini Ushuru wa Usafi wa Mazingira kwa Wageni wanaotembelea Vivutio ndani ya eneo la Halmashauri ya Wilaya ya Longido 19 Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru ya Halmashauri ya Wilaya ya Longido Tangazo la Serikali Na. 559 (Linaendelea) a. Mgeni (Mtu mzima) Tsh Dola 10 za kimarekani b. Watoto chini ya miaka 16 Dola 5 za kimarekani c. Magari yanayobeba wageni 10,000/= yaliyosajiliwa nchini tani 0- 2 d. Magari yanayobeba wageni 100,000/= yaliyosajiliwa nje ya nchi tani 2-10 e. Magari yanayobeba wageni 20,000/= yaliyosajiliwa nchini tani 2-10 f. Ndege za kitalii 52,500/= g. Mgeni anayepanda Mlima Longido 20,000/= Kwa siku na Milima mingine h. Mgeni anayetembelea Boma la 20,000/= kwa siku Kimasai i. Mgeni atakayetembelea maeneo 20,000/= kwa siku mengine j. mgeni anayeingia kwenye misitu 20,000/- kwa kila - 8 Verify source ↗
Section 8
AI-assisted research summary: Wamiliki wa biashara za uchimbaji madini na baadhi ya vifaa vya michezo ya kubahatisha wanaonekana kutozwa ushuru wa usafi wa mazingira, ikiwemo 2% ya bei ya madini yaliyochimbwa na TZS 30,000 kwa mwezi kwa baadhi ya wamiliki wa mashine/pooltable.
8. Makampuni yanayofanya biashara ya kubahatisha i. Ushuru wa Usafi wa Mazingira kwa Makampuni yanayochimba madini ndani ya eneo la Halmashauri. ii. Ushuru wa Usafi wa Mazingira kwa Wafanyabiashara wa Madini Wamiliki wa mashine ya michezo ya kubahatish nasibu au michezo ya kubahatisha Wamiliki wa pooltable 30,000/= kwa Mwezi 2% ya bei ya Madini yaliyochimbwa - 0 Verify source ↗
5% ya bei ya Madini wanayouza
AI-assisted research summary: Maandishi yanaonyesha ada au ushuru wa 0.5% ya bei ya madini yanayouzwa, TZS 30,000 kwa mwezi, na TZS 10,000 kwa kila pool table kwa mwezi, pamoja na fomu ya kukiri kosa na kulipa ushuru na faini badala ya kushtakiwa mahakamani.
0.5% ya bei ya Madini wanayouza 30,000/= kwa Mwezi 10,000/= kwa kila “Pooltable” kwa Mwezi __________ JEDWALI LA PILI ____________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 16) HATI YA KUKIRI NA KUFILILISHA KOSA Mimi ……………………………………………………… nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya …………………………………………. ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashuri ya 20 Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru ya Halmashauri ya Wilaya ya Longido Tangazo la Serikali Na. 559 (Linaendelea) Wilaya ya Longido , kwamba mnamo tarehe …… ya mwezi ……. mwaka …… nilitenda kosa la kukiuka masharti ya Kifungu cha …… cha Sheria Ndogo ya (Ada na Ushuru) ya Halmashauri ya Wilaya ya Longido ya Mwaka 2024. Kwa Mamlaka aliyopewa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Longido, niko tayari kulipa kiasi cha Ushuru ninaodaiwa pamoja na faini badala ya kushtakiwa Mahakamani. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA MIMI MWENYEWE KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU Leo tarehe…………. ya Mwezi…………..… Mwaka ……………. Jina……………………………….. Saini……………………… MBELE YANGU : Jina:……………………………………..……………………..... Saini………………………….…………………………..……… Wadhifa: ………………………………………………………… Tarehe…………………………………………………………… 21 Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru ya Halmashauri ya Wilaya ya Longido Tangazo la Serikali Na. 559 (Linaendelea) Nembo ya Halmashauri ya Wilaya ya Longido imewekwa kwenye Sheria Ndogo hizi kwa kufatia Azimio lililopitishwa kwenye Mkutano wa Halmashauri uliofanyika tarehe 10 mwezi 01 2023 na kushuhudiwa na :- STEPHEN A. ULAYA Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Longido SIMON O. LAIZER Mwenyekiti wa Halmashauri, Halmashauri ya Wilaya ya Longido NAKUBALI L.S Dodoma MOHAMED OMARY MCHENGERWA 20 Disemba, 2023 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Tamisemi 22
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
SHERIA NDOGO YA ADA NA USHURU YA HALMASHAURI YA WILAYA YA LONGIDO YA MWAKA 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in