SHERIA NDOGO YA USIMAMIZI WA MIALO NA USHURU WA SAMAKI YA HALMASHAURI YA WILAYA YA IGUNGA ZA MWAKA 2024
This section states the official name of the by-law.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- SHERIA NDOGO YA USIMAMIZI WA MIALO NA USHURU WA SAMAKI YA HALMASHAURI YA WILAYA YA IGUNGA ZA MWAKA 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This section states the official name of the by-law. This bylaw applies throughout the area of the Igunga District Council. Sehemu hii inafafanua maneno muhimu yanayotumika katika Sheria Ndogo hii. Halmashauri lazima itambue na kusajili uongozi wa mialo yote. The Council may suspend fishing activities in Mialo for three months each year, seize fish caught during the suspension, and sell the fish if the owner or fisher does not comply within one day. The Council is not liable for damage to fish or fishing gear unless its employees were negligent.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of SHERIA NDOGO YA USIMAMIZI WA MIALO NA USHURU WA SAMAKI YA HALMASHAURI YA WILAYA YA IGUNGA ZA MWAKA 2024
Showing 19 of 19
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo
AI-assisted research summary: This section states the official name of the by-law.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Mialo na Ushuru wa Samaki ya Halmashauri ya Wilaya ya Igunga za mwaka 2024. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria ndogo hii itatumika katika eneo lote la
AI-assisted research summary: This bylaw applies throughout the area of the Igunga District Council.
2. Sheria ndogo hii itatumika katika eneo lote la mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya ya Igunga. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii,
AI-assisted research summary: Sehemu hii inafafanua maneno muhimu yanayotumika katika Sheria Ndogo hii.
3. Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo: “afisa mwidhiniwa” maana yake ni afisa yeyote wa Halmashauri aliyeteuliwa kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Igunga; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga pamoja na Afisa yeyote atakayeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi; “Kamati” maana yake ni kamati ya usimamizi wa rasilimali ya uvuvi iliyoteuliwa kusimamia shughuli za uvuvi endelevu katika kambi chini ya Sheria ya uvuvi ya mwaka 2003 na kanuni zake; “kambi” maana yake ni eneo linalotambulika na Halmashauri kwa shughuli za uvuvi; “kibali” maana yake ni idhini au ruhusa ya maandishi; “mwalo” ni kambi iliyoruhusiwa inayotambulika na kuendesha shughuli za uvuvi ndani ya Wilaya ya 1 Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Mialo Na Ushuru wa Samaki ya Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Tangazo la Serikali Na. 560 (Linaendelea) Mialo ya samaki Usimam izi wa mialo Igunga; “wakala” maana yake ni mtu wa mtu, Taasisi, Kampuni au kikundi cha watu walioteuliwa na Halmashauri kukusanya Ushuru kwa niaba ya Halmashauri chini ya Sheria Ndogo hii; “ushuru” maana yake ni tozo inayotozwa kwenye samaki na mazao ya samaki; “mnada” maana yake ni mahali katika mwalo palipotengwa na Halmashauri kwa kusudi la kuuzia samaki baada ya kuvuliwa; “samaki” kwa mujibu wa kanuni hii itajumuisha dagaa; na “zana za uvuvi” maana yake ni nyavu za kuvulia, Ndoano, Migono mitego na zana zote zinazokubalika kisheria. - 4 Verify source ↗
(1) Halmashauri itatambua na kusajili uongozi wa
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima itambue na kusajili uongozi wa mialo yote.
4.-(1) Halmashauri itatambua na kusajili uongozi wa mialo yote. (2) Mialo itatambulika kwa kanda, ambazo zitajulikana kwa majina ya vitongoji husika kama itakavyoamuliwa na kikao cha pamoja kati ya Mkurugenzi na kamati. - 5 Verify source ↗
(1) Halmashauri inaweza kusitisha shughuli za
AI-assisted research summary: The Council may suspend fishing activities in Mialo for three months each year, seize fish caught during the suspension, and sell the fish if the owner or fisher does not comply within one day. The Council is not liable for damage to fish or fishing gear unless its employees were negligent.
5.-(1) Halmashauri inaweza kusitisha shughuli za uvuvi katika Mialo kwa kipindi cha miezi mitatu kuanzia tarehe 1 mwezi Januari hadi tarehe 31 mwezi Machi kila mwaka kwa lengo la kuchochea ongezeko la samaki. (2) Halmashauri inaweza kukamata samaki wa mtu yeyote ambaye atakamatwa akiendesha shughuli za uvuvi ndani ya kipindi ambacho shughuli za uvuvi zitasitishwa. samaki (3) Endapo mmiliki au mvuvi wa waliokamatwa atasindwa kutimiza masharti ya Sheria ndogo hii ndani ya siku moja kwa samaki, Halmashauri baada ya itauza samaki, na fedha kupata amri ya Mahakama zitakazopatikana zote kulipia zitatumika Halmashauri ilizoingia katika ukamataji, kutunza na zoezi la mnada na ushuru utakaokuwa unadaiwa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. gharama (4) Halmashauri haitawajibika kwa namna yoyote ile kwa samaki na zana za uvuvi zilizoharibika kutokana na kutekeleza majukumu yake ya kusimamia Sheria Ndogo hii isipokuwa pale ambapo itathibitika kuwa ni uzembe wa watumishi wake. 2 Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Mialo Na Ushuru wa Samaki ya Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Tangazo la Serikali Na. 560 (Linaendelea) Kamati ya usimamizi wa rasilimali ya uvuvi - 6 Verify source ↗
(1) Halmashauri kwakushauriana na serikali ya
AI-assisted research summary: Halmashauri must consult the village government and establish a fisheries resource management committee for fishing landing sites. The committee must include specified members. A member is removed if absent from the landing site area for 90 days or more, or if removed by the director, and the vacancy is filled under the same rules.
6.-(1) Halmashauri kwakushauriana na serikali ya Kijiji ambapo kuna mialo ya uvuvi wa samaki itaunda kamati ya usimamizi wa rasilimali ya uvuvi kwaajili ya kusimamia mialo hiyo. (2) Kamati iliyoundwa chini ya kanuni ndogo ya (1) itakuwa na wajumbe wafuatao: (a) Mwenyekiti wa kamati, ambaye atakuwa ni mwenyekiti wa kitongoji husika ambapo mwalo huo wa samaki unapatikana, (b) Katibu wa kamati, ambaye atakuwa ni kiongozi wa kambi. (c) Mtendaji wa kijiji husika, ambaye atakuwa ni mwenyekiti wa kamati hiyo, (d) Wavuvi watatu kutoka katika uongozi wa wavuvi; na (e) Wafanyabiashara wawili watakao pendekezwa na Mwenyekiti wa Wafanyabiashara. (3) Mjumbe aliyehama au kuondoka katika eneo la mwalo husika kwa muda wa siku 90 na kuendelea, au aliyeondolewa na mkurugenzi ataondolewa kwenye nafasi yake na utaratibu wa kuwapata wajumbe kwa mujibu wa kanuni hii utatumika kujaza nafasi ya mjumbe huyo. - 7 Verify source ↗
Kamati itakuwa na majukumu yafuatayo
AI-assisted research summary: Kamati inapaswa kuanzisha rejesta za uvuvi, kushirikiana katika ukaguzi wa zana za uvuvi, na kuwasilisha taarifa za utekelezaji kwa Mkurugenzi kila baada ya miezi mitatu.
7. Kamati itakuwa na majukumu yafuatayo: (a) kuanzisha rejesta ya wavuvi, vyombo vya uvuvi na kuruhusu zana za uvuvi zinazokubalika kisheria; (b) kushirikiana na afisa mwidhiniwa au wakala anaefanya ukaguzi wa zana za uvuvi; na (c) kuandaa na kuwasilisha taarifa za utekelezaji wa majukumu yake kwa Mkurugenzi kila baada ya miezi mitatu. Majukumu ya kamati Muda wa kamati - 8 Verify source ↗
Wajumbe wa kamati watahudumu kwa kipindi cha
AI-assisted research summary: Committee members serve for one year from appointment. They may be reappointed if the Director, after consulting the village government, considers it appropriate. The Director may remove a member who breaches these by-laws, after consulting the village government.
8. Wajumbe wa kamati watahudumu kwa kipindi cha mwaka mmoja tangu kuteuliwa kwao. (2) Wajumbe wa kamati wanaweza kuteuliwa tena kwa kadri Mkurugenzi kwa kushauriana na serikali ya Kijiji atavyoona inafaa. (3) Mkurugenzi anaweza kwa kushauriana na serikali ya Kijiji kumwondoa katika kamati mjumbe ambaye 3 Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Mialo Na Ushuru wa Samaki ya Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Tangazo la Serikali Na. 560 (Linaendelea) atakiuka masharti ya Sheria Ndogo hii. Uwasilis haji wa taarifa za mitumb wi Ushuru wa Samaki Wajibu wa kulipa Ushuru Eneo la upimaji Muda wa mnada Muda wa kusafiris ha Samaki - 9 Verify source ↗
Kila mmiliki wa mtumbwi au muwakilishi wake
AI-assisted research summary: Boat owners, or their representatives, must submit the boat’s registration information to the fisheries resources management committee within 7 days of receiving the boat registration.
9. Kila mmiliki wa mtumbwi au muwakilishi wake wake atahakikisha anawasilisha taarifa za usajili wa mtumbwi wake kwa kamati ya usimamizi wa rasilimali ya uvuvi siku saba tangu alipopata usajili wa mtumbwi huo. - 10 Verify source ↗
(1) Halmashauri itakusanya ushuru wa samaki
AI-assisted research summary: Halmashauri must collect the fish levy listed in the First Schedule, and taxpayers must ask for and check the payment receipt.
10.-(1) Halmashauri itakusanya ushuru wa samaki kama ulivyoainishwa kwenye Jedwali la Kwanza. (2) Ushuru unaotozwa chini ya kanuni hii utalipwa kwa Halmashauri au kwa Wakala kwa kadri Halmashauri itakavyoelekeza, ambaye atatoa stakabadhi ya kielektroniki kama kielelezo cha malipo yaliyofanyika. (3) Utakuwa ni wajibu wa kila mlipa ushuru kudai na kuhakiki stakabadhi ya malipo kulingana na kiasi cha fedha alicholipa. (4) Utakuwa sio utetezi kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii, mtu kudai kuwa amelipa ushuru lakini hakupewa stakabadhi ya kielektroniki. - 11 Verify source ↗
Mtu yeyote anayestahili kulipa ushuru atatakiwa
AI-assisted research summary: A person who is liable to pay tax must pay it before leaving the harbor/landing place, and must follow the rates set out in this subsidiary law.
11. Mtu yeyote anayestahili kulipa ushuru atatakiwa kulipa ushuru huo kabla ya kuondoka kwenye mwalo na kwa kuzingatia viwango vilivyoainishwa katika Sheria Ndogo hii. - 12 Verify source ↗
Halmashauri itatenga eneo katika mwalo kwaajili
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima itenge eneo katika mwalo kwa ajili ya kupimia samaki waliovuliwa.
12. Halmashauri itatenga eneo katika mwalo kwaajili ya upimaji wa Samaki waliovuliwa na Samaki wote watapaswa kupelekwa kwenye eneo hilo kwaajili ya upimaji. - 13 Verify source ↗
Mnada wa samaki utafunguliwa kuanzia saa
AI-assisted research summary: Fish auction hours are set: it opens in the morning and closes in the evening.
13. Mnada wa samaki utafunguliwa kuanzia saa moja na nusu asubuhi na kufungwa saa kumi na mbili kamili jioni. - 14 Verify source ↗
(1) Muda wa kusafirisha samaki kutoka mnadani
AI-assisted research summary: Samaki zinaweza kusafirishwa kutoka mnadani kwenye mialo iliyotengwa kati ya saa moja na nusu asubuhi na saa kumi na mbili jioni; nje ya muda huo, kibali maalum kinahitajika.
14.-(1) Muda wa kusafirisha samaki kutoka mnadani kwenye mialo iliyotengwa na Halmashauri kwa shughuli hizo ni kuanzia saa moja na nusu asubuhi na mwisho ni saa kumi na mbili jioni. (2) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (1) samaki wanaweza kusafirishwa nje ya muda uliotajwa kwa 4 Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Mialo Na Ushuru wa Samaki ya Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Tangazo la Serikali Na. 560 (Linaendelea) kibali maalum cha Mkurugenzi au afisa mwidhiniwa kutoka katika eneo la mwalo husika. Uteuzi wa Wakala - 15 Verify source ↗
(1) Halmashauri itakuwa na Mamlaka ya kuteua
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kuteua Wakala kukusanya ushuru kwa niaba yake; Wakala aliyeteuliwa lazima akusanye, apokee na awasilishe makusanyo kwa kufuata masharti na maeneo yaliyopangiwa.
15.-(1) Halmashauri itakuwa na Mamlaka ya kuteua Wakala kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii, kukusanya ushuru kwa niaba yake. (2) Wakala aliyeteuliwa kwa mujibu kanuni ndogo ya (1) atakuwa na wajibu wa: (a) kukusanya na kupokea ushuru kwa niaba ya Halmashauri katika eneo alilopangiwa na kwa viwango vilivyoainishwa katika Sheria Ndogo hii; na (b) kukusanya ushuru kwa kutumia mfumo wa kielektroniki na kuwasilisha makusanyo yote kwa kuzingatia masharti ya mkataba wa uwakala alioingia na Halmashauri. - 16 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa endapo
AI-assisted research summary: Mtu yeyote anaweza kutenda kosa akifanya moja ya vitendo vilivyotajwa kuhusu ushuru, taarifa/hesabu za uongo, kuzuia maafisa, kuharibu taarifa au vifaa vya kukusanyia ushuru, au kushughulikia samaki kinyume cha masharti yaliyotajwa.
16.-(1) Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa endapo- (a) atashindwa kulipa ushuru au atamsaidia mtu mwingine asilipe ushuru; (b) atafanya hesabu za uongo kwa kupunguza ushuru isivyo halali; Makosa (c) atatoa taarifa za uongo kuhusu jambo lolote linaloweza kuathiri wajibu wake au wa mtu mwingine kulipa ushuru; na au kutengenezwa kwa hesabu au kumbukumbu za uongo ambazo zinaweza kuathiri ukokotoaji wa ushuru; (d) ataandaa kusababisha kuandaliwa (e) atamzuia au kujaribu kumzuia Mkurugenzi au au Wakala kutekeleza afisa mwidhiniwa majukumu yake; (f) ataharibu kwa makusudi au kwa uzembe taarifa au mfumo wa taarifa za hesabu; (g) ataharibu kwa makusudi au kwa uzembe vitendea kazi vya kukusanyia ushuru; (h) atauuza au kununua samaki nje ya mnada uliotengwa kwa ajili ya mauzo ya samaki; (i) atauza au kununua samaki zaidi ya muda uliopangwa; (j) atakutwa nje ya mwalo akisafirisha samaki bila 5 Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Mialo Na Ushuru wa Samaki ya Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Tangazo la Serikali Na. 560 (Linaendelea) Adhabu Kufifilis ha kosa kulipia ushuru; au (k) atatenda jambo lolote kinyume na masharti ya Sheria Ndogo hii. - 17 Verify source ↗
Mtu atakayetiwa hatiani kwa kukiuka masharti
AI-assisted research summary: A person convicted of violating any provision of this bylaw must pay a fine, face imprisonment, or both.
17. Mtu atakayetiwa hatiani kwa kukiuka masharti ya Kifungu chochote katika Sheria Ndogo hii atatakiwa kulipa faini ya kiasi kisichopungua Shilingi laki mbili na kisichozidi Shilingi Milioni moja au kifungo kisichopungua miezi kumi na mbili na kisichozidi miezi ishirini na nne au adhabu zote mbili kwa pamoja. - 18 Verify source ↗
Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha
AI-assisted research summary: The Director may compound an offence by charging Shilingi 200,000 if the offender admits the offence, is willing to complete the specified form, and pays the tax owed.
18. Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha kosa kwa kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii kiasi cha Shilingi laki mbili endapo mkosaji atakiri kosa na kuwa tayari kujaza fomu maalum iliyoainishwa katika Jedwali la Pili la Sheria Ndogo hii na kulipa ushuru anaodaiwa. ___________________ JEDWALI LA KWANZA _________________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 10(1)) USHURU WA SAMAKI Namba Aina ya Samaki Kiwango cha Ushuru (Shilingi) kwa Kilo
Part
JEDWALI LA KWANZA
- 5 Verify source ↗
Section 5
AI-assisted research summary: This excerpt lists amounts for certain fish categories and includes a form for admitting an offence and offering to pay money instead of being taken to court.
5. Perege Kambare Kamongo Dagaa 150/= 150/= 150/= 100/= Samaki hawajatajwa wengine ambao 100/= 6 Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Mialo Na Ushuru wa Samaki ya Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Tangazo la Serikali Na. 560 (Linaendelea) _____________ JEDWALI LA PILI _____________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 18) HATI YA KUFIFILISHA KOSA Mimi ........................................................................nakiri KWA HIARI YANGU MIMI MWENYEWE mbele ya........................................................... ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Igunga, kwamba Tarehe ..........ya Mwezi .................. Mwaka................ nilitenda kosa kwa kukiuka masharti ya Aya ya ……..ya Sheria Ndogo za Usimamizi wa Mialo na Ushuru wa Samaki za Halmashauri ya Wilaya ya Igunga za Mwaka 2024. Kwa Mamlaka aliyopewa Mkurugenzi wa Halmashauri niko tayari kulipa kiasi cha shilingi………………………………………………………………………. badala ya kushtakiwa Mahakamani. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA MIMI MWENYEWE KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU. Leo Tarehe ......................ya Mwezi ................................Mwaka …… Jina: ..................................................... Saini: .................................................... MBELE YA: Jina……............................................... Wadhifa: .................................................. Saini: .................................................. Tarehe: ............................................... 7 Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Mialo Na Ushuru wa Samaki ya Halmashauri ya Wilaya ya Igunga Tangazo la Serikali Na. 560 (Linaendelea) Lakari ya Halmashauri ya Wilaya ya Igunga imegongwa kwenye Sheria Ndogo hizi kufuatia Azimio lililopitishwa katika Mkutano wa baraza la Madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Igunga uliofanyika tarehe 11 mwezi Agosti Mwaka 2023 na kushuhudiwa lakari hiyo ikigongwa mbele ya:- SELWA ABDALLA HAMID Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Halmashauri ya Wilaya ya Igunga LUCAS MOGA BUGOTA Mwenyekiti wa Halmashauri, Halmashauri ya Wilaya ya Igunga NAKUBALI L.S Dodoma MOHAMED OMARY MCHENGERWA 13 Mei, 2024 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Tamisemi 8
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
SHERIA NDOGO YA USIMAMIZI WA MIALO NA USHURU WA SAMAKI YA HALMASHAURI YA WILAYA YA IGUNGA ZA MWAKA 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in