KANUNI ZA UCHAGUZI WA MWENYEKITI WA KIJIJI, WAJUMBE WA HALMASHAURI YA KIJIJI NA MWENYEKITI WA KITONGOJI KATIKA MAMLAKA ZA MIJI ZA MWAKA 2024
This provision lists the parties covered by the ethics procedures.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- KANUNI ZA UCHAGUZI WA MWENYEKITI WA KIJIJI, WAJUMBE WA HALMASHAURI YA KIJIJI NA MWENYEKITI WA KITONGOJI KATIKA MAMLAKA ZA MIJI ZA MWAKA 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This provision lists the parties covered by the ethics procedures. Vyama vya siasa na wagombea lazima wafuate kanuni za uchaguzi na kuendesha kampeni kwa amani, uwazi, na kwa kufuata sheria. Vyama vya siasa na wagombea hawaruhusiwi kufanya vitendo vya fujo, matusi, ubaguzi, kuharibu matangazo, kubandika bila idhini, kutoa rushwa, au kuwazuia wengine kushiriki mikutano au kupiga kura. This section concerns conduct during voting, counting, totaling votes, and announcing results. Wakala wa vyama vya siasa, vyama vya siasa, wagombea na viongozi wa vyama lazima washirikiane na wasimamizi wa uchaguzi katika vituo vya kupigia kura, na viongozi wa vyama lazima waelekeze wanachama na wafuasi wao kuondoka eneo la kupigia kura baada ya kupiga kura.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of KANUNI ZA UCHAGUZI WA MWENYEKITI WA KIJIJI, WAJUMBE WA HALMASHAURI YA KIJIJI NA MWENYEKITI WA KITONGOJI KATIKA MAMLAKA ZA MIJI ZA MWAKA 2024
Showing 21 of 21
- 1
AI-assisted research summary: This provision lists the parties covered by the ethics procedures.
1.2 Wahusika wa Taratibu za Maadili Wahusika wa Taratibu za Maadili watakuwa wafuatao: (a) Vyama vya Siasa; (b) Wagombea; (c) Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na (d) Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi. - 2
AI-assisted research summary: Vyama vya siasa na wagombea lazima wafuate kanuni za uchaguzi na kuendesha kampeni kwa amani, uwazi, na kwa kufuata sheria.
2.1 Kila Chama cha Siasa na Wagombea watatakiwa kuzingatia yafuatayo: Wajibu wa Vyama vya Siasa na Wagombea (a) kuheshimu na kutekeleza Kanuni za Uchaguzi, Taratibu za Maadili ya Uchaguzi na Miongozo ya Uchaguzi itakayotolewa kwa mujibu wa Kanuni pamoja na kuzingatia matakwa ya Sheria nyingine za nchi katika kipindi chote cha Uchaguzi; (b) kuelimisha, kuhamasisha na kuwasisitiza wanachama na wafuasi wao kuheshimu Kanuni za Uchaguzi, Taratibu za Maadili ya Uchaguzi na Miongozo ya Uchaguzi itakayotolewa kwa mujibu wa Kanuni pamoja na Sheria nyingine za nchi katika kipindi chote cha Uchaguzi; (c) kuzingatia ratiba ya mikutano ya kampeni; (d) kushirikiana na wanachama na wafuasi wa Vyama vingine vya Siasa kuhakikisha kuwa wanachukua hatua za makusudi ili: (i) kufanya Uchaguzi uwe huru na wa haki; (ii) kuzuia vitendo vya vurugu na vitisho; (iii) kukataa aina yoyote ya ubaguzi katika misingi ya jinsia, maumbile, ulemavu, ukabila, dini au rangi; na (iv) kueneza taarifa sahihi kuhusu mchakato wa Uchaguzi; (e) kuchapisha vijitabu, vipeperushi, vitini, mabango na machapisho ya aina yoyote yanayoelezea sera zao baada ya kuidhinishwa na Msimamizi wa Uchaguzi; (f) kutumia vyombo vya habari kutangaza sera zao kwa kuzingatia sheria zinazosimamia vyombo vya habari na Miongozo ya Uchaguzi; (g) kujenga mazingira ambayo yatawezesha Uchaguzi kufanyika kwa uhuru na haki, ikiwa ni pamoja na kuwezesha makundi maalum kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi; (h) kuhakikisha hifadhi na usafi wa mazingira katika kusambaza matangazo ya kampeni; (i) kuondoa mabango, matangazo na machapisho ya aina yoyote ile yaliyotumika wakati wa kampeni katika sehemu za wazi baada ya Uchaguzi; 57 Kanuni za Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kijiji, Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji na Mwenyekiti wa Kitongoji katika Mamlaka za Miji Tangazo la Serikali Na.573 (Linaendelea.) (j) kutoa taarifa mara moja kwa mamlaka husika wanapofahamu au wanapoona tukio linaloweza kusababisha vurugu au uvunjifu wa amani; (k) kuhakikisha kuwa wanafanya kampeni kwa kuzingatia misingi inayolenga kutangaza sera za Vyama vyao pasipo kujenga chuki, kusababisha mifarakano na migawanyiko katika jamii; (l) kuchukua hatua za lazima kuhakikisha kuwa hakuna migongano ya mikutano ya kampeni na Vyama vingine; (m) kukataza wanachama au wafuasi kutamka kauli mbiu, kuonesha ishara za Vyama vyao, au kuvaa sare zenye rangi ya Chama chao katika mikutano ya hadhara ya Vyama vingine; (n) kuwaelekeza Mawakala wao watakaokuwepo katika Vituo vya kupigia, kuhesabia na kujumlishia kura kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi, Taratibu za Maadili ya Uchaguzi na Miongozo ya Uchaguzi. - 2
AI-assisted research summary: Vyama vya siasa na wagombea hawaruhusiwi kufanya vitendo vya fujo, matusi, ubaguzi, kuharibu matangazo, kubandika bila idhini, kutoa rushwa, au kuwazuia wengine kushiriki mikutano au kupiga kura.
2.2 Mambo yasiyotakiwa kufanywa na Vyama vya Siasa na Wagombea Kila Chama cha Siasa au Mgombea hatatakiwa kufanya yafuatayo: (a) kusababisha au kufanya fujo au vurugu ya aina yoyote katika Mkutano wake au wa Chama kingine; (b) kutumia lugha ya matusi, kashfa, kejeli, udhalilishaji na vitisho au lugha inayochochea uvunjifu wa amani au kuashiria ubaguzi wa kijinsia, dini, rangi, ulemavu au maumbile kwenye mikutano ya kampeni; (c) kubeba sanamu, kinyago au kitu chochote ambacho kinaonyesha kudhalilisha, kukebehi, kufedhehesha au kukejeli Chama kingine cha Siasa au Mgombea au Kiongozi wa Chama kingine cha Siasa au Serikali katika mkutano wowote wa kampeni za Uchaguzi; (d) kutumia vipaza sauti vya aina yoyote kwa shughuli za kisiasa mara baada ya muda wa kampeni za uchaguzi kumalizika; (e) kuchafua, kubandua au kuharibu kwa namna yoyote ile matangazo ya kampeni ya Vyama vingine vya Siasa na matangazo mengine yanayotolewa na Mamlaka za Uchaguzi; (f) kubandika mabango ya kampeni, matangazo au mchoro wowote kwenye nyumba, majengo au vyombo vya usafiri vya watu binafsi au taasisi mbalimbali bila idhini ya wamiliki husika; (g) kubandika mabango ya kampeni, matangazo au mchoro wowote kwenye nyumba za ibada, taasisi za dini na majengo ya Serikali na taasisi zake; (h) kutoa rushwa ili kumshawishi mtu yeyote kupiga kura, kugombea au kujitoa katika kugombea nafasi ya uongozi; (i) kuzuia mtu yeyote, watu au wafuasi wa vyama vingine kuhudhuria mikutano ya kampeni au kupiga kura. - 2
AI-assisted research summary: This section concerns conduct during voting, counting, totaling votes, and announcing results.
2.3 ya Uchaguzi Maadili wakati wa kupiga, kuhesabu, kujumlisha kura na kutangaza matokeo - 2
AI-assisted research summary: Wakala wa vyama vya siasa, vyama vya siasa, wagombea na viongozi wa vyama lazima washirikiane na wasimamizi wa uchaguzi katika vituo vya kupigia kura, na viongozi wa vyama lazima waelekeze wanachama na wafuasi wao kuondoka eneo la kupigia kura baada ya kupiga kura.
2.3.1. Yanayotakiwa Kufanywa (a) Mawakala wa Vyama vya Siasa, Vyama vya Siasa na Wagombea watakuwa na wajibu wa kushirikiana na Wasimamizi wa Uchaguzi, Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi na Wasimamizi wa Vituo katika vituo vya kupigia kura kwa kuzingatia Kanuni za Uchaguzi na Miongozo ya Uchaguzi; (b) Viongozi wa Vyama vya Siasa watakuwa na wajibu wa kuwaelimisha wanachama na wafuasi wao kuwa, watatakiwa kuondoka eneo la kupigia Kura mara tu wamalizapo kupiga kura na kama itawalazimu 58 Kanuni za Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kijiji, Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji na Mwenyekiti wa Kitongoji katika Mamlaka za Miji Tangazo la Serikali Na.573 (Linaendelea.) kubakia katika eneo hilo watatakiwa kukaa umbali wa mita mia mbili kutoka kituo cha kupigia kura. - 2
AI-assisted research summary: Election campaigning is not allowed on voting day, and conduct at polling/counting places is restricted.
2.3.2 Mambo yasiyotakiwa kufanywa (a) Kampeni za uchaguzi hazitaruhusiwa siku ya upigaji kura. Hii ni pamoja na kuvaa vazi lolote au kuwa na kitu chochote kinachoashiria kushawishi watu kumpigia kura Mgombea fulani au utambuzi wa Mgombea fulani au matumizi ya chombo cha usafiri kinachoashiria utambuzi wa Chama au Mgombea wa Chama chochote; (b) Viongozi wa Vyama vya Siasa, Wagombea na wafuasi wao watatakiwa kujiepusha na vitendo vinavyoweza kusababisha fujo au vurugu katika vituo vya kupigia, kuhesabia na kujumlishia kura; (c) Hakuna mtu atakayeruhusiwa kutumia simu ya kiganjani ndani ya kituo cha kuhesabu na kujumlishia kura isipokuwa Msimamizi wa Uchaguzi na Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi na mlinzi wa kituo cha kupigia kura ambao watatumia simu zao pale itakapobidi kwa shughuli za Uchaguzi tu na simu hizo wakati wote ziwe zimeondolewa mlio; (d) Kiongozi wa Chama cha Siasa au mwanachama au mfuasi hatatakiwa: (i) kuvamia au kukaa kwa nguvu ndani ya kituo cha kupigia, kuhesabia na kujumlishia kura; (ii) kuwahamasisha wanachama au wafuasi kupiga kura zaidi ya mara moja katika Uchaguzi mmoja; (iii) kununua kura au kutoa rushwa au aina yoyote ya malipo ya fedha au vifaa kwa mpiga kura au Msimamizi wa Uchaguzi au Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi; (iv) kutumia lugha ya matusi kwa Msimamizi wa Uchaguzi, Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi au Msimamizi wa Kituo katika kituo cha kupigia, kuhesabia na kujumlishia kura. - 3
AI-assisted research summary: Serikali lazima ihakikishe usawa kwa wadau wa uchaguzi, usalama na utulivu wakati wa uchaguzi, na kuwafanya viongozi na watendaji wake wazingatie ukomo wa madaraka yao.
3.0 Wajibu wa Serikali: Serikali itakuwa na Wajibu wa: (a) kutoa fursa sawa kwa wadau wote wa Uchaguzi hususan Vyama vya Siasa na Wagombea ili kuendesha shughuli zao za kisiasa wakati wa Uchaguzi kwa uhuru na kuzingatia sheria za nchi; (b) kuhakikisha hali ya usalama, amani na utulivu wakati wote wa Uchaguzi; (c) kuhakikisha kuwa viongozi na watendaji wake wanazingatia ipasavyo ukomo wa madaraka yao katika shughuli za Uchaguzi. - 4
AI-assisted research summary: This section appears to concern ethical procedures for election supervisors and assistant supervisors.
4.0 Uchaguzi Taratibu za Maadili kwa Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi Wasaidizi wa - 4
AI-assisted research summary: Election supervisors and assistant election supervisors must plan, supervise, and conduct elections so they are free and fair.
4.1 Mambo wanayotakiwa Kufanya Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi watakuwa na wajibu wa kupanga, kusimamia na kuendesha Uchaguzi katika misingi inayowezesha Uchaguzi kuwa huru na wa haki kwa kufanya yafuatayo: (a) kuzingatia Katiba ya Nchi, Kanuni za Uchaguzi na Sheria nyingine za nchi; (b) kuvipa Vyama vya Siasa ratiba na taarifa za Uchaguzi mapema; (c) kutoa Elimu ya Mpiga Kura, kusimamia na kuratibu taasisi na watu wanaotoa Elimu ya Mpiga Kura; (d) kutoa mafunzo kwa wanaohusika na Uchaguzi ili kuwawezesha kuendesha uchaguzi kwa ufanisi; (e) kuvipa Vyama vya Siasa Kanuni, Miongozo ya Uchaguzi na Nyaraka nyingine zinazohusiana na Uchaguzi; 59 Kanuni za Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kijiji, Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji na Mwenyekiti wa Kitongoji katika Mamlaka za Miji Tangazo la Serikali Na.573 (Linaendelea.) (f) kukemea vitendo vyenye nia ya kuharibu Uchaguzi vinavyoweza kufanywa na Viongozi wa Vyama vya Siasa, Wagombea au wafuasi wao; (g) kuendesha na kuziwezesha Kamati za kusimamia Maadili ya Uchaguzi na kusimamia utekelezaji wa uamuzi unaotolewa na Kamati hizo; (h) kukutana na Vyama vya Siasa pale inapobidi kujadili masuala mbalimbali yanayohusu Kampeni za Uchaguzi na Uchaguzi wenyewe; (i) kuhakikisha kuwa hakuna mtu yeyote atakayefanyiwa uonevu au kukoseshwa haki wakati wa shughuli za Uchaguzi; (j) kutambua majukumu ya Vyama vya Siasa, Wagombea na Mawakala wao; (k) kuandaa na kupeleka kwa wakati vifaa kwenye vituo vya kupigia kura; (l) kuendesha zoezi la Uchaguzi kwa uwazi, haki na uadilifu. - 4
AI-assisted research summary: Election officials and assistant election officials must not favor any political party or candidate, change campaign schedules without involving political parties, delay or send insufficient materials to polling stations without good reason, or delay announcing election results without good reason.
4.2 Mambo yasiyotakiwa kufanywa na Wasimamizi wa Uchaguzi na Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi (a) kupendelea Chama chochote cha Siasa au Mgombea yeyote; (b) kubadili ratiba za Kampeni za Uchaguzi bila kuvishirikisha Vyama vya Siasa; (c) kuchelewa au kupeleka vifaa pungufu katika vituo vya kupigia kura bila sababu za msingi; (d) kuchelewa kutangaza Matokeo ya Uchaguzi bila sababu za msingi. - 5
AI-assisted research summary: Kifungu hiki kinaweka kichwa cha sehemu kuhusu usimamizi wa utekelezaji wa taratibu za maadili ya uchaguzi.
5.0 Usimamizi wa Utekelezaji waTaratibu za Maadili ya Uchaguzi - 5
AI-assisted research summary: Msimamizi wa Uchaguzi ataweka Kamati za Maadili za Halmashauri na za Kata.
5.1 Kamati za Maadili za kusimamia Utekelezaji wa Taratibu za Maadili ya Uchaguzi Kutakuwa na Kamati za Maadili zifuatazo zitakazoundwa na Msimamizi wa Uchaguzi: (a) Kamati ya Maadili ya Halmashauri; na (b) Kamati ya Maadili ya Kata. - 5
AI-assisted research summary: This section is titled “Muundo wa Kamati za Taratibu za Maadili ya Uchaguzi” (structure of the election ethics procedures committee).
5.2 Muundo wa Kamati za Taratibu za Maadili ya Uchaguzi - 5
AI-assisted research summary: The Halmashauri Ethics Committee must have specific members, including the election supervisor as chair, party representatives, government representatives, and the elections officer as secretary.
5.2.1 Kamati ya Maadili ya Halmashauri itakuwa na wajumbe wafuatao: Kamati ya Maadili ya Halmashauri (a) Msimamizi wa Uchaguzi katika Halmashauri ambaye atakuwa Mwenyekiti wa Kamati; (b) Mjumbe mmoja kutoka kila Chama cha Siasa kinachoshiriki Uchaguzi katika Halmashauri; (c) Wajumbe wawili watakaoiwakilisha Serikali ambao watateuliwa na Katibu Tawala wa Wilaya husika kwa maandishi na kwa kuzingatia jinsia; na (d) Afisa Uchaguzi ambaye atakuwa ni Katibu wa Kamati ya Maadili ya Uchaguzi. - 5
AI-assisted research summary: The Ward Ethics Committee is made up of specified members.
5.2.2 Kamati ya Maadili ya Kata itakuwa na wajumbe wafuatao: Kamati ya Maadili ya Kata (a) Msimamizi Msaidizi ngazi ya Kata husika ambaye atakuwa Mwenyekiti wa Kamati; (b) Mjumbe mmoja kutoka kila Chama cha Siasa kinachoshiriki katika Uchaguzi kwenye Kata; 60 Kanuni za Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kijiji, Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji na Mwenyekiti wa Kitongoji katika Mamlaka za Miji Tangazo la Serikali Na.573 (Linaendelea.) (c) Wajumbe wawili watakaoiwakilisha Serikali ambao watateuliwa na Katibu Tawala wa Wilaya husika kwa maandishi na kwa kuzingatia jinsia; na (d) Katibu ambaye ni Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi ngazi ya kijiji atakayeteuliwa na Msimamizi wa Uchaguzi. - 5
AI-assisted research summary: The provision bans non-chair ethics committee members, candidates, political parties, and certain election actors from disclosing committee decisions or matters before the committee; it also requires complaints to be filed in writing within 3 days and calls for a committee meeting within 2 days after the chair is satisfied there was a breach.
5.2.3 Utoaji wa taarifa za Kamati za Maadili Itakuwa ni marufuku kwa mtu, mgombea, Chama cha Siasa au mjumbe wa Kamati ya Maadili ambaye sio Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili kutoa taarifa yoyote kuhusu uamuzi wa Kamati au suala lolote lililopo mbele ya Kamati. Uwasilishaji wa Malalamiko Mgombea yeyote, Wasimamizi wa Uchaguzi au Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi, Serikali au Chama chenye mgombea kinachoamini kwamba Maadili ya Uchaguzi yamekiukwa kitawasilisha malalamiko kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Kata kwa maandishi. Muda wa kuwasilisha Malalamiko Malalamiko yoyote yatatakiwa kuwasilishwa ndani ya siku tatu tangu kutokea kwa tukio linalolalamikiwa. Kuitisha kikao cha Kamati ya Maadili ya Uchaguzi Mwenyekiti wa Kamati husika baada ya kupokea malalamiko na kujiridhisha kuwa Taratibu za Maadili zimekiukwa atatakiwa kuitisha kikao ndani ya siku mbili. - 5
AI-assisted research summary: Kamati za maadili zinapaswa kushughulikia malalamiko kwa kusikiliza pande husika, kuamua mapema iwezekanavyo, na kuhakikisha utetezi wa maandishi unawasilishwa ndani ya siku mbili.
5.6 Namna ya kushughulikia Malalamiko (a) Malalamiko yote yatajadiliwa na kuamuliwa katika kikao cha Kamati ya Maadili ya Kata husika; (b) Kamati itashughulikia malalamiko na kutoa uamuzi wake mapema iwezekanavyo; (c) Baada ya kupokea malalamiko, Kamati itamtaka aliyelalamikiwa kuwasilisha utetezi wake kwa maandishi ndani ya siku mbili tangu kupokea malalamiko; (d) Katika kushughulikia malalamiko, Kamati inaweza kumwita mtu yeyote kutoa maelezo ili kusaidia Kamati kufikia uamuzi wa haki; (e) Akidi ya Kikao cha Kamati husika itakuwa zaidi ya nusu ya wajumbe wote wa Kamati; (f) Kamati ya Maadili ya Uchaguzi itaamua malalamiko yote baada ya kusikiliza au kupata maelezo ya utetezi kutoka kwa pande zote mbili ambazo ni mlalamikaji na mlalamikiwa ndani ya siku mbili isipokuwa kama upande unaolalamikiwa utashindwa kuwasilisha maelezo ya utetezi katika muda ulioainishwa Kamati inaweza kufanya uamuzi; (g) Uamuzi utakaofikiwa na Kamati ya Maadili ya Kata yatatekelezwa na pande zinazohusika na uamuzi huo; (h) Ikitokea kuna umuhimu wa kufanya uamuzi kwa kupiga kura, wawakilishi wa Mlalamikaji na Mlalamikiwa hawataruhusiwa kupiga kura; (i) Malalamiko yatakayoshughulikiwa na Kamati za Maadili ni yale tu yaliyotokea katika kipindi cha Kampeni; (j) Malalamiko yatakayotokea siku ya Upigaji Kura yatashughulikiwa kwa kuzingatia Kanuni za Uchaguzi; (k) Kamati itakuwa na mamlaka ya kuchunguza malalamiko yote yatakayowasilishwa kabla ya kufanya uamuzi; 61 Kanuni za Uchaguzi wa Mwenyekiti wa Kijiji, Wajumbe wa Halmashauri ya Kijiji na Mwenyekiti wa Kitongoji katika Mamlaka za Miji Tangazo la Serikali Na.573 (Linaendelea.) (l) Kamati inaweza kuelekeza malalamiko mengine kwenye mamlaka zinazohusika kama itakavyoona inafaa kwa hatua zinazostahili. - 5
AI-assisted research summary: Mtu ambaye hajaridhika na uamuzi wa Kamati ya Maadili ya Kata ana haki ya kukata rufaa kwa Kamati ya Maadili ya Halmashauri ndani ya siku mbili.
5.7 Rufaa Dhidi ya Uamuzi (a) Upande ambao hautaridhika na uamuzi wa Kamati ya Maadili ya Kata, utakuwa na haki ya kukata rufaa kwa Kamati ya Maadili ya Halmashauri ndani ya siku mbili tangu uamuzi wa Kamati ya Maadili ya Kata ulipotolewa; na (b) Uamuzi utakaotolewa na Kamati ya Maadili ya Halmashauri utakuwa ni wa mwisho. - 5
AI-assisted research summary: When a complaint is against the election supervisor, the supervisor must not preside over the hearing unless the Regional Administrative Secretary appoints a senior regional-secretariat public officer to chair it.
5.8 Uchaguzi Malalamiko dhidi ya Msimamizi wa Uchaguzi au Msimamizi Msaidizi wa (a) Pale ambapo malalamiko yaliyowasilishwa ni dhidi ya Msimamizi wa Uchaguzi, ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili`ya Uchaguzi, Msimamizi au Msimamizi Msaidizi, Msimamizi wa Uchaguzi hataendesha Kikao hicho, isipokuwa Katibu Tawala wa Mkoa atateua Afisa yeyote wa Umma Mwandamizi kutoka Sekretarieti ya Mkoa kuwa Mwenyekiti wa kikao hicho; (b) Iwapo Kamati itaona kuwa Msimamizi amekosea Kamati itamtaka linalolalamikiwa Msimamizi wa Uchaguzi kurekebisha mapema iwezekanavyo. tatizo - 5
AI-assisted research summary: Kamati za Maadili ya Uchaguzi za Halmashauri na Kata zinaweza kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya upande uliokiuka maadili, ikiwemo kuagiza marekebisho, onyo la maandishi, tangazo la ukiukaji, na kusimamisha kampeni kwa muda.
5.9 Mamlaka ya Kamati za Maadili ya Uchaguzi ngazi ya Halmashauri na Kata katika kushughulikia Malalamiko na kutoa adhabu zinaweza kuchukua hatua zifuatazo: (a) kuagiza upande uliokiuka maadili kusahihisha kosa au makosa yaliyotendeka na iwapo italazimu, kuomba msamaha hadharani; (b) kutoa onyo au karipio kwa maandishi; (c) kutangaza jina la Chama au Mgombea aliyekiuka Maadili na kueleza kosa au makosa yake kwa njia za Taarifa kwa Umma, redio, televisheni, magazeti na njia nyingine za mawasiliano; (d) Kamati inaweza kukisimamisha Chama au Mgombea kuendelea kufanya Kampeni za Uchaguzi kwa muda itakavyoona inafaa. - 5
AI-assisted research summary: If a candidate or party fails to implement the relevant committee’s decision, the Election Ethics Committee may suspend the party from campaigning.
5.10 Kushindwa Kutekeleza Uamuzi wa Kamati za Maadili Pale ambapo Mgombea au Chama kitashindwa kutekeleza uamuzi wa Kamati husika, Kamati ya Maadili ya Uchaguzi inaweza kukisimamisha Chama husika kufanya kampeni za Uchaguzi. Dodoma, 28 Juni, 2024 MOHAMED OMARY MCHENGERWA, Waziri wa Nchi, OR-TAMISEMI 62
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
KANUNI ZA UCHAGUZI WA MWENYEKITI WA KIJIJI, WAJUMBE WA HALMASHAURI YA KIJIJI NA MWENYEKITI WA KITONGOJI KATIKA MAMLAKA ZA MIJI ZA MWAKA 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in