SHERIA NDOGO YA UANZISHWAJI WA BODI YA MFUKO WA ELIMU YA HALMASHAURI YA MJI WA NEWALA YA MWAKA 2024
This section gives the short title of the by-law.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- SHERIA NDOGO YA UANZISHWAJI WA BODI YA MFUKO WA ELIMU YA HALMASHAURI YA MJI WA NEWALA YA MWAKA 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This section gives the short title of the by-law. This by-law applies throughout the area of Newala Town Council. This section defines key terms used in the bylaw, including the Board, Council, Executive Committee, Education Fund, Member, Director, Education Fund Coordinator, and Chairperson. This section establishes the Council’s Education Fund Board and says it will be known as the Board. Bodi ina majukumu ya kusimamia, kuidhinisha, kushirikiana, na kufadhili shughuli mbalimbali za Mfuko wa Elimu na maendeleo ya elimu.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of SHERIA NDOGO YA UANZISHWAJI WA BODI YA MFUKO WA ELIMU YA HALMASHAURI YA MJI WA NEWALA YA MWAKA 2024
Showing 39 of 39
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo
AI-assisted research summary: This section gives the short title of the by-law.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Uanzishwaji wa Bodi ya Mfuko wa Elimu ya Halmashauri ya Mji wa Newala ya Mwaka 2024. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la
AI-assisted research summary: This by-law applies throughout the area of Newala Town Council.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la Halmashauri ya Mji wa Newala. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the bylaw, including the Board, Council, Executive Committee, Education Fund, Member, Director, Education Fund Coordinator, and Chairperson.
3. Katika Sheria Ndogo hii isipokuwa pale muktadha utahitaji vinginevyo: “Bodi” maana yake ni Bodi ya Mfuko wa Elimu ya Halmashauri ya Mji wa Newala; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Mji wa Newala; “Kamati ya Utendaji ya Mfuko wa Elimu” maana yake ni Kamati ya Utendaji ya Mfuko wa Elimu iliyoanzishwa chini ya Sheria Ndogo hii; “Mfuko wa Elimu” maana yake ni Mfuko wa Elimu ulioanzishwa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii; “Mjumbe” maana yake ni Mjumbe wa Bodi na itajumuisha Mwenyekiti wa Bodi; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Newala au Afisa yeyote ya aliyeteuliwa Mkurugenzi; majukumu kutekeleza “Mratibu wa Mfuko wa Elimu” maana yake ni Mratibu wa Mfuko wa Elimu aliyeteuliwa kwa mujibu wa 1 Sheria Ndogo ya Uanzishwaji wa Bodi ya Mfuko wa Elimu ya Halmashauri ya Mji wa Newala Tangazo la Serikali Na.584 (Linaendelea.) Sheria Ndogo hii; na “Mwenyekiti” maana yake ni Mwenyekiti wa Bodi. Bodi ya Mfuko wa Elimu - 4 Verify source ↗
(1) Kutakuwa na Bodi ya Mfuko wa Elimu ya
AI-assisted research summary: This section establishes the Council’s Education Fund Board and says it will be known as the Board.
4.-(1) Kutakuwa na Bodi ya Mfuko wa Elimu ya Halmashauri ambayo katika Sheria hii itajulikana kama Bodi. (2) Bodi itakuwa na Wajumbe wafuatao: (a) Mwenyekiti; (b) wawakilishi wawili wa jamii ambapo mmoja kati yao atakuwa mwanamke; (c) mwakilishi mmoja wa wakuu wa shule, atakayepatikana kutoka miongoni mwa wakuu wa shule za sekondari za serikali zilizopo katika eneo la Halmashauri; (d) mwakilishi mmoja wa wakuu wa shule za msingi, atakayepatikana kutoka miongoni mwa walimu wakuu wa shule za msingi zilizopo katika eneo la Halmashauri; (e) mwakilishi mmoja kutoka miongoni mwa wamiliki wa shule zisizo za Serikali; (f) Katibu Tawala wa Wilaya ya Newala; na (g) Diwani mmoja kutoka Kamati ya Huduma za Jamii ya Halmashauri. (3) Masharti kuhusu utaratibu wa kuwapata wajumbe wa Bodi, uundaji wa Bodi, muda wa kuhudumu kwa wajumbe wa Bodi na uendeshaji wa shughuli za Bodi yatakuwa kama yalivyoainishwa katika Jedwali la Kwanza. - 5 Verify source ↗
(1) Bodi itakuwa na majukumu yafuatayo
AI-assisted research summary: Bodi ina majukumu ya kusimamia, kuidhinisha, kushirikiana, na kufadhili shughuli mbalimbali za Mfuko wa Elimu na maendeleo ya elimu.
5.-(1) Bodi itakuwa na majukumu yafuatayo: (a) kusimamia uendeshaji wa Mfuko wa Elimu kwa kufuata bajeti iliyoidhinishwa na mkutano mkuu wa mwaka wa Bodi; (b) kujadili na kurekebisha bajeti na mipango ya Mfuko wa Elimu; (c) kupokea, kuchambua na kuidhinisha taarifa za utekelezaji wa malengo ya Mfuko wa Elimu; (d) kusimamiana na kushauri kuhusu utekelezaji wa mipango na mikakati kwa ajili ya 2 Majukumu ya Bodi Sheria Ndogo ya Uanzishwaji wa Bodi ya Mfuko wa Elimu ya Halmashauri ya Mji wa Newala Tangazo la Serikali Na.584 (Linaendelea.) maendeleo ya elimu katika Halmashauri; (e) kusimamia mgawanyo wa misaada kwa shule na tasisi za elimu kufuatana na vipaumbele vya Halmashauri; (f) kusaidia shughuli za maendeleo ya elimu katika Halmashauri; ujenzi (g) kusimamia ukarabati wa miundombinu ya shule na taasisi za elimu za Halmashauri unaofadhiliwa na Mfuko; na (h) kushirikiana na Kamati ya Huduma za Jamii ya Halmashauri; (i) kufadhili shughuli za ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya elimu ndani ya eneo la Halmashauri; (j) kupitisha kanuni za utengaji na utumiaji wa fedha kutoka kwenye Mfuko wa Elimu; (k) kuisimamia Kamati ya Utendaji ya Mfuko wa Elimu katika utekelezaji wa majukumu yake; (l) kubuni vyanzo mbalimbali vya mapato na rasilimali za kuendeshea Mfuko wa Elimu wa Halmashauri; (m) kusimamia shughuli za maendeleo ya elimu katika Halmashauri kulingana na mipango ya kitaifa; na (n) kufanya jambo lolote litakalofanikisha maendeleo ya elimu katika Halmashauri. (2) Katika utekelezaji wa majukumu yake, Bodi itashirikiana na Halmashauri kwa madhumuni ya kuhakikisha kuwa fedha na rasilimali za Mfuko wa Elimu zinasimamiwa kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu zinazosimamia fedha na rasilimali za umma. Ofisi za Bodi - 6 Verify source ↗
Ofisi za Bodi, zitakuwa katika eneo
AI-assisted research summary: Ofisi za Bodi lazima ziwe katika eneo la Halmashauri au mahali pengine Bodi itakapoamua.
6. Ofisi za Bodi, zitakuwa katika eneo la Halmashauri au sehemu itakayoamuliwa na Bodi Kukasimu madaraka - 7 Verify source ↗
(1) Kupitia azimio maalumu, Bodi inaweza
AI-assisted research summary: Bodi inaweza kukasimu majukumu yake kwa kamati, Mratibu au Mjumbe wa Bodi kwa azimio maalumu, na inaweza kuweka masharti ya utekelezaji wa majukumu hayo yaliyokasimiwa.
7.-(1) Kupitia azimio maalumu, Bodi inaweza kukasimu majukumu yake yaliyoainishwa katika Sheria Ndogo hii kwa kamati, Mratibu au Mjumbe yeyote wa Bodi. 3 Sheria Ndogo ya Uanzishwaji wa Bodi ya Mfuko wa Elimu ya Halmashauri ya Mji wa Newala Tangazo la Serikali Na.584 (Linaendelea.) (2) Kwa kuzingatia masharti ya kanuni ndogo ya (1), Bodi inaweza kuweka masharti mbalimbali kuhusu utekelezaji wa majukumu yaliyokasimiwa. (3) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (1), Bodi haitakasimu majukumu yafuatayo: (a) kusimamia uendeshaji wa Mfuko wa Elimu; (b) kujadili na kurekebisha mipango na bajeti ya Mfuko wa Elimu na kuiwasilisha kwenye Baraza la Madiwani; (c) kupokea, kuchambua na kuidhinisha taarifa za utekelezaji wa malengo ya Mfuko wa Elimu; (d) kushauri kuhusu utekelezaji wa mipango na mikakati kwa ajili ya maendeleo ya elimu katika Halmashauri; (e) kupitisha kanuni za utengaji na utumiaji wa fedha kutoka kwenye Mfuko wa Elimu; na (f) kuisimamia Kamati ya Utendaji ya Mfuko wa Elimu katika utekelezaji wa majukumu yake. Ushirikishwaji wa jamii - 8 Verify source ↗
Katika utekelezaji wa majukumu yake, Bodi
AI-assisted research summary: Bodi lazima kuhakikisha jamii inashirikishwa katika kutambua na kutatua changamoto za elimu, kuweka vipaumbele, na kufuatilia na kutathmini utoaji wa huduma za elimu; pia lazima kuwe na uwazi na uwajibikaji.
8. Katika utekelezaji wa majukumu yake, Bodi itahakikisha kuwa- Uwajibikaji wa Bodi Mfuko wa Elimu (a) jamii inashirikishwa katika utambuzi wa changamoto za elimu na utatuziwa changamoto hizo, uwekaji wa vipaumbele, na ufuatiliaji na tathmini kuhusu utoaji wa ufanyikaji wa huduma za elimu. (b) kuna kuwepo na uwazi na uwajibikaji. - 9 Verify source ↗
Katika utekelezaji wa majukumu yake, Bodi
AI-assisted research summary: Bodi must be accountable to Halmashauri when carrying out its duties.
9. Katika utekelezaji wa majukumu yake, Bodi itawajibika kwa Halmashauri. - 10 Verify source ↗
Kutakuwa na Mfuko wa Elimu wa
AI-assisted research summary: The provision says there will be an Education Fund and lists the fund’s purposes.
10. Kutakuwa na Mfuko wa Elimu wa kwa madhumuni utatumika ambao Halmashauri yafuatayo: (a) kuboresha, kuendeleza na kukuza utoaji wa elimu bora kulingana na vipaumbele vya Halmashauri; (b) kugharamia miradi na programu za Mfuko wa Elimu; 4 Sheria Ndogo ya Uanzishwaji wa Bodi ya Mfuko wa Elimu ya Halmashauri ya Mji wa Newala Tangazo la Serikali Na.584 (Linaendelea.) Vyanzo vya mapato ya mfuko wa elimu Kamati ya utendaji ya mfuko wa Elimu (c) kudhamini wanafunzi wasio na uwezo wa kumudu gharama za huduma za elimu; (d) kujenga au kukarabati miundombinu ya shule zilizopo katika eneo la Halmashauri; (e) kununua vifaa vya kufundishia na kujifunzia; (f) kugharamia shughuli nyingine yoyote ambayo kwa maoni ya Bodi ina manufaa kulingana na malengo na madhumuni ya Mfuko wa Elimu; na (g) kugharamia uendeshaji wa Mfuko wa Elimu na Bodi. - 11 Verify source ↗
Mfuko wa Elimu utakuwa na vyanzo vya
AI-assisted research summary: The Education Fund has several revenue sources, including voluntary contributions, specified contributions from working residents in the Council area, grants, loans, 3% of Council internal revenue, and other lawful income sources.
11. Mfuko wa Elimu utakuwa na vyanzo vya mapato vifuatavyo: (a) michango ya hiari ya watu binafsi, wadau wa elimu na washirika wa maendeleo; (b) michango ya kila mwananchi mwenye uwezo wa kufanya kazi anayeishi katika eneo la Halmashauri kwa viwango vilivyoainishwa katika Jedwali la Pili; (c) misaada kutoka kwa wadau mbalimbali; (d) mikopo; (e) mchango wa rasilimali au asilimia tatu (3%) ya fedha kutoka kwenye mapato ya ndani ya Halmashauri; na (f) vyanzo vingine halali vya mapato. - 12 Verify source ↗
Kutakuwa na Kamati ya Utendaji ya Mfuko wa
AI-assisted research summary: This section creates the Education Fund Executive Committee and lists its members.
12. Kutakuwa na Kamati ya Utendaji ya Mfuko wa Elimu ambayo itakuwa na wajumbe wafuatao: (a) Mkurugenzi ambaye atakuwa Mwenyekiti; (b) Mkuu wa Idara ya Elimu Msingi; (c) Mkuu wa Idara ya Elimu Sekondari; (d) Mkuu wa Idara ya Uchumi na Mipango; (e) Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii; (f) Mkuu wa Idara ya Ujenzi; na (g) Mkuu wa Kitengo cha Sheria. 5 Sheria Ndogo ya Uanzishwaji wa Bodi ya Mfuko wa Elimu ya Halmashauri ya Mji wa Newala Tangazo la Serikali Na.584 (Linaendelea.) Majukumu ya kamati ya utendaji Mratibu wa Mfuko wa Elimu - 13 Verify source ↗
Kamati ya Utendaji itakuwa na majukumu
AI-assisted research summary: Kamati ya Utendaji lazima itekeleze majukumu ya kusimamia Mfuko wa Elimu na masuala ya elimu ya Halmashauri.
13. Kamati ya Utendaji itakuwa na majukumu yafuatayo: (a) kuratibu na kuhamasisha uchangiaji wa hiari wa Mfuko wa Elimu; (b) kuandaa mipango kabambe ya Halmashauri katika sekta ya elimu ambayo itatilia mkazo mahitaji yote ya elimu katika Halmashauri kwa kuzingatia Mwongozo wa Kitaifa wa Maendeleo ya Elimu; (c) kubaini, kuanzisha na kuratibu vyanzo vya mapato ya Mfuko wa Elimu; (d) kuwezesha na kuratibu vikao vya Bodi; (e) kuchambua na kubainisha vipaumbele vya masuala ya elimu katika Halmashauri; (f) kuweka taratibu na vigezo vya ufadhili wa wanafunzi na utoaji ruzuku kwa miradi ya elimu katika Halmashuri; na (g) kuandaa taarifa za utekelezaji kuhusu Mfuko wa Elimu na maendeleo ya elimu katika Halmashauri. - 14 Verify source ↗
(1) Kutakuwa na Mratibu wa Mfuko wa Elimu
AI-assisted research summary: Mkurugenzi lazima amteue Mratibu wa Mfuko wa Elimu kutoka kwa watumishi waandamizi wenye sifa zilizotajwa; Mratibu huhudumu kwa miaka minne na pia ndiye Katibu wa Bodi na wa Kamati ya Utendaji.
14.-(1) Kutakuwa na Mratibu wa Mfuko wa Elimu atakayeteuliwa na Mkurugenzi kutoka miongoni mwa watumishi waandamizi wa Halmashauri mwenye uzoefu na ujuzi katika masuala ya elimu, sheria, utawala au Uchumi (2) Mratibu wa Mfuko wa Bodi aliyeteuliwa kwa mujibu wa kanuni ndogo ya (1) atahudumu kwa muda wa miaka minne (3) Bila kuathiri masharti mengine ya kanuni hii, Mratibu atakayeteuliwa Pamoja na majukumu ya Mfuko wa elimu ataendelea kutekeleza majukumu yake ya kawaida ya kiutumishi. (4) Mratibu atakuwa Katibu wa Bodi na Katibu wa Kamati ya Utendaji. Majukumu ya Mratibu - 15 Verify source ↗
Mratibu atakuwa na majukumu yafuatayo
AI-assisted research summary: Mratibu lazima atekeleze majukumu ya uendeshaji wa Mfuko wa Elimu, ikiwemo kusimamia Mfuko na shughuli za Bodi, kuandaa mipango na bajeti, kuwasilisha taarifa, kutunza kumbukumbu na hesabu, na kuratibu utendaji wa shughuli za Mfuko.
15. Mratibu atakuwa na majukumu yafuatayo: (a) kuwa Mtendaji Mkuu wa Mfuko na shughuli za Bodi; 6 Sheria Ndogo ya Uanzishwaji wa Bodi ya Mfuko wa Elimu ya Halmashauri ya Mji wa Newala Tangazo la Serikali Na.584 (Linaendelea.) (b) kuandaa na kutekeleza mipango ya maendeleo pamoja na bajeti ya Mfuko wa Elimu; (c) kuandaa na kuwasilisha taarifa kwenye vikao vya Bodi na mamlaka zinazohusika; (d) kutunza kumbukumbu, nyaraka na mali zote za Mfuko wa Elimu wa Halmashauri kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu; (e) kusimamia na kutunza hesabu zote za mapato na matumizi ya Mfuko wa Elimu; (f) kushauri mbinu mbalimbali za kukuza na kuendeleza Mfuko wa Elimu wa Halmashauri; na (g) kuongoza, kupanga na kuratibu utendaji wa shughuli za Mfuko wa Elimu. Akaunti ya mfuko wa Elimu - 16 Verify source ↗
(1) Kutakuwa na akaunti ya benki ya Mfuko
AI-assisted research summary: The Education Fund must have a bank account to hold all money received for the Fund, and its signatories must be either the Director plus a Board-approved member, or the Coordinator plus a Board-approved member.
16.-(1) Kutakuwa na akaunti ya benki ya Mfuko itatumika kuhifadhi fedha zote wa Elimu ambayo zitakazopokelewa kwa madhumuni ya Mfuko wa Elimu. (2) Katika kuendesha akaunti ya Mfuko wa Elimu, wawekaji saini watakuwa: (a) Mkurugenzi na Mjumbe atakaye idhinishwa na Bodi; au (b) Mratibu na Mjumbe atakayeidhinishwa na Bodi. Usimamizi wa rasilimali - 17 Verify source ↗
Rasilimali au misaada yoyote tofauti na fedha
AI-assisted research summary: Resources or aid other than money given for the Education Fund must be received and entered in a special register.
17. Rasilimali au misaada yoyote tofauti na fedha itakayotolewa kwa ajili ya Mfuko wa Elimu itapokelewa na kuingizwa kwenye rejesta maalum ya Mfuko wa Elimu. Ukaguzi wa Mfuko Taarifa ya kamati ya utendaji ya miezi mitatu - 18 Verify source ↗
Hesabu za mwaka za Mfuko wa Elimu
AI-assisted research summary: The annual accounts of the Education Fund must be audited under the public funds audit procedure.
18. Hesabu za mwaka za Mfuko wa Elimu zitakaguliwa kwa mujibu wa utaratibu wa ukaguzi wa fedha za umma. - 19 Verify source ↗
(1) Kamati ya Utendaji ina wajibu wa kuandaa
AI-assisted research summary: Kamati ya Utendaji must prepare and submit a quarterly performance report to the Board.
19.-(1) Kamati ya Utendaji ina wajibu wa kuandaa na kuwasilisha katika kikao cha Bodi taarifa ya miezi mitatu ya utekelezaji wa majukumu ya Bodi, Kamati ya Utendaji na Mfuko wa Elimu. (2) Bila kuathiri masharti kanuni ndogo ya (1), 7 Sheria Ndogo ya Uanzishwaji wa Bodi ya Mfuko wa Elimu ya Halmashauri ya Mji wa Newala Tangazo la Serikali Na.584 (Linaendelea.) Taarifa ya mwaka ya Kamati ya Utendaji Taarifa ya Bodi ya miezi mitatu taarifa itakayowasilishwa itaainisha yafuatayo: (a) mapato na matumizi kwa kipindi husika; (b) kazi zilizofanyika, mafanikio yaliyopatikana na changamoto; (c) viashiria vya utendaji na taarifa nyingine zinazohusiana navyo; na (d) masuala mengine kadri Bodi itakavyoelekeza. - 20 Verify source ↗
(1) Kamati ya Utendaji itakuwa na wajibu wa
AI-assisted research summary: Kamati ya Utendaji lazima iandae na iwasilishe taarifa ya mwaka katika kikao cha Bodi.
20.-(1) Kamati ya Utendaji itakuwa na wajibu wa kuandaa na kuwasilisha katika kikao cha Bodi taarifa ya mwaka ya utekelezaji wa majukumu ya Bodi, Kamati ya Utendaji na Mfuko wa Elimu. (2) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (1), taarifa itakayowasilishwa itaainisha yafuatayo: (a) mipango na bajeti ya Mfuko kwa mwaka wa fedha unaofuata; (b) utekelezaji wa majukumu katika kipindi cha mwaka mmoja; (c) mapato na matumizi katika kipindi cha mwaka mmoja; (d) mipango ya kimkakati ya kuimarisha Mfuko wa Elimu; na (e) mpango kazi wa Bodi na Kamati ya Utendaji kwa mwaka unaofuata. - 21 Verify source ↗
(1) Bodi itakuwa na wajibu wa kuandaa na
AI-assisted research summary: Bodi lazima iandae na iwasilishe ripoti ya kila miezi mitatu kuhusu utekelezaji wa majukumu yake, ya Kamati ya Utendaji, na ya Mfuko wa Elimu mbele ya Kamati ya Kudumu ya Halmashauri ya Huduma za Jamii.
21.-(1) Bodi itakuwa na wajibu wa kuandaa na kuwasilisha katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Halmashauri ya Huduma za Jamii taarifa ya miezi mitatu ya utekelezaji wa majukumu ya Bodi, Kamati ya Utendaji na Mfuko wa Elimu. (2) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (1), taarifa itakayowasilishwa itaainisha masuala yafuatayo: (a) mapato na matumizi kwa kipindi husika; (b) kazi zilizofanyika, mafanikio yaliyopatikana na changamoto; (c) viashiria vya utendaji na taarifa nyingine zinazohusiana navyo; na (d) masuala mengine kwa kadri Kamati ya Kudumu ya Halmashauri ya Huduma za Jamii 8 Sheria Ndogo ya Uanzishwaji wa Bodi ya Mfuko wa Elimu ya Halmashauri ya Mji wa Newala Tangazo la Serikali Na.584 (Linaendelea.) Taarifa ya Bodi ya mwaka itakavyoelekeza. - 22 Verify source ↗
(1) Bodi itakuwa na wajibu wa kuandaa na
AI-assisted research summary: Bodi lazima iandae na kuwasilisha taarifa ya mwaka kwenye kikao cha Kamati ya Kudumu ya Halmashauri ya Huduma za Jamii.
22.-(1) Bodi itakuwa na wajibu wa kuandaa na kuwasilisha katika kikao cha Kamati ya Kudumu ya Halmashauri ya Huduma za Jamii taarifa ya mwaka ya utekelezaji wa majukumu ya Bodi, Kamati ya Utendaji na Mfuko wa Elimu. (2) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (1), taarifa itakayowasilishwa itaainisha yafuatayo: (a) mipango na bajeti ya Mfuko kwa mwaka wa fedha unaofuata; (b) utekelezaji wa majukumu katika kipindi cha mwaka mmoja; (c) mapato na matumizi katika kipindi cha mwaka mmoja; (d) mipango ya kimkakati ya kuimarisha Mfuko wa Elimu; na (e) Mpango Kazi wa Bodi na Kamati ya Utendaji kwa mwaka unaofuata. Wajibu wa Kamati ya Kudumu ya Huduma za Jamii - 23 Verify source ↗
Kamati ya Kudumu ya Huduma za Jamii ya
AI-assisted research summary: Kamati ya Kudumu ya Huduma za Jamii ya Halmashauri lazima ichunguze taarifa kutoka kwa Bodi na iwasilishe mapendekezo yake kwa Halmashauri kwa uamuzi.
23. Kamati ya Kudumu ya Huduma za Jamii ya Halmashauri itakuwa na wajibu wa kupitia na kuchambua taarifa itakayowasilishwa na Bodi na kuwasilisha mapendekezo yake kwa Halmashauri kwa ajili ya uamuzi wake. Utekelezaji wa Sheria ya Mfuko wa Elimu Sura ya 412 - 24 Verify source ↗
Kwa madhumuni ya kuwezesha utekelezaji wa
AI-assisted research summary: Bodi kupitia kwa Mkurugenzi lazima iwasilishe orodha ya wadau waliochangia kwa Mamlaka ya Elimu Tanzania na ichangie shilingi laki moja kila mwaka katika Mfuko wa Elimu.
24. Kwa madhumuni ya kuwezesha utekelezaji wa Sheria ya Mfuko wa Elimu kuhusu uhamasishaji wa uchangiaji katika sekta ya elimu na utoaji wa tuzo kwa wadau wanaochangia, Bodi kupitia kwa Mkurugenzi itakuwa na wajibu wa: (a) kuwasilisha kwa Mamlaka ya Elimu Tanzania orodha ya majina ya wadau waliochangia katika Mfuko wa Elimu ikionesha kiasi cha fedha au rasilimali nyingine zilizopokelewa na Mfuko wa Elimu; na (b) kuchangia kiasi cha shilingi laki moja kwa mwaka katika Mfuko ulioanzishwa chini ya Sheria ya Mfuko wa Elimu. 9 Sheria Ndogo ya Uanzishwaji wa Bodi ya Mfuko wa Elimu ya Halmashauri ya Mji wa Newala Tangazo la Serikali Na.584 (Linaendelea.) Makosa na adhabu Kufifilisha kosa - 25 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote anatenda kosa chini ya Sheria
AI-assisted research summary: Anyone who hinders the Board or Executive Committee, misuses Education Fund property/resources, or fails to carry out a duty under the By-law commits an offence.
25.-(1) Mtu yeyote anatenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii endapo- (a) atatenda kitu chochote ambacho kitazuia Bodi au Kamati ya Utendaji kufanya kazi zake kwa ufanisi; (b) atatumia vibaya mali au rasilimali za Mfuko wa Elimu; au (c) atashindwa kutekeleza wajibu wake kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. (2) Mtu aliyetenda kosa chini ya kanuni hii akipatikana na hatia atatakiwa kulipa faini ya kiasi kisichozidi shilingi milioni moja au kifungo kisichozidi miezi kumi na mbili au adhabu zote mbili kwa pamoja. - 26 Verify source ↗
Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa kwa kumtoza mkosaji shilingi laki mbili, akiri kosa na akubali kujaza fomu maalum na kulipa anachodaiwa.
26. Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha kosa kwa kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii kiasi cha shilingi laki mbili endapo mkosaji atakiri kosa na kuwa tayari kujaza fomu maalum iliyoainishwa katika Jedwali la Tatu na kulipa mchango au mali au rasilimali anayodaiwa. 10 Sheria Ndogo ya Uanzishwaji wa Bodi ya Mfuko wa Elimu ya Halmashauri ya Mji wa Newala Tangazo la Serikali Na.584 (Linaendelea.) ______ JEDWALI LA KWANZA ______ (Limetengenezwa chini ya aya ya 4(3)) TARATIBU ZA BODI Sifa ya Mjumbe wa Bodi Utaratibu wa kuwapata wajumbe
Part
JEDWALI LA KWANZA
- 1 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote anaweza kuwa Mjumbe wa Bodi endapo atakuwa
AI-assisted research summary: Mtu yeyote anaweza kuwa Mjumbe wa Bodi ikiwa anakidhi masharti ya uraia, umri, afya ya akili, elimu, uadilifu wa jinai, kutokuwa na uongozi wa chama cha siasa, na ukazi wa Halmashauri; baadhi ya masharti hayatumiki kwa wawakilishi fulani, na mtumishi wa Halmashauri au Diwani hawezi kuteuliwa kuwa Mwenyekiti.
1.-(1) Mtu yeyote anaweza kuwa Mjumbe wa Bodi endapo atakuwa na sifa zifuatazo: (a) awe ni raia wa Tanzania; (b) awe na umri usiopungua miaka ishirini na mitano na asizidi miaka sabini; (c) awe na akili timamu; (d) awe na elimu ya Sekondari na kuendelea; (e) asiwe na nafasi yoyote ya uongozi kwenye chama cha siasa; (f) asiwe amewahi kutiwa hatiani kwa kosa lolote la jinai linalohusu ukosefu wa uaminifu; na (g) awe mkazi wa Halmashauri. (2) Masharti ya aya ndogo ya (1)(a) hayatatumika kwa mjumbe anayewakilisha mashirika yasiyo ya kiserikali; na (3) Masharti ya aya ndogo aya ndogo ya (1)(e) hayatatumika kwa mjumbe anayewakilisha Kamati ya Kudumu ya Halmashauri ya Huduma za Jamii. (4) Kwa kuzingatia masharti ya aya ndogo ya (1), mtumishi wa Halmashauri au Diwani hatakuwa na sifa ya kuteuliwa kuwa Mwenyekiti. - 2 Verify source ↗
(1) Mkurugenzi, kwa maelekezo ya Halmashauri, atatangaza
AI-assisted research summary: Mkurugenzi, kwa maelekezo ya Halmashauri, anatakiwa kutangaza nafasi za Mwenyekiti na wajumbe wa Bodi; tangazo lichapishwe na litaainisha sifa, kisha timu ichambue maombi na Halmashauri itawateua.
2.-(1) Mkurugenzi, kwa maelekezo ya Halmashauri, atatangaza kuwepo kwa nafasi ya Mwenyekiti na wajumbe wa Bodi walioainishwa katika aya ya 1(1) ya Jedwali hili. (2) Tangazo litakalotolewa kwa mujibu wa aya ya 1(1) litachapishwa katika gazeti linalosambazwa katika eneo la Halmashauri na mbao za matangazo katika Ofisi za Halmashauri, Kata na Vijiji na litaainisha sifa za wajumbe wa Bodi. (3) Timu ya Menejimenti ya Halmashauri itachambua maombi yatakayowasilishwa na kupendekeza kwa Kamati ya Kudumu ya Halmashauri ya Huduma za Jamii majina ya watu wenye sifa kwa ajili ya kuyapendekeza kwa Halmashauri. (4) Halmashauri baada ya kupokea majina kwa mujibu wa aya ya 2(3) itateua Mwenyekiti na wajumbe wa Bodi. Muda wa kuhudumu - 3 Verify source ↗
(1) Mjumbe wa Bodi atahudumu kwa kipindi cha miaka mitatu na
AI-assisted research summary: Mjumbe wa Bodi anahudumu kwa miaka mitatu na anaweza kuteuliwa tena mara moja. Mwenyekiti au Mjumbe hupoteza nafasi yao iwapo watakufa, watajiuzulu kwa taarifa ya maandishi ya mwezi mmoja, watapata ulemavu au ugonjwa unaowazuia kutekeleza majukumu, watakosa vikao vitatu mfululizo bila sababu za msingi, au watapoteza sifa zao. Nafasi wazi haizuii shughuli za Bodi kuendelea.
3.-(1) Mjumbe wa Bodi atahudumu kwa kipindi cha miaka mitatu na anaweza kuteuliwa tena kwa kipindi kingine kimoja. (2) Bila kuathiri masharti ya aya ndogo ya (1), Mwenyekiti au Mjumbe atapoteza nafasi yake endapo litatokea mojawapo ya yafuatayo: (a) kufariki; (b) kujiuzulu baada ya kutoa taarifa ya maandishi ya mwezi mmoja kwa Mwenyekiti na ikiwa anayejiuzulu ni Mwenyekiti, baada ya kutoa taarifa ya maandishi ya mwezi mmoja kwa Mwenyekiti wa Halmashauri; (c) kupata ulemavu au ugonjwa unaosababisha ashindwe kutekeleza majukumu yake katika Bodi; 11 Sheria Ndogo ya Uanzishwaji wa Bodi ya Mfuko wa Elimu ya Halmashauri ya Mji wa Newala Tangazo la Serikali Na.584 (Linaendelea.) Utaratibu wa kujaza nafasi za Bodi zilizo wazi Uzinduzi wa Bodi Kuvunjwa kwa Bodi Vikao vya kawaida vya Bodi Vikao vya dharura (d) kutohudhuria vikao vitatu mfululizo bila sababu za msingi; au (e) kupoteza sifa iliyomfanya awe Mwenyekiti au Mjumbe wa Bodi. (3) Kuwepo kwa nafasi wazi hakutaathiri uendeshaji wa shughuli za Bodi. - 4 Verify source ↗
Endapo itatokea nafasi wazi katika Bodi, utaratibu wa kuwapata
AI-assisted research summary: If a Board vacancy occurs, it is filled using the procedure set out in the Schedule, unless the Board has less than six months left to run.
4. Endapo itatokea nafasi wazi katika Bodi, utaratibu wa kuwapata wajumbe ulioainishwa katika Jedwali hili, utatumika kujaza nafasi ya Bodi, Isipokuwa kwamba, nafasi wazi haitajazwa ikiwa muda wa uhai wa Bodi ni chini ya miezi sita. - 5 Verify source ↗
Baada ya uteuzi wa Mwenyekiti na wajumbe wa Bodi na
AI-assisted research summary: Baada ya mwenyekiti na wajumbe wa Bodi kuteuliwa na kuidhinishwa na Baraza la Madiwani, Mkurugenzi anaweza kualika viongozi fulani kuizindua Bodi.
5. Baada ya uteuzi wa Mwenyekiti na wajumbe wa Bodi na kuidhinishwa na Baraza la Madiwani, Mkurugenzi anaweza kumwalika Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya, Mwenyekiti au Meya wa Halmashauri kuizindua Bodi. - 6 Verify source ↗
(1) Endapo Bodi itashindwa kutekeleza majukumu yake kwa
AI-assisted research summary: If the Board fails to perform its duties, the Council may dissolve it and start forming a new Board within two months.
6.-(1) Endapo Bodi itashindwa kutekeleza majukumu yake kwa sababu yoyote ile, Halmashauri inaweza kuivunja Bodi na kuanzisha taratibu za kuundwa kwa Bodi mpya ndani ya muda wa miezi miwili. (2) Endapo Bodi itavunjwa, Mwenyekiti na wajumbe wote watapoteza nafasi zao na hawatachaguliwa tena kuwa wajumbe wa Bodi ya Mfuko wa Elimu. (3) Endapo Bodi itavunjwa, majukumu yake yatatekelezwa na Kamati ya Utendaji, mpaka pale Bodi mpya itakapoundwa. - 7 Verify source ↗
(1) Vikao vya kawaida vya Bodi vitaitishwa na Mwenyekiti kila
AI-assisted research summary: The Chair must convene ordinary Board meetings every three months and give seven days’ written notice to all members.
7.-(1) Vikao vya kawaida vya Bodi vitaitishwa na Mwenyekiti kila baada ya miezi mitatu. (2) Vikao vya kawaida vya Bodi vitaitishwa kwa taarifa ya maandishi ya siku saba itakayotolewa kwa wajumbe wote. - 8 Verify source ↗
(1) Bila kuathiri masharti ya aya ya 7 ya Jedwali hili, endapo
AI-assisted research summary: Mwenyekiti wa Bodi anaweza kuitisha kikao cha dharura ikiwa kuna suala lisiloweza kusubiri kikao cha kawaida. Pia, theluthi mbili ya wajumbe wa Bodi wanaweza kuitisha kikao kwa taarifa ya maandishi ya siku tatu ikiwa Mwenyekiti amekataa kuitisha kikao cha dharura na wajumbe hao wanaona suala haliwezi kusubiri kikao cha kawaida.
8.-(1) Bila kuathiri masharti ya aya ya 7 ya Jedwali hili, endapo litajitokeza suala ambalo haliwezi kusubiri kikao cha kawaida cha Bodi, Mwenyekiti anaweza kuitisha kikao cha dharura cha Bodi kwa ajili ya kujadili suala lililojitokeza. (2) Bila kuathiri masharti ya aya ndogo ya (1), theluthi mbili ya wajumbe wa Bodi inaweza kuitisha kikao cha Bodi kwa kutoa taarifa ya maandishi ya siku tatu kwa wajumbe wote endapo; (a) kwa maoni ya wajumbe hao kuna suala ambalo haliwezi kusubiri kikao cha kawaida cha Bodi; na (b) kuwa Mwenyekiti amekataa kuitisha kikao cha dharura baada ya kuombwa na wajumbe hao. Uendeshaji wa vikao vya Bodi - 9 Verify source ↗
Vikao vya Bodi vitaongozwa na Mwenyekiti na endapo
AI-assisted research summary: Vikao vya Bodi vinaongozwa na Mwenyekiti; ikiwa Mwenyekiti hawezi kuendesha kikao kwa sababu yoyote, wajumbe humchagua mjumbe mwingine kuwa mwenyekiti wa kikao hicho.
9. Vikao vya Bodi vitaongozwa na Mwenyekiti na endapo Mwenyekiti, kwa sababu yoyote ile, atashindwa kuendesha kikao, wajumbe watamchagua Mjumbe kutoka miongoni mwao kuwa mwenyekiti wa kikao husika. Akidi ya kikao - 10 Verify source ↗
(1) Akidi ya kikao cha kawaida cha Bodi itakuwa ni nusu ya
AI-assisted research summary: Board meetings need a quorum: half of all members for an ordinary meeting and two-thirds for an emergency meeting.
10.-(1) Akidi ya kikao cha kawaida cha Bodi itakuwa ni nusu ya wajumbe wote. (2) Akidi ya kikao cha dharura cha Bodi itakuwa ni theluthi mbili ya wajumbe wote. (3) Bila kuathiri aya ndogo ya (1), vikao vya Bodi vitahudhuriwa na: (a) Katibu Tawala wa Wilaya au mwakilishi wake; 12 Sheria Ndogo ya Uanzishwaji wa Bodi ya Mfuko wa Elimu ya Halmashauri ya Mji wa Newala Tangazo la Serikali Na.584 (Linaendelea.) (b) wajumbe wa Kamati ya Utendaji au wawakilishi wao; na (c) mtu yeyote ambaye kwa maoni ya Mwenyekiti ni muhimu akahudhuria kikao cha Bodi. (4) Mtu yeyote aliyetajwa katika aya ndogo ya (3) hatakuwa na haki ya kupiga au kupigiwa kura katika vikao vya Bodi. Uamuzi katika vikao - 11 Verify source ↗
Uamuzi wa suala lolote katika vikao vya Bodi utafanywa kwa
AI-assisted research summary: Maamuzi ya kikao cha Bodi hufanywa kwa kura; kila Mjumbe ana kura moja, na kura zikifungana Mwenyekiti au anayeongoza kikao hupata kura ya uamuzi.
11. Uamuzi wa suala lolote katika vikao vya Bodi utafanywa kwa kura na kila Mjumbe atakuwa na kura moja na endapo itatokea kura kufungana, Mwenyekiti au Mjumbe yeyote atakayekuwa anaongoza kikao atakuwa na kura ya uamuzi. Muhtasari na nyaraka za Bodi - 12 Verify source ↗
(1) Katibu wa Bodi atakuwa na wajibu wa kuandika muhtasari
AI-assisted research summary: Katibu wa Bodi lazima aandike muhtasari wa vikao na atunze kumbukumbu na nyaraka za Bodi; muhtasari huo uthibitishwe katika kikao kinachofuata na usainiwe na Mwenyekiti na Katibu.
12.-(1) Katibu wa Bodi atakuwa na wajibu wa kuandika muhtasari wa vikao vya Bodi na kutunza kumbukumbu za vikao na nyaraka nyingine za Bodi. (2) Muhtasari wa kikao cha Bodi utathibitishwa katika kikao kinachofuata cha Bodi na utasainiwa na Mwenyekiti na Katibu wa Bodi. (3) Nyaraka za Bodi zitakazotolewa kwa madhumuni yoyote zitasainiwa na Mwenyekiti au Katibu wa Bodi. 13 Sheria Ndogo ya Uanzishwaji wa Bodi ya Mfuko wa Elimu ya Halmashauri ya Mji wa Newala Tangazo la Serikali Na.584 (Linaendelea.) ________ JEDWALI LA PILI _______ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 17(b)) VIWANGO VYA MICHANGO KATIKA MFUKO WA ELIMU Namba Aina ya Chanzo Kiwango cha Mchango (Shilingi)
Part
JEDWALI LA PILI
- 6 Verify source ↗
Section 6
AI-assisted research summary: Sehemu hii inaweka michango/ada kwa aina mbalimbali za shughuli na biashara zilizoorodheshwa, zikiwemo baadhi ya shule, maduka, huduma na kampuni, ndani ya Halmashauri ya Mji wa Newala.
6. 7 8 9 10 11 12 13 14 15 Michango ya mazao kwa kilo moja korosho mahindi ufuta njugu mbaazi kunde choroko soya ulezi makopa karanga mtama Mazao mengine ambayo hayajatajwa Shule za sekondari na Msingi zisizo za Serikali (a) kutwa (b) bweni (c) kutwa na bweni Nyumba ya kulala wageni Mgahawa Maduka ya vifaa vya umeme Maduka ya vifaa ya ujenzi Maduka mengine ambayo hayajatajwa Supermarket au Mall Maduka ya vifaa au vyombo vya ndani Maduka ya vileo (grocery) Baa Biashara ya chakula, nyama, kuku na samaki choma. Hotel Gereji Fundi selemara Biashara ya kuosha vyombo vya usafiri Kampuni za ulinzi Kampuni za usafi 14 20/= 4/= 20/= 20/= 20/= 20/ 20/= 20/= 20/= 2/= 20/= 10/= 10/= 25,000/= 50,000/= 70,000/= 30,000/= 5,000/= 20,000/= 40,000/= 10,000/= 50,000/= 10,000/= 10,000/= 20,000/= 5,000/= 50,000/= 20,000/= 5,000/= 5,000/= 30,000/= 30,000/= Sheria Ndogo ya Uanzishwaji wa Bodi ya Mfuko wa Elimu ya Halmashauri ya Mji wa Newala Tangazo la Serikali Na.584 (Linaendelea.) 16 17 18 19 20 21 22 23 24 25 26 27 28 29 30 31 32 33 34 35 36 37 38 39 40 41 42 43 44 45 46 47 48 49 50 51 52 53 54 55 Nyumba ya starehe (club au ukumbi ya muziki au kumbi za mikutano) Duka la samaki Duka la nyama (butcher) Salon ya kike au kiume Maduka makubwa ya madawa Maduka ya dawa baridi Maduka ya dawa ya jumla (whole sellers) ya binadamu na wanyama Kituo cha mafuta Maabara Hospitali au kituo cha afya cha binafsi Huduma za stationery au internet Maduka ya simu za mkononi Maduka ya fedha mtandao Maduka ya Televisheni, DVD, VCD, Redio na vifaa vya muziki Mashine za kusaga na kukoboa nafaka. Maghala ya kuhifadhia korosho Makampuni ya kununua korosho Biashara ya kuuza mbao Maduka ya dawa asili Viwanda (factory and heavy industries) Viwanda vidogo vidogo Viwanda vya kubangua korosho Maduka ya nguo Maduka ya kuuza vyombo au vifaa vya usafiri (pikipiki na baiskeli) Maduka ya kuuza vipuli vya pikipiki na baiskeli Kampuni za kuuza vyombo vingine vya usafiri Maduka ya kuuza vitabu na majalada mbalimbali (bookshops) Wauza mitumba (nguo na viatu) Wauza vipuli vya magari (spea) Wauza vifaa vya bomba Taasisi za kifedha Watumishi wa serikali na sekta binafsi wenye ajira za kudumu na wanaofanya kazi katika eneo la Halmashauri Vilabu vya pombe za kienyeji Maduka ya miwani Wauza vinyago Wazabuni na makandarasi (a) Wakandarasi (b) Wazabuni (c) Local fundi Wauza pembejeo, vifaa vya kilimo na mifugo Watu wanaoonyesha michezo, video na maigizo Mashamba ya biashara Wataalamu washauri/ washauri elekezi 15 20,000/= 10,000/= 10,000/= 10,000/= 30,000/= 10,000/= 50,000/= 50,000/= 50,000/= 50,000/= 10,000/= 30,000/= 30,000/= 30,000/= 10,000/= 200,000/= 100,000/= 50,000/= 5,000/= 100,000/= 50,000/= 20,000/= 20,000/= 50,000/= 10,000/= 30,000/= 10,000/= 5,000/= 20,000/= 10,000/= 200,000/= 2,000/= 5,000/= 10,000/= 10,000/= 100,000/= 50,000/= 30,000/= 30,000/= 10,000/= 50,000/= 50,000/= Sheria Ndogo ya Uanzishwaji wa Bodi ya Mfuko wa Elimu ya Halmashauri ya Mji wa Newala Tangazo la Serikali Na.584 (Linaendelea.) 56 57 58 59 60 61 62 63 64 65 Vituo vya kuuza gesi ya kupikia Vituo vya kuuza umeme (LUKU) Maduka ya kuuza simenti Mawakala wa vinywaji Maduka ya vipodozi Biashara ya fenicha Biashara ya majiko ya mkaa au kuni Biashara ya mazuria Vikundi vya wajasiriamali Biashara yoyote ndogo ambayo haijatajwa 10,000/= 30,000/= 20,000/= 30,000/= 20,000/= 10,000/= 5,000/= 10,000/= 20,000/= 5,000/= 16 Sheria Ndogo ya Uanzishwaji wa Bodi ya Mfuko wa Elimu ya Halmashauri ya Mji wa Newala Tangazo la Serikali Na.584 (Linaendelea.) __________ JEDWALI LA TATU ___________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 26) FOMU YA KUKIRI NA KUFIFILISHA KOSA Mimi ……………………………………………………..………. nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya ………………………………. ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Newala, kwamba mnamo tarehe ………… ya mwezi………….. Mwaka ……… nilitenda kosa la kukiuka masharti ya kanuni ya ……………ya Sheria Ndogo ya Uanzishwaji wa Mfuko wa Elimu ya Halmashauri ya Mji wa Newala ya Mwaka, 2024. Kwa Mamlaka aliyopewa Mkurugenzi wa Halmashauri, Niko tayari kulipa kiasi cha mchango au mali au rasilimali ninayodaiwa pamoja na faini. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA MIMI MWENYEWE KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU. Leo tarehe …………………..ya Mwezi …………… Mwaka ………………… Jina: …………………………………………. Saini: ……………………………................... MBELE YA: Jina: ………………………………… Wadhifa: …………………………… Saini: ……………………………….. Tarehe: ……………………………… 17 Sheria Ndogo ya Uanzishwaji wa Bodi ya Mfuko wa Elimu ya Halmashauri ya Mji wa Newala Tangazo la Serikali Na.584 (Linaendelea.) Lakiri ya Halmashauri ya Mji Newala imegongwa kwenye Sheria Ndogo hii kufuatia azimio lililopitishwa katika Mkutano wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Mji Newala uliuofanyika tarehe 27/1/2024 na kushuhudiwa Lakiri hiyo ikigongwa mbele ya:- GEOFREY MOSES NNAUYE, Mkurugenzi, Halmashauri ya Mji NEWALA YUSUPH HALFANI KATEULE Mwenyekiti, Halmashauri ya Mji, NEWALA L.S NAKUBALI, Dodoma, MOHAMED OMARY MCHENGERWA, 30 Mei, 2024 Waziri wa Nchi OR-TAMISEMI 18
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
SHERIA NDOGO YA UANZISHWAJI WA BODI YA MFUKO WA ELIMU YA HALMASHAURI YA MJI WA NEWALA YA MWAKA 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in