AI-assisted research summary: Mwombaji anapewa kibali cha kujenga kituo cha mafuta, lakini lazima atimize masharti yote yaliyoorodheshwa.
3. Mwombaji anapewa kibali cha ujenzi kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha mafuta katika Kiwanja Na. 1, Kitalu “M”, eneo la Lugoba, Wilaya ya Chalinze, Mkoa wa Pwani, kwa masharti yafuatayo: (a) kituo cha mafuta kitajengwa kwa mujibu wa viwango vya Shirika la Viwango Tanzania Na. TZS 1115:2009 na TZS 1079:2008; (b) uangalifu wa kutosha utazingatiwa wakati wa uchimbaji na uwekaji wa matenki ya mafuta chini ya ardhi; (c) mpangilio wa kituo cha mafuta utakidhi 1 Notisi ya Kibali cha Ujenzi wa Kituo cha Mafuta kwa Ngamila Tanzania Limited Tangazo la Serikali Na.650 (Linaendelea.) umbali wa kiusalama kwa mujibu wa viwango vya Shirika la Viwango Tanzania Na. TZS 1079:2008; (d) ufukiaji wa matenki ya kuhifadhi mafuta pamoja na mabomba chini ya ardhi ufanyike kwa namna ambayo italinda usalama wa vifaa hivyo ikiwemo kuzuia kutu; (e) matenki ya kuhifadhia mafuta, pampu na mabomba husika pamoja na vifaa vyote vinavyounganishwa pamoja navyo vitafungwa vizuri ili kuzuia uvujaji wa mafuta; (f) matenki ya kuhifadhia mafuta na pampu za mafuta zitafanyiwa uhakiki wa usahihi wa vipimo na Wakala wa Vipimo Tanzania aliyeanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Vipimo; Sura ya 340 (g) eneo la mbele la kituo cha mafuta na kuzunguka eneo la pampu litasakafiwa kwa zege madhubuti isiyoweza kupenyeza mafuta na kuhakikisha kuwepo kwa mitaro ambayo itakusanya maji na mafuta wakati wa mvua na kuyaelekeza kwenye chemba ya kutenganisha maji na mafuta; (h) kuweka swichi ya dharura katika eneo linaloonekana na kufikika kirahisi ili iwe rahisi wakati wa dharura kuzima umeme wa kituo kizima; (i) kuhakikisha uwepo wa vyoo vya kutosha vya wanawake na wanaume vilivyo safi wakati wote; (j) kuhakikisha usalama zinawekwa sehemu ya kuingia na kutoka kwenye kituo cha mafuta na eneo la pampu zikijumuisha “zima injini”, “zima simu” na “usivute sigara”; alama kuwa za (k) kuhakikisha kila tenki la kuhifadhia mafuta linaunganishwa na bomba la kupumulia lenye urefu usiopungua mita 3.6 kutoka ardhini, bomba hilo linatakiwa kuwa angalau mita 1.5 kutoka kwenye mpaka wa kiwanja na angalau mita 4 kutoka kwenye dirisha au kifaa 2 Notisi ya Kibali cha Ujenzi wa Kituo cha Mafuta kwa Ngamila Tanzania Limited Tangazo la Serikali Na.650 (Linaendelea.) chochote cha kuvuta hewa ikiwemo kiyoyozi; (l) pampu za mafuta na sehemu ya kushushia mafuta zinatakiwa kuwa angalau mita 4.5 kutoka kwenye mpaka wa kiwanja, angalau mita 8 kutoka katika kifaa chochote ambacho kinaweza kuwa chanzo cha moto ikiwemo jokofu na angalau mita 10 kutoka kwenye nyaya za kusafirishia umeme; (m) kuhakikisha kila pampu ya mafuta inalindwa na kizuizi na kitakuwa na urefu wa mita 1 kutoka juu ya ardhi; (n) mifumo ya upakuaji wa mafuta katika kituo cha mafuta itajengwa kwa kufuata kanuni na taratibu zinazokubalika katika sekta ya mafuta; (o) kuhakikisha kuwa kituo cha mafuta kinakuwa na paa linalofunika eneo lote lenye pampu za mafuta na linajengwa kwa mujibu wa viwango na taratibu zinazokubalika katika sekta ya mafuta; na (p) kuhakikisha kuwa kituo cha mafuta kinakuwa na bango la bei ambalo litawekwa sehemu ambayo linaonekana kirahisi ili wateja waweze kuona bei za mafuta kabla ya kuingia kituoni. Ukomo wa kibali cha ujenzi