SHERIA NDOGO YA (UDHIBITI NA USIMAMIZI WA MIFUGO) YA HALMASHAURI YA WILAYA YA NACHINGWEA YA MWAKA 2024
Sheria ndogo hizi zinaweka masharti ya kufuga, kusafirisha, kuuza, kukagua na kuchinja mifugo katika eneo la Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- SHERIA NDOGO YA (UDHIBITI NA USIMAMIZI WA MIFUGO) YA HALMASHAURI YA WILAYA YA NACHINGWEA YA MWAKA 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This page preserves the statute’s identified version, provision structure, official source link, and stored legal text for reading and research.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of SHERIA NDOGO YA (UDHIBITI NA USIMAMIZI WA MIFUGO) YA HALMASHAURI YA WILAYA YA NACHINGWEA YA MWAKA 2024
Showing 1 of 1
- document Verify source ↗
Document text
AI-assisted research summary: Sheria ndogo hizi zinaweka masharti ya kufuga, kusafirisha, kuuza, kukagua na kuchinja mifugo katika eneo la Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea.
Sheria Ndogo ya (Udhibiti Na Usimamizi wa Mifugo) ya Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea Tangazo la Serikali Na.664 (Linaendelea.) TANGAZO LA SERIKALI Na. 664 la tarehe. 2/8/2024 SHERIA YA SERIKALI ZA MITAA (MAMLAKA ZA WILAYA), (SURA YA 287) ________ SHERIA NDOGO ________ (Imetengenezwa chini ya kifungu cha 153) SHERIA NDOGO YA (UDHIBITI NA USIMAMIZI WA MIFUGO) YA HALMASHAURI YA WILAYA YA NACHINGWEA YA MWAKA 2024 Kanuni Jina MPANGILIO WA KANUNI 1. Jina. 2. Matumizi. 3. Tafsiri. 4. Wajibu wa Halmashauri. 5. Wajibu wa mfugaji. 6. Kibali cha kufuga Mifugo. 7. Masharti ya Mfugaji. 8. Kibali cha kusafirisha mifugo. 9. Taratibu za ufugaji. 10. Kudhibiti mifugo inayozurura ovyo. 11. Ukaguzi wa mifugo na bidhaa za mifugo. 12. Taratibu za biashara ya mifugo na mazao yake. 13. Operesheni maalum ya ukaguzi wa mifugo. 14. Udhibiti wa ujichaji wa mifugo. 15. Makosa. 16. Adhabu. 17. Kufifilisha kosa. 1 Sheria Ndogo ya (Udhibiti Na Usimamizi wa Mifugo) ya Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea Tangazo la Serikali Na.664 (Linaendelea.) SHERIA YA SERIKALI ZA MITAA (MAMLAKA ZA WILAYA), (SURA YA 287) ________ SHERIA NDOGO __________ (Imetengenezwa chini ya kifungu cha 153) SHERIA NDOGO YA UDHIBITI NA USIMAMIZI WA MIFUGO YA HALMASHAURI YA WILAYA YA NACHINGWEA YA MWAKA 2024 Jina 1. Sheria Ndogo hizi itajulikana kama Sheria Ndogo ya Udhibiti na Usimamizi wa Mifugo ya Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea ya Mwaka 2024. Matumizi 2. Sheria Ndogo hizi itatumika eneo lote la Mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea. Tafsiri 3. Katika Sheria Ndogo hizi isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo: “afisa mwidhiniwa” maana yake ni Afisa yeyote aliyeteuliwa na Mkurugenzi kwa lengo la kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hizi; “afya” maana yake ni hali timilifu ya kimwili na kiakili ya wanyama wanaofugwa na binadamu; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea; “kibali” maana yake ni idhini ya maandishi inayotolewa na shughuli Halmashauri kwa ajili ya kufanya iliyokusudiwa chini ya Sheria Ndogo hizi; “mazao ya mifugo” maana yake ni nyama, ngozi, pembe, mbolea, kwato, mifupa, maziwa na kila zao litakalo idhinishwa na mamlaka husika kuwa zao la mifugo; “mifugo” maana yake ni ng’ombe, mbuzi, kondoo, kuku, punda, nguruwe, ngamia, farasi, sungura, mbwa na wanyama wengine wafugwao; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi wa Halmashauri 2 Sheria Ndogo ya (Udhibiti Na Usimamizi wa Mifugo) ya Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea Tangazo la Serikali Na.664 (Linaendelea.) ya Wilaya ya Nachingwea au afisa yeyote aliyeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi; “operesheni” maana yake ni mpango maalum uliondaliwa unaohusisha maafisa wa na Halmashauri Halmashauri, wataalam mbalimbali na wadau kutoka vyombo vya usalama kwa ajili ya ukaguzi, ukamataji na uzuiaji wa makosa yatokanayo na migogoro ya ufugaji usiozingatia masharti ya Sheria Ndogo hizi. Wajibu wa Halmashauri 4. Itakuwa ni wajibu wa Halmashauri kuhakikisha kwamba: (a) inaandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi; (b) inaelekeza idadi ya mifugo ambayo kila mfugaji anaruhusiwa kufuga kulingana na ukubwa wa eneo lake; (c) inajenga majosho ya mifugo kwa kushirikiana na wananchi; (d) inatoa elimu ya ufugaji bora kwa jamii ili wafugaji waweze kuvuna mifugo yao kwa kuuza wanyama hai au kwa kuchinja na kuuza nyama yenye tija; (e) inafanya sensa ya mifugo, kuweka alama na kutoa kadi za mifugo; (f) inatoa huduma za chanjo za mifugo kwa kushirikiana na wafugaji; (g) inadhibiti uzururaji holela wa mifugo katika Halmashauri kwa mujibu wa Sheria; (h) inatenga njia maalumu kwa ajili ya kupitisha mifugo; na (i) kubaini mifugo iliyoingizwa bila kufuata utaratibu ulioidhinishwa na Halmashauri. Wajibu wa mfugaji 5. Kila mfugaji atahakikisha kuwa: (a) anaogesha mifugo yake kama atakavyoelekezwa na Halmashauri; (b) mifugo yake inawekwa alama maalumu zinazotolewa na mamlaka husika; (c) anahudhuria mafunzo ya ufugaji kama atakavyo hitajika na Halmashauri; 3 Sheria Ndogo ya (Udhibiti Na Usimamizi wa Mifugo) ya Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea Tangazo la Serikali Na.664 (Linaendelea.) (d) anafuga mifugo yake katika eneo lililoidhinishwa na Halmashauri; (e) anakuwa na kadi ya mifugo itakayo onesha idadi na aina ya mifugo aliyonayo; (f) anaipatia mifugo yake chakula na maji ya kutosha kwa kuzingatia kanuni bora za ufugaji; (g) ana kibali cha kusafirisha mifugo na mazao yake; (h) anafuga kwa kuzingatia mipango ya matumizi bora ya ardhi; (i) anapeleka mifugo yake katika vituo vya chanjo kama itakavyoamriwa na Halmashauri; (j) anauza mifugo yake katika masoko na minada iliyoidhinishwa au eneo lingine kwa taarifa maalum; na (k) anapitisha mifugo yake kwenye njia maalum zilizowekwa wakati wa kwenda na kutoka malishoni, mnadani au sehemu nyinginezo. Kibali cha kufuga Mifugo 6.-(1) Mtu yeyote atakayetaka kufuga mifugo atalazimika kupata kibali cha kufuga kutoka kwa Halmashauri kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Kwanza la Sheria Ndogo hizi. (2) Kibali kilichotajwa katika aya ndogo ya (1) hakitakuwa na gharama na kitakua cha miezi kumi na mbili kuanzia tarehe kilipotolewa. (3) Bila kuathiri masharti ya aya ndogo ya (1) na (2) mtu yeyote atakayekiuka taratibu za ufugaji kulingana na Sheria Ndogo hizi kibali chake kitafutwa na atatakiwa kuhamisha mifugo yake yote. Masharti ya Mfugaji 7.- Mfugaji yeyote hataruhusiwa: (a) kuchunga, kulisha au kunywesha mifugo katika maeneo ambayo hayakutengwa kwa shughuli hiyo; (b) kusafirisha mifugo kwa kuiswaga barabarani; (c) kusafirisha au kuhamisha mifugo kutoka eneo kutoka lingine kibali hadi bila moja Halmashauri; (d) kuingiza mifugo katika eneo la Halmashauri bila 4 Sheria Ndogo ya (Udhibiti Na Usimamizi wa Mifugo) ya Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea Tangazo la Serikali Na.664 (Linaendelea.) kibali; cha Kibali kusafirisha mifugo (e) kuuza, kununua au kufanya biashara ya kubadilishana mifugo katika maeneo ambayo siyo mnada, masoko au magulio ya mifugo yaliyoaidhinishwa na Halmashauri; (f) kufuga mifugo zaidi ya idadi iliyoainishwa katika Sheria Ndogo hizi; na 8.-(1) Mtu yeyote ambaye anataka kusafirisha mfugo au mifugo, kutoka au kuingia katika eneo la Halmashauri, atatakiwa kuwa na kibali maalumu kilichoainishwa katika Jedwali la Pili la Sheria Ndogo hizi. (2) Kabla Halmashauri haijatoa kibali cha kusafirisha mifugo itavingatia vifuatavyo: (a) mfugaji kutoa uthibitisho wa kumiliki mfugo au mifugo kutoka kwa Afisa Mwidhiniwa; na (b) kukagua kibali cha kusafirisha mfugo au mifugo. (3) Afisa Mwidhiniwa atakuwa na uwezo wa kukamata na kumtoza faini mtu yeyote ambaye atasafirisha mifugo kinyume na Sheria Ndogo hizi. Taratibu za ufugaji 9. Mfugaji yeyote atatakiwa kuzingatia masharti ya kufuga kama yalivyoainishwa katika Sheria Ndogo hizi. Kudhibiti mifugo inayozurura ovyo 10.-(1) Halmashauri itakamata mfugo au mifugo yoyote itakayoonekana inazurura hovyo katika eneo la Halmashauri. (2) Mfugo wowote utakaokamatwa chini ya kanuni ndogo ya (1) utalipiwa faini ya shilingi elfu thelathini kwa muda usiozidi siku saba (7). (3) Endapo mfugo uliokamatwa hautachukuliwa na mmiliki ndani ya kipindi cha siku saba tangu kukamatwa, Halmashauri itakuwa na haki ya kuuza kwa mnada mfugo huo baada ya kupata idhini ya Mahakama, na fedha zitakazopatikana zitarejeshwa kwa mmliki wa mfugo huo baada ya kutoa faini inayodaiwa, gharama za kuhifadhi mfugo, gharama ya Mahakama na gharama ya mnada. (4) Bila kuathiri masharti yaliyowekwa katika kanuni ndogo ya 3, kabla ya kuuza mfugo uliokamatwa kwa mnada Halmashauri itatoa taarifa ya siku saba kwa mmiliki 5 Sheria Ndogo ya (Udhibiti Na Usimamizi wa Mifugo) ya Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea Tangazo la Serikali Na.664 (Linaendelea.) na umma juu ya kusudio hilo. Ukaguzi wa na mifugo za bidhaa mifugo (5) Endapo kutatokea kufa kwa mifugo au mfugo uliokamatwa, Halmashauri haitawajibika na ulipaji wa gharama zozote isipokuwa kama vifo hivyo vitakuwa vimesababishwa na uzembe wa watumishi wa Halmashauri. 11.-(1) Afisa Mwidhiniwa atakuwa na uwezo wa kukataa mfugo wowote au bidhaa za mifugo kuingia au kuuzwa ndani ya eneo la Halmashauri, iwapo mifugo hiyo au bidhaa hizo zinaweza kuhatarisha afya au usalama wa mifugo mingine au watumiaji. (2) Afisa Mwidhiniwa anaweza kuingia katika nyumba au jengo lolote kuanzia saa moja na nusu asubuhi hadi saa tisa na nusu alasiri kwa lengo la utekelezaji wa Sheria Ndogo hizi. (3) Bila kuathiri masharti ya aya ndogo ya 2, Afisa Mwidhiniwa anaweza kuingia katika eneo lolote au jengo lolote kwa muda wowote baada ya kupata kibali cha maandishi kutoka kwa Mkurugenzi. Taratibu za biashara ya mifugo na mazao yake 12.-(1) Mfanyabiashara kabla ya kuanza biashara ya mifugo na mazao ya mifugo atatakiwa kuwasilisha katika Halmashauri kwa ajili ya uhakiki vitu vifuatavyo: (a) leseni ya biashara ya mifugo au mazao ya mifugo; (b) barua ya utambulisho kutoka serikali ya kijiji au Mtaa anaoishi; na (c) vibali kutoka Mamlaka husika vinavyohusu kuuza na kununua mifugo na mazao ya mifugo (2) Mfanyabiashara wa mifugo inayopelekwa au kutoka mnadani atatakiwa kuwa na barua ya utambaulisho kutoka serikali ya Kijiji au Mtaa. (3) Mfanyabiashara atakayesafirisha mifugo kutoka nje ya Halmashauri atatakiwa kuwa na kibali kutoka Halmashauri ambayo mifugo hiyo inatoka. (4) Mfanyabiashara wa mifugo atatakiwa kusafirisha mifugo katika vyombo vya usafiri vinavyokubalika kwa mujibu wa Sheria. (5) Mfanyabiashara wa mifugo atauza au kununua mifugo katika minada na masoko yanayotambulika kwa 6 Sheria Ndogo ya (Udhibiti Na Usimamizi wa Mifugo) ya Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea Tangazo la Serikali Na.664 (Linaendelea.) mjibu wa Sheria. (6) Mifugo itakayokamatwa ikisafirishwa bila kibali au kuuzwa eneo ambalo halijaidhinishwa kwa ajili ya shughuli hiyo, mhusika atalazimika kulipa faini ya Shilingi elfu kumi kwa kila mfugo. Operesheni maalum ya ukaguzi wa mifugo Udhibiti wa ujichaji wa mifugo Makosa 13. Kutakuwa maalum na itakayoandaliwa na Halmashauri kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama kwa ajili ya kufanya ufatiliaji na ukaguzi wa mifugo inayofungwa bila ya kuzingatia matakwa ya Sheria Ndogo hizi. operesheni 14. Mifugo yote itachinjwa katika maeneo yaliyotengwa na kuidhinishwa na Halmashauri. 15. Mfugaji yeyote, bila sababu ya msingi, atakuwa ametenda kosa iwapo: (a) atashindwa au kukataa kuogesha au kuchanja mfugo au mifugo yake; (b) atalisha/kunywesha mfugo au mifugo kwenye maeneo yasiyoruhusiwa; (c) hatokuwa na kibali cha ufugaji; (d) atashindwa au atazembea kutoa taarifa juu ya uwepo wa ugonjwa au kifo cha ghafla cha mfugo au mifugo katika banda lake; (e) ataruhusu mfugo au mifugo yake kuzurura hovyo; (f) atashindwa kutoa ushirikiano wa uwekaji wa alama kwa mfugo au mifugo yake; (g) atamzuia Afisa Mwidhiniwa kutekeleza majukumu yake; (h) atasafirisha mfugo/mifugo au mazao yake bila kibali; (i) ataingiza mifugo katika eneo la Halmashauri bila kibali; (j) atachinja mfugo katika eneo lisiloruhusiwa. Adhabu 16. Mtu yeyote atakayekwenda kinyume na masharti ya Sheria Ndogo hizi atakuwa ametenda kosa na akipatikana na hatia atatozwa faini ya kiasi kisichozidi shilingi laki tatu 7 Sheria Ndogo ya (Udhibiti Na Usimamizi wa Mifugo) ya Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea Tangazo la Serikali Na.664 (Linaendelea.) au kifungo kisichozidi miezi kumi na mbili jela au adhabu zote kwa pamoja. Kufifilisha kosa 17. Mkurugenzi anaweza kumtoza faini mtu yeyote aliyetenda kosa chini ya Sheria Ndogo hizi, kiasi cha shilingi elfu hamsini iwapo mkosaji atakiri kosa na kuwa tayari kujaza fomu maalumu iliyoambatanishwa kwenye Jedwali la Tatu la Sheria Ndogo hizi. 8 Sheria Ndogo ya (Udhibiti Na Usimamizi wa Mifugo) ya Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea Tangazo la Serikali Na.664 (Linaendelea.) _________ JEDWALI LA KWANZA ________ (Limetengenezwa chini ya Kanuni ya 6 (1)) KIBALI CHA KUFUGA MIFUGO Jina:………………………………………………………………………… Anwani:…………………………………………………………………… Kata:……………………………………………………………………… Mtaa:……………………………………………………………………… Ameruhusiwa kufuga wanyama wafuatao katika eneo la………………….. Na Aina ya mnyama Idadi 1 Ng’ombe 2 Mbuzi 3 4 5 6 8 9 Kondoo Nguruwe Ngamia Punda Farasi Sungura 10 Mbwa 11 Kuku /Bata 12 Wanyama wengine (wataje) Kibali hiki kitakuwa kwa muda wa miezi kumi na mbili (12) kuanzia tarehe……… hadi tarehe………….. Kimetolewa na : Jina la Afisa aliyeidhiniwa :………………………………………. Cheo:................................................................................................ Sahihi................................................................................................ 9 Sheria Ndogo ya (Udhibiti Na Usimamizi wa Mifugo) ya Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea Tangazo la Serikali Na.664 (Linaendelea.) Tarehe :…………………………………........................................ Muhuri ____________ JEDWALI LA PILI ____________ (Limetengenezwa chini ya Kanuni ya 8 (1)) KIBALI CHA KUSAFIRISHA MIFUGO Jina:…………………………………………….......... Anuani:…………………………………………......... Namba ya Simu:........................................................... Ameruhusiwa kusafirisha Mifugo ifuatayo kutoka ……........…………kupitia njia za……….......hadi…………..….. Namba 1. 2. 3. 4. 5. 6. 8. 9. 10. 11. 12. Aina ya Mfugo Idadi ya Mifugo Ng’ombe Mbuzi Kondoo Nguruwe Ngamia Punda Farasi Sungura Mbwa Kuku au Bata Mifugo wengine Kibali hiki kitakuwa cha muda wa siku…......... kuanzia tarehe…........hadi tarehe………. Kimetolewa na : Jina la Afisa Mwidhiniwa:……………………………………….... Wadhifa:…………………………………………………………… Saini:……………………………………………………………..... Tarehe:…………………………………………………………....... Muhuri:………………………………………................................. 10 Sheria Ndogo ya (Udhibiti Na Usimamizi wa Mifugo) ya Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea Tangazo la Serikali Na.664 (Linaendelea.) ____________ JEDWALI LA TATU ____________ (Limetengenezwa chini ya Kanuni ya 17) FOMU YA KUFIFILISHA KOSA Mimi ……………………………………………………… nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya …………………………………………. ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea, kwamba mnamo tarehe …… ya Mwezi ………. Mwaka ……….…… nilitenda kosa la kukiuka masharti ya Kanuni …… ya Sheria Ndogo ya (Udhibiti na Usimamizi wa Mifugo) ya Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea ya Mwaka 2024. Kwa Mamlaka aliyopewa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea, niko tayari kulipa kiasi cha faini ninayodaiwa. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA MIMI MWENYEWE KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU Leo tarehe…………. ya Mwezi…………..… Mwaka ……………. Jina……………………………….. Saini……………………… MBELE YANGU: Jina:……………………………………..…………………… Saini………………………….…………………………..……… Wadhifa:………………………………………………………… Tarehe………………………………………………………….. 11 Sheria Ndogo ya (Udhibiti Na Usimamizi wa Mifugo) ya Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea Tangazo la Serikali Na.664 (Linaendelea.) Lakiri ya Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea imegongwa kwenye Sheria Ndogo hii kufuatia Azimio lililopitishwa katika Mkutano Mkuu wa Baraza la madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea uliofanyika tarehe 27/1/2023 na kushuhudiwa Lakiri hiyo ikigongwa mbele ya:- MHANDISI CHIONDA M. KAWAWA, Mkurugenzi Halmashauri ya Wilaya, Nachingwea Adinani A. Mpyagila, Mwenyekiti, Halmashauri ya Wilaya, Nachingwea L.S NAKUBALI, Dodoma, 20 Juni, 2024 MOHAMED OMARY MCHENGERWA (MB.), Waziri wa Nchi-OR-TAMISEMI 12
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
SHERIA NDOGO YA (UDHIBITI NA USIMAMIZI WA MIFUGO) YA HALMASHAURI YA WILAYA YA NACHINGWEA YA MWAKA 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in