SHERIA NDOGO YA USHURU WA HUDUMA YA HALMASHAURI YA WILAYA YA KAKONKO YA MWAKA 2024
This section says these bylaws are to be called the Kakonko District Council Service Levy Bylaws, 2024.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- SHERIA NDOGO YA USHURU WA HUDUMA YA HALMASHAURI YA WILAYA YA KAKONKO YA MWAKA 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This section says these bylaws are to be called the Kakonko District Council Service Levy Bylaws, 2024. These by-laws apply within the jurisdiction of Kakonko District Council. Sehemu hii inaweka maana ya maneno yaliyotumika kwenye Sheria Ndogo hizi. Halmashauri must charge and collect service tax from covered business-licence holders, at 0.3% of sales after VAT and excise for those who submit sales accounts to Tanzania Revenue Authority, and at the First Schedule rate for traders who do not submit sales accounts. Mlipa ushuru wa huduma lazima alipe ushuru, aweke kumbukumbu, awasilishe taarifa na hesabu sahihi, na aonyeshe nyaraka kwa ukaguzi.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of SHERIA NDOGO YA USHURU WA HUDUMA YA HALMASHAURI YA WILAYA YA KAKONKO YA MWAKA 2024
Showing 15 of 15
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hizi zitajulikana kama Sheria
AI-assisted research summary: This section says these bylaws are to be called the Kakonko District Council Service Levy Bylaws, 2024.
1. Sheria Ndogo hizi zitajulikana kama Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko ya Mwaka 2024. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hizi zitatumika katika eneo la
AI-assisted research summary: These by-laws apply within the jurisdiction of Kakonko District Council.
2. Sheria Ndogo hizi zitatumika katika eneo la mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hizi isipokuwa kama
AI-assisted research summary: Sehemu hii inaweka maana ya maneno yaliyotumika kwenye Sheria Ndogo hizi.
3. Katika Sheria Ndogo hizi isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “afisa mwidhiniwa” maana yake ni afisa yeyote la aliyeteuliwa na Mkurugenzi kwa kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hizi; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya lengo Kakonko; “hesabu za mwisho” maana yake ni hesabu za mwisho zinazowasilishwa na taasisi au kampuni yoyote ya kibiashara baada ya kipindi cha hesabu pamoja na nyaraka au maelezo yatakayotakiwa kutolewa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii; Sura ya 212 “kampuni” maana yake ni kampuni iliyosajiliwa kwa mujibu wa Sheria ya Kampuni; “kipindi maalum cha hesabu” maana yake ni muda ambao mfanyabiashara anatakiwa kuwasilisha hesabu za biashara kwa Halmashauri; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko au afisa yeyote aliyeteuliwa kutekeleza majukumu ya 1 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko Tangazo la Serikali Na.665 (Linaendelea.) Mkurugenzi chini ya Sheria Ndogo hizi; “mlipa ushuru wa huduma” maana yake ni kampuni, tawi la kampuni au mfanyabiashara mwenye leseni anayefanya la Halmashauri; zake katika shughuli eneo Sura ya 212 Ushuru wa huduma “tawi la kampuni” maana yake ni tawi la kampuni iliyosajiliwa kwa mujibu wa Sheria ya Kampuni; “ushuru wa huduma” maana yake ni ushuru unaotozwa na kukusanywa na Halmashauri kutoka kwa kampuni, la kampuni au mfanyabiashara yeyote tawi mwenye inayotolewa kwa mujibu wa sheria ambaye kutokana na huduma anazopata na kutumia miundombinu ya umma inayomuwezesha kufanya biashara katika eneo la Halmashauri; leseni ya biashara “wakala” maana yake ni mtu binafsi au kikundi cha watu, kampuni, taasisi au shirika ambalo limeteuliwa na Halmashauri kufanya kazi yoyote chini ya Sheria Ndogo hizi kwa niaba ya Halmashauri husika - 4 Verify source ↗
(1) Halmashauri itatoza na kukusanya ushuru
AI-assisted research summary: Halmashauri must charge and collect service tax from covered business-licence holders, at 0.3% of sales after VAT and excise for those who submit sales accounts to Tanzania Revenue Authority, and at the First Schedule rate for traders who do not submit sales accounts.
4.-(1) Halmashauri itatoza na kukusanya ushuru wa huduma kwa kiasi cha asilimia sifuri nukta tatu ya mauzo baada ya kutoa Kodi ya Ongezeko la Thamani na ushuru wa bidhaa kutoka kwa mtu yeyote mwenye leseni ya biashara anayewasilisha hesabu za mauzo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania. (2) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (1), Halmashauri itatoza na kukusanya ushuru wa huduma kwa kiwango kilichoainishwa katika Jedwali la Kwanza la Sheria Ndogo hizi kutoka kwa wafanyabiashara wenye leseni za biashara ambao hawawasilishi hesabu za mauzo Mamlaka ya Mapato Tanzania. Wajibu wa mlipa ushuru wa huduma - 5 Verify source ↗
(1) Mlipa ushuru wa huduma atawajibika
AI-assisted research summary: Mlipa ushuru wa huduma lazima alipe ushuru, aweke kumbukumbu, awasilishe taarifa na hesabu sahihi, na aonyeshe nyaraka kwa ukaguzi.
5.-(1) Mlipa ushuru wa huduma atawajibika kutekeleza yafuatayo: (a) kulipa ushuru wa huduma kwa kiwango kilichoainishwa katika Sheria Ndogo hizi; (b) kuwasilisha taarifa sahihi za mauzo ya kila 2 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko Tangazo la Serikali Na.665 (Linaendelea.) mwezi iwapo anawasilisha taarifa za hesabu za mauzo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania; (c) kuwasilisha hesabu za mwisho sahihi na za kweli; (d) kuwasilisha nyaraka au taarifa inayotakiwa kuwasilishwa kwa Halmashauri katika muda uliowekwa; (e) kutunza kumbukumbu za kitabu cha hesabu; na (f) kuonesha kumbukumbu yoyote au nyaraka kwa ajili ya ukaguzi. (2) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (2), Halmashauri inaweza kukubaliana na mlipa ushuru wa huduma utaratibu wa kulipa ushuru huo. (3) Mlipa ushuru wa huduma atawasilisha kwa Halmashauri hesabu za mwisho katika kipindi cha miezi mitatu tangu kumalizika kwa kipindi cha hesabu. (4) Endapo mlipa ushuru wa huduma hajawasilisha hesabu za mwisho kwa mwaka wa fedha husika na ametakiwa kufanya hivyo kwa notisi ya siku thelathini, Mkurugenzi anaweza kwa kadri atakavyoona inafaa, kuamua kiwango cha hesabu za mlipa ushuru wa huduma huyo kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizi. (5) Ushuru wa huduma uliothaminiwa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizi, utalipwa katika kipindi cha siku thelathini tangu tarehe ya kufanya tathmini. (6) Endapo mlipa ushuru wa huduma hajawasilisha majumuisho ya hesabu zake kwa mwaka wowote wa mapato, na iwapo Mkurugenzi au afisa mwidhiniwa anafikiri kwamba mlipa ushuru wa huduma ana wajibu wa kulipa ushuru kwa mwaka huo, anaweza kwa kadri atakavyoona, kuamua kiwango cha hesabu za mlipa ushuru huyo, isipokuwa tathmini hiyo haitaathiri wajibu wowote wa mlipa ushuru wa huduma anayostahili kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizi, kwa kushindwa kwake kuwasilisha hesabu hizo. Mamlaka ya Mkurugenzi - 6 Verify source ↗
(1) Endapo mlipa ushuru wa huduma anatakiwa
AI-assisted research summary: Mlipa ushuru wa huduma anaweza kutakiwa kuwasilisha taarifa za mauzo, hesabu, na kumbukumbu za biashara; Mkurugenzi pia ana nguvu za kuomba taarifa na kuagiza ukaguzi.
6.-(1) Endapo mlipa ushuru wa huduma anatakiwa kuwasilisha taarifa ya mauzo chini ya Sheria Ndogo hizi atashindwa kuwasilisha taarifa sahihi za mauzo kwa wakati, Mkurugenzi anaweza kutoa notisi ya kumtaka 3 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko Tangazo la Serikali Na.665 (Linaendelea.) mlipa ushuru wa huduma kuwasilisha taarifa hiyo ndani ya siku thelathini kuanzia tarehe ya kutolewa kwa notisi. (2) Mkurugenzi anaweza kumtaka kwa maandishi taarifa kuhusu mfanyabiashara mtu yeyote mwenye anayepaswa kulipa ushuru wa huduma kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizi kuwasilisha taarifa hizo na taarifa husika zitatumika kama taarifa sahihi. (3) Mkurugenzi anaweza kumwagiza kwa maandishi afisa mwidhiniwa kuingia kwenye jengo au eneo la mlipa ushuru wa huduma kwa nia ya kufanya uchunguzi na tathmini ya kumbukumbu za biashara, vitabu vya hesabu na taarifa kwa ajili ya kupata na kujua kiwango sahihi cha ushuru anachotakiwa kulipa. (4) Mkurugenzi anaweza kumteua Kamishna wa kodi ya forodha au kodi ya mapato kwa ajili ya kutathmini na kukusanya ushuru wa huduma na kuwasilisha kwa Halmashauri kwa lengo la kupata ushuru wa huduma pamoja na madeni yake. (5) Mkurugenzi kwa taarifa ya maandishi anaweza kumtaka mlipa ushuru wa huduma yeyote kuwasilisha hesabu zenye taarifa kamili za shughuli za biashara zinazoonesha thamani ya kiasi na thamani ya kifedha ya bidhaa au huduma zilizozalishwa, kutolewa, kusambazwa au kuuzwa katika biashara na taarifa ya fedha katika kipindi maalum kisichozidi siku thelathini tangu tarehe ya taarifa hiyo. (6) Mkurugenzi anaweza kwa taarifa ya maandishi ya siku saba kumtaka mlipa ushuru wa huduma kuwasilisha kumbukumbu za biashara na vitabu vya hesabu kwa nia ya kupata taarifa kwa ajili ya kufanyiwa tathmini au kukusanya ushuru wa huduma. - 7 Verify source ↗
(1) Bila ya kuathiri masharti yaliyowekwa na
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kumteua wakala kukusanya ushuru kwa niaba ya Halmashauri, na wakala huyo lazima akusanye na kuwasilisha makusanyo kulingana na masharti yaliyowekwa.
7.-(1) Bila ya kuathiri masharti yaliyowekwa na Sheria Ndogo hii Mkurugenzi anaweza kuteua Wakala wa kukusanya ushuru kwa niaba ya Halmashauri. (2) Wakala aliyeteuliwa kwa mujibu wa Aya Ndogo ya (1) atakuwa na wajibu ufuatao: (a) kukusanya na kupokea ushuru kwa niaba ya Halmashauri katika eneo alilopangiwa na kwa kiasi au viwango vilivyoidhinishwa katika 4 Uteuzi wa wakala Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko Tangazo la Serikali Na.665 (Linaendelea.) Mamlaka ya afisa mwidhiniwa Ukokotoaji wa ushuru wa huduma Makosa Sheria Ndogo hizi; na (b) kukusanya ushuru kwa kutumia mfumo wa kielektroniki na kuwasilisha makusanyo yote kwa kuzingatia masharti ya mkataba wa uwakala alioingia na Halmashauri. - 8 Verify source ↗
Afisa mwidhiniwa anaweza
AI-assisted research summary: Afisa mwidhiniwa anaweza kupokea, kukubali na kutathmini hesabu za mwisho za mlipa ushuru, au kuzikataa ikiwa ana sababu za msingi za kuamini kuwa si sahihi.
8. Afisa mwidhiniwa anaweza- (a) kupokea na kukubali hesabu za mwisho za mlipa ushuru na kuzifanyia tathmini; au (b) kukataa hesabu za mwisho iwapo atakuwa na sababu za msingi za kuamini kuwa hesabu hizo siyo sahihi. - 9 Verify source ↗
Halmashauri itakokotoa ushuru wa huduma wa
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima ikokotoe ushuru wa huduma kwa mlipa ushuru wa huduma anayetuma taarifa za mauzo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania.
9. Halmashauri itakokotoa ushuru wa huduma wa mlipa ushuru wa huduma anayewasilisha taarifa za mauzo Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa kuzingatia taarifa zinazowasilishwa na mlipa Ushuru wa Huduma katika kipindi maalum cha hesabu. - 10 Verify source ↗
Mtu ambaye
AI-assisted research summary: Mtu anayefanya mojawapo ya vitendo vilivyoorodheshwa, ikiwemo kutoa taarifa zisizo sahihi au za uongo kwa Halmashauri, kushindwa kulipa ushuru wa huduma kwa wakati, au kuzuia utekelezaji wa masharti ya Sheria Ndogo hizi, anatenda kosa.
10. Mtu ambaye- (a) anashindwa kuwasilisha Halmashauri taarifa sahihi za mauzo katika muda ulioainishwa katika Sheria Ndogo hii; (b) anawasilisha Halmashauri taarifa za uongo; (c) anashindwa kulipa ushuru wa huduma katika muda ulioainishwa katika Sheria Ndogo hizi; (d) anamshawishi mlipa ushuru wa huduma kukataa au kukwepa kulipa ushuru wa huduma; (e) anamzuia afisa mwidhiniwa au wakala wa Halmashauri kutekeleza masharti ya Sheria Ndogo hizi; au (f) anatoa taarifa isiyokuwa sahihi kuhusu jambo lolote linaloweza kuathiri jukumu lake au la mtu mwingine la kulipa ushuru wa huduma, (g) anatenda kosa. Adhabu - 11 Verify source ↗
Mtu anayetenda kosa kinyume na masharti ya
AI-assisted research summary: A person who breaches these bylaws and is convicted must pay a fine, go to prison, or both.
11. Mtu anayetenda kosa kinyume na masharti ya Sheria Ndogo hizi, akitiwa hatiani atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi laki mbili na isiyozidi shilingi milioni moja au kifungo kwa kipindi kisichopungua miezi kumi 5 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko Tangazo la Serikali Na.665 (Linaendelea.) Kufifilisha kosa na mbili na kisichozidi miezi ishirini na nne au vyote. - 12 Verify source ↗
(1) Bila kujali masharti ya Sheria Ndogo hizi,
AI-assisted research summary: The Director may compound an offence by charging Sh 200,000 if a person admits the offence voluntarily and is ready to pay the tax due. A person who admits the offence must complete the special form in the Second Schedule.
12.-(1) Bila kujali masharti ya Sheria Ndogo hizi, Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa kwa kutoza kiasi cha Shilingi laki mbili iwapo mtu yeyote atakiri kutenda kosa chini ya Sheria Ndogo hizi kwa hiari na kuwa teyari kulipa ushuru anaodaiwa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizi. (2) Mtu anayekiri kosa chini ya kanuni ndogo ya (1) atajaza fomu maalum iliyoainishwa kwenye Jedwali la Pili la Sheria Ndogo hizi. 6 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko Tangazo la Serikali Na.665 (Linaendelea.) ___________ JEDWALI LA KWANZA ____________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ndogo ya 4(2)) USHURU WA HUDUMA Namb a Aina ya Malipo Leseni ya Biashara
Part
JEDWALI LA KWANZA
- 8 Verify source ↗
Section 8
AI-assisted research summary: The text lists annual service levy amounts in shillings for business licences above TSh 300,000.
8. 1 hadi 15,000/= 20,000/= hadi 35,000/= 40,000/= hadi 45,000/= 50,000/= hadi 60,000/= 65,000/= hadi 100,000/= 105,000/= hadi 150,000/= 155,000/= hadi 200,000/= Malipo ya leseni yoyote ya biashara inayozidi shilingi 300,000/= Kiasi cha malipo ya Ushuru wa Huduma kwa Mwaka (Shilingi) - 0 Verify source ↗
3% ya kila hesabu za mwisho za
AI-assisted research summary: 0.3% applies to each final calculation of sales of goods or services.
0.3% ya kila hesabu za mwisho za mauzo ya bidhaa au huduma - 0 Verify source ↗
3% ya kila hesabu za mwisho za
AI-assisted research summary: Hii ni fomu ya kukiri kosa na kuomba kulipa ushuru unaodaiwa pamoja na faini badala ya kushtakiwa mahakamani, mbele ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko.
0.3% ya kila hesabu za mwisho za mauzo ya bidhaa au huduma 7 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko Tangazo la Serikali Na.665 (Linaendelea.) ____________ JEDWALI LA PILI _____________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 12) FOMU YA KUKIRI NA KUFIFILISHA KOSA Mimi ……………………………………………………… nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya …………………………………………. ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko, kwamba mnamo tarehe …… ya mwezi ……. mwaka …… nilitenda kosa la kukiuka masharti ya kanuni ndogo ya …… ya Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko ya Mwaka, 2024. Kwa Mamlaka aliyopewa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko, niko tayari kulipa kiasi cha Ushuru ninaodaiwa pamoja na faini badala ya kushtakiwa Mahakamani. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA MIMI MWENYEWE KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU Leo tarehe…………. ya Mwezi…………..… Mwaka ……………. Jina……………………………….. Saini……………………… MBELE YANGU: Jina: ……………………………………..…………… Saini………………………….………………………….. Wadhifa: ………………………………………………… Tarehe…………………………………………………………. 8 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko Tangazo la Serikali Na.665 (Linaendelea.) Lakiri ya Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko imegongwa kwenye Marekebisho ya Sheria Ndogo hii kufuatia Azimio lililopitishwa katika Mkutano Mkuu wa Baraza la Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko uliofanyika tarehe 26/8/2022 na kshuhudiwa Lakiri hiyo ikigongwa mbele ya:- NDAKI S. MHULI, Mkurugenzi mtendaji, Halmashauro ya Wilaya, Kakonko FIDEL C. CHIZA, Mwenyekiti, Halmashauro ya Wilaya, Kakonko L.S NAKUBALI, Dodoma, 20 Juni, 2024 MOHAMED OMARY MCHENGERWA (MB.), Waziri wa Nchi-OR-TAMISEMI 9
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
SHERIA NDOGO YA USHURU WA HUDUMA YA HALMASHAURI YA WILAYA YA KAKONKO YA MWAKA 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in