SHERIA NDOGO YA KUZUIA NA KUDHIBITI SUMUKUVU YA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUKOMBE YA MWAKA 2024
This section gives the short title of the by-law: the Bukombe District Council By-Law for Prevention and Control of Sumukuvu, 2024.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- SHERIA NDOGO YA KUZUIA NA KUDHIBITI SUMUKUVU YA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUKOMBE YA MWAKA 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This section gives the short title of the by-law: the Bukombe District Council By-Law for Prevention and Control of Sumukuvu, 2024. This provision says the by-law applies throughout the entire area of Bukombe District Council. This section defines key terms used in the by-law. Halmashauri inaweza kuratibu na kusimamia shughuli za kilimo ndani ya eneo lake ili kuzuia na kudhibiti sumukuvu, na inaweza kufanya ukaguzi katika maeneo fulani kwa ajili ya kusimamia utekelezaji wa sheria ndogo hii. Anyone intending to cultivate must follow proper farm-preparation methods and prepare the farm on time.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of SHERIA NDOGO YA KUZUIA NA KUDHIBITI SUMUKUVU YA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUKOMBE YA MWAKA 2024
Showing 17 of 17
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria
AI-assisted research summary: This section gives the short title of the by-law: the Bukombe District Council By-Law for Prevention and Control of Sumukuvu, 2024.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Kuzuia na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe ya Mwaka 2024. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la
AI-assisted research summary: This provision says the by-law applies throughout the entire area of Bukombe District Council.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the by-law.
3. Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni Afisa yeyote wa Halmashauri na Mkurugenzi aliyeteuliwa kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe; “kanuni bora za kilimo” maana yake ni uandaaji wa shamba kwa usahihi, upandaji mbegu bora kwa wakati na kwa nafasi sahihi, upaliliaji, utumiaji mbolea kwa usahihi, udhibiti wa wadudu na wanyama waharibifu, uvunaji na hifadhi sahihi ya mazao; “kilimo” maana yake ni shughuli ya uzalishaji wa mazao; “kuvu’’ maana yake ni ukungu unaoota kwenye mazao; “mkulima” maana yake ni mtu, taasisi, kampuni au 1 Sheria Ndogo ya Kuzuia Na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Tangazo la Serikali Na.666 (Linaendelea.) kikundi cha watu kinachojihusisha na shughuli za kilimo; “mfanyabiashara’’ maana yake ni taasisi, kampuni, kikundi cha watu au mtu binafsi anayejihusisha na shughuli za kuuza au kununua mazao ya kilimo; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe au Afisa yeyote aliyeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi; “mazao” maana yake ni punje zinazotokana na mmea wa mhindi, mpunga, uwele, mtama, karanga, ngano, ufuta, alizeti, shayiri, ulezi na mazao ya mizizi yatokanayo na mihogo au viazi; “sumukuvu” maana yake ni sumu inayozalishwa na kuvu wanaoota kwenye mazao; “uhifadhi” maana yake ni utaratibu wa kutunza mazao katika sehemu ambayo haisababishi mazingira ya uotaji wa kuvu; “ukaushaji” maana yake ni taratibu sahihi za kupunguza unyevu kwenye mazao kwa ajili ya matumizi au uhifadhi; “usindikaji” maana yake ni hatua ya uchakataji wa zao kwa lengo la kuongeza thamani; “uvunaji” maana yake ni uondoaji wa mazao kutoka kwenye mmea baada ya kukomaa au kukauka; “viashiria vya sumukuvu” maana yake ni dalili zinazoonesha uwepo wa sumukuvu kwenye mazao ya mahindi, mpunga, uwele, mtama, karanga, ngano, ufuta, alizeti, shayiri, ulezi na mazao ambayo hayajakauka vizuri; na “viuatilifu” maana yake ni sumu ya kuua au kuzuia wadudu waharibifu wa mazao. Uratibu na usimamizi wa shughuli za kilimo na udhibiti wa sumukuvu - 4 Verify source ↗
(1) Halmashauri itakuwa na mamlaka ya
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kuratibu na kusimamia shughuli za kilimo ndani ya eneo lake ili kuzuia na kudhibiti sumukuvu, na inaweza kufanya ukaguzi katika maeneo fulani kwa ajili ya kusimamia utekelezaji wa sheria ndogo hii.
4.- (1) Halmashauri itakuwa na mamlaka ya kuratibu na kusimamia shughuli za kilimo ndani ya eneo la Halmashauri kwa lengo la kuzuia na kudhibiti sumukuvu. (2) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (1), Halmashauri itakuwa na mamlaka ya kufanya ukaguzi 2 Sheria Ndogo ya Kuzuia Na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Tangazo la Serikali Na.666 (Linaendelea.) katika mashamba au vyombo vya usafirishaji wa mazao, maghala, kiwanda au eneo la usindikaji kwa lengo la kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii. Uandaaji wa shamba - 5 Verify source ↗
Mtu yeyote anayekusudia kulima, atapaswa
AI-assisted research summary: Anyone intending to cultivate must follow proper farm-preparation methods and prepare the farm on time.
5. Mtu yeyote anayekusudia kulima, atapaswa kuzingatia misingi ifuatayo: (a) kufuata njia sahihi za uandaaji wa shamba; na (b) kutayarisha shamba kwa wakati. Upandaji wa mazao - 6 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayepanda mazao atapaswa
AI-assisted research summary: Anyone planting crops must follow proper planting methods.
6. Mtu yeyote atakayepanda mazao atapaswa kuzingatia njia sahihi za upandaji ikiwa ni pamoja na- (a) kutumia mbegu bora; (b) kupanda kwa kuzingatia kalenda ya kilimo; na (c) kupanda kwa nafasi sahihi. Utunzaji wa mazao shambani - 7 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayepanda mazao atapaswa
AI-assisted research summary: Anyone who plants crops must care for them properly.
7. Mtu yeyote atakayepanda mazao atapaswa kuyatunza kwa kuzingatia njia sahihi za utunzaji wa mazao ikiwa ni pamoja na- (a) kutumia mbolea; (b) kupalilia kwa wakati; na (c) kudhibiti magonjwa, wadudu au wanyama waharibifu. Uvunaji wa mazao - 8 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayevuna mazao atapaswa
AI-assisted research summary: Anyone harvesting crops must do so using good harvesting practices.
8. Mtu yeyote atakayevuna mazao atapaswa kuvuna kwa kuzingatia kanuni bora za uvunaji ikiwa ni pamoja na- (a) kuvuna mara baada ya mazao kukomaa au kukauka; (b) kusafirisha na kuhifadhi vizuri; (c) kutumia vifaa salama vya kuvunia; na (d) kusafisha shamba baada ya kuvuna. Ukaushaji wa mazao - 9 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayevuna mazao anapaswa
AI-assisted research summary: Mtu yeyote anayevuna mazao lazima ayakaushe mara tu baada ya kuvuna kwa njia sahihi.
9. Mtu yeyote atakayevuna mazao anapaswa kuyakausha kwa kutumia njia sahihi mara tu baada ya kuvuna ikiwa ni pamoja na- (a) njia za asili zisizoruhusu kuvu kuota; (b) kutumia maturubai, mikeka na vichanja vinavyozuia uchafuzi wa mazao; na 3 Sheria Ndogo ya Kuzuia Na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Tangazo la Serikali Na.666 (Linaendelea.) (c) kukausha kwa itakayoelekezwa na mtaalamu. njia yoyote sahihi Uhifadhi wa mazao - 10 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote atakuwa na wajibu wa
AI-assisted research summary: Mtu yeyote lazima ahifadhi mazao kwa njia sahihi za asili au za kisasa zinazozuia kuota kwa kuvu.
10.-(1) Mtu yeyote atakuwa na wajibu wa kuhifadhi mazao kwa kutumia njia sahihi za kiasili au za kisasa ambazo zitazuia kuota kwa kuvu. (2) Njia sahihi za kuhifadhi mazao zinazorejewa chini ya kanuni ndogo ya (1) ni pamoja na- (a) mifuko isiyopitisha hewa; (b) magunia ya kawaida kwa ajili ya mazao yaliyowekwa viuatilifu; (c) kihenge na kichanja bora cha asili; (d) silo au pipa maalumu; (e) ghala bora lililo safi; (f) kutumia viuatilifu kwenye mazao kwa kuzingatia ushauri wa kitaalamu; au (g) njia nyingine kadiri itakavyoshauriwa na wataalamu. Wajibu wa Halmashau ri - 11 Verify source ↗
Halmashauri katika utekelezaji wa Sheria
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima itekeleze hatua za kuhamasisha, kutoa elimu, kuwezesha upatikanaji wa pembejeo, kutunza kumbukumbu, na kuanzisha miundombinu ya mafunzo na biashara ya mazao; Mkurugenzi anaweza kumteua Afisa Mwidhiniwa kusimamia utekelezaji.
11. Halmashauri katika utekelezaji wa Sheria Ndogo hii itakuwa na wajibu wa- (a) kuhamasisha na kutoa elimu ya uzalishaji na usimamizi wa mazao; (b) kuhamasisha uhifadhi wa mazao katika ili kuepuka eneo au mahala salama uchafuzi wa sumukuvu; (c) kuweka mazingira wezeshi ya upatikanaji wa pembejeo za kilimo; (d) kutunza kumbukumbu za mashamba yote ya mazao ya kilimo katika kata na vijiji ili kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; (e) kuanzisha na kuendeleza mashamba darasa na vituo maalumu kwa ajili ya kutoa mafunzo ya udhibiti wa sumukuvu; (f) kuanzisha na kuhamasisha wakulima na wadau wengine kujenga sehemu za kuhifadhia mazao; au (g) kuandaa vituo maalumu vya kuuza na kununua mazao. 4 Sheria Ndogo ya Kuzuia Na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Tangazo la Serikali Na.666 (Linaendelea.) (2) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (1), Mkurugenzi anaweza kumteua Afisa Mwidhiniwa kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii. Wajibu wa mkulima Wajibu wa msafirishaji Wajibu wa mfanyabias hara Wajibu wa msindikaji Makosa na adhabu - 12 Verify source ↗
Kila mkulima atakuwa na wajibu wa
AI-assisted research summary: Kila mkulima lazima afuate kanuni bora za kilimo na usimamizi wa mazao, awajulishe Halmashauri dalili za kuvu katika mazao, na ahudhurie mafunzo ya kudhibiti sumukuvu yanayoandaliwa na Halmashauri.
12. Kila mkulima atakuwa na wajibu wa- (a) kufanya za shughuli kwa kuzingatia kanuni bora za kilimo na usimamizi wa mazao kabla na baada ya kuvuna; kilimo (b) kutoa taarifa kwa Halmashauri kuhusu uwepo wa dalili ya kuvu katika mazao; na (c) kushiriki mafunzo yaliyoandaliwa na Halmashauri ya kudhibiti sumukuvu na kutekeleza ujuzi uliopatikana kwenye mafunzo hayo. vifungashio - 13 Verify source ↗
Mtu yeyote anayesafirisha mazao anapaswa
AI-assisted research summary: Mtu anayesafirisha mazao lazima ahakikishe vifaa au njia anazotumia kusafirisha mazao ni vikavu na haziruhusu maji, unyevu, au vumbi kuingia.
13. Mtu yeyote anayesafirisha mazao anapaswa kuhakikisha anavyotumia na kusafirisha mazao ni vikavu au visivyoruhusu maji au unyevu na vumbi kuingia ndani ili kuepusha kuvu kuota kwenye mazao. vifaa kuhakikisha - 14 Verify source ↗
Kila mfanyabiashara wa mazao atakuwa na
AI-assisted research summary: Kila mfanyabiashara wa mazao lazima ahifadhi, asafirishe au kuuza mazao yasiyo na viashiria vya sumukuvu kama vilivyo kwenye Jedwali la Kwanza.
14. Kila mfanyabiashara wa mazao atakuwa na wajibu wa anahifadhi, anasafirisha au kuuza mazao ambayo hayana viashiria vya uwepo wa sumukuvu kama inavyoonekana katika Jedwali la Kwanza la Sheria Ndogo hii. ananunua,
Part
Jedwali la Kwanza la Sheria Ndogo hii.
- 15 Verify source ↗
Kila msindikaji atakuwa na wajibu wa
AI-assisted research summary: Every processor must process produce that does not show signs of the presence of sumukuvu.
15. Kila msindikaji atakuwa na wajibu wa kusindika mazao ambayo hayana viashiria vya uwepo wa sumukuvu kama la Kwanza la Sheria Ndogo hii. inavyoonekana katika Jedwali - 16 Verify source ↗
Mtu yeyote ambaye
AI-assisted research summary: Anyone who mishandles crops or does the listed harmful acts commits an offence and may be fined, imprisoned up to 12 months, or both.
16. Mtu yeyote ambaye- (a) hataandaa, hatapanda au kutunza shamba na mazao kwa usahihi; (b) hatavuna kwa wakati mara baada ya mazao kukomaa; (c) atachelewa kuondoa mazao shambani baada ya kuvuna; 5 Sheria Ndogo ya Kuzuia Na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Tangazo la Serikali Na.666 (Linaendelea.) (d) ataanika mazao kwenye udongo, vumbi au mchanga; (e) atakausha mazao katika mazingira yanayoweza kusababisha sumukuvu; viuatilifu (f) atatumia vilivyozuiliwa kutumika kwenye mazao; (g) atauza mazao yenye viashiria vya sumukuvu; (h) atasafirisha njia mazao zitakazosababisha mazingira ya kuvu kuota; kwa (i) atatumia mazao yenye viashiria vya sumukuvu wakati wa usindikaji; au (j) atatenda jambo lolote lililokatazwa na Sheria Ndogo hii, atakuwa ametenda kosa na akipatikana na hatia atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi elfu hamsini na isiyozidi shilingi laki tatu au kifungo kisichozidi miezi kumi na mbili au vyote kwa pamoja. Kufifilisha kosa - 17 Verify source ↗
Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa kwa kumtoza mtenda kosa hadi shilingi 50,000 ikiwa anakiri kosa na kukubali kujaza fomu ya Jedwali la Pili.
17. Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha kosa kwa kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii kiasi kisichozidi shilingi elfu hamsini endapo mkosaji atakiri kosa na kuwa tayari kujaza fomu maalumu iliyoainishwa katika Jedwali la Pili la Sheria Ndogo hii. 6 Sheria Ndogo ya Kuzuia Na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Tangazo la Serikali Na.666 (Linaendelea.) _____________ JEDWALI LA KWANZA _____________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 14 na 15) VIASHIRIA VYA SUMUKUVU Namba Aina ya Mazao Hali ya Unyevu au Kuvu Mwonekano wa Punje 1 Mahindi Punje kuwa na unyevu Punje kuwa na ukungu au kuvu - rangi kahawia au nyeusi au kijani au njano kuwa na harufu ya uvundo 2 Karanga Punje kuwa na unyevu Punje kuwa na ukungu au kuvu – rangi kahawia au nyeusi au kijani au njano kuwa na harufu ya uvundo 7 Sheria Ndogo ya Kuzuia Na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Tangazo la Serikali Na.666 (Linaendelea.) _____________ JEDWALI LA PILI _____________ (Limetengenezwa chini kanuni ya 17) FOMU YA KUKIRI NA KUFILILISHA KOSA Mimi ……………………………………………………… nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya …………………………………………. ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe, kwamba mnamo tarehe …… ya mwezi ……. mwaka …… nilitenda kosa la kukiuka masharti ya kanuni ya …… ya Sheria Ndogo ya Kuzuia na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe ya Mwaka 2024. Kwa mamlaka aliyopewa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe, niko tayari kulipa kiasi cha Shilingi…………… kwa ajili ya kufifilisha kosa nililotenda chini ya Sheria Ndogo ya Kuzuia na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe ya Mwaka 2024 ninayodaiwa pamoja na faini. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA MIMI MWENYEWE KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU Leo tarehe………….ya mwezi…………..… mwaka ……………. Jina……………………………….. Saini……………………… MBELE YANGU: Jina: ……………………………………..…………………… Saini………………………….…………………………..……… Wadhifa: ………………………………………………………… Tarehe…………………………………………………………. 8 Sheria Ndogo ya Kuzuia Na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe Tangazo la Serikali Na.666 (Linaendelea.) Lakiri ya Halmashauri ya wilaya ya Bukombe imegongwa kwenye Sheria Ndogo hii kufuatia Azimio lililopitishwa katika Mkutano wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe uliofanyika tarehe 18/5/2022 na kushuhudiwa Lakiri hiyo ikigongwa mbele ya:- LUTENGASNO G. MWALWIBA, Mkurugenzi mtendaji, Halmashauri ya Wilaya, Bukombe YUSUPH M. YUSUPH, Mwenyekiti, Halmashauri ya wilaya bukombe L.S Dodoma, 20 Februari, 2024 NAKUBALI, MOHAMED OMARY MCHENGERWA (MB.), Waziri wa Nchi-OR-TAMISEMI 9
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
SHERIA NDOGO YA KUZUIA NA KUDHIBITI SUMUKUVU YA HALMASHAURI YA WILAYA YA BUKOMBE YA MWAKA 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in