Sheria Ndogo ya Kudhibiti Ombaomba ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ya Mwaka 2024
This section gives the short title: the by-law is called the Kinondoni Municipal Council Beggars Control By-law, 2024.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Kudhibiti Ombaomba ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ya Mwaka 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This section gives the short title: the by-law is called the Kinondoni Municipal Council Beggars Control By-law, 2024. This section says the by-law applies throughout the whole area of Kinondoni Municipal Council. This section defines several terms used in the by-laws, including council, beggar, open area, shelter centre, ward executive officer, and authorized officer. Halmashauri must control beggars across the whole Council area, and each Ward Executive Officer must do the same in their area of authority. Mtu anayeonekana akiomba fedha au chakula kwenye eneo la ombaomba anaweza kuchukuliwa kama ombaomba na kukamatwa; Afisa Mwidhiniwa lazima ampige picha aliyechukuliwa.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Kudhibiti Ombaomba ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ya Mwaka 2024
Showing 9 of 9
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo
AI-assisted research summary: This section gives the short title: the by-law is called the Kinondoni Municipal Council Beggars Control By-law, 2024.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Kudhibiti Ombaomba ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ya Mwaka 2024. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la
AI-assisted research summary: This section says the by-law applies throughout the whole area of Kinondoni Municipal Council.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la Mamlaka ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama
AI-assisted research summary: This section defines several terms used in the by-laws, including council, beggar, open area, shelter centre, ward executive officer, and authorized officer.
3. Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni afisa yeyote la aliyeteuliwa na Mkurugenzi kwa kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “Afisa Mtendaji wa Kata” maana yake ni mtumishi yeyote wa umma aliyeajiriwa au kuteuliwa kutekeleza majukumu ya Mtendaji wa Kata iliyopo ndani ya eneo la Halmashauri; lengo “eneo la wazi” maana yake ni eneo lolote la ardhi lenye bustani au ambalo halijaendelezwa na lipo kwa ajili ya matumizi ya umma; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni; 1 Sheria Ndogo ya Kudhibiti Ombaomba ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Tangazo La Serikali Na. 509 (Linaendelea) “kituo cha hifadhi” maana yake ni kituo au mahali au jengo lolote ambalo limetengwa au linatumika katika kuwahifadhi ombaomba, wazee, watoto au watu wenye ulemavu kwa lengo la kuwapa mahitaji ya msingi; “mkazi” maana yake ni mtu yeyote anayeishi au anayefanya shughuli yoyote ndani ya eneo la Halmashauri; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni au Afisa yeyote atakayeteuliwa ya Mkurugenzi; kutekeleza majukumu “mtaa” maana yake ni eneo lolote lililopo ndani ya Halmashauri na inajumuisha maeneo yote ya barabara na hifadhi za barabara na njia ya waenda kwa miguu; “ombaomba” maana yake ni mtu anayeishi kwa kutegemea kuomba chakula, fedha au kitu kingine kutoka kwa mtu mwingine kwenye mitaa na maeneo ya wazi yaliyoko ndani ya eneo la Halmashauri; “Wakala” maana yake ni mtu binafsi au kikundi cha watu, kampuni au shirika ambalo limeteuliwa na Halmashauri kufanya kazi yoyote kwa niaba ya Halmashauri chini ya Sheria Ndogo hizi. - 4 Verify source ↗
(1) Halmashauri itakuwa na wajibu wa kudhibiti
AI-assisted research summary: Halmashauri must control beggars across the whole Council area, and each Ward Executive Officer must do the same in their area of authority.
4.-(1) Halmashauri itakuwa na wajibu wa kudhibiti ombaomba kwenye eneo lote la Halmashauri. (2) Halmashauri inaweza kumteua wakala ambaye atatekeleza la kudhibiti ombaomba kwenye sehemu au eneo lote la Halmashauri kwa niaba ya Halmashauri. jukumu (3) Kila Afisa Mtendaji wa Kata atakuwa na jukumu la kudhibiti ombaomba katika eneo lake la mamlaka. Wajibu wa kudhibiti ombaomba Kutambua na kukamata
Part
sehemu au eneo lote la Halmashauri kwa niaba ya
- 5 Verify source ↗
(1) Mtu atakayekutwa mtaani au kwenye eneo la
AI-assisted research summary: Mtu anayeonekana akiomba fedha au chakula kwenye eneo la ombaomba anaweza kuchukuliwa kama ombaomba na kukamatwa; Afisa Mwidhiniwa lazima ampige picha aliyechukuliwa.
5.-(1) Mtu atakayekutwa mtaani au kwenye eneo la 2 Sheria Ndogo ya Kudhibiti Ombaomba ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Tangazo La Serikali Na. 509 (Linaendelea) ombaomba wazi na Afisa Mwidhiniwa au wakala akiomba fedha au chakula kwa mtu mwingine atahesabika kuwa ni ombaomba na atakamatwa na kuchukuliwa taarifa zake muhimu ikiwemo: (a) jina kamili; (b) jinsi na umri; na (c) kijiji, wilaya na mkoa anaotoka. (2) Afisa Mwidhiniwa atampiga picha mtu yeyote atakayekamatwa kama ombaomba chini ya kanuni ndogo ya (1) na picha hiyo itatumika kwa matumizi ya Ofisi ili kurahisisha utambuzi iwapo mtu huyo atarudia kuwa ombaomba. (3) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (1), ombaomba kufikishwa mahakamani kwa kutenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii. aliyekamatwa anaweza Msaada kwa wenye mahitaji Makosa - 6 Verify source ↗
Mtu, kikundi cha watu au
AI-assisted research summary: Watu, vikundi au taasisi zinazotaka kutoa msaada kwa wahitaji lazima kupeleka msaada huo kwenye kituo cha hifadhi, taasisi ya dini, kituo cha kulelea yatima, wazee, watu wenye ulemavu, watu wasiojiweza au Halmashauri.
6. Mtu, kikundi cha watu au taasisi yoyote inayohitaji kutoa msaada wa aina yoyote kwa watu wanaohitaji msaada itatakiwa kuwasilisha misaada hiyo kwenye kituo cha hifadhi, taasisi ya dini, kituo cha kulelea watoto yatima, wazee au watu wenye ulemavu na watu wengine wasiojiweza au Halmashauri. - 7 Verify source ↗
(1) Mtu ambaye
AI-assisted research summary: Mtu anayefanya mojawapo ya vitendo vilivyoorodheshwa hapa anatenda kosa na anaweza kupewa faini, kifungo, au vyote.
7.-(1) Mtu ambaye- (a) anaomba na kupokea msaada wa fedha, chakula au kitu kingine chochote mitaani, kwenye maeneo ya wazi au mahali popote ambapo siyo kituo cha hifadhi; (b) anatoa msaada wa fedha, chakula au kitu kingine chochote kwa ombaomba yeyote mtaani, kwenye maeneo ya wazi au mahali popote ambapo siyo kituo cha hifadhi; (c) anamtembeza mtu yeyote kwa kutumia chombo au chochote maalumu kumtembeza kwa miguu au kwa njia nyingine yoyote kwa lengo la kuombaomba; cha walemavu 3 Sheria Ndogo ya Kudhibiti Ombaomba ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Tangazo La Serikali Na. 509 (Linaendelea) (d) anamsafirisha kutoka eneo moja hadi lingine kumtumia lengo la mtu kwa yeyote kuombaomba mitaani; Adhabu ya jumla Ufifilishaji wa makosa (e) anamtumikisha mtoto katika shughuli za kuombaomba kwenye magari, barabarania au mahali pengine popote; (f) anashindwa kutoa taarifa au anatoa taarifa za uongo kuhusiana na ombaomba kwa lengo la kukwamisha upatikanaji wao ili wasiondolewe maeneo yasiyo rasmi; au (g) anamzuia afisa yeyote au Wakala kutekeleza majukumu yake yaliyoainishwa chini ya Sheria Ndogo hii, anatenda kosa na akitiwa hatiani atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi elfu hamsini na isiyozidi shilingi laki tatu au kifungo kwa kipindi kisichozidi miezi kumi na mbili au vyote. - 8 Verify source ↗
Mtu anayekiuka masharti ya Sheria Ndogo hii
AI-assisted research summary: A person who breaches this by-law, where no specific penalty is set, commits an offence and may be fined up to 50,000 shillings, imprisoned for up to 3 months, or both if convicted.
8. Mtu anayekiuka masharti ya Sheria Ndogo hii ambapo hakuna adhabu mahsusi iliyowekwa, anatenda kosa na akitiwa hatiani atawajibika kulipa faini isiyozidi shilingi elfu hamsini au kifungo kwa kipindi kisichozidi miezi mitatu au vyote. - 9 Verify source ↗
(1) Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa kwa kutoza faini ya shilingi 50,000 ikiwa mkosaji anakiri kosa na kujaza fomu maalumu; Halmashauri pia inaweza kumrejesha aliyekamatwa akiwa ombaomba kwenda mkoa wake na kumkabidhi kwa Ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa.
9.-(1) Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha kosa kwa kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa kinyume cha Sheria Ndogo hii kiasi cha shilingi elfu hamsini iwapo mkosaji atakiri kosa na kuwa tayari kujaza fomu maalumu iliyoainishwa katika Jedwali. (2) Pamoja na mamlaka ya Mkurugenzi kufifilisha kosa chini ya kanuni ndogo ya (1), Halmashauri inaweza kumrejesha mtu yeyote aliyekamatwa ndani ya maeneo ya Halmashauri akiwa ombaomba kwenye mkoa anaotoka na kumkabidhi katika Ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa husika. 4 Sheria Ndogo ya Kudhibiti Ombaomba ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Tangazo La Serikali Na. 509 (Linaendelea) ______ JEDWALI ______ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 10(1)) FOMU YA KUKIRI NA KUFILILISHA KOSA Mimi ……………………………………………………… nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya …………………………………………. ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni kwamba mnamo tarehe …… ya mwezi ……. Mwaka …… nilitenda kosa la kukiuka masharti ya nanuni ya ………ya Sheria Ndogo ya Kudhibiti Ombaomba ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ya Mwaka 2024. Kwa Mamlaka aliyopewa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, niko tayari kulipa kiasi cha faini ninachodaiwa. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA MIMI MWENYEWE KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU Leo tarehe…………. Jina……………………………….. Saini……………………… ya Mwezi…………..… Mwaka ………… MBELE YANGU: Jina: ……………………………………..……………………… Saini………………………….…………………………..……… Wadhifa: ………………………………………………………… Tarehe…………………………………………………………. 5 Sheria Ndogo ya Kudhibiti Ombaomba ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Tangazo La Serikali Na. 509 (Linaendelea) Lakiri ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni imegongwa kwenye sheria ndogo hii kufuatia azimio lililopitishwa kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni uliofanyika tarehe 24 mwezi 08 Mwaka 2023 na kushuhudiwa Lakiri hiyo ikigongwa mbele ya ; HANIFA SULEIMAN HAMZA Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni SONGORO KHAMISI MNYONGE Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni NAKUBALI L.S Dodoma MOHAMED OMARY MCHENGERWA 10 Disemba, 2023 Waziri wa Nchi ofisi ya Rais (Tawala za mikoa na serikali za mitaa) 6
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Kudhibiti Ombaomba ya Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni ya Mwaka 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in