Sheria Ndogo ya Kuzuia na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Gairo ya Mwaka 2024
This section gives the short title of the by-law.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Kuzuia na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Gairo ya Mwaka 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This section gives the short title of the by-law. This provision says the bylaw applies across the entire area of the Gairo District Council. This section defines terms used in the bylaw. Halmashauri inaweza kuratibu na kusimamia shughuli za kilimo ndani ya eneo lake ili kuzuia na kudhibiti sumukuvu, na inaweza pia kufanya ukaguzi katika maeneo fulani ya kilimo na usindikaji. A person intending to cultivate must follow proper farm-preparation methods and prepare the field on time.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Kuzuia na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Gairo ya Mwaka 2024
Showing 19 of 19
- 1 Verify source ↗
Sheria ndogo hii itajulikana kama Sheria
AI-assisted research summary: This section gives the short title of the by-law.
1. Sheria ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Kuzuia na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Gairo ya Mwaka 2024. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote
AI-assisted research summary: This provision says the bylaw applies across the entire area of the Gairo District Council.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya ya Gairo. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama
AI-assisted research summary: This section defines terms used in the bylaw.
3. Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni Afisa yeyote wa aliyeteuliwa na Mkurugenzi Halmashauri kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Gairo; “kanuni bora za kilimo” maana yake ni uandaaji wa shamba kwa usahihi, upandaji mbegu bora kwa wakati na kwa nafasi sahihi, upaliliaji, utumiaji mbolea kwa usahihi, udhibiti wa wadudu na wanyama waharibifu, uvunaji na hifadhi sahihi ya mazao; “kilimo” maana yake ni shughuli ya uzalishaji wa mazao; “kuvu’’ maana yake ni ukungu unaoota kwenye mazao; 1 Sheria Ndogo ya kuzuia na kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Tangazo la Serikali Na. 514 (Linaendelea) “mkulima” maana yake ni mtu, taasisi, kampuni au kikundi cha watu wanaojishughulisha na shughuli za kilimo; “mfanyabiashara’’ maana yake ni taasisi, kampuni, kikundi cha watu au mtu binafsi anayejihusisha na shughuli za kuuza au kununua mazao ya kilimo; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo au afisa yeyote aliyeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi; “mazao’’ maana yake ni punje zinazotokana na mmea wa mhindi, uwele, mtama, karanga, ngano, ufuta, alizeti, shayiri au ulezi; “sumukuvu” maana yake ni sumu zinazozalishwa na kuvu iliyoota kwenye mazao; “usindikaji” maana yake ni hatua ya uchakataji wa zao kwa lengo la kuongeza thamani; “uvunaji” maana yake ni uondoaji wa mazao kutoka kwenye mmea baada ya kukomaa au kukauka; “viashiria vya sumukuvu” maana yake ni dalili zinazoonesha uwepo wa sumukuvu kwenye mazao ya mahindi, uwele, mtama, karanga, ngano, ufuta, alizeti, shayiri, ulezi uliovunjika au mazao ambayo hayajakauka vizuri; “viuatilifu” maana yake ni sumu ya kuua au kuzuia wadudu waharibifu wa mazao. - 4 Verify source ↗
(1) Halmashauri itakuwa na mamlaka ya
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kuratibu na kusimamia shughuli za kilimo ndani ya eneo lake ili kuzuia na kudhibiti sumukuvu, na inaweza pia kufanya ukaguzi katika maeneo fulani ya kilimo na usindikaji.
4. (1) Halmashauri itakuwa na mamlaka ya kuratibu na kusimamia shughuli za kilimo ndani ya eneo la Halmashauri kwa lengo la kuzuia na kudhibiti sumukuvu. (2) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (1), Halmashauri itakuwa na mamlaka ya kufanya ukaguzi katika mashamba, vyombo vya usafirishaji wa mazao, maghala, viwanda au eneo la usindikaji kwa 2 Uratibu na usimamizi wa shughuli za kilimo na udhibiti wa sumukuvu Sheria Ndogo ya kuzuia na kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Tangazo la Serikali Na. 514 (Linaendelea) lengo la kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii. Uandaaji wa shamba - 5 Verify source ↗
Mtu
AI-assisted research summary: A person intending to cultivate must follow proper farm-preparation methods and prepare the field on time.
5. Mtu anayekusudia kulima atapaswa kuzingatia misingi ifuatayo: (a) kufuata njia sahihi za uandaaji wa shamba; na (b) kutayarisha shamba kwa wakati. Upandaji wa mazao - 6 Verify source ↗
Mtu
AI-assisted research summary: Mtu anayepanda mazao lazima atumie njia sahihi za upandaji, ikiwemo mbegu bora, kufuata kalenda ya kilimo, na kupanda kwa nafasi sahihi.
6. Mtu atakayepanda mazao atapaswa kuzingatia njia sahihi za upandaji ikiwa ni pamoja na- (a) kutumia mbegu bora; (b) kupanda kwa kuzingatia kalenda ya kilimo; na (c) kupanda kwa nafasi sahihi. Utunzaji wa mazao shambani - 7 Verify source ↗
Mtu aliyepanda mazao atapaswa kuyatunza
AI-assisted research summary: Mtu aliyepanda mazao lazima ayatunza kwa njia sahihi, ikiwemo kutumia mbolea, kupalilia kwa wakati, na kudhibiti magonjwa, wadudu na wanyama waharibifu.
7. Mtu aliyepanda mazao atapaswa kuyatunza kwa kuzingatia njia sahihi za utunzaji wa mazao ikiwa ni pamoja na- (a) kutumia mbolea; (b) kupalilia kwa wakati; na (c) kudhibiti magonjwa, wadudu na wanyama waharibifu. Uvunaji wa mazao - 8 Verify source ↗
Mtu atakayevuna mazao atapaswa kuvuna
AI-assisted research summary: Mtu anayevuna mazao lazima avune kwa kufuata kanuni bora za uvunaji.
8. Mtu atakayevuna mazao atapaswa kuvuna kwa kuzingatia kanuni bora za uvunaji ikiwa ni pamoja na- (a) kuvuna mara baada ya mazao kukomaa au kukauka; (b) kusafirisha na kuhifadhi vizuri; (c) kutumia vifaa salama vya kuvunia; na (d) kusafisha shamba baada ya kuvuna. Ukaushaji wa mazao - 9 Verify source ↗
Mtu
AI-assisted research summary: Mtu lazima akaushe mazao kwa njia sahihi mara baada ya kuvuna.
9. Mtu atapaswa kuyakausha kwa kutumia njia sahihi mara baada ya kuvuna ikiwa ni pamoja na- atakayevuna mazao 3 Sheria Ndogo ya kuzuia na kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Tangazo la Serikali Na. 514 (Linaendelea) (a) njia za asili zisizoruhusu kuvu kuota; (b) kutumia turubai, mkeka au kichanja (c) kukausha kinachozuia uchafuzi wa mazao; au yoyote kwa itakayoelekezwa na mtaalamu. njia sahihi Uhifadhi wa mazao - 10 Verify source ↗
(1) Mtu atawajibika kuhifadhi mazao kwa
AI-assisted research summary: A person must store produce using proper traditional or modern methods that prevent mold.
10. -(1) Mtu atawajibika kuhifadhi mazao kwa kutumia njia sahihi za kiasili au za kisasa ambazo zitazuia kuvu kuota. (2) Njia sahihi zinazoelekezwa kutumika chini ya kanuni ndogo ya (1) ni pamoja na- (a) mifuko isiyopitisha hewa; (b) magunia ya kawaida kwa ajili ya mazao yaliyowekwa viuatilifu; (c) kihenge au kichanja bora cha asili; (d) silo au pipa maalumu; (e) ghala bora lililo safi; (f) kutumia viuatilifu kwenye mazao kwa kuzingatia ushauri wa kitaalamu; au (g) njia nyingine kadri itakavyoshauriwa na wataalamu. Wajibu wa Halmashauri - 11 Verify source ↗
(1) Katika utekelezaji wa Sheria Ndogo hii,
AI-assisted research summary: Halmashauri must support crop production and storage, keep farm records, build training facilities, organize market centers, and the Director may appoint a designated officer to supervise implementation.
11. -(1) Katika utekelezaji wa Sheria Ndogo hii, Halmashauri itakuwa na wajibu wa- (a) kuhamasisha na kutoa elimu ya uzalishaji na usimamizi wa mazao; (b) kuhamasisha uhifadhi wa mazao katika eneo au mahali salama ili kuepuka uchafuzi na sumukuvu; (c) kuweka mazingira wezeshi ya upatikanaji wa pembejeo za kilimo; (d) kutunza kumbukumbu za mashamba yote ya mazao ya kilimo katika kata na vijiji ili kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; (e) kuanzisha na kuendeleza mashamba darasa na vituo maalumu kwa ajili ya kutolea 4 Sheria Ndogo ya kuzuia na kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Tangazo la Serikali Na. 514 (Linaendelea) mafunzo ya udhibiti wa sumukuvu; (f) kuanzisha na kuhamasisha wakulima na za sehemu wadau wengine kujenga kuhifadhia mazao; na (g) kuandaa vituo maalumu vya kuuzia na kununua mazao. (1), Mkurugenzi (2) Bila ya kuathiri masharti ya kanuni ndogo anaweza kumteua Afisa ya Mwidhiniwa kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii. - 12 Verify source ↗
Mkulima atakuwa na wajibu wa
AI-assisted research summary: Mkulima lazima afuate kanuni bora za kilimo, aripoti dalili za kuvu kwenye mazao kwa Halmashauri, na ahudhurie mafunzo ya kudhibiti sumukuvu yaliyoandaliwa na Halmashauri.
12. Mkulima atakuwa na wajibu wa- (a) kufanya shughuli za kilimo kwa kuzingatia kanuni bora za kilimo na usimamizi wa mazao kabla na baada ya kuvuna; (b) kutoa taarifa kwa Halmashauri kuhusu uwepo wa dalili ya kuvu katika mazao; na (c) kushiriki mafunzo yaliyoandaliwa na Halmashauri ya kudhibiti sumukuvu na kutekeleza katika mafunzo hayo. uliopatikana ujuzi kwamba, - 13 Verify source ↗
Mtu anayesafirisha mazao anapaswa
AI-assisted research summary: Mtu anayesafirisha mazao lazima ahakikishe vifaa vya kusafirishia ni vikavu na haviruhusu maji, unyevu au vumbi kuingia.
13. Mtu anayesafirisha mazao anapaswa kuhakikisha vifaa anavyotumia kusafirishia mazao ni vikavu na visivyoruhusu maji, unyevu au vumbi kuingia ndani ili kuepusha kuvu kuota katika mazao. vifungashio na kuhakikisha - 14 Verify source ↗
Mfanyabiashara wa mazao atakuwa na
AI-assisted research summary: Mfanyabiashara wa mazao lazima ahifadhi, asafirishe, au auze mazao ambayo hayana viashiria vya uwepo wa sumukuvu kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Kwanza.
14. Mfanyabiashara wa mazao atakuwa na anahifadhi, wajibu wa anasafirisha au kuuza mazao ambayo hayana viashiria vya uwepo wa sumukuvu kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Kwanza. ananunua, Wajibu wa mkulima Wajibu wa msafirishaji Wajibu wa mfanyabiashara Wajibu wa msindikaji
Part
Jedwali la Kwanza.
- 15 Verify source ↗
Kila msindikaji atakuwa na wajibu wa
AI-assisted research summary: Kila msindikaji lazima asindike mazao yasiyo na viashiria vya sumukuvu.
15. Kila msindikaji atakuwa na wajibu wa kusindika mazao ambayo hayana viashiria vya uwepo wa sumukuvu kama ilivyoainishwa katika Sheria 5 Sheria Ndogo ya kuzuia na kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Tangazo la Serikali Na. 514 (Linaendelea) Ndogo hii. Makosa na adhabu - 16 Verify source ↗
Mtu ambaye
AI-assisted research summary: A person who does any of the listed prohibited crop-handling acts commits an offence and, on conviction, is liable to a fine, imprisonment, or both.
16. Mtu ambaye- (a) hataandaa, kupanda, kutunza shamba na mazao kwa usahihi; (b) hatavuna kwa wakati mara baada ya mazao kukomaa; (c) atachelewa kuondoa mazao shambani baada ya kuvuna; (d) ataanika mazao kwenye udongo, vumbi au mchanga; (e) atakausha mazao katika mazingira yanayoweza kusababisha sumukuvu; (f) atatumia viuatilifu vilivyozuiliwa kutumika yenye viashiria vya kwenye mazao; (g) atauza mazao sumukuvu; (h) atasafirisha njia mazao zitakazosababisha mazingira ya kuvu kuota; (i) atatumia mazao yenye viashiria vya kwa sumukuvu wakati wa usindikaji; au (j) atatenda jambo Sheria Ndogo hii, lolote lililokatazwa na anatenda kosa na akitiwa hatiani atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi elfu hamsini na isiyozidi shilingi laki tatu au kifungo kisichozidi miezi kumi na mbili au vyote. - 17 Verify source ↗
Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa na kumtoza mtenda kosa kiasi cha shilingi 50,000 ikiwa mkosaji anakiri kosa na yuko tayari kujaza fomu maalumu ya Jedwali la Pili.
17. Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha kosa kwa kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa kinyume cha Sheria Ndogo hii kiasi cha shilingi elfu hamsini endapo mkosaji atakiri kosa na kuwa tayari kujaza fomu maalumu iliyoainishwa katika Jedwali la Pili. Kufifilisha kosa 6 Sheria Ndogo ya kuzuia na kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Tangazo la Serikali Na. 514 (Linaendelea) _____________ JEDWALI LA KWANZA _____________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 14) Aina ya Mazao Na.
Part
JEDWALI LA KWANZA
- 1 Verify source ↗
Section 1
AI-assisted research summary: This text refers to maize grains and signs of moisture or mold.
1. Mahindi Punje kuwa na unyevu VIASHIRIA VYA SUMUKUVU Hali ya Unyevu au Kuvu - 2 Verify source ↗
Section 2
AI-assisted research summary: Fomu hii inaonyesha mtu anakiri kwa hiari yake mbele ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo kwamba ametenda kosa la kukiuka kanuni na yuko tayari kulipa kiasi cha fedha kwa ajili ya kufifilisha kosa pamoja na faini.
2. Karanga Punje kuwa na unyevu Mwonekano wa Punje Punje kuwa na ukungu au kuvu; rangi ya kahawia, kuwa na nyeusi, kijani au njano; au kuwa na harufu ya uvundo. Punje kuwa na ukungu au kuvu; rangi ya kahawia, nyeusi, kijani au njano; na kuwa na harufu ya uvundo. ____________ JEDWALI LA PILI _____________ FOMU YA KUKIRI NA KUFILILISHA KOSA (Limetemgenezwa chini ya kanuni ya 17) Mimi…...........................……..............……................... nakiri kwa hiari yangu mwenyewe mbele ya........……………............……................... ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo, kwamba mnamo tarehe ….....… ya mwezi ……. Mwaka ….......… nilitenda kosa la kukiuka masharti ya kanuni ya ….....… ya Sheria Ndogo ya Kuzuia na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Gairo ya Mwaka 2024. Kwa Mamlaka aliyopewa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Gairo, niko tayari kulipa kiasi cha Shilingi…………...........… kwa ajili ya kufifilisha kosa nililotenda kinyume cha Sheria Ndogo ya Kuzuia na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Gairo ya Mwaka 2024 ninayodaiwa pamoja na faini. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA MIMI MWENYEWE KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU Leo tarehe…………. Jina……………………………….. ya Mwezi…………..… Mwaka ……………. Saini……………………… MBELE YANGU: Jina:......……………………………………..…………………… Saini:………………………….…………………………..……… Wadhifa: ………………………………………………………… Tarehe:……………………………………………………………. 7 Sheria Ndogo ya kuzuia na kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Gairo Tangazo la Serikali Na. 514 (Linaendelea) Lakiri ya Halmashuri ya Wilaya ya Gairo imegongwa kwenye Sheria ndogo hii kufuatia Azimio lililopitishwa katika Mkutano wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Gairo uliofanyika tarehe 03 Mwezi Disemba 2022 na kushuhudiwa lakari hiyo ikigongwa mbele ya ; SHARIFA YUSUF NABALANG’ANYA Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Gairo RACHEL GODWINI NYANGASI Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya Gairo NAKUBALI, L.S Dodoma. MOHAMED OMARY MCHENGERWA (MB) 15 Mei, 2024 Waziri wa Nchi – Ofisi ya Rais (Tawala za Mikoa na Serikali za mitaa) 8
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Kuzuia na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Gairo ya Mwaka 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in