3. Katika Kanuni hizi, isipokuwa kama muktadha unahitaji vinginevyo- “Sheria” maana yake ni Sheria ya Umeme; “mshirika” maana yake ni chombo chochote cha kisheria chenye hisa kwa mmiliki wa leseni au chombo cha kisheria kingine ambacho mmiliki wa leseni ni mbia; "kiashiria" maana yake ni mfumo unaosikika au unaoonekana unaompa tahadhali mwendeshaji wa chumba cha udhibiti kuwa kifaa, au mfumo wa uendeshaji una kasoro na ni hatari kulingana na vigezo vya usalama; “Mamlaka” maana yake ni Mamlaka ya Kudhibiti Huduma za Nishati na Maji iliyoanzishwa chini ya Sheria ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji; "biashara ya umeme nje ya mipaka ya nchi" maana yake ni biashara ya umeme kati ya nchi mbili zinazopakana 6 Kanuni za Shughuli za Uzalishaji, Usafirishaji Na Usambazaji Umeme Tangazo la Serikali Na. 679 (Linaendelea) kupitia kiunganishi cha umeme, au biashara kati ya nchi mbili zisizokuwa na mipaka ya pamoja, lakini zinaunganishwa kupitia mtandao wa umeme unaohusisha usafirishaji wa nishati ya umeme kati ya nchi husika; “leseni ya kufanya biashara ya umeme nje ya mipaka ya nchi” maana yake ni leseni inayotolewa na Mamlaka la kumuwezesha kufanya lengo kwa mtu kwa biashara ya umeme nje ya mipaka ya nchi; “chumba cha udhibiti” maana yake ni kituo cha uendeshaji chenye wafanyakazi wenye jukumu la kufuatilia na kudhibiti mfumo wote au vitengo vingi vya miundombinu ya umeme; "mwendeshaji wa chumba cha udhibiti " maana yake ni mtu mwenye sifa stahiki mwenye jukumu la kufuatilia na kudhibiti usalama wa mfumo wote au vitengo vingi vya miundombinu ya umeme kupitia SCADA iliyofungwa ndani ya chumba cha udhibiti na ambaye ana mamlaka ya uendeshaji na anawajibika na majukumu ya kila siku ya kufuatilia uendeshaji wa miundombinu ya umeme kama itakavyoelekezwa na mmiliki wa leseni; “mteja” maana yake ni mtu anayepokea au anayenunua huduma zinazodhibitiwa kutoka kwa mmiliki wa leseni; “kanuni za usambazaji” maana yake ni kanuni na viwango vya kiufundi na kiutaratibu vinavyotolewa na Mamlaka vinavyosimamia masuala yanayohusu usambazaji wa umeme; “leseni ya usambazaji” maana yake ni kibali kinachotolewa na Mamlaka kwa ajili ya kuendesha mtandao wa usambazaji; “mmiliki wa leseni ya usambazaji” maana yake ni mtu leseni ya kuendesha mtandao wa aliyepewa usambazaji na Mamlaka na inajumuisha mtu iliyesamehewa kuwa na leseni ya usambazaji kwa mujibu wa kifungu cha 18 cha Sheria; “mtandao wa usambazaji” maana yake ni miundombinu na vifaa vya mmiliki wa leseni ya usambazaji vilivyoundwa kwa ajili ya kusambaza umeme usiozidi msongo wa kilovolti 33 ambayo inajumuisha njia za 7 Kanuni za Shughuli za Uzalishaji, Usafirishaji Na Usambazaji Umeme Tangazo la Serikali Na. 679 (Linaendelea) juu, nyaya za ardhini, mashine umba, vituo vya udhibiti na vifaa vya kupima matumizi umeme; “mteja maalum” maana yake ni mtu yeyote aliyeidhinishwa na Mamlaka kwa mujibu wa kanuni hizi kuingia katika mkataba wa kununua umeme moja kwa moja kutoka kwa mmiliki wa leseni ya uzalishaji; “kituo” maana yake ni eneo au miundombinu ya umeme inakidhi viwango vya kimataifa iliyojengwa na ikijumuisha usafirishaji, usambazaji na mfumo wa kushughulikia majanga ya moto wakati shughuli inayodhibitiwa inatekelezwa; uzalishaji umeme, “kituo cha vifaa vya uzalishaji” maana yake ni majengo, vifaa vya kuzalisha umeme ikiwa ni pamoja na vifaa saidizi, mashine-umba, vifaa vya kushughulikia mafuta, mtambo wa kubadilishia umeme na kiunganishia umeme ambavyo ni muhimu kwa shughuli za kuzalisha umeme kama zitakavyoelezwa kwenye leseni ya kuzalisha umeme; “uzalishaji kwa matumizi binafsi” maana yake ni kuzalisha umeme ambao wote utatumiwa na mmiliki wa leseni pasipo kusambaza kwa mtu mwingine; “leseni ya uzalishaji” maana yake ni kibali kinachotolewa na Mamlaka kwa ajili ya shughuli za uzalishaji; “mmiliki wa leseni ya uzalishaji” maana yake ni mtu aliyepewa leseni na Mamlaka kwa ajili ya kutoa huduma za uzalishaji na inajumuisha mtu yeyote aliyesamehewa kupata leseni ya uzalishaji kwa mujibu wa kifungu cha 18 cha Sheria; “huduma za uzalishaji” maana yake ni huduma za uzalishaji umeme ikiwa ni pamoja na kuzalisha umeme kwa matumizi binafsi na maneno “shughuli ya kuzalisha umeme” yatatafsiriwa kwa namna hiyo; “kanuni za gridi” maana yake ni kanuni na viwango vya kiufundi na kiutaratibu vinavyotolewa na Mamlaka kwa ajili ya usafirishaji na uendeshaji wa mfumo; “mkaguzi” maana yake ni afisa wa Mamlaka au wakala aliyeteuliwa na Mamlaka kwa mujibu wa kifungu cha 31(2) cha Sheria kuwa mkaguzi; "kituo cha kuunganisha" maana yake ni kituo ambacho kinapokea umeme kutoka katika kituo cha uzalishaji na kuingiza kwenye njia za usambazaji au usafirishaji 8 Kanuni za Shughuli za Uzalishaji, Usafirishaji Na Usambazaji Umeme Tangazo la Serikali Na. 679 (Linaendelea) wa umeme; "barua ya kuonesha nia " maana yake ni andiko la nia kutoka kwa mmiliki was leseni ya usambazaji ya kuridhia kuunganisha na kununua umeme wa mpaka megawati 10 utakaozalishwa na mwekezaji; “leseni” maana yake ni leseni ya biashara ya umeme nje ya mipaka ya nchi, leseni ya uzalishaji, leseni ya usafirishaji umeme au leseni ya usambazaji umeme iliyotolewa na Mamlaka; “mmiliki wa leseni” maana yake ni mmiliki wa leseni ya biashara ya umeme nje ya mipaka ya nchi, leseni ya uzalishaji umeme, leseni ya usafirishaji umeme au leseni ya usambazaji umeme; "kituo kilichopewa leseni" maana yake ni majengo na vifaa vya kuzalisha, kusafirisha au kusambaza nishati ya umeme ikijumuisha vifaa visaidizi, mashine umba, vifaa vya kutunzia mafuta, sehemu ya kuzima na kuwasha umeme na viunganishi ambavyo ni muhimu kwa ajili ya kutekeleza shughuli inayodhibitiwa kama ilivyoainishwa katika leseni husika; “mamlaka ya serikali ya mtaa” maana yake ni mamlaka ya wilaya, mamlaka ya miji, mamlaka ya kata au mamlaka ya kijiji iliyoanzishwa chini ya Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) na Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji); “Waziri” maana yake ni Waziri mwenye dhamana na masuala ya umeme; “mkataba wa ununuzi wa umeme” maana yake ni mkataba wa kuuza au kununua umeme ulioingiwa kati ya mmiliki wa leseni ya uzalishaji na mtu mwingine yeyote; “leseni ya muda mfupi” maana yake ni kibali kinachotolewa na Mamlaka kumruhusu mwombaji kufanya matayarisho ya shughuli mbalimbali kama uchunguzi, utafiti na shughuli nyingine muhimu kwa ajili ya kuomba leseni; “Matendo Bora ya Utoaji Huduma" ina maana ya matendo mazuri na bora, mbinu na utaratibu ambao unapatikana kwa kutumia ujuzi, bidii, busara na kubashiri yaliyo mbeleni ambayo kwa kawaida yanatarajiwa kupatikana kutoka kwa mtaalam 9 Sura ya 287 na 288 Sura za 287 na 288 Kanuni za Shughuli za Uzalishaji, Usafirishaji Na Usambazaji Umeme Tangazo la Serikali Na. 679 (Linaendelea) mbobezi wa kimataifa anayefanya kazi hizo au shughuli inayofanana na inayodhibitiwa ndani ya Tanzania na ambayo iko chini ya mazingira yanayofanana na yanakidhi matakwa ya kitaifa na kimataifa ya kiafya, usalama na mazingira; “shughuli inayodhibitiwa” maana yake ni biashara ya umeme nje ya mipaka ya nchi, shughuli ya uzalishaji umeme, usafirishaji umeme au usambazaji umeme na maneno “huduma inayodhibitiwa” yatatafsiriwa kwa namna hiyo; “taarifa za fedha za kiudhibiti” maana yake ni kumbukumbu za fedha au taarifa zilizotayarishwa na kuwasilishwa kwa Mamlaka na inayodhibitiwa kama taasisi ilivyoainishwa katika mwongozo wa utoaji taarifa za fedha za taasisi zinazodhibitiwa; “SCADA” maana yake ni mfumo unaotumia kompyuta au mfumo ambao unakusanya na kuonesha taarifa kuhusu miundombinu ya umeme na una uwezo wa kutuma maagizo kwenda kwenye miundombinu ya umeme au mfumo ambao unajumuisha vifaa vya kompyuta na programu inayotumiwa kupeleka maagizo na kupata takwimu kwa madhumuni ya kufuatilia na kudhibiti miundominu ya umeme; "eneo" maana yake ni sehemu ambayo miundombinu ya uzalishaji imewekwa na maelezo yake yatatolewa kwenye leseni; “mradi mdogo wa umeme” maana yake ni kituo cha kuzalisha umeme kwa kutumia nishati jadidifu au joto la ziada au mchanagnyiko wa vyote isiyozidii Megawati 10; “bei” maana yake ni tozo yoyote, ada, au kiasi kwa madhumuni ya kununua huduma kama itakavyoidhinishwa na Mamlaka; inayodhibitiwa “leseni ya usafirishaji” maana yake ni kibali kinachotolewa na Mamlaka kwa mmiliki wa leseni kwa ajili ya kuendesha mtandao wa usafirishaji; “mbinu ya upangaji bei” maana yake ni njia inayotumika kupanga bei kama ilivyoidhinishwa na Mamlaka; “leseni ya usafirishaji” maana yake ni kibali kinachotolewa na Mamlaka kwa ajili ya kuendesha mtandao wa usafirishaji; 10 Kanuni za Shughuli za Uzalishaji, Usafirishaji Na Usambazaji Umeme Tangazo la Serikali Na. 679 (Linaendelea) “mmiliki wa leseni ya usafirishaji” maana yake ni mtu aliyepewa leseni na Mamlaka kwa ajili ya kuendesha mtandao wa usafirishaji na inajumuisha mtu yeyote aliyesamehewa kupata leseni ya usafirishaji kwa mujibu wa kifungu cha 18 cha Sheria; "mtandao wa usafirishaji" maana yake ni mkusanyiko wa vifaa na miundombinu ya umeme inayomilikiwa na mwenye leseni ya upelekaji umeme katika masafa ya hazi 50 (50Hz) kwa njia ya msongo wa juu wa kilovolti 66 au zaidi, ikijumuisha nyaya za juu, chini ya ardhi, chini ya maji, mashine umba, mtandao wa mawasiliano, vituo vya udhibiti na vifaa vya kupimia umeme; Wajibu wa kuomba leseni Utaratibu wa maombi ya leseni “Mkataba wa kusafirisha umeme” maana yake ni mkataba wa chanzo usafirishaji kilichounganishwa kwenye gridi ya umeme hadi kwa mtumiaji ndani ya gridi; na umeme kutoka katika “Msimamizi” maana yake ni mtu mwenye sifa za kufanya shughuli za ufilisi wa makampuni. SEHEMU YA PILI UTARATIBU WA KUOMBA LESENI