SHERIA NDOGO ZA ADA NA USHURU WA MADINI YA UJENZI ZA HALMASHAURI YA WILAYA YA PANGANI ZA MWAKA 2024
This provision gives the by-law its name: the Pangani District Council Construction Minerals Fees and Levies By-Laws, 2024.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- SHERIA NDOGO ZA ADA NA USHURU WA MADINI YA UJENZI ZA HALMASHAURI YA WILAYA YA PANGANI ZA MWAKA 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This provision gives the by-law its name: the Pangani District Council Construction Minerals Fees and Levies By-Laws, 2024. This section defines key terms used in the by-laws, including fees, permits, designated officers, the council, construction minerals, prohibited areas, the director, levy, and agent. Halmashauri must receive and inspect information about areas planned for construction mineral quarries, and supervise extraction to ensure it follows the law and procedures. An applicant for a building-minerals quarry permit must file the application with the Director using the Council’s prescribed form, and the Director must inspect the site within 7 days and explain any refusal. Halmashauri inaweza kufunga machimbo ya madini ya ujenzi ikiwa itaona ni kwa maslahi yake na ya umma.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of SHERIA NDOGO ZA ADA NA USHURU WA MADINI YA UJENZI ZA HALMASHAURI YA WILAYA YA PANGANI ZA MWAKA 2024
Showing 17 of 17
- 1 Verify source ↗
Sheria ndogo hizi zitajulikana kama Sheria
AI-assisted research summary: This provision gives the by-law its name: the Pangani District Council Construction Minerals Fees and Levies By-Laws, 2024.
1. Sheria ndogo hizi zitajulikana kama Sheria ndogo za Ada na Ushuru wa Madini ya Ujenzi za Halmashauri ya Wilaya ya Pangani za Mwaka 2024. - 2 Verify source ↗
Katika Sheria ndogo hizi, isipokuwa kama
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the by-laws, including fees, permits, designated officers, the council, construction minerals, prohibited areas, the director, levy, and agent.
2. Katika Sheria ndogo hizi, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “ada” maana yake ni malipo yatakayolipwa na mtu yeyote kwa Halmashauri kwa ajili ya kupata kibali kinachotolewa na Halmashauri kwa mujibu wa Sheria ndogo hizi; “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni Afisa yeyote la aliyeteuliwa na Mkurugenzi kwa kusimamia utekelezaji wa Sheria ndogo hizi; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya lengo Pangani; “kibali” maana yake ni idhini au ruhusa ya maandishi inayotolewa kwa mujibu wa Sheria ndogo hizi; “madini ya ujenzi” maana yake ni tarazo, moramu, udongo, kifusi, kokoto, mawe, mchanga, chokaa na madini mengine yanayotumika katika ujenzi; “maeneo yasiyoruhusiwa” maana yake ni maeneo ya mito, madaraja, barabara, mashamba ya watu, mijini pamoja na maeneo mengine yanayofanana na hayo; 1 Sheria Ndogo za Ada Na Ushuru wa Madini ya Ujenzi za Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Tangazo la Serikali Na. 699 (Linaendelea) “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani na ni pamoja na Afisa yeyote atakayeteuliwa kutekeleza majukumu kwa niaba ya Mkurugenzi; “ushuru” maana yake ni tozo inayotozwa na Halmashauri kwa shughuli zinazohusu ununuzi wa madini ya ujenzi katika eneo la Halmashauri; na “Wakala” maana yake mtu, taasisi, kikundi cha watu, kampuni au asasi iliyoteuliwa na Halmashauri kukusanya ushuru wa madini ya ujenzi kwa niaba yake. Wajibu wa Halmashauri Maombi ya kibali cha uchimbaji - 3 Verify source ↗
(1) Halmashauri itakuwa na wajibu wa kupokea
AI-assisted research summary: Halmashauri must receive and inspect information about areas planned for construction mineral quarries, and supervise extraction to ensure it follows the law and procedures.
3.-(1) Halmashauri itakuwa na wajibu wa kupokea taarifa za maeneo yote yanayokusudiwa kuanzishwa machimbo ya madini ya ujenzi na kuyakagua ili taarifa kujiridhisha yametengwa kwa ajili ya uchimbaji wa madini ya ujenzi. kama maeneo yaliyotolewa (2) Kusimamia shughuli za uchimbaji wa madini ya ujenzi ili kuhakikisha kuwa uchimbaji unafanyika kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa ili kuzuia uharibifu wa mazingira. - 4 Verify source ↗
(1) Mtu,
AI-assisted research summary: An applicant for a building-minerals quarry permit must file the application with the Director using the Council’s prescribed form, and the Director must inspect the site within 7 days and explain any refusal.
4.-(1) Mtu, taasisi au kampuni inayokusudia kuanzisha machimbo ya madini ya ujenzi katika eneo la Halmashauri itatakiwa kuwasilisha kwa Mkurugenzi maombi ya kibali cha uchimbaji wa madini ya ujenzi kupitia fomu maalumu itakayotolewa na Halmashauri kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Kwanza. (2) Maombi ya kibali yatakayowasilishwa Halmashauri yataambatana na taarifa zifuatazo: (a) leseni ya uchimbaji wa madini iliyotolewa na mamlaka husika; (b) aina ya madini yanayokusudiwa kuchimbwa; (c) umiliki pamoja na ukubwa wa eneo linalokusudiwa kuchimbwa madini ya ujenzi; (d) mpango wa utunzaji wa mazingira katika eneo la machimbo; na (e) muhtasari wa kijiji ambacho uchimbaji wa madini ya ujenzi utafanyika ukionyesha 2 Sheria Ndogo za Ada Na Ushuru wa Madini ya Ujenzi za Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Tangazo la Serikali Na. 699 (Linaendelea) Uwezo wa kufunga machimbo Ushuru wa Madini ya ujenzi kukubaliana na uchimbaji huo. (3) Mkurugenzi, ndani ya muda wa siku saba baada ya kupokea maombi ya uchimbaji wa madini ya ujenzi atatakiwa kukagua eneo ambalo uchimbaji unaokusudiwa kufanyika ili kujiridhisha iwapo eneo hilo la madini litafaa kwa shughuli za uchimbaji wa madini, na halitakuwa na atahari za kimazingira. (4) Mkurugenzi, ndani ya muda wa siku saba baada ya kukamilika kwa ukaguzi wa eneo linaloombewa kibali anaweza kukubali au kukataa maombi hayo na kama atakataa atatakiwa kutoa sababu za kukataa maombi hayo. (5) Kibali kitakachotolewa chini ya Sheria ndogo hizi kitaeleza aina ya madini yanayochimbwa na eneo litakalochimbwa madini hayo na kitalipiwa ada kama kilivyoainishwa katika Jedwali la Pili. - 5 Verify source ↗
Halmashauri itakuwa na uwezo wa kufunga
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kufunga machimbo ya madini ya ujenzi ikiwa itaona ni kwa maslahi yake na ya umma.
5. Halmashauri itakuwa na uwezo wa kufunga machimbo yoyote ya madini ya ujenzi kama itaona kufanya hivyo ni kwa maslahi ya Halmashauri na umma kwa ujumla. - 6 Verify source ↗
(1) Mtu atakayesafirisha madini ya ujenzi
AI-assisted research summary: Mtu anayesafirisha madini ya ujenzi lazima alipie ushuru kwa tani; ushuru unakuwa unaanza baada ya kununua au kupakia madini, hulipwa kwa Halmashauri au Wakala, na mlipaji anatakiwa kudai risiti.
6.-(1) Mtu atakayesafirisha madini ya ujenzi kutoka eneo yalikochimbwa kwenda maeneo mengine atalipa ushuru kwa tani kulingana na viwango vilivyoainishwa katika Jedwali la Tatu. (2) Ushuru huo utatozwa mara baada ya msafirishaji kununua madini kutoka kwa mchimbaji au kupakia madini hayo katika chombo ambacho atakitumia kwa ajili ya kusafirishia. (3) Ushuru wa madini ya ujenzi utatozwa katika eneo la machimbo, barabara zinazoelekea au kutoka maeneo ya machimbo au eneo lolote lililo chini ya mamlaka ya Halmashauri. (4) Mnunuzi yeyote atakayeshindwa kulipa ushuru anaotakiwa kulipa atatakiwa kupakua madini ya ujenzi kutoka katika chombo au kutochukua madini hayo mpaka hapo atakapolipa ushuru anaodaiwa. 3 Sheria Ndogo za Ada Na Ushuru wa Madini ya Ujenzi za Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Tangazo la Serikali Na. 699 (Linaendelea) (5) Halmashauri itakuwa na uwezo wa kumzuia dereva au gari lolote kujishughulisha na usafirishaji wa madini ya ujenzi ikithibitika kwamba kuna ukiukwaji na uvunjaji wa Sheria ndogo hizi. (6) Ushuru wa madini ya ujenzi utalipwa kwa Halmashauri au Wakala ambaye atatoa stakabadhi ya kielektroniki kama kielelezo cha malipo hayo. (7) Itakuwa ni wajibu wa kila mtu aliyelipa ushuru kudai risiti na haitakuwa utetezi kwa mtu yeyote kudai kuwa amelipa ushuru lakini hakupewa risiti. - 7 Verify source ↗
(1) Shughuli za uchimbaji, uuzaji na ununuzi wa
AI-assisted research summary: Shughuli za uchimbaji, uuzaji na ununuzi wa madini ya ujenzi katika eneo la Halmashauri zifanyike kila siku kati ya saa kumi na mbili asubuhi na saa kumi na mbili jioni; Mkurugenzi anaweza kutoa kibali maalumu cha kufanya kazi nje ya muda huo; na mmiliki wa gari linalosafirisha madini ya ujenzi lazima ahakikishe gari limefunikwa wakati wote wa usafirishaji.
7.-(1) Shughuli za uchimbaji, uuzaji na ununuzi wa madini ya ujenzi katika eneo la Halmashauri zitafanyika kuanzia saa kumi na mbili asubuhi hadi saa kumi na mbili jioni ya kila siku. (2) Bila kujali masharti ya kanuni ndogo ya (1), Mkurugenzi anaweza kutoa kibali maalumu kuruhusu shughuli za uchimbaji, uuzaji na ununuzi wa madini ya ujenzi kufanyika nje ya muda ulioainishwa katika kanuni ndogo ya (1). (3) Kila mmiliki wa gari linalosafirisha madini ya ujenzi atatakiwa kuhakikisha kuwa gari hilo limefunikwa wakati wote wa usafirishaji wa madini ya ujenzi ili kuzuia uharibifu na uchafuzi wa mazingira. - 8 Verify source ↗
(1) Kutakuwa na vituo kwa ajili ya ukaguzi wa
AI-assisted research summary: Vituo vya ukaguzi vinapaswa kuwepo kwa magari yanayobeba madini ya ujenzi, na kila dereva anatakiwa kusimama kituoni na kuonyesha stakabadhi ya kielektroniki ya ushuru; asiye nayo atalipa ushuru kwa viwango vilivyoainishwa.
8.-(1) Kutakuwa na vituo kwa ajili ya ukaguzi wa magari yanayobeba madini ya ujenzi katika njia zinazoingia na kutoka katika maeneo ya machimbo. (2) Itakuwa ni wajibu wa kila dereva kusimama katika kituo cha ukaguzi wa madini ya ujenzi na kuonesha ikiwa stakabadhi ya kielektroniki aliyolipia ushuru, hatakuwa na stakabadhi hiyo atatakiwa kulipa ushuru kwa viwango vilivyoainishwa na Sheria ndogo hizi. Muda wa uchimbaji, uuzaji, na ununuzi Vituo vya ukaguzi Halmashauri kutowajibika kwa hasara - 9 Verify source ↗
Halmashauri haitawajibika kwa hasara yoyote
AI-assisted research summary: Halmashauri siyo yenye kuwajibika kwa hasara ya mnunuzi au msafirishaji wa madini ya ujenzi wakati wa kukusanya ushuru, isipokuwa hasara hiyo ikitokana na uzembe wa afisa.
9. Halmashauri haitawajibika kwa hasara yoyote atakayopata mnunuzi au msafirishaji wa madini ya ujenzi wakati wa kukusanya ushuru isipokuwa kama hasara hiyo itatokana na uzembe uliosababishwa na afisa yeyote wa 4 Sheria Ndogo za Ada Na Ushuru wa Madini ya Ujenzi za Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Tangazo la Serikali Na. 699 (Linaendelea) Uwezo wa Afisa Mwidhiniwa Wakala Kufutwa au kusimamishwa kwa kibali Halmashauri. - 10 Verify source ↗
Bila kuathiri masharti ya Sheria ndogo hizi
AI-assisted research summary: Afisa Mwidhiniwa ana uwezo wa kuingia katika eneo lolote linalochimbwa madini ya ujenzi wakati wa saa za kazi ili kukagua na kukusanya ushuru.
10. Bila kuathiri masharti ya Sheria ndogo hizi Afisa Mwidhiniwa atakuwa na uwezo wa kuingia katika eneo lolote linalochimbwa madini ya ujenzi muda wa saa za kazi kwa ajili ya kukagua na kukusanya ushuru. - 11 Verify source ↗
Halmashauri inaweza kuteua mtu, kikundi cha
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kumteua mtu, kikundi cha watu, taasisi au kampuni kuwa wakala wa kukusanya ushuru kwa niaba yake.
11. Halmashauri inaweza kuteua mtu, kikundi cha watu, taasisi au kampuni kuwa Wakala wa kukusanya ushuru kwa niaba yake. - 12 Verify source ↗
(1) Halmashauri
AI-assisted research summary: The Council may suspend or cancel a building-materials mining permit if it is satisfied there has been a breach of the by-laws or permit conditions.
12.-(1) Halmashauri au kusimamisha kibali cha uchimbaji wa madini ya ujenzi iwapo itajiridhisha kuwa kuna ukiukwaji wa masharti ya Sheria ndogo hizi au masharti ya kibali cha uchimbaji wa madini ya ujenzi. inaweza kufuta (2) Kwa kuzingatia masharti ya kanuni ndogo ya (1), Halmashauri kabla ya kufuta au kusimamisha kibali itatakiwa kutoa notisi ya siku saba kwa mtu, taasisi au kampuni iliyopewa kibali cha kusudio la kufuta au kusimamisha kibali. (3) Notisi itakayotolewa kwa mujibu wa kanuni ndogo ya (1) itaainisha sababu za kufuta au kusimamisha kibali husika. (4) Endapo kibali kitafutwa au kusimamishwa, mtu, taasisi au kampuni iliyopewa kibali cha uchimbaji wa madini ya ujenzi itakoma kuchimba madini hayo. Matumizi ya stakabadhi ya kielektroniki - 13 Verify source ↗
Halmashauri au Wakala atatakiwa kutoza ada
AI-assisted research summary: Halmashauri au Wakala lazima kutoza ada au ushuru kwa kutumia mashine za kielektroniki.
13. Halmashauri au Wakala atatakiwa kutoza ada au ushuru kwa kadri itakavyokuwa kwa kutumia mashine za kielektroniki. Makosa na adhabu - 14 Verify source ↗
Mtu ambaye
AI-assisted research summary: A person who disobeys an authorised officer, interferes with that officer, evades mining fees, mines without permission, or transports construction minerals contrary to the rules commits an offence and may be fined or jailed.
14. Mtu ambaye- (a) atakataa au kushindwa kutii agizo atakalopewa na Afisa Mwidhiniwa; lolote (b) atamzuia Afisa Mwidhiniwa kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria ndogo hizi; (c) atakataa au kujaribu kukataa kulipa ushuru; 5 Sheria Ndogo za Ada Na Ushuru wa Madini ya Ujenzi za Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Tangazo la Serikali Na. 699 (Linaendelea) (d) atashawishi mtu au kundi la watu kukataa kulipa ushuru; (e) atakwepa au atajaribu kukwepa kulipa ushuru; (f) atachimba madini ya ujenzi katika maeneo yasiyoidhinishwa; (g) atachimba madini katika eneo lisiloruhusiwa na Halmashauri hasa maeneo ya barabara na maeneo ya hifadhi; (h) ataanzisha machimbo ya madini ya ujenzi bila kuwa na kibali kutoka Halmashauri; (i) atapeleka maombi ya leseni ya madini ya ujenzi Wizara ya Madini bila kujadiliwa na kuridhiwa na kijiji husika na kupitishwa na Halmashauri; (j) atasafirisha madini ya ujenzi bila kulipa ushuru; (k) atachimba madini ya ujenzi kabla au baada ya muda ulioruhusiwa kuchimba; au (l) atasafirisha madini ya ujenzi katika gari ambalo halijafunikwa, anatenda kosa na akitiwa na hatiani atatozwa faini isiyopungua shilingi laki mbili na isiyozidi shilingi milioni moja au kifungo kisichopungua miezi kumi na mbili na kisichozidi miezi ishirini na nne au vyote kwa pamoja. Kufifilisha kosa - 15 Verify source ↗
Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa kwa
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa kwa kumtoza mhalifu shilingi 200,000 ikiwa anakiri kosa kwa hiari na yuko tayari kujaza fomu maalumu ya Jedwali la Nne.
15. Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa kwa kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa kwa mujibu wa Sheria ndogo hizi kiasi cha shilingi laki mbili iwapo mkosaji atakiri kosa kwa hiari na kuwa tayari kujaza fomu maalumu iliyoainishwa katika Jedwali la Nne. 6 Sheria Ndogo za Ada Na Ushuru wa Madini ya Ujenzi za Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Tangazo la Serikali Na. 699 (Linaendelea) _______________ JEDWALI LA KWANZA ________________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 4(1)) KIBALI CHA KUCHIMBA MADINI YA UJENZI NDUGU; ……………………………………………………..… S.L.P……………………………………….……………………. PANGANI………………………………….………………….... Yah: KIBALI CHA KUCHIMBA MADINI YA UJENZI ni ajili hiki kwa Kibali Kibali kinatolewa kwa ajili ya kufanya shughuli hiyo kama ulivyoomba kwa mujibu wa Sheria. kuchimba ……………..………………………………………………………………………. (mawe, mchanga, kokoto, kifusi, udongo, madini mengine). Katika eneo la shamba/kiwanja cha lililopo/kilichopo ……………………………….Kata ya…………….………………... Halmashauri ya Wilaya ya Pangani. Kibali hiki kitatumika kuanzia tarehe ………............………….. hadi tarehe ………………………………. na kwamba kibali hiki kitatumika katika eneo lililoainishwa tu katika kibali hiki. Kibali hiki kinatolewa kwa wamiliki au watu/kampuni walioingia mkataba na mmiliki/wamiliki wa eneo linaloombewa kibali. cha …………………………. Kitongoji Kijiji ya MAONI YA AFISA MAZINGIRA Kibali kitolewe/kisitolewe, kwani tathmini ya mazingira imefanyika/haijafanyika na imebaini kutakuwa/hakutakuwa na uharibifu wa Mazingira. Jina: ………………………...............…………………………….. Cheo: …………………...............………………………………… Saini: …………………...............………………………………… Tarehe: ………………….................……………………………… MAONI YA AFISA MIPANGO MIJI Kibali kitolewe/kisitolewe, kwani uchimbaji kwenye eneo hilo mpango wa matumizi yake utaathiri/hautaathiri upangaji miji. Jina: ………………..............……………….…………………….. Cheo: ……………………..............………….…………………… Saini: …………………………………...............………………… Tarehe: …………………………………................……………… (N.B) kibali kijazwe nakala mbili moja apatiwe msafirishaji na nyingine iwasilishwe kwa Mkurugenzi Mtendaji (W). 7 Sheria Ndogo za Ada Na Ushuru wa Madini ya Ujenzi za Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Tangazo la Serikali Na. 699 (Linaendelea) ___________ JEDWALI LA PILI ___________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 4(5)) ADA YA KIBALI CHA UCHIMBAJI WA MADINI YA UJENZI NA
Part
JEDWALI LA PILI
- 1 Verify source ↗
Section 1
AI-assisted research summary: Ada ya kibali cha kumiliki eneo la kuchimba madini ya ujenzi ni 1,000,000/= kwa kila kibali.
1. AINA YA MADINI KIWANGO (SHILINGI) Ada ya kibali cha kumiliki eneo la kuchimba madini ya ujenzi 1,000,000/= kwa kila kibali ___________ JEDWALI LA TATU __________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 6(1)) USHURU WA MADINI YA UJENZI AINA YA MADINI NA Tarazo
Part
JEDWALI LA TATU
- 9 Verify source ↗
Makinikia/concentrate
AI-assisted research summary: Section 9 shows a fee/rate schedule for makinikia/concentrate, expressed in shillings per ton.
9. Makinikia/concentrate KIWANGO (SHILINGI) 5,000/= kwa tani 5,000/= Kwa tani 4,000/= kwa tani 6,000/= kwa tani 4,000/= kwa tani 4,000/= kwa tani 6,000/= kwa tani 6,000/= kwa tani 10,000/= kwa tani __________ JEDWALI LA NNE ________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 15) HATI YA KUFIFILISHA KOSA Mimi …………………………………nakiri ya kwa …………………………………… ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani, kwamba, mnamo tarehe ……..… ya mwezi …………. mwaka ……………… nilitenda kosa la kukiuka masharti ya kanuni ya …………….……….…… ya Sheria ndogo za Ada na Ushuru wa Madini ya Ujenzi za Halmashauri ya Wilaya ya Pangani za Mwaka 2024. yangu mwenyewe mbele hiari 8 Sheria Ndogo za Ada Na Ushuru wa Madini ya Ujenzi za Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Tangazo la Serikali Na. 699 (Linaendelea) Kwa mamlaka aliyopewa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani, niko tayari kulipa kiasi cha ada au ushuru na faini nitakayokuwa nadaiwa badala ya kupelekwa Mahakamani. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA MIMI MWENYEWE KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU. Leo tarehe…………. Mwezi…………..… Mwaka ……….............…….…………. Jina………………………………..Saini…………………................…………………. MBELE YANGU: Jina: ……………………………………..…………………… Saini; ………………………….…………………………..……… Wadhifa: ………………………………………………………… Tarehe; …………………………………………………………… 9 Sheria Ndogo za Ada Na Ushuru wa Madini ya Ujenzi za Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Tangazo la Serikali Na. 699 (Linaendelea) Muhuri wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Ulibandikwa kwenye Sheria Ndogo hizi kwa kufuatia azimio lililopitishwa kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani uliofanyika mnamo tarehe 29 mwezi 04 Mwaka 2022 mbele ya:- ISAYA MUGISHAGWE MBENJE, Mkurugenzi Mtendaji, Halmashauri ya Wilaya Pangani AKIDA OMARI BAHORERA, Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya Pangani NAKUBALI, L.S Dodoma, MOHAMED OMARY MCHENGERWA, 30 Novemba, 2024 Waziri wa Nchi-or-Tamisemi 10
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
SHERIA NDOGO ZA ADA NA USHURU WA MADINI YA UJENZI ZA HALMASHAURI YA WILAYA YA PANGANI ZA MWAKA 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in