Kanuni za Matumizi ya Mafao ya Mwanachama kama Dhamana ya Mkopo wa Nyumba za Mwaka 2024
This section states the short title of the rules and introduces the interpretation section.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Kanuni za Matumizi ya Mafao ya Mwanachama kama Dhamana ya Mkopo wa Nyumba za Mwaka 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This section states the short title of the rules and introduces the interpretation section. This section defines key terms used in the regulations, including the Board, Division, Fund, contributions, member, eligible member, operating guidelines, housing loan, the Act, and institutions. Mwanachama anaweza kutumia sehemu ya mafao yake kama dhamana kwa mkopo wa nyumba, na Mfuko lazima utoe dhamana moja tu kwa mwanachama anayestahili baada ya maombi rasmi na uhakiki. The collateral value for a home loan is capped by the lower of the member’s eligible benefit amount (up to 50% at application) and the home’s value, with extra limits for incomplete purchases and home improvement loans. A member may qualify for a Fund guarantee only if they are a Tanzanian citizen, are an eligible member, and the guarantee does not exceed the member’s mandatory retirement age.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Kanuni za Matumizi ya Mafao ya Mwanachama kama Dhamana ya Mkopo wa Nyumba za Mwaka 2024
Showing 16 of 16
- 1 Verify source ↗
Jina
AI-assisted research summary: This section states the short title of the rules and introduces the interpretation section.
1. Kanuni hizi zitajulikana kama Kanuni za Matumizi ya Mafao ya Mwanachama kama Dhamana ya Mkopo wa Nyumba za Mwaka 2024. Tafsiri - 2 Verify source ↗
Tafsiri
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the regulations, including the Board, Division, Fund, contributions, member, eligible member, operating guidelines, housing loan, the Act, and institutions.
2. Katika Kanuni hizi, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “Bodi” maana yake ni Bodi ya Wadhamini ya Mfuko; “Divisheni” maana yake ni Divisheni inayohusika na masuala ya hifadhi ya jamii iliyopo ndani ya Wizara yenye dhamana na masuala ya hifadhi ya jamii; “Mfuko” ina maana iliyotolewa kwenye sheria ya mfuko husika; “michango” maana yake ni michango inayolipwa kwenye Mfuko kama ilivyoainishwa kwenye sheria za mifuko ya pensheni; “mwanachama” maana yake ni mwajiriwa au mfanyakazi inajumuisha aliyesajiliwa mwanachama anayestahili, au anayepokea, mafao chini ya skimu; skimu katika na “mwanachama anayestahili” maana yake ni mwanachama ambaye amechangia kwa kipindi kisichopungua 3 Kanuni za Matumizi ya Mafao ya Mwanachama Kama Dhamana ya Mkopo wa Nyumba Tangazo La Serikali Na. 149 (Linaendelea) miezi mia moja themanini ambapo kati ya miezi hiyo, michango ya miezi kumi na mbili ni lazima iwe imechangwa mfululizo kabla ya tarehe ya kutolewa kwa dhamana; “mwongozo wa uendeshaji” maana yake ni nyaraka ya ndani ya Mfuko inayoelekeza namna ya utekelezaji na utoaji wa dhamana za mikopo chini ya Kanuni hizi; “mkopo wa nyumba” maana yake ni mkopo unaotolewa kwa mwanachama anayestahili kwa malengo ya kununua, kujenga au kuboresha nyumba ya makazi ambayo imedhaminiwa na nyumba yenyewe kama dhamana ya kwanza; “Sheria” maana yake ni Sheria ya Hifadhi ya Jamii; “taasisi” maana yake ni mabenki na taasisi nyingine za fedha zilizosajiliwa na kupata leseni chini ya Sheria ya Benki na Taasisi za Fedha. SEHEMU YA PILI DHAMANA Sura ya 135 Sura ya 342 Matumizi ya mafao kama dhamana
Part
SEHEMU YA PILI
- 3 Verify source ↗
Matumizi ya mafao kama dhamana
AI-assisted research summary: Mwanachama anaweza kutumia sehemu ya mafao yake kama dhamana kwa mkopo wa nyumba, na Mfuko lazima utoe dhamana moja tu kwa mwanachama anayestahili baada ya maombi rasmi na uhakiki.
3.-(1) Mwanachama anaweza kuruhusu sehemu ya stahili ya mafao yake kutoka kwenye Mfuko itumike kama dhamana kwa ajili ya kupata mkopo wa nyumba kutoka kwenye taasisi za fedha ili kumwezesha- (a) kujenga nyumba ya makazi kwenye kiwanja anachomiliki kisheria; (b) kununua nyumba ya makazi; au (c) kuboresha, kubadilisha au kufanya ukarabati wa nyumba ambayo mwanachama anamiliki kisheria. (2) Mfuko hautatoa dhamana zaidi ya moja kwa mwanachama anayestahili. (3) Mfuko utatoa dhamana kwa mwanachama baada ya kuwasilisha maombi rasmi kama ilivyoainishwa kwenye mwongozo wa uendeshaji wa Mfuko. 4 Kanuni za Matumizi ya Mafao ya Mwanachama Kama Dhamana ya Mkopo wa Nyumba Tangazo La Serikali Na. 149 (Linaendelea) (4) Mfuko utahakiki maombi ya mwanachama kwa ajili ya kubaini sifa za mwombaji na mwanachana atajulishwa matokeo ya uhakiki huo. Kiwango cha mafao kwa ajili ya dhamana - 4 Verify source ↗
Kiwango cha mafao kwa ajili ya dhamana
AI-assisted research summary: The collateral value for a home loan is capped by the lower of the member’s eligible benefit amount (up to 50% at application) and the home’s value, with extra limits for incomplete purchases and home improvement loans.
4.-(1) Kiwango cha mafao kitakachotolewa kama dhamana ya mkopo wa nyumba kitakuwa- (a) si zaidi ya asilimia hamsini ya kiwango cha mafao anachostahili mwanachama wakati wa maombi; au (b) kiwango cha thamani ya soko ya nyumba hiyo, ambapo kiwango cha chini kati ya viwango vilivyotajwa katika aya (a) na (b) kitachukuliwa. (2) Pale ambapo ununuzi wa nyumba haujakamilika na bei ya ununuzi imekubaliwa na pande zote mbili, thamani ya nyumba hiyo haitakuwa kwa kiwango cha juu kuliko bei ya ununuzi iliyoainishwa na wahusika kwa madhumuni ya ushuru wa stempu. lengo la mkopo ni kuboresha, kubadilisha au kukarabati nyumba ya makazi, makadirio ya bei ya soko ya nyumba hayatazidi gharama za maboresho, mabadiliko au ukarabati. Iwapo (3) SEHEMU YA TATU MASHARTI YA DHAMANA Masharti ya dhamana kwa mwanachama
Part
SEHEMU YA TATU
- 5 Verify source ↗
Masharti ya dhamana kwa mwanachama
AI-assisted research summary: A member may qualify for a Fund guarantee only if they are a Tanzanian citizen, are an eligible member, and the guarantee does not exceed the member’s mandatory retirement age.
5. Mwanachama atakuwa na sifa ya kupata dhamana ya Mfuko kama amekidhi masharti yafuatayo: (a) awe ni raia wa Tanzania; (b) awe mwanachama anayestahili; na (c) uhai wa dhamana hauzidi umri wa kustaafu wa lazima wa mwanachama. Masharti ya dhamana kwa taasisi - 6 Verify source ↗
Masharti ya dhamana kwa taasisi
AI-assisted research summary: An institution seeking Fund-backed security for a member loan must get Division approval and meet internal control, record-keeping, and reporting requirements.
6. Taasisi itakayohitaji dhamana ya Mfuko kwa ajili ya mkopo kwa mwanachama itapaswa- (a) kupata idhini ya Divisheni; 5 Kanuni za Matumizi ya Mafao ya Mwanachama Kama Dhamana ya Mkopo wa Nyumba Tangazo La Serikali Na. 149 (Linaendelea) Maombi ya idhini (b) kuwa na miongozo toshelezi na mifumo ya udhibiti wa ndani kwa lengo la kusimamia na kuendesha utaratibu wa mikopo; (c) kutunza na kuhuisha taarifa sahihi kuhusu akaunti ya mkopo ya mwenendo wa mwanachama; na (d) kutoa taarifa kadiri itakavyohitajika na Mfuko. - 7 Verify source ↗
Maombi ya idhini
AI-assisted research summary: An institution that wants to lend under these Regulations must apply in writing to the Division for permission, attach specified documents, and the Division must decide within 30 days.
7.-(1) Taasisi yoyote itakayotaka kutoa mkopo chini ya Kanuni hizi itapaswa kuwasilisha maombi kwa maandishi kwenye Divisheni kwa ajili ya kupata kibali cha kutoa mikopo hiyo. (2) Maombi yatakayowasilishwa chini ya kanuni ndogo ya (1) yatapaswa kuambatishwa na nyaraka zifuatazo: (a) nakala ya hati ya usajili wa kampuni; (b) nyaraka za uendeshaji wa kampuni; (c) nakala ya cheti cha usajili kutoka Benki Kuu ya Tanzania; (d) nakala ya leseni halali ya biashara; (e) taarifa za fedha zilizokaguliwa; (f) maelezo na wasifu wa wajumbe wa Bodi ya juu wa Wakurugenzi na uongozi wa mwombaji; (g) maelezo kuhusu uzoefu wa mwombaji katika utoaji wa huduma zinazohusiana na mkopo wa nyumba; na (h) idhini nyingine yoyote kutoka katika mamlaka husika itakayohitajika kwa mujibu wa Kanuni hizi. (3) Divisheni itashughulikia maombi na kutoa idhini kwa maandishi ndani ya siku thelathini tangu tarehe ya kupokea maombi, na endapo itakataa kutoa idhini, itamtaarifu mwombaji kwa maandishi ikieleza sababu za kukataa maombi yake. Masharti ya - 8 Verify source ↗
Masharti ya utoaji wa mikopo
AI-assisted research summary: Mfuko lazima uweke mkataba na taasisi ili kuainisha utaratibu wa utoaji wa mikopo; taasisi hairuhusiwi kutoa mkopo kwa mwanachama bila kuzingatia masharti ya Kanuni hizi.
8.-(1) Mfuko utaingia mkataba na taasisi kwa 6 Kanuni za Matumizi ya Mafao ya Mwanachama Kama Dhamana ya Mkopo wa Nyumba Tangazo La Serikali Na. 149 (Linaendelea) utoaji wa mikopo lengo la kuainisha utaratibu wa utoaji wa mikopo kama ilivyoainishwa kwenye Kanuni hizi. (2) Taasisi haitapaswa kutoa mkopo kwa mwanachama isipokuwa kama masharti ya Kanuni hizi yamezingatiwa. SEHEMU YA NNE KIWANGO CHA DHAMANA Kiwango cha dhamana
Part
SEHEMU YA NNE
- 9 Verify source ↗
Kiwango cha dhamana
AI-assisted research summary: The home-loan guarantee under these Regulations cannot exceed 50% of the member’s benefits at the time of application.
9. Kiwango cha dhamana ya mkopo wa nyumba chini ya Kanuni hizi hakitazidi asilimia hamsini ya mafao anayostahili mwanachama wakati wa kufanya maombi. Dhamana ya mkopo - 10 Verify source ↗
Dhamana ya mkopo
AI-assisted research summary: Mfuko hawezi kutoa dhamana ya mkopo wa nyumba isipokuwa mkopo uwe na nyumba kama dhamana ya kwanza na mwanachama awe ametoa ridhaa. Kabla ya kuidhinisha kiwango cha dhamana, taasisi lazima ihakikishe mkopo na dhamana ya kwanza vimekatiwa bima katika taasisi ya bima inayokubalika kisheria.
10.-(1) Mfuko hautatoa dhamana ya mkopo wa nyumba chini ya Kanuni hizi isipokuwa kama mkopo huo umetolewa kwa masharti yafuatayo: (a) nyumba ya mkopo ndiyo imewekwa kuwa ni dhamana ya kwanza kwenye mkopo huo; na (b) mwanachama ametoa ridhaa kwa Mfuko kuidhinisha kiwango cha mafao ambayo anastahili kutumia kama dhamana chini ya Kanuni hizi. (2) Kabla ya kuidhinisha kiwango cha dhamana, taasisi itapaswa kuuhakikishia Mfuko kwamba mkopo na mali inayotumika kama dhamana ya kwanza imekatiwa bima katika taasisi ya bima inayokubalika kisheria. SEHEMU YA TANO UHAI WA DHAMANA Uhai wa dhamana
Part
SEHEMU YA TANO
- 11 Verify source ↗
Uhai wa dhamana
AI-assisted research summary: Dhamana iliyotolewa chini ya Kanuni hizi hubaki hai hadi moja ya hali zilizotajwa itokee.
11. Dhamana iliyotolewa chini ya Kanuni hizi itakuwa hai hadi yatakopotokea yafuatayo: (a) kukoma kwa uanachama wa mwanachama husika wa Mfuko kwa mujibu wa Sheria ya Mfuko; (b) mwanachama anapokuwa amemaliza kulipa deni la mkopo na kupata uthibitisho kutoka 7 Kanuni za Matumizi ya Mafao ya Mwanachama Kama Dhamana ya Mkopo wa Nyumba Tangazo La Serikali Na. 149 (Linaendelea) kwenye taasisi husika; (c) mwanachama na taasisi wamejihusisha katika makubaliano yanayokiuka masharti ya Kanuni hizi. Kutumika kwa dhamana Usuluhishi wa migogoro kutumika iwapo mwanachama - 12 Verify source ↗
Kutumika kwa dhamana
AI-assisted research summary: Dhamana inaweza kutumika tu baada ya mkopaji kushindwa kulipa na taasisi kuonyesha Mfuko kwamba njia zote za kurejesha mkopo zimetumika; malipo ya dhamana hulipwa kwa taasisi lakini hukatwa kwenye mafao ya mwanachama, na kiasi hakizidi dhamana iliyowekwa.
12.-(1) Dhamana iliyotolewa chini ya Kanuni hizi itaweza atakuwa ameshindwa kulipa mkopo na taasisi imewasilisha kwenye Mfuko ushahidi kwamba njia zote za kurejesha mkopo huo, ikiwa ni pamoja na kutumia dhamana ya kwanza kwa kuzingatia masharti yaliyoainishwa kwenye mkataba, zimetumika kwa ukamilifu. (2) Malipo yoyote yatokanayo na matumizi ya dhamana yatakayolipwa na Mfuko kwenye taasisi kwa mujibu wa masharti ya Kanuni hizi yatakatwa kutoka kwenye mafao ya mwanachama. (3) Kiasi kitakacholipwa na Mfuko kutokana na matumizi ya dhamana hakitazidi kiasi cha dhamana iliyowekwa. - 13 Verify source ↗
Usuluhishi wa migogoro
AI-assisted research summary: If a dispute arises, the Fund resolves disputes between a member and an institution, and the Division resolves disputes between the Fund and an institution.
13.-(1) Iwapo kutatokea mgogoro baina ya mwanachama na taasisi kuhusu utekelezaji wa suala lolote chini ya Kanuni hizi, Mfuko utakuwa msuluhishi wa mgogoro huo. (2) Iwapo kutatokea mgogoro baina ya Mfuko na taasisi kuhusu utekelezaji wa suala lolote chini ya Kanuni hizi, Divisheni itakuwa msuluhishi wa mgogoro huo. Taarifa taarifa - 14 Verify source ↗
Taarifa
AI-assisted research summary: Mfuko lazima kuwasilisha taarifa kwa Divisheni kila robo mwaka kuhusu dhamana zilizotolewa na hali ya mikopo na dhamana zilizotumika au kuisha muda wake.
14. Mfuko utapaswa kuwasilisha kwenye Divisheni kwa kila robo mwaka ikionesha kiwango na idadi ya dhamana zilizotolewa, pamoja na maelezo ya malipo ya mikopo na dhamana zilizotumika na zilizoisha muda wake. 8 Kanuni za Matumizi ya Mafao ya Mwanachama Kama Dhamana ya Mkopo wa Nyumba Tangazo La Serikali Na. 149 (Linaendelea) SEHEMU YA SITA KUHAMA KWA MWANACHAMA KUTOKA MFUKO MMOJA KWENDA MWINGINE Uhamisho kwenda kwenye Mifuko Ujumuishwaji
Part
SEHEMU YA SITA
- 15 Verify source ↗
Uhamisho kwenda kwenye Mifuko
AI-assisted research summary: Uhamisho wa mwanachama kutoka mfuko mmoja wa dhamana kwenda mwingine hauathiri kitu kilichotolewa chini ya Kanuni hizi.
15. Uhamisho wa mwanachama kutoka Mfuko dhamana hautaathiri mmoja iliyotolewa chini ya Kanuni hizi. kwenda mwingine - 16 Verify source ↗
Ujumuishwaji
AI-assisted research summary: A member who has contributed to more than one fund has the right to combine their contribution periods, following the consolidation guidance issued by the Division.
16. Mwanachama yeyote ambaye amechangia kwenye Mfuko zaidi ya mmoja, kwa madhumuni ya Kanuni hizi, atakuwa na haki ya kujumuisha vipindi vya uchangiaji wake kwa mujibu wa mwongozo wa ujumuishaji uliotolewa na Divisheni. Dodoma, JOYCE L. NDALICHAKO 6 Februari, 2024 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu 9
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Kanuni za Matumizi ya Mafao ya Mwanachama kama Dhamana ya Mkopo wa Nyumba za Mwaka 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in