AI-assisted research summary: The applicant must build the natural gas pipeline only under the stated conditions, safety measures, and technical standards.
3. Kibali cha Ujenzi kimetolewa kwa Mwombaji kujenga bomba la kusambaza gesi asilia lenye urefu wa kilomita 2.65 na kipenyo cha milimita 250/315 na vifaa vyake kwa ajili ya kupeleka gesi asilia kwenye Kiwanda cha Vioo cha KEDA kilichopo katika Kijiji cha Msufini Wilaya ya Mkuranga kwa vigezo na masharti yafuatayo: 1 Notisi ya Kibali Cha Ujenzi wa Miundombinu ya Usambazaji wa Gesi Asilia Kwa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania Katika Kijiji Cha Msufini Wilaya ya Mkuranga Tangazo La Serikali Na. 174 (Linaendelea) (a) kuzingatia michoro iliyopitishwa, viwango vya kiufundi, mkuza na sheria; (b) kuhakikisha kuwa bomba la gesi asilia na vifaa vyake vinajengwa kwa kuzingatia viwango vilivyowekwa na Shirika la Viwango la Taifa au sheria; (c) kuhakikisha kuwa ukaguzi wa bomba na vifaa vyake wakati wa ujenzi unafanyika kadri inavyohitajika ili kuhakikisha kuwa ujenzi, vifaa, uchomeleaji, maunganisho na majaribio ya bomba baada ya kukamilika unafanyika kwa mujibu wa viwango vilivyowekwa na Shirika la Viwango la Taifa; (d) kuhakikisha kuwa bomba pamoja na vifaa vyake vinajengwa kwa kufuata mikuza iliyoidhinishwa kwa madhumuni ya kuepusha au kupunguza uwezekano wa hatari za mbeleni zitakazosababishwa na maendeleo ya viwanda au miji, kupanuliwa kwa njia na kutoharibu mazingira au sehemu za kihistoria; (e) kuhakikisha kuwa hakuna usumbufu au kupunguza usumbufu kwa wakazi walio karibu na eneo la ujenzi na usalama kwa umma unazingatiwa zaidi. Endapo ulipuzi utafanyika, ufanywe kwa kuzingatia taratibu za kisheria zilizopo na kufanywa na mtu mwenye sifa za kazi ya ulipuzi kwa kuzingatia usalama kwa umma, mifugo, wanyama, majengo, miundombinu ya simu, umeme, miundombinu ya chini ya ardhi na mali nyingine zilizo karibu na eneo linalofanyia ulipuzi; (f) kuhakikisha kuwa zinakuwepo juhudi za kupunguza uharibifu kwenye ardhi na kuzuia mazingira yatakayosababisha kuziba kwa mifereji ya kupitisha maji na mmomonyoko 2 Notisi ya Kibali Cha Ujenzi wa Miundombinu ya Usambazaji wa Gesi Asilia Kwa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania Katika Kijiji Cha Msufini Wilaya ya Mkuranga Tangazo La Serikali Na. 174 (Linaendelea) wa udongo. Baada ya ujenzi, ardhi itapaswa kurudishwa katika hali iliyokuwepo kwa kadri itakavyowezekana; (g) kuhakikisha kuwa, ujenzi wa bomba linalokatisha reli, barabara, vijito, maziwa, mito na alama za usalama kama vile taa hauathiri vitu hivi kwa usalama wa umma. Kukatisha kwa bomba kwenye vitu hivi kutazingatia sheria zilizopo na makatazo ya wadhibiti kwenye eneo hili. Kabla ya ujenzi wa bomba unaokatisha maeneo tajwa, ni lazima uwepo utaratibu baina ya Mwombaji na wamiliki wa maeneo au miundombinu linakopita bomba; (h) kuhakikisha kuwa njia inapopita bomba imepimwa na kuwekewa vigingi na alama ambazo zitaendelea kuwepo wakati wote wa ujenzi kwa mujibu wa kibali kilichotolewa na mmiliki wa njia; (i) bomba litafuata mkuza ulioainishwa; (j) kuhakikisha kuwa urefu wa mfereji wa bomba ni sahihi kwa kuzingatia eneo, matumizi ya uso wa ardhi, hali ya ardhi na uzito utokanao na barabara na reli. Upana wa mfereji ni lazima uruhusu kuwekwa kwa bomba bila kuharibu rangi yake na kuwezesha kazi ya kupaka rangi na ufungaji wa bomba kufanyika ndani ya mfereji; (k) kuhakikisha kuwa anachukua hatua zote stahiki ili kulilinda bomba na vifaa vyake dhidi ya mafuriko, udongo dhaifu, tetemeko la ardhi na hatari nyingine zinazoweza kusababisha bomba kuhama au kupata uzito wa ziada; (l) kuhakikisha kuwa bomba linalazwa umbali wa nchi 12 (milimita 300) kutoka kwenye 3 Notisi ya Kibali Cha Ujenzi wa Miundombinu ya Usambazaji wa Gesi Asilia Kwa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania Katika Kijiji Cha Msufini Wilaya ya Mkuranga Tangazo La Serikali Na. 174 (Linaendelea) miundombinu mingine iliyo chini ya ardhi ambayo haihusiani na gesi asilia. Endapo haitawezekana kupata umbali huu, bomba lilindwe dhidi ya uharibifu unaoweza kujitokeza kwa kuwa karibu na miundombinu mingine. Ni lazima uwepo umbali wa kutosha kutoka kwenye bomba na miundombinu mingine ya chini ya ardhi ili kuwezesha bomba kufanyiwa matengenezo na kulilinda dhidi ya uharibifu unaoweza kujitokeza kwa kuwa karibu na miundombinu mingine; (m) kuhakikisha kuwa vifaa vinavyotumika kwa ajili ya uchomeleaji ni vya ukubwa na aina sahihi kwa kazi hiyo vitakavyohakikisha uchomeleaji mzuri utakaowezesha bomba kuendelea kutumika na usalama wa watu; (n) kuzingatia viwango vya mazingira, afya na usalama vilivyoainishwa na sheria. Afya na usalama wa watu na vifaa vitapaswa kuzingatiwa na kuhakikisha matumizi ya vifaa vya usalama yaani kwa kifupi chake “PPE” wakati wote kama vile kofia ngumu, miwani na viatu vya usalama na matumizi ya kizima moto; (o) kuhakikisha kuwa miundombinu yote ya utoaji huduma kwa umma bila kujali kuwa inadhibitiwa na Mamlaka ama la inalindwa dhidi ya uharibifu na kuwaarifu wamiliki wake wawepo eneo la ujenzi wakati wa kujenga; (p) kuhakikisha la kuwa limezungushiwa utepe wa tahadhari; ujenzi eneo (q) kuweka mifumo ya ulinzi na ufuatiliaji wa bomba ikiwemo mifumo ya kuzuia kutu, valvu za kuondoa mgandamizo, valvu za kujifunga, kipimo cha mgandamizo, mfumo 4 Notisi ya Kibali Cha Ujenzi wa Miundombinu ya Usambazaji wa Gesi Asilia Kwa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania Katika Kijiji Cha Msufini Wilaya ya Mkuranga Tangazo La Serikali Na. 174 (Linaendelea) wa kugundua uvujaji wa gesi, mfumo wa kusafisha na kufuatilia unene wa bomba na mifumo ya mawasiliano; (s) kuhakikisha (r) kuhakikisha alama mbalimbali kama vile za kuanisha mkuza, bomba na mapumulio zimewekwa eneo lote la bomba; na kuwa zilizowekwa zinakuwa na alama za onyo, taarifa ya tahadhari na namba za simu za dharula. tahadhari Herufi itaandikwa kwa rangi nyeusi kwa maneno “Onyo au Tahadhari” kwenye ubao wenye rangi nyekundu. kwenye taarifa alama ya Ukomo wa Kibali