SHERIA NDOGO YA ADA NA USHURU WA MAZIWA YA HALMASHAURI YA WILAYA YA PANGANI YA MWAKA 2024
This section gives the short title of the by-law: the Pangani District Council Milk Fees and Levies By-Law, 2024.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- SHERIA NDOGO YA ADA NA USHURU WA MAZIWA YA HALMASHAURI YA WILAYA YA PANGANI YA MWAKA 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This section gives the short title of the by-law: the Pangani District Council Milk Fees and Levies By-Law, 2024. This section defines key terms used in the bylaw, including authorized officer, council, milk, trader, director, chairperson, levy, and agent. Halmashauri must establish milk collection centers throughout the Council area. Halmashauri itatoza ushuru wa maziwa wa asilimia 3, unaolipwa na mnunuzi. No one may transport commercial milk outside the Council without a permit; the Council must issue transport permits to buyers as set out in the First Schedule.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of SHERIA NDOGO YA ADA NA USHURU WA MAZIWA YA HALMASHAURI YA WILAYA YA PANGANI YA MWAKA 2024
Showing 11 of 11
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo
AI-assisted research summary: This section gives the short title of the by-law: the Pangani District Council Milk Fees and Levies By-Law, 2024.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Ada na Ushuru wa Maziwa ya Halmashauri ya Wilaya ya Pangani ya Mwaka 2024. - 2 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the bylaw, including authorized officer, council, milk, trader, director, chairperson, levy, and agent.
2. Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni mtumishi wa umma yeyote aliyeteuliwa na Mkurugenzi kusimamia Sheria Ndogo hizi; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Pangani; Sura ya 262 “maziwa” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Tasnia ya Maziwa; “mfanyabiashara” maana yake ni mtu, taasisi, kampuni au mashirika yanayojishughulisha na biashara ya maziwa; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani au afisa yeyote aliyeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi Mtendaji; “mwenyekiti”- (a) kuhusiana na Halmashauri ya Wilaya maana yake ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani; 1 Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru wa Maziwa ya Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Tangazo la Serikali Na.723 (Linaendelea.) (b) kuhusiana na Kijiji maana yake ni Mwenyekiti wa Kijiji; (c) kuhusiana na Kitongoji maana yake ni Mwenyekiti wa kitongoji; “ushuru” maana yake ni tozo ya maziwa itakayotozwa na Halmashauri kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizi; “Wakala” maana yake ni mtu binafsi, kikundi cha watu, kampuni au shirika ambalo limeteuliwa na Halmashauri kufanya kazi yoyote chini ya Sheria ndogo hizi kwa niaba ya Halmashauri. - 3 Verify source ↗
Halmashauri itaanzisha vituo vya kukusanyia
AI-assisted research summary: Halmashauri must establish milk collection centers throughout the Council area.
3. Halmashauri itaanzisha vituo vya kukusanyia maziwa katika eneo lote la Halmashauri. - 4 Verify source ↗
(1) Halmashauri itatoza ushuru wa maziwa kwa
AI-assisted research summary: Halmashauri itatoza ushuru wa maziwa wa asilimia 3, unaolipwa na mnunuzi.
4. -(1) Halmashauri itatoza ushuru wa maziwa kwa kiwango cha asilimia tatu ya bei ya kununulia maziwa katika vituo vya kukusanyia maziwa utakaolipwa na mnunuzi. (2) Ushuru utalipwa kwa Halmashauri au wakala. (3) Malipo ya ushuru yatafanyika kila siku au kwa mwezi au kwa namna yeyote itakayokubalika kulingana na makubaliano yatakayowekwa kati ya Halmashauri na mlipa ushuru. (4) Masharti ya kanuni hii hayatumika kwa wauzaji wa maziwa yenye ujazo usiozidi lita kumi wanaouza maziwa yao katika vituo vya kukusanyia maziwa. - 5 Verify source ↗
(1) Mtu yoyote hataruhusiwa kusafirisha maziwa
AI-assisted research summary: No one may transport commercial milk outside the Council without a permit; the Council must issue transport permits to buyers as set out in the First Schedule.
5.-(1) Mtu yoyote hataruhusiwa kusafirisha maziwa ya biashara nje ya Halmashauri bila kuwa na kibali. (2) Halmashauri itatoa kibali cha kusafirisha maziwa kwa mnunuzi kama kilivyoainishwa kwenye Jedwali la Kwanza.
Part
Jedwali la Kwanza.
- 6 Verify source ↗
(1) Halmashauri
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kumteua Wakala kukusanya ushuru, na Wakala aliyechaguliwa lazima akusanye, apokee, na awasilishe ushuru kulingana na eneo alilopewa, viwango vilivyoidhinishwa, na masharti ya mkataba wa uwakala.
6.-(1) Halmashauri inaweza kumteua Wakala kukusanya ushuru kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizi. (2) Wakala atakayeteuliwa kwa mujibu wa kanuni ndogo ya (1) atakuwa na wajibu wa- 2 Vituo vya kukusanyia maziwa Utozaji wa ushuru Kibali cha kusafirisha maziwa Uteuzi wa Wakala Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru wa Maziwa ya Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Tangazo la Serikali Na.723 (Linaendelea.) Rejesta ya wanunuzi wa maziwa Kutolipia Ushuru wa Maziwa (a) kukusanya na kupokea ushuru kwa niaba ya Halmashauri katika eneo alilopangiwa na kwa viwango vilivyoidhinishwa katika Sheria ndogo hizi; (b) kukusanya ushuru kwa kutumia mfumo wa kielektroniki na kuwasilisha makusanyo yote kwa kuzingatia masharti ya mkataba wa uwakala alioingia na Halmashauri. - 7 Verify source ↗
(1) Kutakuwa na rejesta ya wanunuzi wa maziwa
AI-assisted research summary: Kila kituo cha kukusanyia maziwa lazima kiwe na rejesta ya wanunuzi wa maziwa na kuitunza.
7.-(1) Kutakuwa na rejesta ya wanunuzi wa maziwa kwa kila kituo cha kukusanyia maziwa. (2) Kila kituo cha kukusanyia maziwa kitatunza rejesta yake ya kutunza kumbukumbu za wanunuzi wa maziwa. - 8 Verify source ↗
(1) Endapo mnunuzi atashindwa kulipa ushuru
AI-assisted research summary: If the buyer does not pay the tax, the milk is held for 12 hours and then sold at auction if not redeemed.
8.-(1) Endapo mnunuzi atashindwa kulipa ushuru kwa kuzingatia matakwa ya Sheria ndogo hii, maziwa yatakamatwa na kuhifadhiwa kwa masaa kumi na mbili na baada ya muda huo kupita bila mnunuzi kuyakomboa, maziwa hayo yatauzwa kwa njia ya mnada. (2) Fedha zitakazopatikana baada ya mauzo ya maziwa yaliyokamatwa na kunadiwa chini ya kanuni ndogo ya (2), Halmashauri itachukua ushuru wake, gharama za utunzaji wa maziwa kwa wakati wote maziwa yalipokuwa chini ya uangalizi wa Halmashauri pamoja na gharama za mnada, kiasi kitakachobaki atarudishiwa mnunuzi. Maziwa kupoteza thamani - 9 Verify source ↗
Endapo maziwa yaliyokamatwa chini ya kanuni
AI-assisted research summary: Halmashauri siyo na wajibu wa kufidia upotevu wa thamani wa maziwa yaliyokamatwa na yaliyo chini ya uangalizi wake, isipokuwa kama upotevu huo umesababishwa na Halmashauri au Wakala.
9. Endapo maziwa yaliyokamatwa chini ya kanuni ndogo ya (2) yatapoteza thamani, Halmashauri haitahusika na upotevu wa thamani katika maziwa hayo yaliyopo chini ya uangalizi wake, isipokuwa tu kama kupoteza thamani kumesababishwa na Halmashauri au Wakala. Makosa na adhabu - 10 Verify source ↗
Mtu ambaye
AI-assisted research summary: A person who fails to pay the tax, persuades others to evade or refuse to pay it, or obstructs the Director, Authorized Officer, or Agent commits an offence and may be fined, imprisoned, or both.
10. Mtu ambaye- (a) atashindwa kulipa ushuru kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii; (b) atamshawishi mtu au kundi la watu kukwepa au kukataa kulipa ushuru; na 3 Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru wa Maziwa ya Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Tangazo la Serikali Na.723 (Linaendelea.) (c) atamzuia Mkurugenzi, Afisa Mwidhiniwa au Wakala kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria Ndogo hizi, anatenda kosa, akitiwa hatiani atawajibika kulipa faini ya kiasi kisichopungua shilingi laki mbili na kisichozidi shilingi milioni moja au kifungo kisichopungua miezi kumi na mbili na kisichozidi miezi ishirini na nne au vyote kwa pamoja. - 11 Verify source ↗
Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha
AI-assisted research summary: The Director may compound an offence by charging shilingi laki mbili if the offender admits the offence, completes the prescribed form, and pays the tax owed.
11. Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha kosa kwa kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii kiasi cha shilingi laki mbili ikiwa mkosaji atakiri kosa na kuwa tayari kujaza fomu maalumu iliyoainishwa katika Jedwali la Pili na kulipa ushuru anaodaiwa. Kufifilisha kosa 4 Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru wa Maziwa ya Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Tangazo la Serikali Na.723 (Linaendelea.) _________ JEDWALI LA KWANZA __________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 5(2)) __________ KIBALI CHA KUSAFIRISHA MAZIWA Jina la mwombaji ………….…..……..................……….…………………..… Anwani ya mwombaji………..………..................……………………………. Tarehe ya maombi…………..………………..................………………….….. Kibali kinatolewa kwa ajili ya kufanya shughuli hiyo kama ulivyoomba kwa mujibu wa Sheria. Kibali hiki ni kwa ajili ya kusafirisha maziwa nje ya Mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya ya Pangani. MAELEZO YA MAZIWA YANAYOSAFIRISHWA NJE YA HALMASHAURI YA WILAYA YA PANGANI Jina la mwenye gari ………………………………………………..…......…………. Jina la dereva …………………………………………………………….......……… Sahihi ya dereva ………………………………………………………......………… Kiasi cha maziwa yanayosafirishwa (tani/lita) ……………………….....…………… Sehemu/kampuni/mfugaji/ushirika/mmiliki wa maziwa ………….....……..……… Hali ya maziwa (hayajachakatwa, yamechakatwa, ingine taja) ………....…..……… Yanakopelekwa/kusanywa ………………………………………………....………… Jina la mnunuzi ………………………………………………………....………….… Aina ya usafiri (taja pamoja na namba za usajili) …………………….………….… MAONI YA AFISA MWIDHINIWA Kibali kimetolewa/hakijatolewa (taja sababu) …………..………………………… Ushuru wa maziwa umelipwa/ haujalipwa ………………………………………… Stakabadhi namba .………………………………………………………………… Jina la Afisa Mwidhiniwa …….…………………………………….……………… Cheo/Wadhifa ……………………………………………..………………..……… Tarehe ……………………………………………………………………..……….. (N.B) kibali kijazwe nakala mbili moja apatiwe msafirishaji na nyingine iwasilishwe kwa Mkurugenzi Mtendaji (W). 5 Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru wa Maziwa ya Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Tangazo la Serikali Na.723 (Linaendelea.) ___________ JEDWALI LA PILI __________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 11) HATI YA KUKIRI NA KUFIFILISHA KOSA Mimi ……………………………………………………… nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya ………………………………………….ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani, kwamba mnamo tarehe...................... ya mwezi..............……. Mwaka..................…… nilitenda kosa la kukiuka masharti ya kanuni ya …................… ya Sheria Ndogo ya Ada na Ushuru wa Maziwa ya Halmashauri ya Wilaya ya Pangani ya Mwaka 2024. Kwa mamlaka aliyopewa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani, niko tayari kulipa kiasi cha ada au ushuru na faini ninayodaiwa badala ya kupelekwa Mahakamani. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA MIMI MWENYEWE KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU Leo tarehe…………. mwezi…………..… mwaka ………........…….………. Jina……………………………….. Saini………………………...................……… MBELE YANGU : Jina:………………………..............……………..…………………… Saini:………………………….………….……………………..……… Wadhifa:…….………………………………………………………… Tarehe; ………………….……………………………………………… 6 Sheria Ndogo ya Ada Na Ushuru wa Maziwa ya Halmashauri ya Wilaya ya Pangani Tangazo la Serikali Na.723 (Linaendelea.) Muhuri wa Halmashauri ya Wilaya ya Pangani uliobandikwa kwenye Sheria Ndogo hizi kwa kufuatia Azimio lililopitishwa kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani uliofsanyika mnamo tarehe 29/4/2022 mbele ya:- ISAYA MUGISHAGWE MBENJE, Mkurugenzi mtendaji, Halmashauri ya wilaya, Pangani AKIDA OMARI BAHORERA, Mwenyekiti, Halmashauri ya wilaya, Pangani L.S NAKUBALI, Dodoma, 30 Novemba, 2024 MOHAMED OMARY MCHENGERWA (Mb.), Waziri wa Nchi-OR-TAMISEMI, 7
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
SHERIA NDOGO YA ADA NA USHURU WA MAZIWA YA HALMASHAURI YA WILAYA YA PANGANI YA MWAKA 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in