AI-assisted research summary: Mwombaji anapewa kibali cha kujenga kituo cha mafuta kwa masharti mengi ya usalama, viwango vya TBS, na mpangilio wa eneo.
3. Mwombaji anapewa Kibali cha Ujenzi kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Mafuta katika Kiwanja Na. 1, Kitalu “EE”, Eneo la Chamakweza Wilaya Ya Chalinze, Mkoa wa Pwani kwa masharti yafuatayo: (a) kituo cha mafuta kitajengwa kwa mujibu wa viwango vya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Na. TZS 1115:2009 na TZS 1079:2008; (b) uangalifu wa kutosha utazingatiwa wakati wa uchimbaji na uwekaji wa matenki ya mafuta 1 Notisi ya Kibali Cha Ujenzi wa Kituo Cha Mafuta Kwa Afro Prime Limited Tangazo La Serikali Na. 203 (Linaendelea) chini ya ardhi; (c) mpangilio wa kituo cha mafuta utapaswa kukidhi umbali wa kiusalama kwa mujibu wa viwango vya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) Na. TZS 1079:2008; (d) ufukiaji wa matenki ya kuhifadhi mafuta pamoja na mabomba chini ya ardhi ufanywe kwa namna ambayo italinda usalama wa vifaa hivyo ikiwemo kupata kutu; (e) matenki ya kuhifadhia mafuta, pampu na mabomba husika pamoja na vifaa vyote vinavyounganishwa pamoja navyo vitapaswa kufungwa vizuri ili kuzuia uvujaji wowote wa Mafuta; (f) matenki ya kuhifadhia mafuta na pampu ya Mafuta itapaswa kufanyiwa uhakiki wa usahihi wa vipimo na Wakala wa Vipimo Tanzania aliyeanzishwa kwa mujibu wa Sheria ya Vipimo Tanzania; Sura ya 340 (g) eneo la mbele la kituo cha mafuta na kuzunguka eneo la pampu litasakafiwa kwa zege madhubuti lisiloweza kupenyeza mafuta na kuhakikisha kuwepo kwa mitaro ambayo itakusanya maji na mafuta wakati wa mvua na kuyaelekeza kwenye chemba ya kutenganisha maji na mafuta; (h) kuweka swichi ya dharura katika eneo linaloonekana na kufikika kirahisi ili wakati wa dharura iwe ni rahisi kuzima umeme wa kituo kizima; (i) kuhakikisha kuwepo na vyoo vya kutosha vya wanawake na wanaume vilivyo safi wakati wote; (j) kuhakikisha usalama zinawekwa sehemu ya kuingia na ya kutoka kwenye kituo cha mafuta na eneo la pampu alama kuwa za 2 Notisi ya Kibali Cha Ujenzi wa Kituo Cha Mafuta Kwa Afro Prime Limited Tangazo La Serikali Na. 203 (Linaendelea) zikijumuisha “zima injini”, “zima simu” na “usivute sigara”; (k) hakikisha kila tenki la kuhifadhia mafuta linaunganishwa na bomba la kupumulia lenye urefu usiopungua mita 3.6 kutoka ardhini. Bomba hilo litakuwa angalau mita 1.5 kutoka kwenye mpaka wa kiwanja na angalau mita 4 kutoka kwenye dirisha au kifaa chochote cha kuvuta hewa ikiwemo Air Conditioner; (l) pump za kuuza mafuta na sehemu ya kupakua mafuta itakuwa angalau mita 4.5 kutoka kwenye mpaka wa kiwanja, anagalu mita 8 kutoka kilipo kifaa ambacho kinaweza kuwa chanzo cha moto ikiwemo jokofu na angalau mita 10 kutoka kwenye nyaya za kusafirishia umeme; chochote (m) kuhakikisha kila pampu ya mafuta inalindwa na kizuizi ambacho kitakuwa na urefu wa mita moja kutoka juu ya ardhi; (n) mifumo ya upakuaji wa mafuta kwenye kituo cha mafuta itajengwa kwa kufuata kanuni na taratibu zinazokubalika kwenye sekta ya mafuta; (o) kuhakikisha kuwa kituo cha mafuta kinakuwa na paa linalofunika eneo lote lenye pampu za mafuta na linajengwa kwa mujibu wa viwango na taratibu zinazokubalika kwenye sekta ya mafuta; na (p) kuhakikisha kuwa kituo cha mafuta kinakuwa na bango la bei ambalo litawekwa mahali panapoonekana kirahisi ili wateja waweze kuona bei za mafuta kabla ya kuingia kituoni. 3 Notisi ya Kibali Cha Ujenzi wa Kituo Cha Mafuta Kwa Afro Prime Limited Tangazo La Serikali Na. 203 (Linaendelea) Ukomo wa kibali cha Ujenzi