Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Maegesho na Vituo vya Vyombo vya Usafiri ya Halmashauri ya Mji Mafinga ya Mwaka 2024
This section states the title of the by-law.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Maegesho na Vituo vya Vyombo vya Usafiri ya Halmashauri ya Mji Mafinga ya Mwaka 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This section states the title of the by-law. This by-law applies throughout the area of Mafinga Town Council. This section defines key terms used in the by-laws. Halmashauri lazima itozeshe ushuru wa maegesho kwa vyombo vyote vya usafiri, na mwenye chombo kinachoingia eneo la maegesho lazima alipe; baadhi ya vyombo vya Serikali na vingine vilivyotajwa havitozwi. Baadhi ya maeneo yaliyotengwa na Halmashauri yanakuwa vituo vya maegesho; Halmashauri pia inaweza kuweka mistari au alama za kupangilia maegesho.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Maegesho na Vituo vya Vyombo vya Usafiri ya Halmashauri ya Mji Mafinga ya Mwaka 2024
Showing 21 of 21
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya
AI-assisted research summary: This section states the title of the by-law.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Maegesho na Vituo vya Vyombo vya Usafiri ya Halmashauri ya Mji Mafinga ya Mwaka 2024. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la
AI-assisted research summary: This by-law applies throughout the area of Mafinga Town Council.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la Mamlaka ya Halmashauri ya Mji Mafinga. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii,
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the by-laws.
3. Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “afisa mwidhiniwa” maana yake ni afisa yeyote aliyeteuliwa na Mkurugenzi kwa lengo la kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “chombo cha usafiri” maana yake ni chombo chochote kinachotumika kusafirishia bidhaa, abiria au mizigo; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Mji Mafinga; “karakana” maana yake ni eneo la Halmashauri lililotengwa au litakalotengwa kwa ajili ya shughuli za ufundi na kuhifadhi vyombo vya usafiri; “kituo” maana yake ni eneo maalumu lililotengwa na Halmashauri kwa ajili ya maegesho au kwa ajili ya huduma za usafiri ambapo vyombo vya usafiri vitapakia au kushusha abiria au mizigo; “maegesho” maana yake ni sehemu maalumu iliyotengwa kwa ajili yya kuegesha vyombo vya usafiri; 1 Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Maegesho Na Vituo Vya Vyombo Vya Usafiri ya Halmashauri ya Mji Mafinga Tangazo La Serikali Na. 209 (Linaendelea) “maegesho yaliyohifadhiwa” maana yake ni maeneo maalumu yaliyotengwa na kuhifadhiwa kwa ajili ya maegesho binafsi ya vyombo vya usafiri kwa ajili ya mtu binafsi au taasisi; “stendi” maana yake ni eneo maalumu lililotengwa au kujengwa na Halmashauri kwa ajili ya kupakia na kushusha abiria au mizigo; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga au afisa yeyote aliyeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi; “ushuru wa stendi” maana yake ni kiasi cha fedha kinachotozwa na Halmashauri kwa vyombo vya usafiri vinavyoingia stendi au mtu yoyote anayefanya shughuli katika stendi; “vituo vya njiani” maana yake ni vituo vyote vilivyopo pembeni ya barabara vinavyotumika kupakia na kushusha abiria ambavyo si stendi; “wakala” maana yake ni mtu aliyeteuliwa na Halmashauri kutekeleza majukumu chini ya Sheria Ndogo hii kwa niaba ya Halmashauri. Ushuru wa maegesho - 4 Verify source ↗
(1) Halmashauri itatoza ushuru wa maegesho kwa
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima itozeshe ushuru wa maegesho kwa vyombo vyote vya usafiri, na mwenye chombo kinachoingia eneo la maegesho lazima alipe; baadhi ya vyombo vya Serikali na vingine vilivyotajwa havitozwi.
4.-(1) Halmashauri itatoza ushuru wa maegesho kwa vyombo vyote vya usafiri kwa mujibu wa viwango vilivyoainishwa katika Jedwali la Kwanza. (2) Mtu mwenye chombo cha usafiri kinachoingia katika eneo lolote la maegesho atalipa ushuru wa maegesho kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. (3) Bila kuathiri masharti ya aya ndogo ya (1) na (2), vyombo vya usafiri vinavyomilikiliwa na Serikali, wanadiplomasia, majeshi na magari ya kubeba wagonjwa havitatozwa ushuru wa maegesho. 2 Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Maegesho Na Vituo Vya Vyombo Vya Usafiri ya Halmashauri ya Mji Mafinga Tangazo La Serikali Na. 209 (Linaendelea) Maeneo ya maegesho Uanzishaji wa vituo vya vyombo vya usafiri Utaratibu wa kutumia vituo vya vyombo vya usafiri - 5 Verify source ↗
(1) Kituo Kikuu cha mabasi, kituo cha kuegesha
AI-assisted research summary: Baadhi ya maeneo yaliyotengwa na Halmashauri yanakuwa vituo vya maegesho; Halmashauri pia inaweza kuweka mistari au alama za kupangilia maegesho.
5.-(1) Kituo Kikuu cha mabasi, kituo cha kuegesha magari ya mizigo na maeneo mengine yaliyotengwa au yatakayotengwa na Halmashauri kama maeneo ya maegesho yatakuwa ni vituo vya maegesho. (2) Halmashauri inaweza kugawa maeneo ya maegesho kwa mistari au kwa kutumia alama yoyote itakayoonyesha idadi na sehemu ambayo chombo cha usafiri kinatakiwa kuegeshwa. (3) Bila kuathiri masharti ya aya ndogo ya (2), kukosekana kwa mistari au alama za maegesho hakutaathiri madai ya ada ya maegesho ya chombo cha usafiri kilichoegeshwa ndani ya maeneo hayo. - 6 Verify source ↗
Halmashauri inaweza kuanzisha vituo vya vyombo
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kuanzisha vituo vya vyombo vya usafiri wa umma kwa huduma ndani ya Halmashauri na kwa vyombo vinavyoingia kwa ajili ya kupakia na kushusha abiria na mizigo.
6. Halmashauri inaweza kuanzisha vituo vya vyombo vya usafiri wa umma vinavyotoa huduma ndani ya Halmashauri, na vinavyoingia ndani ya Halmashauri kwa ajili ya kupakia na kushusha abiria na mizigo. ya Halmashauri vinavyotoka nje - 7 Verify source ↗
(1) Mtu anayeendesha chombo cha usafiri wa
AI-assisted research summary: Wahudumu wa usafiri wa umma na watumiaji wa kituo/stendi lazima wafuate kanuni za matumizi ya vituo, ikiwemo kushusha/kupakia tu ndani ya kituo, muda wa kusimama, na matumizi ya lugha ndani ya kituo.
7.-(1) Mtu anayeendesha chombo cha usafiri wa umma hatapakia au kushusha abiria au mizigo nje ya kituo au stendi. (2) Safari zote za mabasi zitaanzia na kumalizika katika stendi ya mabasi isipokua kwa mabasi yanayopita kutoka na kuelekea maeneo mengine ya nje ya Halmashauri. (3) Chombo cha usafiri wa umma hakitasimama kwa zaidi ya dakika tano katika vituo vya njiani. (4) Mtu hatafanya matengenezo au kuosha chombo cha usafiri katika kituo au stendi isipokuwa kwa idhini ya Halmashauri. 3 Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Maegesho Na Vituo Vya Vyombo Vya Usafiri ya Halmashauri ya Mji Mafinga Tangazo La Serikali Na. 209 (Linaendelea) (5) Mtumiaji wa kituo au stendi hatatumia lugha ya matusi, inayoweza kuleta uchochezi, bughudha au inayoweza kuhatarisha usalama na amani ndani ya kituo. Maegesho yaliyohifa dhiwa - 8 Verify source ↗
(1) Baada ya kupokea maombi kutoka kwa mtu
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kutenga eneo la maegesho kama eneo la kuhifadhiwa baada ya kupokea ombi.
8.-(1) Baada ya kupokea maombi kutoka kwa mtu yeyote anayetaka kutengewa eneo la kuegesha chombo cha usafiri, Halmashauri inaweza kutenga eneo la maegesho kuwa ni maegesho yaliyohifadhiwa. (2) Katika kushughulikia maombi chini ya aya hii, Halmashauri itazingatia yafuatayo: (a) athari kwa biashara au shughuli katika eneo husika endapo kibali hicho kitatolewa; (b) uwepo wa maegesho katika eneo hilo; (c) uwepo wa eneo mbadala la maegesho; (d) idadi ya maeneo au nafasi zinazoombwa kuhifadhiwa; na (e) iwapo muda uliopendekezwa kwa ajili ya eneo hilo kuhifadhiwa unafaa. (3) Endapo maombi yatakataliwa, Halmashauri itamtaarifu mwombaji kwa maandishi na kutoa sababu za kukataliwa. (4) Endapo maombi yatakubaliwa na mwombaji kulipa ushuru wa maegesho, ataruhusiwa kutumia sehemu hiyo yeye peke yake bila ya kuingiliwa. - 9 Verify source ↗
(1) Mtu hataegesha chombo chochote cha usafiri
AI-assisted research summary: Mtu haruhusiwi kuegesha chombo cha usafiri katika maeneo yasiyo rasmi au kwa namna isiyoruhusiwa.
9.-(1) Mtu hataegesha chombo chochote cha usafiri katika maeneo yasiyo rasmi kwa ajili ya maegesho au kuegesha kwa namna isiyoruhusiwa. (2) Halmashauri inaweza kuzuia kwa kufunga vifaa maalumu kwenye chombo cha usafiri kilichoegeshwa vibaya au kilichoegeshwa katika eneo lisiloruhusiwa na kumtaka mmiliki au mtumiaji kulipa faini kwa mujibu wa viwango vilivyoainishwa katika Sheria Ndogo hii. (3) Chombo cha usafiri kilichozuiwa kwa mujibu wa aya ndogo ya (2) kwa zaidi ya saa mbili bila ya kulipiwa 4 Maegesho yasiyo rasmi Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Maegesho Na Vituo Vya Vyombo Vya Usafiri ya Halmashauri ya Mji Mafinga Tangazo La Serikali Na. 209 (Linaendelea) Chombo cha usafiri kilichotele kezwa kitavutwa na kupelekwa katika karakana iliyoidhinishwa na Halmashauri kwa gharama za mmiliki wa chombo hicho na Halmashauri haitawajibika kwa uharibifu utakaotokea wakati wa uvutwaji huo. - 10 Verify source ↗
(1) Chombo cha usafiri ambacho kitahifadhiwa
AI-assisted research summary: If a vehicle is kept for 30 days without being redeemed, it is treated as abandoned.
10.-(1) Chombo cha usafiri ambacho kitahifadhiwa thelathini bila katika karakana kwa muda wa siku kukombolewa, kitachukuliwa kuwa kimetelekezwa. (2) Baada ya kipindi cha siku thelathini kupita Halmashauri inaweza kupeleka maombi mahakamani ili iweze kutamka kuwa chombo hicho kimetelekezwa na kutoa kibali chombo hicho kiuzwe kwa njia ya mnada wa hadhara. (3) Bila kuathiri masharti ya aya ndogo ya (2), kabla ya kuuza mali yoyote iliyokamatwa, Mkurugenzi atatoa notisi ya siku saba kwa mdaiwa na umma juu ya kusudio la kuuza chombo hicho. (3) Fedha zitakazopatikana kutokana na mauzo ya chombo cha usafiri zitatumika kulipa ushuru unaodaiwa, pamoja na gharama za kukamata na fedha zitakazobaki zitarejeshwa kwa mmiliki au mwakilishi wake. Maegesho kwa muda maalumu Usajili wa teksi, bajaji na pikipiki - 11 Verify source ↗
Magari makubwa ya mizigo yenye zaidi ya tani
AI-assisted research summary: Magari makubwa ya mizigo yenye zaidi ya tani tano hayapaswi kuegeshwa katikati ya mji isipokuwa kwa kibali maalumu na baada ya kulipa ada iliyoainishwa.
11. Magari makubwa ya mizigo yenye zaidi ya tani tano hayataegeshwa katikati ya mji isipokuwa kwa kibali maalumu na kilipiwa ada iliyoainishwa katika Sheria Ndogo hii. - 12 Verify source ↗
(1) Mmiliki wa teksi, bajaji au pikipiki inayofanya
AI-assisted research summary: Mmiliki wa teksi, bajaji au pikipiki inayofanya kazi ndani ya Halmashauri lazima aisajili kwa Halmashauri na alipe ada ya usajili; Halmashauri pia hutoa stika ya usajili, na mmiliki lazima aibandike pembeni mwa chombo.
12.-(1) Mmiliki wa teksi, bajaji au pikipiki inayofanya kazi ndani ya Halmashauri atasajili kwa Halmashauri na kulipia ada ya usajili ya chombo hicho cha usafiri kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. (2) Halmashauri itatoa stika za usajili wa teksi, bajaji au pikipiki kwa kila mmiliki, na itakuwa wajibu wa kila mmiliki kubandika stika atakayopewa na Halmashauri pembeni mwa chombo chake cha usafiri. Ukusanyaj - 13 Verify source ↗
Ushuru wa vyombo vya usafiri utakusanywa kwa
AI-assisted research summary: This provision concerns collection of transport-vehicle fees/tax and refers to the powers of an authorized officer under the Mafinga Town Council fee-and-tax by-law.
13. Ushuru wa vyombo vya usafiri utakusanywa kwa 5 Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Maegesho Na Vituo Vya Vyombo Vya Usafiri ya Halmashauri ya Mji Mafinga Tangazo La Serikali Na. 209 (Linaendelea) i wa ushuru wa vyombo vya usafiri Mamlaka ya afisa mwidhini wa Makosa mujibu wa Sheria Ndogo ya Ada na Ushuru ya Halmashauri ya Mji Mafinga ya Mwaka 2024. - 14 Verify source ↗
Afisa mwidhiniwa atakuwa na mamlaka ya
AI-assisted research summary: Afisa mwidhiniwa ana mamlaka ya kukamata na kuondoa chombo cha usafiri kilichopaki mahali pasiporuhusiwa.
14. Afisa mwidhiniwa atakuwa na mamlaka ya kukamata na kuondoa chombo cha usafiri ambacho kimeegeshwa katika maeneo yasiyo rasmi kwa ajili ya maegesho au kuegeshwa kwa namna isiyoruhusiwa. - 15 Verify source ↗
Mtu anatenda kosa endapo mtu huyo
AI-assisted research summary: A person commits an offence if they refuse or fail to pay parking fees, encourage others not to pay, park or load/unload in prohibited places, or give false information when required.
15. Mtu anatenda kosa endapo mtu huyo- (a) anakataa au anashindwa kulipa ushuru wa maegesho; (b) anamshawishi mtu yeyote au kundi la watu kukataa kulipa ushuru wa maegesho; (c) anapakia au anashusha abiria au mizigo katika eneo ambalo ambalo nje ya kituo au stendi; (d) anafanya matengenezo au kuosha gari katika katika eneo lililotengwa kwa ajili ya maegesho; (e) anaegesha chombo cha usafiri katika eneo ambalo halijaruhusiwa; (f) anakataa kutoa taarifa au atatoa taarifa za uongo kwa Mkurugenzi, afisa mwidhiniwa au wakala pale zitakapohitajika; (g) anaanzisha eneo la maegesho yaliyohifadhiwa bila idhini ya Halmashauri; au (h) anaegesha chombo cha usafiri nje ya mstari uliochorwa kuainisha eneo la kuegeshea chombo cha usafiri. Adhabu - 16 Verify source ↗
Mtu anayetenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii
AI-assisted research summary: A person convicted of an offence under these by-laws must pay a fine, go to prison, or both.
16. Mtu anayetenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii akitiwa hatiani atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi laki mbili na isiyozidi shilingi milioni moja au kifungo kisichopungua miezi kumi na mbili na kisichozidi miezi ishirini na nne au vyote. 6 Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Maegesho Na Vituo Vya Vyombo Vya Usafiri ya Halmashauri ya Mji Mafinga Tangazo La Serikali Na. 209 (Linaendelea) Ufifilishaj i makosa - 17 Verify source ↗
Mkurugenzi anaweza kumtaka mtu aliyetenda
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kumtaka aliyefanya kosa chini ya Sheria Ndogo hii kulipa kiasi kisichozidi shilingi laki mbili, ikiwa anakiri kosa kwa maandishi kwenye fomu maalumu na kulipa ada au ushuru unaodaiwa.
17. Mkurugenzi anaweza kumtaka mtu aliyetenda kosa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii kulipa kiasi kisichozidi shilingi laki mbili endapo mkosaji atakiri kosa kwa maandishi katika fomu maalumu iliyoainishwa katika Jedwali la Pili na kulipa ada au ushuru anaodaiwa. ________________ JEDWALI LA KWANZA ________________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 4(1)) USHURU WA VYOMBO VYA USAFIRI NA HUDUMA KATIKA STENDI, VITUO NA MAEGESHO (a) Ushuru wa kuingia stendi Namba. Aina ya Chombo
Part
JEDWALI LA KWANZA
- 12 Verify source ↗
Section 12
AI-assisted research summary: The section lists vehicle and service categories for charging entry or use fees at the stand and other council areas.
12. Basi dogo la abiria kati ya 1 – 20 Basi kubwa la abiria kati ya 20 – 28 Basi kubwa la abiria zaidi ya 28 Teksi iliyosajiriwa kufanya kazi stendi Gari dogo binafsi linaloingia na kutoka Magari ya mizigo Pikipiki Bajaji Magari mengineyo Ada ya kuingia mtu mmoja Teksi anayoshusha abiria na kuondoka Huduma ya kutumia choo Stendi na maeneo mengine ya Halmashauri - 13 Verify source ↗
Section 13
AI-assisted research summary: The text lists charges for storing an impounded or held vehicle and for parking vehicles at a stand, with several fees shown in shillings.
13. Ada ya kutunza gari lililo kamatwa au kuzuiliwa (b) Ushuru kulaza chombo cha usafiri stendi Ushuru (Shilingi) 1,000 kwa siku 1,000 kwa siku 3,000 kwa siku 1,000 kwa siku 500 kila inapoingia 1,000 kila inapoingia 500 kila inapoingia 500 kila inapoingia 1,000 kila inapoingia 200 kila inapoingia 500 kila inapoingia 200 kila unapopata huduma 500 kwa huduma ya kuoga 10,000/= Namba. Aina ya Chombo - 4 Verify source ↗
Section 4
AI-assisted research summary: This section sets daily parking charges for different vehicle types.
4. Basi kubwa la abiria kati ya 20-28 Basi kubwa la abiria 28 Basi dogo la abiria kati ya 1-20 Teksi Ushuru wa kulaza chombo cha usafiri kwa siku (Shilingi) 5,000 8,000 4,000 2,000 7 Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Maegesho Na Vituo Vya Vyombo Vya Usafiri ya Halmashauri ya Mji Mafinga Tangazo La Serikali Na. 209 (Linaendelea) - 10 Verify source ↗
Section 10
AI-assisted research summary: This section lists parking charges and related vehicle fees by vehicle type and time period.
10. Gari dogo binafsi Gari ya mizigo yenye uzito usiozidi tani 3 Gari ya mizigo yenye uzito unaozidi tani 3 Magari ya mizigo Magari mengine Pikipiki 2,000 5,000 10,000 4,000 4,000 1,000 (c) Ushuru wa maegesho Namba Aina ya Gari Kwa saa Ushuru (Shilingi) Kwa siku 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 Gari ya mizigo zaidi ya tani 5 Gari la mizigo chini ya tani 5 Pick up/station wagon Lori lenye trela isiyozidi tani 3 Lori lenye trela tani 3 na zaidi Gari la abiria (nje ya stendi) Gari dogo binafsi Bajaji Pikipiki Mitambo na magari mengine 2,000 1,000 1,000 1,000 2,000 1,000 500 200 200 1,000 3,000 2,000 2,000 2,000 3,000 2,000 1,000 500 300 2,000 Kulaza gari/siku 5,000 3,000 3,000 3,000 5,000 5,000 2,000 1,000 1,000 4,000 _________ JEDWALI LA PILI ________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 17) FOMU YA KUKIRI NA KUFIFILISHA KOSA Mimi.....................................................................nakiri kwa hiari yangu mwenyewe mbele ya .....................................................................ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga, tarehe..........ya mwezi.......................Mwaka...........................nilitenda kosa la kukiuka masharti ya aya ya...............ya Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Maegesho na Vituo vya Vyombo vya Usafiri ya Halmashauri ya Mji Mafinga ya Mwaka 2024. kwamba mnamo Nipo tayari kulipa kiasi cha ushuru ninaodaiwa pamoja na faini. Ninathibitisha kuwa maelezo hapo juu ni ya kweli na nimeyatoa mimi mwenyewe kwa hiari yangu na kadri ya ufahamu wangu. Leo tarehe.....................ya Mwezi.........................Mwaka...................................... Jina.................................................... Saini............................................................. 8 Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Maegesho Na Vituo Vya Vyombo Vya Usafiri ya Halmashauri ya Mji Mafinga Tangazo La Serikali Na. 209 (Linaendelea) MBELE YA: Jina:....................................................... Wadhifa:.................................................... Saini.......................................................... Tarehe........................................................ Lakiri ya Halmashauri ya Mji Mafinga imegongwa kwenye Sheria Ndogo hizi kufutia azimio lililopitishwa katika Mkutano wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Mji Mafinga uliofanyika Tarehe 14 mwezi 02 Mwaka 2023 na kushuhudiwa Lakari hiyo ikigongwa mbele ya ;- AYUBU J. KAMBI Mkurugenzi REGNANT Z. KIVINGE Mwenyekiti Halmashauri ya Mji Mafinga NAKUBALI L.S DODOMA 31 Januari, 2024 MOHAMED OMARY MCHENGERWA (MB) Waziri wa Nchi – Ofisi ya Rais 9
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Usimamizi wa Maegesho na Vituo vya Vyombo vya Usafiri ya Halmashauri ya Mji Mafinga ya Mwaka 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in