Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Mji Mafinga ya Mwaka 2024
Kifungu hiki kinaweka jina la Sheria Ndogo hii: Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Mji Mafinga ya Mwaka 2024.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Mji Mafinga ya Mwaka 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
Kifungu hiki kinaweka jina la Sheria Ndogo hii: Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Mji Mafinga ya Mwaka 2024. This bylaw applies throughout the whole area of Mafinga Town Council. Kifungu hiki kinafafanua maneno muhimu yanayotumika kwenye Sheria Ndogo, ikiwemo afisa mwidhiniwa, Halmashauri, Mkurugenzi, mlipa ushuru wa huduma, Wakala, na ushuru wa huduma. Halmashauri lazima itoze na kukusanya ushuru wa huduma kwa mauzo fulani, kwa kiwango cha 0.3% au kiwango kilicho kwenye Jedwali la Kwanza kulingana na aina ya mfanyabiashara. Mlipa ushuru wa huduma lazima alipe ushuru, awasilishe taarifa na hesabu sahihi, ahifadhi kumbukumbu, na atoe nyaraka zinapohitajika; baadhi ya malipo na makadirio yana muda maalum.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Mji Mafinga ya Mwaka 2024
Showing 14 of 14
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo
AI-assisted research summary: Kifungu hiki kinaweka jina la Sheria Ndogo hii: Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Mji Mafinga ya Mwaka 2024.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Mji Mafinga ya Mwaka 2024. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la
AI-assisted research summary: This bylaw applies throughout the whole area of Mafinga Town Council.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la Mamlaka ya Halmashauri ya Mji Mafinga. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii,
AI-assisted research summary: Kifungu hiki kinafafanua maneno muhimu yanayotumika kwenye Sheria Ndogo, ikiwemo afisa mwidhiniwa, Halmashauri, Mkurugenzi, mlipa ushuru wa huduma, Wakala, na ushuru wa huduma.
3. Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “afisa mwidhiniwa” maana yake ni afisa yeyote aliyeteuliwa na Mkurugenzi kwa madhumuni ya kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Mji Mafinga; “hesabu za mwisho” maana yake ni hesabu za mwisho zinazowasilishwa na mfanyabiashara baada ya kipindi cha hesabu pamoja na nyaraka au maelezo yatakayotakiwa kutolewa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii; Sura ya 212 “kampuni” maana yake ni kampuni iliyosajiliwa kwa mujibu wa Sheria ya Kampuni; “kipindi maalumu cha hesabu” maana yake ni muda ambao mfanyabiashara anatakiwa kuwasilisha hesabu za biashara kwa Halmashauri; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga au afisa yeyote aliyeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi chini ya Sheria Ndogo hii; “mlipa ushuru wa huduma” maana yake ni mtu mwenye leseni ya biashara anayefanya shughuli zake katika eneo la Halmashauri; 1 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Mji Mafinga Tangazo La Serikali Na. 210 (Linaendelea) Sura ya 212 “tawi la kampuni” maana yake ni tawi la kampuni iliyosajiliwa kwa mujibu wa Sheria ya Kampuni; kutoka “ushuru wa huduma” maana yake ni ushuru unaotozwa na kukusanywa kwa na Halmashauri mfanyabiashara yeyote mwenye leseni ya biashara ambaye mauzo yake kwa mwaka ni zaidi ya shilingi milioni nne kutokana na huduma anazopata na kutumia miundombinu ya umma inayomuwezesha kufanya biashara katika eneo la Halmashauri; “Wakala” maana yake ni mtu aliyeteuliwa na Halmashauri kwa madhumuni ya kukusanya ushuru kwa niaba ya Halmashauri kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. Ushuru wa huduma - 4 Verify source ↗
(1) Halmashauri itatoza na kukusanya ushuru wa
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima itoze na kukusanya ushuru wa huduma kwa mauzo fulani, kwa kiwango cha 0.3% au kiwango kilicho kwenye Jedwali la Kwanza kulingana na aina ya mfanyabiashara.
4.-(1) Halmashauri itatoza na kukusanya ushuru wa huduma kwa kiwango cha asilimia 0.3% ya mauzo baada ya kutoa Kodi ya Ongezeko la Thamani kutoka kwa mtu yeyote mwenye leseni ya biashara anayewasilisha hesabu za mauzo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania. (2) Bila kuathiri masharti ya aya ndogo ya (1), Halmashauri itatoza na kukusanya ushuru wa huduma kwa kiwango kilichoainishwa katika Jedwali la Kwanza kutoka kwa wafanyabiashara wenye biashara wasiowasilisha hesabu za mauzo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania. leseni za Wajibu wa mlipa ushuru wa huduma wa: - 5 Verify source ↗
(1) Mlipa ushuru wa huduma atakuwa na wajibu
AI-assisted research summary: Mlipa ushuru wa huduma lazima alipe ushuru, awasilishe taarifa na hesabu sahihi, ahifadhi kumbukumbu, na atoe nyaraka zinapohitajika; baadhi ya malipo na makadirio yana muda maalum.
5.-(1) Mlipa ushuru wa huduma atakuwa na wajibu (a) kulipa ushuru wa huduma kwa kiwango kilichoainishwa katika Sheria Ndogo hii; (b) kuwasilisha taarifa sahihi za mauzo ya kila mwezi endapo anawasilisha taarifa za hesabu za mauzo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania; (c) kuwasilisha hesabu sahihi na za kweli; (d) kuwasilisha nyaraka au inayotakiwa kuwasilishwa kwa Halmashauri ndani ya muda ulioainishwa; taarifa (e) kutunza kumbukumbu za vitabu vya hesabu; (f) kuwasilisha kumbukumbu yoyote au nyaraka 2 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Mji Mafinga Tangazo La Serikali Na. 210 (Linaendelea) kwa ajili ya uchunguzi. (2) Mlipa ushuru wa huduma atalipa ushuru ndani ya siku kumi na nne tangu tarehe ya kuwasilisha taarifa za mauzo ya kila mwezi. (3) Bila kuathiri masharti ya aya ndogo ya (2), Halmashauri inaweza kukubaliana na mlipa ushuru wa huduma utaratibu wa kulipa ushuru. (4) Mlipa ushuru atawasilisha kwa Halmashauri hesabu za mwisho katika kipindi cha miezi mitatu tangu kumalizika kwa kipindi cha hesabu. (5) Endapo mlipa ushuru hatawasilisha hesabu za mwisho kwa mwaka wa fedha husika na ametakiwa kufanya hivyo kwa notisi ya siku thelathini, Mkurugenzi anaweza kwa kadiri atakavyoona inafaa, kufanya makadirio ya kiwango cha hesabu za mlipa ushuru huyo kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. (6) Endapo mlipa ushuru hatawasilisha majumuisho ya hesabu zake kwa mwaka wowote wa mapato, na endapo Mkurugenzi au afisa mwidhiniwa anaona kwamba mlipa ushuru huyo ana wajibu wa kulipa ushuru kwa mwaka huo, anaweza kwa kadiri atakavyoona inafaa kufanya makadirio ya kiwango cha hesabu za mlipa ushuru huyo, isipokuwa tathmini hiyo haitaathiri wajibu wowote wa mlipa ushuru chini ya Sheria Ndogo hii, kwa kushindwa kwake kuwasilisha hesabu hizo. (7) Ushuru unaotokana na makadirio kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii, utalipwa katika kipindi cha siku thelathini tangu tarehe ya kufanyika kwa makadirio hayo. Mamlaka ya Mkurugenzi - 6 Verify source ↗
(1) Endapo mlipa ushuru wa huduma anayetakiwa
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kutoa notisi na kuwataka walipa ushuru wa huduma kuwasilisha taarifa, rekodi, na vitabu vya hesabu ndani ya muda uliotajwa.
6.-(1) Endapo mlipa ushuru wa huduma anayetakiwa kuwasilisha taarifa ya mauzo chini ya Sheria Ndogo hii atashindwa kuwasilisha taarifa sahihi za mauzo kwa wakati, Mkurugenzi anaweza kutoa notisi ya kumtaka mlipa ushuru wa huduma kuwasilisha taarifa hiyo ndani ya siku thelathini kuanzia tarehe ya kutolewa kwa notisi. (2) Mkurugenzi anaweza kumtaka, kwa maandishi, taarifa kuhusu mfanyabiashara mtu yeyote mwenye 3 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Mji Mafinga Tangazo La Serikali Na. 210 (Linaendelea) anayepaswa kulipa ushuru wa huduma kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii kuwasilisha kwake taarifa ambazo zitatumika kama taarifa sahihi. (3) Mkurugenzi kwa maandishi, afisa mwidhiniwa kuingia kwenye jengo au eneo la mlipa ushuru wa huduma kwa nia ya kufanya uchunguzi wa kumbukumbu za biashara, vitabu vya hesabu na taarifa kwa madhumuni ya kufanya tathmini ya kiwango sahihi cha ushuru anachotakiwa kulipa. kumuagiza, anaweza (4) Mkurugenzi anaweza kumteua kamishna wa kodi ya forodha au kodi ya mapato kwa ajili ya kutathmini na kukusanya ushuru wa huduma na kuwasilisha Halmashauri kwa madhumuni ya kupata ushuru wa huduma pamoja na madeni yake. (5) Mkurugenzi, kwa notisi, anaweza kumtaka mlipa ushuru kuwasilisha taarifa za hesabu zikijumuisha taarifa kamili za shughuli za kibiashara zikionesha kiasi na thamani ya kifedha ya bidhaa au huduma zilizozalishwa, kutolewa, kusambazwa au kuuzwa pamoja na taarifa ya fedha ndani ya siku thelathini tangu tarehe ya notisi hiyo. (6) Mkurugenzi anaweza kutoa notisi ya siku saba kumtaka mlipa ushuru kuwasilisha kumbukumbu za kibiashara na vitabu vya hesabu kwa madhumuni ya kupata taarifa kwa ajili ya kufanya makadirio au kukusanya ushuru wa huduma. - 7 Verify source ↗
Bila kuathiri masharti ya sheria nyingine, ushuru
AI-assisted research summary: Service levy is to be collected under the Mafinga Town Council Fees and Charges By-laws, 2024, where it affects other laws.
7. Bila kuathiri masharti ya sheria nyingine, ushuru wa huduma utakusanywa kwa mujibu wa Sheria Ndogo ya Ada na Ushuru ya Halmashauri ya Mji Mafinga ya Mwaka 2024. - 8 Verify source ↗
Afisa mwidhiniwa anaweza
AI-assisted research summary: Afisa mwidhiniwa anaweza kupokea, kukubali, na kutathmini hesabu za mlipa ushuru, na pia kukataa hesabu za mwisho ikiwa ana sababu za msingi za kuamini kuwa si sahihi.
8. Afisa mwidhiniwa anaweza- (a) kupokea na kukubali hesabu za mlipa ushuru na kuzifanyia tathmini kuhusu kiwango cha hesabu cha mlipa ushuru endapo hesabu hizo zitakuwa si sahihi; (b) kukataa hesabu za mwisho iwapo atakuwa na sababu za msingi za kuamini kuwa hesabu hizo Ukusanyaji wa ushuru Mamlaka ya afisa mwidhiniwa 4 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Mji Mafinga Tangazo La Serikali Na. 210 (Linaendelea) si sahihi. Ukokotoaji wa ushuru wa huduma Makosa - 9 Verify source ↗
Ushuru wa huduma wa mlipa ushuru
AI-assisted research summary: Provision 9 appears to concern a taxpayer’s service tax and how it is calculated from sales information submitted to the Tanzania Revenue Authority, but the text is incomplete.
9. Ushuru wa huduma wa mlipa ushuru anaewasilisha taarifa za mauzo kwa Mamlaka ya Mapato taarifa Tanzania zinazowasilishwa na mlipa ushuru katika kipindi maalumu cha hesabu. utakokotolewa kuzingatia kwa - 10 Verify source ↗
Mtu anatenda kosa endapo mtu huyo
AI-assisted research summary: Mtu anaweza kufanya kosa akishindwa kuwasilisha taarifa za mauzo kwa Halmashauri, kutoa taarifa zisizo sahihi, kushindwa kulipa ushuru wa huduma kwa wakati, kushawishi mtu asilipe, kuzuia afisa mwidhiniwa, au kutoa taarifa ya uongo kuhusu jukumu la kulipa ushuru.
10. Mtu anatenda kosa endapo mtu huyo- (a) anashindwa kuwasilisha kwa Halmashauri taarifa mauzo ndani ya muda ulioainishwa katika Sheria Ndogo hii; (b) anawasilisha kwa Halmashauri taarifa zisizo sahihi; (c) anashindwa kulipa ushuru wa huduma ndani ya muda ulioainishwa katika Sheria Ndogo hii; (d) anamshawishi mlipa ushuru wa huduma kukataa au kukwepa kulipa ushuru; (e) anamzuia afisa mwidhiniwa kutekeleza masharti ya Sheria Ndogo hii; au (f) anatoa taarifa isiyokuwa sahihi kuhusu suala lolote linaloweza kuathiri jukumu lake au la mtu mwingine la kulipa ushuru. au wakala Adhabu Ufifilishaji makosa Kufutwa kwa TS Na. 37 la mwaka - 11 Verify source ↗
Mtu anayetenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii
AI-assisted research summary: A person convicted of an offence under this by-law is liable to a fine, imprisonment, or both.
11. Mtu anayetenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii akitiwa hatiani atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi laki mbili na isiyozidi shilingi milioni moja au kifungo kisichopungua miezi kumi na mbili na kisichozidi miezi ishirini na nne au vyote. - 12 Verify source ↗
Mkurugenzi anaweza kumtaka mtu aliyetenda
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kumtaka mtu aliyefanya kosa chini ya Sheria Ndogo hii alipe hadi shilingi laki mbili, ikiwa anakiri kosa kwa maandishi kwenye fomu maalumu ya Jedwali la Pili na yuko tayari kutimiza wajibu wake.
12. Mkurugenzi anaweza kumtaka mtu aliyetenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii kulipa kiasi kisichozidi shilingi laki mbili endapo mkosaji atakiri kosa kwa iliyoainishwa katika maandishi katika fomu maalumu Jedwali la Pili na kuwa tayari kutimiza wajibu wake kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii.
Part
Jedwali la Pili na kuwa tayari kutimiza wajibu wake kwa
- 13 Verify source ↗
Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya
AI-assisted research summary: The Mafinga Town Council service tax bylaw from 2017 is repealed.
13. Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Mji wa Mafinga ya Mwaka 2017 imefutwa. 5 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Mji Mafinga Tangazo La Serikali Na. 210 (Linaendelea) 2017 _________ JEDWALI LA KWANZA __________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 4(2)) VIWANGO VYA USHURU WA HUDUMA KWA WAFANYABIASHARA WASIOTUNZA KUMBUKUMBU. Namba Kiwango cha leseni kwa mwaka(Shilingi) Kiwango cha ushuru wa huduma (Shilingi)
Part
JEDWALI LA KWANZA
- 1 Verify source ↗
20,000
AI-assisted research summary: This text lists annual fee amounts for different value bands and provides a form for admitting an offence and agreeing to pay the tax due plus a fine.
1- 20,000 10,000.0 kwa mwaka 20,001-50,000 15,000.00 kwa mwaka 50,001-100,000 20,000.00 kwa mwaka 100,001-150,000 30,000.00 kwa mwaka 150,001- 200,000 40,000.00 kwa mwaka 200,001- 250,000 50,000.00 kwa mwaka 250,000 – na kuendelea 80,000.00 kwa mwaka ___________ JEDWALI LA PILI _____________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 12) FOMU YA KUFIFILISHA MAKOSA Mimi ……………………………………………………… nakiri kwa hiari yangu mwenyewe mbele ya …………………………………………. ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Mafinga, kwamba mnamo tarehe …… ya mwezi ……. Mwaka …… nilitenda kosa la kukiuka masharti ya aya ya ...........ya Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Mji Mafinga ya Mwaka 2024. Nipo tayari kulipa kiasi cha ushuru ninaodaiwa pamoja na faini. Nathibitisha kwamba maelezo hapo juu ni ya kweli na nimeyatoa mimi mwenyewe kwa hiari yangu kadri ya ufahamu wangu. Leo tarehe…………. Jina……………………………….. ya Mwezi…………..… Mwaka ……………. Saini……………………… MBELE YANGU: Jina: ……………………………………..…………………… Saini………………………….…………………………..……… 6 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Mji Mafinga Tangazo La Serikali Na. 210 (Linaendelea) Wadhifa: ………………………………………………………… Tarehe…………………………………………………………. Lakiri ya Halmashauri ya Mji Mafinga imegongwa kwenye Sheria Ndogo hizi kufutia azimio lililopitishwa katika Mkutano wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Mji Mafinga uliofanyika Tarehe 14 mwezi 02 Mwaka 2023 na kushuhudiwa Lakari hiyo ikigongwa mbele ya ;- AYOUBU J. KAMBI Mkurugenzi REGNANT Z. KIVINGE Mwenyekiti Halmashauri ya Mji Mafinga NAKUBALI L.S DODOMA MOHAMED OMARY MCHENGERWA (MB) Waziri wa Nchi – Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Na Serikali za Mitaa 31 Januari, 2024 7
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Mji Mafinga ya Mwaka 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in