Sheria Ndogo ya Afya na Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani ya Mwaka 2024
Kifungu hiki kinaweka jina la sheria hii kuwa Sheria Ndogo ya Afya na Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani ya Mwaka 2024.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Afya na Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani ya Mwaka 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
Kifungu hiki kinaweka jina la sheria hii kuwa Sheria Ndogo ya Afya na Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani ya Mwaka 2024. This section says the law applies throughout the area under the Mtwara-Mikindani Municipal Council. Sehemu hii inaweka maana ya maneno na taasisi muhimu zinazotumika katika sheria hii. Halmashauri must manage sanitation, health, and environmental work in its area and may assign, inspect, enforce, issue guidance, contract others, set waste disposal areas, and support community groups for waste control. Wamiliki au wapangaji wa nyumba za kuishi au biashara lazima watunze usafi wa eneo lao, wawe na chombo cha taka chenye kifuniko kinachofaa, na wazibe mifereji ya maji machafu ikiziba; pia mtu yeyote haruhusiwi kuweka taka yenye hatari kwa binadamu au inayoweza kusababisha moto au mlipuko.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Afya na Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani ya Mwaka 2024
Showing 29 of 29
- 1 Verify source ↗
Sheria hii itaijulikana kama Sheria Ndogo ya Afya
AI-assisted research summary: Kifungu hiki kinaweka jina la sheria hii kuwa Sheria Ndogo ya Afya na Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani ya Mwaka 2024.
1. Sheria hii itaijulikana kama Sheria Ndogo ya Afya na Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani ya Mwaka 2024. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria hii itatumika katika eneo lote lililo chini ya
AI-assisted research summary: This section says the law applies throughout the area under the Mtwara-Mikindani Municipal Council.
2. Sheria hii itatumika katika eneo lote lililo chini ya Mamlaka ya Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara- Mikindani. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria hii isipokuwa pale muktadha utahitaji
AI-assisted research summary: Sehemu hii inaweka maana ya maneno na taasisi muhimu zinazotumika katika sheria hii.
3. Katika Sheria hii isipokuwa pale muktadha utahitaji vinginevyo: “Ada ya uzoaji taka” maana yake ni malipo yanayotozwa na Halmashauri kwa ajili ya huduma ya uzoaji taka; “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni Afisa yeyote aliyeteuliwa na Mkurugenzi kwa lengo la kusimamia utekelezaji wa Sheria hii; “afya” maana yake hali timilifu ya kimwili, kiakili na kijamii na wala sio tu kutokuwa na ugonjwa au kilema; “chakula” maana yake kitu chochote kinacholiwa na kunywewa na binadamu isipokuwa dawa; (a) kitu chochote kinachobadili rangi ya chakula kama binzari n.k; (b) kitu chochote kinachoongeza ladha; au (c) kitu chochote kinachotumika katika matengenezo 1 Sheria Ndogo ya Afya Na Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara- Mikindani Tangazo La Serikali Na. 215 (Linaendelea) ya chakula; “chanzo cha maji” maana yake ni eneo lolote ambalo limetengwa kwa ajili ya kuwa chanzo cha maji kwa matumizi ya jamii ikiwemo visima, mito, chemchemi, vijito, na maeneo yote yanayopatikana maji; “choo” maana yake ni choo chochote cha maji chenye sakafu inayosafishika (kuvuta) au cha shimo; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara - Mikindani; “idhini” maana yake ni kibali cha maandishi kinachotolewa kwa mkazi yeyote wa Halmashauri anayekusudia kufanya ya Halmashauri; katika maeneo jambo fulani “kaya” maana yake mtu mzima anayejitegemea mwanamke au mwanaume, na mtoto au watoto inayoishi aidha kwenye nyumba nzima au ndani ya chumba kimoja kwenye eneo la Halmashauri; “kero au chukizo” maana yake ni kitu chochote ambacho kipo katika hali yoyote iwe kinatumika, kimewekwa, kimejengwa, au ni kichafu kiasi cha kusababisha: (a) harufu mbaya na ya kuudhi; (b) hatari kwa viumbe au maisha ya binadamu; (c) kelele za aina yoyote ile kama sauti kubwa ya redio au mziki; (d) magonjwa kwa binadamu, kuhifadhi mbu, inzi, panya na viumbe wenye madhara. “maduka” maana yake inajumuisha maduka ya bidhaa za nguo, vyakula, madawa, vifaa vya ujenzi na vioski pamoja na maduka mengine yaliyopo katika eneo la Halmashauri ambayo hayakutajwa; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara – Mikindani au Afisa yeyote atakayeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi; “mmiliki” maana yake ni mtu yeyote ambaye anamiliki ardhi, sehemu za starehe, nyumba za kulala wageni, 2 Sheria Ndogo ya Afya Na Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara- Mikindani Tangazo La Serikali Na. 215 (Linaendelea) Sura ya 191 Sura ya 191 Sura ya 191 Wajibu wa Halmasha uri nyumba za kuuzia vyakula, kumbi za starehe, mpangaji, wakala wa mpangishaji nyumba au jengo na makazi yoyote katika mtaa endapo mazingira husika ni mtaa au barabara za mitaani “pipa la taka” maana yake ni chombo chenye mfuniko cha kuhifadhia takataka kabla hazijatupwa au kuchomwa moto au kufukiwa shimoni; “shimo” maana yake ni shimo au ardhi iliyochimbwa kwa ajili ya kumwagia au kutupia uchafu au kupokea na kutia maji machafu; “taka” maana yake ni ile iliyoanishwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; “taka ngumu” kama ilivyo katika Sheria ya usimamizi mazingira; “uchafu Hatari” Kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya usimamizi wa Mazingira; “Wakala” maana yake ni mtu binafsi, kikundi, taasisi au kampuni iliyoteuliwa kukusanya ada na ushuru kwa niaba ya Halmashauri chini ya Sheria hii; - 4 Verify source ↗
(1) Halmashauri itakuwa na Wajibu wa
AI-assisted research summary: Halmashauri must manage sanitation, health, and environmental work in its area and may assign, inspect, enforce, issue guidance, contract others, set waste disposal areas, and support community groups for waste control.
4.-(1) Halmashauri itakuwa na Wajibu wa: (2) Kusimamia utekelezaji wa shughuli za usafi afya na mazingira. (3) Kutoa elimu kwa wananchi juu ya umuhimu wa kufuata kanuni za afya, usafi na kutunza mazingira. (4) Kuteua mtu yeyote, Wakala, kikundi, Taasisi kutekeleza shughuli za usimamizi wa afya, usafi na mazingira kwa niaba ya Halmashauri kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. (5) Kufanya ukaguzi ili kubaini endapo kanuni za afya, usafi na utunzaji wa mazingira zinazingatiwa ndani ya eneo la Halmashauri. (6) Kumchukulia hatua za kisheria mtu yeyote anayekiuka Sheria hii au Sheria nyingine inayohusiana na afya, usafi na usimamizi wa mazingira. (7) Kutunga kanuni, miongozo au kutoa maelekezo 3 Sheria Ndogo ya Afya Na Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara- Mikindani Tangazo La Serikali Na. 215 (Linaendelea) Kukusany a na kuhifadhi taka majumba ni yatakayosaidia kulinda Afya, usafi na Usimamizi wa Mazingira ndani ya eneo la Halmashauri. (8) Kuingia mkataba na mtu yeyote, taasisi au Kampuni kutelekeza shughuli za usimamizi wa afya, usafi na mazingira kwa niaba ya Halmshauri katika eneo ndani ya Halmashauri. (9)) Kutenga maeneo maalum kwa ajili ya kutupa takataka itakayojulikana kama dampo au ghuba na kutoa huduma ya uzoaji taka kwa malipo kutoka kwa wazalishaji. (10) Kuhamasisha uundaji wa vikundi vya kijamii na kuvitambua ili kuviwezesha kufanya shughuli za udhibiti wa taka ngumu pamoja na usafi wa mazingira katika mitaa baada ya kuingia mkataba na Halmashauri. - 5 Verify source ↗
(1) Itakuwa ni wajibu wa mtu yeyote anayemiliki
AI-assisted research summary: Wamiliki au wapangaji wa nyumba za kuishi au biashara lazima watunze usafi wa eneo lao, wawe na chombo cha taka chenye kifuniko kinachofaa, na wazibe mifereji ya maji machafu ikiziba; pia mtu yeyote haruhusiwi kuweka taka yenye hatari kwa binadamu au inayoweza kusababisha moto au mlipuko.
5.-(1) Itakuwa ni wajibu wa mtu yeyote anayemiliki nyumba au mpangaji wa nyumba ya kuishi au ya biashara: (a) kuweka chombo cha kuhifadhia taka chenye ukubwa unaotosheleza na kiwe na mfuniko unaofaa na kuhakikisha kwamba kinatumika. (b) kufagia na kuondoa uchafu au malundo ya uchafu na kuweka eneo linalozunguka nyumba yake katika hali ya safi; (c) kutunza na kuweka hali ya usafi vichochoro vyote vinavyomzunguka; (d) kupanda miti ya kivuli na matunda kwa ajili ya kuboresha mazingira katika eneo lake; na (e) kuzibua mifereji ya maji machafu nayozunguka au kupita kando ya nyumba yake au eneo lake la mara inapokuwa imeziba. (2) Haitaruhusiwa kwa mtu yeyote kuweka katika taka kitu kinachoweza kuleta chombo cha kuhifadhia madhara kwa binadamu au kusababisha moto au mlipuko. (3) Taka zote zihifadhiwe majumbani, sehemu ya biashara au Ofisi mpaka zitakapochukuliwa na Halmashauri au Wakala wake au mhusika azipeleke kwenye dampo 4 Sheria Ndogo ya Afya Na Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara- Mikindani Tangazo La Serikali Na. 215 (Linaendelea) liliotengwa kwa ajili ya kutupa taka. Kuhifadhi taka kwenye magari ya abiria Ada ya uzoaji taka - 6 Verify source ↗
(1) Itakuwa ni wajibu wa kila mmiliki wa chombo
AI-assisted research summary: Vehicle owners carrying passengers in the municipal area must provide a trash container and make sure passengers use it; passengers must not throw anything onto roads or other places in the municipal area.
6.-(1) Itakuwa ni wajibu wa kila mmiliki wa chombo cha usafiri kinachosafirisha abiria katika eneo la Halmashauri kuwa na chombo cha kuhifadhia taka na kuhakikisha kwamba abiria wanatupa taka zao humo. (2) Itakuwa ni kosa kwa abiria aliyeko ndani ya chombo chochote cha usafiri kutupa kitu chochote barabarani au sehemu yoyote katika eneo la Halmashauri. - 7 Verify source ↗
(1) Halmashauri itatoza ada ya uzoaji taka kutoka
AI-assisted research summary: Halmashauri inatoza ada ya uzoaji taka kwa kaya na majengo ya biashara, na malipo ya kila mwezi hulipwa tarehe 28 kwa Afisa Mwidhiniwa.
7.-(1) Halmashauri itatoza ada ya uzoaji taka kutoka kwa kila kaya au mwenye jengo la biashara kwa viwango vilivyoainishwa katika Jedwali la kwanza la Sheria hii. (2) Ada ya kila mwezi italipwa kila tarehe 28 ya kila mwezi ndani ya mwezi husika na italipwa kwa Afisa Mwidhiniwa stakabadhi ya malipo atatoa yatakayolipwa na atajaza katika rejesta ya wazalishaji taka. ambaye (3) Endapo mzalishaji taka atakuwa hajalipa ada ya mwezi kufikia tarehe 5 ya mwezi unaofuata atakuwa ametenda kosa. (4) Iwapo mzalishaji wa taka atashindwa kulipia gharama ya huduma ya uzoaji taka kwa kipindi cha miezi miwili mfululizo Halmashauri itamchukulia hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani. Wajibu wa kushiriki shughuli za usafi wa mazingira - 8 Verify source ↗
(1) Halmashauri imetenga kila siku ya Jumamosi
AI-assisted research summary: Halmashauri huweka Jumamosi ya mwisho ya kila mwezi kuwa siku ya usafi wa wananchi, na wananchi pamoja na baadhi ya wamiliki wa maeneo wanapaswa kushiriki na kusafisha mara kwa mara.
8.-(1) Halmashauri imetenga kila siku ya Jumamosi ya mwisho ya kila mwezi kuwa ni siku ya wananchi kushiriki usafi katika maeneo yatakayoainishwa na Halmashauri. (2) Kila mwananchi atahakikisha anashiriki katika shughuli za usafi wa mazingira katika siku iliyopangwa na Halmashauri. (3) Kila mmiliki wa nyumba au kiwanja au eneo lolote ambalo halijaendelezwa atakuwa na wajibu wa kufanya usafi katika eneo hilo mara kwa mara. 5 Sheria Ndogo ya Afya Na Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara- Mikindani Tangazo La Serikali Na. 215 (Linaendelea) Wajibu wa kutumia Vyoo Ujenzi wa vyoo vya umma - 9 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote au mmiliki wa nyumba au
AI-assisted research summary: Wamiliki au wapangaji wa nyumba lazima wahakikishe nyumba zina choo safi, imara na kinachotumika; vyoo vijengwe mbali na vyanzo vya maji ya binadamu, na wamiliki wa shule, mabweni, viwanda, migahawa, hoteli, sehemu za burudani au maeneo ya umma lazima wajenge vyoo vya wanawake na wanaume vyenye mwanga na hewa ya kutosha.
9.-(1) Mtu yeyote au mmiliki wa nyumba au mpangaji atahakikisha kwamba nyumba yake ina choo safi, imara na madhubuti kwa matumizi ya wakazi wa nyumba hiyo na kuhakikisha kinatumika wakati wote. (2) Choo kinatakiwa kijengwe umbali wa mita sitini kutoka katika kisima au chanzo chochote cha maji kinachotumika kwa matumizi ya binadamu; (3) Kila mtu anayemiliki shule, bweni, kiwanda, mgahawa, hoteli, sehemu za burudani au eneo lolote la umma atahakikisha anajenga vyoo kwa ajili ya matumizi ya wanawake na wanaume na kuhakikisha kuwa vyoo hivyo vina mwanga na hewa ya kutosha. - 10 Verify source ↗
(1) Halmashauri inaweza kumruhusu mtu binafsi,
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kuruhusu watu, vikundi, kampuni au taasisi kujenga vyoo vya umma katika maeneo itakayoona yanafaa.
10.-(1) Halmashauri inaweza kumruhusu mtu binafsi, vikundi vya watu, kampuni au taasisi kujenga vyoo vya umma katika maeneo ambayo itaona inafaa kwa ajili ya ujenzi huo. (2) Vyoo hivyo vitamilikiwa na Halmashauri au kwa ubia na mjenzi na vitakuwa ni vya kulipia kwa gharama zitakazoainishwa katika mkataba kati ya Halmashauri na wakala atakayeteuliwa kusimamia vyoo hivyo. Ilani ya kujenga choo - 11 Verify source ↗
(1) Afisa Mwidhiniwa atatoa
AI-assisted research summary: A health officer must give 30 days’ notice to the owner or tenant to repair toilet conditions when inspection finds no toilet, a full toilet, or one unfit for human use.
11.-(1) Afisa Mwidhiniwa atatoa ilani ya siku thelathini kwa mwenye nyumba au mpangaji kumtaka arekebishe hali ya choo chake, endapo katika ukaguzi wa afya itagundulika kuwa nyumba hiyo haina choo, choo kilichopo kimejaa au hakifai kwa matumizi ya binadamu. (2) Halmashauri itakuwa na uwezo wa kufunga choo chochote ambacho kitaonekana kichafu au cha kuhatarisha maisha ya binadamu na hakitaruhusiwa kutumika mpaka Halmashauri matengenezo yatakayofanyika. itakaporidhika na (3) Bila kuathiri masharti ya kanuni Ndogo ya (1) ya kanuni hii Halmashauri inaweza kuamuru nyumba au jengo hilo lisitumike kwa shughuli za makazi au biashara mpaka 6 Sheria Ndogo ya Afya Na Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara- Mikindani Tangazo La Serikali Na. 215 (Linaendelea) mmiliki wake atakapokuwa ametimiza maelekezo aliyopewa. Ilani ya kuondoa kero Utiririshaj i maji taka ya viwandan i yenye harufu na madhara Usafi wa mifereji ya maji ya mvua Mimea mirefu kutootesh wa mjini Ufugaji mjini - 12 Verify source ↗
(1) Endapo Afisa Mwidhiniwa atagundua kuwa
AI-assisted research summary: Afisa Mwidhiniwa akigundua kero kwenye eneo alilokagua, lazima atoe ilani ya siku 7 kwa wahusika wa eneo hilo ili waiondoe. Asiyetimiza masharti ya ilani ndani ya muda ulioonyeshwa anatenda kosa.
12.-(1) Endapo Afisa Mwidhiniwa atagundua kuwa eneo alilokagua lina kero yoyote, atatoa ilani ya siku saba (7) kwa mmiliki wa nyumba, mpangaji, mtumiaji na au mtu yeyote anayehusika akimtaka kuondoa kero hiyo. (2) Mtu yeyote atakayeshindwa kutekeleza masharti ya ilani aliyopewa ndani ya muda ulioainishwa kwenye ilani atakuwa ametenda kosa. - 13 Verify source ↗
(1) Kuendesha kiwanda kinachotoa maji taka bila
AI-assisted research summary: The provision prohibits operating a factory that releases wastewater, or causing harmful odours, if those effects are not controlled.
13.-(1) Kuendesha kiwanda kinachotoa maji taka bila ya kudhibiti yasisababishe madhara kwa watu wengine. (2) Kuruhusu maji taka toka viwandani, au eneo lolote kuingia katika vyanzo vya maji safi, maeneo ya wazi au ardhini bila kudhibitiwa. (3) Kusababisha harufu yenye madhara inayotokana na shughuli zinazofanyika katika eneo hilo. - 14 Verify source ↗
Kila mmiliki wa nyumba atatakiwa kuondoa
AI-assisted research summary: Kila mmiliki wa nyumba lazima aondoe uchafu kwenye mfereji wa maji ya mvua unaopita karibu na nyumba, eneo la biashara, au kiwanja chake, na aueke mfereji huo safi kila wakati.
14. Kila mmiliki wa nyumba atatakiwa kuondoa uchafu kama vile mchanga, majani, nyasi au vitu vinavyofanana na hivyo kwenye mfereji wa maji ya mvua unaozunguka au kupita kando ya nyumba yake au eneo la biashara yake, kiwanja chake na kuhakiksha mfereji huo unakuwa safi siku zote. - 15 Verify source ↗
Mtu yeyote hataruhusiwa kupanda au kuotesha
AI-assisted research summary: Mtu yeyote haruhusiwi kupanda au kuotesha mazao au mimea mirefu inayozidi futi 3 katika maeneo ya mjini na maeneo mengine yaliyopigwa marufuku na Halmashauri.
15. Mtu yeyote hataruhusiwa kupanda au kuotesha mazao au mimea mirefu yanayozidi futi tatu (3) katika maeneo ya mjini pamoja na maeneo mengine yaliyozuiliwa na Halmashauri. - 16 Verify source ↗
Ufugaji unaoruhusiwa mjini ni ufugaji wa ndani
AI-assisted research summary: In town, livestock keeping is allowed only in an enclosed pen or in designated grazing areas, considering the number of animals allowed for the size of the area.
16. Ufugaji unaoruhusiwa mjini ni ufugaji wa ndani ya zizi kwa kuzingatia idadi ya mifugo inayoruhusiwa kulingana na ukubwa wa eneo au katika maeneo yaliyotengwa kama malisho ya mifugo. Wajibu - 17 Verify source ↗
(1) Kila mfugaji atakuwa na wajibu wa
AI-assisted research summary: Kila mfugaji lazima ahakikishe mifugo yake haizururi ovyo, eneo la kufugia linabaki safi, uchafu wa mifugo unakusanywa na kutupwa vizuri, mifugo haiharibu mali, inapewa chanjo inapohitajika, na kusafirishwa ndani ya Halmashauri kwa kibali maalum.
17.-(1) Kila mfugaji atakuwa na wajibu wa 7 Sheria Ndogo ya Afya Na Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara- Mikindani Tangazo La Serikali Na. 215 (Linaendelea) wa wafugaji kuhakikisha kwamba: (2) Mifugo yake haizururi ovyo mitaani, barabarani au kuchungwa katika maeneo yasiyoruhusiwa. (3) Sehemu anayotumia kufugia inakuwa katika hali ya usafi wakati wote. (4) Anakusanya uchafu wowote utokanao na mifugo kama vile kinyesi, nyasi au mabaki ya vyakula na kwenda kutupwa kwenye dampo au ghuba au kupelekwa shambani kama mbolea. (5) Mifugo yake haiharibu miti, mazao au maua katika bustani za Halmashauri au mali ya mtu mwingine yeyote. (6) Mifugo yake inapatiwa chanjo kila inapohitajika ili kuzuia magonjwa mbalimbali. (7) Kusafirisha mifugo kutoka eneo moja la Halmashauri kwenda eneo jingine kwa kibali maalum cha Halmashauri. Udhibiti wa mifugo - 18 Verify source ↗
(1) Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kuamuru
AI-assisted research summary: The Director may order livestock to be moved if the keeping of the animals violates this law or the town planning law and causes nuisance to nearby residents.
18.-(1) Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kuamuru mifugo ihamishwe ikiwa ufugaji huo unakinzana na masharti ya Sheria hii pamoja na Sheria ya Mipango Miji na kusababisha kero kwa wakazi wa maeneo husika. (2) Halmashauri itakamata mfugo au mifugo yoyote katika maeneo inazurura ovyo itakayoonekana yasiyoruhusiwa kuchungia mifugo. (3) Mifugo au mfugo uliokamatwa chini ya kanuni Ndogo ya (2) ya kanuni hii utalipiwa faini pamoja na gharama za utunzaji. (4) Endapo mwenye mfugo au mifugo iliyokamatwa hataonekana ndani ya muda wa siku tangu kukamatwa kwa mfugo au mifugo hiyo Mkurugenzi atauza mfugo au mifugo hiyo kwa njia ya mnada baada ya kupata kibali cha Mahakama. tatu (3) (5) Baada ya mauzo Mkurugenzi atakata fedha za faini, gharama za mnada, ulinzi na fedha zitakazobaki 8 Sheria Ndogo ya Afya Na Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara- Mikindani Tangazo La Serikali Na. 215 (Linaendelea) Utengene zaji na uuzaji wa vyakula, matunda na miwa atapewa mwenye mfugo au mifugo na endapo hataonekana ndani ya muda wa siku saba fedha hizo zitaingizwa kwenye vyanzo vya mapato ya Halmashauri. (6) Endapo kutatokea kufa kwa mfugo au mifugo Halmashauri haitawajibika na ulipaji wa gharama zozote isipokuwa kama kufa kwa mfugo huo kumesababishwa na uzembe wa watumishi wa Halmashauri au Wakala. (7) Mbwa watakaozurura na ambao hawatachanjwa watauwawa kwa kupigwa risasi. - 19 Verify source ↗
(1) Itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote
AI-assisted research summary: Hii inakataza mtu yeyote kuuza au kutengeneza chakula katika maeneo fulani bila kibali cha Afisa Afya, na inaweka wajibu wa usafi na uhifadhi kwa wauzaji wa vyakula vya kupikwa na wafanyabiashara wa matunda au miwa.
19.-(1) Itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote: (a) kutengeneza kuchoma, kupima, kuchemsha au kuuza chakula cha aina yoyote mahali popote mtaani, uchochoroni, magengeni au kwenye nyumba yoyote mpaka awe ametimiza masharti na kanuni za afya kwa kupata kibali cha Afisa Afya wa Halmashauri. (b) kuuza vyakula visivyopikwa vikiwa vimewekwa chini na kuhakikisha vyakula vyote vinawekwa juu ya meza. (c) kuuza vileo vya aina yoyote kwenye makazi au katika maeneo ambayo hayakutengwa maalum kwa shughuli hizo. (d) kufanya biashara ya matunda au miwa katika sehemu zisizoruhusiwa na Halmashauri. (2) Mtu yeyote anayeendesha biashara ya vyakula vya kupikwa au kukaangwa atakuwa na wajibu wa kuhakikisha kuwa vyakula hivyo vinahifadhiwa kwa namna inayozuia nzi, vumbi na wadudu waletao madhara kwa afya ya binadamu. (3) Kila mfanyabiashara ya matunda au miwa atakuwa na wajibu wa kuhakikisha kuwa ana chombo maalum cha kuhifadhi mabaki ya maganda au matunda. Machinjio
Part
sehemu zisizoruhusiwa na Halmashauri.
- 20 Verify source ↗
Kila mmiliki wa duka la kuuzia nyama atakuwa na
AI-assisted research summary: Mmiliki wa duka la kuuzia nyama lazima ahakikishe duka lake lina masharti ya usafi na vifaa vilivyoorodheshwa, na muuzaji apime afya kila baada ya miezi sita.
20. Kila mmiliki wa duka la kuuzia nyama atakuwa na 9 Sheria Ndogo ya Afya Na Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara- Mikindani Tangazo La Serikali Na. 215 (Linaendelea) na maduka ya nyama Kuuza na kuchinja nyama mahali pasiporuh usiwa Uzuiaji wa shughuli wakati wa magonjw a ya mlipuko Ukamataj i wa vyombo vilivyotu mika kuhifadhi a chakula wajibu wa kuhakikisha kuwa duka lake: (a) Ni jengo la kudumu lililosakafiwa kwa marumaru nyeupe; (b) Lina maji safi na misumeno ya kukatia nyama; (c) Lina kabati la vioo na jokofu la kuhifadhia nyama na sehemu ya mizani; (d) Kuna pipa la kuhifadhia takataka; (e) Muuzaji ana vazi jeupe pamoja na apron nyeupe; (f) Muuzaji anapima afya kila baada ya miezi sita. - 21 Verify source ↗
Mtu yeyote hataruhusiwa kuchinja au kuuza
AI-assisted research summary: Mtu yeyote haruhusiwi kuchinja au kuuza nyama au kuwa na duka la nyama katika maeneo yasiyoruhusiwa na Halmashauri.
21. Mtu yeyote hataruhusiwa kuchinja au kuuza nyama ya aina yoyote au kuwa na duka la nyama katika maeneo yasiyoruhusiwa na Halmashauri. - 22 Verify source ↗
Afisa Mwidhiniwa anaweza kutoa amri ya kuzuia
AI-assisted research summary: Afisa Mwidhiniwa anaweza kuzuia baadhi ya shughuli ikiwa ana sababu ya kuamini zinaweza kueneza magonjwa ya mlipuko na kuathiri maisha ya binadamu.
22. Afisa Mwidhiniwa anaweza kutoa amri ya kuzuia shughuli kama vile utengenezaji wa vyakula, pombe, sherehe na mikusanyiko yoyote ile kwa kutangaza kwa njia ya kipaza sauti, maandishi au kupitia vyombo vya habari endapo atakuwa na sababu ya kuamini kwamba shughuli hiyo inaweza kusababisha kuenea kwa magonjwa ya mlipuko na kuleta athari kwa maisha ya binadamu. - 23 Verify source ↗
(1) Halmashauri
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kukamata vyakula, vyombo na vifaa vinavyotumika kuhifadhia chakula baada ya kutoa amri ya kuzuia shughuli hiyo. Mtu anayekataa kutii amri hiyo atakuwa ametenda kosa.
23.-(1) Halmashauri inaweza kukamata vyakula, vyombo na vifaa vingine vyovyote vitakavyotumika kuhifadhia chakula baada ya kutolewa amri ya kuzuia kufanyika kwa shughuli hiyo na Halmashauri haitahusika na gharama zozote zitakazotokea wakati wa utekelezaji wa amri hiyo. (2) Mtu yeyote atakayekataa kutii amri iliyotolewa atakuwa ametenda kosa kwa mujibu wa Sheria hii. Ada ya ukaguzi wa afya - 24 Verify source ↗
Halmashauri itatoza ada ya ukaguzi wa afya
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima itozeshe ada ya ukaguzi wa afya, inayolipwa kila mwaka kabla ya mwombaji kupewa leseni ya biashara.
24. Halmashauri itatoza ada ya ukaguzi wa afya ambayo italipwa kwa mwaka kabla ya mwombaji kupewa leseni ya biashara kwa viwango vitakavyoainishwa katika 10 Sheria Ndogo ya Afya Na Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara- Mikindani Tangazo La Serikali Na. 215 (Linaendelea) Jedwali la pili la Sheria hii. Uwezo wa Afisa Mwidhini wa
Part
Jedwali la pili la Sheria hii.
- 25 Verify source ↗
Afisa Mwidhiniwa atakuwa na uwezo wa kuingia
AI-assisted research summary: Afisa Mwidhiniwa ana uwezo wa kuingia katika maeneo au majengo yaliyo ndani ya eneo la Halmashauri na kufanya ukaguzi wa usafi kati ya saa 12 asubuhi na saa 12 jioni.
25. Afisa Mwidhiniwa atakuwa na uwezo wa kuingia katika eneo, jengo lolote lililopo katika eneo la Halmashauri na kufanya ukaguzi wa usafi kuanzia Saa kumi na mbili kamili asubuhi hadi Saa kumi na mbili kamili jioni. Makosa - 26 Verify source ↗
Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa kwa mujibu
AI-assisted research summary: Anyone who interferes with an authorised officer, refuses fees or council orders, or engages in listed sanitation and pollution-related acts commits an offence.
26. Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa kwa mujibu wa Sheria hii endapo: (a) atamzuia au kujaribu kumzuia Afisa Mwidhiniwa asitekeleze majukumu yake chini ya Sheria hii. (b) atashindwa, atadharau, atakwepa au atakataa kulipa ada au kutekeleza agizo lolote alilopewa na Halmashuri kwa mujibu wa Sheria hii. (c) atamshawishi mtu au kundi la watu kukataaa au kukwepa kulipa ada. (d) atamwaga takataka katika mtaa, mtaro wa maji ya mvua, uchochoroni au mahali popote hadharani au katika eneo idhini ya Halmashauri. la wazi bila lolote (e) atatiririsha maji machafu barabarani au katika eneo la nyumba ya jirani. (f) atakataa kufanya usafi siku iliyopangwa na Halamshauri. (g) ataosha magari, kufua, kunywesha mifugo na kukoroga dawa za mimea ndani ya mito, mabwawa, lambo au ndani ya chanzo cha maji au ya kisima binadamu. kwa matumizi kinachotumika (h) atafanya matengenezo ya magari, pikipiki na mitambo, kuendesha shughuli za viwanda katika maeneo ya wazi, makazi, barabarani, uchochoroni au katika maeneo yasiyotengwa kwa shughuli hizo bila kuzingatia taratibu za mipango miji. (i) ataenda haja ndogo au kubwa hovyo barabarani, 11 Sheria Ndogo ya Afya Na Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara- Mikindani Tangazo La Serikali Na. 215 (Linaendelea) uchochoroni au mahali popote ambapo siyo chooni. Adhabu Kufifilish a kosa - 27 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayevunja masharti yaliyowekwa
AI-assisted research summary: Anyone who breaches the rules in this by-law commits an offence and, if convicted, may be fined up to 300,000 shillings, imprisoned for up to 12 months, or receive both penalties.
27. Mtu yeyote atakayevunja masharti yaliyowekwa na Sheria Ndogo hii atakuwa ametenda kosa na akipatikana na hatia atatozwa faini isiyozidi shilingi laki tatu au kifungo kisichozidi miezi kumi na mbili (12) jela au adhabu zote mbili kwa pamoja yaani faini na kifungo. - 28 Verify source ↗
Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa ikiwa mkosaji anakiri kwa hiari kwa maandishi, anajaza fomu maalum, na analipa faini ya shilingi 200,000.
28. Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha kosa iwapo mkosaji atakiri kosa kwa hiyari yake mwenyewe kwa maandishi kwa kujaza fomu maalum iliyoambatishwa kwenye Jedwali la Tatu la Sheria Ndogo hii na kulipa faini ya kiasi cha shilingi laki mbili. ____________ JEDWALI LA KWANZA ________________ (Limetengenezwa chini ya Aya ya 7(1) ADA YA UZOAJI TAKA Eneo Na.
Part
JEDWALI LA KWANZA
- 3 Verify source ↗
Mashine ya kukamua mafuta ya alizeti
AI-assisted research summary: Huu ni jedwali la ada za mwezi na ada za ukaguzi wa afya kwa aina mbalimbali za biashara, pamoja na fomu ya kukiri kosa mbele ya Mkurugenzi.
3. Mashine ya kukamua mafuta ya alizeti 4 Maduka la jumla 5 Migahawa(Restaurant) 6 Mashine za kukoboa/kusaga 7 Vilabu vya pombe za kienyeji, baa, grocery, 12 Kiwango cha Ada kwa mwezi (Shilingi) 2,000.00 5,000.00 5,000.00 10,000.00 5,000.00 10,000.00 4,000.00 Sheria Ndogo ya Afya Na Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara- Mikindani Tangazo La Serikali Na. 215 (Linaendelea) 8 Mama lishe/Baba lishe, Nyama choma/chipsi inayojitegemea 9 Viwanda vya uselemala na mashine za mbao 10 Bucha (Maduka ya Nyama na samaki) 11 Nyumba za kulala wageni 12 Saluni (Ususi/Vinyozi) 13 Gereji 14 Godown (Ghala) 15 Kituo cha kuuza mafuta(Filling station) 16 Ofisi za Taasisi mbalimbali 17 Hoteli 18 Stoo za mkaa 19 Mafundi kushona nguo 20 Mafundi vyuma (wahunzi) 21 Kumbi za starehe,sinema 22 Majengo ya kuoshea magari/pikipiki 23 Zahanati/kituo cha afya au hospitali 24 Majengo mengine yasiyotajwa _____________ JEDWALI LA PILI ______________ 13 2000.00 10,000.00 5,000.00 4,000.00 3,000.00 10,000.00 7,000.00 10,000.00 5,000.00 10,000.00 5,000.00 3,000.00 5,000.00 5,000.00 5,000.00 20,000.00 20,000.00 Sheria Ndogo ya Afya Na Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara- Mikindani Tangazo La Serikali Na. 215 (Linaendelea) (Limetengenezwa chini ya Aya ya 24) ADA YA UKAGUZI WA AFYA Na Aina ya biashara 1 Baa na maduka ya vinywaji 2 Mama lishe 3 Nyumba za wageni na hosteli 4 Kumbi za starehe au mikutano 5 Majengo mengine ya biashara 6 7 8 9 Eneo la kugelea Eneo la kuoga Eneo la chakula Karakana 10 Hoteli 11 Night club Kiwango cha Ada kwa mwaka (Shilingi) 5,000.00 2,500.00 30,000.00 10,000.00 10,000.00 10,000.00 10,000.00 10,000.00 10,000.00 50,000.00 50,000.00 _____________ JEDWALI LA TATU ______________ (Limetengenezwa chini ya Aya ya 28) FOMU YA KUKIRI NA KUFIFILISHA KOSA Mimi…………………………………………. nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya …………………………ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara – Mikindani kwamba mnamo tarehe……………ya mwezi……………..Mwaka ……………………….nilitenda kosa la kukiuka masharti ya Aya ya ………………………ya 14 Sheria Ndogo ya Afya Na Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara- Mikindani Tangazo La Serikali Na. 215 (Linaendelea) Sheria Ndogo ya (Afya, Usafi na Usimamizi wa Mazingira) ya Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara – Mikindani ya mwaka 2024. Kwa mamlaka aliyopewa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara – Mikindani, niko tayari kulipa kiasi cha Ada au Ushuru ninayodaiwa pamoja na faini. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU Leo tarehe…ya mwezi……………Mwaka……. Jina…………………………………..….. Saini…………………………………..…. Mbele ya: Jina……………………………………….. Cheo……………………………………… Saini……..……………………………….. Tarehe: …………………………………. 15 Sheria Ndogo ya Afya Na Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara- Mikindani Tangazo La Serikali Na. 215 (Linaendelea) Lakiri ya Halmashauri ya manispaa ya Mtwara- Mikindani imebandikwa kwenye Sheria Ndogo hizi kufutia azimio lililopitishwa kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani uliofanyika Tarehe 07 mwezi Oktoba, Mwaka 2022 mbele ya ;- MWL. HASSAN. B. NYANGE Mkurugenzi wa Manispaa Mtwara- Mikindani MHE. SHADIDA ALLY NDILE Mstahiki Meya wa Manispaa Mtwara -Mikindani NAKUBALI L.S Dodoma, MOHAMED OMARY MCHENGERWA 2 February, 2024 Waziri wa Nchi- Ofisi ya Rais (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa) 16
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Afya na Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani ya Mwaka 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in