Sheria Ndogo ya Mji wa Kihistoria wa Mikindani na maeneo mengine ya Urithi yaliyohifadhiwa ya Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani za Mwaka 2024
This provision states the name of the bylaw.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Mji wa Kihistoria wa Mikindani na maeneo mengine ya Urithi yaliyohifadhiwa ya Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani za Mwaka 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This provision states the name of the bylaw. This provision says the law applies throughout the area of the Mtwara–Mikindani Municipal Council authority. Kifungu hiki kinafafanua istilahi muhimu zinazotumiwa katika Sheria Ndogo hii. Vitu vilivyoorodheshwa chini ya Sheria hii vinatambuliwa kama vya thamani ya urithi na vinapaswa kuhifadhiwa. No person or organization may carry out prohibited activities in the historic conservation area of Mikindani, or in any other area of the Council designated for conservation, unless the Director of National Museums has approved them.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Mji wa Kihistoria wa Mikindani na maeneo mengine ya Urithi yaliyohifadhiwa ya Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani za Mwaka 2024
Showing 30 of 30
- 1 Verify source ↗
Sheria hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya
AI-assisted research summary: This provision states the name of the bylaw.
1. Sheria hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Mji wa Kihistoria wa Mikindani na maeneo mengine ya urithi yaliyohifadhiwa ya Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani za Mwaka 2024. - 2 Verify source ↗
Sheria hii itatumika katika eneo lote la
AI-assisted research summary: This provision says the law applies throughout the area of the Mtwara–Mikindani Municipal Council authority.
2. Sheria hii itatumika katika eneo lote la Mamlaka ya Halmashauri ya Manispaa yaMtwara– Mikindani. - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii
AI-assisted research summary: Kifungu hiki kinafafanua istilahi muhimu zinazotumiwa katika Sheria Ndogo hii.
3. Katika Sheria Ndogo hii isipokwa pale Muktadha utahitaji vinginevyo: - “eneo la Hifadhi ya Urithi” maana yake eneo lote lilioainishwa lililotengwa na Halmashauri maalum kwa madhumuni ya Uhifadhi wa Urithi wa kiutamadauni; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara – Mikindani; “jengo la nyongeza” maana yake ni maboresho katika au matumizi jengo kuu eneo yaliyokusudiwa ni saidizi kwa linalopatikana katika eneo hilo; ambalo matumizi “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni Afisa yeyote la aliyeteuliwa na Mkurugenzi kwa kusimamia utekelezaji wa Sheria hii; lengo “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi wa 1 Sheria Ndogo ya Mji wa Kihistoria wa Mikindani Na Maeneo Mengine ya Urithi Yaliyohifadhiwaya Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani Tangazo La Serikali Na. 218 (Linaendelea) Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara – Mikindani au Afisa yeyote atakayeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi; “shughuli zilizokatazwa” maana yake ni upanuzi, umaliziaji, kazi za ujenzi, ubomoaji, uwekaji alama, ukarabati, kazi za kimuundo, kazi za usanifu na kazi nyingine zozote zinayofanyika bila ruhusa ya mkurugenzi kwa madhumuni ya uhifadhi chini ya Sheria hii; “mambo ya kale” inajumusiha majenzi, masalia na mikusanyo iliyohifadhiwa; “mikusanyo ya kiethnografia” maana yake ni mkusanyo wowote uliotengenezwa, unaohamishika kuundwa, kupakwa rangi, kuchongwa, kuandikwa au vinginevyo kuzalishwa au kuboreshwa na mwanadamu, katika Tanzania baada ya mwaka 1863, kwa matumizi katika shughuli yoyote ya kijamii au ya kiutamaduni, iwe au bado unatumiwa na jamii yoyote katika Tanzania, ila haijumuishi mkusanyo wowote uliotengenezwa, kuundwa, kupakwa rangi, kuchongwa, kuandikwa au vinginevyo kuzalishwa au kuboreshwa na mwanadamu kwa ajili ya kuuzwa kama ukumbusho; “Majenzi ya kihistoria” maana yake ni na yanajumuisha- (a) Jengo lolote, ngome, “interment”, “midden”, bwawa, au muundo wowote ulioinuliwa, kujengwa au kuundwa na mwanadamu katika Tanzania kabla ya mwaka 1863; (b) Michoro yoyote ya mapangoni au mkusanyo mwingine wowote usiohamishika, kuchongwa sanamu, kuchongwa, kukatwa, au kuboreshwa na mwanadamu katika Tanzania kabla ya mwaka 1863; (c) boma la udongo (earth work), mfereji, mlango wa kuingilia, kisima, pango, handaki au 2 Sheria Ndogo ya Mji wa Kihistoria wa Mikindani Na Maeneo Mengine ya Urithi Yaliyohifadhiwaya Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani Tangazo La Serikali Na. 218 (Linaendelea) maboresho mengine yoyote, ya kuchimba udongo au miamba, yaliyochimbwa au yaliyobuniwa vinginevyo na mwandamu katika Tanzania kabla ya mwaka 1863, iwe au la majenzi yaliyoboreshwa, kuongezewa au kurejeshwa katika tarehe ya mbele na iwe au limejumuishwa katika orodha iliyochapishwa na Mkurugenzi wa Mambo ya Kale; Sura 333 (d) eneo au muundo wowote usiohamishika uliotangazwa kuwa mkusanyo wa kihistoria chini ya kifungu cha 3 cha Sheria ya Malikale; inavyoweza kuhitajika kwa dhumuni la uzio, kufunika au vinginevyo kuhifadhi majenzi ya kihistoria; inayoungana (e) ardhi kama “masalia” maana “makumbusho” maana yake ni taasisi za kielimu na kiutamadumi kwa ajili ya ukusanyaji, uhifadhi na utafiti wa vitu vya kisayansi na kiutamaduni; “mikusanyo iliyohifadhiwa” maana yake ni mkusanyo wowote wa kiethnografia au mlango wa mbao au fremu yoyote ya mlango iliyochongwa katika Tanzania, katika mtindo wa kiafrika au wa kiutamaduni kabla ya mwaka 1940; yake ni mkusanyo wowote kuundwa, unaohamishika kupakwa rangi, kuchongwa, kuandikwa au vinginevyo kuzalishwa au kuboreshwa na mwanadamu, katika Tanzania baada ya mwaka 1863, iwe au umeboreshwa, kuongezewa au kurejeshwa katika tarehe ya mbele na inajumusha mwanadamu, au viumbe wengine wenye uti wa mgongo, visukuku au mabaki yoyote ya wanyama na mimea, inayopatikana katika Tanzania; “sifa za usanifu” maana yake ni upande, ukuta, nyuso za kuta kona za bodi, mabano, nguzo, nguzo chomozi, madirisha milango, mazingira ya dirisha na mlango au wigo wa mlango, mchomozo, uliotengenezwa, 3 Sheria Ndogo ya Mji wa Kihistoria wa Mikindani Na Maeneo Mengine ya Urithi Yaliyohifadhiwaya Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani Tangazo La Serikali Na. 218 (Linaendelea) zinara, kenchi pambo, uzio na mapambo, umaliziaji, rangi, vifaa vyake vya usanifu na sifa sawa zingine zote za nje; “sura” inajumuisha sifa za usanifu na za sura ya nchi; “vibali vya ukarabati” maana yake ni kibali kilichoidhinishwa na Makumbusho ya Taifa ya Tanzania na ikiwa kuna ulazima anaweza kumtaarifu Mkurugenzi baada ya kutoa kibali; “sifa za sura ya Nchi” maana yake ni uzio, ukuta wa kuzuia, chemchemi, baraza, mfereji, sanamu, au sifa zingine, ambazo zinapatikana katika eneo na nje ya kuta za nje za jengo; “thamani ya urithi” maana yake ni thamani au manufaa ya mali ya kijamii, kihistoria, kiutamaduni, kiusanifu, kisayansi au kielimu au umuhimu wa matumizi yake; na - 4 Verify source ↗
Kwa madhumuni ya uhifadhi chini ya Sheria
AI-assisted research summary: Vitu vilivyoorodheshwa chini ya Sheria hii vinatambuliwa kama vya thamani ya urithi na vinapaswa kuhifadhiwa.
4. Kwa madhumuni ya uhifadhi chini ya Sheria hii majengo yote, miundombinu, majengo ya kihistoria, majenzi, masalia, mikusanyo na maeneo mengine chini ya Sheria hii yameainishwa kuwa na thamani ya urithi na kwa hiyo yanahifadhiwa kwa mujibu wa Sheria hii. - 5 Verify source ↗
Hakuna mtu, watu au kundi la watu, shirika,
AI-assisted research summary: No person or organization may carry out prohibited activities in the historic conservation area of Mikindani, or in any other area of the Council designated for conservation, unless the Director of National Museums has approved them.
5. Hakuna mtu, watu au kundi la watu, shirika, taasisi au chombo kingine cha aina yoyote kitakachoweza kutekeleza, kufanya au kitasababisha kutekelezwa au kufanyika shughuli zilizokatazwa katika eneo la hifadhi la mji wa kihistoria wa Mikindani au eneo lingine lolote ndani ya Halmashauri ambalo limeainishwa kama eneo la isipokuwa kama shughuli hizo, au matendo urithi mengine na Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa. yameidhinishwa Mikusanyo iliyoorodheshwa Uhifadhi wa Urithi Makatazo - 6 Verify source ↗
Hakuna mtu yeyote, kikundi cha watu au taasisi
AI-assisted research summary: Watu, vikundi vya watu na taasisi haziruhusiwi kufanya vitendo fulani ndani ya maeneo ya urithi yaliyohifadhiwa.
6. Hakuna mtu yeyote, kikundi cha watu au taasisi atakayeruhusiwa kufanya yafuatayo ndani ya maeneo ya urithi yaliyohifadhiwa: (a) kubomoa, au kuruhusu kuharibu au kuruhusu au jengo, muundo kubomolewa kwa 4 Sheria Ndogo ya Mji wa Kihistoria wa Mikindani Na Maeneo Mengine ya Urithi Yaliyohifadhiwaya Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani Tangazo La Serikali Na. 218 (Linaendelea) muonekano ambao uko katika eneo la hifadhi ya urithi au jengo, muundo au muonekano ambao ni mali ya urithi uliyohifadhiwa; (b) kujenga, au kuruhusu kuharibu au kuruhusu ujenzi wa jengo, muundo ambao uko katika eneo la hifadhi ya urithi; (c) kukarabati jengo kwa kutumia vifaa vingine tofauti na vifaa vya asili (d) kutupa taka za aina yoyote isipokuwa katika kasha lililotolewa kwa ajili hiyo; (e) kuteketeza, kuharibu, kujeruhi, kuchana au kuondoa mti, kichaka, nyasi au uoto mwingine uliopo; (f) kuharibu, kuchana au kuondoa ubao wa matangazo, alama ya ishara au jengo lolote au muundo wowote uliojengwa kihalali; (g) kuondoa au kwa namna yoyote kuharibu mwamba wowote kutoka sehemu yake ya asili; (h) kuhamisha au kwa namna yoyote kuharibu kitu chochote kiwe cha bandia au si cha bandia kutoka sehemu yake sahihi; (i) kusababisha moto kwenye nyasi, mimea ya chini au miti ya eneo linalozunguka; na (j) kusababisha au kufanya maandishi ya aina yoyote; - 7 Verify source ↗
Mkurugenzi wa Manispaa au Afisa yeyote
AI-assisted research summary: Mkurugenzi wa Manispaa au afisa aliyeidhinishwa hapaswi kuwajibishwa kwa vitendo au kutotenda vinavyohusiana na utekelezaji wa majukumu yake chini ya Sheria hii, isipokuwa kama hali hiyo imesababishwa na zembe.
7. Mkurugenzi wa Manispaa au Afisa yeyote aliyeidhinishwa hawatakabiliwa kwa kitendo au mienendo mingine yoyote kuhusiana na kitendo chochote alichofanya, au hakufanya ambacho hakijasababishwa na zembe wakati wa utekelezaji wa majukumu yake kwa mujibu wa Sheria hii. - 8 Verify source ↗
Kwa dhumuni
AI-assisted research summary: Mkururugenzi anaweza kuzingatia mambo kadhaa anaposhughulikia vibali vya kuboresha urithi kwa mali ya urithi iliyotambuliwa.
8. Kwa dhumuni jengo, muonekano, mali, eneo au sehemu inaweza kuwa na tabia za urithi au thamani ya urithi chini ya sheria ndogo hizi, la kuamua kama 5 Fidia Thamani ya Urithi Sheria Ndogo ya Mji wa Kihistoria wa Mikindani Na Maeneo Mengine ya Urithi Yaliyohifadhiwaya Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani Tangazo La Serikali Na. 218 (Linaendelea) Vibali vya Kuboresha Urithi Upataji wa vibali vya kuboresha urithi kwa mali ya urithi iliyoainishwa Mkururgenzi anaweza kuzingatia yafuatayo: (a) usanifu, historia, utamaduni, jamii au kiimani umuhimu au ubora wa jengo, muonekano, mali, eneo au sehemu; (b) umri wa jengo; (c) muundo wa kisanifu wa jengo; (d) matumizi ya urithi; na (e) sera na miongozo ya Halmashauri; - 9 Verify source ↗
Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa
AI-assisted research summary: The National Museum Director may issue heritage improvement permits for protected heritage property, certain property in a heritage conservation area, and property tied to heritage or revitalization agreements that require a permit.
9. Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa anaruhusiwa kutoa vibali vya kuboresha urithi kwa: ya (a) mali ya urithi iliyolindwa; (b) mali ndani ya eneo la hifadhi ya urithi, ikiwa na matumizi kibali muonekano au tabia zilizotambuliwa katika Mpango wa Usimamizi wa Uhifadhi kama tabia ya urithi au unavyochangia katika thamani ya urithi ya eneo; na yanahusiana (c) mali inayohusu makubaliano ya urithi ambayo au makubaliano cha kuboresha urithi revitalization yanahitaji kibali kipatikane. - 10 Verify source ↗
Kwa kuzingatia masharti mengine ya sheria
AI-assisted research summary: Mtu haruhusiwi kufanya mabadiliko fulani kwenye mali ya urithi iliyoainishwa kabla ya kupata kibali cha kuboresha urithi.
10. Kwa kuzingatia masharti mengine ya sheria hii, mtu hatafanya lolote kati ya yafuatayo kwa mali iliyoainishwa kabla ya kupata kibali cha kuboresha urithi: (a) kubadili upande wa nje wa jengo ambalo ni mali ya urithi iliyoainishwa; (b) kufanya mabadiliko ya muundo wa jengo la mali ya urithi iliyoainishwa; (c) kubadili, kuondoa au kuchukua hatua ambayo ingeweza kuharibu muonekano wa kisanifu au zana zilizowekwa mahali pa kudumu za usanifu za ndani ambazo ni mali ya urithi iliyoainishwa; (d) kubadili, kuondoa au kuchukua hatua ambayo ingeweza kuharibu muonekano ambao ni mali 6 Sheria Ndogo ya Mji wa Kihistoria wa Mikindani Na Maeneo Mengine ya Urithi Yaliyohifadhiwaya Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani Tangazo La Serikali Na. 218 (Linaendelea) ya urithi iliyoainishwa; au (e) kubadili, kuchimba au kujenga katika ardhi ambayo ni mali ya urithi iliyoainishwa. Shughuli zisizohitaji kibali cha maboresho - 11 Verify source ↗
Licha ya masharti ya sheria hii, kibali cha
AI-assisted research summary: In a heritage conservation area, a heritage alteration permit is not required for certain routine works.
11. Licha ya masharti ya sheria hii, kibali cha kubadili urithi hakihitajiki katika eneo la hifadhi ya urithi na mali ya urithi iliyohifadhiwa kwa: (a) upakaji rangi wa majengo au miundo, ikiwa rangi zinazopendekezwa ni sawa na zilizopo; (b) mabadiliko ya ndani ya jengo au muundo ambayo hayaongezi eneo la sakafu; (c) matengenezo ya jengo ya kawaida; na (d) matengenezo ya bustani ya kawaida. Masharti ya Kibali cha Kuboresha Urithi - 12 Verify source ↗
Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa
AI-assisted research summary: Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa anaweza kutoa vibali vya kubadili urithi ikiwa masharti ya uhifadhi yanazingatiwa.
12. Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa anaruhusiwa kutoa vibali vya kubadili urithi kwa kuzingata vigezo, matakwa au masharti kama, kwa maoni ya Mkurugenzi, yanaendana na dhumuni la uhifadhi wa urithi wa mali kwa masharti masharti yafuatayo: (a) kuheshimu mlolongo na muda wa ujenzi; (b) kuheshimu tabia za mabadiliko au kitendo kitakachoidhinishwa, ikijumuisha mandhari ya eneo, muundo, umati, muonekano wa nje, nyenzo na umaliziaji wa jengo na muonekano wa mandhari ya nchi; (c) kuheshimu mlolongo na muda wa umiliki; na (d) kutaka kwamba muombaji atoe dhamana kwa mujibu wa Sheria hii. Kushindwa kufuata masharti au kibali cha kuboresha urithi - 13 Verify source ↗
Ikiwa, kwa maoni ya Mkurugenzi wa
AI-assisted research summary: Mkurugenzi wa Makumbusho anaweza kumpeleka mwenye kibali aliyevuka masharti kwa Bodi, ili Bodi iamue kama ametokufuata masharti na iagize marekebisho au ujenzi unaohitajika kwa gharama ya mwenye kibali.
13. Ikiwa, kwa maoni ya Mkurugenzi wa Makumbusho, mmiliki aliyepewa kibali cha kuboresha urithi ameshindwa kufuata kigezo, matakwa au sharti la kibali, Mkurugenzi wa Makumbusho anaweza kuwasilisha suala kwa Bodi akiomba: - (a) kufanya uamuzi kama mwenye kibali cha kuboresha urithi ameshindwa kufuata kigezo, matakwa au sharti la kibali; na 7 Sheria Ndogo ya Mji wa Kihistoria wa Mikindani Na Maeneo Mengine ya Urithi Yaliyohifadhiwaya Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani Tangazo La Serikali Na. 218 (Linaendelea) (b) kutekeleza na kukamilisha ujenzi unaohitajika kuridhisha kigezo, matakwa au masharti au au kurekebisha kutokufuatwa, kwa gharama za mwenye kibali. ukiukwaji athari za Kukataliwa kwa kibali cha kuboresha urithi - 14 Verify source ↗
Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa
AI-assisted research summary: The National Museum Director may refuse a permit to alter heritage if the proposed action does not fit heritage preservation purposes.
14. Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa anaweza kukataa kutoa kibali cha kubadili urithi ikiwa, kwa maoni ya Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa, kitendo pendekezwa kilichoidhinishwa hakitalingana na dhumuni la uhifadhi wa urithi wa mali, na kwa kufanya uamuzi huo, Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa anaweza kuzingatia vigezo vifuatavyo: (a) kama muombaji ameshindwa kuwasilisha tathmini ya madhara alivyoamrishwa kufanya hivyo; (b) kama muombaji ameshindwa kufuata vigenzo vilivyoainishwa katika taarifa ya tathmini ya madhara; (c) kama kitendo pendekezwa kingepunguza thamani ya urithi au tabia ya urithi wa mali ya urithi iliyohifadhiwa au mali katika eneo la hifadhi ya urithi, na, katika kufanya uamuzi huo, Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa anaweza kuzingatia vigezo vya sheria hii; na (d) kama mali inaongozwa na sheria ndogo inayotangaza kipindi cha udhibiti wa urithi. Utoaji wa Kibali cha Maendeleo - 15 Verify source ↗
Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa
AI-assisted research summary: The National Museum Director may approve the issue of development permits, but only when the criteria, requirements, or conditions fit the development purpose in a conservation area.
15. Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa anaweza kuidhinisha kutolewa kwa vibali vya maendeleo kwa kuzingatia vigezo, matakwa au masharti hayo ambayo yanalingana na madhumuni ya maendeleo katika eneo la uhifadhi. Kukataliwa kwa kibali cha maendeleo - 16 Verify source ↗
Mkurugenzi anaweza kukataa kutoa kibali cha
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kukataa kibali cha maendeleo ikiwa anaona mradi unapunguza thamani au tabia ya urithi wa mali.
16. Mkurugenzi anaweza kukataa kutoa kibali cha maendeleo ikiwa kwa maoni yake, kitendo pendekezwa kitapunguza thamani ya urithi au tabia ya urithi wa mali 8 Sheria Ndogo ya Mji wa Kihistoria wa Mikindani Na Maeneo Mengine ya Urithi Yaliyohifadhiwaya Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani Tangazo La Serikali Na. 218 (Linaendelea) Kuzuia idhini Taarifa ya kuzuia idhini kwa muombaji Kikomo cha kuzuia idhini ya urithi iliyohifadhiwa na katika kufanya uamuzi huo, Mkurugenzi anaweza kuzingatia vigezo vilivyoainishwa katika Sheria hii. - 17 Verify source ↗
Kwa kuzingatia masharti ya Sheria hii,
AI-assisted research summary: The Director may refuse approval for a development permit or a heritage-change permit in certain heritage-protection cases.
17. Kwa kuzingatia masharti ya Sheria hii, Mkurugenzi anaweza kuzuia idhini ya kibali cha maendeleo au kibali cha kubadili urithi ikiwa, kwa maoni yake kitendo pendekezwa kingebadili au kusababisha kubadilishwa kwa: (a) mali ya urithi iliyolindwa; (b) mali inayopewa uhifadhi wa urithi wa muda; au (c) mali katika rejesta ya urithi. - 18 Verify source ↗
Ikiwa Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa
AI-assisted research summary: Akinyimwa kibali cha maendeleo au cha kubadili urithi, Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa lazima amjulishe mwombaji kwa maandishi sababu za kukataa na kumweleza kwamba anaweza kukata rufaa kwa Bodi.
18. Ikiwa Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa anazuia kibali cha maendeleo au kibali cha kubadili urithi kwa mujibu wa masharti ya Sheria Ndogo hii, atamtaarifu Muombaji kwa maandishi: (a) sababu za kuzuia idhini; na (b) ikiwa hajaridhika na uamuzi anaweza kukata rufaa kwa Bodi; - 19 Verify source ↗
Bila kuathiri masharti ya kanuni ya 18
AI-assisted research summary: The National Museums Director must not withhold approval when the applicant agrees to the Council’s terms and conditions after the Director is satisfied about measures to prevent or reduce harm to heritage value or character.
19. Bila kuathiri masharti ya kanuni ya 18 Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa hatazuia idhini ikiwa muombaji anakubaliana na vigezo na masharti ya Halmashauri baada ya kuridhika kwa Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa kuzuia au kupunguza mazingira ambayo yanaweza kupunguza thamani ya urithi au tabia ya urithi ya mali. Rufaa kwa Bodi - 20 Verify source ↗
Mmiliki au muombaji kibali anaweza kukata
AI-assisted research summary: Mmiliki au muombaji wa kibali anaweza kukata rufaa kwa Bodi dhidi ya baadhi ya maamuzi ya Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa.
20. Mmiliki au muombaji kibali anaweza kukata rufaa kwa Bodi kwa uamuzi uliofanywa na Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa kuhusiana na: (a) kukataa kutoa kibali cha maendeleo ndani ya la uhifadhi kwa mali ya urithi eneo iliyohifadhiwa; (b) utoaji au kukataliwa kwa kibali cha kuboresha 9 Sheria Ndogo ya Mji wa Kihistoria wa Mikindani Na Maeneo Mengine ya Urithi Yaliyohifadhiwaya Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani Tangazo La Serikali Na. 218 (Linaendelea) Uamuzi wa rufaa Amri ya Ukaguzi wa Urithi Watu wanaoruhusiwa kuingia katika eneo la uhifadhi urithi; (c) uamuzi kama matakwa na masharti ya kibali cha kuboresha urithi yamefikiwa; (d) kwa kuwasilisha ombi la maandishi kwa Bodi ndani ya siku 14 za uamuzi, likianisha sababu za ombi. - 21 Verify source ↗
Bodi itaamua rufaa ndani ya muda unaofaa, na
AI-assisted research summary: Bodi lazima iamue rufaa ndani ya muda unaofaa, na inaweza kukubaliana au kutengua uamuzi.
21. Bodi itaamua rufaa ndani ya muda unaofaa, na inaweza kukubaliana au kutengua uamuzi. - 22 Verify source ↗
(1) Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa
AI-assisted research summary: Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa anaweza kuamuru ukaguzi wa urithi na, chini ya masharti fulani, kuingia katika ardhi au jengo wakati wa kazi; pia ana wajibu wa kuwaarifu mmiliki au mkaaji na kutoa nakala ya amri.
22.-(1) Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa anaweza kutoa amri ya ukaguzi wa urithi katika mazingira yafuatayo: (a) endapo utakuwa katika hatari ya kuzorota au kuharibika kutokana na kushindwa kukarabati au kurekebisha mali; (b) ametaarifiwa kwamba ujenzi unafanyika bila kibali; (c) kuna shughuli zisizohalali zinaendelea; au (d) sababu au mazingira mengine yoyote itakapolazimu. (2) Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa atachukua hatua atakapoona inafaa za kumtaarifu mmiliki au mkaaji kabla ya au baada ya kuingia katika ardhi au jengo na atawasilisha nakala ya amri kwa mmiliki au mkaaji. 23-(1) Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa au Afisa Mwidhiniwa wanaruhusiwa kuingia katika ardhi au jengo katika muda wowote wa kazi kuhakikisha uzingatiwaji wa Sheria hii au sheria nyingine yoyote. (2) Wanaweza kuchukua hatua stahiki za kumtaarifu mmiliki au mkaaji kabla ya au baada ya kuingia katika ardhi au jengo; na (3) Endapo kuna uvunjwaji wowote wa Sheria hii, Mkurugenzi atachukua hatua za muhimu na sahihi 10 Sheria Ndogo ya Mji wa Kihistoria wa Mikindani Na Maeneo Mengine ya Urithi Yaliyohifadhiwaya Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani Tangazo La Serikali Na. 218 (Linaendelea) ikijumusha kuitaarifu mamlaka husika. Vipimo na Sampuli - 24 Verify source ↗
Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa
AI-assisted research summary: Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa anaweza kufanya vipimo na kuondoa sampuli zinazohitajika kwa ukaguzi wa urithi, mradi athari zake ziwe ndogo na zisizoonekana kadri inavyowezekana.
24. Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa anaidhinishwa kufanya vipimo na kuondoa nyenzo za sampuli ambazo, kwa maoni yake ni muhimu kwa dhumuni la ukaguzi wa urithi, isipokuwa kwamba anaweza kuhakikisha kwamba mabadiliko yoyote yaliyosababishwa na vipimo hivyo ni madogo na hayaonekani kwa kadri inavyowezekana ukizingatia matakwa ya ukaguzi wa urithi. Taarifa kwa mmiliki - 25 Verify source ↗
Kufuatia kukamilika kwa ukaguzi wa urithi,
AI-assisted research summary: Baada ya ukaguzi wa urithi kukamilika, Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa lazima amjulishe mmiliki kuhusu ukaguzi huo na pia amjulishe kama kulikuwa na mabadiliko yoyote au kuondolewa kwa nyenzo wakati wa ukaguzi.
25. Kufuatia kukamilika kwa ukaguzi wa urithi, Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa: (a) atamtaarifu mmiliki juu ya ukaguzi wa urithi; na (b) atamtaarifu mmiliki ikiwa mabadiliko yoyote yamefanyika au nyenzo kuondolewa wakati wa ukaguzi wa urithi. - 26 Verify source ↗
Ikiwa, kwa maoni ya Mkurugenzi wa
AI-assisted research summary: A museum director may require an applicant to provide an impact assessment or let the director do one, if an approval may affect protected heritage property.
26. Ikiwa, kwa maoni ya Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa, idhini chini ya sheria hii au sheria nyingine inaweza kuathiri mali ya urithi iliyolindwa, anaweza kumtaka muombaji wa idhini: (a) kutoa kwa Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa tathmini ya athari, kwa gharama za muombaji; au (b) kumruhusu Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa kufanya tathmini ya athari. - 27 Verify source ↗
Tathimini ya athari ambayo inafanywa na
AI-assisted research summary: Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa lazima afanye tathimini ya athari kwa usahihi na kwa gharama za Makumbusho ya Taifa.
27. Tathimini ya athari ambayo inafanywa na Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa ni lazima: (a) ifanyike kwa usahihi; na (b) ifanyike kwa gharama za Makumbusho ya Taifa. - 28 Verify source ↗
Taarifa au amri ya Mkurugenzi wa
AI-assisted research summary: The National Museums Director’s notice or order must be in writing, addressed to the permit applicant, and include the required contents listed in the provision.
28. Taarifa au amri ya Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa kwa mujibu wa Sheria ya 11 Tathmini ya Madhara Tathmini ya Athari ya Urithi wa Kiutamaduni kufanywa na Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa Taarifa ya Tathmini ya Sheria Ndogo ya Mji wa Kihistoria wa Mikindani Na Maeneo Mengine ya Urithi Yaliyohifadhiwaya Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani Tangazo La Serikali Na. 218 (Linaendelea) Athari ya Urithi wa Kiutamaduni Usimamizi wa Mazingira: (a) itakuwa kwa maandishi na itaelekezwa kwa muombaji wa idhini; na (b) itajumuisha mtungamano ufuatao: (i) taarifa ambayo ni lazima itolewa katika tathmini ya athari, na (ii) taaluma za muhimu za mtu au watu wanaofanya utafiti kuandaa tathmini ya madhara. Mabadiliko ya mtungamano - 29 Verify source ↗
Mtungamano katika taarifa au amri ambayo
AI-assisted research summary: Taarifa au amri iliyotolewa chini ya Sheria ya Usimamizi wa Mazingira inaweza kubadilishwa tu na Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa kwa idhini ya mmiliki au muombaji.
29. Mtungamano katika taarifa au amri ambayo imetolewa kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa Mazingira na inaweza tu kubadilishwa na Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa kwa idhini ya mmiliki au muombaji. Uchambuzi wa Tathmini ya Athari ya Urithi wa Kiutamaduni - 30 Verify source ↗
Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa
AI-assisted research summary: The National Museums Director may decide whether the assembled matter in a notice or order relating to impact assessment has been achieved.
30. Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa anaruhusiwa kuamua kama mtungamano uliojumuishwa katika taarifa au amri kuhusiana na tathmini ya madhara umefikiwa. Makosa na Adhabu - 31 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayethibitika kuwa amevunja
AI-assisted research summary: Anyone who proves to have violated or acted contrary to this law commits an offence and may be fined, imprisoned, or both.
31. Mtu yeyote atakayethibitika kuwa amevunja au kwenda kinyume na masharti ya Sheria hii atakuwa ametenda kosa na akipatikana na hatia atatozwa faini isiyopungua shilingi elfu hamsini na isiyozidi shilingi laki tatu au kifungo kisichopungua miezi kumi na mbili na kisichozidi miezi ishirini na nne au vyote kwa pamoja, yaani faini na kifungo. 12 Sheria Ndogo ya Mji wa Kihistoria wa Mikindani Na Maeneo Mengine ya Urithi Yaliyohifadhiwaya Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani Tangazo La Serikali Na. 218 (Linaendelea) Lakiri ya Halmashauri ya manispaa ya Mtwara- Mikindani imebandikwa kwenye Sheria Ndogo hizi kufutia azimio lililopitishwa kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani uliofanyika Tarehe 07 mwezi, Oktoba, Mwaka 2022 mbele ya ;- MWL. HASSAN. B. NYANGE Mkurugenzi wa Manispaa Mtwara- Mikindani MHE. SHADIDA ALLY NDILE Mstahiki Meya wa Manispaa Mtwara -Mikindani NAKUBALI L.S Dodoma, MOHAMED OMARY MCHENGERWA 2 February, 2024 Waziri wa Nchi- Ofisi ya Rais (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa) 13
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Mji wa Kihistoria wa Mikindani na maeneo mengine ya Urithi yaliyohifadhiwa ya Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani za Mwaka 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in