Sheria Ndogo ya Kilimo na Usalama wa Chakula ya Halmashauri ya Manispaa Mtwara- Mikindani ya Mwaka, 2024
Hii ni kifungu cha utambulisho cha sheria ndogo; kinaipa jina Sheria Ndogo ya Kilimo na Usalama wa Chakula ya Halmashauri ya Manispaa Mtwara-Mikindani ya Mwaka 2024.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Kilimo na Usalama wa Chakula ya Halmashauri ya Manispaa Mtwara- Mikindani ya Mwaka, 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
Hii ni kifungu cha utambulisho cha sheria ndogo; kinaipa jina Sheria Ndogo ya Kilimo na Usalama wa Chakula ya Halmashauri ya Manispaa Mtwara-Mikindani ya Mwaka 2024. This law applies throughout the area under the Mtwara-Mikindani Municipal Council. This section defines key terms used in the by-law. Halmashauri must carry out a list of actions to support agricultural development, farmer registration, input access, extension services, and crop markets; the Local Government also has duties on pest control, buyer permits, and official markets. Serikali ya mtaa lazima itenge ardhi, kusajili wakulima na mazao, kushauri wananchi, na kuhakikisha sheria za mazao na masoko rasmi vinatekelezwa.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Kilimo na Usalama wa Chakula ya Halmashauri ya Manispaa Mtwara- Mikindani ya Mwaka, 2024
Showing 21 of 21
- 1 Verify source ↗
Sheria hii itaijulikana kama Sheria Ndogo ya
AI-assisted research summary: Hii ni kifungu cha utambulisho cha sheria ndogo; kinaipa jina Sheria Ndogo ya Kilimo na Usalama wa Chakula ya Halmashauri ya Manispaa Mtwara-Mikindani ya Mwaka 2024.
1. Sheria hii itaijulikana kama Sheria Ndogo ya Kilimo na Usalama wa Chakula ya Halmashauri ya Manispaa Mtwara- Mikindani ya Mwaka, 2024. - 2 Verify source ↗
Sheria hii itatumika katika eneo lote lililo chini
AI-assisted research summary: This law applies throughout the area under the Mtwara-Mikindani Municipal Council.
2. Sheria hii itatumika katika eneo lote lililo chini ya Mamlaka ya Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara- Mikindani. - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the by-law.
3. Katika Sheria Ndogo hii isipokuwa pale muktadha utahitaji vinginevyo: “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni Afisa yeyote la aliyeteuliwa na Mkurugenzi kwa kusimamia utekelezaji wa Sheria hii; lengo “Afisa ugani” maana yake ni mtaalamu wa kilimo, mifugo, uvuvi au nyuki katika ngazi za vijiji, mitaa na kata. “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara - Mikindani; “kilimo” maana yake ni shughuli yoyote ya uzalishaji mali inayofanywa na binadamu na itajumuisha kilimo cha mazao, ufugaji wa wanyama, samaki na nyuki; “mazao” maana yake ni mazao yote ya chakula, biashara, maua, matunda na mbogamboga yanayolimwa ndani ya eneo la Halmashauri; 1 Sheria Ndogo Za Kilimo Na Usalama wa Chakula Za Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani Tangazo la Serikali Na.219 (Linaendelea.) “mifugo” maana yake ni wanyama wote wafungwao na binadamu na itajumuisha nyuki, samaki, bata na kuku; “mfugaji” maana yake ni mtu yeyote anaejishughulisha na ufugaji mifugo katika eneo la Halmashauri; “mkazi” maana yake ni raia wa Tanzania ambaye kwa kawaida anaishi kwenye eneo la Halmashauri na ambaye ana kaya au anaishi katika kaya au taasisi iliyopo katika eneo la Halmashauri, isipokuwa mtu: (a) mwenye umri chini ya miaka 18; (b) asiyejiweza kutokana na ulemavu, (c) kuugua au uzee wa zaidi ya miaka sitini au mwanafunzi aliyeko masomoni muda wote. yake ni mtu “mkulima” maana yeyote anayejishiughulisha na shughuli za kilimo; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara – Mikindani au Afisa yeyote atakayeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi; yule “skimu ya umwagiliaji” maana yake ni miundo mbinu ya miradi ya umwagiliaji ambayo imeanzishwa na Serikali au Halmashauri au kijiji, taasisi binafsi au taasisi za umma na kuwapa wananchi ili kuendeleza kilimo cha umwagiliaji; “uvuvi haramu” maana yake ni uvuvi unaotumia zana zisizokubalika katika uvuvi kama vile mabomu, sumu, makokoro, mikuki na vyandarua; “uvuvi holela” maana yake ni uvuvi usio na leseni wala kibali cha Halmashauri; “chanzo cha maji” maana yake ni eneo lolote ambalo limetunzwa kwa ajili ya kuwa chanzo cha maji kwa matumizi ya jamii; “wagani kazi” maana yake ni wananchi ambao wamepata mafunzo ya ugani nje ya vyuo ili kufanya kazi za maafisa ugani pale ambapo maafisa ugani hawapo; “zana haramu” maana yake ni zana zisizokubalika kitaalamu kama vyandarua, baruti, mabomu, sumu, 2 Sheria Ndogo Za Kilimo Na Usalama wa Chakula Za Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani Tangazo la Serikali Na.219 (Linaendelea.) makokoro, nyavu zenye matunda madogo pamoja na mikuki. Wajibu wa Halmashauri - 4 Verify source ↗
Katika kuhamasisha na kutekeleza azma ya
AI-assisted research summary: Halmashauri must carry out a list of actions to support agricultural development, farmer registration, input access, extension services, and crop markets; the Local Government also has duties on pest control, buyer permits, and official markets.
4. Katika kuhamasisha na kutekeleza azma ya Kilimo cha mazao Halmashuri itakuwa na wajibu wa: (a) kuhakikisha viongozi wa Serikali, vyama vya siasa na wadau wengine wa Kilimo wanashiriki ipasavyo katika kuendeleza sekta ya kilimo katika Halmashauri; (b) kuunda vikundi vya sanaa vinavyohamasisha kilimo cha kisasa; (c) kuhakikisha upatikanaji rahisi na kwa wakati wa pembejeo za kilimo; (d) kutekeleza mipango ya msimu wa kilimo unaofuata mara baada ya mwisho wa msimu; (e) kuhakikisha wakulima wote wanasajiliwa kidigitali kwenye mfumo wa M- Kilimo kwa ajili ya kurahisisha utoaji wa huduma za ugani. (f) kuruhusu wakulima (mkulima mmoja mmoja) ambao watakuwa wamekidhi vigezo vya kupata mkopo kwenye benki kupewa mikopo hiyo. (g) kuhakikisha upatikanaji rahisi na kwa wakati wa pembejeo za kilimo. (h) kutekeleza mipango ya msimu wa kilimo unaofwata mara baada ya mwisho wa msimu. (i) kuhakikisha upatikanaji wa maafisa ugani katika kila Mitaa. (j) kuanzisha mfumo wa stakabadhi ya mazao ghalani. (k) kuainisha matumizi bora ya ardhi ili kubainisha na kutofautisha ardhi ya kilimo, kilimo na hifadhi (l) kusimamia upatikanaji wa mbolea na pembejeo zingine za kilimo. (m) kusimamia maadili, mwenendo, na upatikanaji wa mawakala wa mbolea na pembejeo za kilimo. (n) kuhakikisha ubora wa mazao unazingatiwa na mkulima katika hatua zote za uzalishaji. 3 Sheria Ndogo Za Kilimo Na Usalama wa Chakula Za Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani Tangazo la Serikali Na.219 (Linaendelea.) Wajibu wa Serikali ya Mtaa Hifadhi ya mazao (o) kuhakikisha visumbufu na magonjwa ya mazao yanadhibitiwa. (p) kuhakikisha kuwa wanunuzi wa mazao wanakuwa na vibali vya kununua mazao. (q) kuhakikisha kunakuwa na masoko rasmi yanayotambulika. - 5 Verify source ↗
(1) Serikali ya mtaa itakuwa na wajibu wa
AI-assisted research summary: Serikali ya mtaa lazima itenge ardhi, kusajili wakulima na mazao, kushauri wananchi, na kuhakikisha sheria za mazao na masoko rasmi vinatekelezwa.
5.-(1) Serikali ya mtaa itakuwa na wajibu wa: (2) Kutenga ardhi kwa ajili ya kilimo na malisho ya mifugo, maeneo ya ufugaji wa nyuki na mabwawa ya kufugia Samaki. (3) Kushirikiana na uongozi wa kitongoji itahakikisha kuwa kila mkazi anapata ardhi ya kutosha kwa ajili ya kutekeleza kauli mbiu ya kilimo kwanza. (4) Kuwashauri wananchi wanunue chakula cha kutosha kabla bei haijapanda. (5) Kuhakikisha mkulima anamuuzia mazao mnunuzi mwenye kibali cha Halmashauri na leseni ya kununua mazao. (6) Kusajili wakulima na mazao wanayolima. (7) Kuhakikisha kuwa sheria za mazao na kanuni zake zinatekelezwa. na (8) Kuhakikisha inaanzisha masoko rasmi ya kuuza mazao ya wakulima - 6 Verify source ↗
(1) Kila mkazi atakayelima shamba katika eneo
AI-assisted research summary: Residents who farm in the council area must harvest crops when they are ripe or dry and store them safely and cleanly; households must also keep enough food and have a safe, pest-proof storage granary.
6.-(1) Kila mkazi atakayelima shamba katika eneo la Halmashauri atatakiwa kuvuna mazao yake pindi yatakapokomaa au kukauka na kuyahifadhi katika hali ya usafi na usalama ili kutunza ubora wake. (2) Itakuwa ni jukumu la kila mkazi hususani mkuu wa kaya kuhakisha kuwa anahifadhi chakula cha kutosha yeye na familia yake kwa angalau mwaka mmoja. (3) Litakuwa ni jukumu la kila kaya kuwa na ghala la kuhifadhia chakula ambalo litapaswa kuwa katika hali ya usalama na lisiloruhusu wadudu kama vile dudumizi, panya au wadudu wengine kusababisha uharibifu wa chakula hicho. 4 Sheria Ndogo Za Kilimo Na Usalama wa Chakula Za Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani Tangazo la Serikali Na.219 (Linaendelea.) Muda wa mavuno - 7 Verify source ↗
(1) Kila mkazi anayelima shamba katika eneo la
AI-assisted research summary: Residents who farm in the council area must harvest crops when ripe or dry and store them cleanly and safely; households must also keep enough food and have proper storage.
7.-(1) Kila mkazi anayelima shamba katika eneo la Halmashauri atatakiwa kuvuna mazao yake pindi yakikomaa au kukauka na kuyahifadhi katika hali ya usafi na usalma ili kutunza ubora wake. (2) Itakuwa ni jukumu la kila mkazi hususani mkuu wa kaya kuhakikisha kuwa anahifadhi chakula cha kutosha yeye na familia yake kwa angalau mwaka mmoja ua zaidi. (3) Litakuwa ni jukumu la kila kaya kuwa na ghala la kuhifadhia chakula au kutumia vifaa na njia ambazo zinashauriwa kitaalamu katika kuhifadhi mazao kama vile matumizi ya mifuko ya kuhifadhia nafaka, ambazo zinapaswa kuhifadhi chakula katika hali ya usalama isiyoruhusu wadudu waharibifu wa mazao kama vidumizi, panya na wengineo. Masharti kwa mmiliki wa shamba - 8 Verify source ↗
Kila mkazi anayemiliki au atakayemilikishwa
AI-assisted research summary: Mkazi anayemiliki au atakayemilikishwa shamba lazima alilime, alitunze na kuliendeleza kwa kufuata maelekezo ya kitaalamu ya Afisa ugani.
8. Kila mkazi anayemiliki au atakayemilikishwa shamba kwa mujibu wa kanuni ya 5(1) ya Sheria hii atawajibika kulilima, kulitunza na kuendeleza shamba hilo kwa mujibu ya maelezo ya kitaalamu atayopewa na Afisa ugani. Wajibu kwa mmiliki wa shamba - 9 Verify source ↗
(1) Bila kuathiri kanuni ya 8 ya Sheria hii
AI-assisted research summary: Wakulima lazima watekeleze hatua za kilimo na udhibiti wa magonjwa/wadudu, na Afisa Ugani lazima atoe programu ya kilimo ya mwaka.
9.-(1) Bila kuathiri kanuni ya 8 ya Sheria hii itakuwa ni wajibu wa kila mkulima: (a) kupalilia shamba inavyoshauriwa na wataalamu; kwa wakati kama (b) kuweka mbolea; (c) kutoa taarifa kwa mamlaka za kijiji, mtaa, kata au Halmashauri au afisa ugani yeyote kwa njia yoyote atakayoona inafaa kuhusu kuwepo kwa ugonjwa wa mazao au kuwepo kwa wadudu waharibifu; (d) kutumia pembejeo kwa kuzingatia maelezo ya isipokuwa kama kitaalamu kila mwaka itaelekezwa vinginevyo na Afisa Ugani; (e) kuchukua hatua za kuangamiza wadudu au kutibu magonjwa kama waharibifu atakavyokuwa ameelekezwa na Afisa ugani; (f) kuzuia moto unaoweza kuharibu mazingira. 5 Sheria Ndogo Za Kilimo Na Usalama wa Chakula Za Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani Tangazo la Serikali Na.219 (Linaendelea.) Wajibu wa Afisa Mwidhiniwa (2) Kila Afisa Ugani atawajibika kutoa programu ya kilimo ya mwaka kulingana na mwenendo wa hali ya hewa au mazingira katika eneo la Halmashauri yake; (a) programu hiyo itazingatia aina ya mazao kwa msimu (b) aina ya mbegu kwa msimu husika; (c) namna na wakati wa kupanda; (d) namna na wakati gani wa kuvuna; na (e) namna ya kuhifadhi mazao baada ya kuvunwa. - 10 Verify source ↗
(1) Afisa Mwidhiniwa atakuwa na wajibu wa
AI-assisted research summary: Afisa Mwidhiniwa lazima ahakikishe wakulima wanafuata mbinu maalum za kilimo na anaweza kuingia na kukagua shamba wakati wa saa za kazi.
10.-(1) Afisa Mwidhiniwa atakuwa na wajibu wa kuhakikisha kwamba kila mkulima: (a) anaandaa shamba kwa wakati; (b) anapanda mbegu kwa mstari; (c) anazingatia nafasi kati ya mmea na mmea inayotakiwa kitaalamu; (d) anaweka mbolea kwa viwango na kwa wakati; (e) anapalilia kwa wakati palizi mbili au zaidi. (2) Afisa Mwidhiniwa atakuwa na uwezo wa kuingia na kukagua shamba lolote wakati wa saa za kazi ili kujionea kama mkulima anazingatia maelezo ya kitaalamu kama yanavyotolewa na wataalamu wa kilimo. Ukaguzi - 11 Verify source ↗
(1) Afisa Mwidhiniwa kwa kushirikiana na
AI-assisted research summary: Afisa Mwidhiniwa na Afisa Ugani wanaweza kuingia maeneo ya kilimo au nyumba, kukagua hifadhi ya chakula, na kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wanaokiuka Sheria hii; kila Afisa Ugani pia lazima awe na daftari na kupanga ratiba ya kutembelea mashamba.
11.-(1) Afisa Mwidhiniwa kwa kushirikiana na Afisa Ugani aweza : (a) kuingia wakati wowote wa saa za kazi kwenye eneo la kilimo au katika shamba kwa madhumuni ya kusimamia utekelezaji wa Sheria hii; (b) kuingia katika kaya yoyote ili kukagua ghala la chakula kuona kama taratibu za kuhifadhi chakula zinazingatiwa; (c) kumchukulia hatua za kisheria mtu yeyote atakayevunja Sheria hii; (2) Kila Afisa Ugani; (a) atakuwa na daftari linaloonyesha idadi kamili ya wakazi na idadi ya ekari za mazao ya kilimo; (b) atapanga ratiba ya kutembelea mashamba ya wakazi ili kujionea kama wanatekeleza wajibu 6 Sheria Ndogo Za Kilimo Na Usalama wa Chakula Za Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani Tangazo la Serikali Na.219 (Linaendelea.) Uhusiano baina ya Afisa Mwidhiniwa na Afisa Ugani Afisa Mtendaji Idadi ya mifugo inayoruhusiwa kufugwa wa kulima na kutunza mashamba kwa mujibu wa Sheria hii. - 12 Verify source ↗
Afisa Mwidhiniwa atashirikiana na Afisa ugani,
AI-assisted research summary: The appointed officer works with the extension officer, may enter agricultural areas and households for inspection, may take legal action against violators, must keep a register of residents and crop acreage, and must schedule farm visits to check compliance.
12. Afisa Mwidhiniwa atashirikiana na Afisa ugani, ambapo: (a) ataweza wakati wowote wa saa za kazi kuingia kwenye eneo la kilimo kwa madhumuni ya kusimamia utekelezaji wa Sheria hii; (b) ataweza kuingia katika kaya yoyote ili kukagua ghala la chakula kuona kama taratibu za kuhifadhi chakula zinazingatiwa; (c) ataweza kumchukulia hatua za kisheria mtu yeyote atakayevunja Sheria hii; (d) atatakiwa kuwa na daftari linaloonyesha idadi kamili ya wakazi na idadi ya ekari za mazao ya kilimo; (e) atapanga ratiba ya kutembelea mashamba ya wakazi ili kujionea kama wanatekeleza wajibu wa kulima na kutunza mashamba kwa mujibu wa Sheria hii; - 13 Verify source ↗
Kila Afisa Mtendaji wa Kata au Mtaa
AI-assisted research summary: Kila Afisa Mtendaji wa Kata au Mtaa lazima atunze kumbukumbu za mashamba yote ya mazao katika eneo lake na kusimamia moja kwa moja utekelezaji wa Sheria hii.
13. Kila Afisa Mtendaji wa Kata au Mtaa atawajibika kutunza kumbukumbu za mashamba yote ya mazao yaliyomo katika Kata au Mtaa wake na atasimamia moja kwa moja utekelezaji wa Sheria hii. - 14 Verify source ↗
Mfugaji ataruhusiwa kuwa na ng’ombe
AI-assisted research summary: Mkulima anaweza kuwa na ng’ombe wasiozidi watano, kufuga nguruwe wasiozidi watano, na kufuga mbuzi wasiozidi kumi na tano; ng’ombe na mbuzi wa kufugwa ndani tu, na mbwa wa mjini kufungiwa ndani wakati wa mchana.
14. Mfugaji ataruhusiwa kuwa na ng’ombe wasiozidi watano. (2) Ufugaji unaoruhusiwa ni ufugaji wa ndani tu. (3) Kwa mfugaji wa nguruwe ataruhusiwa kufuga nguruwe wasiozidi watano na endapo watakuwa wamezaliana, watoto watakaozaliwa wasikae zaidi ya miezi mitano kabla ya kuondolewa. (4) Mfugaji wa mbuzi, atatakiwa kufuga mbuzi wasiozidi kumi na tano kwa ufugaji wa ndani tu. (5) Mbwa wanaofugwa mjini wanatakiwa kufungiwa ndani wakati wa mchana. 7 Sheria Ndogo Za Kilimo Na Usalama wa Chakula Za Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani Tangazo la Serikali Na.219 (Linaendelea.) Mifugo kutozurura ovyo - 15 Verify source ↗
(1) Kila mfugaji wa mfugo atahakikisha
AI-assisted research summary: Mfugaji wa mifugo lazima ahakikishe mifugo yake inafungwa ndani na haizururi barabarani, mitaani, au sehemu zisizoruhusiwa kwa malisho.
15.-(1) Kila mfugaji wa mfugo atahakikisha kwamba mifugo yake inafungwa ndani, haizururi au kuzagaa ovyo barabarani, mitaani au kwenye sehemu ambazo haziwezi kutumika kama sehemu za malisho ya mifugo. (2) Mfugaji atakavyoelezwa na Manispaa. azingatie eneo kufuatana na (3) Endapo mifugo inayozagaa itakamatwa kwa kuzagaa ovyo mitaani, au kwenye sehemu ambazo hajaruhusiwa kwa ajili ya malisho, mifugo hiyo itakamatwa na wenye mifugo watawajibika kulipa faini iliyoainishwa chini ya Jedwali la Kwanza la Sheria hii. Makosa - 16 Verify source ↗
Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa chini ya
AI-assisted research summary: Anyone commits an offence under this provision if they misuse agricultural land, fail to maintain or harvest crops properly, lack suitable storage, keep insufficient food, or sell or use crops in the listed ways.
16. Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa chini ya Sheria hii endapo: (a) anayemiliki ardhi ya kilimo atashindwa au kukataa au kukataza ardhi hiyo kutumika kwa kilimo; (b) Hatotunza shamba; (c) Hatovuna kwa wakati mazao yaliyoko shambani ambayo yamefikia wakati wa kuvunwa; (d) Hatokuwa na ghala la kuhifadhia mazao au kutotumia njia za kitaalamu zinazoshauriwa kuhifadhi mazao hayo; (e) Hatohifadhi chakula cha kutosha; (f) Atauza mazao bila kuweka akiba kwa mwaka mzima au zaidi; (g) Atauza mazao yakiwa shambani; na (h) Atatumia hifadhi ya mazao kwa matumizi yasiyo ya lazima kama vile kutengeneza pombe. Adhabu yeyote - 17 Verify source ↗
Mtu
AI-assisted research summary: A person who breaches the conditions set by this law commits an offence and, if convicted, may be fined up to 300,000 shillings, imprisoned for up to 12 months, or both.
17. Mtu atakayevunja masharti yaliyowekwa na Sheria hii atakuwa ametenda kosa na akipatikana na hatia atatozwa faini isiyozidi shilingi laki tatu au kifungo kisichozidi miezi kumi na mbili (12) jela au adhabu zote mbili kwa pamoja yaani faini na kifungo. 8 Sheria Ndogo Za Kilimo Na Usalama wa Chakula Za Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani Tangazo la Serikali Na.219 (Linaendelea.) Uwezo wa Mkurugenzi kufifilisha kosa - 18 Verify source ↗
Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa ikiwa mkosaji anakiri kwa maandishi kwa hiari, anajaza fomu maalum ya Jedwali la Pili, na analipa faini ya shilingi laki mbili.
18. Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha kosa iwapo mkosaji atakiri kosa kwa hiyari yake mwenyewe kwa maandishi kwa kujaza fomu maalum iliyoambatishwa kwenye Jedwali la Pili la Sheria hii na kulipa faini ya kiasi cha shilingi laki mbili. Kufutwa kwa T.S Na. 443 la mwaka 2011 - 20 Verify source ↗
Sheria hii inafuta Sheria Ndogo ya (Kilimo
AI-assisted research summary: This section repeals the 2011 local by-law on Kilimo Kwanza for Mtwara–Mikindani Municipal Council.
20. Sheria hii inafuta Sheria Ndogo ya (Kilimo Kwanza) ya Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara – Mikindani ya mwaka 2011. ______________ JEDWALI LA KWANZA ________________ (Limetengenezwa chini ya Aya ya 15(3)) NAMBA AINA YA KIASI CHA FAINI (SHILINGI) MFUGO
Part
JEDWALI LA KWANZA
- 1 Verify source ↗
Section 1
AI-assisted research summary: A penalty of 50,000.00 applies for each cow that is roaming, grazing, or tethered in prohibited areas.
1. Ng’ombe 50,000.00 kwa kila ng;ombe anayezurura au kuchungwa au kufungwa na maeneo ambayo hayaruhusiwi. - 3 Verify source ↗
Section 3
AI-assisted research summary: Kuna ada/faini ya TSh 50,000 kwa kila mbwa anayezurura, na TSh 50,000 kwa kila mbuzi au kondoo.
3. Mbwa 50,000.00 kwa kila mbwa anayezurura Mbuzi au Kondoo 50,000.00 kwa kila mbuzi au kondoo 9 Sheria Ndogo Za Kilimo Na Usalama wa Chakula Za Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani Tangazo la Serikali Na.219 (Linaendelea.) _____________ JEDWALI LA PILI ______________ (Limetengenezwa chini ya Aya ya 18) FOMU YA KUKIRI NA KUFIFILISHA KOSA Mimi…………………………………………. nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya …………………………ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara – Mikindani mwezi…………….Mwaka ……………………….nilitenda kosa la kukiuka masharti ya Aya ya ………………………ya Sheria Ndogo ya (Kilimo na Usalama wa Chakula) ya Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara – Mikindani ya mwaka 2024. tarehe……………ya kwamba mnamo Kwa mamlaka aliyopewa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara – Mikindani, niko tayari kulipa kiasi cha Ada au Ushuru ninayodaiwa pamoja na faini. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU Leo tarehe…ya mwezi……………Mwaka……. Jina…………………………………..….. Saini…………………………………..…. Mbele ya: Jina……………………………………….. Cheo……………………………………… Saini……..……………………………….. Tarehe: …………………………………. 10 Sheria Ndogo Za Kilimo Na Usalama wa Chakula Za Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani Tangazo la Serikali Na.219 (Linaendelea.) Lakiri ya Halmashauri ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani imebandikwa kwenye Sheria Ndogo hizi kufuatia azimio lililopitishwa kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani uliofanyika 7/10/2022, mbele ya:- MWL. HASSAN B. NYANGE, Mkurugenzi wa Manispaa, Mtwara-Mikindani Mhe. Shadida Ally Ndile, Mtsahiki Meya wa Manispaa Mtwara-Mikindani L.S NAKUBALI, Dodoma, MOHAMED OMARY MCHENGERWA, 2 Februari, 2024. Waziri wa Nchi OR-Tamisemi 11
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Kilimo na Usalama wa Chakula ya Halmashauri ya Manispaa Mtwara- Mikindani ya Mwaka, 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in