Sheria Ndogo za Usafi na Uhifadhi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga za Mwaka 2024
This provision states the short title of the by-laws: the Mwanga District Council Hygiene and Environmental Conservation By-laws, 2024.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo za Usafi na Uhifadhi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga za Mwaka 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This provision states the short title of the by-laws: the Mwanga District Council Hygiene and Environmental Conservation By-laws, 2024. This section says the by-laws apply throughout Mwanga District Council and defines key terms used in them. Mmiliki wa nyumba, kiwanja au biashara lazima aweke eneo lake safi, asimamie taka kwa njia inayoelekezwa na Halmashauri, ajenge shimo la taka na choo kinachofaa, na aondoe mazalia ya mbu, panya na wadudu wengine hatarishi. Kila mkazi anayemiliki nyumba, kiwanja au biashara lazima aweke eneo lake safi, ashughulikie taka kama Halmashauri inavyoelekeza, ajenge na atumie choo kinachotakiwa, na aondoe mazalia ya wadudu hatarishi. Wamiliki wa nyumba, viwanda au maeneo ya biashara lazima wawe na karo la kuhifadhi maji taka, wayanyonye maji taka likijaa, na wasiruhusu maji kutoka vyooni, bafuni, karoni au viwandani kuelekezwa barabarani, mtoni, kwenye vyanzo vya maji au sehemu nyingine zisizotengwa kwa maji taka.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo za Usafi na Uhifadhi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga za Mwaka 2024
Showing 23 of 23
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hizi zitajulikana kama Sheria
AI-assisted research summary: This provision states the short title of the by-laws: the Mwanga District Council Hygiene and Environmental Conservation By-laws, 2024.
1. Sheria Ndogo hizi zitajulikana kama Sheria Ndogo za Usafi na Uhifadhi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga za Mwaka 2024. Matumizi Tafsiri - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hizi zitatumika katika eneo lote la
AI-assisted research summary: This section says the by-laws apply throughout Mwanga District Council and defines key terms used in them.
2. Sheria Ndogo hizi zitatumika katika eneo lote la mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga. Katika Sheria Ndogo hizi isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo: “ada” maana yake ni yake ni malipo yanayolipwa kwa Halmashauri kwa ajili ya huduma ya kuzoa taka; “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni Afisa aliyeteuliwa kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hizi; “chakula” maana yake ni kitu chochote kinacholiwa au kunywewa na binadamu isipokuwa madawa; “choo bora” maana yake ni choo chochote cha maji chenye sakafu inayosafishika, banda imara la kudumu, kimeezekwa, kina mlango imara, bomba la kutolea hewa chafu na chenye mfuniko kwenye tundu la choo na shimo salama na safi kwa ajili ya kutupa kinyesi na mkojo wa binadamu, kilichojengwa kwa vifaa vya kudumu; “chukizo au kero” maana yake ni kitu chochote ambacho kipo katika hali yoyote iwe kinatumika, kimewekwa, kimejengwa, au ni kichafu kiasi cha kusababisha: (a) hatari kwa viumbe na maisha ya binadamu; 1 Sheria Ndogo Hizi Zitajulikana Kama Sheria Ndogo Za Usafi Na Uhifadhi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Tangazo la Serikali Na.223 (Linaendelea) (b) harufu mbaya au harufu ya kuudhi au kuleta kinyaa; (c) kuzaliana kwa wadudu hatari kama vile inzi, mende, sisimizi, panya, nyoka, nyuki, kunguni au viumbe wengine hatari; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga au Afisa aliyeteuliwa ya Mkurugenzi; majukumu kutekeleza “kizimba cha taka” maana yake ni eneo maalum lililotengwa na Halmashauri kwa ajili ya kuhifadhi taka ngumu; “mkazi” maana yake ni mtu ambaye kwa kawaida anaishi kwenye eneo lililopo chini ya mamlaka ya Halmashauri na ambaye ana kaya au anaishi katika kaya au taasisi iliyopo katika eneo la Halmashauri; “maji taka” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; “taka” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; na “taka ngumu” Maana yake ni kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira. Sura ya 191 Sura ya 191 Sura ya 191 Wajibu wa Kufanya Usafi wa Mazingira - 3 Verify source ↗
Itakuwa ni wajibu wa kila mkazi anayemiliki
AI-assisted research summary: Mmiliki wa nyumba, kiwanja au biashara lazima aweke eneo lake safi, asimamie taka kwa njia inayoelekezwa na Halmashauri, ajenge shimo la taka na choo kinachofaa, na aondoe mazalia ya mbu, panya na wadudu wengine hatarishi.
3. Itakuwa ni wajibu wa kila mkazi anayemiliki eneo la nyumba, kiwanja au biashara kuhakikisha kwamba: (a) mazingira yanayozunguka eneo lake yanakuwa safi wakati wote; (b) taka zote zinakusanywa na kufukiwa au kuondolewa kwa njia itakayoelekezwa na Halmashauri; (d) anajenga (c) anachimba shimo la kutupia taka litakalokuwa na urefu usiopungua kimo cha futi 3 na upana usiopungua futi 2; choo kudumu imara kilichojengwa kwa matofali na kuezekwa kwa bati, tembe, majani, vigae chenye mlango unaofunga na kufunguka na kuhakikisha kwamba choo kinatumika wakati wote na cha 2 Sheria Ndogo Hizi Zitajulikana Kama Sheria Ndogo Za Usafi Na Uhifadhi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Tangazo la Serikali Na.223 (Linaendelea) katika choo hicho kuwe na chombo cha maji tiririka na sabuni ya kunawa mikono; na (e) eneo lake halina mazalia ya mbu, panya na wadudu wengine hatarishi. Wajibu wa Kufanya Usafi wa Mazingira - 4 Verify source ↗
Itakuwa ni wajibu wa kila mkazi anayemiliki
AI-assisted research summary: Kila mkazi anayemiliki nyumba, kiwanja au biashara lazima aweke eneo lake safi, ashughulikie taka kama Halmashauri inavyoelekeza, ajenge na atumie choo kinachotakiwa, na aondoe mazalia ya wadudu hatarishi.
4. Itakuwa ni wajibu wa kila mkazi anayemiliki eneo la nyumba, kiwanja au biashara kuhakikisha kwamba: (a) mazingira yanayozunguka eneo lake yanakuwa safi wakati wote; (b) taka zote zinakusanywa na kufukiwa au kuondolewa kwa njia itakayoelekezwa na Halmashauri; (d) anajenga (c) anachimba shimo la kutupia taka litakalokuwa na urefu usiopungua kimo cha futi 3 na upana usiopungua futi 2; choo kudumu imara kilichojengwa kwa matofali na kuezekwa kwa bati, tembe, majani, vigae chenye mlango unaofunga na kufunguka na kuhakikisha kwamba choo kinatumika wakati wote na katika choo hicho kuwe na chombo cha maji tiririka na sabuni ya kunawa mikono; na (e) eneo lake halina mazalia ya mbu, panya na cha wadudu wengine hatarishi. Kuhifadhi Maji taka - 5 Verify source ↗
Kila mmiliki wa nyumba, kiwanda au eneo la
AI-assisted research summary: Wamiliki wa nyumba, viwanda au maeneo ya biashara lazima wawe na karo la kuhifadhi maji taka, wayanyonye maji taka likijaa, na wasiruhusu maji kutoka vyooni, bafuni, karoni au viwandani kuelekezwa barabarani, mtoni, kwenye vyanzo vya maji au sehemu nyingine zisizotengwa kwa maji taka.
5. Kila mmiliki wa nyumba, kiwanda au eneo la biashara anatakiwa: (a) kuhakikisha kuwa analo karo la kuhifadhi maji taka; (b) kunyonya maji taka pale karo linapojaa; na (c) Kuhakikisha kuwa hatiririshi au haelekezi maji kutoka vyooni, bafuni, karoni au viwandani kwenda barabarani, uchochoroni, mtoni, kwenye vyanzo vya maji, maeneo ya wazi, kwenye mfereji wa maji ya mvua au sehemu yoyote isiyotengwa kuhifadhia maji taka. 3 Sheria Ndogo Hizi Zitajulikana Kama Sheria Ndogo Za Usafi Na Uhifadhi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Tangazo la Serikali Na.223 (Linaendelea) Kutengenez a na kuuza Vyakula - 6 Verify source ↗
Mtu yeyote anayetengeneza, kuchoma, kupika,
AI-assisted research summary: A person who makes, burns, cooks, boils, or sells any kind of food in the Halmashauri area must comply with health requirements and health rules.
6. Mtu yeyote anayetengeneza, kuchoma, kupika, kuchemsha au kuuza chakula cha aina yoyote katika eneo la Halmashauri atatakiwa kutimiza masharti na kanuni za afya. Ada ya Ukaguzi wa kiafya Kupima Afya Uwezo wa Afisa Mwidhiniw a Vifaa vya Kuhifadhi Taka ngumu Ada ya kuzoa taka - 7 Verify source ↗
Kutakuwa na Ada ya ukaguzi wa kiafya na
AI-assisted research summary: Ada ya ukaguzi wa kiafya italipwa na mmiliki au mhudumu wa baadhi ya maeneo ya biashara na huduma yaliyoorodheshwa.
7. Kutakuwa na Ada ya ukaguzi wa kiafya na italipwa na mmiliki au Mhudumu katika majengo ya biashara, vituo vya afya, zahanati za watu binafsi, famasi, maduka ya madawa, hoteli, migahawa, Mama Lishe, Baba Lishe, Watoa tiba asili, majengo ya biashara, vioski na maeneo mengine kama ilivyoainishwa katika katika Jedwali la Kwanza.
Part
Jedwali la Kwanza.
- 8 Verify source ↗
Itakuwa ni wajibu wa kila mhudumu wa hoteli,
AI-assisted research summary: Watu wanaohudumu au kuuza chakula katika maeneo yaliyoorodheshwa lazima wapime afya zao kila baada ya miezi sita.
8. Itakuwa ni wajibu wa kila mhudumu wa hoteli, migahawa, baa, nyumba za kulala wageni, bucha, waoka mikate, au watu wanaoshughulika na kuuza vyakula vilivyopikwa kuhakikisha kwamba wanapima afya zao kila baada ya miezi sita. - 9 Verify source ↗
(1) Afisa Mwidhiniwa atakuwa na uwezo wa
AI-assisted research summary: Afisa Mwidhiniwa anaweza kuingia eneo lolote ndani ya Halmashauri wakati wa kazi na anaweza kushauri au kuelekeza watu kuacha kuishi katika jengo linalohatarisha afya au maisha.
9.-(1) Afisa Mwidhiniwa atakuwa na uwezo wa kuingia katika eneo lolote ndani ya Halmashauri wakati wa muda wa kazi kwa lengo la kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hizi. (2) Afisa Mwidhiniwa atakuwa na uwezo wa kushauri au kuelekeza watu au mtu kuacha kuishi katika jengo ambalo linahatarisha afya au maisha ya watu na viumbe hai. - 10 Verify source ↗
(1) Kila mmliki wa jengo la makazi au
AI-assisted research summary: Certain residential property owners, tenants, and business operators in the Council area must have a covered waste container and collect waste at designated collection points; owners or tenants in green-belt areas that have not been surveyed must also have a large pit for solid waste.
10.-(1) Kila mmliki wa jengo la makazi au mpangaji wa jengo la makazi au mtu yeyote anayefanyia biashara katika eneo lolote ndani ya Halmashauri atatakiwa kuwa na chombo cha kuhifadhia taka chenye mfuniko na atawajibika kukusanya taka hizo kwenye vizimba vya kuzolea taka katika maeneo yaliyoainishwa. (2) Kila mmiliki wa jengo au mpangaji wa nyumba iliyopo katika ukanda wa kijani katika maeneo ambayo la hayajapimwa atatakiwa kuwa na shimo kubwa kukusanya taka ngumu katika eneo lake. - 11 Verify source ↗
Halmashauri
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima ikusanye taka ngumu kutoka kwenye vizimba vya taka vilivyoainishwa, na wazalishaji wa taka watalipa ada au ushuru wa kukusanya taka.
11. Halmashauri taka ngumu kutoka katika vizimba vya taka vilivyoainishwa itawajibika kukusanya 4 Sheria Ndogo Hizi Zitajulikana Kama Sheria Ndogo Za Usafi Na Uhifadhi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Tangazo la Serikali Na.223 (Linaendelea) Kukusanya Taka ngumu Eneo la Kutupa Taka katika kila kata na wazalishaji taka watalipa ada au ushuru wa kukusanya taka kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Pili. - 12 Verify source ↗
(1) Halmashauri itawajibika kukusanya taka
AI-assisted research summary: Halmashauri must collect solid waste from designated waste bins in each ward, and people must not put liquid waste or explosive/harmful items in waste bins or burn/bury solid waste without a Halmashauri permit.
12.-(1) Halmashauri itawajibika kukusanya taka ngumu kutoka katika vizimba vya taka vilivyoainishwa katika kila kata. (2) Taka ngumu zote zitakazokusanywa kwenye mapipa ya taka zitabaki kuwa mali ya mkazi au mmliki wa eneo hilo mpaka zitakapokuwa zimefikishwa kwenye kizimba cha taka au zimeondolewa na Wakala kutoka katika eneo hilo. (3) Hairuhusiwi kuweka uchafu wenye asili ya maji maji kwenye pipa la taka au kitu chochote kinachoweza kulipuka na kusababisha madhara. (4) Hairuhusiwi mtu kuchoma au kufukia taka ngumu bila kibali cha Halmashauri. - 13 Verify source ↗
Halmashauri itakuwa na wajibu wa
AI-assisted research summary: Halmashauri must set aside a waste disposal area, place special waste containers in its areas, provide waste collection services for a fee, and charge dumping costs according to the Third Schedule.
13. Halmashauri itakuwa na wajibu wa: (a) kutenga eneo maalum kwa ajili ya kutupia taka; (b) kuweka vyombo maalum vya kutunzia taka katika maeneo ya Halmashauri; na (c) kutoa huduma ya kuzoa taka kwa malipo kutoka kwa wazalishaji wa taka na kupeleka kwenye dampo. (2) Halmashauri itatoza gharama za kutupa taka ka tika dampo kutoka kwa mawakala, wamiiliki wa taasisi mbalimbali, viwanda, makampuni pamoja na wazalishaji wengine wa taka kwa kuzingatia viwango vilivyoainishwa katika Jedwali la Tatu. Siku ya Usafi - 14 Verify source ↗
(1) Kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi
AI-assisted research summary: Kila mwisho wa mwezi, Jumamosi ya mwisho ni siku ya kufanya usafi wa mazingira; wakazi wa kijiji na kitongoji lazima washiriki, na mtu lazima ahakikishe maeneo yake ya makazi, biashara, na jirani ni safi.
14.-(1) Kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi itakuwa ni siku maalamu ya kufanya usafi wa mazingira katika maeneo ya makazi na umma. (2) Itakuwa ni wajibu na lazima kwa kila mkazi katika kijiji na kitongoji kushiriki usafi wa mazingira kwa siku iliyopangwa na Halmashauri katika maeneo yao na maeneo ya umma. 5 Sheria Ndogo Hizi Zitajulikana Kama Sheria Ndogo Za Usafi Na Uhifadhi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Tangazo la Serikali Na.223 (Linaendelea) Wajibu wa kuwa na choo na kukitumia (3) Mtu atahakikisha eneo la makazi yake na vichochoro vilivyomzunguka, eneo analofanyia biashara, eneo la wazi lililokaribu naye kwa umbali wa mita kumi na eneo la mazingira ya Ofisi ni safi. - 15 Verify source ↗
(1) Mmiliki wa nyumba au mpangaji atakuwa
AI-assisted research summary: Mmiliki wa nyumba au mpangaji lazima ahakikishe nyumba ina choo safi na imara, na kuwe na sehemu ya kunawia mikono yenye maji safi na sabuni ya kimiminika.
15.-(1) Mmiliki wa nyumba au mpangaji atakuwa na wajibu wa kuhakikisha kwamba: (a) nyumba yake ina choo safi na imara kwa matumizi ya wakazi wa nyumba hiyo; na (b) anaweka sehemu maalum ya kunawia mikono ikiwa na maji safi na sabuni maalum ya kimiminika. (2) Choo kinatakiwa kijengwe umbali wa mita sitini kutoka chanzo chochote cha maji. Vyoo vya umma - 16 Verify source ↗
(1) Halmashauri inaweza kujenga Choo cha
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kujenga choo cha umma au kuruhusu watu au taasisi kujenga vyoo vya umma katika maeneo inayoona yanafaa.
16.-(1) Halmashauri inaweza kujenga Choo cha Umma au kumruhusu mtu binafsi, vikundi vya watu au taasisi kujenga vyoo vya Umma katika maeneo ambayo Halmashauri itaona inafaa. (2) Vyoo vitakavyojengwa vitatakiwa kuwa vya kudumu na viwe na: (a) matundu yasiyopungua mawili kwa wanawake na mawili kwa wanaume; (b) mfumo madhubuti wa maji na uwepo wa maji ya kutosha yaliyo safi na salama; (c) chombo cha kuhifadhia maji ya akiba; (d) bafu la wanaume na wanawake; (e) chumba maalumu cha Kuvutia sigara; (f) sehemu ya haja ndogo kwa wanaume; na (g) chombo maalumu chenye mfuniko cha kuhifadhia taka zisizoweza kusukumwa na maji; Vyoo vya muda katika mikusanyik o - 17 Verify source ↗
Ni wajibu wa mtu, kikundi au taasisi yenye
AI-assisted research summary: Mtu, kikundi, au taasisi inayokusanya watu kwa mkutano, sherehe, au mkusanyiko lazima ijenge au iweke vyoo vya muda ikiwa eneo halina choo cha kudumu, na lazima iombe idhini kutoka Halmashauri.
17. Ni wajibu wa mtu, kikundi au taasisi yenye lengo la kukusanya watu kwa madhumuni ya kufanya mkutano au sherehe au mkusanyiko wowote kuweka au kujenga vyoo vya muda endapo katika eneo hilo hakuna choo cha kudumu na atatakiwa kuomba idhini kutoka Halmashauri. 6 Sheria Ndogo Hizi Zitajulikana Kama Sheria Ndogo Za Usafi Na Uhifadhi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Tangazo la Serikali Na.223 (Linaendelea) Vikundi vya Usafi Katazo - 18 Verify source ↗
Halmashauri
AI-assisted research summary: Halmashauri must encourage the formation and recognition of Community Groups so they can carry out solid waste control and environmental cleanliness activities in streets after contracting with the Halmashauri.
18. Halmashauri itahamasisha uundwaji wa Vikundi Jamii na kuvitambua ili kuviwezesha kufanya shughuli za udhibiti wa taka ngumu pamoja na usafi wa mazingira katika mitaa baada ya kuingia mkataba na Halmashauri. - 19 Verify source ↗
Ni marufuku
AI-assisted research summary: Kifungu hiki kinapiga marufuku vitendo kadhaa vya uchafuzi, matumizi yasiyoidhinishwa ya maeneo, na shughuli fulani bila vibali au leseni zinazohitajika.
19. Ni marufuku: (a) mtu kuendesha biashara ya kupuliza dawa au kuua wadudu au wanyama waharibifu katika nyumba yoyote au mahali popote bila kuwa na taaluma kinachotambuliwa na cheti cha Serikali na leseni kutoka Halmashauri; (b) mfanyabiashara kupanga bidhaa nje ya jengo lake la biashara au barabarani au vichochoroni au katika eneo lolote ambalo halikuidhinishwa kwa ajili ya shughuli hiyo; (c) mtu kutupa taka za aina yoyote barabarani au katika eneo lolote la wazi au vichochoro au kwenye chanzo chochote cha maji au eneo lolote ambalo halikutengwa kwa ajili ya shughuli hiyo; (d) mtu aliye ndani ya gari kudondosha taka ngumu nje ya gari likiwa ndani au nje ya kituo cha magari na sehemu yoyote ile ambapo gari hilo linapita; (e) mtu kuweka kitu chochote kwenye maji taka ambacho kinaweza kumuathiri mtu yeyote au kuharibu mfumo wa tiba ya maji taka au kinachoweza kusababisha kuzuia mtiririko wa maji taka; (f) mtu kulima matuta kilimo yanayosababisha maji kutuama ndani ya eneo la katikati ya mji; cha (g) kuchimba mchanga, kokoto au mawe katika vyanzo vya maji au mito barabarani; (h) kuchafua, kuoga, kufua au kuvuruga maji yanayotumika kwa ajili ya matumizi ya binadamu au wanyama; (i) kuuza mchanga, kokoto na mawe kandokando mwa barabara; 7 Sheria Ndogo Hizi Zitajulikana Kama Sheria Ndogo Za Usafi Na Uhifadhi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Tangazo la Serikali Na.223 (Linaendelea) (j) kufanya biashara ya pombe ya aina yoyote katika nyumba au maeneo ya akiba ya barabara au mitaani; (k) kuuza matunda au bidhaa nyingine za vyakula barabarani au kuanzisha masoko au magenge ya kuuzia matunda au vyakula au biashara nyingine ndogo bila ruhusa ya Halmashauri; (l) kuunganisha bomba la taka vimiminika katika mifereji ya maji ya mvua; (m) kufungulia au kutiririsha maji ya choo au taka vimiminika katika mkondo asili wa maji ya mvua au barabara au mfereji wa barabara wa maji ya mvua; (n) kujisaidia haja ndogo au haja kubwa barabarani au mtaani au sehemu yoyote isiyokusudiwa kwa madhumuni hayo; (o) kubomoa jengo lolote kwa njia yeyote ile bila kupata kibali cha Halmashauri; (p) kufanya mikusanyiko ya kidini au kiutamaduni au kijamii wakati wa milipuko ya magonjwa ya kuambukiza, isipokuwa kwa ruhusa maalum ya Halmashauri na usimamizi wa Afisa Afya; na (q) kuweka uchafu wenye asili ya maji maji taka au kitu chochote kusababisha la kulipuka na kwenye pipa kinachoweza madhara. Makosa - 20 Verify source ↗
Itakuwa ni kosa kwa mtu
AI-assisted research summary: Kifungu hiki kinakataza mtu kufanya vitendo mbalimbali vya usafi na utupaji taka, ikiwemo kujenga choo karibu na vyanzo vya maji, kutupa taka ovyo, kutolipa ada ya taka, na kufanya baadhi ya shughuli bila kibali cha Halmashauri.
20. Itakuwa ni kosa kwa mtu: (a) kujenga choo chini ya umbali wa mita 60 kutoka kisimani, bwawani, mtoni, au chanzo kingine cha maji yanayotumika kwa matumizi ya binadamu; (b) kutoa kinyesi au kusababisha kinyesi, mkojo, maji machafu yenye kinyesi kutoka kwenye choo chake au bafu lake au karo la kuoshea vyombo au nguo au kutoka kwenye bomba lolote linalochukua maji machafu na kuyatitirisha kwenye barabara, mitaa, au 8 Sheria Ndogo Hizi Zitajulikana Kama Sheria Ndogo Za Usafi Na Uhifadhi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Tangazo la Serikali Na.223 (Linaendelea) kwenye mifereji ya maji ya mvua, au mfereji wowote uliowazi; (c) kutupa taka au kusababisha mtu mwingine atupe taka mahali popote pasiporuhusiwa na Halmashauri; (d) kutolipa ada ya taka kwa miezi miwili mfululizo; (e) kutembeza vyakula mitaani bila kibali cha Halmashauri; (f) kutokuwa na pipa la taka lenye mfuniko katika eneo la biashara; (g) kutokuwa na choo au kukutwa na choo kibovu au kilichojaa; (h) kukutwa na shimo la maji taka lililojaa au ambalo halina mfuniko; (i) kutokuwa na chombo maalum cha kukusanyia taka ndani ya gari la abiria; na (j) kufanya biashara ya kuosha gari, pikipiki au mtambo wowote katika eneo la makazi, eneo la wazi au eneo ambalo halikutengwa kwa shughuli hiyo au kuruhusu eneo lake kutumika kwa shughuli za kuosha vyombo vya moto katika maeneo ambayo hayakutengwa kwa shughuli hizo bila kupata kibali rasmi kutoka Halmashauri. Adhabu - 21 Verify source ↗
Mtu anayevunja masharti yaliyowekwa na
AI-assisted research summary: A person who breaks the conditions set by these subsidiary laws commits an offence and may be fined up to 300,000 shillings, imprisoned for up to 12 months, or both.
21. Mtu anayevunja masharti yaliyowekwa na Sheria Ndogo hizi atakuwa ametenda kosa na akipatikana na hatia atatozwa faini isiyozidi shilingi laki tatu au kifungo kisichozidi miezi kumi na mbili jela au adhabu zote mbili kwa pamoja. Kufifilisha Kosa - 22 Verify source ↗
Mkurugenzi anaweza kumtoza mtu aliyetenda
AI-assisted research summary: The Director may impose a fine of Shilingi 50,000 on a person who has committed an offence under these By-laws if the offender voluntarily admits the offence and is willing to complete the attached form in the Fourth Schedule.
22. Mkurugenzi anaweza kumtoza mtu aliyetenda kosa chini ya Sheria Ndogo hizi kiasi cha Shilingi elfu hamsini iwapo mkosaji atakiri kosa kwa hiari na kuwa tayari kujaza fomu maalum iliyoambatishwa kwenye Jedwali la Nne. 9 Sheria Ndogo Hizi Zitajulikana Kama Sheria Ndogo Za Usafi Na Uhifadhi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Tangazo la Serikali Na.223 (Linaendelea) _____________ JEDWALI LA KWANZA ______________ (Limetengenezwa Chini ya aya ya 7) Ada ya Ukaguzi wa kiafya Namba Eneo la Ukaguzi Kiwango cha Ada Kwa mwezi (Shilingi) 10,000/= 5,000/=
Part
JEDWALI LA KWANZA
- 3 Verify source ↗
Section 3
AI-assisted research summary: Section 3 sets monthly fees for waste collection and waste disposal under Mwanga District Council’s sanitation bylaw.
3. 4 5 6 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17 18 19 20 Nyumba za kulala wageni Hoteli, mighahawa, nyumba za kuuzia vyakula vilivyopikwa Bucha za kuuzia nyama Kibanda na maeneo ya kuchomea nyama Vibanda au maeneo ya kuchomea nyama, kukaanga chips, nyama na mayai Kumbi za muziki, disko, dansi, Baa 10,000/= Vibanda vya biashara na maeneo ya biashara nyinginezo 3,000/= Maghala ya bidhaa za vyakula Vinywaji. Nyumba za makazi na mazingira ya Nyumba za makazi 2,000 3,000/= 2,000/= 2,000/= 10,000/= Maduka ya madawa baridi ya binadamu au mifugo Zahanati, kliniki na vituo vya Afya vya na taasisi za watu binafsi Maeneo ya biashara yaliyofungwa baada ya ukaguzi wa awali na kuomba kufanyiwa ukaguzi mpya Duka au kibanda cha biashara ya jumla Ukaguzi wa Vioski na glosari Majengo ya Taasisi Vyoo vya kibiashara vinavyoendeshwa na watu binafsi. Karakana na gereji za magari na mitambo Karakana za vyuma na viwanda vya mbao Mtoa tiba Asilia Saluni ya kiume 10,000/= 10,000/= 10,000/= 5,000/= 5,000/= 10,000/= 10,000/= 5,000/= 5,000/= 5,000/= 3,000/= 10 Sheria Ndogo Hizi Zitajulikana Kama Sheria Ndogo Za Usafi Na Uhifadhi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Tangazo la Serikali Na.223 (Linaendelea) ___________ JEDWALI LA PILI ___________ (Limetengenezwa Chini ya aya ya 11) Ada ya Huduma ya Ukusanyaji na Uzoaji wa Taka. Namba. Aina ya Biashara na mchangiaji Kiwango cha Ada kwa Mwezi (Shilingi) 3,000/= 1 2 3 4 5 7 8 9 10 11 12 13 14 15 16 17 18 19 20 21 22 22 23 24 25 26 27 28 29 30 31 32 33 34 35 36 37 Mgahawa mdogo, kibanda cha kuuzia chai au chakula 3,000/= Kioski na Glosari 3,000/= Nyumba ya kulala wageni 5,000/= Zahanati kwa Taka zisizo hatari 5,000/= Kituo cha Afya kwa Taka zisizo hatari 5,000/= Fundi Seremala 2,000/= Fundi chuma 5,000/= Karakana au gereji za magari Karakana nyinginezo 5,000/= Duka la jumla, Super markets au mini Super markets 5,000/= 2,000/= Duka la reja-reja 2,000/= Duka dogo la vyakula 3,000/= Duka kubwa la vyakula 5,000/= Baa 5,000/= Kumbi za Starehe, disko 3,000/= Duka la kuuza samaki au nyama na bucha ya samaki au nyama Kibanda au kituo cha Nyama choma au chips kinachojitegemea Duka la Dawa la Jumla Duka la dawa la reja—reja Kiwanda kidogo kwa kila trip Kiwanda kikubwa kwa kila trip Fundi cherehani Saluni ya Wanaume au Wanawake Kibanda au mwavuli wa kuuza vocha za simu Kituo cha Kuuzia nishati ya mafuta Washona viatu Wauza viatu vya mitumba au dukani Wauza nguo za mitumba Toroli la bidhaa au matunda Stoo za mkaa Stoo za mbao Mama au Baba Lishe Duka la kuuzia vipuli vy magari Kila Kaya Kila meza ndani ya Soko Ofisi za Taasisi kama benki, posta na nk Stationaries na maduka ya kuuza vitabu 3,000/= 2,000/= 20,000/= 30,000 1,000/= 3,000/= 500/= 5,000/= 2,000/= 2,000/= 2,000/= 1,000/= 5,000/= 5,000/= 3,000/= 10,000/= 2,000/= 300/= 10,000/= 5,000/= 3,000/= 11 Sheria Ndogo Hizi Zitajulikana Kama Sheria Ndogo Za Usafi Na Uhifadhi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Tangazo la Serikali Na.223 (Linaendelea) 38 39 Duka la Dawa baridi za binadam, duka la dawa za mifugo au pembejeo za kilimo Maghala 3,000/= 5,000/= _____________ JEDWALI LA TATU ______________ (Limetengenezwa Chini ya aya ya 13(2)) Gharama za kutupa Taka Kwenye Jalal la Taka la Halmashauri. Namba. 1 2 Kiasi cha Taka Taka za aina yoyote kwa kiwango cha ujazo chini ya tani moja Taka za aina yoyote kwa kiwango cha ujazo tani moja hadi tani saba Ada kwa Mwezi (Shilingi)) 10,000/= 20,000/= 12 Sheria Ndogo Hizi Zitajulikana Kama Sheria Ndogo Za Usafi Na Uhifadhi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Tangazo la Serikali Na.223 (Linaendelea) ___________ JEDWALI LA NNE ___________ (Limetengenezwa Chini ya aya ya 22) HATI YA KUFIFILISHA KOSA Mimi; ………………………………………………………. nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya; ……………………………………. ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga, kwamba mnamo tarehe;…… ya Mwezi;….…. Mwaka; …….… nilitenda kosa la kukiuka masharti ya aya ya …… ya Sheria Ndogo ya Usafi na Uhifadhi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga za Mwaka 2024. Kwa Mamlaka aliyopewa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga, niko tayari kulipa kiasi cha Ada au Ushuru ninaodaiwa pamoja na faini. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA MIMI MWENYEWE KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU: Leo tarehe;…....... ya Mwezi;………… Mwaka;………….. Jina;…………………………………..……………………. Saini; …………………………..…………………………… MBELE YANGU : Jin;…………………………….………..………………… Wadhifa; ………………………………………………….. Saini; ……………………………………………………… Tarehe; ……………………………………………………. 13 Sheria Ndogo Hizi Zitajulikana Kama Sheria Ndogo Za Usafi Na Uhifadhi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Tangazo la Serikali Na.223 (Linaendelea) Lakiri ya Halmashauri ya Manispaa ya Mwanga imebandikwa kwenye Sheria Ndogo hizi kufuatia azimio la mkutano wa Baraza la Halmashauri ya ya Wilaya ulioitishwa na kufanyika tarehe 1/3/2023, mbele ya:- MWAJUMA A. NASOMBE, Mkurugenzi mtendaji, Halmashauri ya Wilaya, Mwanga MHE. DR. SALEHE R. MKWIZU, Mwenyekiti, Halmashauri ya Wilaya, Mwanga L.S NAKUBALI, Dodoma, MOHAMED OMARY MCHENGERWA, 30 Januari, 2024. Waziri wa Nchi OR-Tamisemi 14
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo za Usafi na Uhifadhi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga za Mwaka 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in