Sheria Ndogo ya Kuzuia na kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Bahi ya Mwaka 2024
This section gives the short title of the by-law: the Bahi District Council by-law for preventing and controlling aflatoxin for 2024.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Kuzuia na kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Bahi ya Mwaka 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This section gives the short title of the by-law: the Bahi District Council by-law for preventing and controlling aflatoxin for 2024. This by-law applies throughout the entire area of Bahi District Council. This section defines key terms used in the bylaw, including officer, council, farmer, trader, director, crops, storage, drying, processing, and inspector-related terms. Halmashauri ina mamlaka ya kuratibu na kusimamia shughuli za kilimo ndani ya eneo lake ili kuzuia na kudhibiti sumukuvu, na pia kufanya ukaguzi katika maeneo na vifaa vinavyohusiana na mazao. A person intending to farm must follow proper land-preparation methods, prepare the farm on time, and not burn it.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Kuzuia na kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Bahi ya Mwaka 2024
Showing 17 of 17
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo
AI-assisted research summary: This section gives the short title of the by-law: the Bahi District Council by-law for preventing and controlling aflatoxin for 2024.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Kuzuia na kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Bahi ya Mwaka 2024. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la
AI-assisted research summary: This by-law applies throughout the entire area of Bahi District Council.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la Halmashauri ya Wilaya ya Bahi. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the bylaw, including officer, council, farmer, trader, director, crops, storage, drying, processing, and inspector-related terms.
3. Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni afisa yeyote aliyeteuliwa na Mkurugenzi kwa lengo la kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Bahi; “kanuni bora za kilimo” maana yake ni uandaaji wa shamba kwa usahihi, upandaji mbegu bora kwa wakati na kwa nafasi sahihi, upaliliaji, utumiaji mbolea kwa usahihi, udhibiti wa wadudu na wanyama waharibifu, uvunaji na hifadhi sahihi wa mazao; “kilimo” maana yake ni shughuli ya uzalishaji wa mazao; “kuvu’’ maana yake ni ukungu unaoota kwenye mazao; “mkulima” maana yake ni mtu, taasisi, kampuni au kikundi cha watu kinachojihusisha na shughuli za kilimo; “mfanyabiashara’’ maana yake ni taasisi, kampuni, kikundi cha watu au mtu binafsi anayejihusisha na shughuli za kuuza au kununua mazao ya kilimo; 1 Sheria Ndogo ya Kuzuia Na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Tangazo la Serikali Na.224 (Linaendelea.) “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi au afisa yeyote aliyeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi; “mazao’’ maana yake ni punje zinazotokana na mmea wa mhindi, mpunga, uwele, mtama, karanga, ngano, ufuta, alizeti, shayiri, ulezi na mazao ya mizizi yatokanayo na mihogo au viazi; “sumukuvu” maana yake ni sumu inayozalishwa na kuvu wanaoota kwenye mazao; “uhifadhi” maana yake ni utaratibu wa kutunza mazao katika sehemu ambayo haisababishi mazingira ya uotaji wa kuvu; “ukaushaji” maana yake ni taratibu sahihi za kupunguza unyevu kwenye mazao kwa ajili ya matumizi au uhifadhi; “usindikaji” maana yake ni hatua ya uchakataji wa zao kwa lengo la kuongeza thamani; “ushuru” maana yake ni tozo inayotozwa na Halmashauri kwa shughuli au huduma mbalimbali zinazofanywa katika eneo la Halmashauri; “uvunaji” maana yake ni uondoaji wa mazao kutoka kwenye mmea baada ya kukomaa au kukauka; “viashiria vya sumukuvu” maana yake ni dalili zinazoonesha uwepo wa sumukuvu kwenye mazao ya mahindi, mpunga, uwele, mtama, karanga, ngano, ufuta, alizeti, shayiri, ulezi zilizovunjika, na mazao ambayo hayajauka vizuri; “viuatilifu” maana yake ni sumu ya kuua au kuzuia wadudu waharibifu wa mazao; “wakala” maana yake ni mtu binafsi, kikundi, taasisi au kampuni iliyoteuliwa kukusanya ada na ushuru kwa niaba ya Halmashauri chini ya Sheria Ndogo hii. Uratibu na Usimamizi wa Shughuli za kilimo na Udhibiti wa Sumukuvu
Part
sehemu ambayo haisababishi mazingira ya uotaji wa
- 4 Verify source ↗
(1) Halmashauri itakuwa na mamlaka ya kuratibu
AI-assisted research summary: Halmashauri ina mamlaka ya kuratibu na kusimamia shughuli za kilimo ndani ya eneo lake ili kuzuia na kudhibiti sumukuvu, na pia kufanya ukaguzi katika maeneo na vifaa vinavyohusiana na mazao.
4.-(1) Halmashauri itakuwa na mamlaka ya kuratibu na kusimamia shughuli za kilimo ndani ya eneo la Halmashauri kwa lengo la kuzuia na kudhibiti sumukuvu. (2) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (1), Halmashauri itakuwa na mamlaka ya kufanya ukaguzi katika mashamba, vyombo vya usafirishaji wa mazao, maghala, 2 Sheria Ndogo ya Kuzuia Na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Tangazo la Serikali Na.224 (Linaendelea.) kiwanda au eneo la usindikaji kwa lengo la kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii. Uandaaji wa shamba - 5 Verify source ↗
Mtu anayekusudia kulima, atapaswa kuzingatia
AI-assisted research summary: A person intending to farm must follow proper land-preparation methods, prepare the farm on time, and not burn it.
5. Mtu anayekusudia kulima, atapaswa kuzingatia misingi ifuatayo: (a) kufuata njia sahihi za uandaaji wa shamba; (b) kutayarisha shamba kwa wakati; na (c) kutochoma moto. Upandaji wa mazao. - 6 Verify source ↗
Mtu atakayepanda mazao atapaswa kuzingatia njia
AI-assisted research summary: A person planting crops must use proper planting methods, including good seed, planting when the planting rains begin, and using correct spacing.
6. Mtu atakayepanda mazao atapaswa kuzingatia njia sahihi za upandaji ikiwa ni pamoja na- (a) kutumia mbegu bora; (b) kupanda mazao mara tu mvua za kupandia zinapoanza kunyesha; na (c) kupanda kwa nafasi sahihi. Utunzaji wa mazao shambani - 7 Verify source ↗
Mtu aliyepanda mazao atapaswa kuyatunza kwa
AI-assisted research summary: A person who planted crops must care for the crops using proper methods.
7. Mtu aliyepanda mazao atapaswa kuyatunza kwa kuzingatia njia sahihi za utunzaji wa mazao ikiwa ni pamoja na- (a) kutumia mbolea; (b) kupalilia kwa wakati; na (c) kudhibiti magonjwa, wadudu au wanyama waharibifu. Uvunaji wa mazao - 8 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayevuna mazao atapaswa kuvuna
AI-assisted research summary: Anyone harvesting crops must do so using good harvesting practices.
8. Mtu yeyote atakayevuna mazao atapaswa kuvuna kwa kuzingatia kanuni bora za uvunaji ikiwa ni pamoja na- (a) kuvuna mara baada ya mazao kukomaa au kukauka; (b) kusafirisha na kuhifadhi vizuri; na (c) kusafisha shamba baada ya kuvuna. Ukaushaji wa mazao - 9 Verify source ↗
Mtu atakayevuna mazao anapaswa kuyakausha
AI-assisted research summary: Mtu anayevuna mazao lazima ayakaushe mara moja baada ya kuvuna kwa njia sahihi.
9. Mtu atakayevuna mazao anapaswa kuyakausha kwa kutumia njia sahihi mara tu baada ya kuvuna ikiwa ni pamoja na: (a) njia za asili zisizoruhusu kuvu kuota; (a) kutumia maturubai, mikeka na vichanja vinavyozuia uchafuzi wa mazao; na (b) kukausha kwa itakayoelekezwa na mtaalamu. njia yoyote sahihi 3 Sheria Ndogo ya Kuzuia Na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Tangazo la Serikali Na.224 (Linaendelea.) Uhifadhi wa mazao - 10 Verify source ↗
(1) Mtu atawajibika kuhifadhi mazao kwa
AI-assisted research summary: Mtu lazima ahifadhi mazao kwa njia sahihi za kiasili au za kisasa zinazozuia kuota kwa kuvu.
10.-(1) Mtu atawajibika kuhifadhi mazao kwa kutumia njia sahihi za kiasili au za kisasa ambazo zitazuia kuota kwa kuvu. (2) Njia sahihi zinazoelekezwa kutumika kuhifadhi mazao ni pamoja na- (a) mifuko isiyopitisha hewa; (b) magunia ya kawaida kwa ajili ya mazao yaliyowekwa viuatilifu; (c) kihenge na kichanja bora cha asili; (d) silo au pipa maalumu; (e) ghala bora lililo safi; (f) kutumia viuatilifu kwenye mazao kwa kuzingatia ushauri wa kitaalamu; au (g) njia nyingine kadri itakavyoshauriwa na wataalamu. Wajibu wa Halmashau ri - 11 Verify source ↗
Katika utekelezaji wa Sheria Ndogo hii,
AI-assisted research summary: Halmashauri must carry out a set of implementation duties under this by-law, and it may appoint an Authorized Officer to supervise implementation.
11. Katika utekelezaji wa Sheria Ndogo hii, Halmashauri itakuwa na wajibu ufuatao: (a) kuhamasisha na kutoa elimu ya uzalishaji na usimamizi wa mazao; (b) kuhamasisha uhifadhi wa mazao katika eneo au ili kuepuka uchafuzi wa mahala salama sumukuvu; (c) kuweka mazingira wezeshi ya upatikanaji wa pembejeo za kilimo; (d) kutunza kumbukumbu za mashamba yote ya mazao ya kilimo katika kata na vijiji ili kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; (e) kuanzisha na kuendeleza mashamba darasa na vituo maalumu kwa ajili ya kutoa mafunzo ya udhibiti wa sumukuvu; (f) kuanzisha na kuhamasisha wakulima na wadau wengine kujenga sehemu za kuhifadhi mazao; na (g) kuandaa uwepo wa vituo maalumu vya kuuza na kununua mazao. (2) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (1), kumteua Afisa Mwidhiniwa Halmashauri kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii. inaweza - 12 Verify source ↗
Kila mkulima atakuwa na wajibu ufuatao
AI-assisted research summary: Kila mkulima lazima afanye kilimo kwa kanuni bora, aripoti dalili za kuvu kwa Halmashauri, na ashiriki mafunzo ya kudhibiti sumukuvu.
12. Kila mkulima atakuwa na wajibu ufuatao: 4 Sheria Ndogo ya Kuzuia Na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Tangazo la Serikali Na.224 (Linaendelea.) Wajibu wa mkulima (a) kufanya shughuli za kilimo kwa kuzingatia kanuni bora za kilimo na usimamizi wa mazao kabla na baada ya kuvuna; (b) kutoa taarifa kwa Halmashauri kuhusu uwepo wa dalili za kuvu katika mazao; na (c) kushiriki mafunzo na sumukuvu na Halmashauri ya kudhibiti kutekeleza ujuzi uliopatikana kwenye mafunzo hayo. yaliyoandaliwa Wajibu wa msafirishaji - 13 Verify source ↗
Mtu anayesafirisha mazao anapaswa kuhakikisha
AI-assisted research summary: Mtu anayesafirisha mazao lazima ahakikishe vifungashio na vifaa vya kusafirisha mazao ni vikavu au vinazuia maji, unyevu na vumbi kuingia.
13. Mtu anayesafirisha mazao anapaswa kuhakikisha vifungashio na vifaa anavyotumia kusafirisha mazao ni vikavu au visivyoruhusu maji, unyevu na vumbi kuingia ndani ili kuepusha kuvu kuota kwenye mazao. Wajibu wa mfanyabias hara - 14 Verify source ↗
Kila mfanyabiashara wa mazao atakuwa na
AI-assisted research summary: Trader of produce must ensure that produce bought, stored, transported, or sold has no signs of sumukuvu as listed in the First Schedule.
14. Kila mfanyabiashara wa mazao atakuwa na wajibu wa kuhakikisha ananunua, anahifadhi, anasafirisha au kuuza mazao ambayo hayana viashiria vya uwepo wa sumukuvu kama vilivyoanishwa katika Jedwali la Kwanza. Wajibu wa msindikaji - 15 Verify source ↗
Kila msindikaji atakuwa na wajibu wa kusindika
AI-assisted research summary: Kila msindikaji lazima asindikie mazao ambayo hayana viashiria vya uwepo wa sumukuvu kama yalivyoainishwa katika Jedwali la Kwanza.
15. Kila msindikaji atakuwa na wajibu wa kusindika mazao ambayo hayana viashiria vya uwepo wa sumukuvu kama vilivyoainishwa katika Jedwali la Kwanza. Makosa na adhabu - 16 Verify source ↗
Mtu ambaye
AI-assisted research summary: A person who handles crops in any of the listed prohibited ways commits an offence and may be fined, imprisoned for up to 12 months, or both.
16. Mtu ambaye- (i) (ii) (iii) (iv) (v) (vi) (vii) hataandaa, hatapanda au kutunza shamba na mazao kwa usahihi; hatavuna kwa wakati mara baada ya mazao kukomaa; atachelewa kuondoa mazao shambani baada ya kuvuna; ataanika mazao kwenye udongo, vumbi au mchanga; atakausha mazao katika mazingira yanayoweza kusababisha sumukuvu; atatumia viuatilifu vilivyozuiliwa kutumika kwenye mazao; atauza mazao yenye viashiria vya sumukuvu; 5 Sheria Ndogo ya Kuzuia Na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Tangazo la Serikali Na.224 (Linaendelea.) (viii) (ix) (x) atasafirisha mazao kwa njia zitakazosababisha mazingira ya kuvu kuota; atatumia mazao yenye viashiria vya sumukuvu wakati wa usindikaji; au atatenda jambo lolote lililokatazwa na Sheria Ndogo hii, anatenda kosa na endapo atapatikana na hatia atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi elfu hamsini na isiyozidi shilingi laki tatu au kutumikia kifungo kisichozidi miezi kumi mbili au vyote kwa pamoja. Ufifilishaji wa makosa - 17 Verify source ↗
Mkurugenzi anaweza kumtaka mtu aliyetenda
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kumtaka mkosaji aliyeikiri kosa kwa maandishi kulipa hadi shilingi 50,000.
17. Mkurugenzi anaweza kumtaka mtu aliyetenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii kulipa kiasi kisichozidi shilingi elfu hamsini endapo mkosaji atakiri kosa kwa maandishi katika fomu maalumu iliyoainishwa katika Jedwali la Pili la Sheria Ndogo hii. 6 Sheria Ndogo ya Kuzuia Na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Tangazo la Serikali Na.224 (Linaendelea.) ___________ JEDWALI LA KWANZA ____________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 14 na 15) Namba AINA YA MAZAO VIASHIRIA VYA SUMUKUVU HALI YA UNYEVU AU KUVU Punje kuwa na unyevu Mahindi 1 2 MWONEKANO WA PUNJE Punje kuwa na ukungu au kuvu - rangi kahawia au nyeusi au kijani au njano kuwa na harufu ya uvundo Punje kuwa na ukungu au kuvu – rangi kahawia au nyeusi au kijani au njano kuwa na harufu ya uvundo Karanga Punje kuwa na unyevu 7 Sheria Ndogo ya Kuzuia Na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Tangazo la Serikali Na.224 (Linaendelea.) ___________ JEDWALI LA PILI ___________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 17) FOMU YA KUFIFILISHA MAKOSA Mimi ……………………………………………………… nakiri kwa hiari yangu mwenyewe mbele ya ………………………………………….ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashuri ya Wilaya ya Bahi, kwamba mnamo tarehe …… ya mwezi ……. mwaka …… nilitenda kosa la kukiuka masharti ya aya ya …… ya Sheria Ndogo ya Kuzuia na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Bahi ya Mwaka 2024. Na kwamba niko tayari kulipa kiasi cha shilingi .................................. kwa ajili ya kufifilisha kosa nililotenda. Nathibitisha kwamba maelezo niliyotoa hapo juu ni ya kweli na nimeyatoa mimi mwenyewe kwa hiari yangu kadri ya ufahamu wangu. Leo tarehe…………. ya mwezi…………..… mwaka ……………. Jina……………………………….. Saini……………………… MBELE YANGU : Jina:……………………………………..……………………..... Saini………………………….…………………………..……… Wadhifa: ………………………………………………………… Tarehe…………………………………………………………… 8 Sheria Ndogo ya Kuzuia Na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Tangazo la Serikali Na.224 (Linaendelea.) Lakiri ya Halmashauri ya Manispaa ya Bahi imegongwa kwenye Sheria Ndogo hizi kufuatia azimio lililopitishwa kwenye mkutano wa Baraza la Mwadiwani la Halmashauri ulioitishwa na kufanyika tarehe 25/6/2022, mbele ya:- Zaina mfaume mlawa,, Mkurugenzi mtendaji(W), Halmashauri ya Wilaya, Bahi Donald simando mejitii, Mwenyekiti, Halmashauri ya Wilaya, Bahi L.S NAKUBALI, Dodoma, MOHAMED OMARY MCHENGERWA, 30 Januari, 2024. Waziri wa Nchi OR-Tamisemi 9
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Kuzuia na kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Bahi ya Mwaka 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in