Sheria Ndogo ya (Kuzuia na kudhibiti Sumukuvu) ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo ya Mwaka 2024
This provision gives the name of the bylaw: the Namtumbo District Council bylaw on preventing and controlling Sumukuvu, 2024.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya (Kuzuia na kudhibiti Sumukuvu) ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo ya Mwaka 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This provision gives the name of the bylaw: the Namtumbo District Council bylaw on preventing and controlling Sumukuvu, 2024. This by-law applies throughout the area of the Namtumbo District Council. This section defines key terms used in the by-law, including officer, council, agriculture, farmer, trader, director, crops, mold, aflatoxin, storage, drying, processing, harvesting, signs of aflatoxin, and pesticides. Halmashauri ina mamlaka ya kuratibu na kusimamia kilimo ndani ya eneo lake ili kuzuia na kudhibiti sumukuvu, na inaweza kufanya ukaguzi katika mashamba, vyombo vya usafirishaji wa mazao, maghala, kiwanda au maeneo ya usindikaji. A person intending to farm must follow proper land-preparation methods, prepare the field on time, and not burn fire.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya (Kuzuia na kudhibiti Sumukuvu) ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo ya Mwaka 2024
Showing 19 of 19
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itaitwa Sheria Ndogo ya
AI-assisted research summary: This provision gives the name of the bylaw: the Namtumbo District Council bylaw on preventing and controlling Sumukuvu, 2024.
1. Sheria Ndogo hii itaitwa Sheria Ndogo ya (Kuzuia na kudhibiti Sumukuvu) ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo ya Mwaka 2024. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la
AI-assisted research summary: This by-law applies throughout the area of the Namtumbo District Council.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la Mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria ndogo hii isipokuwa muhtadha
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the by-law, including officer, council, agriculture, farmer, trader, director, crops, mold, aflatoxin, storage, drying, processing, harvesting, signs of aflatoxin, and pesticides.
3. Katika Sheria ndogo hii isipokuwa muhtadha utahitaji vinginevyo- “afisa mwidhiniwa” maana yake ni afisa yeyote wa Halmashauri na Mkurugenzi aliyeteuliwa kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo; “kilimo” maana yake ni shughuli ya uzalishaji wa mazao; “mkulima” maana yake ni mtu, taasisi, kampuni au kikundi cha watu wanaojihusisha na shughuli za kilimo; “mfanyabiashara” maana yake ni taasisi, kampuni, kikundi cha watu au mtu binafsi anayejihusisha na shughuli za kuuza na au kununua mazao ya kilimo; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo au afisa yeyote aliyeteuliwa kutekeleza majukumu ya 1 Sheria Ndogo ya Kuzuia Na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Tangazo La Serikali Na. 263 (Linaendelea) Mkurugenzi; “mazao” maana yake ni punje zinazotokana na mmea wa mhindi, mpunga, uwele, mtama, karanga, ngano, ufuta, alizeti, shayiri, ulezi na mazao ya mizizi yatokanayo na mihogo,viazi; “kuvu” maana yake ni ukungu unaoota kwenye mazao; “sumukuvu” maana yake ni sumu zinazozalishwa na kuvu wanao ota kwenye mazao; “uhifadhi ” maana yake ni utaratibu wa kutunza mazao katika sehemu ambayo haisababishi mazingira ya uotaji wa kuvu; “ukaushaji” maana yake ni taratibu sahihi za kupunguza unyevu kwenye mazao kwa ajili ya matumizi au uhifadhi; “usindikaji” maana yake ni hatua ya uchakataji wa zao kwa lengo la kuongeza thamani; “uvunaji” maana yake ni uondoaji wa mazao kutoka kwenye mmea baada ya kukomaa au kukauka; “viashiria vya sumukuvu” maana yake ni dalili zinazoonesha uwepo wa sumukuvu kwenye mazao ya mahindi, mpunga, uwele, mtama, karanga, ngano, ufuta, alizeti, shayiri, ulezi zilizovunjika, na mazao ambayo hayajauka vizuri; na “viuatilifu” maana yake ni sumu ya kuua au kuzuia wadudu waharibifu wa mazao. - 4 Verify source ↗
(1) Halmashauri ina mamlaka ya kuratibu na
AI-assisted research summary: Halmashauri ina mamlaka ya kuratibu na kusimamia kilimo ndani ya eneo lake ili kuzuia na kudhibiti sumukuvu, na inaweza kufanya ukaguzi katika mashamba, vyombo vya usafirishaji wa mazao, maghala, kiwanda au maeneo ya usindikaji.
4.-(1) Halmashauri ina mamlaka ya kuratibu na la kusimamia shughuli za kilimo ndani ya eneo Halmashauri kwa lengo la kuzuia na kudhibiti sumukuvu. (2) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (1) Halmashauri itakuwa na mamlaka ya kufanya ukaguzi katika mashamba au vyombo vya usafirishaji wa mazao au maghala au kiwanda au eneo la usindikaji kwa lengo la kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii. Uratibu na usimamizi wa shughuli za kilimo na udhibiti wa sumukuvu Uandaaji wa shamba - 5 Verify source ↗
Mtu yeyote anayekusudia kulima, atapaswa
AI-assisted research summary: A person intending to farm must follow proper land-preparation methods, prepare the field on time, and not burn fire.
5. Mtu yeyote anayekusudia kulima, atapaswa 2 Sheria Ndogo ya Kuzuia Na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Tangazo La Serikali Na. 263 (Linaendelea) kuzingatia misingi ifuatayo: (a) kufuata njia sahihi za uandaaji wa shamba; (b) kuandaa shamba kwa wakati; na (c) kutochoma moto. Upandaji wa mazao - 6 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayepanda mazao atapaswa
AI-assisted research summary: Anyone who plants crops must use proper planting methods.
6. Mtu yeyote atakayepanda mazao atapaswa kuzingatia njia sahihi za upandaji ikiwa ni pamoja na- (a) kutumia mbegu bora; (b) kupanda mara mvua za kupandia zinapoanza kunyesha; na (c) kupanda kwa nafasi sahihi. Utunzaji wa mazao shambani - 7 Verify source ↗
Mtu yeyote aliyepanda mazao atapaswa
AI-assisted research summary: Mtu aliyepanda mazao lazima ayatunze kwa njia sahihi, ikiwemo kutumia mbolea, kupalilia kwa wakati, na kudhibiti magonjwa, wadudu au wanyama waharibifu.
7. Mtu yeyote aliyepanda mazao atapaswa kuyatunza kwa kuzingatia njia sahihi za utunzaji wa mazao ikiwa ni pamoja na- (a) kutumia mbolea; (b) kupalilia kwa wakati; na (c) kudhibiti magonjwa, wadudu na au wanyama waharibifu. Uvunaji wa mazao - 8 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayevuna mazao atapaswa
AI-assisted research summary: Anyone harvesting crops must follow good harvesting practices.
8. Mtu yeyote atakayevuna mazao atapaswa kuvuna kwa kuzingatia kanuni bora za uvunaji ikiwa ni pamoja na- (a) kuvuna mara baada ya mazao kukomaa au kukauka; (b) kusafirisha na kuhifadhi vizuri; na (c) kusafisha shamba baada ya kuvuna. Ukaushaji wa mazao - 9 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayevuna mazao anapaswa
AI-assisted research summary: Anyone who harvests crops must dry them properly immediately after harvesting.
9. Mtu yeyote atakayevuna mazao anapaswa kuyakausha kwa kutumia njia sahihi mara tu baada ya kuvuna ikiwa ni pamoja na- (a) njia za asili zisizoruhusu kuvu kuota; (b) kutumia maturubai, mikeka na vichanja vinavyozuia uchafuzi wa mazao; na (c) kukausha kwa itakayoelekezwa na mtaalamu. njia yoyote sahihi 3 Sheria Ndogo ya Kuzuia Na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Tangazo La Serikali Na. 263 (Linaendelea) Uhifadhi wa mazao - 10 Verify source ↗
(1) Mtu anapaswa kuhifadhi mazao kwa
AI-assisted research summary: Mtu anapaswa kuhifadhi mazao kwa njia sahihi za asili au za kisasa ili kuzuia kuota kwa kuvu.
10.-(1) Mtu anapaswa kuhifadhi mazao kwa kutumia njia sahihi za kiasili au za kisasa ambazo zitazuia kuota kwa kuvu. (2) Njia sahihi zinazoelekezwa kutumika kuhifadhi mazao ni pamoja na- (a) mifuko isiyopitisha hewa; (b) magunia ya kawaida kwa ajili ya mazao yaliyowekwa viuatilifu; (c) kihenge na kichanja bora cha asili; (d) silo au pipa maalumu; (e) ghala bora lililo safi; (f) kutumia viuatilifu kwenye mazao kwa kuzingatia ushauri wa kitaalamu; au (g) njia nyingine kadri itakavyoshauriwa na wataalamu. Wajibu wa Halmashauri - 11 Verify source ↗
(1) Halmashauri katika utekelezaji wa Sheria
AI-assisted research summary: Halmashauri must carry out several implementation duties for these bylaws, including education, storage promotion, input access, record keeping, demonstration farms, storage facilities, and market facilities; it may also appoint an authorized officer to oversee implementation.
11.-(1) Halmashauri katika utekelezaji wa Sheria Ndogo hizi itakuwa na wajibu wa: (a) kuhamasisha na kutoa elimu ya uzalishaji na usimamizi wa mazao; (b) kuhamasisha uhifadhi wa mazao katika eneo au uchafuzi wa mahala salama ili kuepuka sumukuvu; (c) kuweka mazingira wezeshi ya upatikanaji wa pembejeo za kilimo; (d) kutunza kumbukumbu za mashamba yote ya mazao ya kilimo katika Kata na Vijiji ili kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; (e) kuanzisha, kuendeleza mashamba darasa na vituo maalumu kwa ajili ya kutolea mafunzo ya udhibiti wa sumukuvu; (f) kuanzisha na kuhamasisha wakulima na wadau wengine kujenga sehemu za kuhifadhia mazao; au (g) kuandaa uwepo wa vituo maalumu vya kuuza na kununua mazao. 4 Sheria Ndogo ya Kuzuia Na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Tangazo La Serikali Na. 263 (Linaendelea) (2) Bila ya kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (1) Halmashauri inaweza kumteua afisa mwidhiniwa kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii. Wajibu wa mkulima - 12 Verify source ↗
Kila Mkulima atakuwa na wajibu wa
AI-assisted research summary: Kila mkulima ana wajibu wa kufuata kanuni bora za kilimo, kutoa taarifa kwa Halmashauri kuhusu dalili za kuvu kwenye mazao, na kushiriki mafunzo ya kudhibiti sumukuvu.
12. Kila Mkulima atakuwa na wajibu wa- (a) kufanya shughuli za kilimo kwa kuzingatia kanuni bora za kilimo na usimamizi wa mazao kabla na baada ya kuvuna; (b) kutoa taarifa kwa Halmashauri kuhusu uwepo wa dalili za kuvu katika mazao; na (c) kushiriki mafunzo na Halmashauri ya kudhibiti sumukuvu na kutekeleza ujuzi uliopatikana kwenye mafunzo hayo. yaliyoandaliwa Wajibu wa msafirishaji - 13 Verify source ↗
Mtu yeyote anayesafirisha mazao anapaswa
AI-assisted research summary: Anayet transport mazao lazima ahakikishe vifungashio na vifaa ni vikavu au vinazuia maji, unyevu na vumbi kuingia.
13. Mtu yeyote anayesafirisha mazao anapaswa kuhakikisha vifungashio na vifaa anavyotumia kusafirisha mazao ni vikavu au visivyoruhusu maji au unyevu na vumbi kuingia ndani ili kuepusha kuvu kuota kwenye mazao. Wajibu wa mfanyabiashar a - 14 Verify source ↗
Kila Mfanyabiashara wa mazao anapaswa
AI-assisted research summary: Every produce trader must only buy, store, transport, or sell produce without signs of aflatoxin, as listed in the First Schedule.
14. Kila Mfanyabiashara wa mazao anapaswa kuhakikisha ananunua, anahifadhi au anasafirisha au kuuza mazao ambayo hayana viashiria vya uwepo wa sumukuvu kama inanyoonishwa katika Jedwali la Kwanza. Wajibu wa Msindikaji Makosa na adhabu - 15 Verify source ↗
Kila Msindikaji atakuwa na wajibu wa
AI-assisted research summary: Kila msindikaji lazima asindike mazao ambayo hayana viashiria vya sumukuvu, kulingana na Jedwali la Kwanza.
15. Kila Msindikaji atakuwa na wajibu wa kusindika mazao ambayo hayana viashiria vya uwepo wa sumukuvu. kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Kwanza. - 16 Verify source ↗
Mtu yeyote ambaye
AI-assisted research summary: Mtu yeyote anayefanya vitendo vilivyoorodheshwa kuhusu mazao na sumukuvu anatenda kosa na anaweza kuadhibiwa kwa faini au kifungo.
16. Mtu yeyote ambaye (a) hataandaa, kupanda, kutunza shamba na mazao kwa usahihi; (b) hatavuna kwa wakati mara baada ya mazao kukomaa; (c) atachelewa kuondoa mazao shambani baada ya kuvuna; 5 Sheria Ndogo ya Kuzuia Na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Tangazo La Serikali Na. 263 (Linaendelea) (d) hataanika kwenye udongo, vumbi au mchanga; (e) atakausha mazao katika mazingira yanayoweza kusababisha sumukuvu; (f) atatumia viuatilifu vilivyozuiliwa kutumika kwenye mazao; (g) atauza mazao yenye viashiria vya sumukuvu. (h) atasafirisha mazao kwa njia zitakazosababisha mazingira ya kuvu kuota. (i) atatumia mazao yenye viashiria vya sumukuvu wakati wa usindikaji; au (j) atatenda jambo lolote lililokatazwa na Sheria Ndogo hii, anatenda kosa na akipatikana na hatia atatozwa faini isiyozidi shilingi elfu ishirini au kifungo kisichozidi miezi mitatu au vyote. - 17 Verify source ↗
Mkurugenzi anaweza kumtoza mtu yeyote
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kumtoza mtu aliyefanya kosa chini ya Sheria Ndogo hii Shilingi 20,000 ikiwa mkosaji anakiri kosa kwa hiari na kujaza fomu maalumu ya Jedwali la Pili.
17. Mkurugenzi anaweza kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii kiasi cha Shilingi elfu ishirini iwapo mkosaji atakiri kosa kwa hiari na kujaza fomu maalumu iliyoainishwa kwenye Jedwali la Pili. Kufifilisha kosa 6 Sheria Ndogo ya Kuzuia Na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Tangazo La Serikali Na. 263 (Linaendelea) _______________ JEDWALI LA KWANZA __________________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 14 na 15) VIASHIRIA VYA SUMUKUVU Namba AINA YA MAZAO
Part
JEDWALI LA KWANZA
- 1 Verify source ↗
Section 1
AI-assisted research summary: Neno hili linaonekana kuhusisha mahindi na hali ya unyevu wa punje.
1. Mahindi HALI YA UNYEVU AU KUVU Punje kuwa na unyevu - 2 Verify source ↗
Section 2
AI-assisted research summary: Sehemu hii inaonyesha maelezo ya punje zenye unyevu au zenye ukungu/kuvu na fomu ya kukiri kosa, ikieleza pia kuwa fomu husainiwa mbele ya Mkurugenzi wa Halmashauri na inaweza kuhusisha malipo ya kufifilisha kosa.
2. Karanga Punje kuwa na unyevu MWONEKANO WA PUNJE Punje kuwa na ukungu au kuvu – rangi kahawia au nyeusi au kijani au njano kuwa na harufu ya uvundo Punje kuwa na ukungu au kuvu – rangi kahawia au nyeusi au kijani au njano kuwa na harufu ya uvundo ______________ JEDWALI LA PILI _______________ (Limetengenezwa chini yakanuni ya 17) FOMU YA KUFIFILISHA KOSA Mimi ………………………………. Nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya…………………………………….…ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo kwamba mnamo tarehe…………ya Mwezi….......... Mwaka ……………. nilitenda kosa la kukiuka masharti ya aya ya cha ………. Cha Sheria Ndogo za (Kuzuia na kudhibiti Sumukuvu) ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo ya Mwaka 2024. Kwa mamlaka aliyopewa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo, Niko tayari kulipa kiasi cha Shilingi…………… kwa ajili ya kufifilisha kosa nililotenda chini ya Sheria Ndogo za (Kuzuia na kudhibiti Sumukuvu). NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA MIMI MWENYEWE KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU. Leo tarehe………..ya Mwezi……………………Mwaka………………….. Jina………………………………..…………….Saini………………………. MBELE YA: 7 Sheria Ndogo ya Kuzuia Na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Tangazo La Serikali Na. 263 (Linaendelea) Jina……………………………………………….….. Wadhifa………………………..…………………….….. Saini…………………………………………………… Tarehe…………………………………………………. 8 Sheria Ndogo ya Kuzuia Na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Tangazo La Serikali Na. 263 (Linaendelea) Lakiri ya Halmashauri ya wilaya ya Kiteto Imegongwa katika Sheria Ndogo hii kwa kufutia azimio lilopitishwa Katika Mkutano Wa Baraza La Madiwani la Halmashauri ya Wilaya Kiteto Tarehe 23 mwezi 06 Mwaka 2022 na Kushuhudiwa lakari hiyo ikogongwa Mbele ya ;- CPA, HAWA ABDUL HASSAN Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya Kiteto ABDALLAH BUNDALA Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya Kiteto L.S NAKUBALI / Dodoma, MOHAMED OMARY MCHENGERWA 30 January, 2024 Waziri wa Nchi- Ofisi ya Rais (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa) 9
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya (Kuzuia na kudhibiti Sumukuvu) ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo ya Mwaka 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in