Sheria Ndogo ya (Kuzuia na kudhibiti Sumukuvu) ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo ya Mwaka 2024
This section gives the short title of the by-law: the Namtumbo District Council By-Law on preventing and controlling Sumukuvu, 2024.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya (Kuzuia na kudhibiti Sumukuvu) ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo ya Mwaka 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This section gives the short title of the by-law: the Namtumbo District Council By-Law on preventing and controlling Sumukuvu, 2024. This bylaw applies throughout the area of the Namtumbo District Council. This section defines key terms used in the by-law on agriculture and control of sumukuvu. Halmashauri inaweza kuratibu, kusimamia, na kukagua shughuli za kilimo ndani ya eneo lake ili kuzuia na kudhibiti sumukuvu. A person intending to cultivate must follow proper farm-preparation methods, prepare the farm on time, and must not burn fire.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya (Kuzuia na kudhibiti Sumukuvu) ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo ya Mwaka 2024
Showing 19 of 19
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itaitwa Sheria Ndogo ya
AI-assisted research summary: This section gives the short title of the by-law: the Namtumbo District Council By-Law on preventing and controlling Sumukuvu, 2024.
1. Sheria Ndogo hii itaitwa Sheria Ndogo ya (Kuzuia na kudhibiti Sumukuvu) ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo ya Mwaka 2024. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la
AI-assisted research summary: This bylaw applies throughout the area of the Namtumbo District Council.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la Mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria ndogo hii isipokuwa muhtadha
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the by-law on agriculture and control of sumukuvu.
3. Katika Sheria ndogo hii isipokuwa muhtadha utahitaji vinginevyo- “afisa mwidhiniwa” maana yake ni afisa yeyote wa na Mkurugenzi aliyeteuliwa Halmashauri kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo; “kilimo” maana yake ni shughuli ya uzalishaji wa mazao; “mkulima” maana yake ni mtu, taasisi, kampuni au kikundi cha watu wanaojihusisha na shughuli za kilimo; “mfanyabiashara” maana yake ni taasisi, kampuni, kikundi cha watu au mtu binafsi anayejihusisha na shughuli za kuuza na au kununua mazao ya kilimo; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa 1 Sheria Ndogo ya Kuzuia Na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Tangazo La Serikali Na. 269 (Linaendelea) Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo au afisa yeyote aliyeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi; “mazao” maana yake ni punje zinazotokana na mmea wa mhindi, mpunga, uwele, mtama, karanga, ngano, ufuta, alizeti, shayiri, ulezi na mazao ya mizizi yatokanayo na mihogo,viazi; “kuvu” maana yake ni ukungu unaoota kwenye mazao; “sumukuvu” maana yake ni sumu zinazozalishwa na kuvu wanao ota kwenye mazao; “uhifadhi ” maana yake ni utaratibu wa kutunza mazao katika sehemu ambayo haisababishi mazingira ya uotaji wa kuvu; “ukaushaji” maana yake ni taratibu sahihi za kupunguza unyevu kwenye mazao kwa ajili ya matumizi au uhifadhi; “usindikaji” maana yake ni hatua ya uchakataji wa zao kwa lengo la kuongeza thamani; “uvunaji” maana yake ni uondoaji wa mazao kutoka kwenye mmea baada ya kukomaa au kukauka; “viashiria vya sumukuvu” maana yake ni dalili zinazoonesha uwepo wa sumukuvu kwenye mazao ya mahindi, mpunga, uwele, mtama, karanga, ngano, ufuta, alizeti, shayiri, ulezi zilizovunjika, na mazao ambayo hayajauka vizuri; na “viuatilifu” maana yake ni sumu ya kuua au kuzuia wadudu waharibifu wa mazao. Uratibu na usimamizi wa shughuli za kilimo na udhibiti wa sumukuvu - 4 Verify source ↗
(1) Halmashauri ina mamlaka ya kuratibu na
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kuratibu, kusimamia, na kukagua shughuli za kilimo ndani ya eneo lake ili kuzuia na kudhibiti sumukuvu.
4.-(1) Halmashauri ina mamlaka ya kuratibu na la kusimamia shughuli za kilimo ndani ya eneo Halmashauri kwa lengo la kuzuia na kudhibiti sumukuvu. (2) Bila kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (1) Halmashauri itakuwa na mamlaka ya kufanya ukaguzi katika mashamba au vyombo vya usafirishaji wa mazao au maghala au kiwanda au eneo la usindikaji kwa lengo la kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii. 2 Sheria Ndogo ya Kuzuia Na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Tangazo La Serikali Na. 269 (Linaendelea) Uandaaji wa shamba - 5 Verify source ↗
Mtu yeyote anayekusudia kulima, atapaswa
AI-assisted research summary: A person intending to cultivate must follow proper farm-preparation methods, prepare the farm on time, and must not burn fire.
5. Mtu yeyote anayekusudia kulima, atapaswa kuzingatia misingi ifuatayo: (a) kufuata njia sahihi za uandaaji wa shamba; (b) kuandaa shamba kwa wakati; na (c) kutochoma moto. Upandaji wa mazao - 6 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayepanda mazao atapaswa
AI-assisted research summary: Anyone planting crops must follow proper planting methods.
6. Mtu yeyote atakayepanda mazao atapaswa kuzingatia njia sahihi za upandaji ikiwa ni pamoja na- (a) kutumia mbegu bora; (b) kupanda mara mvua za kupandia zinapoanza kunyesha; na (c) kupanda kwa nafasi sahihi. Utunzaji wa mazao shambani - 7 Verify source ↗
Mtu yeyote aliyepanda mazao atapaswa
AI-assisted research summary: Mtu yeyote aliyepanda mazao lazima ayatunza kwa njia sahihi, ikiwemo kutumia mbolea, kupalilia kwa wakati, na kudhibiti magonjwa, wadudu, au wanyama waharibifu.
7. Mtu yeyote aliyepanda mazao atapaswa kuyatunza kwa kuzingatia njia sahihi za utunzaji wa mazao ikiwa ni pamoja na- (a) kutumia mbolea; (b) kupalilia kwa wakati; na (c) kudhibiti magonjwa, wadudu na au wanyama waharibifu. Uvunaji wa mazao - 8 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayevuna mazao atapaswa
AI-assisted research summary: Anyone harvesting crops must follow good harvesting practices.
8. Mtu yeyote atakayevuna mazao atapaswa kuvuna kwa kuzingatia kanuni bora za uvunaji ikiwa ni pamoja na- (a) kuvuna mara baada ya mazao kukomaa au kukauka; (b) kusafirisha na kuhifadhi vizuri; na (c) kusafisha shamba baada ya kuvuna. Ukaushaji wa mazao - 9 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayevuna mazao anapaswa
AI-assisted research summary: Anyone who harvests crops must dry them properly immediately after harvesting.
9. Mtu yeyote atakayevuna mazao anapaswa kuyakausha kwa kutumia njia sahihi mara tu baada ya kuvuna ikiwa ni pamoja na- (a) njia za asili zisizoruhusu kuvu kuota; (b) kutumia maturubai, mikeka na vichanja vinavyozuia uchafuzi wa mazao; na 3 Sheria Ndogo ya Kuzuia Na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Tangazo La Serikali Na. 269 (Linaendelea) (c) kukausha kwa itakayoelekezwa na mtaalamu. njia yoyote sahihi Uhifadhi wa mazao - 10 Verify source ↗
(1) Mtu anapaswa kuhifadhi mazao kwa
AI-assisted research summary: A person must store crops using proper traditional or modern methods that prevent fungal growth.
10.-(1) Mtu anapaswa kuhifadhi mazao kwa kutumia njia sahihi za kiasili au za kisasa ambazo zitazuia kuota kwa kuvu. (2) Njia sahihi zinazoelekezwa kutumika kuhifadhi mazao ni pamoja na- (a) mifuko isiyopitisha hewa; (b) magunia ya kawaida kwa ajili ya mazao yaliyowekwa viuatilifu; (c) kihenge na kichanja bora cha asili; (d) silo au pipa maalumu; (e) ghala bora lililo safi; (f) kutumia viuatilifu kwenye mazao kwa kuzingatia ushauri wa kitaalamu; au (g) njia nyingine kadri itakavyoshauriwa na wataalamu. Wajibu wa Halmashauri - 11 Verify source ↗
(1) Halmashauri katika utekelezaji wa Sheria
AI-assisted research summary: The council must carry out a set of crop-production and storage support duties, and it may appoint an authorized officer to oversee implementation.
11.-(1) Halmashauri katika utekelezaji wa Sheria Ndogo hizi itakuwa na wajibu wa: (a) kuhamasisha na kutoa elimu ya uzalishaji na usimamizi wa mazao; (b) kuhamasisha uhifadhi wa mazao katika eneo au uchafuzi wa mahala salama ili kuepuka sumukuvu; (c) kuweka mazingira wezeshi ya upatikanaji wa pembejeo za kilimo; (d) kutunza kumbukumbu za mashamba yote ya mazao ya kilimo katika Kata na Vijiji ili kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; (e) kuanzisha, kuendeleza mashamba darasa na vituo maalumu kwa ajili ya kutolea mafunzo ya udhibiti wa sumukuvu; (f) kuanzisha na kuhamasisha wakulima na wadau wengine kujenga sehemu za kuhifadhia mazao; 4 Sheria Ndogo ya Kuzuia Na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Tangazo La Serikali Na. 269 (Linaendelea) au (g) kuandaa uwepo wa vituo maalumu vya kuuza na kununua mazao. (2) Bila ya kuathiri masharti ya kanuni ndogo ya (1) Halmashauri inaweza kumteua afisa mwidhiniwa kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii. Wajibu wa mkulima - 12 Verify source ↗
Kila Mkulima atakuwa na wajibu wa
AI-assisted research summary: Each farmer must follow good agricultural practices and crop management before and after harvesting, report signs of mold in crops to the Council, and attend Council training and apply the skills learned.
12. Kila Mkulima atakuwa na wajibu wa- (a) kufanya shughuli za kilimo kwa kuzingatia kanuni bora za kilimo na usimamizi wa mazao kabla na baada ya kuvuna; (b) kutoa taarifa kwa Halmashauri kuhusu uwepo wa dalili za kuvu katika mazao; na (c) kushiriki mafunzo na Halmashauri ya kudhibiti sumukuvu na kutekeleza ujuzi uliopatikana kwenye mafunzo hayo. yaliyoandaliwa Wajibu wa msafirishaji - 13 Verify source ↗
Mtu yeyote anayesafirisha mazao anapaswa
AI-assisted research summary: Mtu anayesafirisha mazao lazima ahakikishe vifungashio na vifaa vya usafirishaji ni vikavu au haviruhusu maji, unyevu, au vumbi kuingia.
13. Mtu yeyote anayesafirisha mazao anapaswa kuhakikisha vifungashio na vifaa anavyotumia kusafirisha mazao ni vikavu au visivyoruhusu maji au unyevu na vumbi kuingia ndani ili kuepusha kuvu kuota kwenye mazao. Wajibu wa mfanyabiashar a - 14 Verify source ↗
Kila Mfanyabiashara wa mazao anapaswa
AI-assisted research summary: Mfanyabiashara wa mazao lazima ahakikishe mazao anayoinunua, kuhifadhi, kusafirisha au kuuza hayana viashiria vya sumukuvu kama vilivyoorodheshwa katika Jedwali la Kwanza.
14. Kila Mfanyabiashara wa mazao anapaswa kuhakikisha ananunua, anahifadhi au anasafirisha au kuuza mazao ambayo hayana viashiria vya uwepo wa sumukuvu kama inanyoonishwa katika Jedwali la Kwanza. Wajibu wa Msindikaji Makosa na adhabu - 15 Verify source ↗
Kila Msindikaji atakuwa na wajibu wa
AI-assisted research summary: Kila Msindikaji lazima asindike mazao yasiyo na viashiria vya uwepo wa sumukuvu.
15. Kila Msindikaji atakuwa na wajibu wa kusindika mazao ambayo hayana viashiria vya uwepo wa sumukuvu. kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Kwanza. - 16 Verify source ↗
Mtu yeyote ambaye
AI-assisted research summary: Mtu yeyote anayeorodheshwa hapa anatenda kosa ikiwa anashughulikia mazao kwa njia zilizokatazwa, na anaweza kupewa faini hadi shilingi 20,000 au kifungo hadi miezi 3, au vyote.
16. Mtu yeyote ambaye (a) hataandaa, kupanda, kutunza shamba na mazao kwa usahihi; 5 Sheria Ndogo ya Kuzuia Na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Tangazo La Serikali Na. 269 (Linaendelea) (b) hatavuna kwa wakati mara baada ya mazao kukomaa; (c) atachelewa kuondoa mazao shambani baada ya kuvuna; (d) hataanika kwenye udongo, vumbi au mchanga; (e) atakausha mazao katika mazingira yanayoweza kusababisha sumukuvu; (f) atatumia viuatilifu vilivyozuiliwa kutumika kwenye mazao; (g) atauza mazao yenye viashiria vya sumukuvu. (h) atasafirisha mazao kwa njia zitakazosababisha mazingira ya kuvu kuota. (i) atatumia mazao yenye viashiria vya sumukuvu wakati wa usindikaji; au (j) atatenda jambo lolote lililokatazwa na Sheria Ndogo hii, anatenda kosa na akipatikana na hatia atatozwa faini isiyozidi shilingi elfu ishirini au kifungo kisichozidi miezi mitatu au vyote. Kufifilisha kosa - 17 Verify source ↗
Mkurugenzi anaweza kumtoza mtu yeyote
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kumtoza mtu aliyefanya kosa chini ya Sheria Ndogo hii shilingi 20,000 ikiwa mkosaji anakiri kosa kwa hiari na kujaza fomu maalumu ya Jedwali la Pili.
17. Mkurugenzi anaweza kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii kiasi cha Shilingi elfu ishirini iwapo mkosaji atakiri kosa kwa hiari na kujaza fomu maalumu iliyoainishwa kwenye Jedwali la Pili. 6 Sheria Ndogo ya Kuzuia Na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Tangazo La Serikali Na. 269 (Linaendelea) _______________ JEDWALI LA KWANZA __________________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 14 na 15) VIASHIRIA VYA SUMUKUVU Namba AINA YA MAZAO
Part
JEDWALI LA KWANZA
- 1 Verify source ↗
Section 1
AI-assisted research summary: The text refers to maize grain moisture condition.
1. Mahindi HALI YA UNYEVU AU KUVU Punje kuwa na unyevu - 2 Verify source ↗
Section 2
AI-assisted research summary: Hii ni fomu ya kukiri kosa na kukubali kulipa kiasi fulani cha fedha ili kufifilisha kosa chini ya Sheria Ndogo za Kuzuia na Kudhibiti Sumukuvu za Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo.
2. Karanga Punje kuwa na unyevu MWONEKANO WA PUNJE Punje kuwa na ukungu au kuvu – rangi kahawia au nyeusi au kijani au njano kuwa na harufu ya uvundo Punje kuwa na ukungu au kuvu – rangi kahawia au nyeusi au kijani au njano kuwa na harufu ya uvundo ______________ JEDWALI LA PILI _______________ (Limetengenezwa chini yakanuni ya 17) FOMU YA KUFIFILISHA KOSA Mimi ………………………………. Nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya…………………………………….…ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo kwamba mnamo tarehe…………ya Mwezi….......... Mwaka ……………. nilitenda kosa la kukiuka masharti ya aya ya cha ………. Cha Sheria Ndogo za (Kuzuia na kudhibiti Sumukuvu) ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo ya Mwaka 2024. Kwa mamlaka aliyopewa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo, Niko tayari kulipa kiasi cha Shilingi…………… kwa ajili ya kufifilisha kosa nililotenda chini ya Sheria Ndogo za (Kuzuia na kudhibiti Sumukuvu). NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA MIMI MWENYEWE KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU. Leo tarehe………..ya Mwezi……………………Mwaka………………….. Jina………………………………..…………….Saini………………………. MBELE YA: Jina……………………………………………….….. Wadhifa………………………..…………………….….. Saini…………………………………………………… Tarehe…………………………………………………. 7 Sheria Ndogo ya Kuzuia Na Kudhibiti Sumukuvu ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Tangazo La Serikali Na. 269 (Linaendelea) Lakiri ya Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo imegongwa kwenye Sheria Ndogo hizi kufutia azimio lililopitishwa kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya Namtumbo ulioitishwa na kufanyika Tarehe 10 Mwezi Juni Mwaka 2022 na kushuhudiwa Lakari hiyo ikigongwa mbele ya;- CHIRIKU HAMISI CHILUMBA Mkurugenzi Mtandaji Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo JUMA ALFAN PANDU Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo L.S NAKUBALI Dodoma, MOHAMED OMARY MCHENGERWA 31 Januari, 2024 Waziri wa Nchi- Ofisi ya Rais (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa) 8
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya (Kuzuia na kudhibiti Sumukuvu) ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo ya Mwaka 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in