Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo ya Mwaka 2024
This provision gives the short title of the bylaw.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo ya Mwaka 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This provision gives the short title of the bylaw. This by-law applies throughout the entire area of Namtumbo District Council. This provision defines key terms used in the by-law, including fees, authorized officers, waste, solid waste, residents, households, and related sanitation terms. Residents and area owners must keep the area clean, manage waste properly, maintain a suitable toilet and refuse pit, prevent pest breeding, and ensure drinking water is safe. Mmiliki wa nyumba, kiwanda au eneo la biashara lazima awe na karo la kuhifadhia maji taka, anyonye maji taka karo linapojaa, na asiyaelekeze maji taka barabarani, mtoni, au sehemu zisizotengwa.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo ya Mwaka 2024
Showing 47 of 47
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo
AI-assisted research summary: This provision gives the short title of the bylaw.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo ya Mwaka 2024 Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la
AI-assisted research summary: This by-law applies throughout the entire area of Namtumbo District Council.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii isipokuwa muktadha
AI-assisted research summary: This provision defines key terms used in the by-law, including fees, authorized officers, waste, solid waste, residents, households, and related sanitation terms.
3. Katika Sheria Ndogo hii isipokuwa muktadha utahitaji vinginevyo- “ada” maana yake ni malipo yanayolipwa kwa Halmashauri kwa ajili ya huduma ya zinazotolewa na Halmashauri; “afisa mwidhiniwa” maana yake ni afisa yeyote atakayeteuliwa kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “chakula” maana yake ni kitu chochote anachokula au kunywa na binadamu isipokuwa madawa; hali katika “chukizo au kero” maana yake ni kitu chochote ambacho kipo kinatumika, yoyote kimewekwa, kimejengwa, au ni kichafu kiasi cha kusababisha: (a) hatari kwa viumbe na maisha ya binadamu; (b) harufu mbaya au harufu ya kuudhi au kuleta iwe 1 Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Tangazo La Serikali Na. 270 (Linaendelea) kinyaa; (c) kuzaliana kwa wadudu hatari kama vile nzi, mende, sisimizi, panya, nyoka, nyuki, kunguni au viumbe wengine hatari; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo; “jengo la biashara” maana yake jengo lolote lililojengwa na kuidhinishwa na Halmashauri kwa ajili ya kufanya biashara iliyokusudiwa; “kaya” maana yake mtu mzima anayejitegemea mwanamke au mwanaume, na mtoto anayeishi aidha kwenye nyumba nzima au ndani ya chumba kimoja kwenye eneo la Halmashauri; “kizimba cha taka” maana yake ni eneo maalumu lililotengwa na Halmashauri kwa ajili ya kuhifadhi taka ngumu; “mkazi” maana yake ni mtu yeyote ambaye kwa kawaida anaishi kwenye eneo lililoko chini ya mamlaka ya Halmashauri na ambaye ama ana kaya au anaishi katika kaya au taasisi iliyopo katika eneo la Halmashauri; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo au afisa yeyote atakayeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi; “taka” maana yake ni kitu chochote kama kioevu, kigumu, gesi au mionzi, ambayo hutolewa au kuwekwa kwenye mazingira kwa kiasi, muundo au njia inayoweza kusababisha mabadiliko ya mazingira, na inajumuisha taka kama zilizoainishwa chini ya Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; na Sura ya 191 “taka ngumu” maana yake ni malighafi zisizo za kimiminika zitokanazo na shughuli za majumbani, na mitaani, inajumuisha takataka, vifaa visivyo na maji vitokanavyo na shughuli za ujenzi na ubomoaji, biashara, viwanda kilimo na 2 Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Tangazo La Serikali Na. 270 (Linaendelea) ukataji bustani na uchimbaji madini, wanyama waliokufa na mabaki ya magari yaliyotelekezwa. Wajibu wa kufanya usafi wa mazingira - 4 Verify source ↗
Itakuwa ni wajibu wa kila mkazi anayeishi,
AI-assisted research summary: Residents and area owners must keep the area clean, manage waste properly, maintain a suitable toilet and refuse pit, prevent pest breeding, and ensure drinking water is safe.
4. Itakuwa ni wajibu wa kila mkazi anayeishi, la nyumba, kiwanja au biashara anayemiliki eneo kuhakikisha kwamba- (a) mazingira yanayozunguka eneo lake yanakuwa safi wakati wote; (b) taka zote zinakusanywa na kufukiwa au itakayoelekezwa na kuondolewa kwa njia Halmashauri; (c) anachimba shimo la kutupia taka litakalokuwa na urefu usiopungua kimo cha futi tatu na upana usiopungua futi mbili; (d) anajenga choo imara cha kudumu kwa matofali na kuezeka kwa bati, tembe, majani, vigae, chenye mlango unaofunga na kufunguka na kuhakikisha kwamba choo kinatumika wakati wote na kuwe na chombo cha maji tiririka na sabuni ya kunawa mikono; (e) eneo lake halina mazalia ya mbu, panya na wadudu wengine hatarishi; na (f) maji yote yanayotumika kwa kunywa ni safi na salama bila kujali yametoka kwenye chanzo gani cha maji. Uhifadhi wa maji taka - 5 Verify source ↗
Kila mmiliki wa nyumba, kiwanda au eneo la
AI-assisted research summary: Mmiliki wa nyumba, kiwanda au eneo la biashara lazima awe na karo la kuhifadhia maji taka, anyonye maji taka karo linapojaa, na asiyaelekeze maji taka barabarani, mtoni, au sehemu zisizotengwa.
5. Kila mmiliki wa nyumba, kiwanda au eneo la biashara anatakiwa- (a) kuhakikisha kuwa ana karo la kuhifadhia maji taka; (b) kunyonya maji taka kila wakati karo linapojaa; na (c) kutotiririsha au kutoelekeza maji kutoka vyooni, bafuni, karoni au viwandani kwenda barabarani, uchochoroni, mtoni, kwenye vyanzo vya maji, maeneo ya wazi, kwenye mfereji wa maji ya 3 Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Tangazo La Serikali Na. 270 (Linaendelea) mvua au sehemu yoyote ambayo haijatengwa kwa ajili ya kuhifadhia maji taka. Utengenezaji na uuzaji wa vyakula - 6 Verify source ↗
Mtu yeyote anayetengeneza, kuchoma, kupika,
AI-assisted research summary: Anyone who makes, roasts, cooks, boils, or sells any food in the council area must comply with health requirements and regulations.
6. Mtu yeyote anayetengeneza, kuchoma, kupika, kuchemsha au kuuza chakula cha aina yoyote katika eneo la Halmashauri atatakiwa kutimiza masharti na kanuni za afya. Upimaji wa afya Uwezo wa afisa mwidhiniwa - 7 Verify source ↗
Kila mhudumu wa hoteli, migahawa, baa,
AI-assisted research summary: Food-service and hospitality workers listed in this section must have a health check every six months.
7. Kila mhudumu wa hoteli, migahawa, baa, nyumba za kulala wageni, bucha, waoka mikate au watu wanaoshughulika na kuuza vyakula vilivyopikwa ana wajibu kuhakikisha anapima afya yake kila baada ya miezi sita. - 8 Verify source ↗
(1) Afisa mwidhiniwa atakuwa na uwezo wa
AI-assisted research summary: Afisa mwidhiniwa anaweza kuingia maeneo ya Halmashauri saa maalum za mchana, kushauri watu wasiishi katika jengo hatarishi, kuzuia shughuli wakati wa mlipuko wa magonjwa, kukamata vifaa hatarishi, na kufunga au kuagiza kufungwa kwa biashara au jengo lisilokaguliwa au linalokiuka kanuni za afya.
8.-(1) Afisa mwidhiniwa atakuwa na uwezo wa kuingia katika eneo lolote ndani ya Halmashauri kuanzia saa moja na nusu asubuhi hadi saa tisa na nusu alasiri kwa lengo la kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii. (2) Afisa mwidhiniwa atakuwa na uwezo wa kushauri au kuelekeza watu kutoishi katika jengo ambalo linahatarisha afya au maisha ya watu na viumbe hai. (3) Afisa mwidhiniwa anaweza kuzuia shughuli mbalimbali wakati wa mlipuko wa magonjwa ikiwa pamoja na kukamata vyombo au vifaa vingine vinavyotumika na ambavyo vinaweza kuleta madhara kwa wakazi wa Halmashari. (4) Afisa Mwidhiniwa anaweza kufunga au kuagiza kufungwa kwa biashara yoyote au jengo ambalo halijakaguliwa au lililokaguliwa na kukutwa limekiuka kanuni na masharti ya afya. Ada ya ukaguzi wa afya - 9 Verify source ↗
Halmashauri itatoa huduma ya ukaguzi wa afya
AI-assisted research summary: Halmashauri must provide health inspection services for every building every six months or whenever needed, and the building owner must pay the inspection costs.
9. Halmashauri itatoa huduma ya ukaguzi wa afya kwa kila jengo kila baada ya miezi sita au wakati wowote itakapohitajika kufanya ukaguzi na gharama za ukaguzi zitalipiwa na mmliki wa ilivyoainishwa kwenye Jedwali la Kwanza. jengo kama 4 Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Tangazo La Serikali Na. 270 (Linaendelea) Vifaa vya kuhifadhia taka ngumu Ada ya uzoaji taka Ada za utupaji taka kwenye dampo la Halmashauri Ukusanyaji taka ngumu - 10 Verify source ↗
(1) Kila mmliki wa jengo la makazi au mpangaji
AI-assisted research summary: Certain residential owners/tenants and business operators in the Council area must have a covered waste container and collect waste in designated receptacles; in village areas, owners or tenants must have a large pit for collecting solid waste.
10.-(1) Kila mmliki wa jengo la makazi au mpangaji wa jengo la makazi au mtu yeyote anayefanyia biashara katika eneo lolote ndani ya Halmashauri atatakiwa kuwa na chombo cha kuhifadhia taka chenye mfuniko na anapaswa kukusanya taka hizo kwenye vizimba vya kuzolea taka katika maeneo yaliyoainishwa. (2) Kila mmiliki wa jengo au mpangaji wa nyumba iliyoko katika maeneo ya vijiji anapaswa kuwa na shimo kubwa la kukusanyia taka ngumu katika eneo lake. - 11 Verify source ↗
Halmashauri inapaswa kukusanya taka ngumu
AI-assisted research summary: Halmashauri must collect solid waste from designated waste bins in each ward, and waste producers must pay the collection fee or tax set out in the Second Schedule.
11. Halmashauri inapaswa kukusanya taka ngumu kutoka katika vizimba vya taka vilivyoainishwa katika kila kata, na wazalishaji taka watalipia ada au ushuru wa kukusanya taka kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Pili. - 12 Verify source ↗
Halmashauri itatoza gharama za utupaji taka
AI-assisted research summary: Halmashauri itatoza gharama za utupaji taka kwenye dampo lake kwa mawakala, wamiliki wa taasisi, viwanda, kampuni na wazalishaji wengine wa taka kulingana na viwango vya ada vya Jedwali la Tatu.
12. Halmashauri itatoza gharama za utupaji taka katika dampo la Halmashauri kwa mawakala, wamiliki wa taasisi, viwanda, kampuni na wazalishaji wengine wa taka kwa kuzingatia viwango vya ada kama vilivyoainishwa kwenye Jedwali la Tatu. - 13 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote hataruhusiwa kuweka uchafu
AI-assisted research summary: Mtu yeyote haruhusiwi kuweka uchafu wenye asili ya maji maji kwenye pipa au chombo cha taka ngumu au kwenye kitu chochote kinachoweza kulipuka na kusababisha madhara.
13.-(1) Mtu yeyote hataruhusiwa kuweka uchafu wenye asili ya maji maji kwenye pipa au chombo chochote cha taka ngumu au kitu chochote kinachoweza kulipuka na kusababisha madhara. (2) Taka ngumu zote zitakazokusanywa kwenye pipa au chombo cha taka zitabaki kuwa mali ya mkazi au mmliki wa eneo lile mpaka zitakapokuwa zimefikishwa kwenye kizimba cha taka au zitakapokuwa zimetolewa na Wakala kutoka katika eneo lake. Eneo la kutupa taka - 14 Verify source ↗
Halmashauri inapaswa
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima itenge eneo la kutupa taka, iweke vyombo vya kutunzia taka, na itoe huduma ya uzoaji taka kwa malipo.
14. Halmashauri inapaswa- (a) kutenga eneo maalumu kwa ajili ya kutupa taka; (b) kuweka vyombo maalumu vya kutunzia taka katika maeneo ya Halmashauri; na 5 Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Tangazo La Serikali Na. 270 (Linaendelea) (c) kutoa huduma ya uzoaji taka kwa malipo kutoka kwa wazalishaji wa taka hadi kwenye dampo. Taratibu za kubomoa jengo - 15 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote haruhusiwi kubomoa au
AI-assisted research summary: You must not demolish or cause a building or part of a building to collapse without notifying the council.
15.-(1) Mtu yeyote haruhusiwi kubomoa au kusababisha kubomoka jengo au sehemu ya jengo bila kutoa taarifa kwa Halmashauri. (2) Mtu yeyote atakayeomba na kupata kibali cha kubomoa jengo au sehemu ya jengo anapaswa kuondoa lililobomolewa kwa gharama zake jengo mabaki ya mwenyewe hayo mahali kutupa mabaki na atakapoelekezwa. Mabaki ya ujenzi - 16 Verify source ↗
Mtu yeyote hataruhusiwa kubomoa au
AI-assisted research summary: Anyone is not allowed to demolish or cause the collapse of a building or part of a building without instructions from the Council.
16. Mtu yeyote hataruhusiwa kubomoa au kusababisha kubomoka kwa jengo au sehemu ya jengo bila kupata maelekezo ya Halmashauri. Wajibu wa mmiliki wa duka la kuuza nyama Siku ya usafi - 17 Verify source ↗
Kila mmiliki wa duka la kuuzia nyama
AI-assisted research summary: Mmiliki wa duka la kuuzia nyama lazima ahakikishe duka na vifaa vyake vina mazingira ya usafi, na muhudumu awe na mavazi maalum na afanyiwe uchunguzi wa afya kila baada ya miezi sita.
17. Kila mmiliki wa duka la kuuzia nyama anapaswa kuhakikisha kwamba- (a) ana jengo la kudumu lililosakafiwa na kuwekwa marumaru nyeupe kwenye sakafu na kuta kwa urefu wa futi sita kutoka usawa wa sakafu; (b) jengo lina maji safi, gogo na misumeno ya kukatia nyama; (c) kuna pipa la kuhifadhia taka; (d) muhudumu ana koti jeupe pamoja na viatu vyeupe aina ya buti; (e) muhudumu anapima afya kila baada ya miezi sita. - 18 Verify source ↗
(1) Kila jumamosi ya mwisho wa mwezi
AI-assisted research summary: Kila mwisho wa mwezi, siku maalumu ya usafi wa mazingira hufanyika, wakazi wa vijiji na vitongoji wanapaswa kushiriki, na kila mtu lazima ahakikishe eneo lake linakuwa safi.
18.-(1) Kila jumamosi ya mwisho wa mwezi itakuwa ni siku maalumu ya kufanya usafi wa mazingira katika maeneo yote ya Halmashauri. (2) Kila mkazi katika Kijiji na Kitongoji anapaswa kushiriki usafi wa mazingira kwa siku iliyopangwa na Halmashauri katika maeneo yao na maeneo ya umma. (3) Kila mtu atahakikisha eneo lake la makazi na 6 Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Tangazo La Serikali Na. 270 (Linaendelea) Usafi katika kaya Wajibu wa kuwa na choo na kukitumia Udhibiti utupaji wa taka linalomzunguka, eneo analofanyia biashara, eneo la wazi lililokaribu naye kwa umbali wa mita kumi na eneo la mazingira ya ofisi ni safi kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. - 19 Verify source ↗
(1) Kila mkazi mwenye nyumba, mmiliki au
AI-assisted research summary: Wakazi, wamiliki na wapangaji lazima wawe na choo, waendelee kusafisha na kutunza eneo safi, na waweke madirisha makubwa kwa kiwango cha chini cha 1/8 ya ukubwa wa chumba au kama Halmashauri itakavyokubali.
19.-(1) Kila mkazi mwenye nyumba, mmiliki au mpangaji anapaswa kuwa na choo, kupalilia majani, kufagia kila mara na kutunza mazingira safi umbali wa ft. 10 toka ukuta wa jengo kama ilivyo katika vipimo vilivyowekwa na kukubalika na Halmashauri. (2) Kila mkazi mwenye nyumba, mmiliki au mkabidhiwa atapaswa kuweka lake madirisha makubwa yasiyopungua 1/8 ya ukubwa wa chumba au vipimo vilivyowekwa na kukubaliwa na Halmashauri. jengo - 20 Verify source ↗
Kila mmiliki wa nyumba au mpangaji anapaswa
AI-assisted research summary: Kila mmiliki wa nyumba au mpangaji lazima ahakikishe nyumba ina choo safi na imara, pa kunawia mikono palipo na maji safi na sabuni ya kimiminika, na choo kijengwe mita 60 kutoka chanzo chochote cha maji.
20. Kila mmiliki wa nyumba au mpangaji anapaswa kuhakikisha kwamba- (a) nyumba yake ina choo safi, imara kwa matumizi ya wakazi wa nyumba hiyo; (b) anaweka sehemu maalumu ya kunawia mikono ikiwa na maji safi na sabuni maalumu ya kimiminika; na (c) choo kinajengwa umbali wa mita sitini kutoka chanzo chochote cha maji. - 21 Verify source ↗
(1) Watumiaji wa vyombo vya usafiri binafsi au
AI-assisted research summary: Watumiaji wa vyombo vya usafiri binafsi au vya umma hawapaswi kutupa taka nje ya vyombo wanavyotumia au kuzitupa ovyo katika maeneo yaliyotajwa; wanapaswa pia kuziweka taka kwenye chombo cha kuhifadhia taka kilichopo ndani ya chombo husika.
21.-(1) Watumiaji wa vyombo vya usafiri binafsi au vya umma hawapaswi- (a) kutupa taka nje ya vyombo wanavyotumia; na (b) kutupa taka ovyo katika maeneo ya makazi, biashara, mifereji ya maji ya mvua, hifadhi ya ambapo au mahali barabara hapajatengwa kwa ajili ya kutupa taka. popote (2) Taka zilizorejewa chini ya kanuni ndogo ya (1) zitawekwa kwenye chombo cha kuhifadhia taka kilichopo kwenye chombo husika. (3) Mtu yeyote au mkazi anapaswa kuhakikisha taka katika vyombo maalumu anatupa uchafu au 7 Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Tangazo La Serikali Na. 270 (Linaendelea) Uhifadhi maji taka Vyoo vya muda katika mikusanyiko Vyoo katika majengo ya biashara Vikundi vya usafi vilivyowekwa kwa ajili ya kutunzia taka katika maeneo maalumu yaliyotengwa. - 22 Verify source ↗
(1) Kila mmiliki wa nyumba anatakiwa
AI-assisted research summary: Mmiliki wa nyumba lazima awe na sehemu ya kuhifadhi maji taka na ayanyonye yanapojaa. Pia, mtu yeyote haruhusiwi kuachilia maji taka au kinyesi kwenye mifereji ya maji ya mvua, mabonde, maji yanayotembea, au sehemu nyingine zisizoruhusiwa.
22.-(1) Kila mmiliki wa nyumba anatakiwa kuhakikisha kuwa ana karo la kuhifadhi maji taka na atawajibika kunyonya maji taka pale karo linapojaa. (2) Mtu yeyote hapaswi kufungulia na kutiririsha maji taka au kinyesi kutoka chooni au sehemu yoyote wakati wa mvua au wakati wowote kwenye mifereji ya maji ya mvua, mabonde au maji yanayotembea au sehemu nyingine yoyote isiyoruhusiwa. taasisi yenye - 23 Verify source ↗
Mtu, kikundi au
AI-assisted research summary: Mtu au kikundi kinachokusanya watu kwa ajili ya mkutano, sherehe au mkusanyiko mwingine lazima kiombe idhini ya Halmashauri kabla ya kuweka au kujenga vyoo vya muda ikiwa eneo halina choo cha kudumu.
23. Mtu, kikundi au la kukusanya watu kwa madhumuni ya mkutano, sherehe au mkusanyiko wowote inatakiwa kuomba idhini kutoka Halmashauri ili kuweka au kujenga vyoo vya muda endapo eneo hilo hakuna choo cha kudumu. lengo - 24 Verify source ↗
Kila mmiliki wa jengo la biashara anatakiwa
AI-assisted research summary: Mmiliki wa jengo la biashara lazima ajenge vyoo vinavyokubalika kwa matumizi ya wateja, vikizingatia jinsia zote.
24. Kila mmiliki wa jengo la biashara anatakiwa kujenga vyoo vyenye viwango vinavyokubalika chini ya Sheria Ndogo hii kwa ajili ya matumizi ya wateja wake kwa kuzingatia jinsia zote. - 25 Verify source ↗
Halmashauri itahamasisha uundaji wa vikundi
AI-assisted research summary: Halmashauri must encourage and recognize community groups so they can help manage solid waste and environmental cleanliness in villages and hamlets, after contracting with the Halmashauri.
25. Halmashauri itahamasisha uundaji wa vikundi jamii na kuvitambua ili kuviwezesha kufanya shughuli za udhibiti wa taka ngumu pamoja na usafi wa mazingira katika Vijiji na Vitongoji baada ya kuingia mkataba na Halmashauri. Ilani ya kujenga au kurekebisha choo - 26 Verify source ↗
Endapo katika ukaguzi wa afya itagundulika
AI-assisted research summary: If a health inspection finds a house has no toilet, an overflowing toilet, or a toilet unfit for human use, the authorized officer must issue a notice to the owner or tenant setting out the required corrective conditions.
26. Endapo katika ukaguzi wa afya itagundulika kuwa nyumba yoyote haina choo au choo kilichopo kimejaa au hakifai kwa matumizi ya binadamu, afisa mwidhiniwa ilani kwa mmiliki wa nyumba au mpangaji atatoa akiainisha masharti ya kurekebisha hali hiyo kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Nne. 8 Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Tangazo La Serikali Na. 270 (Linaendelea) Uzuiaji wa shughuli wakati wa magonjwa ya mlipuko Ukamataji wakati wa zuio - 27 Verify source ↗
Mkurugenzi anaweza kutoa amri ya kuzuia
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kuzuia shughuli fulani zisifanyike ikiwa ana sababu ya kuamini zinaweza kusababisha kuenea kwa magonjwa ya mlipuko na kuathiri maisha ya binadamu.
27. Mkurugenzi anaweza kutoa amri ya kuzuia shughuli yoyote isifanyike kama vile utengenezaji wa vyakula, pombe, mijumuiko, sherehe na mikusanyiko yoyote kwa kutangaza kwa njia ya kipaza sauti, maandishi au kupitia vyombo vya habari endapo atakuwa na sababu ya kuamini kwamba shughuli hiyo inaweza kusababisha kuenea kwa magonjwa ya mlipuko na kuleta athari kwa maisha ya binadamu. - 28 Verify source ↗
(1) Halmashauri
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kumkamata mtu anayekiuka zuio la uuzaji wa vyakula wakati wa magonjwa ya mlipuko, kuharibu vyakula vinavyoharibika haraka, na kuhifadhi vyakula visivyoharibika hadi zuio liishe.
28.-(1) Halmashauri itakuwa na mamlaka ya kumkamata mtu yeyote ambaye atakaidi amri ya zuio la kufanyika kwa shughuli ya uuzaji wa vyakula wakati wa magonjwa ya mlipuko. (2) Endapo mtu aliyekamatwa alikuwa anauza vyakula ambavyo vinaharibika kwa haraka Halmashauri itaharibu vyakula hivyo. (3) Bila kuathiri kanuni ndogo ya (1) na (2), endapo vyakula haraka Halmashauri ina jukumu la kuvihifadhi hadi mwisho wa amri ya zuio. vilivyokamatwa haviharibiki kwa (4) Halmashauri haitahusika na gharama zozote huo zitakazotokea umesababishwa na uzembe wa afisa wa Halmashauri. isipokuwa uharibifu kama Ilani ya kuondoa kero - 29 Verify source ↗
Endapo Afisa mwidhiniwa atagundua kuwa
AI-assisted research summary: If an authorized officer finds a nuisance in an inspected area, the officer must issue a notice within seven days telling the house owner, tenant, user, or any concerned person to remove it as listed in the Fifth Schedule.
29. Endapo Afisa mwidhiniwa atagundua kuwa eneo alilokagua lina kero yoyote atatoa ilani ndani ya siku saba kwa mmiliki wa nyumba, mpangaji, mtumiaji au mtu yeyote anayehusika akimtaka kuondoa kero hiyo kama ilivyoainishwa kwenye Jedwali la Tano. Uteuzi wa Wakala - 30 Verify source ↗
(1) Halmashauri inaweza kumteua Wakala kwa
AI-assisted research summary: The Council may appoint an agent to provide cleaning and waste collection services on its behalf. An appointed agent must also have a contract with the Council and collect and dispose of the waste at the Council’s main dump.
30.-(1) Halmashauri inaweza kumteua Wakala kwa ajili ya kutoa huduma ya usafishaji na ukusanyaji taka kwa niaba yake. (2) Wakala aliyeteuliwa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii ana wajibu wa kuhakikisha kuwa- 9 Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Tangazo La Serikali Na. 270 (Linaendelea) Makosa (a) ameingia mkataba na Halmashauri kwa ajili ya kutoa huduma ya usafi wa mazingira. (b) anakusanya na kutupa taka hizo kwenye dampo kuu la Halmashauri. - 31 Verify source ↗
Mtu yeyote
AI-assisted research summary: Mtu yeyote haruhusiwi kutupa au kumwaga taka, kufanya uchafuzi, kuvuta sigara au kufanya shughuli zilizoelezwa kwenye maeneo yaliyotajwa bila kutengwa au bila kibali rasmi pale panapotakiwa.
31. Mtu yeyote- (a) atakayetupa taka au uchafu wowote au kuacha takataka au uchafu kwenye nyumba, kiwanja, mfereji wa maji ya mvua, barabara au eneo linalopakana na nyumba yoyote au ardhi yoyote au karibu na maeneo ya nyumba au mahali popote ambapo hapajatengwa kwa shughuli hiyo; (b) atakaye mzuia au kujaribu kumzuia au kumshawishi mtu au kundi la watu kumzuia afisa mwidhiniwa asitekeleze wajibu wake chini ya Sheria Ndogo hii; (c) atakayemwaga taka barabarani, kwenye mtaro wa maji ya mvua, uchochoroni, au mahali popote hadharani au katika eneo lolote lisiloruhusiwa; (d) atakayeendesha biashara ya pombe ndani ya nyumba ya makazi; (e) atakayetiririsha maji machafu barabarani au katika eneo la nyumba ya jirani; (f) atakayeosha magari, kufua, kunywesha mifugo na kukoroga dawa za mimea ndani ya mito, mabwawa, lambo au ndani ya chanzo au kisima kinachotumika kwa matumizi ya binadamu; (g) atakayepika vyakula pembezoni mwa barabara au nje ya majengo mengine; (h) atakayeuza vyakula maeneo yasiyo rasmi na kushindwa kuhifadhi chakula kwenye kabati safi lililofunikwa na lenye kioo; (i) atakayefanya matengenezo ya magari, pikipiki na mitambo, katika maeneo ya wazi, makazi, 10 Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Tangazo La Serikali Na. 270 (Linaendelea) barabarani, uchochoroni, au katika maeneo ambayo hayajatengwa kwa shughuli hizo bila kuzingatia taratibu za mipango miji; (j) atakayevuta sigara hadharani au mahali pa jumuiya au kwenye vyombo vya usafiri; (k) atakayetema mate hovyo au kutema mate barabarani au mahali pa jumuiya; (l) atakayeacha nyumba anayoishi au kumiliki au kufanyia shughuli zake katika hali ya uchafu yenye kuleta kero au chukizo; (m) atakayeacha chombo cha usafiri katika hali ya uchafu; (n) atakayeendesha shughuli za viwanda katika maeneo barabarani, ya wazi, makazi, uchochoroni, au katika maeneo ambayo hayajatengwa bila kwa kuzingatia taratibu za mipango miji; shughuli hizo (o) atakayeanzisha au kufungua karakana katika majengo, majumba au maeneo ya makazi; (p) atakayeenda haja ndogo au kubwa hovyo barabarani, uchochoroni, upenuni; (q) atakayefanya biashara ya kuosha gari, pikipiki au mtambo wowote katika eneo la makazi, eneo la wazi au eneo ambalo halikutengwa kwa shughuli hiyo au kuruhusu eneo lake kutumika kwa shughuli za kuosha vyombo vya moto katika maeneo ambayo hayakutengwa kwa shughuli hizo bila kupata kibali rasmi kutoka Halmashauri, anatenda kosa. Adhabu - 32 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayekiuka masharti yaliyowekwa
AI-assisted research summary: Anyone who breaches the conditions set by this bylaw commits an offence.
32. Mtu yeyote atakayekiuka masharti yaliyowekwa na Sheria Ndogo hii anatenda kosa na akipatikana na hatia atawajibika kulipa faini isiyozidi shilingi elfu ishirini au kifungo kisichozidi miezi mitatu au vyote. 11 Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Tangazo La Serikali Na. 270 (Linaendelea) Kufifilisha kosa - 33 Verify source ↗
Mkurugenzi anaweza kumtoza mtu yeyote
AI-assisted research summary: The Director may fine a person who commits an offence under these By-Laws Tsh 20,000 if the offender admits the offence voluntarily and is ready to complete the specified form.
33. Mkurugenzi anaweza kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii kiasi cha shilingi elfu ishirini iwapo mkosaji atakiri kosa kwa hiari yake na kuwa tayari kujaza fomu maalumu iliyoainishwa kwenye Jedwali la Sita. 12 Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Tangazo La Serikali Na. 270 (Linaendelea) _____________ JEDWALI LA KWANZA ________________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 9) ADA YA UKAGUZI WA AFYA Na. Aina/ Eneo la Ukaguzi Kiwango cha Ada (Tshs.)
Part
JEDWALI LA KWANZA
- 9 Verify source ↗
Section 9
AI-assisted research summary: The section lists premises and business places, including guest houses, hotels, restaurants, butcheries, meat-grilling areas, bars, depots, and residential houses and their surroundings.
9. Nyumba za kulala wageni (guest houses) Hoteli, mighahawa, nyumba za kuuzia vyakula vilivyopikwa Bucha za kuuzia nyama Kibanda na maeneo ya kuchomea nyama Vibanda au maeneo ya kuchomea nyama, kukaanga chips, nyama na mayai Kumbi za muziki, (disko, dansi), baa Vibanda vya biashara na maeneo ya biashara nyinginezo Maghala ya bidhaa za vyakula vinywaji (depots) Nyumba za makazi na mazingira ya nyumba za makazi - 10 Verify source ↗
Maduka ya madawa baridi ya binadamu au mifugo
AI-assisted research summary: Section title on shops selling human or veterinary cold medicines.
10. Maduka ya madawa baridi ya binadamu au mifugo - 11 Verify source ↗
Section 11
AI-assisted research summary: This provision is titled about dispensaries, clinics, health centers, and private institutions.
11. Zahanati, kliniki na vituo vya afya na taasisi za watu binafsi - 12 Verify source ↗
Maeneo ya biashara yaliyofungwa baada ya ukaguzi wa awali na kuomba
AI-assisted research summary: This section refers to business premises that were closed after an initial inspection and then requested to be inspected again.
12. Maeneo ya biashara yaliyofungwa baada ya ukaguzi wa awali na kuomba kufanyiwa ukaguzi mpya (reinspection) Duka au kibanda cha biashara ya jumla Ukaguzi wa Viosk (groceries) - 18 Verify source ↗
Section 18
AI-assisted research summary: This section lists commercial toilets operated by individuals, workshops, vehicle and machinery garages, metal workshops, and wood industries.
18. Vyoo vya kibiashara vinavyoendeshwa na watu binafsi Karakana, gereji za magari na mitambo Karakana za vyuma na viwanda vya mbao - 20 Verify source ↗
Section 20
AI-assisted research summary: This section lists charges for waste collection and disposal for different types of businesses and places, including some free entries.
20. Saluni ya kiume 5, 000/= 3, 000/= 3, 000/= 1,000/= 1,000/= 5,000/= 3,000/= 5, 000/= BURE 5,000/= 3,000/= 3,000/= 3,000/= 2,000/= 2,000/= 3,000/= 3,000/= 2,000/= 1,000/= 2,000/= 13 Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Tangazo La Serikali Na. 270 (Linaendelea) _______________ JEDWALI LA PILI _______________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 11) GHARAMA ZA UKUSANYAJI NA UZOAJI TAKA Na. Aina ya Biashara/ mchangiaji Zahanati (Taka zisizo hatari) Fundi Seremala Fundi chuma Kituo cha Afya (Taka zisizo hatari) Karakana au gereji za magari Karakana nyinginezo Duka la jumla/ Super markets au mini Super markets Duka la reja-reja Mgahawa mdogo/ kibanda cha kuuzia chai au chakula Kioski na Glosari Nyumba ya kulala wageni (Guest house)
Part
JEDWALI LA PILI
- 16 Verify source ↗
Section 16
AI-assisted research summary: This section is titled for a fish or meat selling shop (bucha ya samaki au nyama).
16. Duka la kuuza samaki au nyama (bucha ya samaki au nyama) - 17 Verify source ↗
Kibanda au kituo cha Nyama choma/ chips kinachojitegemea
AI-assisted research summary: Section heading for an independent nyama choma/chips kiosk or food outlet.
17. Kibanda au kituo cha Nyama choma/ chips kinachojitegemea - 23 Verify source ↗
Kibanda au mwavuli wa kuuza vocha za simu
AI-assisted research summary: Section 23 concerns a kiosk or umbrella used for selling phone vouchers.
23. Kibanda au mwavuli wa kuuza vocha za simu - 24 Verify source ↗
Kituo cha kuuzia nishati ya mafuta (Filling station)
AI-assisted research summary: This section is titled “Kituo cha kuuzia nishati ya mafuta (Filling station)”.
24. Kituo cha kuuzia nishati ya mafuta (Filling station) - 35 Verify source ↗
Ofisi za Taasisi kama benki, posta na nk
AI-assisted research summary: Section on offices for institutions such as banks and post offices.
35. Ofisi za Taasisi kama benki, posta na nk - 36 Verify source ↗
Section 36
AI-assisted research summary: Hii sehemu inaorodhesha aina za biashara na kiwango cha ada ya kila mwezi (Tshs) kinachohusiana nazo.
36. Stationaries na maduka ya kuuza vitabu Toroli la bidhaa au matunda Stoo za mkaa Stoo za mbao 14 Kiwango cha Ada kwa Mwezi (Tshs) 3,000/= 3,000/= 3, 000/= 3, 000/= 3, 000/= 5,000/= 2, 000/= 5,000/= 5,000/= 5,000/= 2,000/= 2, 000/= 3,000/= 5,000/= 5,000/= 3,000/= 3,000/= 2, 000/= 1,000/= 30, 000/= 2,000/= 3000/= 5,00/= 5,000/= 2,000/= 1,000/= 1,000/= 1,000/= 5,000/= 5,000/= 2,000/= 10,000/= 1,000/= 200/= 10,000/= 5,000/= Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Tangazo La Serikali Na. 270 (Linaendelea) - 37 Verify source ↗
Duka la Dawa la Dawa baridi za binadamu, duka la dawa za mifugo au
AI-assisted research summary: Section 37 mentions human medicine shops, veterinary drug shops, and a figure of 3,000/=.
37. Duka la Dawa la Dawa baridi za binadamu, duka la dawa za mifugo au 3,000/= pembejeo za kilimo - 38 Verify source ↗
Maghala
AI-assisted research summary: The text shows a Tshs 5,000/= entry for “Maghala” and includes sanitation-related notice forms.
38. Maghala 5,000/= 15 Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Tangazo La Serikali Na. 270 (Linaendelea) _________________ JEDWALI LA TATU _________________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 12) GHARAMA ZA UTUPAJI TAKA KWENYE DAMPO Na. 1 2 Kiasi cha Taka Taka za aina yoyote kwa kiwango cha ujazo chini ya tani moja Taka za aina yoyote kwa kiwango cha ujazo tani moja hadi tani saba Ada kwa Mwezi (Tshs) 10,000/= 20,000/= ________________ JEDWALI LA NNE ________________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 26) HALMASHAURI YA WILAYA YA NAMTUMBO ILANI YA KUJENGA CHOO SEHEMU ‘A’ Mtaa/Kijiji……………Kata Ndugu…………………………………………wa ya………………………………………………..unaarifiwa kwamba katika ukaguzi uliofanyika ya Tarehe………..Mwezi…………Mwaka……………… Biashara/kuishi/kutolea eneo la……………………..………… kitongoji/Mtaa*……………Kijiji Katika cha…………………Kata ya………………… Imekuwa haina choo/choo kimejaa/kimeharibika * hivyo unaamriwa kutekeleza mambo yafuatayo: (1)……………………………………………………………………… (2)……………………………………………………………………… (3)……………………………………………………………………... namba..………………….iliyopo huduma* nyumba Katika yako SEHEMU ‘B’ Unapewa muda wa siku thelathini tu tangu siku ya kupokea ilani hii kutekeleza maelekezo yote yaliyoelekezwa katika sehemu ‘A’ ya Ilani hii. SEHEMU ‘C’ Ukaguzi wa kuthibitisha utekelezaji wa maelekezo uliyopewa utafanyika tarehe…………… endapo utashindwa kutekeleza maelekezo ndani ya muda uliopewa Halmashauri itakuchukulia hatua kali za kisheria bila kukupa taarifa nyingine. IMEPOKELEWA NA: Jina……………………………. …… Saini…………………………… …… Wadhifa……………………………… Tarehe…………………………. …… 16 Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Tangazo La Serikali Na. 270 (Linaendelea) KWA MATUMIZI YA OFISI TU Kimetolewa na: Jina la Afisa Mwidhiniwa…………………………………..Saini……… Wadhifa:……………………………………………………………….. Tarehe:………………… Muhuri:…………………………………………… *futa lisilohusika 17 Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Tangazo La Serikali Na. 270 (Linaendelea) _________________ JEDWALI LA TANO _________________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 29) HALMASHAURI YA WILAYA YA NAMTUMBO ILANI YA KUONDOA KERO SEHEMU ‘A’ Mtaa/Kijiji………………………Kata Ndugu………………………………………………wa ya………………. uliofanyika Tarehe…….....mwezi…………mwaka………… katika nyumba yako ya Biashara/Kuishi/Kutolea Huduma* iliyopo eneo la……………………………….kumekutwa na adha zifuatazo: unaarifiwa kwamba ukaguzi katika (1)……………………………………………………………… (2)……………………………………………………………… (3)……………………………………………………………… (4)……………………………………………………………… (5)……………………………………………………………… SEHEMU ‘B’ Kwa ilani hii unaamriwa kufanya yafuatayo:- (1)……………………………………………………………… (2)……………………………………………………………… (3)……………………………………………………………… (4)………………………………………………………………… (5)………………………………………………………………… SEHEMU ‘C’ Unapewa muda wa siku ……… tangu siku ya kupokea ilani hii, unatakiwa kutekeleza yote yaliyoelezwa katika sehemu ‘B’ ya ilani hii, kushindwa kwako kutekeleza ndani ya muda uliopewa Halmashauri italazimika kukuchukulia hatua kali za Kisheria bila kulazimika kukupa taarifa nyingine. IMEPOKELEWA NA: Jina……………………………. …… Saini…………………………… …… Wadhifa……………………………… Tarehe…………………………. …… KWA MATUMIZI YA OFISI TU Kimetolewa na: Jina la afisa mwidhiniwa…………………………………..Saini……… Wadhifa:……………………………………………………………….. Tarehe:………………… Muhuri:…………………………………………… *futa lisilohusika 18 Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Tangazo La Serikali Na. 270 (Linaendelea) _______________ JEDWALI LA SITA _______________ (Limetengenezwa chini ya kanuni ya 33) KUFIFILISHA KOSA Mimi………………………………………………………. nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya……………………………………. ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashuri ya Wilaya ya Namtumbo, kwamba mnamo tarehe;…… ya Mwezi;….…. Mwaka…….… nilitenda kosa la kukiuka masharti ya kifungu cha….… cha Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo ya Mwaka 2024. Kwa Mamlaka aliyopewa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo, niko tayari kulipa kiasi cha Ada au Ushuru ninaodaiwa pamoja na faini. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA MIMI MWENYEWE KWA HIARI YANGU KADIRI YA UFAHAMU WANGU: Leo tarehe;…....... ya Mwezi;………… Mwaka;………….. Jina;…………………………………..……………………. Saini;…………………………..…………………………… MBELE YANGU : Jina;…………………………….………..…………………… Wadhifa;…………………………………………………..……. Saini;………………………………………………………… Tarehe;……………………………………………………… 19 Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo Tangazo La Serikali Na. 270 (Linaendelea) Lakiri ya Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo imegongwa kwenye Sheria Ndogo hizi kufutia azimio lililopitishwa kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya Namtumbo ulioitishwa na kufanyika Tarehe 10 Mwezi Juni Mwaka 2022 na kushuhudiwa Lakari hiyo ikigongwa mbele ya;- CHIRIKU HAMISI CHILUMBA Mkurugenzi Mtandaji Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo JUMA ALFAN PANDU Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo NAKUBALI / L.S Dodoma, MOHAMED OMARY MCHENGERWA 31 Januari, 2024 Waziri wa Nchi- Ofisi ya Rais (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa) 20
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Usafi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Namtumbo ya Mwaka 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in