Sheria Ndogo ya Afya, Usafi na Usimamizi wa Mazingira ya Halmashauri ya wilaya ya Songwe ya Mwaka 2024
This section states the short title of the by-law: the Songwe District Council Health, Sanitation and Environmental Management By-Law, 2024.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Afya, Usafi na Usimamizi wa Mazingira ya Halmashauri ya wilaya ya Songwe ya Mwaka 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This section states the short title of the by-law: the Songwe District Council Health, Sanitation and Environmental Management By-Law, 2024. This by-law applies throughout the area of the Songwe District Council Authority. This section defines key terms used in the by-law, including fees, appointed officers, the council, the director, and agents collecting fees and levies. Halmashauri ina mamlaka ya kusimamia, kukagua, kutoa elimu, kuteua wengine, kuchukua hatua za kisheria, kutunga kanuni au maelekezo, na kuingia mikataba kuhusu usafi, afya na mazingira. Wakazi na wafanyabiashara wenye biashara lazima wadumishe usafi wa nyumba au eneo la biashara kwa kufanya kazi za usafi na usimamizi wa taka zilizoorodheshwa.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Afya, Usafi na Usimamizi wa Mazingira ya Halmashauri ya wilaya ya Songwe ya Mwaka 2024
Showing 31 of 31
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo
AI-assisted research summary: This section states the short title of the by-law: the Songwe District Council Health, Sanitation and Environmental Management By-Law, 2024.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Afya, Usafi na Usimamizi wa Mazingira ya Halmashauri ya wilaya ya Songwe ya Mwaka 2024. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la
AI-assisted research summary: This by-law applies throughout the area of the Songwe District Council Authority.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la Mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya ya Songwe. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the by-law, including fees, appointed officers, the council, the director, and agents collecting fees and levies.
3. Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “ada” maana yake ni yake ni malipo yanayolipwa kwa Halmashauri kwa ajili ya huduma ya kuzoa taka; “adha” maana yake ni hali yoyote mbaya yenye kuleta madhara juu ya afya ya watu na viumbe hai kwa ujumla; “afya” maana yake ni hali timilifu ya kimwili, kiakili na kijamii na wala si tu kutokuwa na ugonjwa au kilema; “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni Afisa yeyote aliyeteuliwa na Mkurugenzi kwa lengo la kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “chakula” maana yake ni kitu chochote kinacholiwa na 1 Sheria Ndogo ya Afya, Usafi Na Usimamizi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Songwe Tangazo La Serikali Na. 271 (Linaendelea) binadamu na inajumuisha maji na dawa; “chanzo cha maji” maana yake ni eneo lolote ambalo limetengwa kwa ajili ya kuwa chanzo cha maji kwa ikiwemo visima, mito, matumizi ya chemchemi, vijito, na maeneo yote yanayopatikana maji; jamii sakafu inayosafishika, banda “choo bora” maana yake ni choo chochote cha maji chenye la kudumu, limeezekwa, lina mlango imara, bomba la kutoa hewa chafu na lenye mfuniko kwenye tundu la choo na shimo salama na safi kwa ajili ya kutupa kinyesi na mkojo wa binadamu, lililojengwa kwa vifaa vya kudumu; imara “chukizo la kiafya” maana yake ni kitu chochote kinachoweza kuleta kinyaa machoni kwa kuona, kunusa, hewa chafu, madhara au kuhatarisha afya za binadamu na wanyama; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Songwe; “hifadhi ya mazingira” maana yake ni utunzaji endelevu wa ardhi; mimea, hewa, viumbe hai na visivyo hai na vyanzo vya maji vinavyozingatia masharti na maelekezo yatakayotolewa na Afisa Mwidhiniwa chini ya Sheria Ndogo hii au Sheria nyingine yoyote; “jengo la biashara” maana yake ni jengo lolote lililojengwa na kuidhinishwa na Halmashauri kwa ajili ya kufanya biashara iliyokusudiwa; “kaya” maana yake mtu mzima anayejitegemea mwanamke au mwanaume, na mtoto au watoto inayoishi aidha kwenye nyumba nzima au ndani ya chumba kimoja kwenye eneo la Halmashauri; “kelele” maana yake ni kero inayosababishwa na sauti ambayo kwa asili inaweza kusababisha athari mbaya kwa afya ya binadamu au inakataliwa au 2 Sheria Ndogo ya Afya, Usafi Na Usimamizi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Songwe Tangazo La Serikali Na. 271 (Linaendelea) mazingira; “kero” au ”chukizo” maana yake ni kitu chochote kilicho katika hali yoyote iwe kinatumika, kimewekwa, kimejengwa, au ni kichafu kiasi cha kusababisha- (a) hatari kwa viumbe na maisha ya binadamu; (b) harufu mbaya au harufu ya kuudhi au kuleta kinyaa; (c) kuzaliana kwa wadudu hatari kama vile inzi, mende, sisimizi, panya, nyoka, nyuki, kunguni au viumbe wengine hatari; “kibali” maana yake ni idhini ya maandishi inayotolewa na Halmashaur i kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii; “kikundi cha mazingira” au “kikundi cha usafishaji” maana yake ni kikundi chochote cha watu kilichosajiliwa kufanya usafi na usimamizi wa mazingira na udhibiti wa uharibifu wa mazingira katika maeneo ya Halmashauri; “mabwawa ya maji taka” maana yake ni mabwawa yaliyojengwa kwa madhumuni ya kuhifadhi na kutakasa maji taka yanayotokana na kuosha vyombo, kutoka vyooni, kutoka bafuni, kufua nguo, kuosha nywele au shughuli zozote za nyumbani na viwanda; “magonjwa ya mlipuko” maana yake ni magonjwa ya yanayotokea kwa muda mfupi kuambukiza na kuenea kwa haraka na kuathiri watu wengi ndani ya muda mfupi yanayoweza kutolewa amri ya taadhari; “maji taka” maana yake ni maji yenye mchanganyiko wa kinyesi, mkojo, na maji kutoka masinki ya kuogea, 3 Sheria Ndogo ya Afya, Usafi Na Usimamizi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Songwe Tangazo La Serikali Na. 271 (Linaendelea) Sura ya 323 kutema mate na kunawia mikono, pamoja na maji yenye mchanganyiko wa vitu vingine vyenye asili chemikali au visivyo na chemikali; ya “mazalia ya wadudu” maana yake ni sehemu ambayo wadudu hufanya mazalio au kuishi kwa minajiri ya kufanya mzunguko wa maisha na baadae kuleta maadhara kwa binadamu; “mazao ya misitu” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa katika Sheria ya Misitu; “mazingira” maana yake ni masuala yote yanayohusisha maumbile halisi yanayowazunguka binadamu ikiwa ni pamoja na hewa, ardhi, maji, tabia ya nchi, sauti, mwanga, harufu, radha, vijiumbe, hali za kibaiolojia za wanyama na mimea, rasilimali za kitamaduni na jamii na binadamu na masuala ya uchumi inahusisha mazingira asilia na yaliyoundwa na binadamu na jinsi yanavyoingiliana; “mifugo” maana yake ni ng’ombe, punda, nguruwe, mbuzi, mbwa, kondoo, kuku na wanyama wengine wote wanaofugwa majumbani; “mgahawa” maana yake ni shughuli zote za uuzaji wa chakula na vinywaji zinazofanyika katika sehemu ya nje ya jengo maalumu la mgahawa au hoteli; “misitu” maana yake ni eneo la ardhi ambalo limefunikwa angalau kwa asilimia 10 na miti, uoto wa asili au uliopandwa, au asilimia 50 au zaidi ya vichaka na miti inayoota au ambayo itajumuisha na yote ya misitu ya hifadhi ambayo itatangaza chini ya sheria za misitu na mazao yote ya misitu ikijumuisha majani na nyasi ndani ya eneo la Halmashauri; “mkazi” maana yake ni mtu yeyote anayeishi katika eneo la Halmashauri na ambaye ana kaya au anaishi katika kaya au taasisi iliyopo katika eneo la Halmashauri; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe au Afisa yeyote aliyeteuliwa 4 Sheria Ndogo ya Afya, Usafi Na Usimamizi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Songwe Tangazo La Serikali Na. 271 (Linaendelea) Sura ya 191 kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi chini ya Sheria Ndogo hii; “mzalishaji wa maji taka” maana yake ni mtu, shirika, kiwanda au taasisi ambapo shughuli zake kwa namna yoyote zinazalisha maji taka; “taka” maana yake ni kitu chochote ambacho baada ya kukitumia hakina thamani kwa wakati huo na uwepo wake katika eneo hilo unaweza kusababisha chukizo la kiafya na kuhatarisha afya ya jamii; “taka hatarishi” maana yake ni kama ilivyoainishwa katika Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; “taka za biashara” maana yake ni aina yoyote ya taka ambazo hupatikana au hutokana na shughuli mbalimbali za kibiashara; “taka ngumu” maana yake ni kitu chochote ambacho baada ya kukitumia hakina thamani yoyote kwa jamii inayohusika, uwepo wake katika eneo husika unaweza kusababisha machukizo ya kiafya na kuhatarisha afya ya jamii; “taka za majumbani” maana yake ni mabaki ya vyakula, maganda ya matunda, majivu, nguo chakavu, karatasi za aina mbalimbali, kinyesi cha mifugo, taka za bustani na vitu vingine ambavyo baada ya kuvitumia hutupwa; “taka za viwandani” maana yake ni aina yoyote ya taka ambazo hutokana na uzalishaji wa shughuli mbalimbali viwandani; “ugonjwa wa kuambukizwa” maana yake ni ugonjwa wowote unaoweza kuambukizwa kutoka kwa mtu na mtu, mtu kwa mnyama au mtu kwa mdudu; “vitu hatari” maana yake ni kama ilivyotafsiriwa katika Sura ya 191 Sheria ya Usimamizi wa Mazingira; “Wakala” maana yake ni mtu binafsi, kikundi, taasisi au kampuni iliyoteuliwa kukusanya ada na ushuru kwa 5 Sheria Ndogo ya Afya, Usafi Na Usimamizi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Songwe Tangazo La Serikali Na. 271 (Linaendelea) niaba ya Halmashauri chini ya Sheria Ndogo hii. Mamlaka ya Halmashauri - 4 Verify source ↗
Halmashauri itakuwa na mamlaka ya kufanya
AI-assisted research summary: Halmashauri ina mamlaka ya kusimamia, kukagua, kutoa elimu, kuteua wengine, kuchukua hatua za kisheria, kutunga kanuni au maelekezo, na kuingia mikataba kuhusu usafi, afya na mazingira.
4. Halmashauri itakuwa na mamlaka ya kufanya yafuatayo: (a) Kusimamia utekelezaji wa shughuli za usafi afya na mazingira; (b) Kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kufuata kanuni za afya, usafi na kutunza mazingira; (c) Kuteua mtu yeyote, wakala, kikundi au taasisi kutekeleza shughuli za usimamizi wa afya, usafi na mazingira kwa niaba ya Halmashauri kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii; (d) Kufanya ukaguzi ili kubaini endapo kanuni za afya, usafi na utunzaji wa mazingira zinazingatiwa ndani ya eneo la Halmashauri; (e) Kumchukulia hatua za kisheria mtu yoyote anayekiuka Sheria Ndogo hii au Sheria nyingine inayohusiana na afya, usafi na usimamizi wa mazingira zilizotungwa na Bunge; (f) Kutunga kanuni, miongozo au kutoa maelekezo yatakayosaidia kulinda afya, usafi na usimamizi wa mazingira ndani ya eneo la Halmashauri; na (g) Kuingia mkataba na mtu yeyote, taasisi au kampuni kutelekeza shughuli za usimamizi wa afya, usafi na mazingira kwa niaba ya Halmshauri katika eneo ndani ya Halmashauri. Usafi wa mazingira - 5 Verify source ↗
(1) Kila mkazi au mfanyabiashara anayemiliki
AI-assisted research summary: Wakazi na wafanyabiashara wenye biashara lazima wadumishe usafi wa nyumba au eneo la biashara kwa kufanya kazi za usafi na usimamizi wa taka zilizoorodheshwa.
5.-(1) Kila mkazi au mfanyabiashara anayemiliki la biashara atakuwa na wajibu wa jengo au eneo kuhakikisha kwamba: (a) majani yanayozunguka jengo lake au makazi yanakatwa au kupaliliwa na kuondolewa katika eneo lake lote; (b) taka ngumu zote ikiwa ni pamoja na mifuko ya 6 Sheria Ndogo ya Afya, Usafi Na Usimamizi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Songwe Tangazo La Serikali Na. 271 (Linaendelea) plastiki zinakusanywa, kupelekwa katika eneo Halmashauri; kuhifadhiwa na lililoruhusiwa na (c) maji taka yanaelekezwa ndani ya mfumo wa maji taka; (d) anaboresha na kupaka rangi jengo lake kila inapochakaa; (e) anakuwa na choo kilicho bora na kisafi wakati wote; (f) anashiriki siku ya usafi ya Jumamosi ya kila mwisho wa mwezi; (g) anaondoa uchafu ikiwemo mchanga, majani, nyasi au vitu vingine vinavyofanana na hivyo katika mfereji wa maji ya mvua inayomzunguka au kupita kando ya nyumba yake au eneo la biashara yake, kiwanja chake na kuhakikisha mifereji hiyo inakuwa safi wakati wote; (h) hakuna mkusanyiko wa maji machafu, takataka au kitu chochote cha majimaji au kigumu ambacho kinaweza kuathiri upitishaji wa maji ya mvua na hivyo kuruhusu kuwepo kwa mazalia ya mbu au wadudu wengine wenye madhara kwa afya ya binadamu na mazingira kwa ujumla; (i) anafanya uchambuzi wa taka; (j) ana chombo imara chenye mfuniko kwa ajili kuhifadhi taka ngumu kabla hazijachukuliwa kwa ajili ya kwenda kutupwa katika eneo lililotengwa kwa ajili ya kuhifadhi taka; (k) anatunza na kuhifadhi vyombo vya kuhifadhia taka vinavyowekwa na Halmashauri; (l) kwa mfanyabiashara wa matunda au miwa, ana chombo maalumu cha kuhifadhi maganda au mabaki ya matunda. 7 Sheria Ndogo ya Afya, Usafi Na Usimamizi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Songwe Tangazo La Serikali Na. 271 (Linaendelea) Ada ya uzoaji taka Udhibiti wa kelele kwa shughuli mbalimbali za kijamii Kutiririsha maji taka - 6 Verify source ↗
(1) Kutakuwa na ada ya uzoaji taka ambayo
AI-assisted research summary: Halmashauri hutoza ada ya uzoaji taka; mzalishaji wa taka analipa kila tarehe 30 ya mwezi kwa Afisa Mwidhiniwa, na afisa huyo hutoa stakabadhi na kurekodi malipo.
6.-(1) Kutakuwa na ada ya uzoaji taka ambayo itatozwa na Halmashauri kwa la kufanikisha utekelezaji wa shughuli za usimamizi wa mazingira kwa viwango vilivyoainishwa kwenye Jedwali la Kwanza la Sheria Ndogo hii. lengo (2) Ada ya uzoaji taka italipwa kila tarehe 30 ya kila mwezi ndani ya mwezi husika na italipwa kwa Afisa Mwidhiniwa ambaye atatoa stakabadhi ya malipo kwa njia ya kieletroniki na atajaza katika rejista ya wazalishaji taka. (3) Iwapo mzalishaji wa taka atashindwa kulipia gharama ya huduma ya uzoaji taka kwa kipindi cha miezi miwili mfululizo Halmashauri itamchukulia hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani. - 7 Verify source ↗
Mtu yeyote haruhusiwi kusababisha au
AI-assisted research summary: Mtu yeyote haruhusiwi kusababisha au kuongeza kelele kupita kiasi without getting permission from the authorized officer.
7. Mtu yeyote haruhusiwi kusababisha au kufungulia kelele kupita kiasi iwe muziki, kelele za kiwanda, jenereta au kitu kingine chochotebila kupata kibali cha Afisa Mwidhiniwa. - 8 Verify source ↗
(1) Mtu yeyote hataruhusiwa, wakati wa mvua au
AI-assisted research summary: No one may discharge sewage or excreta onto roads, alleys, storm drains, water sources, or other undesignated places. Factories that produce sewage must connect it or build storage drains and ponds, and house owners must provide sewage storage pits and empty them when full.
8.-(1) Mtu yeyote hataruhusiwa, wakati wa mvua au wakati wowote, kutiririsha, kumwaga, kuruhusu au kusababisha kutiririsha au kumwaga maji taka au kinyesi kutoka chooni au sehemu yoyote barabarani, uchochoroni, kwenye mifereji ya maji ya mvua, kwenye vyanzo vya maji au sehemu yoyote isiyotengwa kwa ajili ya kuhifadhi maji taka. (2) Kila kiwanda kinachozalisha maji taka kitakuwa na wajibu wa kuhakikisha kuwa kinaunganisha maji taka au kujenga mifereji na mabwabwa kwa ajili ya kuhifadhi maji taka. (3) Kila mmiliki wa nyumba anatakiwa kuhakikisha kuwa ana karo la kuhifadhi maji taka na atawajibika kunyonya maji taka pale karo la kuhifadhi linapojaa 8 Sheria Ndogo ya Afya, Usafi Na Usimamizi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Songwe Tangazo La Serikali Na. 271 (Linaendelea) Taka za viwanda - 9 Verify source ↗
(1) Ni wajibu wa kila mwenye kiwanda
AI-assisted research summary: Kila mwenye kiwanda lazima ahakikishe taka na moshi vinadhibitiwa ili visilete madhara kwa watu na viumbe hai wengine, na kiwanda hakiruhusiwi kutoa uchafu, maji machafu, harufu mbaya, vumbi au kelele zinazosababisha kero kwa wakazi.
9.-(1) Ni wajibu wa kila mwenye kiwanda kuhakikisha kuwa taka kama vumbi, maganda, moshi na taka nyingine zinazoweza kuleta kero au adha kwa ujumla haziwafikii au kuleta madhara kwa binadamu na viumbe hai wengine. (2) Ni marufuku kwa kiwanda chochote kutoa au kusababisha kutoa uchafu wa aina yoyote, maji machafu au harufu mbaya, vumbi au kelele na kusababisha kero kwa wakazi. Taka hatarishi - 10 Verify source ↗
Ni marufuku kwa mtu yeyote, kampuni, wakala
AI-assisted research summary: Ni marufuku kuendesha uchomaji wa taka hatarishi bila kibali kutoka Halmashauri.
10. Ni marufuku kwa mtu yeyote, kampuni, wakala au taasisi kuendesha shughuli za uchomaji wa taka hatarishi bila kupata kibali kutoka Halmashauri. Utengenezaji na uuzaji wa vyakula - 11 Verify source ↗
Mtu yeyote hataruhusiwa kutengeneza,
AI-assisted research summary: Mtu yeyote haruhusiwi kutengeneza, kupika au kuuza chakula chochote mahali popote au nyumbani mpaka atimize masharti na kanuni za afya.
11. Mtu yeyote hataruhusiwa kutengeneza, kuchoma, kupika, kuchemsha au kuuza chakula cha aina yoyote mahali popote au kwenye nyumba yoyote mpaka awe ametimiza masharti na kanuni za afya. Uuzaji wa vyakula vilivyopikwa - 12 Verify source ↗
(1) Kila mtu anayeendesha biashara ya vyakula
AI-assisted research summary: Watu wanaoendesha biashara ya vyakula vya kupikwa au kukaangwa lazima wahifadhi chakula kwenye sanduku la mbao safi lenye kioo kinachozuia inzi, vumbi na wadudu; pia kuna marufuku kadhaa ya kushughulikia au kuweka vyakula na kuchafua hewa kwa moshi.
12.-(1) Kila mtu anayeendesha biashara ya vyakula vya kupikwa au kukaangwa atakuwa na wajibu wa kuhakikisha vyakula hivyo vinahifadhiwa kwenye sanduku lililotengenezwa kwa mbao safi na kuwekwa kioo kinachozuia inzi, vumbi na wadudu waletao madhara kwa afya ya binadamu. (2) Ni marufuku kwa mtu yeyote- (a) kuuza vyakula vikiwa vimewekwa chini, vyakula vyote vitatakiwa kuwekwa juu ya meza; visivyopikwa (b) kupanga vyakula nje ya duka la vyakula; na (c) mfanyabiashara, hospitali, taasisi, kaya, jengo au shughuli za viwanda kuchafua anga hewa kwa kuachilia moshi angani unaoweza kuleta madhara kwa binadamu, mimea na viumbe hai. 9 Sheria Ndogo ya Afya, Usafi Na Usimamizi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Songwe Tangazo La Serikali Na. 271 (Linaendelea) Usalama wa matumizi ya maji - 13 Verify source ↗
(1) Kila mkazi anapaswa kuhakikisha kwamba
AI-assisted research summary: Residents must ensure drinking water is clean and safe, and well owners must test well water for safety.
13.-(1) Kila mkazi anapaswa kuhakikisha kwamba maji yote yanayotumika kwa kunywa ni safi na salama bila kujali chanzo chake. (2) Kila mmiliki wa kisima atapaswa kuhakikisha maji ya kisima yanapimwa ili kuwa salama kwa matumizi. Uzuiaji wa shughuli wakati wa magonjwa ya mlipuko Ukamataji wakati wa zuio - 14 Verify source ↗
Mkurugenzi anaweza kutoa amri ya kuzuia
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kutoa amri ya kuzuia shughuli fulani au yoyote isifanyike ikiwa ana sababu ya kuamini inaweza kusababisha kuenea kwa magonjwa ya mlipuko na kuathiri maisha ya binadamu.
14. Mkurugenzi anaweza kutoa amri ya kuzuia shughuli yoyote isifanyike kama vile utengenezaji wa vyakula, pombe, mijumuiko, sherehe na mikusanyiko yoyote kwa kutangaza kwa njia ya kipaza sauti, maandishi au kupitia vyombo vya habari endapo atakuwa na sababu ya kuamini kwamba shughuli hiyo inaweza kusababisha kuenea kwa magonjwa ya mlipuko na kuleta athari kwa maisha ya binadamu. - 15 Verify source ↗
(1) Halmashauri
AI-assisted research summary: Halmashauri may arrest anyone who disobeys a ban on food sales during an epidemic.
15.-(1) Halmashauri itakuwa na mamlaka ya kumkamata mtu yeyote ambaye atakaidi amri ya zuio la kufanyika kwa shughuli ya uuzaji wa vyakula wakati wa magonjwa ya mlipuko. (2) Endapo mtu aliyekamatwa alikuwa anauza vyakula ambavyo vinaharibika kwa haraka Halmashauri itaharibu vyakula hivyo. (3) Bila kuathiri aya ndogo za (1) na (2), endapo vyakula vilivyokamatwa vitakuwa haviharibiki kwa haraka Halmashauri itakuwa na jukumu la kuvihifadhi hadi mwisho wa amri ya zuio. (4) Halmashauri haitahusika na gharama zozote zitakazotokea isipokuwa kama uharibifu huo utakuwa umesababishwa kwa uzembe wa Afisa wa Halmashauri. Upimaji wa afya - 16 Verify source ↗
(1) Itakuwa ni wajibu wa kila mhudumu wa
AI-assisted research summary: Certain food and hospitality workers must have health checks every six months, and owners must not let staff work without a health check.
16.-(1) Itakuwa ni wajibu wa kila mhudumu wa hoteli, migahawa, baa, bucha, sehemu za kuoka mikate, nyumba za kulala wageni, grosari au mtu yeyote 10 Sheria Ndogo ya Afya, Usafi Na Usimamizi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Songwe Tangazo La Serikali Na. 271 (Linaendelea) Uwezo wa kukagua Udhibiti wa ubebaji kokoto, mawe na mchanga Mabaki ya ujenzi Udhibiti utupaji wa taka anayetengeneza chakula kwa ajili ya kuuza kupima afya kila baada ya miezi sita. (2) Itakuwa ni kosa kwa mmiliki yeyote kuruhusu mhudumu yeyote kufanya kazi bila kupima afya yake. - 17 Verify source ↗
(1) Afisa Mwidhiniwa atakuwa na uwezo wa
AI-assisted research summary: Afisa Mwidhiniwa ana uwezo wa kukagua utekelezaji wa Sheria hii wakati wa saa za kazi au wakati wowote kwa ukaguzi maalumu; Mkurugenzi anaweza kuagiza hatua kuhusu jengo lililofungwa kwa biashara, lisilokaguliwa, au lililokutwa likikiuka masharti ya afya.
17.-(1) Afisa Mwidhiniwa atakuwa na uwezo wa lolote muda wowote kukagua kuingia katika utekelezaji wa Sheria hii wakati wa saa za kazi na wakati wowote inapotakiwa kufanyika kwa ukaguzi maalumu. jengo (2) Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kuagiza jengo ambalo kufungwa kwa biashara yoyote au halijakaguliwa au lililokaguliwa na kukutwa limekiuka kanuni na masharti ya afya. - 18 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayesafirisha mawe, mchanga au
AI-assisted research summary: Anyone transporting stones, sand, or gravel within a Halmashauri area must cover the vehicle or container used for transport.
18. Mtu yeyote atakayesafirisha mawe, mchanga au kokoto katika eneo la Halmashauri atahakikisha kuwa chombo anachotumia kusafirisha kimefunikwa ili kuzuia kumwagika na kuchafua mazingira. - 19 Verify source ↗
Mtu yeyote hataruhusiwa kubomoa au
AI-assisted research summary: A person may not demolish or cause a building or part of a building to collapse without notifying the Council and paying the costs set out in Schedule Two.
19. Mtu yeyote hataruhusiwa kubomoa au kusababisha kubomoka kwa jengo au sehemu ya jengo bila kutoa taarifa kwa Halmashauri na kulipa gharama kama ilivyoainishwa katika Jedwali la Pili la Sheria Ndogo hii. - 20 Verify source ↗
(1) Watumiaji wa vyombo vya usafiri binafsi au
AI-assisted research summary: Users of private or public transport must not throw waste outside the vehicle, and everyone must use designated waste containers instead of littering.
20.-(1) Watumiaji wa vyombo vya usafiri binafsi au vya umma hawataruhusiwa kutupa taka nje ya vyombo wanavyotumia na taka zote zitawekwa kwenye chombo cha kuhifadhia taka kilichomo kwenye chombo cha usafiri husika. (2) Ni marufuku kwa mtu yeyote kutupa taka ovyo katika maeneo ya makazi, biashara, mifereji ya maji ya mvua, hifadhi ya barabara au mahali popote pasipotengwa kwa ajili ya kutupa taka. (3) Mtu yeyote atakuwa na wajibu wa kuhakikisha 11 Sheria Ndogo ya Afya, Usafi Na Usimamizi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Songwe Tangazo La Serikali Na. 271 (Linaendelea) kwamba anatupa uchafu au taka katika vyombo maalumu vilivyowekwa kwa ajili ya kutunzia taka katika maeneo maalumu yaliyotengwa. Uanzishwaji wa Vikundi Jamii - 21 Verify source ↗
Halmashauri itakuwa na jukumu la kuhamasisha
AI-assisted research summary: Halmashauri must encourage the formation of community groups and recognize them so they can carry out solid waste control and environmental cleanliness activities after contracting with Halmashauri.
21. Halmashauri itakuwa na jukumu la kuhamasisha uundaji wa Vikundi Jamii na kuvitambua ili kuviwezesha kufanya shughuli za udhibiti wa taka ngumu pamoja na usafi wa mazingira baada ya kuingia mkataba na Halmashauri. Wajibu wa kuwa na choo na kukitumia - 22 Verify source ↗
Kila mmiliki wa nyumba au mpangaji atakuwa
AI-assisted research summary: House owners or tenants must ensure the house has a clean, sturdy toilet, a handwashing area with clean water and liquid soap, and that the toilet is built 60 metres from any water source.
22. Kila mmiliki wa nyumba au mpangaji atakuwa na wajibu wa kuhakikisha kwamba- (a) nyumba yake ina choo safi, imara kwa matumizi ya wakazi wa nyumba hiyo; (b) anaweka sehemu maalumu ya kunawia mikono ikiwa na maji safi na sabuni ya kimiminika; na (c) choo kinajengwa umbali wa mita sitini kutoka chanzo chochote cha maji. Vyoo vya umma - 23 Verify source ↗
(1) Halmashauri inaweza kujenga choo cha
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kujenga choo cha umma au kuruhusu wengine kujenga vyoo vya umma katika maeneo inayoona yanafaa.
23.-(1) Halmashauri inaweza kujenga choo cha umma au kumruhusu mtu binafsi, vikundi vya watu au taasisi kujenga vyoo vya umma katika maeneo ambayo Halmashauri itaona inafaa. (2) Vyoo vitakavyojengwa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii vitakuwa vya kudumu na: (a) matundu yasiyopungua mawili kwa wanawake na mawili kwa wanaume; (b) mfumo madhubuti wa maji na uwepo wa maji ya kutosha yaliyo safi na salama; (c) kuwa na chombo cha kuhifadhi maji ya akiba; (d) kuwa na bafu ya wanaume na wanawake; (e) kuwa na chumba maalumu cha kuvutia sigara; (f) kuwa na sehemu ya haja ndogo kwa wanaume; 12 Sheria Ndogo ya Afya, Usafi Na Usimamizi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Songwe Tangazo La Serikali Na. 271 (Linaendelea) (g) kuwa na chombo maalumu chenye mfuniko cha kuhifadhia taka zisizoweza kusukumwa na maji. Vyoo vya muda katika mikusanyiko - 24 Verify source ↗
Ni wajibu wa mtu yeyote, kikundi au taasisi
AI-assisted research summary: Watu, vikundi au taasisi zinazoandaa mikutano, sherehe au mikusanyiko lazima ziweke au zijenge vyoo vya muda baada ya kuomba idhini ya Halmashauri ikiwa eneo hilo halina choo cha kudumu.
24. Ni wajibu wa mtu yeyote, kikundi au taasisi yenye lengo la kukusanya watu kwa madhumuni ya mkutano, sherehe au mkusanyiko wowote kuweka au kujenga vyoo vya muda baada ya kuomba idhini kutoka Halmashauri endapo katika eneo husika hakuna choo cha kudumu. Vyoo katika majengo ya biashara Ilani ya kujenga au kurekebisha choo Ilani ya kuondoa kero - 25 Verify source ↗
Kila mmiliki wa jengo la biashara atatakiwa
AI-assisted research summary: Mmiliki wa jengo la biashara lazima ajenge vyoo vinavyokubalika kwa wateja wake.
25. Kila mmiliki wa jengo la biashara atatakiwa kujenga vyoo vyenye viwango vinavyokubalika chini ya Sheria Ndogo hii kwa ajili ya matumizi ya wateja wake kwa kuzingatia jinsi zote. - 26 Verify source ↗
Endapo katika ukaguzi wa afya itagundulika
AI-assisted research summary: If a health inspection finds a house has no toilet, an overfull toilet, or a toilet unfit for human use, the authorized officer must issue a notice to the owner or tenant.
26. Endapo katika ukaguzi wa afya itagundulika kuwa nyumba yoyote haina choo au choo kilichopo kimejaa au hakifai kwa matumizi ya binadamu, Afisa Mwidhiniwa atatoa ilani kwa mmiliki wa nyumba au mpangaji akiainisha masharti ya kurekebisha hali hiyo. - 27 Verify source ↗
(1) Endapo Afisa Mwidhiniwa atagundua kuwa
AI-assisted research summary: Afisa Mwidhiniwa akiona kero kwenye eneo alilokagua, lazima atoe ilani ndani ya siku saba kwa mhusika aiondoe. Mtu anayeshindwa kutekeleza masharti ya ilani ndani ya muda uliotajwa anatenda kosa.
27.-(1) Endapo Afisa Mwidhiniwa atagundua kuwa eneo alilokagua lina kero yoyote atatoa ilani ndani ya siku saba kwa mmiliki wa nyumba, mpangaji, mtumiaji au mtu yeyote anayehusika akimtaka kuondoa kero hiyo. (2) Mtu yeyote atakayeshindwa kutekeleza masharti ya ilani aliyopewa ndani ya muda ulioainishwa kwenye ilani atakuwa ametenda kosa. Uteuzi wa Wakala - 28 Verify source ↗
(1) Halmashauri itakuwa na mamlaka ya kuteua
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kuteua wakala wa kukusanya ada kwa niaba yake. Wakala aliyechaguliwa lazima akusanye ada zinazohusu afya, usafi na usimamizi wa mazingira, atumie mfumo wa kielektroniki, awasilishe makusanyo yote, na atekeleze masharti ya mkataba.
28.-(1) Halmashauri itakuwa na mamlaka ya kuteua Wakala wa kukusanya ada kwa niaba yake kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. (2) Wakala atakayeteuliwa chini ya Sheria hii atakuwa na wajibu wa: 13 Sheria Ndogo ya Afya, Usafi Na Usimamizi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Songwe Tangazo La Serikali Na. 271 (Linaendelea) Makosa (a) kukusanya, kwa niaba ya Halmashauri, ada mbalimbali zinazohusiana na afya, usafi na usimamizi wa mazingira, eneo alilopangiwa na kwa viwango vilivyoidhinishwa chini ya Sheria Ndogo hii; katika (b) kukusanya ada kwa kutumia mfumo wa kielekitroniki na kuwasilisha makusanyo yote kwa kuzingatia masharti ya mkataba wa uwakala alioingia na Halmashauri; na (c) kutekeleza masharti yote ya mkataba. - 29 Verify source ↗
Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa endapo
AI-assisted research summary: Mtu yeyote anatenda kosa akifanya mojawapo ya vitendo vilivyoorodheshwa, ikiwemo kutupa taka, kuchafua mazingira, kuvuta sigara hadharani, au kufanya shughuli fulani bila kibali.
29. Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa endapo- (a) atatupa taka au uchafu wowote au kuacha takataka au uchafu kwenye nyumba, kiwanja, mfereji wa maji ya mvua, barabara au eneo linalopakana na nyumba yoyote au ardhi yoyote au karibu na maeneo ya nyumba au mahali popote pasipotengwa kwa shughuli hiyo; (b) atamzuia au kujaribu kumzuia au atamshawishi mtu au kundi la watu kumzuia Afisa Mwidhiniwa asitekeleze wajibu wake chini ya Sheria Ndogo hii; (c) atamwaga taka barabarani, katika mtaro wa maji ya mvua, uchochoroni au mahali popote hadharani au katika eneo lolote lisiloruhusiwa; (d) ataendesha biashara ya pombe ndani ya nyumba ya makazi; (e) atatiririsha maji machafu barabarani au katika eneo la nyumba ya jirani; (f) ataosha magari, kufua, kunywesha mifugo na kukoroga dawa za mimea ndani ya mito, mabwawa, lambo au ndani ya chanzo au kisima kinachotumika kwa matumizi ya binadamu; (g) atapika vyakula pembezoni mwa barabara au nje 14 Sheria Ndogo ya Afya, Usafi Na Usimamizi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Songwe Tangazo La Serikali Na. 271 (Linaendelea) ya majengo mengine; (h) atauza vyakula maeneo yasiyo rasmi na kushindwa kuhifadhi chakula kwenye kabati safi lililofunikwa na lenye kioo; (i) atafanya matengenezo ya magari, pikipiki na mitambo, katika maeneo ya wazi, makazi, barabarani, uchochoroni, au katika maeneo yasiyotengwa kwa shughuli hizo bila kuzingatia taratibu za mipango miji; (j) atavuta sigara hadharani au mahali pa jumuiya au kwenye vyombo vya usafiri; (k) atatema mate ovyo au kutema mate barabarani au mahali pa jumuiya; (l) ataacha nyumba anayoishi, anayomiliki au kufanyia shughuli zake katika hali ya uchafu yenye kuleta kero au chukizo; (m) ataacha chombo cha usafiri katika hali ya uchafu; (n) ataendesha shughuli za viwanda katika maeneo ya wazi, makazi, barabarani, uchochoroni au katika maeneo yasiyotengwa kwa shughuli hizo bila kuzingatia taratibu za mipango miji; (o) ataanzisha au kufungua karakana katika majengo au majumba au maeneo ya makazi; (p) ataenda haja ndogo au kubwa ovyo barabarani, uchochoroni au upenuni; au (q) atafanya biashara ya kuosha gari, pikipiki au mtambo wowote katika eneo la makazi, eneo la wazi au eneo ambalo halikutengwa kwa shughuli hiyo au kuruhusu eneo lake kutumika kwa shughuli za kuosha vyombo vya moto katika maeneo ambayo hayakutengwa kwa shughuli hizo bila kupata kibali rasmi kutoka Halmashauri. 15 Sheria Ndogo ya Afya, Usafi Na Usimamizi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Songwe Tangazo La Serikali Na. 271 (Linaendelea) Adhabu Kufifilisha kosa - 30 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayepatikana na hatia kwa
AI-assisted research summary: A person convicted of an offence under this subsidiary legislation must pay a fine of up to 300,000 shillings, or go to prison for up to 12 months, or both.
30. Mtu yeyote atakayepatikana na hatia kwa kutenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii atawajibika kulipa faini isiyozidi shilingi laki tatu au kifungo kisichozidi miezi kumi na mbili jela au vyote kwa pamoja. - 31 Verify source ↗
Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kufifilisha kosa kwa kumtoza mkosaji kiasi kisichozidi shilingi 200,000 ikiwa mkosaji anakiri kosa, anakubali kujaza fomu ya Jedwali la Tatu, na analipa ada au ushuru unaodaiwa.
31. Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha kosa kwa kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii kiasi kisichozidi shilingi laki mbili endapo mkosaji atakiri kosa na kuwa tayari kujaza fomu maalumu iliyoainishwa katika Jedwali la Tatu la Sheria Ndogo hii na kulipa ada au ushuru anaodaiwa. _______________ JEDWALI LA KWANZA _______________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 6(1)) SEHEMU A: ADA YA UZOAJI WA TAKA Namba. 1 2 3 4 5 6 7 8 9 10 11 Aina ya Biashara Makazi (Kaya) Mgahawa Mdogo Mgahawa Mkubwa Nyumba ya kulala wageni Zahanati (Taka zisizo hatari) Hospitali Kiwanda cha Kuuza Mbao Fundi Selemala Wakubwa Fundi Selemala wa Kati Fundi Selemala Wadogo Fundi Chuma 16 Viwango (Shilingi) 3,000/= kwa mwezi 5,000/= kwa mwezi 15,000/= kwa mwezi 10,000/= kwa mwezi 5,000/= kwa mwezi 10,000/= kwa safari 10,000/= kwa mwezi 30,000/= kwa mwezi 20,000/= kwa mwezi 5,000/= kwa mwezi 15,000/= kwa Sheria Ndogo ya Afya, Usafi Na Usimamizi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Songwe Tangazo La Serikali Na. 271 (Linaendelea) 12 13 14 15 16 17 18 19 20 21 22 23 24 25 26 27 28 29 30 31 32 33 34 35 36 37 Karakana Kiwanda kidogo Kiwanda Kikubwa Duka la Jumla Duka la rejereja/huduma Shule ya msingi ya Bweni (Binafsi) Shule ya Msingi ya Kutwa (Binafsi) Shule ya Sekondari ya Bweni(Binafsi) Shule ya Sekondari ya kutwa(Binafsi) Kituo cha kulea watoto Kituo cha kutunzia watu wenye mahitaji maalumu Duka dogo la Chakula Duka kubwa la chakula Baa Klabu ya Usiku Kumbi za Sherehe Duka la kuuza Nyama na Samaki Dukala Dawa (jumla) Dobi Mdogo Dobi Mkubwa Fundi wa vifaa vya Umeme Fundi Cherehani Saluni Kituo cha kuuza mafuta Stoo Ghala 17 mwezi 20,000/= kwa mwezi 50, 000/= kwa mwezi 200,000/= kwa mwezi 10,000/= kwa mwezi 5,000/= kwa mwezi 20,000/= kwa mwezi 10,000/= kwa mwezi 30,000/= 15,000/= kwa mwezi 5,000/= kwa mwezi 5,000/= kwa mwezi 5,000/= kw3a mwezi 10,000/= kwa mwezi 10,000/= kwa mwezi 10,000/= kwa mwezi 20,000/= kwa mwezi 10,000/= kwa mwezi 10,000/= nkwa mwezi 3,000/= kwa mwezi 5,000/= kwa mwezi 5,000/= kwa mwezi 5,000/= kwa mwezi 5,000/= kwa mwezi 10,000/= kwa mwezi 5,000/= kwa mwezi 10,000/= kwa mwezi Sheria Ndogo ya Afya, Usafi Na Usimamizi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Songwe Tangazo La Serikali Na. 271 (Linaendelea) 38 39 40 41 42 43 44 45 46 47 48 Hoteli Taasisi Klabu ya pombe za asili Dahalia Kituo cha Michezo Uwanja wea Michezo Washona Viatu: Katikati ya Mji Pembezoni mwa Mji Stoo za Mkaa Mama lishe/ Baba lishe Vituo vya kuoshea magari Aina nyingine ya Biashara/ huduma 20,000/= kwa mwezi 20,000/= kwa mwezi 5,000/= kwa mwezi 20,000/= kwa mwezi 5,000/= kwa mwezi 10,000/= kwa mwezi 3,000/= 1,000/= 10,000/= kwa mwezi 5,000/= kwa mwezi 5,000/= kwa mwezi Ada itapangwa na kamati ya huduma husika na chanzo hicho kila itakapohitajika SEHEMU B GHARAMA ZA UTUPAJI TAKA KWENYE JAA LA TAKA Namba. 1 2 Kiasi cha taka Chini ya tani moja kwa safari Tani moja kwa safari Kiwango (Shilingi) 10,000/= 15,000/= ____________ JEDWALI LA PILI _____________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 19) GHARAMA ZA UBOMOAJI NA UONDOAJI WA MABAKI YA UJENZI Namba. 1 Eneo kwa mita ya ujazo Mita moja ya Mraba Kiwango 5,000/= _____________ 18 Sheria Ndogo ya Afya, Usafi Na Usimamizi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Songwe Tangazo La Serikali Na. 271 (Linaendelea) JEDWALI LA TATU _______________ (Limetungwa chini ya aya ya 31) KUFIFILISHA KOSA Mimi…………………………………………. nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya ………………………… ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe kwamba mnamo tarehe…………… ya mwezi…………….. Mwaka ………………………. nilitenda kosa la kukiuka masharti ya aya ndogo ya………… ya Sheria Ndogo ya (Afya, Usafi na Usimamizi wa Mazingira) ya Halmashauri ya Wilaya ya Songwe ya Mwaka 2024. Kwa mamlaka aliyopewa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe. niko tayari kulipa kiasi cha Ada au Ushuru ninayodaiwa pamoja na faini. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU Leo Tarehe…ya Mwezi……………Mwaka……. Jina…………………………………..….. Saini…………………………………..…. Mbele ya: Jina…………………………………………. wadhifa……………………………………… Saini……..………………………………….. Tarehe: …………………………………….. 19 Sheria Ndogo ya Afya, Usafi Na Usimamizi wa Mazingira ya Halmashauri ya Wilaya ya Songwe Tangazo La Serikali Na. 271 (Linaendelea) Nembo na muhuri wa Halmashauri ya wilaya ya SONGWE imebandikwa kwenye Sheria Ndogo hizi kufutia Azimio Na SDC/ MB/09/2023 lililopitishwa na Mkutano wa Baraza la Madiwani kilichoketi Tarehe 02/1/2023 na ubandikwaji huo kushuhudiwa na;- CPA CECILIA D KAVISHE Mkurugenzi Mtandaji Halmashauri ya Wilaya ya Songwe ABRAHAM KAGULUKA SAMBILA Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya Songwe NAKUBALI / L.S Dodoma, MOHAMED OMARY MCHENGERWA 30 Januari, 2024 Waziri wa Nchi- Ofisi ya Rais (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa) 20
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Afya, Usafi na Usimamizi wa Mazingira ya Halmashauri ya wilaya ya Songwe ya Mwaka 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in