Sheria Ndogo ya Kilimo, Chakula, Mifugo na Uvuvi ya Halmashauri ya Wilaya ya Songwe ya Mwaka 2024
This section gives the by-law its name: the Songwe District Council Agriculture, Food, Livestock and Fisheries By-law, 2024.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Kilimo, Chakula, Mifugo na Uvuvi ya Halmashauri ya Wilaya ya Songwe ya Mwaka 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This section gives the by-law its name: the Songwe District Council Agriculture, Food, Livestock and Fisheries By-law, 2024. This bylaw applies throughout the area of the Songwe District Council. This section defines key terms used in the by-law, including officials, the Council, farming, livestock, farmers, residents, irrigation schemes, special agricultural zones, and illegal fishing. Halmashauri ina wajibu wa kutekeleza hatua kadhaa za kusaidia kilimo katika kila kijiji. Serikali ya Kijiji ina wajibu wa kutenga ardhi kwa matumizi ya kilimo na ufugaji, kusaidia wakazi kupata ardhi ya kutosha, na kuhakikisha vijiji vina chakula cha kutosha pamoja na kilimo cha angalau ekari moja kwa mkazi anayehusika.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Kilimo, Chakula, Mifugo na Uvuvi ya Halmashauri ya Wilaya ya Songwe ya Mwaka 2024
Showing 28 of 28
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya
AI-assisted research summary: This section gives the by-law its name: the Songwe District Council Agriculture, Food, Livestock and Fisheries By-law, 2024.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Kilimo, Chakula, Mifugo na Uvuvi ya Halmashauri ya Wilaya ya Songwe ya Mwaka 2024. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la
AI-assisted research summary: This bylaw applies throughout the area of the Songwe District Council.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la Mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya ya Songwe. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii,
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the by-law, including officials, the Council, farming, livestock, farmers, residents, irrigation schemes, special agricultural zones, and illegal fishing.
3. Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni Afisa yeyote la aliyeteuliwa na kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; Mkurugenzi kwa lengo “Afisa Ugani” maana yake ni mtaalamu wa kilimo, mifugo, uvuvi na nyuki katika ngazi za Wilaya, Kata au Kijiji; “Bonde la Songwe’’ Maana yake ni eneo lote linalojumuisha kata za Ifwenkenya, Kanga, Galula, Mbuyuni, Mwambani, Chang’ombe, Magamba, Totowe, Mpona, Namkukwe, Manda, kijiji cha Maleza kata ya Mbangala na kijiji cha Mwambani kata ya Mwambani; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya 1 Sheria Ndogo ya Kilimo, Chakula, Mifugo na Uvuvi ya Halmashauri ya Wilaya ya Songwe Tangazo La Serikali Na. 272 (Linaendelea) Songwe; “kilimo” maana yake ni shughuli yoyote ya uzalishaji mali inayofanywa na binadamu na inajumuisha kilimo cha mazao, ufugaji wa wanyama hai, nyuki au samaki; “mfugo” maana yake ni ng’ombe, mbuzi, kondoo, kuku au wanyama wengine wafugwao na binadamu; “mfugaji” maana yake ni mtu yeyote anayejishughulisha na ufugaji wa mifugo katika eneo la Halmashauri kwa mujibu wa taratibu na miongozo itakayotolewa na Halmashauri; “mkazi” maana yake ni raia wa Tanzania ambaye kwa kawaida anaishi kwenye eneo la Halmashauri na ambaye ana kaya au anaishi katika kaya au taasisi iliyopo katika eneo la Halmashauri; “mkulima” maana yake ni mtu yeyote anayejishughulisha na uzalishaji au kilimo cha mazao ya chakula, biashara na matunda; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Songwe au Afisa yeyote atakayeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi; “skimu za umwagiliaji” maana yake ni miundombinu ya miradi ya maji ambayo imeanzishwa na Serikali kuu, Halmashauri au wadau wa maendeleo na kuwapa wananchi ili kuendeleza kilimo cha umwagiliaji; “uhawilishaji” maana yake ni kitendo cha uzalishaji wa wanyama kwa njia ya kisasa kwa kutumia mbegu za madume bora ili kupata kizazi kipya cha wanyama bora zaidi; “ukanda maalumu wa kilimo” maana yake ni eneo linalotumika kwa shughuli za kilimo kwa misimu miwili kwa mwaka, ikijumuisha vijiji vya Mwambani, Iseche-kikondo, Mbala-Mapolomoko, Mbuyuni- Ndanga, Kanga-Karibu na Mto Zira na Maleza; na “uvuvi haramu” maana yake ni uvuvi unaotumia zana zisizokubalika katika uvuvi kama vile mabomu, sumu, 2 Sheria Ndogo ya Kilimo, Chakula, Mifugo na Uvuvi ya Halmashauri ya Wilaya ya Songwe Tangazo La Serikali Na. 272 (Linaendelea) makokoro, vyandarua. nyavu zisizoruhusiwa, mikuki au Wajibu wa Halmasha uri SEHEMU YA PILI MASHARTI KUHUSU KILIMO
Part
SEHEMU YA PILI
- 4 Verify source ↗
Halmashauri itakuwa na wajibu wa
AI-assisted research summary: Halmashauri ina wajibu wa kutekeleza hatua kadhaa za kusaidia kilimo katika kila kijiji.
4. Halmashauri itakuwa na wajibu wa- (a) kuweka mabango kwenye kila kijiji yanayoeleza kanuni bora za kilimo zinazopaswa kuzingatiwa na mkulima kwa mazao yanayolimwa kwenye eneo hilo; (b) kuanzisha mashamba darasa ya mfano katika kila kijiji; (c) kuhakikisha upatikanaji wa maafisa ugani katika kila kijiji; (d) kuanzisha vituo vya kukuzia na kufundishia wanyama kazi; vyama (e) kuhamasisha vya uanzishwaji wa wakulima vya kuweka na kukopa au vyama vya msingi kwa lengo la kujipatia mikopo ya benki; (f) kuanzisha vituo maalumu kwa ajili ya kutoa mafunzo ya utumiaji na utunzaji wa zana bora za kilimo; (g) kuhamasisha matumizi ya wanyama kazi katika maeneo ambayo wafugaji hujishughulisha pia na kilimo cha mazao; (h) kushindanisha wakulima bora na maafisa ugani bora katika vijiji, kata na hatimaye halmashauri; (i) kuainisha matumizi bora ya ardhi ili kubainisha na kutofautisha ardhi ya mifugo, kilimo na hifadhi; (j) kusimamia upatikanaji wa mbolea na pembejeo nyingine za kilimo; na (k) kuhamasisha serikali za vijiji na wananchi kwa ujumla kujenga maghala ya chakula vijijini. Wajibu wa - 5 Verify source ↗
Serikali ya Kijiji itakuwa na wajibu wa
AI-assisted research summary: Serikali ya Kijiji ina wajibu wa kutenga ardhi kwa matumizi ya kilimo na ufugaji, kusaidia wakazi kupata ardhi ya kutosha, na kuhakikisha vijiji vina chakula cha kutosha pamoja na kilimo cha angalau ekari moja kwa mkazi anayehusika.
5. Serikali ya Kijiji itakuwa na wajibu wa: 3 Sheria Ndogo ya Kilimo, Chakula, Mifugo na Uvuvi ya Halmashauri ya Wilaya ya Songwe Tangazo La Serikali Na. 272 (Linaendelea) Serikali ya Kijiji (a) kutenga ardhi kwa ajili ya kilimo na malisho ya mifugo, maeneo ya ufugaji wa nyuki, mabwawa ya kufugia samaki; (b) kwa kushirikiana na uongozi wa kitongoji kuwezesha wakazi kupata ardhi ya kutosha kwa ajili ya kilimo; (c) kwa kushirikiana na uongozi wa kitongoji kuhakikisha kijiji anajitosheleza kwa chakula kwa kuwa na angalau gunia tatu za nafaka kwa mwaka; na kila mkazi wa kuwa Wajibu wa Afisa Mwidhini wa Hifadhi ya mazao (d) kuhakikisha kuwa kila mkazi katika eneo la kijiji anayemiliki ardhi ya kilimo na mwenye uwezo wa kufanya kazi, analima mazao ya chakula na biashara angalau ekari moja. - 6 Verify source ↗
Afisa mwidhiniwa atakuwa na wajibu wa
AI-assisted research summary: Afisa mwidhiniwa lazima ahakikishe kila mkulima anafanya maandalizi ya shamba, upandaji, nafasi ya kitaalamu, uwekaji wa mbolea, na palizi kwa wakati na kwa njia iliyotajwa.
6. Afisa mwidhiniwa atakuwa na wajibu wa kuhakikisha kwamba kila mkulima- (a) anaandaa mashamba kwa wakati; (b) anapanda mbegu kwa mstari; (c) anazingatia nafasi inayotakiwa kitaalamu; (d) anaweka mbolea kwa viwango na kwa wakati; na (e) anapalilia kwa wakati palizi mbili au zaidi. - 7 Verify source ↗
(1) Kila mkazi atakayelima shamba katika eneo la
AI-assisted research summary: Wakazi wanaolima mashamba katika eneo la Halmashauri lazima wavune mazao yanapokomaa na kuyahifadhi kwa usalama, na kila kaya inapaswa kuwa na chakula cha kutosha na ghala salama.
7.-(1) Kila mkazi atakayelima shamba katika eneo la Halmashauri atatakiwa kuvuna mazao yake yanapokomaa na kuyahifadhi katika njia ya usalama. (2) Itakuwa ni jukumu la kila mkazi hususani mkuu wa kaya kuhakikisha kuwa anahifadhi chakula cha kutosha yeye na familia yake kwa angalau mwaka mmoja au zaidi. (3) Litakuwa ni jukumu la kila kaya kuwa na ghala la kuhifadhia chakula ambalo litapaswa kuwa katika hali ya usalama na lisiwe na uwezekano wowote wa kuruhusu wadudu kuingia na kusababisha uharibifu wa chakula hicho. Wajibu wa Mkulima - 8 Verify source ↗
Itakuwa ni wajibu wa kila mkulima
AI-assisted research summary: Kila mkulima lazima atimize majukumu ya shamba la mazao, ikiwemo kupalilia, kuweka mbolea, kuripoti magonjwa au wadudu kwa Halmashauri, kutumia pembejeo kwa maelekezo, na kuchukua hatua za kudhibiti magonjwa na wadudu kwa maelekezo ya afisa ugani.
8. Itakuwa ni wajibu wa kila mkulima- (a) kupalilia shamba lenye mazao katika wakati 4 Sheria Ndogo ya Kilimo, Chakula, Mifugo na Uvuvi ya Halmashauri ya Wilaya ya Songwe Tangazo La Serikali Na. 272 (Linaendelea) stahili isipokuwa kama itaelezwa vinginevyo; (b) kuweka mbolea; (c) kutoa taarifa kwa Halmashauri kwa njia itakayokuwa inafaa kuhusu uwepo wa ugonjwa wa mazao au wadudu waharibifu; (d) kutumia pembejeo kwa kuzingatia maelekezo ya kama isipokuwa kila mwaka kitaalamu itaelekezwa vinginevyo na afisa ugani; na (e) kuchukua waharibifu atakavyokuwa ameelekezwa na afisa ugani. za kutibu magonjwa kuangamiza wadudu kama hatua au Ukaguzi - 9 Verify source ↗
Afisa mwidhiniwa, kwa kushirikiana na afisa
AI-assisted research summary: Afisa mwidhiniwa, pamoja na afisa ugani, anaweza kuingia mashambani au majumbani kwa nyakati zilizotajwa, kukagua ghala la chakula, kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wanaokiuka sheria ndogo, na anatakiwa kuweka daftari na kupanga ratiba ya ukaguzi wa mashamba.
9. Afisa mwidhiniwa, kwa kushirikiana na afisa ugani- (a) ataweza wakati wowote kuanzia saa kumi na mbili kamili asubuhi hadi saa kumi na mbili kamili jioni kuingia kwenye eneo la kilimo au katika shamba kwa madhumuni ya kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; (b) ataweza kuingia katika kaya yoyote kuanzia saa moja kamili asubuhi hadi saa kumi kamili jioni ili kukagua ghala la chakula kuona kama taratibu za kuhifadhi chakula zinazingatiwa; (c) ataweza kuchukua hatua za kisheria dhidi ya mtu yeyote atakayevunja Sheria Ndogo hii; (d) atatakiwa kuwa na daftari linaloonesha idadi kamili ya wakazi na idadi ya ekari zao za kilimo; na (e) atapanga ratiba ya kutembelea mashamba ya wakazi ili kuona kama wanatekeleza wajibu wa kulima na kutunza mashamba kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. Ukanda maalumu wa kilimo - 10 Verify source ↗
(1) Halmashauri inaweza kutangaza eneo lolote
AI-assisted research summary: Halmashauri inaweza kutangaza eneo lolote kuwa ukanda maalumu wa kilimo, na watu wanakatazwa kufanya uchimbaji, ukataji miti, au kuingiza mifugo kwa shughuli zisizo za kilimo katika ukanda huo wakati fulani wa mwaka.
10.-(1) Halmashauri inaweza kutangaza eneo lolote kuwa ukanda maalumu wa kilimo. (2) Itakua marufuku kwa mtu yeyote kufanya 5 Sheria Ndogo ya Kilimo, Chakula, Mifugo na Uvuvi ya Halmashauri ya Wilaya ya Songwe Tangazo La Serikali Na. 272 (Linaendelea) yafuatayo katika ukanda maalumu wa kilimo: (a) kufanya shughuli za uchimbaji; (b) kufanya shughuli za ukataji miti; na (c) kuingiza mifugo kwa nia ya kufanya shughuli yoyote isiyohusiana na kilimo kuanzia tarehe 15 Novemba hadi tarehe 1 Juni ya kila mwaka. (3) Bila kuathiri masharti ya aya ndogo ya (2), mifugo itaruhusiwa kuingia katika ukanda maalumu wa kilimo kuanzia tarehe 2 Juni hadi tarehe 14 Novemba ya kila mwaka baada ya kupata kibali kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji. SEHEMU YA TATU MASHARTI KUHUSU MIFUGO Wajibu wa Halmasha uri
Part
SEHEMU YA TATU
- 11 Verify source ↗
Halmashauri itakuwa na wajibu wa kufanya
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima ifanye kazi kadhaa za usimamizi wa ardhi na mifugo, ikiwemo kupanga matumizi ya ardhi, kudhibiti idadi ya mifugo, kutoa elimu, chanjo, na kusimamia miundombinu ya mifugo.
11. Halmashauri itakuwa na wajibu wa kufanya mambo yafuatayo: (a) kuandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi; (b) kuelekeza idadi ya mifugo ambayo kila mfugaji anaruhusiwa kufuga kulingana na ukubwa wa eneo lake; (c) kujenga majosho ya mifugo kwa kushirikiana na wananchi; (d) kutoa elimu ya ufugaji bora kwa jamii ili kuongeza tija; (e) kufanya sensa ya mifugo, kuweka alama na kutoa kadi za mifugo; (f) kutoa chanjo kwa kushirikiana na wafugaji ili kudhibiti magonjwa ya mifugo yasiyoambukiza na yanayoambukiza binadamu; (g) kudhibiti uzururaji holela wa mifugo na wanyama katika Halmashauri kwa mujibu wa Sheria; (h) kuanzisha kamati za majosho kwenye kila Kata au Kijiji ambapo majosho hayo yameanzishwa; (i) kusaidia kuanzisha vituo vya uhamilishaji wa mifugo ili kupata madume bora ya kisasa na mifugo yenye tija; 6 Sheria Ndogo ya Kilimo, Chakula, Mifugo na Uvuvi ya Halmashauri ya Wilaya ya Songwe Tangazo La Serikali Na. 272 (Linaendelea) (j) kuhakikisha upatikanaji wa mabwawa ya maji ya kunyweshea mifugo kwa kushirikiana na wafugaji; (k) kuanzisha machinjio ya wanyama ambayo ni ya kisasa na salama ili kurahisisha uvunaji wa mifugo kwa njia ya uchinjaji; na (l) kuhakikisha udhibiti wa ufugaji wa kuhamahama ili kuhifadhi mazingira. Wajibu wa mfugaji kuwa- - 12 Verify source ↗
Kila mfugaji katika Halmashauri atahakikisha
AI-assisted research summary: Kila mfugaji katika Halmashauri lazima atimize masharti ya kufuga, kutunza, kuchanja, na kuuza mifugo yake kwa njia zilizoelekezwa.
12. Kila mfugaji katika Halmashauri atahakikisha (a) anaogesha mifugo yake ili kudhibiti magonjwa ya na atakavyoelekezwa kama wanyama Halmashauri; Sura ya 154 (b) mifugo yake alama maalumu zinazotolewa kwa mujibu wa Sheria ya Ustawi wa Wanyama; inawekwa (c) anahudhuria mafunzo ya ufugaji kama atakavyohitajika na Halmashauri; (d) anakuwa na kadi ya mifugo itakayoonesha idadi na aina ya mifugo aliyonayo; (e) anaipata mifugo yake malisho au chakula na maji ya kutosha kwa kuzingatia kanuni bora za ufugaji; (f) anafuga kwa kuzingatia mipango ya matumizi bora ya ardhi; (g) anapeleka mifugo yake katika vituo vya chanjo kama itakavyoamriwa na Halmashauri na atalipia chanjo hiyo kama atatakiwa kufanya hivyo kwa mujibu wa viwango vitakavyoainishwa na mamlaka husika; na (h) anauza mifugo yake katika masoko na minada taarifa lingine kwa iliyoidhinishwa au eneo maalumu. Idadi ya mifugo - 13 Verify source ↗
Kila mfugaji aliye katika bonde la Songwe
AI-assisted research summary: Every livestock keeper in Songwe valley must keep animals within set herd limits.
13. Kila mfugaji aliye katika bonde la Songwe atatakiwa kufuga mifugo kama ifuatavyo: 7 Sheria Ndogo ya Kilimo, Chakula, Mifugo na Uvuvi ya Halmashauri ya Wilaya ya Songwe Tangazo La Serikali Na. 272 (Linaendelea) ipasayo kufugwa Masharti kwa mfugaji (a) ng’ombe na punda kwa pamoja wasiozidi mia moja; (b) mbuzi na kondoo kwa pamoja wasiozidi mia moja na hamsini. - 14 Verify source ↗
Kila mfugaji hataruhusiwa
AI-assisted research summary: Mfugaji haruhusiwi kufanya shughuli kadhaa za mifugo bila kibali au nje ya maeneo yaliyotengwa.
14. Kila mfugaji hataruhusiwa- (a) kuchunga, kulisha au kunywesha maji mifugo katika maeneo ambayo hayakutengwa kwa shughuli hiyo; (b) kusafirisha mifugo kwa kuiswaga barabarani; (c) kusafirisha au kuhamisha mifugo kutoka eneo lingine bila kibali kutoka moja kwenda Halmashauri; (d) kuingiza mifugo katika eneo la Halmashauri bila kibali; (e) kuuza au kununua mifugo katika maeneo ambayo si mnada, masoko au magulio ya mifugo yaliyoaidhinishwa bila kibali maalumu cha Halmashauri; (f) kufuga mifugo zaidi ya idadi iliyoainishwa katika Sheria Ndogo hii; (g) kununua, kuuza au kufanya biashara ya kubadilishana aina yoyote ya mfugo au mifugo katika eneo la Halmashauri bila kibali maalumu au magulio isipokuwa yaliyotengwa kwa shughuli hiyo na Halmashauri; na kwenye minada (h) kufuga nguruwe kwa kuwaachia nje na kuzagaa mitaani au mashambani bila kuwafungia katika mabanda. Kibali cha kusafirisha mifugo - 15 Verify source ↗
Mtu yeyote anayekusudia kusafirisha mfugo au
AI-assisted research summary: Mtu anayetaka kusafirisha mfugo, mifugo, au mazao yake kwenda au kutoka eneo la Halmashauri lazima awe na kibali maalumu cha Halmashauri.
15. Mtu yeyote anayekusudia kusafirisha mfugo au mifugo na mazao yake kutoka au kuingia katika eneo la Halmashauri atatakiwa kuwa na kibali maalumu cha Halmashauri kilichoainishwa katika Jedwali la Kwanza la Sheria Ndogo hii. 8 Sheria Ndogo ya Kilimo, Chakula, Mifugo na Uvuvi ya Halmashauri ya Wilaya ya Songwe Tangazo La Serikali Na. 272 (Linaendelea) Wajibu wa Serikali ya Kijiji Kudhibiti mifugo inayozurur a ovyo - 16 Verify source ↗
Serikali ya kijiji kwa ushirikiano na uongozi wa
AI-assisted research summary: Serikali ya kijiji pamoja na uongozi wa kitongoji lazima wahakikishe mpango wa matumizi bora ya ardhi unaandaliwa na unasimamia mipaka ya ardhi, idadi ya mifugo, uanzishwaji wa majosho, na uhamasishaji wa uvunaji wa mifugo; wataalamu wa ugani wa kijiji nao wanatoa elimu ya ufugaji wa kisasa.
16. Serikali ya kijiji kwa ushirikiano na uongozi wa kitongoji itahakikisha- (a) inaandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi katika kijiji; (b) inasimamia na kulinda mipaka ya ardhi ya kilimo na mifugo iliyobainishwa na mpango wa matumizi bora ya ardhi; (c) inasimamia idadi ya mifugo ambayo kila mfugaji ataruhusiwa kuwa nayo; (d) inasimamia uanzishwaji wa majosho ya mifugo kwa ushirikiano na wafugaji; (e) inahamasisha wafugaji kuvuna mifugo yao mara kwa mara ili kuwa na idadi ya mifugo yenye kuleta tija na idadi inayokubalika kisheria; na (f) wataalamu wa ugani waliopo katika kijiji wanatoa elimu ya ufugaji wa kisasa ili kupata mifugo bora na mazao bora ya mifugo. - 17 Verify source ↗
(1) Halmashauri itakamata mfugo au mifugo
AI-assisted research summary: The Council may impound livestock that is roaming around in its area, and the owner must pay a daily fine if the livestock was impounded.
17.-(1) Halmashauri itakamata mfugo au mifugo la inazurura ovyo katika eneo itakayoonekana yoyote Halmashauri. (2) Mmiliki wa mfugo wowote utakaokamatwa chini ya aya ndogo ya (1) atalipa faini ya shilingi elfu kumi kwa kila siku. (3) Endapo mmiliki hatachukua mfugo uliokamatwa ndani ya kipindi cha siku saba tangu kukamatwa, Halmashauri itakuwa na haki ya kuuza kwa mnada mfugo huo baada ya kupata idhini ya Mahakama, na fedha zitakazopatikana zitarejeshwa kwa mmliki wa mfugo huo baada ya kutoa faini inayodaiwa, gharama za kuhifadhi mfugo, gharama ya mahakama na gharama ya mnada. (4) Bila kuathiri aya ndogo ya (3), kabla ya kuuza mfugo kwa mnada, Halmashauri itamjulisha mmliki na umma kuhusu kusudio hilo. 9 Sheria Ndogo ya Kilimo, Chakula, Mifugo na Uvuvi ya Halmashauri ya Wilaya ya Songwe Tangazo La Serikali Na. 272 (Linaendelea) (5) Endapo kutatokea kufa kwa mifugo au mfugo kutokana na sababu yoyote, Halmashauri haitawajibika na ulipaji wa gharama zozote isipokuwa kama vifo hivyo vitakuwa vimesababishwa kwa uzembe wa watumishi wa Halmashauri. Wajibu wa Afisa Mwidhiniw a - 18 Verify source ↗
Afisa Mwidhiniwa au Afisa Ugani atatakiwa
AI-assisted research summary: Afisa Mwidhiniwa au Afisa Ugani lazima ahakikishe uchanjaji na uogeshaji wa mifugo, aendelee na daftari la usajili wa wafugaji, atoe taarifa kwa Halmashauri kuhusu milipuko ya magonjwa, na aingie majumbani au majengoni kwa utekelezaji wa Sheria Ndogo katika saa za mchana.
18. Afisa Mwidhiniwa au Afisa Ugani atatakiwa- (a) kuhakikisha kuwa mfugaji anachanja na kuogesha ili kuepuka mifugo yake mara kwa mara magonjwa ya mifugo; (b) kuwa na daftari la usajili wa wafugaji wote ndani ya Halmashauri linaloonyesha idadi kamili ya mifugo kwa kila mfugaji; (c) kutoa taarifa kwa Halmashauri mara anapogundua kuna mlipuko wa magonjwa ambayo yanahitaji msaada kutoka ngazi za juu; na (d) kuingia katika nyumba au jengo lolote kuanzia saa kumi na mbili kamili asubuhi hadi saa kumi na mbili kamili jioni kwa lengo la utekelezaji wa Sheria Ndogo hii. SEHEMU YA NNE MASHARTI KUHUSU UVUVI Wajibu wa Halmasha uri katika shughuli za uvuvi
Part
SEHEMU YA NNE
- 19 Verify source ↗
Halmashauri itakuwa na wajibu wa kufanya
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima ichukue hatua za kukuza, kuanzisha na kusimamia ufugaji wa samaki wa kisasa, kuanzisha mabwawa ya mfano, kuwezesha maafisa ugani, kuhakikisha upatikanaji wa vifaranga, na kuhamasisha wananchi.
19. Halmashauri itakuwa na wajibu wa kufanya mambo yafuatayo: (a) kuhamasisha, kuanzisha na kusimamia ufugaji wa samaki wa kisasa katika eneo lake; (b) inaanzisha mabwawa ya mfano ya samaki katika angalau kila kata; (c) inawezesha upatikanaji wa maafisa ugani wa uvuvi kwenye kata; (d) kuhakikisha vifaranga vya samaki vinapatikana ili kupandikizwa katika mabwawa ya wananchi; na (e) kuhamasisha wananchi juu ya uanzishaji wa kilimo cha ufugaji wa Samaki. 10 Sheria Ndogo ya Kilimo, Chakula, Mifugo na Uvuvi ya Halmashauri ya Wilaya ya Songwe Tangazo La Serikali Na. 272 (Linaendelea) Wajibu wa Serikali ya Kijiji Wajibu wa Afisa Mwidhini wa - 20 Verify source ↗
Serikali ya kijiji kwa ushirikiano na uongozi wa
AI-assisted research summary: The village government must work with sub-village leadership to set aside land for model fish ponds or fish farms, establish village fish ponds, and work with the district council on fish farming training.
20. Serikali ya kijiji kwa ushirikiano na uongozi wa kitongoji itahakikisha: (a) inatenga ardhi ya kuanzisha mabwawa ya mfano au mashamba darasa ya ufugaji wa samaki; (b) inaanzisha mabwawa ya samaki ya kijiji ili kukuza kipato cha makusanyo ya maduhuli ya kijiji; na (c) inashirikiana na Halmashauri ya Wilaya kuanzisha mafunzo ya nadharia na vitendo kuhusiana na ufugaji bora wa samaki. - 21 Verify source ↗
Afisa Mwidhiniwa au Afisa Ugani atatakiwa
AI-assisted research summary: Afisa Mwidhiniwa au Afisa Ugani lazima awe na rejesta ya wafugaji wa samaki, aanzishe mashamba darasa ya mfano, na ahakikishe wafugaji wanatumia nyavu sahihi wakati wa kuvuna.
21. Afisa Mwidhiniwa au Afisa Ugani atatakiwa- (a) kuwa na rejesta ya wafugaji wote wa samaki katika kata au kijiji; (b) kuanzisha mashamba darasa ya mfano kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa vitendo kwa wafugaji wa samaki; na (c) kuhakikisha wafugaji samaki wanatumia nyavu sahihi wakati wa kuvuna samaki katika mabwawa yao ili kutokuharibu mazalia na kutovuna samaki wadogo. Wajibu wa Mvuvi - 22 Verify source ↗
Mvuvi yeyote wa samaki ndani ya Halmashauri
AI-assisted research summary: Mvuvi yeyote wa samaki ndani ya Halmashauri lazima awe na vibali na leseni halali, atumie nyavu zinazokubalika kitaalamu, asifanye uvuvi haramu kwa mabomu, makokoro, sumu au vyandarua, asajili vyombo vya uvuvi, na asibebe samaki wakichanganywa na mazao mengine.
22. Mvuvi yeyote wa samaki ndani ya Halmashauri atawajibika- (a) kuwa na vibali na leseni halali za uvuvi; (b) kufanya shughuli za uvuvi kwa kutumia nyavu zinazokubalika kitaalamu; (c) kutokufanya uvuvi haramu wa kutumia mabomu, makokoro, sumu auvyandarua; (d) kusajili vyombo vyote vya uvuvi; na (e) kutobeba samaki kwa kuchanganya na mazao mengine. SEHEMU YA TANO MAKOSA NA ADHABU 11 Sheria Ndogo ya Kilimo, Chakula, Mifugo na Uvuvi ya Halmashauri ya Wilaya ya Songwe Tangazo La Serikali Na. 272 (Linaendelea) Makosa yanayotok ana na shughuli za kilimo Makosa yanayotok ana na shughuli za mifugo
Part
SEHEMU YA TANO
- 23 Verify source ↗
Itakuwa ni kosa chini ya Sheria Ndogo hii kwa
AI-assisted research summary: Kifungu hiki kinataja kuwa kosa kwa mtu yeyote kufanya au kuacha kufanya vitendo fulani vya kilimo, ikiwemo kuuza mazao shambani, kutohifadhi chakula cha kutosha, kutotunza au kutovuna shamba, kukosa ghala, au kulima karibu sana na mto.
23. Itakuwa ni kosa chini ya Sheria Ndogo hii kwa mtu yeyote- (a) anayemiliki ardhi ya kilimo kushindwa, kukataa au kukataza shamba kulimwa mazao ya chakula, biashara au matunda; (b) kuuza mazao yakiwa shambani; (c) kutohifadhi chakula cha kutosha; (d) kutotunza shamba; (e) kutovuna mazao yaliyo shambani ambayo yamefikia wakati wa kuvunwa; (f) kutokuwa na ghala la kuhifadhia mazao; na (g) kulima ndani ya mita sitini toka ulipo mto. - 24 Verify source ↗
Mfugaji yeyote atakuwa ametenda kosa iwapo
AI-assisted research summary: Mfugaji yeyote anatenda kosa akifanya mojawapo ya vitendo vilivyokatazwa, kama vile kushindwa kuogesha au kuchanja mifugo, kulisha kwenye maeneo yasiyoruhusiwa, kutotoa taarifa ya ugonjwa au kifo cha ghafla, kuuza/kufuga mahali pasiporuhusiwa, kusababisha kero, kuruhusu mifugo kuzurura, kukataa ushirikiano wa alama, kumzuia Afisa Mwidhiniwa, kuuza mifugo eneo lisiloruhusiwa, au kuingiza mifugo kutoka nje ya Halmashauri bila kibali.
24. Mfugaji yeyote atakuwa ametenda kosa iwapo: (a) atashindwa au kukataa kuogesha au kuchanja mfugo au mifugo yake ili kuzuia magonjwa; (b) atalisha mfugo au mifugo kwenye maeneo yasiyoruhusiwa; (c) atashindwa au atazembea kutoa taarifa kuhusu uwepo wa au dalili za ugonjwa au kifo cha ghafla cha mfugo au mifugo katika banda lake; (d) atauza au kufuga mfugo au mifugo pembezoni mwa barabara au sehemu ambayo hairuhusiwi; (e) atasababisha kero ya harufu mbaya na kelele ya mfugo au mifugo yake kwa jamii; (f) ataruhusu mfugo au mifugo yake kuzurura hovyo; (g) atashindwa kutoa ushirikiano wa uwekaji wa alama kwa mfugo au mifugo yake; Afisa Mwidhiniwa (h) atamzuia kutekeleza majukumu yake; (i) atauza mifugo kwenye eneo ambalo haliruhusiwi; au (j) ataingiza mifugo kutoka nje ya Halmashauri bila ya kibali. 12 Sheria Ndogo ya Kilimo, Chakula, Mifugo na Uvuvi ya Halmashauri ya Wilaya ya Songwe Tangazo La Serikali Na. 272 (Linaendelea) Makosa yanayotok ana na shughuli za vuvi - 25 Verify source ↗
Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa iwapo
AI-assisted research summary: Mtu yeyote atatenda kosa akifanya mojawapo ya vitendo vilivyoorodheshwa, kama kuvua samaki kwa mabomu au bila kibali/leseni halali.
25. Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa iwapo- (a) atavua samaki kwa kutumia mabomu, makokoro, sumu, milipuko, mikuki au vyandaru; (b) atavua bila kuwa na kibali halali; (c) atavua bila kuwa na leseni halali; (d) atafanya biashara ya samaki bila kuwa na leseni; (e) atakataa au kukwepa kulipa ushuru wa Halmashauri; (f) atatumia nyavu zisizokubalika kitaalamu; (g) atauza au kununua samaki katika maeneo yanayokatazwa chini ya Sheria Ndogo hii au Sheria nyingine yoyote; (h) ataendesha shughuli za uvuvi bila ya kujiandikisha kwenye rejesta ya wavuvi ya kata au kijiji; (i) atavua katika maeneo ya hifadhi au eneo lolote lisiloruhusiwa kisheria; (j) atapatikana akivua au akiuza samaki wadogo wadogo; na (k) atatumia mtumbwi, ngalawa au boti ambayo haijasajiliwa. Adhabu - 26 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayepatikana na hatia kwa kutenda
AI-assisted research summary: Anyone convicted of an offence under this bylaw is liable to a fine of up to 300,000 shillings, imprisonment of up to 12 months, or both.
26. Mtu yeyote atakayepatikana na hatia kwa kutenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii atawajibika kulipa faini isiyozidi shilingi laki tatu au kifungo kisichozidi miezi kumi na mbili jela au adhabu zote kwa pamoja. Kufifilisha kosa - 27 Verify source ↗
Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kumtoza mtu aliyekiri kosa chini ya Sheria Ndogo hii kiasi kisichozidi shilingi elfu hamsini.
27. Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha kosa kwa kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii kiasi kisichozidi shilingi elfu hamsini endapo mkosaji atakiri kosa na kuwa tayari kujaza fomu maalumu iliyoainishwa katika Jedwali la Pili la Sheria hii. ____________ JEDWALI LA KWANZA 13 Sheria Ndogo ya Kilimo, Chakula, Mifugo na Uvuvi ya Halmashauri ya Wilaya ya Songwe Tangazo La Serikali Na. 272 (Linaendelea) ________________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 15) KIBALI CHA KUSAFIRISHA MIFUGO AU MAZAO YA MIFUGO Jina: ……………………………………………. Anuani: ………………………………………… Ameruhusiwa kusafirisha Mifugo ifuatayo kutoka ………………kupitia njia za…………………….. hadi…………..….. Idadi ya Mifugo Namba Aina ya Mfugo
Part
JEDWALI LA KWANZA
- 12 Verify source ↗
Section 12
AI-assisted research summary: This provision shows a temporary livestock permit form and a form for admitting an offence and agreeing to pay a fine.
12. Ng’ombe Mbuzi Kondoo Nguruwe Ngamia Punda Paka Farasi Sungura Mbwa Kuku au Bata Mifugo wengine Kibali hiki kitakuwa cha muda wa siku ….. kuanzia tarehe….... hadi tarehe………. Kimetolewa na : Jina la Afisa Mwidhiniwa: ………………………………………. Saini: …………………………………………………………….. Wadhifa: …………………………………………………………….. Tarehe: ………………………………………………………….... Muhuri: ……………………………………… ____________ JEDWALI LA PILI ___________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 27) _______ FOMU YA KUKIRI NA KUFIFILISHA KOSA Mimi ……………………………………………………… nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya …………………………………………. ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe, kwamba mnamo tarehe …… ya Mwezi ………. Mwaka ……….…… nilitenda kosa la kukiuka masharti ya aya …… ya Sheria Ndogo ya Kilimo, Chakula, Mifugo na Uvuvi ya Halmashauri ya Wilaya ya Songwe ya Mwaka 2024. Kwa Mamlaka aliyopewa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe, niko tayari kulipa kiasi cha faini ninayodaiwa. 14 Sheria Ndogo ya Kilimo, Chakula, Mifugo na Uvuvi ya Halmashauri ya Wilaya ya Songwe Tangazo La Serikali Na. 272 (Linaendelea) NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA MIMI MWENYEWE KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU Leo tarehe…………. ya Mwezi…………..… Mwaka ……………. Jina ……………………………….. Saini……………………… MBELE YANGU: Jina: ……………………………………..……………………..... Saini………………………….…………………………..……… Wadhifa: ………………………………………………………… Tarehe …………………………………………………………… 15 Sheria Ndogo ya Kilimo, Chakula, Mifugo na Uvuvi ya Halmashauri ya Wilaya ya Songwe Tangazo La Serikali Na. 272 (Linaendelea) Nembo na muhuri wa Halmashauri ya wilaya ya SONGWE imebandikwa kwenye Sheria Ndogo hizi kufutia Azimio Na SDC/ MB/09/2023 lililopitishwa na Mkutano wa Baraza la Madiwani kilichoketi Tarehe 02/1/2023 na ubandikwaji huo kushuhudiwa na;- CPA CECILIA D KAVISHE Mkurugenzi Mtandaji Halmashauri ya Wilaya ya Songwe ABRAHAM KAGULUKA SAMBILA Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya Songwe NAKUBALI L.S Dodoma, MOHAMED OMARY MCHENGERWA 30 Januari, 2024 Waziri wa Nchi- Ofisi ya Rais (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa) 16
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Kilimo, Chakula, Mifugo na Uvuvi ya Halmashauri ya Wilaya ya Songwe ya Mwaka 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in