Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Songwe ya Mwaka 2024
This provision gives the short title of the by-law: the Songwe District Council Service Tax By-Law, 2024.
AI-assisted research synopsis — verify against the official legal text below.
- Jurisdiction
- Tanzania
- Instrument
- Regulation
- Citation
- Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Songwe ya Mwaka 2024
- Version
- Undated source snapshot
- Language
- sw
- Official source
- View official record ↗
Statute overview
About this statute
This provision gives the short title of the by-law: the Songwe District Council Service Tax By-Law, 2024. This provision says the by-law applies throughout the area of the Songwe District Council. This section defines key terms used in the by-law, including the council, director, authorized officer, service levy payer, and the service levy threshold. The Council must charge and collect a service levy: 0.3% of sales, after VAT and excise duty deductions, from business-licensed persons who submit sales accounts to the Tanzania Revenue Authority; and the First Schedule rate from business-licensed traders who do not submit sales accounts. Kila mlipa ushuru wa huduma ana wajibu wa kulipa na kuripoti taarifa/hesabu kwa Halmashauri, kutunza kumbukumbu, na kuziweka kwa ukaguzi ndani ya muda uliowekwa.
Search within this statute
Search all stored provisions in this version.
Legal text
Provisions of Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Songwe ya Mwaka 2024
Showing 14 of 14
- 1 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya
AI-assisted research summary: This provision gives the short title of the by-law: the Songwe District Council Service Tax By-Law, 2024.
1. Sheria Ndogo hii itajulikana kama Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Songwe ya Mwaka 2024. Matumizi - 2 Verify source ↗
Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la
AI-assisted research summary: This provision says the by-law applies throughout the area of the Songwe District Council.
2. Sheria Ndogo hii itatumika katika eneo lote la Mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya ya Songwe. Tafsiri - 3 Verify source ↗
Katika Sheria Ndogo hii,
AI-assisted research summary: This section defines key terms used in the by-law, including the council, director, authorized officer, service levy payer, and the service levy threshold.
3. Katika Sheria Ndogo hii, isipokuwa kama muktadha utahitaji vinginevyo- “Afisa Mwidhiniwa” maana yake ni Afisa yeyote aliyeteuliwa na Mkurugenzi kwa lengo la kusimamia utekelezaji wa Sheria Ndogo hii; “Halmashauri” maana yake ni Halmashauri ya Wilaya ya Songwe; “hesabu za mwisho” maana yake ni hesabu za mwisho zinazowasilishwa na taasisi yoyote ya kibiashara baada ya kipindi cha hesabu pamoja na nyaraka au maelezo yatakayotakiwa kutolewa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii; Sura ya 212 “kampuni” maana yake ni kampuni iliyosajiliwa kwa mujibu wa Sheria ya Kampuni; “kipindi maalumu cha hesabu” maana yake ni muda ambao 1 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Songwe Tangazo La Serikali Na. 273 (Linaendelea) mfanyabiashara anatakiwa kuwasilisha hesabu za biashara kwa Halmashauri; “Mkurugenzi” maana yake ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe au Afisa yeyote aliyeteuliwa kutekeleza majukumu ya Mkurugenzi chini ya Sheria Ndogo hii; Sura ya 212 Ushuru wa huduma tawi “tawi au mfanyabiashara mwenye “mlipa ushuru wa huduma” maana yake ni kampuni, tawi la leseni kampuni anayefanya shughuli zake katika eneo la Halmashauri; la kampuni” maana yake ni la kampuni iliyosajiliwa kwa mujibu wa Sheria ya Kampuni; “ushuru wa huduma” maana yake ni ushuru unaotozwa na kukusanywa na Halmashauri kutoka kwa kampuni, tawi la kampuni au mfanyabiashara yeyote mwenye leseni ya biashara ambaye mauzo yake kwa mwaka ni zaidi ya shilingi milioni nne kutokana na huduma anazopata na kutumia miundombinu ya umma inayomuwezesha kufanya biashara katika eneo la Halmashauri; “Wakala” maana yake ni mtu binafsi au kikundi cha watu, kampuni limeteuliwa na Halmashauri kwa lengo la kukusanya ushuru kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. ambalo shirika au - 4 Verify source ↗
(1) Halmashauri itatoza na kukusanya ushuru wa
AI-assisted research summary: The Council must charge and collect a service levy: 0.3% of sales, after VAT and excise duty deductions, from business-licensed persons who submit sales accounts to the Tanzania Revenue Authority; and the First Schedule rate from business-licensed traders who do not submit sales accounts.
4.-(1) Halmashauri itatoza na kukusanya ushuru wa huduma kwa kiwango cha asilimia sifuri nukta tatu (0.3%) ya mauzo baada ya kutoa Kodi ya Ongezeko la Thamani na ushuru wa bidhaa kutoka kwa mtu yeyote mwenye leseni ya biashara anayewasilisha hesabu za mauzo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania. (2) Bila kuathiri aya ndogo ya (1), Halmashauri itatoza na kukusanya ushuru wa huduma kwa kiwango kilichoainishwa katika Jedwali la Kwanza la Sheria Ndogo hii kutoka kwa wafanyabiashara wenye leseni za biashara ambao hawawasilishi hesabu za mauzo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania. 2 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Songwe Tangazo La Serikali Na. 273 (Linaendelea) Wajibu wa Mlipa Ushuru wa Huduma - 5 Verify source ↗
(1) Kila mlipa ushuru wa huduma atakuwa na
AI-assisted research summary: Kila mlipa ushuru wa huduma ana wajibu wa kulipa na kuripoti taarifa/hesabu kwa Halmashauri, kutunza kumbukumbu, na kuziweka kwa ukaguzi ndani ya muda uliowekwa.
5.-(1) Kila mlipa ushuru wa huduma atakuwa na wajibu wa: (a) kulipa ushuru wa huduma kwa kiwango kilichoainishwa katika Sheria Ndogo hii; (b) kuwasilisha taarifa sahihi za mauzo ya kila mwezi endapo anawasilisha taarifa za hesabu za mauzo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania; (c) kuwasilisha hesabu sahihi na za kweli; (d) kuwasilisha nyaraka au inayotakiwa taarifa Halmashauri ndani ya muda kuwasilishwa uliowekwa; (e) kutunza kumbukumbu za kitabu cha hesabu; na (f) kuonesha kumbukumbu yoyote au nyaraka kwa ajili ya uchunguzi. (2) Kila mlipa ushuru wa huduma atatakiwa kulipa ushuru huo si zaidi ya siku kumi na nne tangu tarehe ya kuwasilisha taarifa za mauzo ya kila mwezi. (3) Bila kuathiri aya ndogo ya (2), Halmashauri inaweza kukubaliana na mlipa ushuru wa huduma utaratibu wa kulipa ushuru. (4) Kila mlipa ushuru atatakiwa kuwasilisha Halmashauri hesabu za mwisho katika kipindi cha miezi mitatu tangu kumalizika kwa kipindi cha hesabu. (5) Endapo mlipa ushuru hajawasilisha hesabu za mwisho kwa mwaka wa fedha husika na ametakiwa kufanya hivyo kwa notisi ya siku thelathini, Mkurugenzi anaweza kwa kadri atakavyoona inafaa, kuamua kiwango cha hesabu za mlipa ushuru huyo kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii. (6) Ushuru uliothaminiwa kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii utalipwa katika kipindi cha siku thelathini tangu tarehe ya kufanya tathmini. (7) Endapo mlipa ushuru hajawasilisha majumuisho ya hesabu zake kwa mwaka wowote wa mapato, na endapo Mkurugenzi au Afisa Mwidhiniwa anafikiri kwamba mlipa ushuru ana wajibu wa kulipa ushuru kwa mwaka husika, 3 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Songwe Tangazo La Serikali Na. 273 (Linaendelea) Mamlaka ya Mkurugen zi anaweza kwa kadri atakavyoona kuamua kiwango cha hesabu za mlipa ushuru huyo, isipokuwa tathmini hiyo haitaathiri wajibu wowote wa mlipa ushuru anayostahili kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii, kwa kushindwa kwake kuwasilisha hesabu hizo. - 6 Verify source ↗
(1) Endapo mlipa ushuru wa huduma anayetakiwa
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kuwataka walipa ushuru na watu wengine kutoa taarifa, kumbukumbu, na hesabu za biashara; anaweza pia kuagiza ukaguzi na kumteua mtaalamu wa kodi kwa ajili ya tathmini na ukusanyaji.
6.-(1) Endapo mlipa ushuru wa huduma anayetakiwa kuwasilisha taarifa ya mauzo chini ya Sheria Ndogo hii atashindwa kuwasilisha taarifa sahihi za mauzo kwa wakati, Mkurugenzi anaweza kutoa notisi ya kumtaka mlipa ushuru wa huduma kuwasilisha taarifa hiyo ndani ya siku thelathini kuanzia tarehe ya kutolewa kwa notisi. (2) Mkurugenzi anaweza kumtaka kwa maandishi mtu yeyote mwenye taarifa kuhusu mfanyabiashara anayepaswa kulipa ushuru wa huduma kwa mujibu wa Sheria Ndogo hii kuwasilisha kwake taarifa ambazo zitatumika kama taarifa sahihi. (3) Mkurugenzi anaweza kumuagiza kwa maandishi Afisa Mwidhiniwa kuingia kwenye jengo au eneo la mlipa ushuru wa huduma kwa nia ya kufanya uchunguzi na tathmini ya kumbukumbu za biashara, vitabu vya hesabu na taarifa kwa ajili ya kupata na kujua kiwango sahihi cha ushuru anachotakiwa kulipa. (4) Mkurugenzi anaweza kumteua Kamishna wa kodi ya forodha au kodi ya mapato kwa ajili ya kutathmini na kukusanya ushuru wa huduma na kuwasilisha halmashauri kwa lengo la kupata ushuru wa huduma pamoja na madeni yake. (5) Mkurugenzi kwa taarifa ya maandishi anaweza kumtaka mlipa ushuru yeyote kuwasilisha hesabu zenye taarifa kamili za shughuli za kibiashara zikionesha thamani ya kiasi na thamani ya kifedha ya bidhaa au huduma zilizozalishwa, kutolewa kusambazwa au kuuzwa kibiashara na taarifa ya fedha katika kipindi maalumu kisichozidi siku thelathini tangu tarehe ya taarifa hiyo. (6) Mkurugenzi anaweza kwa taarifa ya maandishi ya 4 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Songwe Tangazo La Serikali Na. 273 (Linaendelea) siku saba kumtaka mlipa ushuru kuwasilisha kumbukumbu za kibiashara na vitabu vya hesabu kwa nia ya kupata taarifa kwa ajili ya kufanyiwa tathmini au kukusanya ushuru wa huduma. Uteuzi wa Wakala - 7 Verify source ↗
(1) Bila ya kuathiri masharti mengine ya Sheria
AI-assisted research summary: Mkurugenzi anaweza kuteua wakala wa kukusanya ushuru kwa niaba ya Halmashauri.
7.-(1) Bila ya kuathiri masharti mengine ya Sheria Ndogo hii, Mkurugenzi anaweza kuteua Wakala wa kukusanya ushuru kwa niaba ya Halmashauri. (2) Wakala aliyeteuliwa kwa mujibu wa aya ndogo ya (1) atakuwa na wajibu wa: (a) kukusanya na kupokea ushuru kwa niaba ya Halmashauri katika eneo alilopangiwa na kwa viwango vilivyoidhinishwa katika Sheria Ndogo hii; na (b) kukusanya ushuru kwa kutumia mfumo wa kielektroniki na kuwasilisha makusanyo yote kwa kuzingatia masharti ya mkataba wa uwakala alioingia na Halmashauri. - 8 Verify source ↗
Afisa Mwidhiniwa anaweza
AI-assisted research summary: Afisa Mwidhiniwa anaweza kupokea na kukubali hesabu za mlipa ushuru kwa ajili ya tathmini, au kukataa hesabu za mwisho ikiwa ana sababu za msingi kuamini kuwa si sahihi.
8. Afisa Mwidhiniwa anaweza- (a) kupokea na kukubali hesabu za mlipa ushuru na kuzifanyia tathmini kuhusu kiwango cha hesabu cha mlipa ushuru endapo hesabu hizo zitakuwa ni sahihi; au (b) kukataa hesabu za mwisho iwapo atakuwa na sababu za msingi za kuamini kuwa hesabu hizo si sahihi. - 9 Verify source ↗
Halmashauri itakokotoa ushuru wa huduma wa
AI-assisted research summary: Halmashauri lazima ikokotoe ushuru wa huduma kwa mlipa ushuru anayewasilisha taarifa za mauzo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania, ikizingatia taarifa zinazowasilishwa katika kipindi maalumu cha hesabu.
9. Halmashauri itakokotoa ushuru wa huduma wa mlipa ushuru anaewasilisha taarifa za mauzo kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania kwa kuzingatia taarifa zinazowasilishwa na mlipa ushuru wa huduma katika kipindi maalumu cha hesabu. - 10 Verify source ↗
Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa endapo
AI-assisted research summary: Anyone commits an offence if they fail to file correct sales information on time, file incorrect information, fail to pay the service levy on time, persuade a service levy payer to refuse or avoid payment, obstruct the authorised officer or council agent, or give false information about a matter that may affect another person’s levy liability.
10. Mtu yeyote atakuwa ametenda kosa endapo: (a) atashindwa kuwasilisha Halmashauri taarifa sahihi 5 Uwezo wa Afisa Mwidhini wa Ukokotoaj i wa ushuru wa huduma Makosa Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Songwe Tangazo La Serikali Na. 273 (Linaendelea) za mauzo ndani ya muda ulioainishwa katika Sheria Ndogo hii; (b) atawasilisha Halmashauri taarifa zisizo sahihi; (c) atashindwa kulipa ushuru wa huduma ndani ya muda ulioainishwa katika Sheria Ndogo hii; (d) atamshawishi mlipa ushuru wa huduma kukataa au kukwepa kulipa ushuru; (e) atamzuia Afisa Mwidhiniwa au Wakala wa Halmashauri kutekeleza masharti ya Sheria hii; au (f) atatoa taarifa isiyo sahihi kuhusu jambo lolote la mtu lake au jukumu linaloweza kuathiri mwingine la kulipa ushuru. Adhabu - 11 Verify source ↗
Mtu yeyote atakayepatikana na hatia kwa kutenda
AI-assisted research summary: A person convicted of an offence under this bylaw must pay a fine, face imprisonment, or both.
11. Mtu yeyote atakayepatikana na hatia kwa kutenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii atawajibika kulipa faini isiyopungua shilingi laki mbili na isiyozidi shilingi milioni moja au kifungo kisichopungua miezi kumi na mbili na kisichozidi miezi ishirini na nne au vyote kwa pamoja. Kufifilisha Kosa - 12 Verify source ↗
Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha kosa
AI-assisted research summary: The Director may compound an offence by charging up to TZS 200,000 if the offender admits the offence voluntarily, is ready to complete the specified form, and pays the tax due.
12. Mkurugenzi atakuwa na uwezo wa kufifilisha kosa kwa kumtoza mtu yeyote aliyetenda kosa chini ya Sheria Ndogo hii kiasi kisichozidi shilingi laki mbili endapo mkosaji atakiri kosa kwa hiari na kuwa tayari kujaza fomu maalumu iliyoainishwa katika Jedwali la Pili la Sheria Ndogo hii na kulipa ushuru anaodaiwa. ____________ JEDWALI LA KWANZA ____________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 4(2)) USHURU WA HUDUMA KWA WAFANYA BIASHARA WASIOTUNZA KUMBUKUMBU. Namba
Part
JEDWALI LA KWANZA
- 1 Verify source ↗
Section 1
AI-assisted research summary: Inaonyesha viwango vya ada ya biashara ya kila mwaka na ushuru wa huduma wa kila mwaka kwa Shilingi.
1. 2, Kiwango cha ada ya biashara kwa mwaka (Shilingi) 0 hadi 15,000/= 20,000/= hadi 35,000/= leseni ya Kiasi cha malipo ya ushuru wa huduma kwa mwaka (Shilingi). 5,000/= 22,500/= 6 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Songwe Tangazo La Serikali Na. 273 (Linaendelea) - 4 Verify source ↗
Section 4
AI-assisted research summary: Fomu hii inaonyesha mtu akikiri kwa hiari kwamba amekiuka masharti ya Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Songwe na yuko tayari kulipa ushuru unaodaiwa pamoja na faini.
4. 40,000/= hadi 100,000/= 105000/= hadi 200,000/= 32,500/= 40,000/= ____________ JEDWALI LA PILI _____________ (Limetengenezwa chini ya aya ya 12) _____________ FOMU YA KUKIRI NA KUFIFILISHA KOSA Mimi ……………………………………………………… nakiri KWA HIARI YANGU MWENYEWE mbele ya …………………………………………. ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe, kwamba mnamo tarehe …… ya mwezi ……. Mwaka …… nilitenda kosa la kukiuka masharti ya aya ........... ya Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Songwe ya Mwaka 2024. Kwa Mamlaka aliyopewa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe, niko tayari kulipa kiasi cha ushuru ninaodaiwa pamoja na faini. NATHIBITISHA KWAMBA MAELEZO HAPO JUU NI YA KWELI NA NIMEYATOA MIMI MWENYEWE KWA HIARI YANGU KADRI YA UFAHAMU WANGU ya Mwezi…………..… Mwaka ……………. Saini……………………… Leo tarehe…………. Jina……………………………….. MBELE YANGU: Jina: ……………………………………..…………………… Saini………………………….…………………………..……… Wadhifa: ………………………………………………………… Tarehe…………………………………………………………. 7 Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Songwe Tangazo La Serikali Na. 273 (Linaendelea) Lakari ya Halmashauri ya wilaya ya Songwe iliyogongwa katika Sheria Ndogo hizi kwa kufutia Azimio Na SDC/ MB/09/2023 la Kikao cha Halmashauri ya Wilaya Songwe cha Tarehe 02/1/2023 na imebaandikwa na kushuhudiwa mbele ya;- CPA CECILIA D KAVISHE Mkurugenzi Mtandaji Halmashauri ya Wilaya ya Songwe ABRAHAM KAGULUKA SAMBILA Mwenyekiti Halmashauri ya Wilaya ya Songwe NAKUBALI L.S Dodoma, MOHAMED OMARY MCHENGERWA 30 Januari, 2024 Waziri wa Nchi- Ofisi ya Rais (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa) 8
Provision text is displayed from LexChat’s stored statute record. Use the official source links to verify amendments, commencement, and current legal force.
Ask AI about this statute
Sheria Ndogo ya Ushuru wa Huduma ya Halmashauri ya Wilaya ya Songwe ya Mwaka 2024
Sign in to ask AI about this statute
Sign in to start authenticated, citation-grounded statute research.
Sign in